|
Mfalme Mswati III akiwasili nchini Uingereza akiwa na mmoja wa wake zake. |
|
Malkia Nothando Dube |
|
Malkia Elizabeth akiwa pamoja na mgeni wake King Mswati III alipowasili nchini Uingereza. |
|
Huyu ni mmoja wa wake wa mfalme Mswati aliyekumbwa na kashfa ya kutembea kimapenzi na mmoja wa mawaziri wa King Mswati III |
|
|
|
Mfalme Mswati akijiandaa kushiriki tamasha la kuchagua mke. |
|
Mkuu akiwa amepozi kwenye kiti cha Enzi |
|
Wakati mwingine mkuu hutupia magwanza kama mavazi rasmi anapokuwa katika shughuli za kiserikali |
|
hapa mkuu anajiwinda kuchagua binti atakayeona kuwa anamfaa. |
|
wakati mwingine mkuu anaweza akatupia pamba nyepesi za uhakika kabisa. |
|
Yes hapa naona mkuu ametokea katika pozi la uhakika. |
|
na hapa je? mkuu ameshapambwa tayari |
|
Na huyu naye ni mmoja wa malkia anayekwenda kwa jina la Malkia Nothando Dube huyu ndiye aliyepata kashfa |
|
|
Hapa ni wakati wakiwa katika amani ya kweli kabla ya kashfa. |
|
Mfalme akiwa na Malkia na kulia kwako ndiye waziri aliyefumaniwa na walinzi wa mfalme |
|
Add caption | | | | | |
|
Hawa ni wake wa Mfalme Mswati III |
|
Add caption |
|
Wakati tunapowanyooshea vidole watu wa ulaya kuhusu suala
la utamaduni wao je? ni kweli kwamba huku kwetu Afrika tuko salama sana
kiasi cha kuwalaumu wengine, kwa uchache tuangalie picha za mabinti
mabikira waliochaguliwa na kuandaliwa maalumu kupita mbele ya mfalme ili
achague mmoja wao hii hufanyika kila mwaka mara moja.
MATATIZO KWA WAKE WA MFALME MSWATI III |
TANGU Waziri wa
Haki wa Swaziland, Ndumiso Mamba, anaswe na mke wa Mfalme wa nchi hiyo,
Makhosetive Dlamini ‘Mfalme Mswati III’, hali ni mbaya kwa wake wa kiongozi
huyo.
Mamba, alinaswa kwenye kitanda cha mke wa 13 wa
mfalme huyo, Nothando Dube na tangu wakati huo, walinzi wa Mfalme Mswati,
wamepewa madaraka makubwa ikiwemo kuwacharaza bakora hata barabarani na mbele
za watu.
Inaelezwa kwamba wake wa Mfalme Mswati
wanafungiwa ndani kama kuku, inapotokea wanakwenda sehemu wanakuwa chini ya
ulinzi mkali.
Ripoti zinasema kuwa endapo barabarani mke wa
mfalme atachepuka kwenda hata msalani bila taarifa au atasalimiana na mtu
ambaye walinzi wanamjua, hata kama ni ndugu yake, mwanamke husika hucharazwa
bakora kama ng’ombe.
“Ukiwa mke wa Mfalme Mswati ni mateso makubwa.
Unavyoishi haina tofauti na ng’ombe anavyochungwa. Ukiwa unatembea barabarani
unatakiwa ufuate uelekeo anaotaka bodigadi, ukikosea kidogo unachapwa bakora na
vIrungu.
“Mambo yalikuwa mabaya lakini sasa ni
mabaya mno. Kwa sasa nataka kutoka lakini mfalme hataki kuruhusu niondoke. Nipo
kama mfungwa, saa 24 nachungwa, sina uhuru hata kidogo,” alisema Nothando.
Mwanaharakati wa demokrasia anayepingana na
mtindo wa maisha ya Mfalme Mswati, Lucky Lukhele, aliwahi kuwaambia waandishi
wa habari kwamba siyo Nothando tu, wake wake wote wa kiongozi huyo wanaishi
katika mazingira magumu afadhali ya wafungwa.
“Kuna mke mmoja wa mfalme alikutwa getini na
walinzi, tena getini kwenyewe kwa ndani halafu geti lilikuwa limefungwa na
funguo wanazo walinzi. Ajabu ni kwamba walinzi walipomkuta pale hawakuuliza
mara mbili, walimpiga na kumuumiza mno,” alisema Lukhele bila kutaja jina la
mke huyo wa mfalme.
Kwa upande mwingine, inaelezwa kuwa mtindo wa
maisha ya Mfalme Mswati na wakeze, umesababisha mpaka sasa akimbiwe na wanawake
watatu.
Mke wa sita wa mfalme huyo, Angela “LaGija”
Dlamini, ndiye anatajwa kuwa mwanamke wa hivi karibuni zaidi kuondoka katika
himaya ya mfalme huyo.
Mke wa 12 wa mfalme, Inkhosikati LaDube,
alitimuliwa Desemba mwaka jana kwa kile kilichobainishwa kwamba aligombana na
bodigadi wake.
Taasisi ya Swaziland Solidarity Network ilieleza
kwamba Dlamini, alikimbia makazi ya mfalme baada ya kuwa kwenye mateso kwa
miaka kadhaa.
Dlamini, aliaga anakwenda kuwasalimia wazazi
wake kwenye Mji wa Hhohho, lakini aliporuhusiwa alitimka jumla.
Mfalme Mswati pamoja na tabia ya kupenda kuoa
mabikra, vilevile anatuhumiwa kujilimbikizia utajiri wa kutisha, hivi karibuni
Jarida la Forbes lilimtaja kwamba anamiliki utajiri wenye thamani ya zaidi ya
dola milioni 200 (shilingi bilioni 300).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni