LAANA
NI NINI?
Laana ni mkusanyiko wa
mabaya yote yanayompata mtu: misukosuko katika kazi au ndoa n.k. laana huleta
mateso mengi.
Katika kumbukumbu
imeandikwa
“Bwana
atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako
kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako,
uliyoniacha kwayo. 21 Bwana atakuambatanisha na tauni, hata atakapokwisha
kukuondoa katika nchi uingiayo kwa kuimiliki. 22 Bwana atakupiga kwa kifua
kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa
ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie. 23 Na mbingu zako zilizo
juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma. 24
Bwana atafanya mvua ya nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako
kutoka mbinguni hata uangamie. 25 Bwana atakufanya upigwe mbele ya adui zako;
utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini utakimbia mbele yao kwa njia saba;
nawe utatupwa huko na huko katika falme zote za duniani. 26 Na mzoga wako
utakuwa chakula cha ndege wote wa angani, na wanyama wote wa duniani, pasiwe na
mtu wa kuwafukuza. 27 Bwana atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa
bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa. 28 Bwana atakupiga
kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni; 29 utakwenda kwa
kupapasapapasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika
njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa
kukuokoa. ). KUMBUKUMBU
28:20-29
Haya ndiyo mambo yanayowatokea wanadamu hata sasa. Unapotumia maneno ya
kinyume dhidi yako, maneno hayo hugeuka na kuwa laana. Yale
unayoyaona kwa sasa ni matokeo ya maneno uliyowahi kutamkiwa au
kujitamkia mwenyewe: Hii ni kwa sababu Biblia inasema "maneno
ni roho". Na unapotaka kuwa huru dhidi ya laana, anza kwa
kushughulikia chanzo cha tatizo. Chombo cha kupokelea laana yoyote
ile ni DHAMBI. Bila dhambi, laana haiwezi kukupata, na hii ni kwa sababu
Biblia inasema
“Kama shomoro katika kutangatanga
kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; Kadhalika
laana isiyo na sababu haimpigi mtu.” MITHALI 26:2
Laana ikikosa pa
kwenda inamrudia yule anayeituma kwa maana ya aliyeinena. Unapaswa
kuchukua hatua kwa kumwendea Bwana nje ya lango, na Bwana atawashikisha
kishindo maadui zako kama ambavyo wale wakoma wanne nje ya lango walipoleta
ufumbuzi wa tatizo la njaa kule Samaria.
Wapo watu
waliojifungia ndani lakini wana matatizo mengi sana na ambayo chanzo cha hayo
matatizo ni viumbe wa rohoni. Mtu unapokuwa na dhambi, laana hukaa. Inategemea
na maamuzi unayochukua katika maisha yako. Kupitia ulimi wako unao uwezo wa
kuamua hatima yako itakuwa je!!? Chagua leo kuwa na uzima ili uishi au uendelee
kuwa na dhambi upate mauti, kwa kuwa "mshahara wa dhambi ni
mauti". Zipo laana za wanadamu, laana ya Mungu, laana ya wachawi,
laana ya kumuibia Mungu zaka n.k.
BIBLIA
INATUFUNDISHA AINA MBALIMBALI YA LAANA:
Laana ya
kuchonga au kuifanya sanamu.
“Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu
ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi,
akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina). KUMBUKUMBU
27:15
Laana ya Kuondoa mpaka. Wapo watu wanaoweza kuondoa mpaka wa maisha yako.
(Na alaaniwe
aondoaye mpaka wa jirani yake. Na watu wote waseme, Amina.) KUMBUKUMBU
27:17
Kitendo cha kumpotosha mtu nayo ni laana.
(Na alaaniwe
ampotezaye kipofu akakosa njia. Na watu wote waseme, Amina.). KUMBUKUMBU
27:18
Laana ya Kutowaheshimu wazazi. Hii huleta laana kwa maisha yako.
