NYOTA WA
MUZIKI WA INJILI AFRIKA YA KUSINI VUYO MOKOENA HATUNAYE TENA.
Kwa wapenzi wa muziki wa injili wa Afrika kusini jina la Vuyo Mokoena sio jina geni kabisa na unaweza usitofautishe na majina kama Rebeka Malope,Sipho Mukabane na akina Jabu
Afrika ya kusini ni nchi ambayo imebarikiwa sana katika suala zima la
muziki pamoja na mambo mengine,taifa hili pia limepoteza waimbaji wengi
wakiwemo wa muziki wa nje ya kanisa na ule wa kanisani na moja ya nyota
iliyozimika katika muziki wa injili nchini humo ni Vuyo Mokoena ambaye
alijulikana rasmi kwenye tasnia ya muziki nchini humo mnamo mwaka 1999 wakati
aliposhiriki mashindano ya kuibua vipaji kisha akawa ni mtu wa kuitikia nyimbo
na waimbaji(backup) katika kundi la Pure Magic kabla hajatoka rasmi kivyake
mwaka 2003 kama mwimbaji wa kujitegemea.
Vuyo ambaye hakuchukua muda mrefu kwenye medani ya muziki kujulikana ameshiriki
kikamilifu katika kundi la Joyous Celebration kwa takribani miaka saba na
rafiki yake Jabu Hlongwane katika nyimbo mbalimbali,pia alikuwa rafiki wa
karibu sana na malkia wa muziki wa injili barani Afrika Rebecca Malope ambaye
kutokana na ukaribu walionao marehemu alimkabidhi mkewe aitwaye Tebogo wimbo
ambao aliutunga yeye siku nne kabla hajafariki dunia na kumtaka mkewe
kuukabidhi wimbo huo kwa Rebecca endapo jambo lolote litatokea(ikiwa kama
atafariki) ili aje kumwimbia siku ya mazishi yake, jambo ambalo Rebecca
alilifanya.
Mwimbaji huyo maarufu kwa wimbo wake ''Njalo'' ameacha mke na watoto wanne
alifariki dunia mwaka 2008 kwa ugonjwa wa kansa ya damu,ugonjwa ambao
ulimlaza kitandani mara nyingi kabla ya kifo chake,taarifa ya kifo hicho
ilitolewa na kampuni yake ya muziki iitwayo Big Fish Music,ambapo katika
mazishi yake waimbaji wengi walihudhuria wakiwemo kundi la Joyous,Rebecca
Malope,rafiki yake Sipho Makhabane na waimbaji wengine wengi.Mwimbaji huyo
kabla ya kufariki dunia tayari alishanyakua tuzo katika medani ya muziki wa
injili nchini humo.
Baadhi
ya waimbaji wa kundi la Joyous wakiimba kwenye jukwaa
|
Ibada ya mazishi ya
mwimbaji huyo ilifanyika sehemu mbili katika kanisa la Grace Bible Church na
Duduza Multipurpose Centre na mazishi kufanyika katika makaburi ya Nigel
huko huko Afrika ya kusini.Lakini pia kitendo cha kuhuzunisha kilichotokea
katika ibada ya mazishi kanisa la Grace Bible ni kwamba licha ya ulinzi mkali
wezi wapatao wawili waliiba gari aina ya Rav4 ya mwanamuziki mwingine maarufu
nchini humo aitwaye Khanyo Maphumulo ambaye alikuwa akihudhuria ibada ya
mazishi kanisani hapo
Moja ya jambo lililofanywa na rafiki zake wa karibu pastor Jabu,Lindelani
pamoja na Rebecca Malope walishirikishwa kwenye makala maalumu ya maisha ya
mwanamuziki huyo ambaye mpaka hii leo bado anakumbukwa nchini kwake na sehemu
mbalimbali duniani kutokana na huduma yake njema aliyoifanya ya kumuinua Kristo
duniani.Rebeka malope mwanamuziki mkongwe wa
nyimbo za injili Afrika Kusini
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni