Ijumaa, 30 Agosti 2013

KIFO CHA MOSES KULOLA NA SWALI GUMU

ukitaka kujua kwamba bado nchi yetu iko kwenye giza kubwa sana la kiroho ni wakati huu ambapo nchi yetu imepoteza mojawapo kati ya majemadari wakuu wa injili katika nchi Yetu.Ninamzungumzia mzee wetu Askofu Moses Kulola, hii habari niliisikia nikiwa ndani ya gari na nikathibitisha kupitia katika mitandao
Marehemu Mkieto "Sharo
milionea" akiwa na MC katika shughuli zake za sanaa


Askofu Moses Kulola akiwa katika kazi ya Mungu
michache ya kijamii, hata watu wa familia yangu nilipowauliza wanafahamu nini kimetokea kuhusu Askofu Kulola waliniambia hawajui kitu, hiyo ilikuwa ni karibu ya saa mbili usiku. sasa kilichonishangaza ni pale wanapokufa wasanii,hata kama ni wadogo kiasi gani habari hutembea haraka sana na vyombo vyote vya habari hujikita hujielekeza huko mfano kifo cha marehemu Steven Kanumba au kifo cha kijana wetu wa Muheza Sharobalo habari zao zilivuma kuanzia dakika ile ambayo ameanguka sasa hii inakuwaje kwa watu waliofanya kazi ya kulibadilisha Taifa na kulielekeza katika kumjua Mungu kama huyu mzee wetu, ndio maana nauliza uzito wa kifo cha Askofu Moses Kulola  unazidiwa na kifo cha Sharobalo?
 katika nchi yetu sasa hivi kazi anayofanya mzee wangu King Majuto inathamani kubwa sana kuliko kazi wanayofanya watumishi wa Mungu,ukiona hivyo ujue tupo katika taifa ambalo hatujitambui jinsi tulivyo wala hatujui wajibu wetu katika nchi yetu.
Mwalimu C Mwakasege
 ndio maana wahubiri wakubwa kama Askofu Zakaria Kakobe alionekana kuthaminiwa zaidi katika sehemu mbalimbali alizokwenda kuliko heshima ambayo alikuwa anapewa hapa nyumbani,hii yote ni kwa sababu tupo kwenye giza nene
Askofu Zacharia Kakobe sasa hivi haonekani nchini yupo zaidi nje ya nchi akitumika huko.

Marehemu Steven Kanumba ambaye msiba wake uliitikisa nchi kiasi kwamba barabara za Dar es salaam zilifungwa,wengi walifananisha msiba wake ulitpitwa kidogo na wa Rais wa kwanza Mwalimu JK Nyerere

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni