Dunia inapita katika kipindi cha mabadiliko makubwa Sana katika Nyanja ya sayansi na teknolojia. Kasi ambayo dunia inakwenda ni kubwa sana kuliko tunavyofikiri, Na inagusa karibu katika nyanja zote za maisha ya kila siku ya binadamu ikiwemo hata na ndani ya kanisa.
Biblia inaposema kwamba katika nyakati za mwisho maarifa ya wanadamu yataongezeka,watu wengi hudhani kwamba kanisa halitahusika na mabadiliko hayo lakini ukweli ni kwamba kanisa ni mdau wa mabadiliko na kamwe haliwezi kujitenga na mabadiliko yanayotokea duniani kisayansi,kiutamaduni,kijamii n.k.
Mara nyingine wakati nchi yetu ambayo iko katika
kundi la nchi zilizoko katika dunia ya tatu inapojiandaa kuingia katika
mabadiliko fulani ambayo nchi zilizoendelea na zinazoendelea imefikia, inakuta
dunia ya kwanza na ya pili zimeshahama huko na kwenda hatua ya mbali zaidi.
Hali hii imesababisha kanisa kuburuzwa na
mabadiliko haya na kuwa kama mchezaji
mlalamishi katika uwanja wenye mabadiliko ya sheria na kanuni za mchezo wa
maisha katika jamii. Wenzetu walioipigania injili walijitahidi sana kujaribu
kupingana na mabadiliko haya yasiingie ndani ya kanisa lakini walishindwa hii
ni kwa sababu waliotuletea dini hizi walileta bia na utamaduni wao ambao wao
wanauita ustaarabu na ndio maana dini za kikrito waliotuletea dini hii walitoka
ulaya na ndio waliotuletea ustaarabu wa kuvaa suruali na mashati na wakati
unahubiri ni vizuri uvae koti japo na tai tofauti na walioleta dini ya kiislamu
ambao wanatoka mashariki ya kati na ambao vazi lao la heshima
ni kanzu na vinginevyo hawakuelewi. Mtumishi mmoja aliniambia kwamba zamani ilikuwa ni marufuku hata kutumia gitaa kwenye ibada, ile kukubali tu kutumia magitali ndani ya kanisa lao ilikuwa ni mjadala mgumu sana na hata ilipokubaliwa walikuwa na aina ya mapigo waliyotakiwa kupiga. siku moja walipiga wimbo mmoja kwa mtindo wa regae ya Jamaika ambayo kwa wakati huo ilikuwa inavuma sana miaka hiyo ya 1970. Baada ya ibada kwisha kwaya nzima walisimamishwa na wengine wakatengwa. Lakini siku hizi hakuna kitu kama hicho na kanisa kama halina magitaa watu ni vigumu sana kuhisi kama kweli wameabudu. Hapo tunaweza kusema utandawazi umeingia mpaka kanisani
.
ni kanzu na vinginevyo hawakuelewi. Mtumishi mmoja aliniambia kwamba zamani ilikuwa ni marufuku hata kutumia gitaa kwenye ibada, ile kukubali tu kutumia magitali ndani ya kanisa lao ilikuwa ni mjadala mgumu sana na hata ilipokubaliwa walikuwa na aina ya mapigo waliyotakiwa kupiga. siku moja walipiga wimbo mmoja kwa mtindo wa regae ya Jamaika ambayo kwa wakati huo ilikuwa inavuma sana miaka hiyo ya 1970. Baada ya ibada kwisha kwaya nzima walisimamishwa na wengine wakatengwa. Lakini siku hizi hakuna kitu kama hicho na kanisa kama halina magitaa watu ni vigumu sana kuhisi kama kweli wameabudu. Hapo tunaweza kusema utandawazi umeingia mpaka kanisani
.
Wengine walijaribu kuzuia kwa kufunga na
kuomba ili kwamba matumizi ya internet yasiingie Tanzania na hata yakiingia
yasiguse kanisani wakiamini kabisa kwamba ni mtandao wa mping Krito lakini
haikuwezekana hatimaye yaliingia na hatimaye wao wenyewe siku hizi wanayatumia
na wanaona yana faida kubwa sana katika kazi ya Mungu na makanisa ambayo
hayatumii mtandao yanajirudisha nyuma na kujiweka katika wakati mgumu kupambana
na mazingira yanayobadilika kila kunapokucha.
Sasa hivi wataalamu wanafikiria kutengeneza
memory card kama zinazotumika kwenye simu kwa ajili ya kuweka na kupata taarifa
za binadamu ambazo zitachomekwa ndani ya
miili ya watu,kama vile walivyokuwa wanapandikiza vijiti katika uzazi wa mpango
ambavyo
Vitawawezesha kila mtu anaposafiri hakutakuwa
na haja ya kuchukua pasiport ila
kutakuwa na mashine maalumu mipakani,kwenye viwanja vya ndege na kwenye ofisi
za uhamiaji ambazo mtu akipita zitasoma taarifa na kumbukumbu zake zote.
Haya ndio maandalizi ya kuifanya dunia kuwa
kijiji kimoja, na kuivunjilia mbali kabisa mipaka ya mataifa. Jambo hili Biblia
ilishaliona na kwa kweli halikwepeki tutake ama tusitake ni lazima hatimaye
dunia itakuwa na kiongozi mmoja. Na tutatumia sarafu moja na watu hawataulizana
juu ya utaifa wa mtu, haya mabadiliko tunayoyaona ya jumuiya za kikanda kama
SADC, ECOWAS n.k. ni maandalizi ya huko tunakoelekea
UTANDAWAZI
NINI MAANA YAKE NA UNA NIA GANI.
Nia kubwa ya utandawazi ni kuvunjilia mbali
mipaka ya nchi na kuifanya dunia hatimaye kuwa kama kijiji kimoja katika nyanja
za elimu, mawasiliano, sayansi na Teknolojia.
Tangu zama za mawe dunia imekuwa ikipita
katika mabadiliko mbalimbali yenye lengo la kumsaidia mwanadamu na
kumrahisishia kukabiliana na maisha yake katika mazingira yake. Mtoto mmoja wa
kizungu alimwambia mtoto mwenzake wa kiafrika ambaye alimuona akihangaika
kujumlisha mahesabu kwa kuandika akiona aibu kutumia kikokoteo cha hesabu
(Caluculator) akamwambia sasa babu zetu walihangaikia nini kubuni chombo hiki
kama hutaki kukitumia, ilikuwa ni wajibu wao kuturahisishia sisi maisha ili na
sisi tuwarahisihie watoto wetu maisha. Na hii nikweli tunajua kwamba binadamu
alianza kusafiri kwa miguu, punda wenye
mikokoteni Na kila siku watu wamekuwa
wakibuni vitu mbalimbali kwa lengo la kurahisisha maisha ya mwanadamu, ndio
maana tunaweza kusema kwamba wale watu waliotajirika sana duniani ni wale
waliobuni vitu ambavyo vilikuja kuwasaidia sana wanadamu kutatua matatizo yao,
fikilia kwa mfano mtu aliyevumbua vyombo vya usafiri kama vile gari, ndege n.k.
Katika karne ya 21 dunia iliingia katika
mabadiliko makubwa Sana pamoja na kwamba watu wengi walihisi kwamba kompyuta
zingeshindwa kuusoma mwaka 2000 kwa sababu mwaka huo haukuingizwa kwenye
kompyuta lakini wataalamu wakabuni kitu kilichojulikana kama Y2K ili kuendeleza na kubuni mambo
mengine makubwa zaidi ambayo kwa kiasi kikubwa yameleta mabadiliko makubwa katika
ulmwengu wa sayansi kwa lengo la kumsaidia mwanadamu kukabiliana na maisha
yake.
Tangu wakati huo teknolojia ya habari na
mawasiliano (Teknohama)
imekuwa ni muhimili mkubwa sana unaobeba mabadiliko haya. Wakati Biblia inatoa
tahadhali kwamba katika nyakati za mwisho maarifa ya wanadamu yataongezeka Sana,
watu waliookoka ndani ya makanisa wanadhani kwamba andiko hilo haliwahusu wao
bali linawahusu watu wa dunia. Matokeo
yake kanisa linajikuta linaburuzwa na mabadiliko ya dunia bila kuwa na
maandalizi ya kimkakati ili kupambana na mabadiliko yanayoletwa na sayansi na
teknolojia kwa sababu hayana budi kuja na ni lazima yaje. Paulo mtumishi wa
Mungu aliwahi kuwaeleza wakorintho kwamba alipowaambia wajitenge na dunia,
hakuwa na maana kwamba waondoke kabisa hapa duniani. Bali aliwataka wajitenge
na tabia za kidunia.
TUNAWEZAJE
KUJITENGANISHA NA TABIA ZA KIDUNIA?
MTINDO WA KUWAZUWIA NA KUWAFUKUZA WATU KANISANI
Hakuna
mwanadamu aliyekufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu na kanisa ni mali ya Bwana
Yesu ni makosa kumfukuza mtu kanisani wakati aliyemfia bado anamuhitaji.
Makanisa Mengine yamefikia hatua ya kuwazuwia
au kuwafukuza watu kuingia kanisani. Cha kusikitisha zaidi ni kwamba watu hao
ni jamii ya watu ambao bado hawajaamini ambao wamewasindikiza ndugu zao kwenda
kwenye maombezi kanisani. Lakini wakifika milangoni wanakuta kuna watu
wamewekwa na kanisa kwa nia ya kuwakagua na wakiwaona labda wamevaa au
wametengeneza nywele saluni, basi wanawalazimisha wafunge vilemba au wavae
kanga na magauni marefu.
Ukifikiria
sana utaona kwamba hapo kuna tatizo kubwa sana na kuna maswali mengi
sana ya kujiuliza na swali la muhimu sana hapo ni kuuliza ni jukumu la nani? Kumsaidia
mtu huyu aweze Kubadilika na kuwa mtu mwenye kiwango cha kufaa kuingia katika
majengo ya kanisa lenu?.
Mtu anapokwenda mashine kusaga nafaka ili
kupata unga akiwa mashine ataona vitu vitatu muhimu. Kwanza ataona kinu hii ni sehemu ambayo
ukifika mashine unaweka nafaka na mara nyingi kuna mtu anayekuwa pale
kuhakikisha zile nafaka zote zinakwenda kwenye mkondo unaotakiwa na kuzielekeza
kwenda sehemu ya pili ambayo ni kwenye mashine yenyewe mortal. Kazi ya mortal ni kuisaga nafaka hii ili iwe unga na
kisha ataona kitu cha tatu ambacho mara
nyingi huwa ni mfano wa bomba ambalo limezungushiwa kitambaa cheupe na sehemu
hii ndiko unakotokea unga safi uliotokana na nafaka iliyosagwa na mortal. Kwa maana hiyo, kama itatokea
nafaka ambayo haikusagwa basi ujue kwamba haikupita katika mortal kwa mfano huu ni kwamba watu wa dunia ni mavuno (nafaka).
Wakristo waliookoka ni sawa na watenda kazi ya kwenda shamba na (kuvuna watu wa dunia na kuwapeleka kwenye kanisa) kuleta nafaka mashine. Wakifika mashine kuna mtu wanayemkabidhi nafaka hizo ili aziweke kwenye kinu, tayari kwa kuzisaga kuwa unga ambapo kwa mfano huu kinu ni kanisa la Mungu ambapo watenda kazi (washirika wa kanisa) kazi yao ni kuleta nafaka mashine na wakifika hapo mashine kuna mtu (Mchungaji), yupo hapo kwa ajili kuziongoza hizo nafaka kuelekea kwenye mortal (Roho Mtakatifu). Kwa hali yoyote nafaka zikifika kwenye kinu haziwezi kubadilika na kuwa unga bila kupita kwenye mortal ambayo ni mafundisho na maisha ya kiroho yanayoletwa na Roho Mtakatifu, na kumbadilisha mtu taratibu hatua kwa hatua.
Wakristo waliookoka ni sawa na watenda kazi ya kwenda shamba na (kuvuna watu wa dunia na kuwapeleka kwenye kanisa) kuleta nafaka mashine. Wakifika mashine kuna mtu wanayemkabidhi nafaka hizo ili aziweke kwenye kinu, tayari kwa kuzisaga kuwa unga ambapo kwa mfano huu kinu ni kanisa la Mungu ambapo watenda kazi (washirika wa kanisa) kazi yao ni kuleta nafaka mashine na wakifika hapo mashine kuna mtu (Mchungaji), yupo hapo kwa ajili kuziongoza hizo nafaka kuelekea kwenye mortal (Roho Mtakatifu). Kwa hali yoyote nafaka zikifika kwenye kinu haziwezi kubadilika na kuwa unga bila kupita kwenye mortal ambayo ni mafundisho na maisha ya kiroho yanayoletwa na Roho Mtakatifu, na kumbadilisha mtu taratibu hatua kwa hatua.
Kwa kutokulijua hili au kwa ghiliba za
shetani, watenda kazi wasiokuwa na ujuzi wa vita vya kiroho badala ya kufurahia
na kushukuru Mungu kwamba mavuno yamekuja yenyewe kwenye kinu bila
kuyafuatilia. Badala ya kutulia na hao watu na kuwaelekeza kwenye kinu kwa
upole na upendo mwingi.
Wao wanataka watu hao wageuke unga ghafla bila kupitia kwenye mortal kitu ambacho kwa kweli hakiwezekani. Nafaka ikiwa kwenye kinu hata ukemee mpaka Mapovu ya damu yakutoke, Nafaka bila kupita kwenye mortal haiwezi kugeuka na kuwa unga. Hata kama ukikemea na kuomba mpaka siku Yesu akirudi punje ya nafaka itabaki kuwa punje, ni mpaka utakapofuata kanuni za Mungu, kwa sababu ni Mungu anayetupa mabadiliko ya kweli katika wokovu. Inawezekana yule anayewazuwia watu wasiingie kanisani wakati watu wanaotaka kukutana na Mungu wao aliyewanunua kwa damu yake ya thamani. halafu yeye anawazuwia kana kwamba yeye aliokolewa kwa sababu alikuwa mtakatifu sana. Mtu huyo nina mashaka naye sana kama sio wakala wa shetani, basi hajui anachokifanya na ama hajui sababu ya kifo cha Bwana Yesu pale kalvary.
Inawezekana mtu huyo akawa sio muhimu kwako
wala kwa kanisa lako lakini mbele za Mungu ni mtu muhimu sana na anajulikana
sana kwenye ufalme wa mbinguni.
Wakati fulani nilikwenda kutembelea kanisa
moja nje kidogo ya Mji wetu, na baada ya kumaliza kufanya huduma, Mchungaji wa
kanisa lile akaniongoza ofisini kwake kwa Mapumziko na mazungumzo mafupi.
Wakati tunaendelea na mazungumzo hayo
aliingia ofisini mshirika mmoja wa kike kwa shughuli za kiutumishi, na baadae
alipotoka nje ya ofisi mchungaji alitaka kupata mawazo yangu na maoni yangu
kuhusiana na muonekano na hasa mavazi aliyokuwa amevaa yule mwanadada.
Kwanza sikuelewa mchungaji anataka kusema
nini juu yake, hata hivyo nilikuwa naamini kuna kitu anataka kunifundisha
kutokana na swali hilo hivyo ilinibidi niwe makini kueleza jinsi ninavyomuona
kwa hisia zangu mwenyewe. Nikamwambia mchungaji huyu dada amevaa vizuri sana na
ningependa wakina dada wote makanisani mwetu wavae mavazi ya heshima kama
aliyovaa yule dada, kwanza ni mavazi ya kisasa na unaweza ukaingia nayo mahali
popote kwenye hadhi kubwa.
Nikaona mchungaji anacheka kisha akaniambia
alitegemea majibu kama hayo kutoka kwangu ila akaniambia kuna kitu kikubwa sana
ambacho yeye binafsi Mungu amemfundisha kupitia katika maisha ya yule dada.
Akasema huyu dada alikutana na Bwana Yesu akiwa kwenye shughuli za ukahaba changudoa akiwa kwenye danguro (sehemu ambako
watu wanajiuza miili yao) na alikutana na Bwana Yesu akiwa huko na akamuongoza
kuja katika kanisa hili analolichunga na yeye akampokea. Anasema kama
unavyofahamu, Maisha ya watu wa aina hii hakuwa na nguo ya maana hata moja.
Nguo zake nyingi zilikuwa ni zile alizokuwa
anazivaa kwenye shughuli zake za kujitafutia riziki kwa njia haramu. Anasema
alipofika kanisani washirika hawakumkubali na wengine walikuwa wakimtolea
maneno ya kashfa kwamba anawadhalilisha, wengine walitaka aondoke kabisa
kanisani.
Hili jambo ni lazima watu walifahamu kwamba kanisa ni mali ya Yesu mwenyewe na yeye ndiye anayejua nani ampeleke katika kanisa gani, si jukumu letu kulalamika kwamba mbona kanisa ninalolichunga halina matajiri au wafanyakazi wenye hadhi kubwa (waheshimiwa) kanisa lipo kwa ajili ya watu wote.
Hili jambo ni lazima watu walifahamu kwamba kanisa ni mali ya Yesu mwenyewe na yeye ndiye anayejua nani ampeleke katika kanisa gani, si jukumu letu kulalamika kwamba mbona kanisa ninalolichunga halina matajiri au wafanyakazi wenye hadhi kubwa (waheshimiwa) kanisa lipo kwa ajili ya watu wote.
Dunia ni kama bahari iliyochafuka na kanisa ni
kama meli ya usalama iliyoko juu ya bahari. Watu wanapookoka inakuwa ni sawa na
watu waliozama baharini wanategemea wakiokolewa na kuingia kwenye Meli (kanisa) watakuwa salama na
watafundishwa namna ya kuishi kwenye meli hiyo. Sasa hawawezi kujifunza kwa
siku moja au mbili wengine inaweza kuwachukua miaka kadhaa kuweza kujua namna
ya kuishi katika chombo hicho (kanisa) Mchungaji yule anasema mara nyingi yule
dada alikuwa anakwenda ofisini kwake akiwa analia na kueleza jinsi ambavyo
anabaguliwa na kusemwa vibaya na washirika wenzake ndani ya kanisa.
Mchungaji alimwambia kwamba wala asisikilize
neno la mtu awaye yeyote kuhusu kitu chochote kama kuna kitu kibaya yeye
mchungaji ndio atamwambia. Kwa maana yeye ndio mchungaji wake. Maneno yale
yalikuwa yanamfariji sana yule dada na kumpa bidii ya kuhudhuria vipindi karibu
vyote vya kanisani. Baadae alianza kubadilika na akawa anavaa vizuri kushinda
hata wale waliokuwa wanataka kumfukuza kanisani. na kwa kweli ni mtu anayempenda sana Bwana
Yesu na hata wakati huo alikuwa ni msaada mkubwa sana kwa mchungaji wake na kanisa
lake kwa ujumla.
Muda mwingi Yule dada anautumia kanisani kwa kuombea
watu wanaofika kanisani na kufanya usafi wa kanisa.
Hii ilikuwa ni habari ya ajabu sana kuhusu
nguvu ya Roho mtakatifu inavyoweza kumbadilisha mtu kutoka katika shimo la giza
na kumfanya kuwa nuru na kielelezo kwa wengine. Mchungaji anasema katika
mafundisho aliyokuwa akipewa na Mungu kwa ajili ya kanisa kwa kipindi chote cha
mabadiliko ya yule dada hakukuwa na mafundisho kabisa yanayohusu mavazi au
mabadiliko ya tabia, mafundisho mengi yalihusu imani na nguvu za Mungu.
Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu.
Nimekupa ushuhuda huu makusudi ili uweze
kufahamu kwamba
Imani huwa inazaliwa na imani huwa inakuwa
ama inaongezeka kulingana na jinsi ambavyo unavyojitoa mbele ya Mungu, na jinsi
vile Mungu anavyoonekana kwako. Kwa sababu imani ni mchakato na maisha ya
wokovu ni kuzaliwa mara ya pili haitawezekana mtoto akazaliwa mara moja akaanza kuongea na kutembea
ni lazima tufahamu kwamba, mtoto kabla hajakuwa mtu mzima kuna hatua nyingi
anazopitia na anahitaji uangalizi wa hali ya juu sana . Kuna makosa mengine
mtoto akifanya wala huwezi kumlaumu bali utawalaumu walezi wake au wasimamizi
wake, lakini kuna kipindi ambacho mtoto anapoendelea kukua inabidi kumwelekeza
kwa bidii juu ya nini anachotakiwa kukifanya na kipi hatakiwi kukifanya na kuna
kipindi kinapofika huna haja tena ya kumwelekeza mtoto nini cha kufanya hapo
ndipo utakapoweza kumuadhibu lakini inapotokea mtoto amezaliwa tu na wewe
unaanza kumchapa hata kabla hajajua maisha yanakwenda vipi. Ukifanya hivyo wewe
mzazi watu watakulaumu na ikibidi serikali itakupokonya mtoto huyo alelewe na
mtu mwingine. Maana wewe utamuua mtoto (kwa maana wewe hujui kulea kuna kumwogesha
kumnawisha akijichavua na kumtunza kwa upendo,kama kuna mchungaji hajui jambo
hili basi ni hatari kwamba imani yetu itakuwa imevamiwa kwa kiasi cha kutisha
sana au huyo
mchungaji atakuwa ama amechukua washirika kutoka kwa wachungaji wengine au labda anachunga malaika kutoka mbinguni lakini kama ni wanadamu wa kizazi cha leo ni lazima awe mpole na afanye kazi ya Mungu kwa uvumilivu sana, kitendo chochote cha kumfukuza mshirika ama kumzuwia kuingia katika jengo la dini yako ni kukwepa wajibu wa kiutumishi, kwa sababu watu hawawezi kufanana na unaweza ukamuona wewe mtu Fulani hafai na matokeo yake akaja kuwa mtenda kazi hodari kabisa nyumbani kwa Mungu na akawa msaada mkubwa kwa ufame wa Mungu na ukashangaa kabisa, haya mambo yameshatokea sana kwa watumishi wengi waliwafukuza watu na baadae wakaja kugundua kuwa ama hawakushauriwa vizuri au hawakutulia vizuri kumsikiliza Mungu. Maisha ya Kiroho Sio Mepesi Kama Tunavyofikiri.
mchungaji atakuwa ama amechukua washirika kutoka kwa wachungaji wengine au labda anachunga malaika kutoka mbinguni lakini kama ni wanadamu wa kizazi cha leo ni lazima awe mpole na afanye kazi ya Mungu kwa uvumilivu sana, kitendo chochote cha kumfukuza mshirika ama kumzuwia kuingia katika jengo la dini yako ni kukwepa wajibu wa kiutumishi, kwa sababu watu hawawezi kufanana na unaweza ukamuona wewe mtu Fulani hafai na matokeo yake akaja kuwa mtenda kazi hodari kabisa nyumbani kwa Mungu na akawa msaada mkubwa kwa ufame wa Mungu na ukashangaa kabisa, haya mambo yameshatokea sana kwa watumishi wengi waliwafukuza watu na baadae wakaja kugundua kuwa ama hawakushauriwa vizuri au hawakutulia vizuri kumsikiliza Mungu. Maisha ya Kiroho Sio Mepesi Kama Tunavyofikiri.
TUNAPAMBANA NA SHETANI YULEYULE WA KWENYE
BUSTANI YA EDEN LAKINI KATIKA MAZINGIRA YALIYOBADILIKA SANA.
Kama
kijidudu cha maralia tumekibadilishia dawa mara nyingi sana, lakini bado
kijidudu hiki kimeendelea kuua watu wengi zaidi kuliko ugonjwa wa aina yeyote
na kwa kweli dawa yake halisi ni quinen. Lakini tumekibadilishia dawa za aina
mbalimbali kama vile cloloquine maralaquin shelaquin n.k. na kama
unavyoona katika kila dawa ilipobadilishwa qunine ilikuwepo ndani yake.
Hapo ina maana kwamba kila walipokuwa
wakitibu kijidudu hiki kiliporudi kilikuja kikiwa kimejiimarisha zaidi na
kujikinga ili kuzuwia Quinen isikipate, pengine kiliweka gamba gumu na kufumba
mdomo wake. Matokeo yake dawa inaonekana haifai.
Hapo inabidi itafutwe dawa ambayo kwanza
itakwenda kuvunja lile gamba na kisha itakibana mdomo kile kijidudu na ndipo
Quinen itapitapenya na kukipata kile kijidudu na kukiua. Ndio maana siku hizi
kuna dawa mseto ya maralia maana yake ni mchanganyiko wa dawa zaidi ya moja hii
ndio maana ya neon mseto.
Nimetoa mfano huu kukuonyesha kwamba kama
kijidudu kidogo cha maralia kimetusumbua na tumekibadilishia dawa mara nyingi
kiasi hicho nab ado kinatusumbua je itakuwaje kwa shetani. Ni wazi kwamba
hatuwezi kupambana na shetani kwa staili ileile iliyotumika kwa mfano miaka
kumi tu iliyopita.
Kwa sababu hiyo hakukuwa na wizi kabisa,
katika nyumba zingine watu waliweka pazia tu wala wezi hawakuiba,lakini baadae
baada ya kutoka kwenye misingi ile ya ujamaa ambayo ilijali zaidi utu wa mtu na
kuingia katika siasa zinazochanganyikana na ubinafsi watu walianza wizi,ilibidi
watu wabadilishe na waanze kutengeneza milango mingine ya mabati na baadae
milango ya mbao. Lakini wezi nao walikuwa wanabadilisha mbinu na kuvunja
milango ya mbao kwa kutumia mawe makubwa yanayowekwa kwenye magunia na kurushwa
kwa nguvu kwenye milango ya mbao na kuivunjilia mbali. Mawe haya wanayaita jina
la “fatuma.”
Siku
hizi watu wanajenga majumba makubwa yenye milango ya chuma na walinzi wenye
bunduki na majibwa wakali lakini bado wezi wanaiba. Mlinzi analeweshwa au
ananyongwa,mbwa wanapewa maini ya sumu na wezi wanakuja na gesi ya kukatia
vyuma wanaingia na kuharibu
Tena katika hali nyingine ni afadhali nyumba
yako uweke vitasa kuliko kuweka kufuli maana ukiweka kufuli ni sawa na kuweka
tangazo kwamba mwenye nyumba hii hayupo.
Mifano hii miwili ingawa inaweza kuwepo na
mingine mingi ambayo itatusaidia kufahamu kwamba mbinu zinabadilika kulingana
na hali na nyakati.
Tukumbuke kwamba kila nyakati zina watu wake
na stahili zao za maisha, wakati Yohana mbatizaji analeta injili kwa watu wa
kizazi chake walimpokea na walimkubali kwa staili aliyoingia nayo ya kuvaa
mavazi ya ngozi na kula asali na matunda watu walimuelewa na walitubu. Lakini wewe mtu wa kizazi cha leo ukija na staili
kama hiyo ya Yohana mbatizaji ni lazima ukamatwe na ndugu zako na utapelekwa
kwenye wadi za wagonjwa wa akili. Maana mahali ilipofikia dunia huwezi
ukaipeleka kwa staili hiyo utakuwa pia hujaitende haki.
Wakati nchi yetu ya Tanganyika inapata uhuru Elimu ya rais wa wakati
huo JK Nyerere ya digrii mbili ilitosha kabisa kuendesha nchi na kwa sehemu
kubwa mpaka leo hii bado watu wanamheshimu na kumuona kwamba alikuwa na akili
nyingi sana .
Lakini leo hii hao watu wenye digrii mbili ni watoto wadogo sana na wengine bado hawajapata kazi za
uhakika. Kuna makanisa mengine yana vyama vya akina mama ambao wengi wao
wamezidi miaka 45 na kutokana na mavazi yao kwa umri walionao wanataka na
mabinti wa chini ya miaka 18 wavae mavazi kama wanayovaa wao,ambayo hata wao
walipokuwa mabinti hawakuvaa mavazi kama hayo. Ni lazima tukubaliane kwamba
kila nyakati zina watu wa aina yake na mitindo yake ya mavazi, hata siku hii ya
leo unaweza ukavaa aina Fulani ya mavazi na watu wakakushangaa kwamba huyu
ndugu mbona amevaa mavazi ya zamani sana .
Hapo ni lazima tukubaliane kwamba lengo kubwa la mavazi ni kusitiri maungo ya
miili yetu na suala la kujipamba au kupendeza ni kitu kingine. Mchungaji mmoja
rafiki yangu alitoa onyo kwa akina mama wa kanisa lake
kuacha kuwasumbua mabinti wanaokuja
kanisani kuhusiana na mavazi na mapambo ya nywele aliwaambia ni afadhali kama
wao wanaona shida kukaa nao basi waondoke wao na wasifanye kazi ya kuwafukuza
vijana hao kwani hata wao wakati wanaingia kanisani hawakuwa kama
walivyo sasa.
KANISA
NI NINI?
Je kanisa ni jengo? Hapana! Kanisa ni mtu
aliyezaliwa mara ya pili na ambaye amejazwa na roho mtakatifu na Mungu
anamtumia katika kuujenga ufalme wake. Hii hasa ndio tafsiri halisi ya kanisa.
Tukilijua hili litatuwezesha kufikiria namna ya kumtayarisha mkristo mmojammoja
kibinafsi na hatimaye tukiwa kama kikundi ndio tunapoweza kuwa na kanisa imara
la mahali. Hatutaweza kuacha jukumu la wito wetu kwa Mungu na kuanza kushindana
na kupigana vijembe kwa mambo yasiyokuwa na maana baina ya watumishi au
kufukuzana kwenye majengo ya dini zetu. Huu ni wakati wa kuwafundisha watoto wa
Mungu jinsi ya kujipanga na kupambana na changamoto mbalimbali wakati dunia
inakwenda na mabadiliko ya kasi kubwa. huu ni wakati wa viongozi wa kiroho
kuzisoma nyakati na kujipanga kukabiliana na changamoto zinazolikabili kanisa
kama mtu mmojammoja na kanisa kama kundi la watu wa mahali fulani katika zama hizi za utandawazi na information
Technolgy. Ni lazima tujue tunatumiaje maarifa yaliyoko duniani katika kuujenga
ufalme wa Mungu na sio kupingana nao.
Wakati matumizi ya Internet yanaanza kuingia
kuna baadhi ya makanisa walifanya maombi maalumu ya kufunga na kuomba kuzuwia
mitandao ya yahoo na mingineyo isiingie katika nchi yetu kwa madai kwamba ni
alama ya mpinga Kristo lakini walishindwa na leo hii wao wenyewe ndio
wanaonufaika nayo kwa kuwasiliana na watumishi wenzao wan chi za mbali. Tukijua
kwamba kanisa ni mtu basi ni lazima tuhakikishe tunamuandaa mtu kwa umakini
mkubwa kulingana na mazingira yaliyopo, siku hizi kuwa mtu wa kiroho sio lazima
uwe mtu wa kuzubaazubaa na kuvaa makoti makubwa kama mtu wa kutoka mashambani.
Kuwa mtu wa kiroho siku hizi ni kuwa na maono na maono ni mipango ya namna
utakavyoutumia wakati na mazingira yaliyopo katika kujenga ufalme wa Mungu,
hapo haijalishi kwamba umeweka dawa nywele au una nywele zako za kipilipili.
Hapa tutaangalia una uwezo gani wa kuwapelekea ndugu zetu wa mataifa ya kiarabu
ambao bado hawajafikiwa na injili ukaongea nao
COPY
AND PASTE SYNDROME (KUNAKIRI NA KUCHOMEKA)
Mojawapo ya mambo ambayo athali zake
zinaonekana haraka sana katika utandawazi ni tabia ya kuiga haraka tabia na
utamaduni wa mataifa mengine ambapo pengine huku kwetu ni tatizo.na vijana wengi wanafikiri kuwa kila kitu wanachofanya vijana wa ulaya kinakubalika na jamii ya watu wote walioko huko. ukweli ni kwamba yapo mambo mengi ambayo watu wa ulaya hawakubaliani nayo,lakini yakifika huku kwetu tunayaona ya maana na kuiga.
baadhi ya mavazi ambayo hayakubaliki kabisa na inatakiwa kukabiliana nayo kwa nguvu za kiroho na kimwili.
Lakini pamoja na hayo yote hakuna sehemu hata
moja ambayo inaweza kukwepa mabadiliko haya iwe kwa kutaka ama kwa kutokutaka.
Kwa hali hiyo hata kanisa haliwezi kukwepa kuingia katika mabadiliko haya.woga
wa aina yoyote utakuwa ni woga ambao hauna sababu,
Hii ni kwa sababu kanisa linavuna waumini
wake kutoka katika jamii ya watu waliopo katika sehemu lilipo kanisa kwa hiyo
ni lazima watu walio katika jamii hiyo wataingia kanisani wakiwa katika hali
waliyonayo kabla mabadiliko ya kiroho yatakayoletwa kwa msaada wa roho
mtakatifu na sio kwa nguvu ya kianadamu na roho mtakatifu atawafinyanga watu
katika namna ambayo anaitaka mwenyewe kwa manufaa ya Mungu.
Ni jambo la kusikitisha sana kuona baadhi ya
makanisa yanawazuwia watu wanaokuja makanisani kwao wakiwa katika hali Fulani
ambayo inaoneana wameathiriwa na mambo ya utandawazi na tabia zake.
Kuongezeka
kwa kasi ya uvukaji wa mipaka
Katika eneo hili ni lazima litakuwa na faida
lakini pia litakuwa na athari kwa kanisa na hasa makanisa ya mijini itakuwa ni
vigumu sana kwa wachungaji kuwasimamia watu wanaowachunga kwa sababu hakutakuwa
na utulivu wa watu makanisani kwani watu wengi watakuwa wanaingia na kutoka,na
kila wanapotoka na kuingia watakuwa na mitazamo tofauti kulingana na mila na
desturi za sehemu wanakotoka na sehemu wanazotembelea,kwa sababu ya changamoto
hii ni lazima kanisa litegemee kukabiliana na migogoro mingi itakayohusiana na
tabia mbaya za kuambukiza kutoka sehemu nyingine. hii ni changamoto kwa kanisa kuanza kujiandaa kukabiliana na mabadiliko bila kulalamika.