- Kulingana na taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO), tatizo hili la wanaume dhaifu linaongezeka kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kuendekeza ulevi, matumizi ya tumbaku/sigara, kutokula kwa kuzingatia mchanganyiko wa vyakula (ulaji usiofaa) na watu kutopenda mazoezi.
SHARE THIS STORY
Ni
vigumu kufahamu haya, lakini ndio ukweli kuwa kuna kasi ya kuongezeka kwa
wanaume dhaifu nchini na ulimwengu kwa ujumla.
Kulingana
na taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO), tatizo hili la wanaume dhaifu
linaongezeka kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kuendekeza ulevi, matumizi
ya tumbaku/sigara, kutokula kwa kuzingatia mchanganyiko wa vyakula (ulaji usiofaa)
na watu kutopenda mazoezi.
Hapa
nchini hakuna utafiti thabiti uliofanywa lakini nafikiri tutakubaliana kuwa
tatizo hili lipo tena ni kubwa, kwani kinyume na hilo kusingekuwa na watu wengi
wanaojitangaza kwamba wanatibu. Marekani wamefanya utafiti, Shirika
liitwalo National Ambulatory Medical Care Survey (NAMCS) ambalo linasifika kwa
kufanya tafiti mbalimbali za masuala ya afya, linasema kwamba ukionana na
Wamarekani 1,000 ujue kwamba 22 ni wanaume dhaifu.
NAMCS
ikasema pia kwamba zaidi ya wanaume milioni 2.6 wanatumia dawa za kuongeza
nguvu; ndio nasema kwamba sisi Tanzania hatujafanya utafiti rasmi uliotangazwa
na Serikali, lakini wewe bila shaka utakuwa shahidi kwamba ziko dalili kwamba
hali ni mbaya.
Kuna
mtafiti mmoja maarufu kutoka India, Dk Srini Vasakumar, kutoka kituo cha
utafiti wa tiba kiitwacho Institute of Biology and Clinical, India, ambaye
amekuwa akitoa huduma za kuponya tatizo hilo la udhaifu katika maeneo
mbalimbali hapa nchini, anasema hili ni tatizo linaloweza kupona, shida ya
wengi ni kutochukua hatua; wengi wanalia, badala ya kuchukua hatua.
Daktari
huyo mwenye Shahada ya pili ya Tiba kwa kutumia vyakula na Shahada ya uzamivu
ya tiba kwa ujumla, anasema wengi wanaendelea kuwa na tatizo hili kwa
kutochukua hatua thabiti; wengi wamesoma na wanafahamu kuna aina za vyakula
vinasaidia wanga, nguvu, mafuta na vitamini... lakini wanakula ili mradi tumbo
lijae.
Aliyekuwa
Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi, Janet Bina Kahama, Aprili
10, mwaka 2007 katika kikao cha saba cha Bunge aliuliza swali namba 8
(b); je, Serikali inafahamu ni sababu gani zinasababisha kupungua kwa nguvu za
kiume kunakotangazwa sana na waganga wa jadi? Aliyekuwa Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii, Prof. David Mwakyusa alijibu kuwa tatizo hili linasababishwa
na mambo mengi, baadhi yao ni lishe duni hasa mboga za majani, kutokula aina
mbalimbali za jamii ya karanga, matumizi yasiyofaa ya ulevi kama pombe.
Sababu
nyingine ni matumizi ya sigara, dawa za kulevya, dawa zinazotibu baadhi ya
magonjwa kama kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya akili na kutopumzika
kunakosababishwa na shughuli nyingi za kijamii hivyo kusababisha uchovu.
Kwa
uzoefu wangu kama mtu ambaye nimekuwa nikitoa ushauri kuhusu masuala ya ndoa ni
kwamba tatizo hili lina athari kubwa katika ndoa, baadhi ya wanawake sasa
hawaangalii uzuri wa mwanaume, wala utajiri au elimu yake ama tabia,
kwanza wanatamani kujua kama mume mtarajiwa ni mume dhaifu au la.
Athari
za kuwa dhaifu ni kwamba baadhi ya wanawake unaweza kumpa mamilioni ya
fedha, magari nk lakini unachohonga akaenda kuhongwa mwingine. Unamnunulia
gari, unaweza kushangaa unakutana naye anatembea kwa miguu, gari kapewa
kijana atanue nalo.
Ninachotaka
kusema ni kwamba kila wanaume kuchukua tahadhari juu ya jambo hili ambalo
linaonekana wazi kuwakwaza wanawake wengi kiasi cha baadhi kuamua kuvunja
uhusiano. Hata hivyo kama mwenzi wako ana tatizo ni vizuri kuangalia namna ya
kulitibu, sio kukimbiana, kwani hakupenda kuwa hivyo.
CHANZO: Mwananchi Ijumaa,Januari 24 2014
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni