JINSI YA KUIMBA
Zab 150:1-6, 33:1-3, 98:1-9, 100:1-4
Maandiko haya yanatuelekeza jinsi ya kumwabudu Mungu kwa
vifaa mbalimbali vinavyotumika katika muziki, ikiwa ni pamoja na hali ya mtu
anayeabudu inavyotakiwa kuwa. Huduma ya muziki wa kikristo ni muhimu iwe na
mwelekeo wa kibiblia mifumo na malengo pamoja na utekelezaji wake lazima
upatikane ndani ya maandiko matakatifu.
- Kwa maana lolote tulifanyalo tunalifanya kama kwa Bwana.
Basi kama ni hivyo tuyaangalie maandiko mbalimbali:
“Tumwimbie Bwana wimbo mpya,
tumshangilie, tumpe shangwe, na sifa, shukrani, furaha, faraja na kumtukuza,
vigelegele na kucheza”. (Zab 98:1)
- Mambo haya ni sehemu ya muziki wa kikristo na wa kiroho.
- Ni muhimu na lazima tuimbe kwa ustadi na kwa ubora, kwa ari kubwa na
shauku, kwa kupania bila kujibakiza wala kujihurumia, hii ni kazi nzito sana.
“Akawaagiza baadhi ya walawi kwamba watumike mbele ya
sanduku la BWANA, wamfanyie ukumbusho, na shukrani, na sifa, BWANA, Mungu wa
Israeli Asafu mkuu wao, na wa pili wake Zekaria, na Yeieli, Shemiramothi, na Yehieli,
na Matithiya, na Eliabu, na Benaya, na Obed –edomu na Yeieli, wenye vinanda na
vinubi; naye Asafu mwenye kupiga matoazi; nao makuhani Benaya na Yahazieli wenye
baragumu daima, mbele ya sanduku la Agano la Mungu…………….(I Nyak 16:4-11,
23-34)
- Hapa tunaona uimbaji ni huduma ya makuhani
- hii ndiyo ofisi ya mwimbaji ni kuhani wa Mungu afukizaye
uvumba mbele ya madhabahu kwa sadaka za sifa na shukrani, (INyak 6:31)
- tunaona Walawi waliimba kwa utaratibu ulioeleweka (INyak
16:4-11, 23:35)
- Waliimba kwa zamu, walikaa kwa mtindo wa kueleweka wakati
wa huduma.
- Walijifunza kwa waalimu wao kwa bidii. walitabiri kwa kinubi, waimbaji ni manabii
wanatabiri kwa vinanda wanavyovipiga kwa ustadi. (1Nyak 25:1-9)
HALI YA MOYO NA JINSI YA KUTUMIKA
Mungu ndiye anatoa karama na huduma hii, basi ni lazima
watumishi waishi maisha matakatifu na moyo safi. Na unyofu wa moyo yaani mwenendo
wenye tabia njema. hilo halikwepeki, wakiwa wamejitakasa mwili na roho, Ibada ni tendo la kumcha Mungu. IIKor 7:1 Amos 5:21
Yatupasa kumwimbia Mungu tukiwa na vifaa vya muziki au
vyombo vya muziki. Accompanyments au vikolezo.
Maandiko yanakazia sana kuimba pamoja na vyombo vinubi,
vinanda, zeze la nyuzi kumi, filimbi na matari,
Mungu wetu ni mpenzi wa muziki kuliko mfalme yoyote wa
duniani. Ili ibada ya sifa na kuabudu ikamilike, muziki wa vyombo ni muhimu,
bila kusahau mfumo, mtindo na utaratibu mzuri.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni