SIKU YA KUSIMIKA TIMU YA KUSIFU
NA KUABUDU YA JIJI LA TANGA
Leo ni siku ya historia kubwa sana katika jiji la Tanga kwa
sababu yamezaliwa mawazo mapya ambayo hayajawahi kufanyika tangu injili ianze
kuhubiriwa katika jiji hili na ninamshukuru Mungu kwamba wewe mchungaji Dominic
Singano unakuwa ni sehemu ya historia hii. Watu wanaweza wasielewe sana ni nini
kinafanyika na kina umuhimu gani katika familia ya waimbaji wa nyimbo za injili
katika jiji la Tanga,lakini Bwana leo anafanya jambo jipya kama ambavyo
waimbaji wameimba katika wimbo wao. Ambalo linakwenda kuleta mabadiliko makubwa
na mapinduzi kwa waimbaji wote wa nyimbo za injili wa jiji la Tanga ambao kwa
muda mrefu uimbaji wao umekuwa wa kiwango cha kanisani kwao tu. Lakini sasa
jambo hili litakwenda kubadilisha mawazo yao na kuwafanya wajiandae kufanya
huduma hii kwa lengo la kimataifa zaidi. Ni kweli kwamba tumechelewa sana kuwa
na timu kama hii kulinganisha na mikoa
|
mingine iliyo juu kwa waimbaji wa nyimbo za injili Tanzania,lakini pia ni lazima tukubali kwamba sasa ni wakati wa Mungu kwa sababu pia timu hii isingeweza kuanza bila kuwepo watu walioandaliwa na Mungu kuisimamia Timu hii na sisi tunaamini kwamba wewe Mchungaji Singano Mungu amekupa jukumu hili akijua kwamba unaweza kuwalea vijana japo wanatoka katika katika makanisa mbalimbali na sisi tunakuahidi kukupa ushirikiano,utii na nidhamu ya hali ya juu katika kufanikisha maono ambayo Mungu ameyaweka ndani yako. |
|
Tunaposema chombo hiki kitakuwa ni ukombozi kwa waimbaji wa nyimbo za injili Tanga, tuna maana ya kwamba kitashughulika zaidi na huduma hii ya kusifu na kuabudu,kwa maana hiyo tutahakikisha zana zote zinazotakiwa kutumika katika huduma hii ya kusifu na kuabudu tunakuwa nazo na tunazimiliki wenyewe na tukizimiliki sisi ina maana waimbaji wote waliopo katika jiji hili la Tanga watanufaika nazo kwa maana ya kwamba watakuwa na uhuru wa kuvitumia kwa utaratibu ambao tutakuwa tumeweka ambao utakuwa nafuu zaidi tofauti na sasa ambapo vyombo vingi vinamilikiwa na makanisa na utaratibu wa kuvitumia kwa makanisa mengi ni mgumu sana, na hasa ukizingatia kwamba makanisa mengi vyombo vyao havijakamilika na kama ukitaka kupata seti iliyokamilika inabidi kuunganisha vyombo vya makanisa zaidi ya moja sasa hapo si kazi ndogo. |
|
Lakini pamoja na changamoto hizo tunapenda kuwashukuru watu wote ambao wanatupenda na kutuelewa nini tunachotaka kufanya na kwa namna ya pekee kabisa niwashukuru viongozi na washirika wa kanisa lako kwa upendo wanaotuonyesha na kuhakikisha wanatusaidia kila tunapokwama hata kama wewe haupo.
Tunashukuru kituo cha malezi ya vijana Novelty pamoja na kanisa la FPTC ambao tumekuwa tukitumia kanisa lao pamoja na vyombo katika matayalisho yetu.
Tunamshukuru Rev Steven Bombo wa kanisa la Elim Elim Pentekoste kwa kutupa nafasi ya kutumia vyombo pamoja na kanisa lake kwa mazoezi.
Tunamshukuru Rev na mama James GH Lee ambao wamekuwa karibu na sisi kutusaidia kila tunapokwama.
Tunamshukuru Mchungaji Bright Mashauri ambaye hata kwa sasa hivi mnamuona anaendelea kuchukua picha za kumbukumbu za tukio hili. Kwa ujumla watu wengi wameonyesha kutuunga mkono baada ya kujua nini tunachokifanya.
|
Kuhusu vijana ambao utawasimika leo ili waanze kufanya kazi
katika timu hii ni vijana ambao tumekuwa nao na tumewapima katika kipindi hiki
kigumu ambacho ni kama tupo kwenye giza,lakini tunawaonyesha vijana kwamba
wasihofu kuna nuru kubwa sana mbele,tunawapenda wanatupenda,wanatutia moyo
wakati mwingine tunakata tama kama mipango yetu haijakaa sawa lakini wao
wanatutia moyo kwamba tunapoona mambo magumu hapo ndio tujue kwamba kuna Mungu.
Kwa kweli sisi tumefurahi sana kuanza na vijana hawa wakati huu ambao tupo
kwenye giza, kwa sababu kuna wengine wanakuja wanachungulia wakiona giza
hawarudi tena, na sisi tunawasubiri wakija kwenye nuru tutawakataa. Hawa vijana
wamekuwa wakija kwenye mazoezi kwa kujitegemea na karibu wote ni wanakwaya na
wanategemewa katika makanisa yao,hivyo ni lazima wamalize kwanza huduma
walizonazo katika makanisa yao ndipo wautumie muda wa ziada kuja kwetu bure. Na
wengine wanalipwa na makanisa yao kwa huduma hii ya kusifu na kuabudu,lakini
wameona ni bora tukae gizani pamoja ili nuru itukute kwa pamoja,napenda
kukuhakikishia kwamba thamani ya vijana hawa kwetu itakuwa kubwa kuliko hao
ambao watakuja wakati timu imeanza kuwa na jina.
Kulingana na maagizo uliyotupa kwamba unataka timu hii isiwe
ya kufanya matamasha ya burudani bali iwe timu ya huduma,imebidi hata kazi ya
kuwachagua vijana hawa ifanyike kwa umakini wa hali ya juu kwa sababu
tunategemea timu hii ihudumu katika viwango vya kimataifa ndani na nje ya nchi
yetu kwa hiyo tunahitaji wawakilishi waliochaguliwa vizuri watakaoleta sifa kwa
waimbaji wa jiji la Tanga,nchi yetu na kwa Kristo,tunahitaji kuwa na vijana
wasiopungua 16 hivi lakini leo utawawekea mikono vijana tisa tu, ambao tayari
tumeshawapima kwamba tunaweza kuhudumu pamoja nao. Tumeandaa nyimbo kama ishirini
hivi lakini lakini leo tutaonyesha nyimbo chache ili na wenzetu wapate nafasi,
na baada ya ibada hii jukumu litakalofuata ni kujitambulisha sehemu mbalimbali
lakini pia na kuzitambulisha kazi zetu. Tunapenda ikiwezekana tungo zetu ndizo zitumike na watu wengi
katika sifa na kuabudu. Tunaomba ndugu zetu waimbaji ambao mko hapa tufahamu
kwamba tunahitajiana sana kwa sababu
sisi ni kama madereva wa kampuni moja ya Yesu,mwenzako akikwama njiani msaidie
au ukimkuta njiani amesimama unamuuliza tatizo ni nini kama spea msaidie
atakurudishia mbele hii ni kazi ya Mungu. Mwisho napenda kukuhakikishia kwamba
kazi hii itasimama kwa sababu si ya kwetu ni ya Yesu Kristo hata kama sisi au
wewe ukihama Tanga utaendelea kuwa mlezi wa timu hii.