VITA VYA KIROHO : SEHEMU YA KWANZA
Biblia inasema.
10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
11 Vaeni silaha zote za Mungu,mpate kuweza kuzipinga hila za shetani
12 kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya
falme na mamlaka,juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya
katika ulimwengu wa roho.
13 kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu,mpate kuweza kushindana siku
ya uovu,na mkiisha kuyatimia yote kusimama.
14 Basi simameni hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa darii ya haki
kifuani,
15 nakufungiwa miguu utayari wa injili ya amani.
16 Zaidi ya yote mkitwaa ngao ya imani ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima
mishale yote yenye moto ya Yule mwovu
17 tena ipokeeni chepeo ya wokovu, na upanga wa roho ambao ni neno la
Mungu
18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati
katika roho.
Ili tuwe kulewa vizuri na kwa urahisi somo
hili ni muhimu kuanza na mistari hii ya Biblia ili kujenga msingi wa somo hili.
Tunasoma hapa mtume Paulo anawaelezea Waefeso
aina ya vita tunayopigana na namna ambavyo tunatakiwa kupigana kwa mbinu, maana
vita si lelemama kwa hiyo ili tuweze kushinda tunahitaji kujifunza mbinu za
kivita. Maisha ya wokovu sio maisha mepesi kama tunavyoaminishwa na baadhi ya
wainjilisti kwamba kwa Yesu ni tambarare, hiyo sio kweli ukishaambiwa kuna vita
na unatakiwa kupigana basi ni lazima ujue kwamba wewe sio raia bali ni askari.
Na kwa kawaida askari ni raia aliyepewa mafunzo maalumu ya kupigana vita kwa
kutumia zana mbalimbali za kivita. Ndio maana inakuwa muhimu sana kujifunza
aina ya vita na mbinu ambazo zitatusaidia kupata ushindi. katika mstari wa 12 Mtume
Paulo anasema
12 kwa maana
kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka,
juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Katika mstari huu Biblia inatujulisha kuhusu
aina ya vita tunayopigana, tunapigana na nani, lakini pia ametufahamisha kuhusu
aina mbili za ulimwengu, kwamba kumbe kuna ulimwengu wa damu na nyama ambao
ndio dunia hii ambayo sisi tunayoishi.
Lakini pia kuna ulimwengu wa roho ambao sisi
kwa macho na kwa akili za kawaida hatuwezi kuuona wala viumbe vinavyokaa katika
ulimwengu huo hatuwezi kuviona katika macho ya kawaida, ulimwengu huo ndio ambao
nataka tuuangalie kwa undani.
Inawezekana tukawa tunajua mambo machache
kuhusu ulimwengu wa roho, lakini kwa uchache ulimwengu wa roho ndio ulimwengu
halisi na dunia ni kivuli cha ulimwengu wa roho, ulimwengu huo ulikuwepo kabla
ya dunia kuwepo na Mungu wakati anaiumba hii dunia alikuwa anaiumba akiwa
katika ulimwengu wa roho.
Kwa kifupi ni kwamba ulimwengu wa roho ndio
wenye nguvu kubwa sana kiasi cha kwamba dunia yetu pamoja na uzito wake wa
mabilioni ya tani imeshikwa na nguvu kidogo sana kutoka katika ulimwengu wa
roho, na inajizungusha yenyewe kwa masaa ishirini na nne kupata usiku na
mchana. Lakini pia inalizunguka jua kwa siku 365 au 366 ili kupata mwaka bila
kupoteza majira na mwelekeo wake. Watu wanaosoma elimu ya unajimu wanajua
kwamba nguvu iliyoko katika ulimwengu wa roho inatawala maisha ya wanadamu
walioko katika dunia hii tunayoishi.
Tangu
zamani, wanadamu wamechunguza miendo hususa ya nyota na sayari katika mbingu za
usiku na pia mahali tofauti-tofauti ambapo nyota na sayari hizo zinakuwa
kulingana na majira.
Mungu akasema, na iwe mianga katika anga la mbingu ili
itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndio dalili na majira na siku na
miaka; (Mwanzo 1:14)
Hata hivyo,
iwe tunajua au hatujui, mienendo ya nyota na sayari ina uvutano wa moja kwa
moja katika maisha yetu. Dunia huzunguka jua ambalo ni nyota inayotusaidia
kujua urefu wa siku na mwaka. Mwezi ni “kwa ajili ya nyakati zilizowekwa,” au
‘kutupimia majira.
’ Aliufanya mwezi kwa ajili ya nyakati, jua
latambua kuchwa kwake
(Zaburi 104:19;
Nazo nyota
ni mwongozo unaotegemeka katika usafiri, na hata wanaanga wanaweza kutumia
nyota wanapoongoza vyombo vyao vya angani. Kwa hiyo, wengi wangependa kujua kama
nyota zinaweza kufanya mengi zaidi ya kutuonyesha wakati na majira, na
kutusaidia tuthamini kazi za uumbaji za Mungu.
Je, nyota zinaweza
kutusaidia kujua wakati ujao au kutuonya kuhusu majanga na misiba? Najaribu
kukuchambulia nguvu ambayo iko katika ulimwengu wa roho.
Unajimu,
ambao ni mazoea ya kutazama mbingu ili kutafuta ishara za kuongoza maisha yetu
duniani, ulianzia Mesopotamia ya kale, yaelekea katika miaka ya
2000 K.W.K. Wanajimu wa kale walitazama mbingu kwa makini.
Elimu ya
nyota ilianzishwa na juhudi zao za kuchora miendo ya nyota na sayari, kujua
mahali kila nyota ilipo, kutengeneza kalenda na kutabiri kupatwa kwa jua au
mwezi. Lakini wanajimu hawachunguzi tu uvutano wa mwezi na jua katika mazingira
yetu. Wanajimu wanadai kwamba mpangilio wa jua, mwezi, sayari, nyota, na
makundi ya nyota, una uvutano juu ya matukio makuu duniani na pia juu ya maisha
ya kila mtu.
Wanajimu
fulani wanatazama nyota na sayari ili wajue mambo au hatari za wakati ujao. Na watu wanaouelewa
wanaweza kuutumia ujuzi huo na kunufaika nao kwa njia mbalimbali. Wengine
wanahisi kuwa unajimu unaonyesha kile ambacho kimeamuliwa mapema tufanye.
Sasa
kwa sababu hiyo mtume Paulo anatuonya kwamba tusijaribu kushindana katika mwili maana
kwa kufanya hivyo tunakuwa tumechelewa, kwa sababu mambo yote yanakuwa tayari
yameshaamriwa katika ulimwengu wa roho na ni mpaka ujue namna ya kuingia katika
ulimwengu wa roho na kupata habari hapo ndio unaweza kushindana.
ninayo mambo
mengi sana ya kushuhudia jinsi mambo ambayo niliyaona mapema katika ulimwengu
wa roho yalikuja kutimia baada ya majuma au miezi kadhaa.
Watu
wasiomjua Mungu unajimu unaweza kuwasaidia kujua wakati unaofaa wa kushiriki
katika utendaji fulani au kuanza kufanya mambo fulani.
Inasemekana kwamba
habari hizi zinaweza kujulikana kwa kutazama mpangilio wa nyota au sayari
fulani na kuchunguza uhusiano kati ya nyota na sayari hizo na pia uhusiano wake
na dunia.
Inasemekana kuwa uvutano wa nyota na sayari juu ya maisha ya mtu
binafsi unategemea mpangilio wake wakati wa kuzaliwa kwa mtu huyo.
Wanajimu wa
kale walifikiri kuwa dunia ndiyo kitovu cha ulimwengu, na kwamba sayari na
nyota zilikuwa zimefungiwa katika miviringo ya kimbingu ambayo iliizunguka
dunia.
Pia walifikiri kwamba jua linasafiri angani kati ya makundi ya nyota
likifuata njia fulani hususa katika mzunguko wa kila mwaka.
Waliigawanya
njia hii ya jua ya kila mwaka katika sehemu au maeneo 12. Sehemu hizo zote
zilikuwa na makundi ya nyota, na kila sehemu ilipewa jina kulingana na kundi la
nyota ambamo jua lilipitia.
Sehemu hizo
zikawa zile ishara 12 za nyota na kuitwa “nyumba za mbinguni,” kwa sababu
zilionwa kuwa makao ya miungu. Hata hivyo, wanasayansi waligundua baadaye kuwa
jua haliizunguki dunia bali dunia ndiyo inayozunguka jua. Uvumbuzi huo
ulithibitisha kuwa unajimu si sayansi yenye kutegemeka.
Kutoka
Mesopotamia ulikoanzia, unajimu ulienea hadi karibu sehemu zote za dunia na
ukatumiwa kwa njia moja au nyingine katika maeneo yote yenye ustaarabu mkubwa
duniani. Baada ya Uajemi kushinda Babiloni, unajimu ulienea hadi Misri,
Ugiriki, na India.
Kutoka India, wamishonari Wabudha waliueneza hadi Asia ya
Kati, China, Tibet, Japani, na Asia ya Kusini-Mashariki. Yaonekana kuwa unajimu
uliopo leo ulianzishwa huko Misri wakati wa utawala wa Ugiriki, na umeathiri
sana maoni ya Wayahudi, Waislamu, na watu wa dini zinazojidai kuwa za Kikristo.
Bado hata sasa katika nchi nyingi watu
hawatoki majumbani kwao bila kujua nyota yake inasemaje kuhusu siku hiyo, kwa
hiyo ni lazima wapate magazeti yenye kurasa maalumu za watabiri wa nyota.
Wakati wa
utawala wa Mfalme Nebukadneza wa Babiloni, makuhani na wanajimu
walishindwa kufasiri ndoto ya mfalme. Danieli, nabii wa Mungu wa kweli, alionyesha
sababu zilizofanya washindwe kufasiri ndoto hiyo aliposema:
“Siri ambayo mfalme anauliza, watu wenye hekima, wala
wafanya-mazingaombwe, wala makuhani wenye kufanya uchawi wala wanajimu hawawezi
kumwonyesha mfalme. Hata hivyo, kuna Mungu mbinguni ambaye Ni Mfunuaji WA siri,
naye amemjulisha Mfalme Nebukadneza mambo yatakayotokea katika siku za mwisho.”
Danieli
alimtumaini Mungu ambaye ni “Mfunuaji wa siri”— bali si jua, mwezi, au nyota—na
akamweleza mfalme maana ya kweli ya ndoto yake.—Danieli 2:36-45.
Kwa maana nyingine ni kwamba
Mamlaka ya Mungu katika ulimwengu wa roho ilikwisha amua juu ya hatma ya ufalme
wa Nebukadneza, kwa hiyo Nebukadneza hata angejitahidi kupambana wakati anguko
lake linatokea angekuwa anapigana katika damu na nyama.
ndipo mtume Paulo
anakataa kwamba hatutakiwi kupigana katika damu na nyama. Ni sawa na kwamba tumesha chelewa.
Neno la
Mungu linafunua wazi kwamba ‘matendo yenye nguvu na ishara za uwongo na mambo
ya ajabu,’ ni “utendaji wa Shetani.”—2 Wathesalonike 2:9.
Kama vile
ambavyo kuvuta bangi kunaweza kumfanya mtu awe mtumwa wa walanguzi wa dawa za
kulevya, kujihusisha na unajimu kunaweza kumfanya mtu atawaliwe na yule
mdanganyifu mkuu, Shetani.
Hivyo basi, wale wanaompenda Mungu na kweli,
wanapaswa kuukataa kabisa unajimu na badala yake kutii shauri hili la Biblia:
“Chukieni yaliyo mabaya, pendeni yaliyo mema.”—Amosi 5:15.
Unajimu
umeenea sana kwa sababu watu wanatamani kujua mambo ya wakati ujao. Je,
inawezekana kujua mambo hayo? Ikiwa ndivyo, tunaweza kuyajua jinsi gani? Biblia
inasema kwamba hatuwezi kujua ni nini ambacho kitampata kila mmoja wetu kesho,
mwezi ujao, au mwaka ujao. (Yakobo 4:14)
Hata hivyo,
Biblia inatufunulia mambo ambayo yatawapata wanadamu kwa ujumla wakati ujao.
Inatuambia kwamba karibuni, Ufalme utakuja, kama tunavyoomba katika Sala ya
Bwana.
Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni
atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa
enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu nao
utasimama milele na milele
Basi ninyi
salini hivi: Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe,ufalme wako
uje,mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni.
Pia
inatuambia kwamba kuteseka kwa binadamu kutaisha hivi karibuni na hatutasumbuka
tena.
Maana
tazama, mimi naumba mbingu mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala
hayataingia moyoni.
(Isaya 65:17;
tutaendelea 0713 461593
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni