Mwl : Furaha Amon
KUNENA
KWA LUGHA NI KUJIJENGA NAFSI
Yeye
anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake, bali ahutubuye hulijenga kanisa. Na
mimi nataka ninyi nyote mnene kwa lugha lakini zaidi sana mpate kuhutubu maana
yeye ahutubuye ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri ili
kanisa lipate kujengwa (1Wakorinto 14:5)
Mkristo anayenena kwa lugha
hujijenga nafsi yake na yeye ahutubuye ni mkuu kuliko anenaye kwa lugha
kuhutubu maana yake ni kuhutubia au kuhubiri.
Tafsiri nyingine za Biblia
neno kutabiri. Hapo ina maana kuwa wakorinto wakati huo baada ya kujazwa Roho
Mtakatifu na kunena kwa lugha kama mkristo angesimama kuhubiri kusanyiko,
badala ya kuhubiri kwa lugha inayoeleweka kwa wale anaowahubiria ili waelewe
mahubiri anayohubiri au kama alikuwa anafundisha neno la Mungu wale wanaomsikiliza
waelewe kilichofundishwa, wakorinto baada ya kuhubiri kwa lugha inayoeleweka
wao walianza kunena kwa lugha.
Hili jambo huwa linatokea
hata leo, tumeona wakristo wamejazwa Roho Mtakatifu wakafurika sana na wakati
huo wakatoka kanisani wakaelekea majumbani kwao na walipokutana na watu njiani
walishindwa kuongea lugha zinazoeleweka bali kila alipofungua midomo walianza
kunena kwa lugha, lakini pia tumeona wakristo wamejazwa Roho Mtakatifu wakaanza
kucheka, wengine wakaanza kuimba.
Wakristo wa jinsi hii
wanahitaji mafundisho ili wajue kunena kwa lugha matumizi ya hadhara na
matumizi ya faragha. Wasipofundishwa wanaweza kuendeleza unenaji wa lugha
usiokuwa na utaratibu na hivyo kuleta makwazo.
Ni kweli kabisa Roho
Mtakatifu wakati mwingine huwavuvia watu kwa nguvu sana kiasi analazimika
kunena kwa lugha tumeona hata wahubiri mbalimbali wanapohubiri mikutano mikubwa
ya injili, wakati mwingine wanajikuta wananena kwa lugha japokuwa huithibiti
hali hiyo kutokana na kwamba wao wanajua matumizi ya kunena kwa lugha.
Tumeona hata viongozi wa
sifa katika ibada mbalimbali wengine wameshindwa kuongoza sifa wakaanza kunena
kwa lugha, tumeona hata waumini wanaochaguliwa kuomba sala mbalimbali kanisani
kwa niaba yaw engine, wanaomba lakini lakini katikati ya sala zao wameshindwa
kuendelea kuomba kwa lugha inayoeleweka badala yake wamenena kwa lugha.
Paulo ilibidi awafundishe
wakorintho kwa sababu hali hii ilizidi sana huko korinto. Wakorinto wao waliona
sawa tu kwa vile walikuwa hawajafundishwa matumizi ya kunena kwa lugha. Neno la
Mungu linasema, yeye anenaye kwa lugha anajijenga nafsi yake, anayehutubu
analijenga kanisa. Anayejenga kanisa analifundisha kanisa neno la Mungu, kwa
maana hiyo anayehutubu ni mkuu kuliko yeye anayejijenga nafsi yake peke yake.
Anayehutubu anafundisha watu wengi wamjue Mungu. Hapa ina maana kuwa wewe
umetakiwa kuhutubia badala yake umenena kwa lugha.
Maandiko yamezungumza vitu vitatu, kuhutubu,kuomba kwa akili na
kunena kwa lugha. Maandiko yanaposema yeye AHUTUBUYE ni mkuu kuliko yeye
anenaye kwa lugha. Haina maana kusema yeye AOMBAYE KWA AKILI ni mkuu kuliko
anenaye kwa lugha. Maandiko yanasema ahutubuye ni mkuu kuliko anenaye kwa lugha,
wakristo wengi wanachanganya sana eneo hili. Anayeomba kwa akili hawezi kuwa
mkubwa kuliko anenaye kwa lugha. Anayenena kwa lugha anajijenga nafsi yake
mwenyewe na anenaye kwa lugha anasema mambo ya siri kati yake na Mungu.
Anayeomba kwa akili hawezi kunufaika na Baraka zinazopatikana katika kunena kwa
lugha.
“Nami
nataka ninyi nyote mnene kwa lugha” (Wakorinto 14:5)
Kuna mafundisho potofu
yasemayo kunena kwa lugha si muhimu kwa kila muumini kunena. Viongozi wengine
wa dini wamekuwa wakiwazuwia wakristo wanapojazwa Roho Mtakatifu wasinene kwa
lugha.
Maandiko yanawakataza wale
wanaozuia wakristo kunena kwa lugha, wasizuwie kwa sababu kunena kwa lugha ni
muhimu. Mkristo anayeomba kwa akili hawezi kujijenga nafsi yake, wala hawezi
kusema mambo ya siri kati yake na Mungu. Hivyo maandiko yanasisitiza kuwa;-
“Wala
msizuwie kunena kwa lugha” (1 Wakorinto 14:39)
Kunena kwa lugha ni muhimu
sana kwa kila muumini, Wakristo ambao wamekataa kuliwekea kipaumbele jambo hili
wana hasara kubwa. Biblia inasema
Kwa
hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu,kusema Yesu
amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho
Mtakatifu (1 Wakorinto 12:3)
Kwa maana hiyo katika
kunena kwa lugha hakuwezi kumfanya mnenaji kulaani badala ya kubariki.
HATUJUI KUOMBA
“Kadhalika
Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo:
lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa” (Warumi 8:26).
Kama tulivyotangulia kusema
kwamba Roho Mtakatifu anazifanya kazi zake zote kupitia karama tisa. Roho
mtakatifu hutuombea kupitia karama hii ya kunena kwa lugha. Roho Mtakatifu
hutuombea kwa sababu sisi hatujui hatujui kuomba, wakristo wengi husema kuwa
wao wanajua kuomba sana. Lakini Mungu anajua kuwa sisi hatujui kuomba ndiyo
maana Mungu akaweka kazi mojawapo ya Roho Mtakatifu iwe ni kutuombea. Paulo
alijua hili ndiyo maana alikuwa ananena kwa lugha kuliko wengine maana yake
alikuwa anampa Roho Mtakatifu muda mwingi wa kumwombea.
Wanadamu tuna mipaka ya
kuelewa mambo yanayotukia hapa duniani. Huwezi kuelewa mambo yote yanayotokea
hapa duniani kwa wakati huo; wanadamu tuna ukomo wa kuelewa. Huwezi kuelewa
mambo yatakayotokea wakati ujao; huwezi kuelewa mambo yaliyotokea huko nyuma
kabla ya kuzaliwa, huwezi kuelewa mambo yaliyoko katika ulimwengu war oho;
huwezi ukaelewa mambo ambayo shetani amekupangia katika ulimwengu wa roho.
Ufahamu wa binadamu una
mipaka kutokana na mwili. Mwili ndiyo unaotuwekea mipaka. Roho Mtakatifu yeye
hana mipaka. Yeye ni Roho anao uwezo wa kujua mambo yajayo; yanayotendeka wakati
huu duniani kote na anajua yaliyotendeka duniani huko nyuma. Kutokana na hili
wewe ukiomba kwa ufahamu wako kwa akili zako. Hutaweza kuombea zile shida za
muhimu kulingana na uhitaji wako.
Mfano unapoombea siku ya
kesho unaombea mambo yaliyo katika ufahamu wako. Hivyo hutajua mambo mengine
mengi ambayo shetani ameyapanga kukufanyia siku hiyo ya kesho. Lakini Roho
Mtakatifu anajua mitego yote ambayo shetani amepanga kukufanyia siku hiyo ya
kesho. Lakini Roho mtakatifu anajua mitego yote ambayo shetani amekutegeshea,
ukiomba katika Roho Mtakatifu, atakuombea kwa ajili ya mitego hiyo ya shetani
ili Mungu atume Malaika wake ili aitegue mitego hiyo ya shetani. Biblia
inasema;-
“Na
yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo kwa kuwa huwaombea watakatifu
kama apendavyo Mungu” (Warumi 8:27)
Maombi ya Roho Mtakatifu
ndiyo maombi ambayo yanampendeza Mungu, Roho mtakatifu yeye anamjua Mungu,maana
ametokana na Mungu, hivyo anajua ni jinsi gani Mungu anapenda. Ili maombi yako
yawe na uhakika kwa asilimia mia 100% kwamba yamempendeza Mungu basi ni katika
kuomba kwa Roho Mtakatifu. Najua unafahamu kwamba kuna aina saba za maombi kwa
watakatifu ambayo ni
1. Kuomba
kwa imani
2. Kuomba
kwa jina la Yesu
3. Kuomba
kwa ahadi za Mungu
4. Maombi
ya mapatano
5. Maombi
ya Roho Mtakatifu
6. Maombi
ya kufunga
7. Kuomba
bila kukoma
Kila aina ya kuomba
inatakiwa tuitumie, kwa sababu kuna shida nyingine haziwezekani katika aina
fulani ya maombi bali inawezekana katika milango mingine. Hivyo kuna mahitaji
mengi sana ambayo hayawezekani kwenye milango mingine isipokuwa kwenye mlango
huu wa kuomba katika Roho.
KUTUBU DHAMBI
Hakuna dhambi kubwa wala
dhambi ndogo, kwa Mungu dhambi ni dhambi zote ziko sawa. Wakristo wengi
wanapofikiria kuhusu dhambi wao huzungumzia juu ya dhambi zinazoonekana wazi,
ama zile amri kumi za Mungu. Yesu alipokuwa anawaosha wanafunzi wake miguu,
Petro alikataa kuoshwa. Yesu akamwambia kama hutaki kuoshwa na mimi basi, basi
wewe sio mwenzetu. Petro aliposikia hivyo alisema basi kama ni hvyo basi si
miguu tu, nioshe mwili mzima. Aliyeoga si wa kurudiwa kuoga bali kuoshwa vumbi
miguu.
Hatujui kuomba jinsi
itupasavyo. Roho Mtakatifu hutuombea hata dhambi ambazo tumezitenda tukasahau
kuzitubu. Hakuna dhambi ndogo wala kubwa, dhambi ni dhambi tu. Mtu akivaa nguo
ya rangi nyeupe safi halafu abebe gunia la mkaa kwenye mabega yake, baada ya
dakika tano alitue lile gunia, atajikuta ile nguo nyeupe safi sio safi tena,
tena haitamaniki kuvaliwa tena, itakuwa imechafuka hadi ifuliwe. Huo ni uchafu
umeingia mara moja, lakini kuna mtu mwingine anafanya kazi ofisini kwenye
kiyoyozi naye pia ana nguo nyeupe akienda kazini kwa gari pia lenye kiyoyozi
akirudi nyumbani ile nguo inakuwa bado iko safi na anweza kuivaa na siku
nyingine, lakini baada ya siku chache inakuwa haiwezi kuvaliwa tena inakuwa
imechafuka na kutoa harufu. Hi nguo inakuwa imechafuliwa na uchafu unaoingia
kidogo kidogo lakini mwisho umeichafua nguo sawa na Yule aliyeichafua kwa mara
moja kwa dakika tano tu. Wakristo wengi wanaona dhambi ni zile kubwa
zinazoonekana na watu, dhambi ndogondogo hawazijali wala hawazitubu
wanapozitenda. Pamoja na kuokoka kwao hizo dhambi ndogondogo ndizo zinzopeleka
watu jehanumu. Dhamb ndogo ndogo ndizo zinaweka kutu kwenye nyaya za simu ya
mawasiliano yako na Mungu. Ndipo unakuta mtu wa Mungu pamoja na kuomba sana
kwake lakini hapati mpenyo wala hapati majibu. Mawasiliano na Mungu
yalishakatika siku nyingi. Mtu wa Mungu unapokuwa unanena kwa lugha, Roho
Mtakatifu anakuombea hata dhambi ambazo wewe hujui kuwa hii ni dhambi lakini
unazitenda, Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya kukuombea hata hizo dhambi.
Kuna msemo ambao unapenda
kutumiwa na Wakristo ambao hawaamini katika kujazwa Roho Mtakatifu na ishara ya
kunena kwa lugha kuonekana, kabla ya kuomba hupenda kusema kuwa tujitakase, kwa
mtu anayemjua Mungu kujitakasa ni kugeuka na kuacha njia mbaya. Sawa Mungu
aliwaambia wana wa Israeli katika mlima wa Sinai kuwa jitakase siku tatu;
lakini tunakuta kwenye agano jipya maandiko yanatuambia kuwa sisi baada ya
kumpokea Yesu tunakuwa watakatifu.
“Watakatifu
walioko dunian ndio walio bora. Hao ndio niliopendezwa nao” (Zaburi 16:2)
Neno la Mungu halisemi
tujitakase bali linasema tuzidi kutakaswa. Wakristo wengi msemo huu
umewapotosha hivyo wanakuwa bado wanaendelea kutenda dhambi wakitegemea
kujitakasa. Haya ni mapokeo yanayotoka kwenye dini yakimtaka mkristo baada ya
kutenda dhambi aende kwenye chumba cha kitubio akatubu dhambi mbele ya kasisi,
baada ya hapo dhambi zinaondolewa na anapewa malipizi ya kufanya hapo hapo.
Sasa mtindo huu umeingizwa kwenye wokovu na baadhi ya watu wasiojua vizuri neno
la Mungu. Sasa kwenye wokovu kwa kuwa hakuna kutubu mbele ya wakuu wa dini,
bali kwenye wokovu kila mtu anatubu mbele za Mungu, wakristo ambao hawataki
kubadili njia zao, hata baada ya kuokoka wamen’gang’ania madhaifu fulani fulani
ambayo wanayatenda kila siku, hivyo wanapofikia suala la kumwomba Mungu
wanaanza na kujitakasa. Sisemi kwamba kutubu kabla ya maombi hakutakiwi, bali
toba hiyo haitakusaidia kama huwezi kugeuka na kuacha kabisa.
Hapa kinachofundishwa hapa
ni kukuondoa kwenye wazo la kuendekeza kuwa hata nikitende dhambi nitajitakasa, hata nikitenda dhambi
nitatubu. Inatakiwa kujitakasa kwako kuendane na tendo la kugeuka na kuacha hilo
kosa ndipo kujitakasa kwako kutakapokuwa na maana, kujitakasa au kutubu lakini
huku unaendelea kuishi kwenye kosa hakutakusaidia. Baada ya kuokoka unatakiwa
ujifunze kwa bidii sana neno la Mungu, neno ndilo litakuchonga na kukubadilisha
uishi sawa na ulivyojifunza na kutenda sawa na mafundisho siyo kuhusiana na
dhambi tu, lakini kuhusiana na maeneo yote ya wokovu, kama kuomba, kushuhudia,
kumtolea Mungu, upendo, utakatifu, n.k. mtu akijua neno asipotenda kwake hiyo
ni dhambi. Hivyo neno la Mungu ndiyo linalotutakasa, basi kama ni neno la Mungu
basi Mungu mwenyewe ndiye anayetutakasa.
“Mtakatifu
na azidi kutakaswa” (ufunuo wa Yohana 22:11)
Inatakiwa tujitakase;
tutubu lakini huku kusitufanye tukavunja uwezo wa kupambana na dhambi, hivyo
tukawa hatuna juhudi katika kuacha kutenda dhambi kwa sababu tunatumainia kuwa
tutajitakasa.
Hata hivyo kujitakasa kwa
kuomba kwa akili hakutoshelezi, makosa tuliyoyafanya bila ya sisi kujua
hatuwezi kuyaombea kwa akili maana akili zetu tayari haiyajui. Kunena kwa lugha
ndiyo njia pekee ya kutakaswa. Unajijenga nafsi, mtu anayenena kwa lugha
hutakaswa kwa kiwango kikamilifu.
“Unikumbushe;
na tuhojiane; eleza mambo yako upate kupewa haki yako” (Isaya 43: 26)
Biblia inasema,
nikumbusheni mpate kupewa haki zenu. Mungu amechagua mwenyewe njia ya sisi
kumkumbusha ili tuweze kupewa haki zetu. Kuna maombi ambayo umeomba miaka mingi
iliyopita lakini maombi hayo hadi