Viongozi wa timu ya kusifu na kuabudu kutoka kushoto Dan Manimba, Elizabeth Yohanna na Furaha Mwakasege |
Baada ya kuwasimika waimbaji wa timu ya kusifu na kuabudu ya
mkoa wa Tanga,jukumu la kuongoza timu hii wamekabidhiwa viongozi watatu ambao
ni Ndugu Furaha Mwakasege yeye anakuwa ni mratibu mtendaji wa timu, Daniel
Manimba yeye anakuwa msimamizi wa ufundi na jukwaa na Elizabeth Yohana yeye
anakuwa msimamizi wa waimbaji wa kike katika timu. Akiongea baada ya kuwekewa mikono katika nafasi hiyo Daniel Manimba amemuelezea blogger kwamba anajihisi amekabidhiwa dhamana kubwa na atahakikisha anaitumikia kwa akili na kwa nguvu zake zote. Akiongea baada ya kumalizika ibada hiyo Mratibu wa timu hii furaha Mwakasege alisema kwamba muundo wa katiba unahitaji timu hii kuwa na mwenyekiti,katibu na viongozi wengine ambaoa kwa sasa bado hawajachaguliwa ila viongozi waliopo sasa hivi ni wa muda na ikifika wakati wajumbe wenyewe ndio watakaochagua viongozi wao. Akiwaweka mikononi mwa Mungu Mchungaji Singano amewaeleza watu katika ibada hiyo kwamba kwa majukumu yake kama mchungaji ni vigumu sana kwake kusimamia kikamilifu timu hii,ndio maana anawaweka viongozi watakaomsaidia.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni