Usijaribu kushindana
katika mwili
Ukitaka
kupata maana nzuri ya maombi ni vizuri na muhimu kusoma Biblia katika waraka wa
mtume Paulo kwa waefeso 6.12 anasema kushindana kwetu sisi si juu ya damu na
nyama,bali ni juu ya falme na mamlaka juu ya wakuu wa giza hili,juu ya majeshi
ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Mstari huu pamoja na kutueleza ugumu
wa mapambano lakini pia umeugawa ulimwengu katika sehemu kuu mbili ambazo ni
ulimwengu wa damu na nyama na ulimwengu war oho.,.ulimwengu wa damu na nyama ndio
huu ulimwengu tunaoishi ambao tunaona kila kitu kwa macho na ambao tumefungwa
na mwili kuoweweza kufahamu mambo mengine ambayo yapo nje ya upeo wa macho
yetu. Na ulimwengu wa roho ni ulimwengu ambao upo lakini.
hauonekani kwa macho
lakini ni ulimwengu kamili wenye kila kitu na viumbe ambavyo sisi hatuwezi
kuviona ila vyenyewe vinaweza kutuona sisi. Katika sehemu hizi mbili za
ulimwengu ulimwengu wenye nguvu sana ni ulimwengu wa roho. Mungu na shetani
wanaishi katika ulimwengu wa roho,na wakati Mungu anaumba ulimwengu huu Mungu
alikuwa anaumba kutokea katika ulimwengu wa Roho,ulimwengu war oho ndio wenye
kuamua mambo yote yanayotokea kaika
dunia hii. Hakuna jambo linalokuja duniani bila kwanza kujadiliwa katika
ulimwengu war oho ndio maana katika Biblia huwezi kuona neno bahati mbaya labda bikira akachukua mimba
akazaa mtotoo mwanamume, utaona neno likisisitizia kwamba kama ilivyoandikwa na
nabii Fulani. Kwa sababu hiyo ndio maana mtume Paulo anatushauri kuwa
tunapopambana katika vita ya kiroho usipambane katika hali ya ulimwengu wa damu
na nyama,bali anza kushindana katika
ulimwengu war oho amabko ndiko mipango na
vikao vyote vya kukumaliza vinakaa huko. Mambo ya kiroho tunapambana nayo
kiroho na wala si kiakili,ukijaribu kupambana kiakili unakuwa umechelewa.
Unaposhindana katika damu na nyama ni sawa na kushindana na matokeo inabidi tu
uwe mpole kwa sababu unakuwa umechelewa na unaweza kupata shida zaidi kama
ukihamaki. Ulimwegu war oho ndio wenye nguvu kubwa sana na ndio wenye uamua
nani afe na lini na sababu ya kifo chake iwe nini, kama ni ajali ya kugongwa na
gari utaona mtu ameshavuka barabara lakini tena anarudi na kugongwa. Hiyo ni
kwa sababu iliandikwa afe kifo hicho katika muda na saa hiyohiyo iliyotokea
ajali. Dunia yetu pamoja na uzito wake wote
imeshikiliwa na nguvu ndogo sana katika ulimwengu wa roho ambao
unaizungusha bila kupoteza majira wala nyakati na inajizungusha kwenye mhimili
wake bila kupoteza njia wala kugongana na sayari nyingine. Lakini kama Biblia
inavyosema kwamba katika ulimwengu huu wana wa dunia wana hekima kuliko wana wa
nuru wana wa nur baada ya kumpokea Yesu wanaridhika haraka sana. Hawataki tena
kujifunza au kutafuta mambo zaidi ya rohoni,wanaridhika na ahadi kwamba
wanalindwa na malaika. Tofauti na wana wa giza
wao wamejua kwamba ipo nguvu kubwa ya asili ambayo inaitawala dunia,na
wamejifunza sana namna ya kuitumia nguvu
hii kwa manufaa yao. Nguvu hii ya asili inatawala maisha ya wanadamu wote
wanaoishi hapa duniani kasoro
waliookoka peke yao Paulo anasema sisi hatuishi
kwa kufuata taratibu za dunia hii. Wana wa dunia wamejifunza kwamba hii nguvu ya asili katika ulimwengu war oho
imegawanyika katika sehemu kumi na mbili 12. Sehemu hizi wamzigawa kulingana na
tarehe ya kuzaliwa mtu zinaitwa nyota na wamezipa majina hebu angalia mfano huu
disemba 22
Feb 18 Mbuzi Capricon
januari 20
feb
ukweli ni
kwamba ukiondoa watu waliookoka watu wengine wote watake wasitake nyota hizi
hutawala maisha yao ya kila siku na zina nguvu kweli. Watu wanaokwenda kutafuta
usaidizi kwa wachawi huangalia kwanza nyota zao. Ndio maana ukifika kwa wachawi
wanaoagua anaweza kukutajia shida yako hata bila yaw ewe mwenyewe kumueleza ni
kwa sababu anajua watu waliozaliwa tarehe Fulani wako katika kundi la nyota
Fulani na watu wa kundi hili kwa kipindi hiki wanasumbuliwa na shida Fulani ama
katika biashara,kazini,familia n.k. na wanajua ili wafanikiwe wanatakiwa
wafanye nini kama una kesi mahakamani na wewe ni mtuhumiwa na akijua tarehe
ambayo mtasimama mahakamani ataangalia kati ya nyota yako nay a anayekutuhumu
ni ya nani iko juu.na kama ya kwako iko juu atakwambia nenda hata kama mdai
wako ana haki lakini atajichanganya na anaweza akashindwa hata kujibu maswali
yako
hekima ya
wana wa dunia wanajua kuwa ili ufanikiwe katika mambo yako katika dunia ni
lazima upatatane na mtawala wa dunia na kwamba huwezi kufanikiwa mambo ya
kidunia bila ya kupatana na mtawala. Ili mambo yako yawe mazuri katika nchi hii
ya Tanzania ni lazima uwe na uhusiano mzuri na watawala wan chi na ukitaka
upate shida aza kupingana na Serikali. Biblia inatueleza katika Mwanzo 1.26
Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu,kwa sura yetu,wakatawale samaki wa
baharini na ndege wa angani na wanyama… Mungu aliiumba dunia na kumbabidhi
Adamu aitawale lakini tunafahamu pia kwamba Adamu aliipoteza haki ya kuitawala
dunia kwa kuitoa kwa hiari yake na kumpa shetani tangu wakati huo ili mtu wa
dunia afanikiwe ni lazima kwanza aende kwa shetani kuomba msaada.na shetani
vile hana adabu ukienda kwake yeye anataka kusujudiwa tu kama alivyomwambia Bwana Yesu kule
jangwani watu wa dunia hii wanamsujudia shetani kwa namna nyingi sana. Wapo
wanaozini na wanyama ,maiti n.k. Mungu wetu ni Mungu wa haki na anatupenda sana
hakubishana na shetani juuya utawala wa dunia
alijua kwamba shetani ana haki ya
kuuchukua utawala wa dunia. Kwa sababu Mungu alitoa maelekezo kwa Adamu na
masharti ya mti waliokula Adamu alikuwa
na hiari ya kukubali au kukataa kwa sababu Mungu wetu ni Mungu wa haki ilibidi
ashuke tena duniani kwa mfano wa mwanadamu na kuja kukaa na wanadamu miaka 33
kati ya miaka hiyo alitumia miaka 30 kuizowea dunia na mazingira yake,miaka
mitatu ya kutufundisha mbinu ya kumnyaganya shetani haki ya kuitawala
dunia na baada ya kukamilisha kazi yote
alitupa mamlaka ya kukanyaga nguvu zote za shetani wakati wote
unapokuwa umesimama
kwenye mamlaka Mungu anakuwa nyuma yako kutekeleza kile unachokisema au
unachokiamrisha. Ndio maana anasema kabla hujaomba yeye anajua yote lakini
anataka bado tutamke neno. Maana yake tunapomwambia mgonjwa apone Mungu anamwambia shetani apishe maana Mungu anatambua kuwa
sisi ndio tunaotawala dunia.