(Na alaaniwe
amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina.). KUMBUKUMBU
27:16...
Pia imeandikwa katika
(Enyi
watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. 2 Waheshimu
baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, 3 Upate
heri, ukae siku nyingi katika dunia.). WAEFESO 6:1-3
Wapo watu wengi sana wanajisahau wakeshafika
mijini, na matokeo yake mabo yao hayawezi kunyooka.
Laana ya Kudhulumu haki ya mtu.
(Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na
yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina. KUMBUKUMBU
27:19
Laana ya Kulala na mke wa Baba yako,
Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa
kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Amina.). KUMBUKUMBU 27:20
Hii ni kama Reubeni alivyofanya, wakati huo
mzee Yakobo alilaani kitendo kile cha Reubeni kuwa asiwe mkuu kwa kuwa aliuruka
mpaka kama maji. Imeandikwa katika
(Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza,
Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa
nguvu. 4 Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu, Kwa sababu ulikipanda
kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu.)
MWANZO 49:3-4....
Laana ya Kulala na wanyama.
(Na alaaniwe
alalaye na mnyama wa aina yo yote. Na watu wote waseme, Amina.) KUMBUKUMBU
27:21...
Laana ya Kulala na dada yako.
imeandikwa
(Na alaaniwe
alalaye na umbu lake, binti ya babaye, au binti ya mamaye. Na watu wote waseme,
Amina.). KUMBUKUMBU
27:22
Mfano rahisi ni Amnoni mwanane Daudi aliyelala
na dada yake Tamari, na mwishowe akaja kuuwa na nduguye aitwae Absalom.
Laana ya Kulala na mkwe wako (mama wa mke wako). Imeandikwa katika
(Na alaaniwe
alalaye na mkwewe, mamaye mkewe. Na watu wote waseme, Amina.) KUMBUKUMBU
27:23
Laana ya Kumpiga mwenzako kwa siri. Hii ni kama vile kumsema mwenzako, au kumsengenya.
(Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri.
Na watu wote waseme Amina.) KUMBUKUMBU 27:24
Laana ya Kuua mtu au kutoa mimba. Imeandikwa katika
(“Na
alaaniwe atwaaye ujira wa kumwua asiye makosa. Na watu wote waseme, Amina.”)
KUMBUKUMBU 27:25....
·
Laana ya kutoshika
sheria ya Mungu. Imeandikwa katika KUMBUKUMBU 27:26“Na
alaaniwe asiyeyaweka imara maneno ya torati hii kwa kuyafanya. Na watu wote
waseme, Amina”).
·
Laana ya Kumlaani
aliyeokoka. Hata kama wewe ni mzazi, laana ya aina hii yaweza kukurudia kwa
kuwa tayari wewe umebarikiwa.
·
Kutenda kinyume na
maneno ya watumishi wa Bwana. Wengi wa watu wameharibikkiwa hapa. Na hili
linathibitishwa pale ambapo mambo fulani unayotaka yaondoke katika
maisha yako lakini hayaondoki. Kuhani ni daraja kati ya hiyo madhabahu na Mungu
katika ulimwengu wa roho. Endapo utatenda kinyume na kuhani wako au kusema
vibaya juu ya kuhani huyu ujue ni laana.
DALILI ZA MTU MWENYE
LAANA
Tunajifunza kuusu hizi dalili ili kukusaidia
wewe pale unapoona mtu mwenye dalili hizo au wewe mwenywe ujue kuwa utafanya
kitu gani. Shetani ni mshataki wetu mbele za Mungu, lakini Biblia inasema
katika UFUNUO 12:11 “Nao wakamshinda kwa damu ya MwanaKondoo,
na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.”
Lengo la laana ni kumzuia mtu asiende pale ambapo Mungu amekusudia wewe kwenda.
Zifuatazo ni dalili za mwenye laana:
1. Kutofanikiwa
kwa kila uendako. Imeandikwa katika KUMBUKUMBU 28:16 (Utalaaniwa
mjini, utalaaniwa na mashambani.). Kwa nini inakuwa ngumu kwa mtu
mwenye laana kufanikwa? Ni kwa sababu unalaaniwa mjini na unalaaniwa
mashambani. Wapo wanaokimbia kufanya biashara zao mijini wakakimbilia vijijini,
lakini hilo nalo halisaidii, kwa sababu hata huko laana inakufuatilia.
Inapotamkwa baraka kwako, ni vizuri kujua ni Baraka ya aina gani anakutamkia.
Kama ni kupata watoto, na aseme “Ubarikiwe upokee watoto” na wewe
useme “Amen”.
Yupo mtu mmoja katika Biblia ambaye
alibarikiwa wakati wa kwenda na wakati wa kurudi. Huyu ni Yakobo. Wakati wa
kuondoka alibarikiwa na Isaka babaye, na kupitia Rebeka mama yake akapata
Baraka zilizokusudiwa kwa nduguye Esau.
2. Kukosa mwelekeo (KUMBUKUMBU
28:33). Wapo watu wa aina hii, leo yupo Kanisa la Siloamu kesho yupo KKKT
n.k. Hata hivyo, kokote unapodondokea, watu wanajua hakika huyu mtu anazo
dalili za laana.
3. Kutokupiga hatua katika
maisha. Miaka nenda rudi, mtu anabaki kuwayule yule. Ukiziona dalili
kama hizi, achana na kitanda, anza kuchukua hatua kwa kufanya maombi
ya kushindana.
(Basi Yeriko ulikuwa umefungwa kabisa kwa sababu ya
wana wa Israeli; hapana mtu aliyetoka wala hapana mtu aliyeingia. 2 Bwana
akamwambia Yoshua, Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme wake,
na mashujaa wake. 3 Nanyi mtauzunguka mji huu, watu wote wa vita, mkiuzunguka
mji mara moja. Fanya hivi siku sita. 4 Na makuhani saba
watachukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume, mbele ya hilo sanduku; na
siku ya saba mtauzunguka mji mara saba, nao makuhani watapiga tarumbeta zao. 5
Kisha itakuwa watakapopiga hizo pembe za kondoo waume kwa nguvu, nanyi
mtakaposikia sauti ya tarumbeta, watu wote watapiga kelele kwa sauti kuu; na
ukuta wa mji utaanguka chini pale pale, na hao watu watapanda, kila mtu
akiendelea mbele kukabili.). YOSHUA 6:1-3 ...
Tena imeandikwa katika YOSHUA
6:26 ... (Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule,
akasema, Na alaaniwe mbele za Bwana mtu yule atakayeinuka na kuujenga tena mji
huu wa Yeriko; ataweka msingi wake kwa kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake, tena
atayasimamisha malango yake kwa kufiliwa na mtoto wake mwanamume aliye mdogo.)...
Ni kwamba, laana zimeodoka lakini asiwepo mtu wa kuujenga
upya tena Yeriko. Laana zinapoondoka Baraka hutokea. Na chapa ya
mwanakondoo itawekwa kwenye paji la uso wako.
Utimilifu wa ile laana aliyotamka
Yoshua ipo katika 1WAFALME 26:34...(Katika siku zake, Hieli
Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa
wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu;
sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni.).
UKIRI
LEO
TUNATAMKA, NA KILA ATAKAYEKULAANI JAMBO LIWEPO LA
KUMPATA.
KWA JINA LA YESU,
BWANA YESU NINAKUJA MBELE ZAKO, NINAOMBA UNISAIDIE.
|
Unachotakiwa sasa ni kutoruhusu chombo cha kupokelea laana
kisipatikane kwako, yaani usiwe na DHAMBI. Usiwepo mlango wowote wa laana
katika maisha yako. Wewe ambaye hujaokoka leo ni siku muhimunsanakwako kumpa
Yesu maisha yako