Ali
Ali ni mkubwa kati ya watoto tisa lakini
hana kumbukumbu yoyote nzuri ya kuwa miongoni mwa familia kubwa hivyo. Walikuwa
wakimtania na kumwambia kuwa alikuwa hafanani na mtu yeyote katika familia
yake. Mama yake alisema kuwa alikuwa akimchukia na kwamba alikuwa ni mtoto
ambaye amefanana naye kidogo sana. Kila siku Ali alijihisi kukataliwa na
familia yake na hivyo alipokuwa mtoto alilia sana.
Kwa muda wa miezi minne kila mwaka, Ali
alifanya kazi ya kuchunga kondoo. Alianza kazi hiyo alipokuwa na umri wa miaka
nane na kuendelea na kazi hiyo hadi alipofikia umri wa miaka kumi na nane.
Aliwapeleka kondoo milimani na kwa vile alitumia muda mwingi peke yake
alihitaji mtu mwingine wa kuongea naye “alijitengenezea mungu“ moyoni mwake.
Mungu huyu alikuwa kama rafiki yake. Angeweza kuongea naye kwa mazungumzo
marefu kama vile:“ni vizuri kama nini viumbe vyako ulivyoviumba,“
alipoyaangalia maua, jua, miamba na nyasi. Pengine angeweza kumwuliza huyo
mungu swali hili: „Je, utamu wa tunda la apple unatokana na nini?“ Maana
aliamini kuwa kulikuwa na Mungu aliyetengeneza au kuviumba vitu vyote vizuri.
Alipokuwa na umri wa miaka ishirini,
alianza kunywa pombe sana. Na alipofikia miaka ishirini na mitano alikuwa mlevi
wa kupindukia. Wakati mwingine alianza kunywa kabla hata ya saa tatu asubuhi!
Aliporudi nyumbani mkewe mara nyingi alikuwa akimwuliza endapo ametoka kunywa
pombe. Jambo hili lilimkasirisha mno na kwa hiyo akaanza kumpiga kila siku.
Watoto wake walishuhudia manyanyaso hayo na walikuwa na hofu kurudi nyumbani
baada ya kutoka shule, kwa hiyo walienda kwenye nyumba za marafiki zao mpaka
walipojua kuwa baba yao ameshalala. Ali alitaka sana kuacha kunywa pombe na
alichukia sana kwa jinsi alivyokuwa akimnyanyasa mkewe. Hivyo aliamua kuhamia
Saudi Arabia ili kufanya kazi kama mkandarasi (fundi mwashi) kwa sababu alikuwa
amesikia kuwa ulevi ni kitu kilichokuwa kimekatazwa kisheria. Hata hivyo usiku
wa kwanza alipokuwa Saudi Arabia aliona kilevi na akanywa.
Pamoja na kwamba Ali hakuwa ni mtu wa dini,
familia yake walisema kuwa ni waislamu lakini hawakujua zaidi kuhusu dini yao.
Ali aliamua kwenda Mekka, akitumaini kuwa kwa kutembelea kule kungeweza
kumfanya huru kutokana na shida yake ya ulevi. Alisema: „Nilifanya maamuzi
moyoni mwangu. Ninaenda kufanya hija ya kweli. Nitakuwa mwislamu halisi na
nitaacha kabisa kunywa pombe.“ Usiku ule ule wa kwanza alipokuwa Mekka, Ali
aliota ndoto. Katika ndoto ile, alimwona Yesu akishika mkono wake na kumwambia:
„Wewe ni wangu.“ Pia aliweka kidole chake kwenye paji la uso la Ali na kusema:
“Unahitaji kutoka mahali hapa na kuondoka sasa.” Ali alipoamka alihisi kama
alikuwa akielea hivyo akaligusa zulia lake kuhakikisha kuwa alikuwa kwenye nchi
kavu. Aliendelea kuisikia sauti ya Yesu ikisema: „Unahitaji kufuatana nami,
wewe ni wangu.“ Marafiki zake Ali waliona alama iliyokuwa iking’aa katika paji
lake la uso mahali pale ambapo Yesu mwenyewe alikuwa amemgusa, lakini yeye
mwenyewe Ali alipojitazama kwenye kioo hakuona chochote. (Alama hii kwenye paji
lake ilionekana kama vile „sim,“ aina ya mng’ao ambao hutumika kwa kuwapamba
mabibiarusi wa kituruki.)
Ali aliendelea na hija yake. Hata hivyo
gari lake alilokuwa nalo kwa mwezi mmoja hivi, liligoma kuwaka ili lianze
kutembea. Aliendelea kuisikia sauti ya Yesu: „Unahitaji kuondoka hapa.“ Mara tu
alipobadilisha mawazo yake na kuondoka pale Mekka, gari lake liliwaka na kuanza
kutembea! Alienda nyumbani kwenye chumba chake alichokuwa amepanga na akasikia
sauti ile ile tena. Hapa Bwana Yesu alimwambia kuwa anatakiwa aende Uturuki.
Baada ya siku tatu alikuwa Uturuki kwenye sherehe ya „kumkaribisha nyumbani“.
Hapo tena akasikia sauti. Wakati huu Yesu alimwambia kuwa awaambie watu wote
waliokuwepo pale kuwa, yeye amekuwa Mkristo sasa. Alifanya hivyo, lakini watu
hawakutilia maanani juu ya jambo lile la kuokoka.
Hakujua hilo mpaka baada ya miaka michache
baada ya ile ndoto ndipo Ali alipoanza kufahamu ina maana gani kuwa Mkristo
aliyeokoka. Alikuwa akisikiliza redio aliposikia sauti ikisema: „Yesu alikufa,
akafufuka kutoka kwa wafu baada ya siku tatu na sasa anakaa mkono wa kuume wa
baba.“ Alimwita mkewe na kumwambia kwamba ameshaipata sauti ya Yesu – ndani ya
redio. Kupitia kipindi hicho katika redio, alipokea masomo ya Biblia na pia alipokea
Agano Jipya mpya! Alikuwa na umri wa miaka 38 wakati ule na alisema kuwa siku
aliyopokea Agano Jipya lile kwa njia ya posta “pengine ilikuwa ni siku ya
furaha kubwa maishani mwake kuliko siku yoyote.” Baada ya kumaliza baadhi ya
masomo kwa njia ya posta, Ali pamoja na familia yake walihamia Istanbul ili
kuweza kusoma shule ya Biblia.
Mpaka leo anaendelea kushuhudia imani yake
ya kikristo kwa uwazi na hata bila ya aibu. Ulevi haukuendelea tena kumtawala,
na akawa akimtunza na kumpenda mkewe ambaye hapo kwanza alikuwa akimtenda
vibaya. Kweli, sasa amekuwa ‚kiumbe kipya ndani ya Kristo.‘
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni