Aina gani ya muziki wa injili unafaa makanisani?
Naomba
nianze kwa kuwapongeza na kuwaombea baraka nyingi za Mungu watumishi woote
ambao wanamtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji. Mungu azidi kuwainua na kuumba
kitu kipya ndani yenu kila siku. Kazi yenu inatuinua na kutubariki sana na kwa
kweli inachangia sana katika kulikuza kundi la Bwana.
Mara
nyingi nimekutana na watu ambao wamesema kwamba muziki wa injili au muziki wa
kanisani umeingiliwa na mamluki kibao na unakuwa hauna tena utukufu wa Mungu.
Mimi sipingi na wala sikubali kirahisi pia!! Lakini ninaomba wapendwa
tusaidiane katika jambo hili. Kwa kuwa huwa tunakuwa wepesi sana kusema kwamba
baadhi ya midundo (beats) kama Taarab, Reggae, Rap, Rock n Roll n.k haifai
kwenye injili basi ninaomba tujue ni aina gani ya mdundo(beat) inayofaa kwenye
muziki wa Injili?
Kwamba
ni slow Rock, jazz, ballad, March, zouk n.k Nadhani hii itakuwa ndio solution
ya malumbano yooote. Tukumbuke kwamba hapa nimeongelea aina ya muziki
nikitegemea kwamba mashairi katika muziki huu yaani lyrics ni za kumtukuza
Mungu pekee. Naomba tusaidiane katika kuujenga mwili wa Kristo! Ndimi Mshirika,
Lameck
Mimi nadhani muziki wa
injili hasa katika nchi yetu ya tanzania unaacha mwelekeo kwani wengi wanaimba
kwa ajili ya biashara kiasi kwamba wanaugeuza muziki wa injili kama ni muziki
wa dansi. Mungu alisema nisifuni kwa zeze na vinubi kwa kuimba na kucheza
lakini sasa watu wanaiga beats za miziki ya dansi kiasi kwamba maana na ujumbe
katika muziki wa injili unapotea. Tusimtukuze mungu kwa kutaka kuonekana kwenye
luninga na kwingineko bali tumtukuze mungu kwa moyo na tulihimidi jina lake
siku zote.watu wanaimba muziki kwa kutuma ujumbe wa masengenyo nadhani si
mahali pake.muziki wa injili ni ujumbe kwa jamii kutoka katika biblia na si
vinginevyo
Asante saana kwa mada hii njema. Naamini inagusa wengi na ni swali ambalo
limekuwa likiulizwa na wengi.
Narejea niliyosema kwenye “post” ya MAKOMA miezi kadhaa iliyopita kuwa muziki ni asili, na suala la wapi unaonekana ni wa kimataifa yategemea wanapata na kutumia miziki hiyo kwa namna gani. Mfano ni kwamba ukienda Jamaica na kusema huwezi kumuimbia Mungu kwa midundo ya reggae hutaeleweka, kama ambavyo utaenda Congo ukasema midundo yao ni ya kimataifa. Lakini kwanini twaamini kuwa midundo kama ya kikongo ni ya kimataifa? Ni kwa kuwa kwetu ilianza kuja ikiambatana na mashairi yasiyo ya kiMungu na hilo (kama yalivyo mengine mengi) LIKARIRIWA kuwa ni muziki wa kiMataifa. Lakini sidhani kama ukiweka nyimbo zinazoheshimika na kupendwa na kukubalika zaidi Tanzani na kuzicheza Israeli, ama Marekani ama Carribean ama Amerika ya Kusini utapata jibu la huo ndio muziki wa injili.
Narejea tena kuwa TUMEKARIRISHWA VIBAYA kuwa kuna midundo ya kumtukuza Mungu. Hili si sahihi, maana midundo mingi ina asili na kote wanaitumia kumtukuza Mungu. Hivi mmeshaona wasanii nyota na wanaoheshimika kwa muziki wa Injili hapa Marekani wanatumia midundo gani? Ingia you tube utafute kina Kirk Franklin ama Yolanda Adams ama Bobby Jones ama familia nzima ya kina Winans (kwa pamoja ama mmoja mmoja) uone wanatumia midundo gani. Kuanzia Mdumange, Chakacha, Taarab, Hip Hop mpaka REGGAE ni midundo inayokubalika katika kueneza injili. Matumizi kuendana na jamii ni muhimu lakini si makosa kuitumia.
Blessings

Kitu chochote
tunachofanya watu wa Mungu ikiwa ni pamoja na kwaya, lazima kimtukuze Mungu, na
pia hata wasioamini wasiwe na neno kwacho tunachokifanya. Maandiko yanasema,
“Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na mafarisayo, hamtaingia kamwe
katika ufalme wa mbinguni”, Mathayo 5:20.
Iwapo watu wasioamini,
wanaweza kufanya mambo mazuri yanayohusiana na imani zao kwa kukwepa kukwaza
wengine, si zaidi sana sisi tunaosema kuwa tunamjua Mungu? Iwapo hatutaweza
kuwazidi hao, maandiko yanasema hatutaurithi kwamwe ufalma wa Mungu. Kama watu
wa Mungu tunapaswa kuliangalia hilo.
Watu wengi wenye nia ya
kumtafuta Mungu, wanashindwa kuuamini wokovu, kwa sababu tu ya mambo yetu mengi
tunayoyafanya katika ucha Mungu wetu ambayo hayana ushuhuda. Mambo hayo ni
pamoja na hizo kwaya zinazoimbwa nyakati hizi n.k. Siku hizi nyimbo za kwaya
tunazozitunga tunazitunga kwa kutazama tu jinsi sisi tutakavyopendezwa kwazo,
hatutazami jinsi wasioamini watakavyoziona na kutuelewa!. Hatuangalii upande wa
pili, na hiyo ndiyo sehemu ambayo shetani anapata goli kwetu.
Kuna namna nyingi tu na
nzuri za kumwimbia Mungu, na kila mtu hata asiyeamini akaweza kusema kweli kuna
Mungu eneo hilo. Namna hizo si lazima ziigizwe kwa mtindo wa tamaduni yoyote
duniani. Tukiwa katika Roho katika kuimba, tunaweza kufanya namna zetu za
kuimba zikawa moja duniani kote. Kinachotatiza sasa hivi ni kwa sababu, watu
wanampenda Mungu na hapo hapo bado wanaipenda dunia, namna hiyo lazima
tutachanganya tu, dunia na ya Mungu.
Nakumbuka kuanzia
katikati ya miaka ya themanini na kuendelea, kulikuwa na kwaya moja ya
Ulyankurlu Tabora, nyakati hizo nilikuwa sijaokoka bado, niliipenda sana ile
kwaya, na niliinunua kanda yake ya kaseti.
Kununua kwangu kwa ile
kanda hakukuwa kwa sababu ya kuburidika, bali kwa sababu ya ujumbe na umakini
wa kiroho uliokuwemo katika kanda ile. Japo mimi nilikuwa si mtu wa Rohoni
nyakati hizo, lakini kila nilipokuwa nasikia nilikuwa naguswa! Kutokana na
jinsi nilivyokuwa mtu wa dini, ilikuwa si rahisi kuikubali kanda ile na nyimbo zake
kama ingekuwa kama zilivyo kanda za nyimbo za nyakati hizi zenye vionjo vya
miziki ya kidunia.
Kwaya ile kwa kweli kwa
wale wanaoifahamu, watanielewa ninachokielezea, ilikuwa ni kwaya ambayo haikuwa
na vionjo wala utamaduni wowote wa kidunia, lakini ilipendeza na iliweza kuliza
watu, hasa kwa wimbo moja uliokuwa unajulikana kwa jina la, “Wakati ule wa
Nuhu, watu walimwasi Bwana”. Je, nyakati hizi ndiyo haiwezekani kuwa na kwaya
kama zile? Je hatuoni kuwa tunazidi kuporomoka na kuingia anga jingine kiroho?
Ukiangalia hali halisi,
inaonesha kuwa watu wasioamini wanaufahamu sana wa mambo ya Mungu kuliko sisi
tunaosema tumeokolewa. Tunapingana na kila Neno jema la Mungu na kuweka ya
kwetu wenyewe.
Ninavyofahamu mimi
kuimba, ni kwa ajili ya kumtukuza Mungu, na wala si kwa ajili ya kuwafurahisha
wanadamu wanokuwa wanasikiliza au kuona kimwili. Kama ni kuwafurahisha hao
wanadamu, basi ni kuwafurahisha kwa kuwafanya kufikia toba kwa nyimbo
tunazoziimba.
Nyimbo zinapaswa
kuheshimiwa na kuogopwa na watu wasioamini kama wanavyoyaheshimu na kuyaogopa
mahubiri ya watumishi wa Mungu. Iwapo watapata neema ya kusikiliza basi wafikie
toba kama vile wamesikia mahubiri.
Mahubiri mengine ya
watumishi wa Mungu, yanaheshimiwa na kuogopwa kusikilizwa hata na watu
wanaodhaniwa kuwa wameokoka. Wanayaogopa wasije wakayasikia na kuelewa, na
wakabadili misimamo yao ya mafundisho yao ya awali. Iwapo katika mahubiri ya
Neno la Mungu kuna nguvu kiasi hicho, kwa nini nyimbo zetu za kwaya nazo zisiwe
na nguvu ya Mungu kama ilivyo katika mahubiri hayo?. Bila shaka kwaya zetu
zingekuwa hivyo, shetani asingekuwa na nafasi kabisa ya kulichezea Kanisa la
Mungu?
Shalom watu wa Mungu,
huo ni mtizamo wangu kuhusiana na mziki unaopaswa kuwa makanisani!. Tuendelee
kuelimishana.
4.
Wow! Nimependezwa na maelezo ya Kaka Bernard. Lakini bado
nadhani swali linabaki lilelile kuwa AINA GANI YA MUZIKI WA INJILI UNAFAA?
Ulyankulu ilikuwa kwaya bora na itaendelea kuwa kwenye historia. Lakini bado
nasema kuwa muziki ni asili na unatokana na mahali ulipo. Unless kama Kaka
Godlove angesema kanisani wapi (kama ni Tanzania ama Dar ama mahala fulani)
siwezi kusema kuna aina ya muziki ambao ni kwa ajili ya injili.
Ninalomaanisha hapa ni kwamba ukienda nchi nyingine huo muziki wa Ulyankulu hautakuwa akilini mwao na kama muziki pekee toka Tanzania ma awa midundo hiyo wanaoufahamu ni wa kimataifa, basi na huo utakuwa wa kimataifa.
Kwa hiyo kama twazungumzia wa Injili duniani basi hakuna muziki maalum, labda muziki wa aina fulani kulingana na mazingira ya wananchi wa eneo hilo.
Amani kwenu

Mimi nafikiri Inategemea
na mtu mwenyewe anavyoguswa ki imani, Mimi ninakisikiza nyimbo za kwaya za
zamani ambazo zilikuwa hazitumii hii mitindo ya sasa naguswa sana , hizi
zinazopigwa kama muziki wa dansi nafurahia ala zake lakini kiimani hazinigusi
sana, kutokana na kwamba nimekuwa sana kwenye muziki wa dansi na ninashindwa
kuzitofautisha kabisa kwenye mawazo yangu
Labda kutokana na umri
au sababu sijajengeka sana kwenye wokovu, lakini nikiangalia kwa vijana wadogo
wao kama wamekulia kwenye muziki tuu huu wa dansi sidhani kama wanaweza kuguswa
na muziki usio wa mitindo ya dansi
Kitu kingine ni uvaaji
na uchezaji ukishaafanana sana inakuwa vigumu sana kwa watu kutofautisha muziki
wa dini na wa dansi
Hivyo Makanisani kwangu
mimi ni kuangalia wana watu wa aina gani, ndiyo maana kwenye makanisa
zamani(sijui kuhusu siku hizi niko nje kwa muda), kulikuwa na kwaya ya Vijana
na Kwaya Kuu, kwaya ya vijana ilikuwa inatumia ala za kisasa na Kwanya kuu
ilikuwa wanaaimba sana sana kutumia Kinanda
Huu ni mtizamo wangu tuu
Kwanza nizungumze kidogo kuhusu waimbaji, na waandishi wa nyimbo za injili.
Kutokukuwa kiroho kwa waimbaji na waandishi wa nyimbo za injili kumefanya
nyimbo za injlili zionekane tuu kama mdundo na sio injili kama tunavyodhania.
Leo hii mtu anaokoka na kipaji chake cha kuimba, hapo hapo utamsikia ametangaza
concerts, sasa unategemea mtu huyo afanye vitu gani jukwani ama kanisani? Si ni
uzoefu wake tuu wakuwafurahisha watu, japo utasikia haleluya yuma yake!!!
Ninapo zungumza hilo, ninauhakika maana na mimi pia ni muimbaji wa nyimbo za
injli. Nimekuwa mwalimu wa kwaya miaka mingi na kwambia nimeona mengi sana.
Siku ya kwanza mtu anafika kanisani, kinacho mvutia tuu ni kujiunga na kwaya na
kuwa muimbaji maramoja, hata nikaweka sheria kwenye kwaya kwamba mtu atafanya
mazoezi kwanza miezi sita kabla aanze kuimba mbele ya kanisa, nikaomba
mchungaji wa kanisa aweke kwenye agenda kila week mafundisho yawaimbaji
wanaotaka kujiunga na kwaya ili wafundishwe huduma ya uimbaji ni nini. Hayo
yalifanya watu wasikimbilie sana kwenye kwaya maana uimbaji sio takataka.
Ninapowasikiriza waimbaji wengine nchini Tanzania, hata sehemu zingine,
nashindwa kuelewa kwamba wamefundishwa na wachungaji wao huduma ya uimbaji ni
nini. Kama kwaya ya Ulyankulu iliweza kubariki watu kwa nyimbo zao miaka ile,
ni kwasababu ya kanisa lao lilowaelekeza hata na kuwawekea mipaka ili huduma
yao isiingiliwe na ibilisi. Sasa swali ninalo jiuliza, je wachungaji wa siku
hizi wanayo mamlaka kwa waimbaji? Wengi hao waimbaji wameanguka na kurudi nyuma
baada ya kufanikiwa katika huduma hiyo, yote hayo ni kwasababu hawajafundishwa
vizuri kabla ya kujiingiza kwenye uimbaji. Mdundo wa nyimbo, hutokana na jinsi
mtu amepata wimbo. Kama umefunuliwa maneno ya wimbo, hakika na beat ya wimbo
huo itaenda sawa na maneno ulioyafunuliwa. Malanyingi sana unapofunuliwa wimbo,
unafuliwa melody ya wimbo huo. Zipo nyimbo zingine zinazotungwa juu ya wazo fulani
mtu amekuwa nalo, na hapo ndipo hatari ilipo sasa. Maana nyimbo hizo unakaa na
kutafakari lipi la kufanya ili wazo lako liweze kufanikiwa. Ndio maana muimbaji
anajikuta ametafuta kuiga midundo ya nyimbo alizowahi kuzisikia ama
anazosikiriza zilizoleta mafanikio kwa watunzi na waimbaji hao. Mala nyingi
nyimbo hizo zinakuwa za kidunia. Na wengi hao waimbaji hawanamda wa kukaa na
wapigamziki wao ili wa buni kitu kipya, huwa wanaenda kununuwa beats hizohizo
na wanaweka maneno yao. Hilo linasababisha mtu atakaposikiriza wimbo huwo
hakiri yake yote itaishia kwa mtunzi wa mziki ule, na hataweza kusikiriza
ujumbe uliomo.
Suala hili lizungumziwe ili tuweze kujifunza kwa undani, shetani asituweze kwa nyimbo tunazoziimba na kuzitunga kwa midundo tofauti.
Suala hili lizungumziwe ili tuweze kujifunza kwa undani, shetani asituweze kwa nyimbo tunazoziimba na kuzitunga kwa midundo tofauti.
Mziki ni mziki tu
hakuna chakusema kama miziki ya ki 80′s ina nguvu/upako wa roho sana kushinda yakileo. Hata iwe reggea na mingine midundo tofauti it doesn’t matter, what matters is
hakuna chakusema kama miziki ya ki 80′s ina nguvu/upako wa roho sana kushinda yakileo. Hata iwe reggea na mingine midundo tofauti it doesn’t matter, what matters is
Watu wengi sasahivi
wanaimba kwakupenda kujionyesha, wapenda sifa (kuabudiwa) watu hatujui tena
maana ya uimbaji wa nyimbo za injili na tunapokua katika hali kama hii ni
vigumu sana kwa kuongozwa na Roho wa Mungu, na nyimbo zetu zinakua hazina upako
wa Roho mtakatifu, wala hazina Nguvu kama mahuri ya watu wa Mungu wengine
Haijalishi aina gani ya
mziki/mdungo bali uhusiano wako na Roho wa Mungu.
Isaack:)
Kwa upande wangu mimi
nafikiri uimbaji unatakiwa ufanyike kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu,haijalishi
muziki utakuwa katika mahadhi ya Leggae,Rhumba,Rap n.k.Kama tukisema kwamba
muziki uliopigwa katika mahadhi ya Leggae au Rhumba si wa ki – Mungu tutakuwa
tunakosea.Mtu anaweza akaimba muziki ambao kwa kuusikiliza ukaonekana ni wa Ki
– Mungu lakini hauna mguso wowote Kiroho.Kwa upande wangu naweza kutoa mfano wa
nyimbo za Marehemu Angela Chibalonza,ni nyimbo zilizo katika mahadhi ya
Kikongo.lakini nikizisikiliza kwa upande wangu naona zina nigusa ki –
kwelikweli.Na pia kuna nyimbo nyingine inaweza kuimbwa kwa Taratibu (Nyimbo ya
kuabudu) lakini isilete mguso wowote Kiroho.Kwa hiyo kwa upande wangu nafikiri
inategemea na Jinsi Roho Mtakatifu atakavyopenda.Nakubaliana moja kwa moja na
Mpendwa pale juu Mubelwa T.Bandio.
N:B.Hiyo ni kwa upande
wangu jinsi nionavyo.Itategemea Roho Mtakatifu atakavyokuongoza wewe
binafsi,Ndio maana kuna Makanisa mengi,mengine watu wanaimba wamesimama
wima,yapo kwa ajili ya wasiopenda kurukaruka..MUNGU ATUTIE NGUVU..
Ndugu zangu naamini
hakuna kanuni ya namna ya kumwimbia ama kumtukuza Mungu.Maswali yanakuja pale
tunapoona kuwa mtu anaimba ama kutukuza asichokijua, anachoimba ni kinyume na
maisha yake, wanaimba kwa ajili ya wanadamu na siyo Mungu maana wanafanya
biashara.
Matunda ya kazi yao ni
kuleta Babeli, yana kupotosha kweli.Uimbaji wa injili kwa sasa una malengo ya
kutajirisha waimbaji wenyewe na siyo kumtukuza Mungu, utitiri wa waimbaji
unazidi kuleta upotoshaji, hakika thawabu yao ipo tayari.
Kuguswa kwa wengi
kunakoelezwa hakuhusiani na Mungu bali hisia zao ndiyo maana hakuna mabadiliko
endelevu.
Ndugu zangu Mungu bado
anatafuta watakao mwabudu Mungu katika roho na kweli, jihoji wenyewe ni nani
anafanya hivyo.Ujisijidanganye.
Mtu yeyote anayeimba na
kuuza anachoimba tayari amepotosha maana ya anachokiimba. Tena nawaonya waache
upuuzi huu mara moja.
Ni wapi katika Biblia
imeandikwa uimbaji ni huduma inayojitegemea? Ni wapi uimbaji unauzwa katika
Biblia?
Tena tusijidanganye;
hata mtu anayenunua nyimbo naye ameingia katika mchezo wa hujuma ya kweli ya
Kristo na maana ya kumwimbia na kumwabudu Mungu.
Hii sumu ya kujinufaisha
imeenea sana.Mtu anayeimba na kuuza nyimbo zake hamjui Mungu na haujui mwili wa
Kristo.
Namna ya uimbaji na
vyombo gani si la msingi zaidi ya maana na kusudi la uimbaji wenyewe.Huyu ni
shetani mwenyewe!
Kadri uimbaji huu wa
sumu unavyoendelea ndivyo hali ya maadili na hofu ya Mungu inavyopungua maana
Mungu hayupo katika uimbaji huu.
Na siyo uimbaji tu bali
hata mahubiri mengi.Sumu naweza kusema imeanzisha USA na kuenea kwa kasi sana
duniani kote. Utungaji wa vitabu vya kiroho na kuuza, video na cd.
Tunatengeneza mamilionea kwa kuupotosha ukweli na uhalisia wa Mwili wa Kristo.
Uchafu umehamia
kanisani.Je, huoni? Mwahoji vyombo na namna ya uimbaji?
KAMA HATUTAITA DHAMBI
KWA JINA LAKE BASI TUMEPOTEA.
LAZIMA TUKEMEE SUMU HII
YA UTUMISHI WA MANUFAA BINAFSI NA KUWA BARAKA KWA WOTE.KAMWE TUSIUMEGE MWILI WA
KRISTO.NDUGU ZANGU MAMBO YATAKUWA MAGUMU ZAIDI SIKU ZA USONI NA MTAONA USHAHIDI
WA UOVU WA WAIMBAJI HAYA MAANA ITATHIBIKA JINSI WASIVYOMJUA MUNGU.
BWANA AWE NA ROHO YAKO
Amani, Heshima na Upendo kwenu nyote.
Nafurahia saana jamvi hili kwa kuwa linaelimisha na kutoa maoni mbalimbali kulingana na uamini wa mtu. Kaka Fred hapo juu amenikumbusha hadithi ya mtu ambaye alisema “KAMA HUTAKI WAKUONE WEWE FUMBA MACHO” akimaanisha kuwa kama huwaoni basi hawakuoni japo si sahihi. Nimefurahia na NINAHESHIMU mawazo ya ndugu Fred hapo juu lakini kusema kwamba “Mtu yeyote anayeimba na kuuza anachoimba tayari amepotosha maana ya anachokiimba. Tena nawaonya waache upuuzi huu mara moja.Ni wapi katika Biblia imeandikwa uimbaji ni huduma inayojitegemea? Ni wapi uimbaji unauzwa katika Biblia?” na kusema “Mtu yeyote anayeimba na kuuza anachoimba tayari amepotosha maana ya anachokiimba. Tena nawaonya waache upuuzi huu mara moja.” nina wasiwasi kama tafsiri yako si kwa kuwa umefumba macho. Si kila aimbaye na kuuza anakuwa na malengo ya kujinufaisha. Yaonekana ndugu yangu wafuatilia saana Biblia na pengine kama kuna unaweza ku-mention waliposema kuhusu kuwalipa wachungaji mishahara ama kuhusu watu kulipia huduma kama hizi unazotumia kuwasiliana na sote ulimwenguni ama kuchangia huduma za kusambaza injili kwa wasioijua huko kwenye kazi za kimisionari na mengine mengi yanayoendelea katika mzunguko mzima wa uenezaji injili sasa ungesaidia kuyataja. Unaposema kanda zisiuzwe kwa kuwa haijaandikwa kwenye biblia napata shaka na imani ama tafsiri yako ya BIBLIA. Kumbuka Biblia haisomwi kama kitabu cha Algebra na kutafsiri kila usomacho bila kukumbuka kuwa Yesu mwenyewe aliongea kwa mifano kunaweza kukuweka kwenye nafasi ambayo ukajikuta mkosolewa badala ya mkosoaji.
Ni kweli kuwa wapo watu wanaofanya BIASHARA ndani ya neno la Mungu. Na ni kweli kuwa hata baadhi ya wachungaji feki wanafanya hivyo na nina mifano kamili ambapo kuna kanisa niliwahi kuhudhuria tukaambiwa tutaombewa na urefu wa sala utategemea na kiasi cha dola unachoweka kwenye pesa ya maombi. Sikurejea tena. Kwa hiyo ni kweli kuwa wapo, lakini si kweli kuwa akishauza kanda basi ni “mpuuzi”
NO. NO. NO.
CHANGAMOTO YANGU KWAKO NDUGU FRED ni kutaja nyimbo tatu ama za wanamuziki angalau watatu unazoona ni za injili kwelikweli na kisha uniambie kama hawakugharamika kuzitengeneza na hawakurejesha gharama hizo.
Kama utataja za wasanii watatu basi ujue kuwa ulizisikia na zikakugusa kwa kuwa kuna mtu alilipia utengenezaji na usambazaji na ndio maana ukabarikiwa nazo na kama huna basi hauna cha kuchangia pia maana huna unalopenda katika muziki wa injili.
Nadhani unastahili kuwaomba watumishi msamaha kwa kuwaita wapuuzi

Of coz Ndg Fred hapo umesema chamaana
tusiende mbali. Nakumbuka mimi mara ya kwanza nimepewa kuongoza nyimbo ya kuabudu kanisani heheee, nakwambia ilikua balaa!! kwanini coz nilikua bado sijakamilika na nilikua sijui nini maana ya kuabudu. So it depends actually on who is singing

Mungu awe nanyi Ndg
zangu:)
12.
Ndugu zangu,
Bwana Yesu asifiwe!
Na mimi nimeona nitoe mchango katika hili. Kutokana na muda kuwa mfinyu, nitakuwa very brief, lakini nitajitahidi kufikisha kile Roho anatamani kiwafikie!
Bwana Yesu asifiwe!
Na mimi nimeona nitoe mchango katika hili. Kutokana na muda kuwa mfinyu, nitakuwa very brief, lakini nitajitahidi kufikisha kile Roho anatamani kiwafikie!
Moja, lazima tujue kuwa
shetani alikuwa ni Kerubi Afunikaye: ambaye ni Muziki unaoishi! Lakini pia
lazima tujue kuwa baada ya anguko shetani aliharibu hekima yake, ikiwemo pia
uimbaji. So Lazima alitengeneza namna ya muziki wake. Baada ya hayo, ningependa
niende kwenye Jibu la swali la brother Godlove kama ifuatavyo:
Kwanza lazima
tukubaliane, muziki wa injili si jina sahihi, bali ni muziki wa kumsifu Mungu.
Muziki huu wa kumsifu Mungu ni kwa ajili ya kumsifu Mungu. Pili lazima
tukubaliane kuwa, Mwili wetu ni rafiki mkuu wa shetani. Hata Yesu mwenyewe
alishindana na mwili wake kuelekea Kalvari. Tatu Lazima tukubali Mungu siku
zote huweka tofauti namna anavyotaka tumwabudu, na siku zote huwa ni tofauti na
mungu wa dunia hii. Na Mwisho lazima tukubaliane kuwa, tunaelekea katika siku
za Babeli, Nuhu na Sodoma & Gomora; zikiwa ni dalili za kurudi mwana wa
Adamu. Uamsho wa upagani sasa upo juu mno na unavamia kanisa kwa kasi ya ajabu!
1. Muziki wa kumsifu
Mungu, lazima uiinue roho yako imsifu na kumwabudu Mungu. Muziki ambao
utakufanya uanguke mbele za Mungu wako, na kujiona namna gani ulivyo mwanadamu
asiye kitu na jinsi yeye alivyo Mungu mtakatifu. Ni muziki unaokufanya uone
huruma na rehema za Mungu na kukufanya umsifu kwa aliyokutendea. Ni maelezo
marefu lakini natumaini mmenielewa.
Muziki ambao unauamsha
na kuutia mwili tashwishi ili ujifurahishe na kuruka na kumweka Mungu pembeni,
huo ni wa dunia bila kujali mashairi yake. Muziki wa kumsifu Mungu ni kwa ajili
ya Mungu na si vinginevyo. Muziki ambao kazi yake ni kuufanya mwili ujisikie
vizuri, si muziki wa sifa kwa Mungu wetu.
2. Muziki wa kumsifu
Mungu huimbwa kwa kicho cha hali ya juu. Ni muziki ambao wanaoimba wanajua ya
kuwa Mungu wanayemwimbia ni Mungu mtakatifu. Kuna kipindi nilikuwa nasikiliza
muziki fulani nyumbani, na kuna ustadhi mmoja akasema “mziki huu kweli ni wa
Mungu na huyu jamaa anamwimbia Mungu. Huu mziki hauwezi kupigwa baa.” Imagine!
Ni kwa sababu mwimbaji, vyombo vilivyopigwa na wimbo wenyewe, vilikuwa na kicho
cha Mungu.
3. Muziki wa sifa una
lengo la kumwinua Mungu pekee na si mwanadamu. Mungu hachangii utkufu na awaye
yeyote. Kwa hiyo Muziki wa sifa ni kwa ajili ya kumwinua Mungu na si mwanadamu.
Kila jambo linalofanyika, kila neno linalotamkwa lazima yawe na utukufu kwa
Mungu. Muziki unaomwinua mwanadamu, awe mwimbaji au wasikilizaji, huo si muziki
wa kumsifu Mungu
4. Balance ya vyombo vya
Muziki. Wasomaji wa Biblia wanajua kuwa ngoma (Drum Kick) haipo katika Biblia.
Hii inaleta maana unapojua kuwa ngoma ipo kwa ajili ya kuongoza vyombo vya
muziki viende pamoja (sync.) Sasa pale ngoma (Drum kick/ryhthm) inapokuwa juu,
huu unakuwa si muziki wa kumsifu Mungu bali ni Ngoma za kupandishia majini.
Fikiria, kwa nini Mungu hakuweka kick ktk listi ya vyombo vya muziki kwenye
Biblia? Ni kwa sababu ngoma ina nguvu ya kuuamsha mwili na kuusisimua. Ngoma
ikiwa juu na ya kasi, mtu anaweza kuwa high, akafanya jambo lolote. Kama
ingetokea mwimbaji yeyote /producer akafuata standards za Mungu, na kupanga
vyombo ambavyo Biblia imeagiza, huo muziki utakaotoka utakuwa “heaven class”
music! Ninachosema ni kuwa Biblia inautambua muziki katika melody na si rhythm.
4. Muziki wa kumsifu
Mungu lazima uwe sahihi kibiblia. Nyimbo zote, lazima zipatane na Biblia kwa
asilimia mia moja! Kinyume na hapo ni muziki wa shetani, maana utauita jina
gani muziki unaoimbwa huku maneno yake yakipingana na Biblia?
5. Mwisho, kutokana na
wakati, Muziki wa kumsifu Mungu lazima usiambatane wala ku-promote utamaduni mwingine
wowote ule. Tafsiri ya utamaduni ni namna nzima ya maisha. Hii inajumlish namna
ya kuvaa, kuongea, kuabudu n.k. Yesu alipokuja duniani, alianzisha namna mpya
ya maisha, utamaduni wa Kikristo. Ndio maana mtu akimgeukia Kristo, anageuzwa
kwa Roho wa Kristo, kufuata utaratibu huu wa maisha, wa raia wa mbinguni.
Baada ya kusema hayo,
muziki wa kumsifu Mungu, ni lazima u-promote utamaduni wa Kikristo kama ambavyo
umeainishwa ktk Biblia. Naomba nitaje kwa ufupi baadhi ya muziki na tamaduni
zinazokuwa zinahubiriwa na aina husika ya Muziki ambazo haziwezi kuwa Muziki wa
kumsifu Mungu, hata kama tutaongeza viambata kama Jesus.. au Gospel.. n.k:
–> Reggae —- Urastafari
–> Rap —- Hip Hop
–> Taarab — Utamaduni wa pwani(Samahani kama hujaishi pwani, sina muda wa kuelezea)
–> Rock n Roll — Ushetani na Uabudu Shetani(satanism & Devil worship)
–> Muziki wa kizazi kipya — Vuguvugu la enzi za zama mpya (The New Age Movement)
–> Ngoma za asili — dini za asili za kabila husika (Nyimbo za kutambika, za mavuno n.k)

Listi ni ndefu, lakini
natumai kwa mwongozo mfupi sana hapo juu, unaweza kupata picha, muziki wa
Kikristo unafananaje.
CHANGAMOTO:
(a) Hebu fikiria Yesu akiwa katikati ya kundi la makutano. Kabla ya kuanza kufundisha, Petro akasimama na kuchana mashairi kadhaa ya rap na kisha Mary magdalene akashusha gospel R n B la nguvu, kabla ya Yohana kuwanyanyua makutano wakatengeneza duara kisha wote kwa pamoja… vidole juu. Baada ya watu “kusifu na kuabudu” Yesu akaanza kufundisha…Think about that!

(b) Paulo na Sila
walifungwa gerezani. Katikati ya usiku, ghafla Paulo akalianzisha Gospel reggae
la nguvu, na alipomaliza Sila akadakia na Gospel Ragga Muffin, kabla Paulo
hajarudi tena na Gospel Hip hop akichana verse na Sila akipiga Chorus. Wakati
wafungwa wanashangaa shangaa, Sila akanzisha ngoma za kigiriki huku akihubiri
kwa hayo mashairi, na kisha Gospel sebene la nguvu, kabla ya Paulo kumalizia
session ya Sifa, huku akifuta jasho kwa taarabu la nguvu…hapo ndipo Mungu
Yehovah akalitikisa gereza na kufanya jambo ambalo liliacha milango wazi, pingu
zikaachia…..Think about that!
(c) Yehoshaphati
alikabiliwa na vita ngumu na baada ya maombi alitakiwa atangulize vikosi vya
waimbaji. Na hivi ndivyo mfalme alivyoamuru: Mstari wa mbele, Gospel Hip hop
kisha Gospel sebene, halafu Gospel Rock n Roll na reggae. Walipoanza Ku-rock na
Ku-roll, Bwana akaweka waviziaji na akawaua maadui zao wengi…blah blah…Think
about this!
Bwana Yesu atusaidie,
maana la sivyo; siku hiyo tutakuwa na kesi nyingi za kujibu mbele yake!
Neema ya Mungu na izidi
kwenu watakatifu wake
Ndugu zangu naomba
tusiingie kwenye hukumu bila sababu, narejea tena kusema kwamba lazima tutambue
majira tuliyo nayo na kwamba ikiwa hatuna amani juu ya kitu tutulie na
kutafakari na Bwana kabla ya kupiga hatua.
Kwamba nimeandika
haimaanishi natoa maoni kwa kuwa naamini kuwa nami nina roho.
Theolojia ndiyo imezaa
haya yaliyoleta mada hii nami huko siko bali katika kweli yote.
Ndugu zangu hapa
tujikumbushe NAMNA YA KUMWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI.Ukiona unahisi
kumtumikia Mungu na huna zana za kumtumikia ujue saa bado, ukitumia nguvu zako
kutimiza unayodhani ni maelekezo ya Mungu utaishia pengine.
Dhamira yangu iko huru
na sijahukumiwa kwa niliyoandika. Nina ujasiri kwa kilichoandikwa.
Ndugu zangu kuna mengi
yanayohitaji uharaka katika utekelezaji, machache niliyataja katika mada
iliyopita. Ushahidi wa kutotambua majira ni mwendelezo wa maelezo yanayompa
ibilisi nafasi.
Mtumishi wa Mungu
atakayehisi ametukanwa na ujumbe nilioandika na atafakari vema kuhusu kazi yake
na amhoji Mungu kwa kina kisha atatambua ikiwa amesimama katika huduma hiyo kwa
uaminifu wote. Vita si vyetu ila vya Bwana.
Saa yaja na hakika mambo
yatakuwa magumu, tutahitajiana kuliko mwanzo.
Mwenye kusikia na
ayasikie haya.
Natumaini hamjambo katika jina la Yesu.
ninavyo ona hapa kwanza watu tuna shindwa kujibu swali lililo ulizwa nakuanza kuzungumzia ujumbe unao takiwa kubebwa katika nyimbo.
ninavyo ona hapa kwanza watu tuna shindwa kujibu swali lililo ulizwa nakuanza kuzungumzia ujumbe unao takiwa kubebwa katika nyimbo.
swali limeuliza, ni aina
gani ya muziki wa injili unafaa makanisani?
tukitaka kuorodhesha
aina ya miziki iliyopo ni mingi sana hasa inayofahamika sana inaweza
kuwani;reggae,hip hop,ragga, taarabu, ngoma za asili lumba, zuku nk aina za
miziki hii ukisikia tu muziki au ala zake bila kusikia ujumbe uliomo utagundua
kwamba muziki huu niaina fulani ya muziki. Nadhani hapo ndipo swali limelala
sio ujumbe kama baadhi ya wachangiaji walivyo sema hasa Bw, Steve kama ukisema
miziki ya taratibu ndio inavuta uwepo wa Mungu mbona kuna nyimbo za taratibu
zinaimbwa watu wasio okoka na zina captvate yaani zina uwepo au mvuto wa aina
yake ndio maana miziki yao haikosi mashabiki.
Ukitaka kutafuta aina ya muziki wa kumuimbia Mungu inawezekana
usipate kitu kipya na hata ukipata bado watu wa dunia wanaweza kuuchukua na
wakautumia watakavyo kwahiyo siku zote utakuwa huna chako. Kwa kumalizia niseme
mziki ni mziki tofaut ni mashairi au ujumbe uliobebwa kwenye huo muziki ndio
unao ufanya mziki kutambulika kwa aina yake.
kuna mtu anaimba mziki anamsifia mpenzi wake namwingine anaimba mziki anamsifia Mungu wake,mwingine anafanya mziki anamtukana adui, mwingine anafanya muziki anapatanisha maadui nk.
so mziki ni mziki tafauti ni mashairi pokeeni baraka katika jina la Bwana,

Hili suala la muziki wa
injili ni changamoto pia. Ndugu Pona mfano unasikia muziki wako unapigwa Bar!
Je unajisikiaje? mtu anakunywa kilevi huku akitikisa mguu na kichwa
akijiburudisha na muziki wa Injili? mi nadhani kila muziki kuna roho inayoenda
nayo. Ndio maana wanamuziki wengine kama mfano Michal Jackson miziki yake
inamfanana na wanaopenda miziki yake wana roho wanayopokea. Kwa sasa kuna
muziki unaitwa mpenzi jini watu wanaufurahia na kuna roho ndani yake,
tukija kwa muziki wa
injili ni tofauti inabidi iwepo roho ndani yake Roho wa MUngu ambaye itamfanya
yule anayeusikiliza muziki huo kumuhamasisha kumuabudu Mungu na kubadilisha
maisha yake. Kama anafanya dhambi au anafanya dhihaka ahisi kumkosea Mungu
heshima na kuacha mara moja. Hapo sasa suala la midundo na muziki mi sielewe
zaidi, ila ni ufahamu wangu tu kuhusu wasikilizaji wa Muziki wa injili,
Mimi nadhani, tukisema
mziki ni mziki eti kinachotakiwa ni maneno yaliyomo katika muziki huo tutakuwa
tunazidi kwenda mbali na mapenzi ya Mungu.
Sidhani kama tumeishiwa
kabisa melody za miziki mpaka kufikia kuweka melody ya miziki ya kidunia, kama
Raggae, Rap, Taarab, Mziki wa kizazi kipya, Bumping Twist Rumba n.k.
Naomba moja aniambie,
hivi zile nyimbo za Urlyankulu Tabora za miaka ile ya themanini themanini na
nyingine zinazofanana na hizo, ambazo zilifanya baadhi ya watu kukabidhi maisha
yao kwa Yesu, zilikuwa za mahadhi gani? Ni Rock? Rumba?, Raggae? Rap? au ni
nini?.
Niwaeleze ndugu zanguni,
ni kwamba nyimbo za zamani hakuna mpagani aliyethubutu kuzisikiliza kama Mungu
hakumkusudia. Zilikuwa zina upako usio wa kawaida na zilikuwa hazina mahadhi
yoyote ya dunia hii ya sasa. Ukisikia zinaimbwa katika mtaa ujue kuna mlokole
eneo hilo!
Nyimbo za sasa hivi?
Kila mtu anazo, wengine mpaka wameziweka kwenye simu zao, lakini wapagani,
wanasema hakuna kuokoka duniani, lakini nyimbo za walokole wa kizazi kipya
wanazo ukiwauliza wanasema zinaburudisha sana! Jamani, tumekuja kuburudisha
watu au kuwafanya waokoke? Ashamed upon us!
Tunapotea, Tunapotea,
Tunapotea.
Amani ya Kristo iwe
nanyi nyote.
Amani, Heshima na Upendo kwenu.
Nianze na kuchangia maoni ya ndugu Steve M. YAONESHA WAJIKIMBIA KATIKA KUJITAFUTA. Yaani wewe wataka mtu aamini kuwa akiimba muziki kwa mahadhi ya asili anakuwa anaabudu miungu ya asili? AM SORRY kwa hilo nadhani umekosea. Kusema kuwa Reggae ni U-Rastafari nakupinga maana nautambua vema muziki wa Reggae, natambua u-rasta na imani zao maana nimezisoma na hakuna uhusiano wa moja kwa moja. Kuna imani, kuna muziki na kuna wenye vyote, wenye kimoja na wasio na vyote. Kwa hilo nikuweke sawa. Pengine nikupongeze kwa kuweka uhusiano wa miziki na muonekano wa watu wengi na namna waaminivyo lakini hilo ni kwa mujibu wa mapokeo yetu. Miaka ya nyuma hatukujua kama kuna wa-Kongo waimbao injili na muziki wa Kongo uliokuja kwetu ulikuwa wa ki-dunia na kutufanya tuamini kuwa aina ya muziki ndio ya kidunia ilhali ni muziki wao wa asili na wapo wanaoutumia kumsifu Mungu.Tatizo linabaki kwenye ku-kariri kuwa HYMS ndio nyimbo za MUNGU jambo ambalo si sahihi. Usijikimbie, kuikimbia asili yako na kutukuza isiyo sahihi. Na ninalosema hapa ni kwamba hata kama nyingi za nyimbo ulizosikia wewe za asili ni za kitamaduni na kutukuza miungui yao, haimaanishi kuwa ndivyo ilivyo. Kuna haja ya kuwa makini tunapochangia.
Kaka Bernard. Wasioamini wanapoburudika na yaimbwayo na wenye imani haimaanishi kuwa waimbaji ndio wana makosa. Wewe mwenyewe ulisema ulivyokuwa ukifurahia na kuburudishwa na nyimbo za ulyankulu na wakati huo hukuwa na imani. Mbona huwalaumu Ulyankulu kwa uimbaji uliokugusa wakati ukiwa si mlokole? Tuache mambo ya MY WAY OR NO WAY katika kutangaza injili. Asiyeamini ana haki ya kupenda ama kutopenda muziki na hilo halimfanyi muimbaji kuwa na makosa kama hakutoka katika njia sahii ya kumuimbia Mungu kum’burudisha asityeamini.
Kuhusu nyimbo za Ulyankulu, haimaanishi kwamba kwa kuwa hujui ama nami sijui mahadhi yake basi ni mahadhi ya dini. Na nashukuru umemalizia kwa kusema na hapa nanukuu (japo sina hakika na usahihi wa sentensi) “ASHAMED UPON US” Ni kweli kuwa shame upon all those who try to think and force things to be only their way. Kama kuna dhehebu lililojitahidi kutunza midundo ni wa-Katoliki lakini hata wao hawataweza kuwa na ujasiri wa kusimama na kusema kuwa nyimbo zao ndio midundo ya dini. Haijalishi mahadhi ya ulyankulu yalikuwa yapi, lakini kama yalikufaa haimaanishi kuwa ndio ya dini. Tuanche hii selfishness ya kudhani tuko sahihi na wengine wako wrong kwa kuwa tunajua tujuavyo hata kama tujuavyo si sahihi.
Steve M. Changamoto zako sijui zimelenga nini. Sijui ni kwa ajili ya kuonesha nini na sijui unaweza kudhihirisha vipi kuwa hao walioimba enzi hizo hawakutumia mahadhi yoyote ambayo sasa wapo wayatumiayo kwa muziki wa aina nyingine?
Umesema ngoma (drum) haijatajwa kwenye Biblia lakini hujaonesha palipoandikwa Blogs, Websites, Microphones na hata Tai na suti ambazo pengine wapenda kuvaa.
Kumbuka kuwa hasira hupunguza busara hivyo kama una hasira usiandike maoni
Pleasee

Amani kwenu,
BADO TUNACHANGANYA MADA HUO MZIKI WA ZAMANI UKIUFUATILIA KILA KITU KILICHOMO UTAGUNDUA AIDHA NI MCHANGANYIKO WA MIZIKI YA KISASA NA ILE YA ASILI NDIO MAANA UNAKUWA UNASHIDWA KUUWEKA KWENYE GROUP LOLOTE.

TAFADHALI BW, BERNARD
ELEKEZA MOJA KWA MOJA NI AINA GANI YA MUZIKI WA INJILI UNAOTAKIWA UNAOPASWA
KUIMBWA MAKANISANI,MAANA HATA MIZIKI YA DUNIA KUNA ZILIPENDWA NAHII UTASEMA
INAOKOA. PLEASE BE SPECIFIC.
Asante sana wapendwa,
Bw. Bubelwa Bandio na Bw. Pona. Hii ni changamoto kwenu na kwetu sote kama
wa-Kristo kuhusiana na suala la miziki ya Injili.
Nadhani unapoona baadhi
ya watu wakisema kuwa, kitu chako ni kizuri, lakini kina kasoro za hapa na pale
na pale, kama ni mwenye busara utashukuru na kuchukua hatua za kurekebisha
maeneo yanayodhaniwa au kusemwa kuwa na kasoro. Lakini kama utazidi
kung`ang`ania tu na kusema kuwa, hakuna tatizo, hakuna tatizo, ni mtazamo tu wa
kimadhehebu itakuwa siyo busara. Hapa mjue kuwa tunaochangia ni watu wa kutoka
madhehebu mbalimbali, na kama ni hivyo ilikuwa ni wakati wenu mzuri wa
kurekebisha kasoro zinazosemwa hapa, maana hapa tupo katika kuujenga mwili wa
Kristo na wala si vinginevyo.
Ni ukweli usiopingika
kuwa miziki ya kwaya ya nyakati hizi, hata mataifa wanatushangaa, kwamba ni
kitu gani tunafanya. Sasa kama wapendwa wenzangu mnaona hakuna tatizo, basi
muendelee kwani ukweli ndio huo.
Mtu anayepinga kuwa
hakuna kuokoka duniani, tunajua wazi kuwa mtu huyo hajakutana na Yesu. Watu
tuliookoka haitarajiwi kuwa tutapingana kuwa hakuna kuokoka duniani, kwa sababu
tayari wote tumekutana na Yesu, yaani ametuokoa.
Tunapopingana juu ya
swala hili la kwaya/miziki ya Injili juu ya namna ya uimbaji wakati wote
tunasema kuwa tumeokolewa na Yesu, basi kuna kasoro kubwa katika wokovu wetu,
katika hili inatubidi tuogope.
Bw. Bandio amesema mbona
mimi nilisikiliza nyimbo za ulyankuru na nikaburudika wakati nilikuwa sijaokoka
na je, niwalaumu Ulyankurlu? Kama utakuwa umesoma vizuri katika meseji yangu
hapo juu, niliandika hivi; “Niwaeleze ndugu zangu,ni kwamba nyimbo za zamani
hakuna mpagani aliyethubutu kuzisikiliza KAMA MUNGU HAKUMKUSUDIA. Kwa hiyo hapa
ni Mungu mwenyewe kwa neema yake hakikuwa kitu cha kawaida. Kama mimi
nilisikiliza nyimbo hizo ni Mungu tu alinikusudia. Nakumbuka wakati huo,
waliokuwa wanasikia nyimbo zile nyumbani kwangu walikuwa wananiuliza iwapo ni
mlokole! Kama mmepata kufuatilia moja ya maelezo yangu huko nyuma katika blog ,
mimi kabla ya wokovu nilikuwa na magonjwa. Hivyo katika kusikiliza nyimbo hizo
ilikuwa ni sehemu ya kuona kama ningeweza kupata uponyaji. Ilikuwa si kitu cha
kawaida kusikia nyimbo za mlokole kama hujaokoka.
Bw. Pona ameniambiwa
niwe specific, ni mziki gani wa injili ninaoona unafaa. Kwa kifupi ni kwamba
mziki wa injili unaofaa ni ule usio na makwazo wala maswali kwa wasikilizaji.
Tunapoimba tuangalie pande zote, kwetu waimbaji na wasikilizaji, kwamba
watakaposikiliza watatuchukuliaje. Kama hivi tunapoona wengine wanapinga juu ya
uimbaji wetu, tujue kuwa tunazo kasoro katika uimbaji wetu. Kana ni wenye
busara tutatafuta namna ya kurekebisha kasoro hizo, ili hata watu walio wa aina
ya Bw. Bernard na Bw. Steve waridhike, huko ndiko kuboresha kazi ya Mungu!
Najua hawataridhika wote, lakini angalau kile tunachokisikia kutoka kwa wapendwa
walio wengi kama hivi , tukitilie maanani na kukifanyia kazi!
Wewe unataka nitaje
specific kwamba ni aina mf. RAGAE ndiyo inayofaa! Hapana, hatuna specific
lakini kutokuwa na specific, kusitufanye tuchukue aina ya ragae. Kwa nini
tuchukue makombo ya shetani na kuanza kuyaboresha? Je, sisi hatuna Roho
Mtakatifu wa kutuwezesha kubuni mtindo wa Mungu?.
Mimi binafsi niwaeleze
ukweli leo, ni kwamba baadhi ya nyimbo za kwaya hata katika TV za Kikristo
zikiimbwa tu, huwa nahama `station` siwezi kuzivumilia kuangalia!
BWANA WA AMANI
ATUFUNIKE!
S H A L O M !
Kweli tuko watu wa aina nne.
Wenye kujua na wanajua kuwa wanajua
Wenye kujua lakini hawajui kuwa wanajua
Wenye kutojua na wanajua kuwa hawajui
na mbaya zaidi ni wale
Wenye kutojua na hawajui kuwa hawajui.
Wenye kujua na wanajua kuwa wanajua
Wenye kujua lakini hawajui kuwa wanajua
Wenye kutojua na wanajua kuwa hawajui
na mbaya zaidi ni wale
Wenye kutojua na hawajui kuwa hawajui.
Narudia tena. Si lazima kuchangia kila mada kwa kuwa si kila mtu
ana ujuzi na uelewa wa kila mada. Nyakati nyingine tunajishushia hadhi kwa
kung’ang’ania kufafanua kile ambacho wanaokijua wanatambua kuwa hatujui.
Sijui tunakaririshwa huko tuendako, ama tunakaririshwa na hawa tunaoshirikiana nao ama ni elimu yetu ya kusoma Biblia kama kitabu cha Algebra kwamba kila 1+1=2 ama ni kuchanganya kukaririshwa na watu na elimu yetu ama kukosa vyote kunakosababisha haya.
Lakini ndhani tuwe makini katika kuchagua kipi cha kuchangia maana kuna mada ambazo nakubaliana na wapendwa humu kwa kuwa wanajua wanachosema na wanachangia kwa ufasaha, lakini unapokmkuta mpendwa huyohuyo kwenye mada nyingine akijitumbuatumbua unaweza kutilia shaka hata zile BARAKA ulizopata kwenye mada ambazo anazifahamu.
Ni ushauri tu na yeyote anaweza kuutumia kama kioo kujiangalia.
Amani Kwenu

Huu muziki wa kufokafoka (rap) nao unaweza kuwa wa dini?
Nimeweka hii clip katika blogu yangu na sijui nyie wataalamu wa mambo ya wokovu mna maoni gani. Kwa maoni yangu nadhani hiki ni kizazi kipya kinajaribu kujitambulisha na kumsifu Mungu. Tembelea link ifuatayo:

22.
Baraka kwenu
Nadhani wakati mwingine
kukubaliana na ukweli au halisi pia ni jambo la muhimu na linaweza kuondoa
mlolongo mrefu wa mjadala, kuliko kuendelea na nadhalia ambazo zinakuwa hazina
mwisho na hazileti suluhu katika jambo ambalo tunaliona ni tatizo wakati si
tatizo kwa Mungu, isipokuwa ni tatizo letu.
kuwa na msimamo si jambo baya ila msimamo huo ukiwa umejengwa
kwenye msingi ambao sio imara yaani kinyume na neno la Mungu huo msimamo ni
batili.
Jambo lakuzingatia mara zote nipale tunapo kosoa jambo basi tuwe na njia mbadala, au kama jambo hilo ni dhambi kuwe na namana ya kumfanya mhusika atambue kwamba anamkosea Mungu ikwezekana atubu na sio kuhukumu kama baadhi yetu tunavyo fanya japo ukimwambia furani unahukumu hatukubali kwakuwa neno linamhukumu nae pia lakini ukichunguza kwa kina maelezo yaliyo tolewa utagundua yanalenga hukumu.
kama hatuwezi kuorodhesha aina gani ya miziki ya injili itumike makanisani.
basi miziki iliyopo Mungu ameiruhusu.kama sio tupate huo ufunuo wa ni aina gani ya miziki ya injili itumike makanisani.

MUNGU NI MWEMA
SAAAAAAAAAAAAAAANA HUWEZI JUA
Asante Ndg Pona kwa maoni yako. Ni vema kutohukumu.
Na kwa yeyote anayeweza kunijibu hili na naamini tunajua kuwa TWASTAHILI KUSEMA KWELI NA KWELI HIYO NDIYO ITAKAYOTUWEKA HURU. Maswali yangu ni haya.
1:Je! nyimbo za wanamuziki kama Cosmas Chidumule, Remmy Ongala na hata Mzee Makassy si za injili na hazifai kutumika makanisani kwa kuwa tu walikuwa wakitumia mirindimo iendanayo na hii ya sasa walipokuwa hawajaokoka?
2:Je wasanii kama Beatrice Muhone, Bahati Bukuku, Rose Mhando, Kijitonyama na wengine wengi wanaoimba na kugusa watu sasa hazifai kwa kuwa tu zina mirindimo iendanayo na baadhi ya hiyo mnayoiita ya kidunia?
3:Kwani muziki asili yake wapi na muziki wa dini asili yake wapi?

Kaka Bernard umesema na hapa nakunukuu kuwa “Hapana, hatuna
specific lakini kutokuwa na specific, kusitufanye tuchukue aina ya ragae. Kwa
nini tuchukue makombo ya shetani na kuanza kuyaboresha? Je, sisi hatuna Roho
Mtakatifu wa kutuwezesha kubuni mtindo wa Mungu?.” Ina maana unakubali kuwa
hakuna muziki wa Injili lakini unasema kuwa kuna unayosikiliza na mingine
unahama “station”. Sasa kama hakuna wa injili huoni kuwa wowote unaosikiliza ni
wa kidunia?
Anyway, maswali mawili ya mwanzo ndiyo ya muhimu zaidi.
Baraka kwenu
Anyway, maswali mawili ya mwanzo ndiyo ya muhimu zaidi.
Baraka kwenu
wapendwa,
mnapoendelea na hii mijadala mkumbuke na kuzingatia maonya haya: “Lakini maswali ya upuuzi ujiepushe nayo,na nasaba,na magomvi, na mashidano ya sheria. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana. Mtu alie mzushi, baada ya kumuonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae, ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi, maana amejihukumu hatia yeye mwenyewe.” Tito 3:9-11.
“Ee Timotheo, ilinde hiyo amana, ujiepushe na maneno yasiyo ya dini, yasiyo na maana, na mashidano ya elimu, iitwayo elimu ya uongo..” 1 Tim. 6:20

Mch. Malisa,
nimependezwa sana na kauli yako pamoja na hilo andiko. Blog hili nadhani kama
ilivyo, iwe ya kuelimishana na kuonyana kadiri tuonavyo siku zile zinakaribia.
Maandiko yanatukumbusha juu ya kulihubiri Neno, kukemea,
kuonyana kwa uvumilivu wote. Katika 2Timotheo 4:2 maandiko yanasema [lihubiri
Neno, uwe tayari wakati ukufaao na wakati usiofaa, karipia kemea na kuonya kwa
uvumilivu wote na mafundisho. Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho
yenye uzima; ILA KWA KUZIFUATA NIA ZAO WENYEWE, watajipatia walimu makundi
makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti, nao watajiepusha wasisikie yaliyo
kweli, na watazigeukia hadithi za uwongo]. Pia pamoja na kuonyana, maandiko
mengine yanatukumbusha kama alivyosema Mch Malisa kuwa tuyakatae maswali ya
upumbavu yasiyo na elimu tukijua kuwa huzaa magonvi [2Timotheo 2:23], asante
sana, na Mungu azidi kutusaidia tusiingie katika mitego hii.
Amen!
Amen!
I knew this was coming. It’s what i say everyday that “THE WAY
YOU SEE THE PROBLEM IS THE PROBLEM”.
Ok. Let it be “someone’s way” to be educative for you
Ok. Let it be “someone’s way” to be educative for you
Kwa kweli hii mada ina
changamoto kubwa.
Nami natamani kuchangia
kutokana na ambavyo ninalielewa suala hili la muziki huu unaoitwa wa injili.
Lakini kabla
sijachangia, ninakuomba radhi ndugu Pona kwamba ninatamani sana kama swali
ambalo dada Miriam Joseph aliuliza tarehe 6/03/2009 ungelijibu. Ninategemea
kujifunza kitu kutokana na jibu utakalotoa. Lakini hii haimaanishi mchango
wangu unategemea jinsi jibu la swali hili litakavyokuwa!
Swali lenyewe liko hivi:
“Ndugu Pona mfano
unasikia muziki wako unapigwa Bar! Je unajisikiaje? mtu anakunywa kilevi huku
akitikisa mguu na kichwa akijiburudisha na muziki wa Injili?”
Narudia tena kwamba
ninakuomba msamaha ndugu Pona kama kwa namna yoyote ninaweza kuwa nimemkwaza
kwa kuhitaji majibu ya swali hili. Lakini ninaamini katika kujibu kwako swali
hili kunaweza kupatikana point muhimu sana katika kuliweka sawa jambo hili.
Nasubiri kwa hamu kusoma
jibu la swali hilo.
Amani!
Amani kwenu
asante sana Bw.John Paul kwakukazia swali lililo ulizwa na dada Miriam Joseph swali lenyewe lina sema; Ndugu Pona mfano unasikia mziki wako unapigwa Bar ungejisikiaje? mtu anakunywa kilevi huku akitikisa mguu na kichwa akijiburudisha na muziki wa injili.

JIBU
Ningejisikia vizuri tu tena kawaida SAANA maana hata mimi sifahamu huyo mlevi baada ya kutoka hapo atatubu au hata tubu kama atakufa au hata kufa lakini ninacho fahamu akili yake inajua kwamba anakunywa kilevi huku anajiburudisha na muziki wa injili na hata Mungu anakuwa na taarifa hiyo wakati huo hata baada ya hapo,

Mimi mwenyewe sikuokoka
kwasababu nilihubiliwa na wainjilisti, au wachungaji siku niliyookoka nilikuwa
nimevuta mmea yaani nililewa lakini nilifanya maamuzi sahihi ambayo ni matokeo
ya Pona wa leo. Hata hivyo sikutaka nijibu swali la huyo dada kwa sababu
asilimia kubwa ya swali lake linataka majibu ya ku-assume na mimi siishi kwaku
assume mimi niko REAL ndio maana nimetoa huo ushuhuda mfupi kwa ajili ya kuona
jinsi gani wakati mwingine mipango ya Mungu inavyokuwa tofauti kabisa na
mitazamo yetu.
SWALI LINGINE TAFADHALI
MBARIKIWE
Asante ndugu Pona kwa jibu lako. Mimi sina swali jingine bali
hilo ndilo lilikuwa swali pekee. Na wala kwa kukuuliza hivyo sikuwa na maana ya
kuanza mlolongo mwingine wa maswali na majibu.
Asante
Asante
ni muhimu kuangalia kwa makini na kwa undani kile Biblia inafundisha
kuhusu uimbaji na muziki kwa jumla, msipofanya hivyo sioni jibu sahihi katika
swali hili. mengi yaliyotolewa mpaka sasa ni maoni binafsi ya wachangiaji
yakiwa na mafundisho kidogo toka kwenye Biblia.
Pona amejibu, nanyi mnasemaje?
Pona amejibu, nanyi mnasemaje?
Nimebarikiwa sana na
jibu lako kaka Pona na hasa sentesi ya mwisho “…jinsi gani wakati mwingine
mipango ya Mungu invyokuwa tofauti kabisa na mitazamo yetu.”
Mara nyingine nadhani
huwa sisi wanadamu tena ambao Mungu ametusaidia kuijua kweli tunapenda sana
kumpangia Mungu jambo la kufanya. Kama watu wanaokoka wakiwa “high” na mmea
then hata Muziki wa Injili ukipigwa Bar kuna mtu kati ya wengi ambao Mungu
amemkusudia kukutana naye!!
Sisi inatupasa kuifanya
kazi ya Bwana na hata katika kumsifu inatupasa kumsifu katika roho na kweli na
hayo mengine tumwachie yeye kuyashughulikia. Tusiwe kama Yona ambaye baada ya
kuihubiria Ninawi na kuona Mungu ameghairi kuiangamiza yeye akachukia. Najua
kuna watu wanatamani waimbaji fulani wa sifa wapigwe radi na Mungu wakiwa
madhabahuni! Jamani Mungu hayuko hivyo!!
Barikiwa kaka Pona na
Amani ya Bwana ikae nayi nyote!!
Nami naungana nanyi nyote kumshukuru Ndg Pona kwa jibu lako. Ni
zaidi ya ushuhuda. Ni utimilisho wa mipango ya MUNGU na ni lazima tujue kuwa
kwa namna yoyote ile itatimia. TUTAKE TUSITAKE.
Kwa Mch Malissa nafurahi kuona unaendelea kufuatilia mjadala huu. Ningependa kujua hilo ulilosema kuwa Biblia inafundisha juu ya uimbaji na muziki kwa ujumla.
Ndg Godlove nimependa saana maelezo yako hasa uliposema “tunapenda kumpangia Mungu jambo la kufanya”. Na huo kwangu ndio ukweli. Kuwa watu wanadhani kwa kuwa wameokoka kwa njia hii ama wamelelewa kwa imani na mafundisho haya basi ni hayo pekee yaliyo na nguvu za kumuokoa mwingine ama ni mwendo na namna hiyo pekee yenye wokovu.
Tunakimbia uwezo wa Mungu. Tunataka kuwa tutakavyo kwa namna tutakavyo na tuwezavyo ilhali Mungu anataka tuwe alivyopanga tuwe. Na ili hili litimie kuna njia mbalimbali. Tatizo ni kuwa wapo tunaoona maisha yao lakini si kamili na tunadhani ndiko walikoishia. Kujua kilichomsibu Ayubu bila kusoma hitimisho lake kutakufanya usitambue mpango wa Mungu kwake. Hivyohivyo tumeona watu wakiokokea magerezani na sehemu nyingine zijumuishazo wahalifu na wakitoka huko wanakuwa nuru halisi. Kama alivyosema ndg Pona kuwa aliokoka akiwa “high” na sasa ni Pona mwenye ushuhuda wa nguvu, unadhani aliokoka bila kuijua hiyo njia ya wokovu akiwa high? Ina maana kuna wakati ambao kuwafikia wenye uhitaji ni wakati muafaka wa kuyageyuza na kuyashuhudia maisha ya wengi ambao watabadilika na kuwa nuru ya jamii.
Kwangu muziki bado utaendelea kuwa wenye kumsifu MUNGU na usioenda nje ya maandiko kuiridhisha hadhira.
Aina na midundo wala si tatizo kwangu maana vyote vina asili.

Nimesikitika nimekuta huu mjadala kama unaenda mwisho hivi,
anyway na mimi nichangie hivohivo.
Nadhani wengi wa wakristo wa sasa tuna mapokeo ya zamani(ambayo yalikua mema wakati huo)lakini hayafaidii u-kiroho wa mtu leo. kabla hujazungumzia muziki wa injili lazima ujue muziki ni nini. Ni mada ndefu kidogo lakini kuzalishwa kokote kwa sauti kunaweza fanywa muziki(kulingana na mtumiaji anavyotaka). Genre(sijui nikiita aina napatia au vipi) inaweza tumiwa kwa injili bila matatizo mradi kinachozungumziwa ndani kiwe injili sababu hakuna aina maalum ya muziki ambao umekua certified(sijui na nani!)kua utumike kwa injili.hao ulyankulu waliotolewa mfano ni watumishi wazuri wa Mungu kwa uimbaji lakini pia wamepiga reggae,country,bosa nk.nyingi ya kwaya za zamani zilipiga hizihizi chakacha na aina zingine za muziki ambazo ungezisikia zikipigwa na bendi za kidunia lakini zikiwa zimeboreshwa. Cha msingi kwa muimbaji na wakristo kwa ujumla ni kujua UHODARI WAKO KISANAA peke yake, japo ni mzuri, haupelekei watu kuguswa maisha yao na Yesu unaemuimba kama maisha yako si safi lakini pia zaidi sana kama huna ufahamu wa unachokifanya! maana hata ibada ya sifa kwa makanisa mengi siku hizi ni ka-ratiba tu au ‘kutifua mioyo’kabla hajaja muhubiri ambayo si sahihi ndugu zangu! Muziki kama muziki hauna shida kabisa maana kwanza hutofautiana kulingana na tamaduni na mambo kama hayo. Kama ambavyo mbwembwe na uhodari wa kutunga hotuba wa muhubiri haubadilishi maisha ya mtu zaidi ya kumsisimua,vivyohivyo aina ya muziki haina tatizo ila hali ya rohoni na ufahamu wa mwanamuziki kwa anachokifanya ndo hupelekea mguso wa Mungu kwa watu,sio msisimko wapendwa. blesses

34.
Shalom wapendwa,
Nimekuwa nikitafakari juu ya hii mijadala ya Neno la Mungu katika blog hii, nimegundua kuwa kila mtu anatamani mwingine aandike kila ambacho yeye anakiona kinafaa. Akiandika tofauti anaambiwa kuwa anamtizamo wa kibinafsi au wa kidhehebu.

Nadhami blog hii ni kwa
ajili ya kufundishana kuelimishana na kubadilishana uzoefu wa kiimani. Iwapo
mwingine atakuwa yupo kinyume na mwingine, yule aliye kinyume asilaumiwe na
kuonekana kama hana ufahamu wa Neno la Mungu. Iwapo mwingine atakuwa na msimamo
mkali juu ya kile anachokiamini, basi nayo yachukuliwe kuwa ni mafundisho kwa
wengine wenye kuyapokea, kwamba kuna watu wa aina hiyo katika imani.
Iwapo tutataka kuwa kila
mtu ajihadhali na msimamo wa wengine ili kwenda sambamba, hakuna tutakachokuwa
tunajifunza hapa, sana sana tutakuwa tumebaki katika KUFARIJIANA.
Tuelezane ukweli, kila
mtu aeleze kile anachokiamini kuhusiana na Neno la Mungu, ili mwenye kuamini
kile kinachoelezwa akifuate, na asiyeamini asishutumu. Iwapo atataka kutoa
hoja, atoe kwa uwazi bila kuingiza misemo, mafumbo na nahau!
Hili ni eneo la
kuelimishana mambo ya rohoni, mambo ya kutufikisha mbinguni. Shetani hawezi
kukaa mbali na maeneo kama haya, anaweza akamtumia mtu moja na wote wakajikuta
wanakwazika kwa huyo, pasipokujua hata wao kuwa wamekwazika.
Hivyo wapendwa katika
Kristo, tuliangalie sana hili. Maandiko yanasema mwenye hekima huvuta roho za
watu [Mithali 11:30]. Tumwombe Mungu atupe ufahamu wa yepi ya kuandika na iwapo
mwingine ataonekana ameandika tunayoona hayafai bado tujue ni sehemu ya
kujifunza, tumtie moyo kwa upole na uvumilivu wote. Tusitoe lawama na kumwona
kuwa anakengeuka, tutafute hekima ya kumweleza ili naye ajione anasehemu katika
mchango wake.
Tukifanya hivyo, bila
shaka mada katika blog hii zitakuwa haziishi kabisa, kila siku itakuwa ni mpya
kwetu. Lawama zinawafanya wengine kuanza kuwa waoga, kuwa wasije wakachangia
kitu ambacho kitawaudhi wengine na wakaonekana kuwa hawana ufahamu juu ya Neno
la Mungu.
S H A L O M !
35.
Asante saana King kwa maelezo mwanana. Nadhani hapo
umedhihirisha kuwa hata watu wenye mtazamo mmoja wanaweza kuwa na maelezo
yanayomaanisha kitu kimoja lakini kukawa na UBORA wa kuyafupisha na kuyaeleza.
Naamini ulichosema umewakilisha asilimia mia moja ya niliyokuwa nayawaza.
Labda kwa kuongeza tu ndugu zanguni ni kuwa MUZIKI kwa maana ya midundo hauna tatizo. Ntatoa mfano wa kompyuta ambazo asilimia zaidi ya 50 ya search inahusisha masuala ya ngono (kwa mujibu wa taarifa) lakini wewe usomaye hapa umeamua kuingia na kuitumia ipasavyo kujijenga mna kujenga nyoyo za wengine kuelekea mbinguni. Vivyo hivyo na muziki. Muziki una upana mkubwa saaana. Ni “silaha” pekee inayotumika kotekote. Kwenye sherehe na huzuni, makanisani na clubs. Kwenye kukusanya watu kumsikiliza mtumishi wa Mungu na kinyume chake. Kwa hiyo kama ambavyo huwezi kusema kompyuta zote ni haramu kwa kuwa wengi wanazitumia visivyo, vivyo hivyo huwezi kusema hilo kwa muziki na hata wanamuziki.
Mimi napenda saana muziki wa asili na Reggae. Na hata katika blog yangu nimekuwa nikisindikiza mambo mengi kwa muziki huu. Na hata Jumapili pia nimekuwa nikiweka muziki wa mahadhi haya kusindikiza siku yangu hiyo. Na wiki iliyopita nilikuwa na “somo” toka Math 5:3-12 na hata kabla ya hapo nimeshakuwa na mengi kuhusu Mungu (japo waweza kutofautiana namna umuitavyo) lakini bado kuna watu wengi wanaofuatilia kila Jumapili na nisipoweka (kutokana na sababu mbalimbali) huwa napata emails kuuliza kulikoni.
Pengine wanaobisha kuhusu nguvu ya mahadhi hayo (kama ndugu Steve M ambaye KIMAKOSA alichambua miziki kulingana na mtazamo wake na si maudhui yake)wanaweza kusikiliza japo wimbo wa jumapili iliyopita ama wa Jumapili ijayo kisha wanieleze kama kuna kasoro ya kuimba muziki wa injili ama dini katika mahadhi ya reggae.
Bofya h

Ubarikiwe saana!! na wachangiaji wote.
37.
Ninakubaliana na
aliyoyaandika ndugu Bernad juu ya namna watu wengine wanavyoyachukulia baadhi
ya maoni ya watu wengine kwa sababu tu yanatofautiana na ufahamu au mtazamo wa
mtu huyo. Ni kweli hapa ni mahali pa kujifunza Neno la Mungu. Ninaamini kila
mmoja [anayemwamini Yesu] ni mwanafunzi wa Bwana Yesu hapa, kwa hiyo lugha yetu
inatakiwa kuwa ni ya amani, heshima, upendo na kuvumiliana. Mimi ninatambuwa
kwamba tunaufahamu na ujuzi tofauti wa mambo mbali mbali , kama alivyoandika
ndugu Mubelwa tarehe 7/3/2009. Kinachotuunganisha hapa ni Neno la Mungu tu.
Hivyo mimi naona ni vema sana tunapochangia maoni hapa {mada hii na nyinginezo}
TUZINGATIE sana Neno la Mungu linasemaje. Elimu za duniani ziko nyingi, imani
mbali mbali ziko nyingi sana pia, bila kutazama Neno la Mungu linavyosema
tunaweza tukajikuta tumepoteza mwelekeo na kuanza kufuata mawazo na mitazamo ya
watu na mwisho wake tukajikuta tumepoteza kujifunza na kubaki TUNAFARIJIANA kutokana
na makundi ya ki-mtazamo.
Tukifanikiwa kuwa na
lugha ya upendo na kuthaminiana ni kweli kabisa mada zitakuwa haziishi. Kila
siku zitakuwa ni mpya. Na ninaamini kadri tunavyoendelea kujadiliana kwa upendo
ndipo vipengere vipya vitavyozidi kuibuka. Kuibuka kwa vipengere vipya
kutafanya mada zizidi kueleweka zaidi. Kwa mfano mada hii inavyozidi kupanuka
tunaweza kujikuta pande zote zimeelimika. Watu wanaosema muziki ni muziki tu
wanaweza jikuta wameelewa kwamba kumbe kuna mipaka [kama ipo] na wale wanaosema
kwamba muziki fulani una matatizo wanaweza nao wakajikuta wameelewa ni kwa vipi
muziki peke yake unaweza usiwe tatizo. [kama ni ndivyo ilivyo]. Na wale ambao
hawako upande wowote wakajikuta nao wameielewa kweli kwa kuchanganya maoni toka
pande zote mbili. Na mwisho wa siku kila mtu akafurahia kwa kukutana na mjadala
huu. Lakini katika yote dira yetu ni Neno la Mungu.
Huku nikizingatia kwa
makini aliyoyaandika ndugu Bernad Mwenda na niliyoyaandika nami pia ninaomba
kupata ufafanuzi wa mambo fulani ambayo yamejitokeza kutokana na uchambuzi
aliouandika ndugu Mubelwa T. Bandio:
1. Ndugu Mubelwa
umeandika kwamba MUZIKI kwa maana ya MIDUNDO hauna tatizo. Mimi naona kama vile
unatafsiri nyingine ya MUZIKI ambayo maana yake ni tofauti na MIDUNDO. Maana
hiyo ya muziki iliyotofauti na maana ya “Muziki kama MIDUNDO” labda ndipo
panaweza kuwa pana Tatizo. Tafadhali fafanua hapa kidogo. [Katika kufafanua
hili unaweza kujibu pia swali hili: Je, Muziki ni MIDUNDO?]
2. Pia ndugu Mubelwa
umeandika jinsi muziki unaweza KUTUMIKA kwenye sherehe na huzuni, makanisani na
clubs, kwenye kukusanya watu kumsikiliza mtumishi wa Mungu na kinyume chake.
Natumaini kuna mengi ungeyaandika lakini umefupisha kwa sababu ya nafasi na
muda pia.
Mimi nafikiri hapa pia
pana swali muhimu lililojitokeza. Swali lenyewe ni kwamba:
a). Je, muziki
uliotumika kwenye CLUBS ni huo huo unaweza kutumika KANISANI? au Muziki
unaotumika kwenye SHEREHE ni huo huo unaweza kutumika kwenye HUZUNI?]
b). Kutokana na hoja
kwamba muziki ni muziki tu tofauti ni maneno, nauliza Je, kubadilisha maneno
peke yake kutoka katika muziki fulani uliotumika kwenye tukio moja kunaweza
kuufanya muziki huo huo UFAE KIKAMILIFU kutumika kwenye tukio jingine lolote
tofauti? [mfano kubadilisha MANENO peke yake kwa muziki uliotumika kwenye
SHEREHE zilizojaa vifijo na nderemo kunaweza kuufanya muziki HUO HUO ukatumika
kwenye HUZUNI palipojaa vilio na machozi?]
c). Baadaye ukaandika
maneno haya:
“Kwa hiyo kama ambavyo
huwezi kusema kompyuta zote ni haramu kwa kuwa wengi wanazitumia visivyo, vivyo
hivyo huwezi kusema hilo kwa muziki na hata wanamuziki.”
Kama ulivyoandika
hukukosea chochote mimi naona maneno yako haya yanakubaliana na maoni ya watu
wanaosema kwamba kunatakiwa kufanyika umakini katika kuchagua aina gani ya
muziki [kama swali lilivyouliza] utumike makanisani. Sijasoma popote ambapo
kuna maoni kwamba muziki wote ni haramu au kwamba wanamuziki [natumaini
unamaanisha wanaoimba habari za Neno la Mungu] wote wanafanya vibaya [ingawa
inawezekana ikawepo sehemu iliyoandikwa hivyo]. Maana niliyoipata mimi ni
kwamba muziki uchambuliwe na kupata aina inayofaa kutumika kanisani na
wanamuziki nao wajichunguze na kujipima na Neno la Mungu ili wasiweze kulaumiwa
kwa aina yoyote [iliyo kinyume na mwenendo wa waaminio] katika utumishi wao.
Kama ilivyoandikwa katika 2Korintho 6:3-10.
Natumaini tunavyoendelea
kujadili hapa tunaweza kufikia mahali ambapo tunaweza kupata [kama vipo] VIGEZO
vya kuzingatia juu ya AINA GANI YA MUZIKI UNAOFAA KUIMBWA MAKANISANI.
Tuendelee kujifunza!
38.
Suala la uimbaji na aina ya muziki katika makanisa ni changamoto
kwetu sote tuliokombolewa na Kristo. Kanisa limevamiwa na mamluki wa muziki wa
injili. Kama ilivyo kawaida yake Lucifer amejigeuza kama malaika wa nuru katika
eneo hili la muziki kanisani.
Nitaelezea baadae ninacho maanisha, lakini kwanza nataka tuangalie “neno” linasemaje kuhusu muziki na injili.
Muziki katika Biblia umegawanyika katika maeneo yafuatayo:
• Uimbaji kwa sauti tu bila vyombo ( Vocal Praise) Tunasoma katika Kut. 15:1-18, Waamuzi 5:1-, Mat. 26:30. Kuna vifungu vingi lakini hivi vinatosha , unaweza kusoma vifungu zaidi wewe mwenyewe.
• Uimbaji pamoja na ala (Instrumental Praise) aina hii ya uimbaji ilikuwa ya kawaida sana haswa katika Agano la Kale, tunasoma katika Kut. 15:20-21, 1 Sam.10:5, pia katika Agano Jipya kwa kiasi kama Ufu. 5:8-9, etc.
• Uimbaji wakati wa furaha au huzuni . Kwenye huzuni Mat.9:23, 1 Sam.16:15, kwenye furaha Muhubiri 2:8, n.k.
Mwanzoni kabisa mwa uumbaji tunaona suala la uimbaji kwa kutumia vyombo katika maisha ya kawaida ya wanadamu linatajwa katika Mwa. 4:21, huyu Yubali hakutumia vyombo hivi kumsifu Mungu kwani wakati huo tayari uasi ulikuwa mwingi.
Mungu Baba alipowaumba malaika mmoja wao aliitwa Lucifer ambae baada ya kuasi anajulikana kama shetani. Mungu aliweka ndani yake karama ya uimbaji na muziki kama tunavyosoma katika Ezekieli 28:13-15. Lucifer alipoasi aliamua kuharibu kila kitu chema alichokifanya Mungu Baba ikiwa ni pamoja na muziki. Kwa hiyo ni sahihi kabisa kusema kuwa leo hii kuna muziki wa kiroho na wa kidunia, kama vile kulivyo na mambo ya kiroho na ya kidunia. Kila alieokolewa na Kristo ni muhimu tena ni lazima kutambua tofauti hii.
Utatambuaje tofauti katika ya muziki wa kiroho na wakidunia? Nadhani hili ndio swali kubwa hapa. Wengine wameona tofauti ni maneno tu, yaani kama maneno ni ya kimungu haijalishi mudundo ni wa namna gani, kwao huo ni muziki wa kiroho (injili), wengine wameona ni lazima hata mdundo nao ufanane kiroho. Hili linawachanganya wengi kwa sababu hakuna mahali po pote kwenye Biblia pana sema mdundo wa aina Fulani ndio unaokubalika mbele za Mungu. Kwa sababu ni kweli kuwa shetani amechafua hata uimbaji, ni lazima kuwa na tahadhari katika aina ya muziki wa injili.
Ukisoma neno kwa makini, utaona kuwa watoto wa Mungu hawapaswi kuenenda kama watu wa dunia katika maeneo yote ya maisha yao, na je! Sio zaidi sana katika eneo la kumsifu na kumwabudu Mungu kwa uimbaji wetu? Warumi 12:2 “Wala msiifuatishe namna ya dunia hii, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu…”
Mt. Paulo anasema, “Lakini sisi hatukupokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.” 1 kor. 2:12.
Tujihadhari tusiilete dunia kanisani, bali tulipeleke kanisa duniani mwote!
Tatizo la muziki wa injili ni pana zaidi ya aina ya muziki wenyewe. Leo imekuwa ni kawaida kuona waimbaji “nyota wa injili” wakidai kulipwa mamilioni ili kuimba, hivi sasa kuna biashara kubwa ya nyimbo za injili. Waimbaji hawa wa injili huwezi kuwapata mpaka uwasiliane na mameneja wao!!!! Hivi sasa mkazo mkubwa katika nyimbo za injili ni katika uwezo wa mwimbaji kunen’gua na kutawala jukwaa. Mambo ya ajabu kabisa haya! Hakuna tena tofauti kati ya Twanga Pepeta, Msondo Ngoma na hao waimbaji wa muziki wa injili. Ndio maana hata kampuni za Pombe zinawapa waimbaji wa injili tuzo za uimbaji bora, nasisi tumebaki kuulizana upi ndio muziki sahihi wa injili!
Sio waimbaji wote wa injili wako kama nilivyoeleza hapo juu, na kiri kuwa kuna wachache, tena wachache sana, wanaomwimbia Mungu wao katika roho na kweli ,na hawa wazidi kubarikiwa ili kutenganisha nuru na giza. Bwana Yesu asifiwe!
Hivi kanisa lisipoamka sasa, litaamka lini? Hivi waliookoka wasipoamka sasa wataamka lini? Shetani haji kushambulia kanisa akiwa amevaa pembe kichwani na moto ukimtoka mdomoni, bali huja kama malaika wa nuru.

39.
Kwako ndugu king,
Wakati tukiendelea
kutafakari ujumbe aliouandika hapa Mchungaji Malisa naomba kurejea kwenye
mchango wako uliouandika tarehe 17/3/2009. Katika mchango wako huo uliandika
maneno haya:
“Nadhani wengi wa
wakristo wa sasa tuna mapokeo ya zamani(ambayo yalikua mema wakati huo)lakini
hayafaidii u-kiroho wa mtu leo.”
Kutokana na maneno haya
mimi nimepata tafsiri kwamba kwa upande wako u-kiroho wa mtu wa leo ni tofauti
na u-kiroho wa mtu wa jana (wakati uliopita). Kwamba u-kiroho unabadilika
kutokana na wakati! Au kwa kufupisha ni kwamba wokovu wa ZAMANI ni tofauti na
wokovu wa SASA.
Kama maana yako ni hiyo
ninaomba ufafanue zaidi suala hili katika Mada ya Swali kuhusu Wokovu wa Zamani
na wa sasa ya terehe 27/1/2009. Lakini kama ni kwa sababu sijakuelewa unaweza
kufafanua hapa hapa.
Tukirudi kwenye suala
letu la aina gani ya muziki, umeandika pia maneno haya:
“hao ulyankulu
waliotolewa mfano ni watumishi wazuri wa Mungu kwa uimbaji lakini pia wamepiga
reggae,country,bosa nk.nyingi ya kwaya za zamani zilipiga hizihizi chakacha na
aina zingine za muziki ambazo ungezisikia zikipigwa na bendi za kidunia lakini
zikiwa zimeboreshwa.”
…kwamba Ulyankulu walipiga
reggae na aina zingine za muziki lakini pia bendi za kidunia zikapiga aina hizo
hizo za muziki. Lakini ili zikubalike kwa wasikilizaji wake bendi za kidunia
inabidi ZIBORESHE aina hiyo ya miziki. [kutokana na ulivyoandika wewe].
Changamoto iliyoko hapa
ni kwamba UBORESHAJI huu wa muziki unaofanywa na bendi za kidunia ndiyo
unaotofautisha vionjo vya muziki.
Mimi naona hapa tunaweza
kuwa tumepata kigezo kimoja kwamba UTOFAUTI WA UBORESHWAJI WA AINA YA MUZIKI
KUNAWEZA KUFANYA MUZIKI HUO UFAE KUTUMIKA KATIKA MAZINGIRA TOFAUTI. Kwamba
‘Genre’ fulani ikipigwa kinamna fulani inaweza kufaa kutumika kanisani lakini
isifae kwenye Clubs na aina hiyo hiyo ya genre ikipigwa kwa namna fulani kwenye
Clubs inaweza isifae kutumika kanisani!
Ndugu king wewe unaonaje
kuhusu hili?
40.
Ubarikiwe sana mtumishi
wa Mungu Dkt Malisa, mimi kama mimi ninakubaliana kabisa na maelezo yote
uliyoyatoa. Hali kwa kweli ndivyo ilivyo.
Hata hivyo kwa wapendwa
wote, naomba mwenye kufahamu maana halisi ya andiko la Wakolosai 3:15
atusaidie, nalo linalosema “Na AMANI ya Kristo iamue mioyoni mwenu”.
Ninaomba msaada huo kwa
sababu mara nyinyi andiko hili, limekuwa likitumika na wapendwa wengi kuelezea
kuwa amani ya Kristo ndicho kipimo chetu cha kuamua mambo, na ndivyo ilivyo.
Ninaomba nifafanuliwe kwa sababu nashindwa kuelewa kwa nini tunatofautiana
wakati Kristo ni moja? Katika jambo hilo hilo moja, wengine wanasema wanayo
AMANI kulifanya na wengine wanasema hawana AMANI kulifanya, kwa nini?
Mwenye ufahamu
atufafanulie kwa upole, unyenyekevu na uvumilivu wote, maana halisi ya neno
AMANI kama Kristo alivyokusudia.
S H A L O M !
41.
Amani, Heshima na Upendo kwenu nyote. Kwanza nikubaliane na Ndg
Bernard katika kile alichoandika kuhusu michango ya wapendwa humu. Lakini kuna
haja ya kujiuliza kinachowafanya hao wachangiaji wamcharukie mtu. Hapa ni vema
kutoa maoni kulingana na mada na kama unapinga ama la, lakini si kuwaita
uwapingao wapuuzi maana huna ushahidi wowote kuwa uaminivyo ndio sahihi. Kwa
hiyo ni vema kutambua kuwa CHANZO CHA TATIZO NDILO TATIZO. Pengine hayo
yasiposemwa ama mtu akijitahidi kutetea upande wake na si kudhalilisha ama
kuponda upande mwingine na kuukashifu tutaendelea kuelimishana tuu.
Kwako Kaka John nashukuru kwa uchangiaji wako na pia maswali yako nami nitayajibu kama ifuatavyo.
1: Muziki una tafsiri nyingi na pana kulingana na jamii, lakini kwa namna yoyote ile UNAANGUKIA KWENYE TAFSIRI YA KUWA MPANGILIO WA SAUTI. Kwa maana hiyo kila midundo iliyopangiliwa ni muziki japo si kila muziki una midundo.
2: Maswali ya pili ntayajibu kama ifuatavyo. Unless unataka kupinga kuwa muziki hautumiki huko nilikosema, mimi nasema kuwa muziki katika matukio unaendana na mahadhi kulingana na mazingira. Na hili naamini unalijua vema. Tatizo nilionalo hapa ni kuwa wakati wengine tunazungumzia muziki wa injili ki-ulimwengu wapo wanaozungumzia muziki ndani ya mkoa kama si nchi. Na unajua kuwa bolingo waweza kuwa muziki wa asili huko Kongo na usiwe na tatizo kutumika kanisani wakati nyumbani wanautumia kwenye clubs. Sasa je unadhani hapo “mtego” ama “fumbo” liko wapi? Ama wakati wapo ambao wanadhani Reggae ni muziki wa ki-rasta ilhali si ijulikanavyo huko visiwani unadhani kuna mkanganyiko na mchanganyiko gani hapo?
Maswali haya ninayotaka ujiulize ndio majibu ya swali la pili kuwa ukiangalia muziki wa injili kwa nchi ama jimbo ama wilaya ama mkoa fulani inaweza kuwa na maana kuliko kuongelea muziki kidunia. Na mara zote tumekuwa tukitofautiana katika mambo mengi kiimani kwa kuwa wapo wanaoamini kuwa namna dini inavyoaminiwa na kuabudiwa Tanzania ndio njia pekee na sahihi jambo ambalo sina hakika nalo na ndio maana sijawahi kukubaliana nalo.
Kwa hiyo naomba nawe ujitahidi kufafanua maswali hayo katika dhana ya ki-dunia na si ki-Tanzania na hapo tutaendelea kuelimishana.
Kama kuna swali sijajibu na ama unapenda kuuliza basi kuwa huru kufanya hivyo.

Kwa upande wa Mch Malisa nashukuru kwa maelezo yako. Lakini pia
nina maswali maana licha ya kunukuu Biblia juu ya kile inachosema kuhusu aina
za muziki bado hujajibu swali lililoulizwa na ambalo hata wewe umelizungumza
kwenye aya yako uliposema “Utatambuaje tofauti katika ya muziki wa kiroho na
wakidunia? Nadhani hili ndio swali kubwa hapa. Wengine wameona tofauti ni
maneno tu, yaani kama maneno ni ya kimungu haijalishi mudundo ni wa namna gani,
kwao huo ni muziki wa kiroho (injili), wengine wameona ni lazima hata mdundo
nao ufanane kiroho. Hili linawachanganya wengi kwa sababu hakuna mahali po pote
kwenye Biblia pana sema mdundo wa aina Fulani ndio unaokubalika mbele za Mungu.
Kwa sababu ni kweli kuwa shetani amechafua hata uimbaji, ni lazima kuwa na
tahadhari katika aina ya muziki wa injili.”
Kwa hiyo licha ya maelezo mazuri ya aina za muziki kwa mujibu wa Biblia na historia ya Lucifer na alichokimbia nacho, bado swali la ndg Godlove halijajibiwa katika maelezo yako. Unapingana na sisi tusemao kuimba kwa roho na kweli bila kujali midundo lakini husemi sasa MIDUNDO GANI AMBAYO IKIENDANA NA UIMBAJI WA ROHO NA KWELI ITAKUWA YA KIDINI.
Na pengine niulize kama unadhani waimbaji kuwa na mameneja ni kosa. Maana natambua kuwa kama wewe ni Mchungaji mwenye kanisa lenye watu na thamani kubwa unahitaji UONGOZI na kadri linavyozidi kukua ndivyo linavyohitaji watu mbalimbali kuanzia mtunza hazina, mwongoza muziki, anayeshughulikia kupiga picha za video, ku-edit na hata kurusha matangazo kama kanisa linafikia wakati wa kupeleka huduma ulimwenguni kote. Na hapo ndipo utakapoanza kuhitaji mtu wa kushughulikia transmission zako katika Tv mbalimbali na hata safari zako. Unadhani hapo utakuwa si mtumishi kwa kuwa uko ORGANIZED na WELL MANAGED?
Unaonaje juu ya hili?

Kwa kumalizia na kwa masikitiko niseme kuwa nimefuatilia
mijadala kadhaa humu na kilichoonenaka ni kuwa baadhi ya watu wanapoulizwa
maswali mengi na ya undani zaidi na kisha kuonekana kutokuwa na uhakika ama
uwezo wa kuyatetea vema wanakuja na nukuu za kwenye Biblia zinazozungumzia juu
ya kuwa makini na mabishano na kujichunga na wasioamini. Hiyo ni dhana mbaya
ambayo inataka kuifanya dini kuwa ya vitisho kila unapotaka kujua kitu kwa
ufasaha zaidi. Nadhani hili ni la kuacha pia maana kuna haja ya kuwa wakweli
pale tusipojua tunachotetea na inapobidi basi kutojiingiza katika mijadala
ambayo huna ufahamu nayo .
Mwisho kabisa niseme kuwa kuna maswali yangu ambayo nyote mmeamua kutoyajibu na ningefurahi kama nayo yangejibiwa na kwa kufanya hivyo nayaweka hapa kuyakumbusha nikiamini kuwa kama msemacho ndicho muaminicho, mtakuwa huru kuusimamia huo ukweli. Nauliza hivi
1:Je! nyimbo za wanamuziki kama Cosmas Chidumule, Remmy Ongala na hata Mzee Makassy si za injili na hazifai kutumika makanisani kwa kuwa tu walikuwa wakitumia mirindimo iendanayo na hii ya sasa walipokuwa hawajaokoka?
Mwisho kabisa niseme kuwa kuna maswali yangu ambayo nyote mmeamua kutoyajibu na ningefurahi kama nayo yangejibiwa na kwa kufanya hivyo nayaweka hapa kuyakumbusha nikiamini kuwa kama msemacho ndicho muaminicho, mtakuwa huru kuusimamia huo ukweli. Nauliza hivi
1:Je! nyimbo za wanamuziki kama Cosmas Chidumule, Remmy Ongala na hata Mzee Makassy si za injili na hazifai kutumika makanisani kwa kuwa tu walikuwa wakitumia mirindimo iendanayo na hii ya sasa walipokuwa hawajaokoka?
2:Je wasanii kama
Beatrice Muhone, Bahati Bukuku, Rose Mhando, Kijitonyama na wengine wengi
wanaoimba na kugusa watu sasa hazifai kwa kuwa tu zina mirindimo iendanayo na
baadhi ya hiyo mnayoiita ya kidunia?
3:Kwani muziki asili
yake wapi na muziki wa dini asili yake wapi?
BARAKA KWENU
42.
Ndugu Mubelwa, tuko
pamoja!
Jambo moja ambalo
nafikiri ni kwamba hapa HATUPINGANI bali tunajifunza Neno la Mungu. [Kupingana
kutokana na kitu mtu anachokiamini hakutatufaidia kitu bali kila mtu kujipima
na Neno la Mungu. Kuamini kitu fulani, hata kama ni kizuri namna gani
kibinaadamu, kama kitu hicho ni tofauti na lisemavyo na kuonya Neno la Mungu
basi kuamini huko ni bure]. Nimeshaandika jinsi ambavyo tunatakiwa kufanya hivi
kwa lugha ya amani na upendo na heshima. Kama huyu anaamini hivi na mwingine
anaamini tofauti TUNATAKIWA KULIANGALIA NENO LA MUNGU LINAVYOSEMA JUU YA JAMBO
HILO na mwishoni ukweli kujulikana ili kwamba ANAYEKUBALI UKWELI aamuwe
kuufuata na yule ambaye BADO ANASHIKILIA ANACHOKIAMINI, hata kama BIBLIA
IMEWEKA WAZI UKWELI WAKE, aendelee kuamini kinyume na Neno la Mungu. [Hili
ndilo aliloandika Mch. Malisa tarehe 12/3/2009 kwamba ni lazima tuangalie
linavyosema Neno, naye tayari ameshaanza kuleta mafundisho haya kwa kuweka
vipengere vya Biblia vinavyohusiana na jambo hilo]. Lakini NAAMINI lengo la
mijadala hii ni kwamba YULE ASIYEIFAHAMU KWELI YA NENO LA MUNGU aifahamu na
KUIFUATA ili awe mfuasi mkamilifu wa Yesu Kristo aliye katika safari ya kwenda
Mbinguni.
Tuendelee kujadili:
Mimi najibu sehemu yangu
na wengine uliowajumuisha hapa kila mtu ataandika kwa wakati wake.
Kutokana na tafsiri ya
muziki uliyoiweka hapa kwamba ” kila midundo iliyopangiliwa ni muziki japo si
kila muziki una midundo” naomba kuuliza tena kwamba:
1. Kutokana na ukweli
kwamba muziki huwa unatengenezwa kwa kujumuisha milio mbali mbali zikiwemo
ngoma, magitaa, vifaa vya kupuliza na vifaa vingine vyenye milio mbali mbali.
Je, kwako wewe MIDUNDO inamaanisha nini katika mchanganuo wa muziki?
2: Swali la pili bado
sijapata jibu, inawezekana hatukuelewana. Ulichofanya ni kufafanua ulichoandika
mwanzo. kwa ufupi umeandika hivi” mimi nasema kuwa muziki katika matukio
unaendana na mahadhi kulingana na mazingira.” Hiki ndicho ulichoandika kwamba
muziki hutumika kwenye sherehe, kanisani, kwenye clubs, kwenye huzuni nk.
Mambo haya uliyoyaandika
yanatokea duniani kote. Si Tanzania tu na wala si Kenya tu. Kongo, ulikotolea
mfano nako kuna huzuni, sherehe, kanisa, clubs nk. Ninaamini hata huko Kongo
wana nyimbo ambazo hutumika kwenye huzuni, sherehe, clubs nk.
Hata hivyo Bolingo ni
‘Mtindo wa muziki’ na si aina ya muziki kwa maana ya ‘Style’ kama Salsa, Waltz,
Disco, March nk. [Kama nimekosea nisahihishe!]
Kwa kutumia mfano wa
Bolingo ulioutoa naomba tena kuuliza swali la pili nililoliuliza kwamba:
Bolingo iliyotumika
kwenye sherehe ikiimbiwa wimbo wa vifijo na nderemo, Bolingo hiyo hiyo
IKIWEKEWA MANENO YA HUZUNI (bila kubadilisha kitu kingine chochote, maneno peke
yake) inaweza kufanya Bolingo hiyo hiyo itumike kwenye mazingira ya huzuni?
Hata hivyo mimi natoa
mchango wangu hapa kwa kuzingatia WOKOVU na Ukristo kwa ujumla. Sitowi maoni
kwa kuzingatia utaifa, u-bara au utamaduni fulani!
3. Suala la tatu ni vema kwa kuwa umesema HUNA UHAKIKA nalo.
Umezungumzia jinsi watu wanavyoabudu DINI Tanzania wakifikiri ndiyo ilivyo
duniani kote.
Napenda kuweka wazi kwamba Ukishaingia kwenye masuala ya DINI lazima kuwe na utofauti. Na ninawapa pole watu WANAOABUDU DINI. Kuabudu DINI kunaweza kutofautiana lakini KUMWABUDU MUNGU ALIYE HAI, JEHOVA ni kule kule Duniani kote. Kwa maana MUNGU NI ROHO nao WAMWABUDUO imewapasa kumwabudu katika ROHO na KWELI.[Yohana 4:24]. Huu ni ujumbe kwa wanadamu wote ulimwenguni!

Neno la Mungu ndilo
KIONGOZI wetu. Bila kuzingatia hili tunaweza kujikuta tunatofautiana katika
mambo mengi kwa kuwa tu kumbe kuna wengine wanaweza kuwa wanachangia hoja hapa
kwa kuzingatia mazingira wanayoishi, au kutokana na imani zao za dini, au kwamba
wako nchi masikini, au labda nchi tajiri, au kwa sababu ya mila ya nchi fulani
au kwa sababu ya utajiri alionao mtu binafsi. Bila kulitambuwa tatizo hili
HATUWEZI KUFIKIA KUNIA MAMOJA kama Biblia inavyotufundisha. Yesu ni mmoja,
Wokovu ni mmoja na Roho ni mmoja.[Efeso 4:4-6] Kwa hiyo sisi tunaomwamini na
kumfuata Yesu MWELEKEO WETU unatakiwa kuwa mmoja. Ikija HATARI kila mtu
aitambuwa kuwa ile ni HATARI. Likija jambo jema kila mtu atambuwa kwamba lile
ni JAMBO JEMA. Bila kuufikia umoja huu katika Roho Hatari itakuja, wengine
wakaiona kuwa ni hatari wakajiepusha nayo lakini wengine wakaiona kama ni jambo
jema na hatimaye wakaangamia.
Kunapokuwa na utofauti
wa mitazamo juu ya jambo fulani la Ki-Mungu SABABU ya tofauti hiyo ni SISI
BINAADAMU na wala si NENO LA MUNGU. Ili kuondoa tofauti hizi ndiyo maana
tunafundishana hapa tukionyana na kushauriana, kwa kuzingatia Neno la Mungu,
ili tuweze KUUFIKIA UMOJA wa ROHO na msimamo wetu KINYUME na ADUI WA ROHO ZETU
WOTE,[Ibilisi] uwe ni MMOJA bila kujali nchi atokayo mtu au tamaduni fulani au
aina hali yoyote inayotofautisha watu wa jamii moja na nyingine!
4. Maswali yako
uliyomalizia sijuwi sana kama yananihusu na mimi pia. Maana mimi bado sijasema
lolote juu ya muziki wa injili au muziki wa kidunia na wa kiroho. Nilichoanza
nacho ni kuwekana wazi kwanza juu ya ufahamu wa MUZIKI. Tukishapata vipengere
fulani muhimu ndipo nitahitimisha. Kwa hiyo maswali yako hayo sitayajibu sasa
hadi hapo nitakapokuwa tayari kufanya hivyo, lakini natumaini mtu yeyote mwenye
majibu anaweza kuyajibu.
Lakini naomba kuuliza
swali moja kwamba kwa kusema ‘MIRINDIMO’ una maana ni MIDUNDO au ni nini tena?
nisaidie hapa tafadhali!
43.
Wapendwa wachangiaji,
Bwana Yesu asifiwe,
kabla ya kujibu maswali niliyoulizwa, naomba kuambatanisha hapa article inayoelezea jinsi muziki wa kishetani ulivyopenya katika jumuia na hata kanisani. katika makala yangu hapo juu nilionyesha kuwa kuna muziki wa kiroho na wakidunia. Makala hii ni nzito hivyo inahitaji ukomavu katika kuisoma na kuielewa. Sisi tutaendelea kuulizana muziki upi unafaa, lakini shetani yeye yuko busy already!!!!

THE SATANIC ROOTS OF ROCK:
Today, at almost any “heavy-metal” rock concert one can hear the audience being exhorted to rape and murder in the name of Satan. Lyrics such as the following are typical:
“We come bursting through your bodies
Rape your helpless soul
Transform you into a creature
Merciless and cold
We force you to kill your brother
Eat his blood and brain
Shredding flesh and sucking bone
Till everyone’s insane
We are pestilent and contaminate
The world Demonic legions prevail”

Any loving parent today
would be horrified and shocked to learn that their sons and daughters are
eagerly listening to such evil. Perhaps though, some may think privately, “If
only we could return to the ‘good old days,’ with the music of the Beatles.”
Little do most people suspect that it was with those innocent-looking Beatles,
that most of the trouble started.
Modern electronic-rock
music, inaugurated in the early 1960s, is, and always has been, a joint
enterprise of British military intelligence and Satanic cults. On the one side,
the Satanists control the major rock groups through drugs, sex, threats of
violence, and even murder. On the otherside, publicity, tours, and recordings
are financed by record companies connected to British military intelligence
circles. Both sides are intimately entwined with the biggest business in the
world, the international drug trade.
The so-called “rock
stars” are pathetic puppets caught in a much larger scheme. From the moment
they receive their first recording royalties, the groups are heavily immersed
in drugs. For example, much-admired “stars” such as John Lennon of the Beatles
and Keith Richard of the Rolling Stones, were heroin addicts. Richard had to
obtain blood transfusions, replacing his entire heroin-laced blood supply, in
order to get a visa to enter the United States.
The “rock stars” are
also totally artificial media creations. Their public image, as well as their
music, is fabricated from behind the scenes by controllers. For example, when
the Beatles first arrived in the United States in 1964, they were mobbed at the
airport by hundreds of screaming teenage girls. The national press immediately
announced that “Beatlemania” had besieged the U.S.A. But the girls had all been
transported from a girl’s school in the Bronx, and paid for their screaming
performance by the Beatles’ promoters.
The money of the 1960s
rock groups, which in somes cases mounted to hundreds of millions of dollars,
was also totally under the control of mob-connected promoters. From 1963 to
1970, the Rolling Stones made over $200 million, yet the group’s members were
all nearly bankrupt. None of them had any idea of where their money went.
Between 1963 and 1964
the Beatles and the Rolling Stones laid siege to Western European and American
culture. This two-pronged invasion from England was well-planned and
well-timed. America had just suffered the shock of the assassination of
President John Kennedy, while in the streets the mass-based civil rights
movement had just held a Washington, D.C. rally, led by Martin Luther King, of
500,000 people. The rock counterculture would be used as a weapon to destroy
such political movements.
Later in 1968 and 1969,
years which saw a mass strike of students and workers in the United States and
Europe, huge, open-air rock concerts were used to head off the growing
discontent of the population. The rock concerts were devised as a means for
mass recruitment to the drug-saturated, free-sex counterculture. For the
millions who came to these concerts, thousands of tablets of the hallucinogenic
drug, LSD, were made freely avaliable. These drugs were secretly placed in
drinks such as Coca-Cola, turning thousands of unsuspecting victims into raving
psychotics. Many committed suicide.
Less than a half century
ago, our young children studied violin and piano, learning about the great
classical composers such as Bach, Mozart, and Beethoven. As will be shown, the
same record companies who today promote Satanic “heavy-metal” rock have run
covert operations to destroy the musical heritage of these great classical
composers.
For the past thirty
years, Western society has been under the gun of a deliberate plan of cultural
warfare, with the purpose of eliminating Judeo-Christian civilization as we
know it. These plans must not succeed. So that the reader can better combat
this evil, we’ll go back nearly thirty years, when those four innocent lads
from Liverpool, England, the Beatles, were just starting out.
44.
AMIN NGULUMA
Nimefurahi kuwa mjadala huu umerudishwa tena baada ya
kusimamishwa miezi kadhaa iliyopita. Sijui ni kwa sababu niliuliza.
Hata hivyo napenda kuweka sawa hoja ya ndugu yangu mpendwa Fred juu ya kile anachoona kuwa USA ndio kiini cha kazi ya Mungu kuuzwa(Hapa namaanisha nyimbo na mahubiri ya injili)
Inavyoonekana bado tupo katika hatua ya chini kabisa katika kuifikia kweli ya Injili ya Kristo Yesu katika mambo kadhaa na ya kuwa karibu wengi tumefungwa na mipaka ya mafundisho na theolojia za madhehebu yetu.
Hata hivyo ndugu yangu Fred naomba utambue kuwa uimbaji wa nyimbo za injili si huduma ya kuokolea bali ni sehemu ya ibada kwa mkristo awaye yote. Unaweza kujifunza kwa kuangalia namna mwinjilisti Luka alivyoandika akionyesha hatua mbali mbali kabla ya mateso ya Yesu,na wakati wanafunzi wa Yesu wakisubiri ahadi ya Baba. Mara zote walikuwa akielezea kuwa waliimba(wakiwa bustanini,na siku zote walizokuwa wakidumu katika kumngojea Roho mtakatifu)-Soma kwa makini injili ya Luka na Matendo ya mitume.
Lakini kanisa limekuwa likitumia nyimbo katika ibada zake karibu karne zote za uhai wake na baadaye kuziweka nyimbo hizi katika vitabu mbali mbali za nyimbo kama vile (Hapa nitataja vitabu vya kiswahili) Nyimbo za dini,Tenzi za Rohoni,Nyimbo za wokovu,Nyimbo za kikristo n.k. vitabu hivi vinauzwa havitolewi bure. Teknolojia ya kutunza nyimbo kwa njia ya sauti yaani VHS,DVD na VCD inaelekea kuchukua nafasi ya vitabu katika karne hii.
Ndugu yangu Fredi je vitabu vya nyimbo ama hata Biblia inatolewa bure? na kama vinauzwa unasemaje sasa.
Je udhambi wa kuuza kanda za nyimbo za injili unazaliwa wapi endapo Biblia ambalo ndicho kitabu mama cha kikristo kinauzwa?
Tuache kuingiza cults kwenye imani ya kikristo tutaelekea kubaya.

Niendelee kuwashukuru ndugu wote ambao mmetia mioyo yenu katika
kuelimisha kanisa la Mungu
AMANI IWE KWENU NYOTE.
AMANI IWE KWENU NYOTE.
45.
Mumebarikiwa kujua yote
hata hamhitaji mtu awafundishe kumjua Mungu.
Ndugu zangu naomba
niwafahamisha kwamba mjadala huu haujaleta amani rohoni na ikiwa tunashindwa
kutambua kwamba adui amekwishaingia hapa basi upofu umekwishashika mizizi.
Mti wa mema na mabaya
huleta kifo na ndicho kinachoendelea hapa.Tukumbuke kwamba hata kama unaeleza
ukweli na taarifa sahihi LAKINI kukawa hakuna amani juu ya unachosema basi kuna
tatizo.Na ndicho ninachopata katika mjadala huu.
Maelezo yote haya
yanayotolewa kimsingi yanapaswa kuzungumzia jinsi ya KUMWABUDU MUNGU KATIKA
ROHO NA KWELI.Ikiwa tumeona kwamba huu ndio moyo wenyewe basi tungekuwa
tumepiga hatua na kujua nini hasa kinapaswa kufanyika majira haya.
Kuna maswali yameelekezwa
kwangu.Kimsingi ikiwa kuna mtu anaamini kwamba kuna mafunuo mapya juu ya
kilichoandikwa kwenye Biblia na kwamba wengine hawawezi kujua kwa kuamini na
kukitendea kazi kilichoandika hadi wamefunuliwa basi kuna kazi.
Kamwe usiitumainia akili
zako.Jihoji kwanini umeambiwa umepokea bure utoe bure.Je, wajua maana yake?
mipaka yake ikoje?
Hakuna orodha ya dhambi.
Dhambi ni chochote kilicho kinyume na AMANI.Je, wajua kwamba kinachoendelea
sasa katika mada hii hakileti AMANI?Na kwanini watu wanaendelea kuchangia?
Kinatoka wapi wanachochangia?
Waefeso 4. Tunapata
msingi wa namna tunapaswa kuishi.Je, unapata ukweli wa andiko hilo kwenye mada
inayoendelea?
Ikiwa wajua maana ya
kumwabudu Mungu katika roho na kweli.Unachochangia ni nini?
Kwa kuuliza yote hayo haimaanisha
ninahitaji majibu bali nakusihi umhoji Mungu nini hasa anakitaka kwetu majira
haya na ikiwa kuna maisha katika mada hii na mengine ambayo yamekuwa
jakichangiwa.
Amani ikifundishe
yote.Amen
46.
Ninamshukuru Mungu wa mbinguni kuwa mawazo yangu yalipata kibali
cha kuwemo katika blog hii kuhusiana na nilichochangia ambacho sina mashaka
kuwa ni sehemu ya kile ambacho Mungu muumba mbingu na nchi amekipanda ndani
yangu kwa neno lake lililo hai na lenye nguvu ya kutambua mawazo na makusudi ya
moyo.
Niendelee kusisitiza kuwa tusipoangalia msingi wa imani yetu tutafikia mahala tutatoka katika mpango sahihi wa Mungu kama wana wa Israeli walivyojikuta wakikwazwa na sheria ambayo waliahidi mbele za Musa na hata Yoshua kuwa wataishika.
Naomba tufunguliwe macho yetu ya rohoni kujua kuwa msingi wa imani yetu ni katika NENO LA MUNGU na si kwa jinsi tulivyo na amani kwani amani ya kweli inapatikana kwa Yesu ambaye ndiye neno la MUNGU na ndiye Mungu mwenyewe. Hivyo amani yoyote isiyo na msingi na shina la neno la Mungu amani hiyo si ile iliyoachwa na Yesu.
Pili niweke sawa jambo hili kuwa kuabudu si kuimba pekee ila ni maisha halisi ya kiroho kwa kila anayemwani Bwana Yesu na aliyemkabidhi maisha yake huyo (YESU). Ni maisha yaliyo uhai kamili kwa kila aliyekombolewa na kufahamu thamani ya wokovu wake na katika hili kuimba kunakuwa sehemu tu ya kuonyesha maisha hayo. Hii ikiwa ni pamoja na kusifu na kumwadhimisha Bwana Yesu.
Pia niwe muwazi kusema jambo hili ambalo sasa linatumiwa kama njia ya kuwafanya watu waishi kwa woga na tahadhari inayowafanya kupoteza uhuru wao halisi uliotangazwa na Bwana Yesu (LUKA4:18). Shetani yupo wakati wote huu ambao tunasubiri siku ile kuu ya pambazuko la roho. Anatenda kazi kwa namna mbali mbali na pia kwa habari ya kulivamia kanisa amefanya hivi kwa karne nyingi sana tangu kanisa la kwanza (soma waraka wa kwanza wa Yohana:1-2). Ndio maana tuna utitiri wa madhehebu duniani kudhihirisha kuwa uvamizi ndani ya kanisa umekuwepo. Lakini Mungu anawajuwa watu wake kwani wameshapigwa muhuri tayari na Roho Mtakatifu na wao wanaijua sauti ya Mchungaji mwema. Kinachofuata sasa si kupiga kelele za shetani amelivamia kanisa bali tuinue macho yetu juu kumtazama Kristo alipo ameketi mkono wa kuume wa Mungu baba mwenyezi kwa kujua sana kweli yake ambayo ni neno lake. Pia kuomba kwa bidii mbele zake ili upate kuwafahamu ndugu sahihi walio na roho moja nawe (Efeso4:4). Na si kuogopa namna watu wanavyonengua kwenye uimbaji ama kubarikiwa na kundi fulani ambalo linapokutanika kuna kunena kwa lugha ama matendo ya miujiza.
Mungu awabariki sana ndugu wapendwa kwa moyo wenu wa kumtumikia Mungu kwa njia hii ya kubadilishana mawazo na si kurumbana kusiko na faida.
AMEN

47.
Amani, heshima na upendo kwenu nyote. Na naendelea kushukuru kwa
kila anayechangia.
Nilipotezwa na majukumu kiasi na namshukuru MUNGU kuwa nimerejea kujifunza zaidi na zaidi. Kwako kaka John
1: Midundo inaweza kuwa kiashiria cha utamaduni wa asili ya muziki. Mfani kuna midundo ambayo ikisikika watu watajua kuwa ni muziki wa Latin America, lakini pia muziki unakuwa na kama ilivyo kwa vitu vingine visivyo na mipaka” huwezi kuu-limit kuwa utakuwa umetokea ama umepigwa huko kwa kuwa tu ni asili yake. Na ndio maana leo hii tunasikiliza Gospel za midundo na mahadhi ya aina zote. Ninalomaanisha hapa ni kuwa MIDUNDO HAIBEBI UJUMBE BALI ASILI NA TAMADUNI.
2: Sina hakika na tofauti ya Bolingo na Salsa kiutendaji (zaidi ya kimatamshi na asili). Lakini kama unaamini kuwa Bolingo si aina basi naamini na salsa pia. Kwa hiyo nahisi ama niseme kuwa naamini kuwa vyote viko pamoja. Na kuhusu kubadili maneno “bila kubadili kitu kingine chochote” nadhani unaweza kufanya hivyo kwa dhamira ya kubishana tu na si katika uhalisia wa mambo. Ni sawa na kumwambia mtu ALIE KWA TABASAMU. Ninavyofahamu mimi ni kuwa nyimbo zitawekewa maneno ziendane na midundo na / mahadhi kama lengo ni kufikisha ujumbe sahihi. Kwa hiyo REALLISTICALLY sioni MANTIKI ya kubadili maneno na kuweka ya huzuni kwenye wimbo wa sherehe. Hiyo kwangu ni dhana ya kudhihirisha kitu ama kutengeneza parody na si kwa lengo kamili la muziki.
3: Hili nahisi umelielezea na kuweka utata zaidi. Umesema huabudu dini bali MUNGU ALIYE HAI. Natambua kuwa wewe ni MKRISTO na kama hauukani sasa basi unaabudu Mungu aliye hai kwa kuwa wewe ni mkristo na UKRISTO ni dini ya wale ambao wanamcha na kumfuata KRISTO (naamini wewe ni mmoja wapo labda useme vinginevyo). Na pia natambua kuwa kuna wengi wanaomuabudu Mungu japo kwa njia tofauti na Kristo na ndio maana si waKristo, kwa hiyo kusema huabudu dini bali wamwabudu Mungu unaweza kuwa na maelezo tofauti na nilivyoelewa mimi na niaendelea kutunza haki ya kukosea na kukosolewa. Kwa hiyo ukihisi sijakuelewa basi nikosoe tafadhali.
4: Kwa swali hili ningefurahi, kushukuru na kufarijika kama ungeeleza tofauti uliyonayo kati ya MIRINDIMO na MIDUNDO.

Kisha nami ningefurahi
kuona upande uliopo katika hili, kujua una mtazamo gani na namna unavyoweza
kutuelimisha kulingana na mtazamo wako.Na pia ningependa kujua nyimbo
unazopenda kusikiliza ambazo unaamini NDIZO NYIMBO ZA DINI / ZIFAAZO MAKANISANI
Nikirejea kwa Dr Malisa,
umeanza kwa kusema “kabla ya kujibu maswali niliyoulizwa, naomba kuambatanisha
hapa article inayoelezea jinsi muziki wa kishetani ulivyopenya katika jumuia na
hata kanisani.” Na baada ya hapo hujajibu maswali. Sijui ulikuwa ukimaanisha
kuwa utayajibu wakati mwingine ama la!! Lakini katika maoni yako yote uliyotoa
sijaona ukijaribu kujibu maswali yaliyoulizwa kuhusu Muziki ufaao. Na pia umetoa
article ambayo hujaeleza umeitoa wapi na hao walioiandaa walifikia vipi katika
takwimu walizotoa. Pengine work citations husaidia kusaka kwa undani umakini wa
mtayarishaji maana kuna kazi nyingi huandikwa na kuonekana zafaa kwa wengine na
baadae kuja kugundulika kuwa hazikuwa na ukweli. Ndio maana kwenye uandishi
huzingatia “work citations” katika kila unakilicho. Lakini nawe pia ningependa
kupata majibu hasa juu ya MUZIKI UFAAO MAKANISANI. Na ombi la ziada ni kujua
nyimbo unazopenda zaidi kusikiliza ambazo unaamini NDIZO NYIMBO ZA DINI
Kwa Kaka Fred. Kwanza
maswali yangu ya tarehe 2 hayakujibiwa na ningetamani saana kama ungefanya
hivyo ili kujua hao ambao wewe unawasikiliza ukiamini kuwa wanaimba ama wana
muziki wa injili ufaao makanisani. Na katika maoni yako ya tarehe 24 umesema
“Mti wa mema na mabaya huleta kifo na ndicho kinachoendelea hapa.Tukumbuke
kwamba hata kama unaeleza ukweli na taarifa sahihi LAKINI kukawa hakuna amani
juu ya unachosema basi kuna tatizo.Na ndicho ninachopata katika mjadala huu.”
Pengine ingependeza kama ungefafanua unachomaanisha. Maana unatambua fika kuwa
si kila mtu ana uelewa mkubwa kama wako na bila ufafanuzi hakutakuwa na
kutimilika kwa lengo la kuelimishana.
Mwisho narejesha maswali yangu kwa mara ya tatu na naamini ntajibiwa
Nauliza hivi
1:Je! nyimbo za wanamuziki kama Cosmas Chidumule, Remmy Ongala na hata Mzee Makassy si za injili na hazifai kutumika makanisani kwa kuwa tu walikuwa wakitumia mirindimo iendanayo na hii ya sasa walipokuwa hawajaokoka?
Nauliza hivi
1:Je! nyimbo za wanamuziki kama Cosmas Chidumule, Remmy Ongala na hata Mzee Makassy si za injili na hazifai kutumika makanisani kwa kuwa tu walikuwa wakitumia mirindimo iendanayo na hii ya sasa walipokuwa hawajaokoka?
2:Je wasanii kama Beatrice
Muhone, Bahati Bukuku, Rose Mhando, Kijitonyama na wengine wengi wanaoimba na
kugusa watu sasa hazifai kwa kuwa tu zina mirindimo iendanayo na baadhi ya hiyo
mnayoiita ya kidunia?
3:Kwani muziki asili
yake wapi na muziki wa dini asili yake wapi?
BARAKA KWENU
48.
Kwa ndugu Mubelwa,
Pole kwa majukumu!
..nayo ni baraka pia.
Nashukuru kwa majibu
yako. Katika unayoyaandika kuna mambo ambayo najifunza pia.
1.Tafsiri yako ya
MIDUNDO nitaiacha kama ilivyo kwa kuwa umeandika unavyoelewa wewe. Ni haki
yako!
2.Jambo hili la pili ni
moja ya mambo ambayo inabidi tuwekane sawa.
i). Suala la Bolingo
kuwa ni mtindo na si aina ya muziki ni la kimuziki [taaluma] zaidi. Bolingo ni
mtindo kama ilivyo kwa Taarabu. Bolingo hupigwa kwa kutumia [mara nyingi]
mdundo wa Disco na Taarabu nayo hutengezwa kwa kutumia zaidi mdundo wa Slow
Rock. Salsa ni ‘style’ kama zilivyo Disco na Slow Rock. Hata hivyo maelezo haya
ni ya kitaaluma ya muziki kwa hiyo mtu kama hafanyi muziki ni vigumu kuyaelewa.
Lakini maelezo haya machache nafikiri yanatosha kuweka ACBs.
ii). Kama ambavyo muziki
uliopigwa kwenye ‘sherehe’ hauwezi kufaa ukipigwa kwenye ‘huzuni’ [kama
ulivyo], hali kadhalika muziki uliopigwa kwenye ‘club’ hauwezi kufaa ukipigwa
kanisani, [pasipo kuubadili chochote]. Unless hatukubali kwamba muziki
hubadilika kutokana na mazingira na hali ya unapopigwa!.
Kwa hiyo hapa tunaona
kwamba SI KWELI tukisema ‘muziki ni muziki tu’ bali ‘maneno ndiyo hubeba
ujumbe’. Kama ingekuwa ni kweli basi muziki uliopigwa kwenye ‘sherehe’
tungebadili maneno tu na huo huo tukaupiga kwenye ‘huzuni’ muziki uliopigwa
kwenye ‘club’ tungebadilisha maneno tu na tukatumia muziki huo huo kanisani.
Lakini hili haliko hivyo kama ambavyo umeeleza kwamba ni sawa na kumwambia mtu
‘alie kwa tabasamu’.
Mazingira ya kwenye
sherehe ni tofauti na mazingira ya kwenye huzuni. Mazingira ya kwenye sherehe
za siku ya wafanya kazi duniani ni tofauti na mazingira ya kwenye mkutano wa
Injili. Mazingira ya kwenye Vilabu vya pombe ni tofauti na mazingira ya
makanisani. Furaha ya kanisani ni tofauti na furaha ya kwenye Club. Hivyo hata
kama ni muziki wa ‘sherehe’ ukapigwa kwenye club, muziki huo haufai kuupiga
kwenye ‘sherehe’ ya kanisani kwa kuwa mazingira ya sehemu hizi ni tofauti. Kwa
hiyo basi muziki unaopigwa kwenye sehemu hizi lazima uwe UMEPANGWA VEMA
KULINGANA NA HALI YA SEHEMU HUSIKA ili kufikisha ujumbe sahihi.
Tukisema ‘muziki ni
muziki tu cha maana ni maneno’ tutasababisha muziki fulani, pasipokuzingatia
ujumbe unaokusudiwa, upigwe sehemu isiyo yake na kwa njia hiyo tutakuwa
tunatengeneza parody na si kwa lengo kamili la muziki.
3. Dini ziko nyingi na
kila dini ina utaratibu wake wa kuabudu. Utaratibu huu waweza kubadilika toka
sehemu moja hadi nyingine. Ndiyo maana hata Padri Privatus Karugendo alishawahi
kulalamika kwamba jinsi dini yao inavyoendeshwa hapa Tanzania ni tofauti na
jinsi inavyoendeshwa sehemu nyingine za ulimwengu. Watu wengi wana dini lakini
si wote wanaommwamini na kumfuata Yesu Kristo. Hata baadhi ya wale wenye dini
zinazoitwa za Kikristo wengine wao hawafuati mafundisho ya Bwana Yesu lakini ni
wafuasi wazuri wa mafundisho ya dini zao. Ni waumini wazuri wa dini lakini si
waumini wa Bwana Yesu. Watu hawa ndio wanaoabudu Dini.
Watu wanaomwamini na
kumfuata Yesu hawa humwabudu Mungu. Huishi na kufuata mafundisho ya Bwana Yesu
kama yalivyoandikwa kwenye Biblia. Utaratibu wao wa kuabudu ni kulingana na
Biblia. Hawa ndio waabuduo halisi. Hawa ndio Yesu Kristo alisema kwamba Mungu
Baba anawatafuta; wanaoabudu katika Roho na kweli. Ndiyo maana nikakuambia
kwamba WATU WOTE WALIOOKOKA WANATAKIWA KUMWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI. Ni
utaratibu wa ulimwengu wote.
4. i).Umenirudishia
swali ambalo nilikuomba unisaidie. Nitalijibu ili tufupishe dialogue:
Kwa maana na tofauti
niliyonayo mimi MRINDIMO ni Muungurumo. Ni mlio wa sauti nzito unaoendelea kwa
muda fulani. Mlio wa sauti nzito ambao ni wa muda mfupi ni Kishindo. Mfano ni
kama vile radi ikipiga ule muungurumo unaojitokeza pale ni mrindimo; na
MDUNDO ni mlio wa ngoma.
Inaweza kuwa ‘electronic’ au ‘acaustic’ drum. Ni mlio unaosikika baada ya ngoma
kupigwa.
ii. Nyimbo ninazopendelea kusikiliza ni zile ambazo muziki wake
umepigwa kwa kuzingatia ujumbe wa Kikristo unaokusudiwa kuwafikia watu. Kwa
upande wa pili sipendi kusikiliza nyimbo ambazo muziki wake umepigwa kwa kigezo
cha muziki ni muziki tu pasipo kuzingatia ujumbe unaokusudiwa uwafikie watu.
Hiyo ni vurugu.
Kwa hiyo mimi siko upande wowote, niko kati kati!
Kwa hiyo mimi siko upande wowote, niko kati kati!
Ninaandaa maelezo, kama somo fulani, ambayo nitayaleta mwishoni
baada ya kuwa tumekubaliana juu ya mambo kadhaa ya msingi.
Kama kuna mahali hujanielewa unaweza kuuliza swali maana mimi niko tayari kujibu kila swali linalojitokeza kutokana na ninachokiandika hapa. Huwa sina tabia ya mtu aniulize swali halafu nikamrudishia swali hilo.

Kwa sasa nitajibu kwa
kiasi fulani maswali yako ambayo umeyauliza kwa mara ya tatu sasa:
1. Nyimbo za wanamuziki
uliowataja, na wengine wengi, ni za injili na zinafaa kutumika makanisani kwa
kuwa zina ujumbe unaohusu Injili na Neno la Mungu kwa ujumla.
Wengi wa watu ambao
walikuwa wanapiga muziki secular halafu wakaokoka kuna badiliko kubwa sana
kwenye muziki wanaoupiga baada ya kuokoka. Tofauti hii inaweza isieleweke kwa
mtu ambaye hajuwi kutotofautisha ‘lugha’ ya muziki. Waimbaji kama Cosmas
Chidumule, na wengine wengi, muziki wao wa sasa unatofauti kubwa sana na
unastahili kabisa kubeba ujumbe wa Neno la Mungu. Wako baadhi ya wanamuziki
ambao walipookoka hawakulijuwa hilo na kuendelea kupiga muziki kama ule ule wa
zamani. Watu hawa hata ukisikiliza nyimbo zao haziko vizuri maana ni
mchanganyiko wa mambo na wala hazidumu angani! Siwezi kutaja mmoja mmoja hapa
kwa kuwa hapa hatuko mahakamani kuhukumiana lakini tunachoweka hapa ni kama
kioo ili kila mtu ajiangalie yuko sehemu gani.
2. Wasanii kama Beatrice
Muhone, Bahati Bukuku, Rose Muhando, Kitonyama na wengine wanaoimba na kugusa
watu sasa nyimbo zao zinafaa. Waimbaji uliowataja ni baadhi ya waimbaji ambao
nyimbo zao zimepigwa muziki kulingana na wimbo wenyewe. Msisitizo [emphasis]
katika nyimbo zao ni ujumbe na sio muziki [intrumental]. Nyimbo nyingi za
waimbaji uliowataja zimepigwa muziki rahisi ambao humfanya msikilizaji asikilize
maneno zaidi kuliko muziki. Ingawa ziko baadhi ya nyimbo ambazo zingepigiwa
muziki mbadala ujumbe wake ungemfikia zaidi msikilizaji kuliko zilivyo sasa.
Hapa pia sitataja nyimbo hizo kwa sababu niliyoiandika hapo juu.
3. i).Muziki asili yake
ni mbinguni.
ii). Kwangu mimi hakuna
muziki wa dini kwa sababu ala za muziki zinazotumika ni hizo hizo kwenye nyimbo
zinazohusu Neno la Mungu na nyimbo zisizohusu Neno la Mungu. Gitaa hilo hilo
hupigwa kwenye muziki wa kidunia na muziki wa Neno la Mungu na vivyo hivyo kwa
vyombo vingine vyote vya muziki. Kinachobadilika ni namna chombo hicho
kinavyotumika.
Ninachoweza kujibu ni
kwamba Muziki wa Injili asili yake ni kwa watu wanaoimba habari za Neno la
Mungu. Watu ambao wanakusudia kuihubiri Injili kupitia nyimbo zao.
Kama kuna mahali popote
ambapo sijaeleweka au sijajibu ipasavyo nakaribisha swali kwa moyo wa
kujifunza!
Changamoto
ninachokuachia ndugu yangu Mubelwa ni hii:
March 18 uliandika
kwamba wewe hupendelea sana muziki wa Reggae. Swali ni kwamba Je,unaifahamu
sababu inayokufanya upendelee muziki huo?
Utakapokuwa unalijibu swali hili [mimi sihitaji jibu lake hapa]
zingatia yafuatayo:
i). Sababu hiyo si Ujumbe – Kwa sababu ujumbe wa Neno la Mungu unaimbwa katika muziki wa aina mbali mbali na kama lengo ni ujumbe basi ungependelea kila aina ya nyimbo ili uweke kupata ujumbe wake.
ii). Sababu hiyo siyo muziki wenyewe – Kwa sababu muziki hauna maneno. Milio ya gitaa na vinanda na ngoma haiwezi kutafsiriwa kwa maneno ambayo yanaweza kuwa na ujumbe kwa mtu. Kwa hiyo kama ni kwa sababu ya muziki wenyewe basi hakuna lolote unalojifunza kutokana na kupendelea muziki huo.
iii). Sababu hiyo si asili – Kwa sababu wewe asili yako si kule ambako muziki huo ulianzia.

Kwa hiyo nakuanchia
changamoto hii ili ufahamu ni nini kinakufanya upendelee muziki aina ya Reggae.
Tuendelee kujifunza.
49.
Ndugu zangu neema iwe nanyi.
Namshukuru Mungu kwa yote.
Niweke wazi mapema kuwa
huu mjadala haujengi na kwa kiwango kikubwa umeruhusu Babeli kupata nafasi
zaidi.
Ndugu Mubelwa T Bandio
usimpe ibilisi nafasi, acha ubishi, una roho udadisi usio na msingi(critical
spirit) wa kujenga, uwe makini, tubu na umtii Bwana.Hali hiyo lazima ikome mara
moja.
Kuna watu humu ndani
lazima vinywa vyao vizibwe.
Wakolosai 3:15.
Hatuwezi kufika kwa
utaratibu huu.
Mwenye masikio ya
kusikia na ayasikie haya.
Amani iwe nanyi.
50.
Wow!
Mwenye macho na asome maoni yako yote Fred
Amani iwe nawe pia.
Mwenye macho na asome maoni yako yote Fred
Amani iwe nawe pia.
51.
Hello watakatifu wa Bwana,
Nashukuru Mungu kwa kunipa nafasi hii tena ya kushirikiana nanyi mambo ambayo ameweka katika moyo wangu. Ni muda kidogo nimepotea, na hii ni kutokana na majukumu ya hapa na pale. Nashukuru kuona mijadala inaendelea hapa SG, lengo likiwa ni kujifunza na kukua kiroho, katika safari yetu ya kwenda mbinguni!

Ningependa nianze kusema
kuwa sitaweza kujibu baadhi ya maswali kwa leo, maana siajapata muda wa
kuyapitia. Lakini wakati ninaendelea kupitia maswali, nimeona niseme machache
juu ya mjadala huu.
Kwanza lazima ifike
mahali tuone kwa namna sahihi maisha ya kikristo na wokovu. Tunapomkubali Yesu
Kristo, na damu yake iliyolipa gharama za makosa yetu, tu watakatifu mbele za
Mungu, na toka hapo tunakuwa tumeokolewa na kama ukifa, unaenda mbinguni.
Lakini Mungu kwa makusudi kabisa, hatuondoi duniani tukiisha kuokolewa, KWA
NINI? Kwa sababu anataka tuishi maisha yanayoonyesha kuna kitu kisicho cha
kawaida kimefanyika. Anataka tuwe nuru na chumvi ya ulimwengu. Hapa ndipo
wapendwa wengi wanakwazika.
Maisha ya Kikristo ni
maisha ya kujitenga na ulimwengu. Waefeso 5:11 inasema tusiwe na shirika na
kazi za giza bali tuzikemee. Kwa hiyo ulimwengu unatakiwa kujifunza toka kwa
Kanisa na si kinyume! Haya ndiyo matendo ya nuru.
Wapi ninaelekea? Ni
kwenye Muziki unaofaa mbele za macho ya Mungu. Biblia iko wazi ya kuwa Mungu
hajengi juu ya kitu ambacho msingi wake hakuuweka. Mambo ya walawi 10 tunasoma
jinsi Mungu alivyo makini kuliko tunavyotaka awe. Hiyo imekuwa kanuni ya Mungu.
Wakati shetani anaweza kutumia chochote kutimiza matakwa yake, kwa Mungu wetu
ni tofauti. Hatumii chochote ambacho hajakiwekea msingi.
Tatizo lililopo sasa ni
kuwa wapendwa wana miungu yao waliyoijenga kwenye fahamu zao ambao kwa hakika
hawapo! Mathalani mtu atasema mungu wangu hafanyi hiki au kile. Lakini utakuta
jambo analosema haliko katika Neno la Mungu. Huyo Mungu anayemsema ni mazao ya
mafikirio yake. ni sanamu!
Nikifika kwenye suala la
muziki, kumekuwa na maoni mbalimbali, lakini je ukweli ni upi? Kwa msingi
nilioujenga hapo juu utajua kuwa Muziki wowote ambao asili yake haikuwa
kumtukuza Mungu, yaani ambao Mungu hakuweka Msingi, haufai kanisani! Hapa
nitatoa baadhi ya mifano kuonesha ninachomaanisha.
Lakini kabla sijatoa
mifano hiyo ni lazima tufahamu tofauti ya utamaduni na muziki. Mfano, kuna
utamaduni wa kinyaturu(utaratibu wa maisha wa wanyaturu). Hii inajumuisha ngoma
zao, ibada zao, nk. Utaona muziki ni kasehemu ka utamaduni wao. Pia Lazima
tujue kuwa ukristo,tangu misingi yake, ni utamaduni uliowekwa na Yehova. Kuna
namna ya kuabudu, miiko, nk.
Sasa turudi kwenye
mifano. Nitaanza na hip hop. Wapendwa wengi wamekosea kuita Hip hop muziki! Kwa
wanaoufahamu, ni utamaduni(namna ya maisha). Akihojiwa na mtangazaji mmoja,
Kirk Franklin alikiri kuwa Hip hop ni utamaduni na kanisa ni lazima likumbatie
utamaduni huu ili kuwafikia walio katika utamaduni huu. Hii ni kinyume kabisa
na waefeso 5:11. Aina ya muziki ambayo inatumika kama mashua ya kubeba
utamaduni wa hip hop ni rap. Kwa msingi huo, rap haiwezi kutumika kanisani
kwani ikiruhusiwa kanisani kama ambavyo ilivyo sasa, tutashuhudia (kama tunavyooona
sasa) vijana wakiukumbatia utamaduni huu ambao misingi yake ni kuzimu! Mungu,
kama ambavyo hakukubaliana na Nadabu na Abihu, hakubaliani na Hip hop! nani ana
ujasiri wa kusema kuwa mbinguni tutamwimbia Baba kwa kufoka-foka?
Mfano mwingine ni Sebene!
Kwa bahati tangu utotoni nimekuwa mfuatiliaji wa Muziki huu toka Kongo. Wengi
tunafahamu namna muziki huu usivyofaa kutazama hata katika macho, lakini hata
leo nashangaa jinsi ulivyoingizwa kanisani. Lengo la sebene ni kuwaburudisha
watazamaji kwa viuno na mavazi machafu. Kwa hakika, mara nyingi baada ya kutoka
jukwaani, wanenguaji hupata ofa mbalimbali toka kwa wanaume wazinzi. Sasa
ilikuwaje na inakuwaje tunakuwa na muziki wa namna hii kanisani? Jibu ni kuwa,
haya yote yamepata mlango pale tulipogeuza muziki toka kumsifu Mungu hadi kuwa
starehe! Ni pale tulipogeuza makanisa kuwa Klabuza jamii!
Mfano mwingine ni
taarabu. Watu wa pwani wanafahamu kuwa taarabu ni sehemu ya utamaduni huu.
Mambo yanayofanyika ktk taarabu hayafai kuyaandika. Kwa hakika, taarabu ni moja
ya miziki inayochochea uzinzi na uasherati. Sasa kwa msingi huu, ilikuwaje
taarabu ikaingia kanisani? Je Mungu amebadili misingi ya utendaji wake? Jibu ni
hapana, ila sisi tumetengeneza mungu mwingine ambaye kwake taarabu, hip hop au
chochote kile ni sawa, maadamu tu kibadilishiwe lebo kiwe gospel XXX na
mashairi pia yafanane na ukristo. Huyo si Jehova, bali ni baali, ndama
tuliyojitengenezea.
Kuna mifano mingi tu,
lakini hii inatosha kuonesha ambayo Mungu ameweka katika moyo wangu. Kama
ambavyo ndugu G. Craige Lewis aliuliza ningependa pia niulize, lebo ya 666
ikibadilika na kuitwa Gospel 666 utakubali kuipokea? Bila kujali lebo 666 ni
666 tu!
Ni muda wa kuacha
kung’ang’ania mambo mafu na yenye misingi ya giza, turudi katika misingi halisi
ya Imani yetu. Moja kati ya sifa za Mkrsto aliyekua ni kukubali kugeuka, pale
anapokosea. Kung’ang’ania mambo ya dunia ni utoto wa kiroho, lazima ifike
mahali tukue!
Je hii ina maana kuwa
wanaoimba Hip hop, taarabu, reggae sebene n.k ni wabaya? Siyo lazima iwe hivyo!
Ni naamini ni kwa kuwa wamedanganywa kuwa shetan aliiba muziki wetu hivyo
lazima tuurudishe. Wanahitaji tu kujua matatizo yaliyo katika miziki hiyo!
Mwisho ningeomba
tujadili kwa kufuata Neno la Mungu badala ya mawazo binafsi! Mimi naweza
kuamini kwa mawazo yangu kuwa hakuna mji wa Kericho, na Jirani yangu akaamini
upo lakini ni sayari ya Mars na mwingine akasema Uko phillipines! Bila kuweka
Ramani na kuangalia tutapotea. Mwongozo wetu ni Biblia. Hivyo mijadala yetu iwe
na mipaka ndani ya Biblia.
Neema na amani ya Kristo iwe nanyi!
Amina
Amina
52.
Hapa nimejifunza. Na nimejifunza kwenu nyote. Nawashukru Kaka
Steve M na John Paul kwa haya. Naamini kutakuwa na uwanja wa hili maana nahisi
linaelekea kwenye uhitaji wa ufafanuzi.
Amani kwenu
Amani kwenu
53.
It doesn’t matter what
style music it is as long as the music gives glory to God. God likes any style
of music that glorifies Him.
54.
Kwa ndugu Bernad Mwenda,
Mimi naomba kuchangia
katika swali lako kuhusu AMANI YA KRISTO, ulilouliza tarehe 20/3/2009, kama
ifuatavyo:
Katika Wakolosai 3:15
tunapata andiko muhimu kuhusu suala hili kwamba “Na amani ya Kristo iamuwe
mioyoni mwenu”
Lakini tukisoma sura
hiyo ya 3 kuanzia mwanzo na kuendelea tunapata mambo muhimu sana juu ya mtu
mwenye MOYO au TABIA AMBAYO KWAKE AMANI YA KRISTO INAWEZA KUFANYA KAZI. Baadhi
ya mambo yaliyoandikwa hapo ni yafuatavyo:
i). Mtu aliyefufuka pamoja na Kristo (kuzaliwa mara ya pili)
ii). Mtu anayetafuta mambo ya mbinguni
iii). Mtu aliyevifisha viungo vya mwili asienende kwa kufuata ulimwengu huu
iv). Mtu asiyesema uongo
v). Mtu aliyefanywa upya fahamu zake ili awe na ufahamu sahihi
vi). Mtu ambaye katika maisha yake Kristo ndiyo kila kitu
vii). Mtu mwenye moyo wa rehema, unyenyekevu, upole uvumilivu na mambo yafananayo na hayo
viii). Mtu ambaye amejaa upendo,
ix). Mtu mwenye neno la Kristo kwa wingi ndani yake
x). Mtu ambaye kila analolifanya anafanya kwa jina la Bwana Yesu.

Hayo ni baadhi ya mambo
yaliyoandikwa katika sura hiyo ya kitabu cha Wakolosai.
Kwa hiyo tunaweza kuona
kwamba ili AMANI YA KRISTO iweze kutenda kazi ndani ya mtu, mtu huyo anatakiwa
awe mkamilifu kweli kweli katika Kristo. Mtu ambaye ana uwezo wa kuisikia sauti
ya Mungu ndani yake kupitia Roho mtakatifu.
Mtu aliyeokoka dhamiri
yake huwa ni hai. [Ebrania 9:14] Uhai huu hufanywa katika Roho wa Mungu. Roho
wa Mungu huzungumza ndani ya mtu aliyeokoka kwa kumjulisha kila kitu
anachofanya kuwa ni sawa au si sawa; kwamba ni salama au ni hatari. Ni kama
kipimo fulani cha kiroho ndani ya mcha Mungu. Mambo yanapokuwa ni shwari Amani
hii huwepo moyoni. Amani hii humuongoza mtu kwa masuala yote, yaani mambo
yahusuyo Mungu na mambo yahusuyo binaadamu.
Suala linalotofautisha
utendaji wa Amani hii ndani ya mtu mmoja na mwingine ni mifumo ya maisha
inayotofautiana. [Hapa ni kwa mambo yanayotuhusu sisi binaadamu]. Tofauti hii
yaweza kusabishwa na mambo kama Huduma ambayo mtu huyo ameitiwa katika mwili wa
Kristo; Umri; Mazingira anayoishi mtu na jamii inayomzunguka; Hali ya kiuchumi
ya mtu na mambo mengine ambayo yanaweza kusabisha jambo fulani la kibinaadamu
lifanyike kutokana na utofati huo.
Amani ya Kristo huamuwa
katika mambo mengi. Jambo fulani laweza kuwa si sahihi kufanywa na mtu fulani
au kufanyika kwa mtu fulani wakati jambo hilo hilo likawa si tatizo kama
litafanywa na mtu mwingine. Amani ya Kristo HUONGOZA KATIKA MAMBO MENGINE PIA
AMBAYO SI LAZIMA YAWE NI DHAMBI.
Nitatoa mifano kadhaa:
a). Kazi fulani yaweza
sababisha kukosekana kwa amani ya kristo ndani ya moyo wa mtu ambaye kazi hiyo
inaweza kukwamisha huduma yake aliyoitiwa katika mwili wa kristo lakini kazi
hiyo hiyo inaweza isiwe tatizo moyoni mwa mtu asiye na huduma hiyo husika.
b). Mtu fulani anaweza
asipate amani moyoni kwenda kwa mtu fulani kwa sababu kumbe kama angeenda
asingemkuta
c). Mtu anaweza asipate
amani kusafiri na gari fulani halafu baadaye akasikia gari lile alilokuwa
asafiri nalo lilikwenda akupata ajali.
KUTOFAUTIANA KATIKA
BAADHI YA MAMBO
Kuna mambo ambayo mtu
mmoja anaweza asipate Amani lakini mwingine akasema ana Amani. Kwa mambo
yanayotuhusu sisi wenyewe binaadamu inawezekana kabisa, binaadamu tuna mifumo
tofauti ya maisha. Kama nilivyoandika juu kwamba tuna mambo mengi
yanayotutofautisha. Na haya yanayotutofautisha ni ya kwetu wenyewe binaadamu.
Katika Mambo yanayohusu Mungu huwa hakuna tofauti kwa sababu Kristo ni mmoja na
Roho Mtakatifu ni mmoja.
Huwa inatokea watu
wakatofautiana katika jambo fulani linalohusu maisha ya Kiroho huku kila mmoja
akisema anajisikia Amani. Katika hali kama hii ni lazima upande mmoja uwe na
matatizo. Haiwezekani jambo fulani likawa ni uovu kwa mtu mmoja halafu kwa
mwingine likawa si uovu. Tofauti hii inapokuwa imetokea yaweza kusababishwa na
moja ya sababu zifuatazo:
i). Kuchanganya Amani ya Kristo na Hisia za kibinaadamu
ii). Kuizimisha kwa makusudi Sauti ya Roho mtakatifu
iii). Kutokufahamu kabisa amani ya Kristo na utendaji kazi wake.
ii). Kuizimisha kwa makusudi Sauti ya Roho mtakatifu
iii). Kutokufahamu kabisa amani ya Kristo na utendaji kazi wake.
Maelezo kwa ufupi:
i). Kuchanganya Amani ya
Kristo na Hisia za kibinaadamu
Kuna mtu ambaye anaweza
kuwa ameokoka kabisa na dhamiri yake ikawa hai kwa kutambuwa uongozi wa Amani
ya Kristo katika kujiepusha na mambo mbali mbali ambayo ni machukizo mbele za
Mungu. Lakini katika mwendo wa maisha inaweza ikafika mahali mtu huyo asiweze
kutofautisha kwa usahihi Uongozi wa amani ya Kristo na Hisia zake mwenyewe. Hii
inaweza kusababisha MSISIMKO uchukuliwe kama ndio amani ya Kristo yenyewe. Hali
inapokuwa namna hii lazima kuwe na utofauti kati ya mtu mwenye tatizo hili na
mtu asiyenalo.
Mfano tunaoweza kuutumia
hapa ni kama vile unaweza kuta mkaka ameokoka kabisa lakini katika pilika za
kutafuta mchumba akakutana na mdada ambaye kutokana na umbile lake lilivyo
mkaka huyo akasisimuka na kuona kama huyo ndiye mke wake halisi. Lakini inaweza
kutokea rafiki yake wa karibu akamwambia kwamba hajisikii Amani moyoni na
kumuomba waombe Mungu ili kupata uthibitisho wa suala hili. Lakini mkaka huyo
atabisha na hatimaye kumuoa mdada huyo ambaye baada ya muda utasikia kuna
matatizo mengi sana katika ndoa hiyo.
ii). Kumzimisha kwa
makusudi Roho mtakatifu.
Mtu mmoja anaweza kuwa
anasikia kabisa moyoni mwake kwamba hakuna Amani moyoni juu ya jambo fulani
lakini mtu huyu akang’ang’ana na jambo hilo tofauti na wapendwa wengine
wanavyojisikia. Mtu huyu huwa anakaidi tu kwa makusudi. Ndiyo maana Andiko la
“Msimzimishe Roho” likaandikwa. [1Thesalonia 5:19]. Andiko hili ni kwa mtu
anayefahamu utendaji kazi wa Roho Mtakatifu.
iii). Kutokufahamu
kabisa Amani ya Kristo na utendaji kazi wake.
Kuna watu wengi ambao huwa wanaiga mwenendo wa watu waliookoka.
Ni wakristo waungwana lakini hawajaokoka kwa hiyo mambo ya rohoni kwao
hayaeleweki. Waigaji hawa huweza kubainika wazi linapotokea suala linalotakiwa
litatuliwe kwa mtazamo wa Rohoni na si mwilini. Waigaji hawa, kwa
kutokulipambanua jambo hilo katika Roho, hulazimisha kwa mtazamo wa kibinaadamu
kwamba suala hilo si Tatizo wakati katika mtazamo wa rohoni suala hilo ni
ugonjwa wa kufisha. Wakati mwingine watu wa namna hii hufikiri pia mafundisho
ya mapokeo wanayofundishwa kwenye makanisa yao ndiyo kipimo pia cha Amani ndani
yao.
Katika hali ya namna hii lazima kuwe na tofauti katika jambo hilo hilo moja.
Katika hali ya namna hii lazima kuwe na tofauti katika jambo hilo hilo moja.
Si kila mtu aliye
Mkristo huwa ameokoka na mbaya zaidi Si kila mtu anayesema kuwa ameokoka huwa
ameokoka kweli. Kwa hiyo linapokuwa limetokea jambo fulani la Kiroho ni lazima
tofauti hii ionekane hata kwa watu ambao wote wanasema wameokoka.
HITIMISHO
Amani ya Kristo hufanya
kazi ndani ya moyo wa mtu ambaye ameokoka kikamilifu na anaishi maisha
matakatifu. Amani ya Kristo kwa maneno mengine ni chombo ambacho Roho mtakatifu
hutumia kuwasiliana na wana wa Mungu, watakatifu walioko duniani ambao Mungu
hupendezwa nao, katika kuwaongoza kwenye mapito mbali mbali ya mambo ya rohoni
na hata ya mwilini pia.
Hivi ndivyo nilivyoweza
kuchangia kwa sasa. Kama sijaeleweka mahali fulani au nimekosea, maswali
yanakaribishwa ili kwa pamoja tuendelee kujifunza.
55.
Asante saana mtakatifu
wa Bwana John Paul!.
Mimi binafsi nimeshiba
na kuridhika kabisa kwa maelezo na ufafanuzi wa kina, uliojaa nguvu ya Roho
Mtakatifu, kuhusiana na maana ya `AMANI YA KRISTO` Bwana akuzidishie na azidi
kukutumia,
Amin!.
56.
Ndugu Bernad,
Namshukuru Mungu pia
kama umeridhika kwa maelezo na ufafanuzi nilioutoa kuhusu AMANI YA KRISTO.
Tuzidi kuombeana katika
safari hii ya mbinguni.
57.
Bwana wetu Yesu apewe
sifa,Asante sana kwa kuweka mjadala huu Mungu awabariki sana.Wapo watu wengi
hujiuliza na kuuliza wenzao hata kulaumu kuhusu jinsi wakristo wanavyo msifu na
kumtukuza Mungu wao kwa nyimbo.Mimi kwa maoni yangu MUZIKI AU BEATS ZOTE KWA
LUGHA ZOTE KWA NCHI ZOTE HAZINA MIPAKA WA KUMSIFU NA KUMTUZA MUNGU.Hakuna asili
ya miziki wa Injili, wakristo wanaimba kulingana na utamaduni wa nchi zao,mfano
watu wa Jamaica wanaimba kwa mtindo wa reggae au wafrika ya kusini wanaimba
kulingana na utamaduni wao,hapo huwezi kumkosoa mtu eti ametumia mdundo usiofaa
au unafaa.Wakati Bwana wetu Yesu Kristo alikua hapa duniani hakusema kwamba eti
kwenye masinagogi mtakua mukimsifu kwa kumwimbia Mungu kwa mdundo huu…kama
tunavyo soma katika Maandiko Matakatifu kwamba Mfalme Daudi alimuimbia na
kumchezea Mungu hapo hatujui ni mdundo wa aina gani alioutumia. Kwa hiyo
wakristo tusiende mbali kama sisi wanadamu tunayo mambo mengi yanayo
tutofautisha na mifumo tofauti,nilazima tuseme hawa au wale hawafae kumsifu au
kumtukuza Mungu hivo.Asanteni sana, mubarikiwe…
58.
Baraka kwenu
Ningefurahi saana kama Bw Stev angeorodhesha kabisa ni aina gani ya miziki inatakiwa itumike makanisani kuliko kuunyesha tu ninamna gani miziki haifai,
Ningefurahi saana kama Bw Stev angeorodhesha kabisa ni aina gani ya miziki inatakiwa itumike makanisani kuliko kuunyesha tu ninamna gani miziki haifai,
Mwishoni umesema
tujitahidi kujadili kwakuzingatia Neno au Biblia lakini wewe umezungumza sana
kutokana na mtizamo wako uzoefu wako huoni kwamba unajaribu kuwa selfish na
kutoa miongozo ambayo wewe mwenyewe huifuati???
Unapo weka mfano wa Kirk
franklin na majibu yake huoni kwamba unaulekeza umma sehemu yakujitizama ambayo
sio sahihi kwakuwa Kirk naye ni binadamu kama wewe?
Bw Steve unaweza saana
kukosoa sidhani na sina hakika kama unaweza kujikosoa.
Wapendwa kama tungekuwa
tunaweza kuwa safi au watakatifu kwanguvu zetu wenyewe ingekuwa haina haja ya
Mungu kumtuma Yesu, au Kupata wokovu kwa Neema,simaanishi kwasababu ya hayo
tutende dhambi la hasha ila kwa sababu hatuwezi kuwa watakatifu kwanguvu zetu
wenyewe ndio maana Yesu akaja Neema ikaja na Roho Mtakatifu yote haya ni kwa
ajili ya kutukamilisha.
59.
Amani, Heshima na Upendo kwenu nyote.
Jinsi ninavyorejea maoni na mafunzo ya wengi ndivyo ninavyojifunza zaidi na zaidi na kisha kujiuliza mengi katika nia ya kutaka kujifunza zaidi na zaidi.
Katika baadhi ya maoni nimeelewa (na kama nimekosea nitaomba kukosolewa na / kuelimishwa) kuwa suala kuu si mahadhi tu, wala ujumbe, bali msanii mwenyewe. Anamaanisha vipi katika analoimba na ni vipi amejitolea kumtumikia MUNGU na si kutengeneza pesa kwa kutumia kivuli cha Nyimbo za Injili.
Swali langu ni kuwa tunapozungumzia msanii tunajumuisha “mfumo” mzima wa utayarishaji mpaka utoaji na upatikanaji wa muziki ama? Ninalomaanisha ni kuwa Je! ni sahihi kwa msanii wa nyimbo za injili kumtumia yeyote asiye MKRISTO katika kuitayarisha na hata kuisambaza kazi yake? (Tukumbuke yaliyoandikwa humu kwenye web hii juu ya kutochangamana na wasioamini). Sasa je! wanamuziki wacheza ala wakiwa si waamini ama mtayarishaji, ama mmiliki wa studio, ama msambazaji, hilo litaweza kuharibu utumishi wa nyimbo hizo za injili? Na kama ndio, kuna yeyote anayeweza kusema kuwa anafanya kazi zake na waamini pekee?
Naendelea kujifunza

60.
Mungu ni mwema
Asante sana kaka Mubelwa T Bandio kwa maswali,kabla sijajibu nikubaliane nawe kwamba jambo la msingi si mahadhi ya mziki tu bali inategemea ninamna gani msanii amejitoa kwa Mungu nasio kutumia kivuli cha muziki au nyimbo za injili kwa maslahi binafsi,

Msanii anaye muishia Mungu na kumtanguliza katika mambo yake
yote Mungu atamuongoza Msanii huyo katika maandalizi ya muziki wake.
Haijalishi atampeleka kwa wapagani au walio okoka ilimladi Mungu anaongoza kokote kule ni sahihi.
Haijalishi atampeleka kwa wapagani au walio okoka ilimladi Mungu anaongoza kokote kule ni sahihi.
Mfano mziki wangu
nimerekodia katika studio ya Mchungaji John Said inatambulika kama Hosana
Production,Pruducers ni Ozzeey, Norbert na Amour wote wameokoka,
kuna watu wanaukubali mziki wangu nawengine hawaukubali,
kuna wasanii wa injili wamerekodi kwenye Studio za watu ambao hawajaokoka na bado nyimbo zina nguvu ya Mungu ile ile nanyi mnabarikiwa mkisikiliza nyimbo zao hata kujazwa Roho mara watumishi hawa wanapo hudumu.

Msanii ni mtu yeyote
anae weza fanya kitu chochote kwakutumia ujuzi, akili, maarifa,kipaji,ubunifu
nakazalika.
Mwanzilishi wa sanaa ni
Mungu mwenyewe maana anaujuzi wote akili zote, ubunifu wote, vipaji
vyote,maarifa yote ndio maana ameumba vyote lakini kwa makusudi mema.
Wanadamu tumepewa sehemu
ndogo yakufanya yale tunayo fanya kamwe hatuwezi kufanana na Mungu.
Msanii anaweza kuwa mtu
mbaya yaani muovu au mtu mwema ilimladi anasifa nilizozitaja hapo juu huyo ni
msanii ndio maana hata matapeli tunawaita wasanii kwasababu wametumia akili,
ubunifu,ujuzi,maarifa hadi waka fanikiwa azima yao.
Nisahihi kabisa kwa
msanii wa injili kufanya kazi na mtu yeyote awe mkristo au la. MLADI TU MUNGU
ANAMUONGOZA KUFANYA HIVYO.
MBARIKIWE NA MNAZARETI
ALIYE FUFUKA TOKA KWA WAFU.
61.
Asante saana Ndg Pona.
Nafurahia maelezo ya mtu anayefanya kinachozungumziwa na ama anayekitambua
vema. Huu ni uelimishaji ambao nimekuwa nikitafuta kuweka bayana dhana hii.
Nakumbuka kuna walioandika kuwa “tusichangamane na wenye dhambi/ ambao
hawajaokoka” nami nikajiuliza kama nikimualika ambaye hajaokoka anipigie bass
guitar naweza kuwa nimetengua wokovu wa kazi yangu? Nashukuru kwa majibu yako
na NAENDELEA KUJIFUNZA ZAIDI
62.
ninapenda kuwashukuru woote mlisema chochote katika mada hii
Mungu awabariki. mimi ninadhani kwamba Roho Mtakatifu ndo wa muhimu maana ,
nikiwa na maana kuwa mahusiano na Mungu yakoje yeye ndiye aongozaye mambo
yoote, kwa hiyo haijalishi beat ikoje , wimbo ukiimbwa na mtu aliye jaa roho
watu watabarikiwa na mtu asiyeongozwa na roho aimbe kwa beat tunayodhani kuwa
ni ya kitakatifu nadhani watu wataguna . la msingi ni maisha matakatifu siyo
beat . nimeona wahindi waliookoka wakimwinua Mungu kwa beat za kihindi , je hao
tutasema hawajaokoka ? si hao tu. nimeona pia waarabu. n.k
mbarikiwe.
mbarikiwe.
63.
Tarehe 29/3/2009,
niliahidi kwamba ningeandaa maelezo/somo fulani juu ya mada hii. Na sasa wakati
tunaendelea kusubiri jibu kutoka kwa ndugu Pona kwenye swali aliloulizwa na
ndugu Mubelwa, ninaomba tutafakari yafuatayo ambayo ndiyo mwanzo wa maelezo
ambayo niliahidi ningeyaandaa.
Tuendelee…..
Binaadamu ana milango
mitano [5] ya fahamu katika ulimwengu wa vitu vinavyoonekana. Milango hii ni
KUONA, KUONJA, KUNUSA, KUGUSA na KUSIKIA. Na kila mlango wa fahamu hutafsiri
vionjo wa kitu husika katika mlango huo:
Kwa macho tunaweza kuona
kitu na kutoa maamuzi kwamba kitu hicho ni kizuri au kibaya, kwamba hakifai au
kinafaa kwa namna moja au nyingine, kutokana na mazingira, wakati, umri nk.
Kwa ulimi tunaweza
kuonja kitu na kutambuwa kuwa ladha yake ni mbaya au nzuri kwamba inafaa au
haifai kwa namna moja au nyingine.
Kwa pua tunaweza kunusa
harufu fulani na kutambuwa kabisa kwamba harufu hii ni nzuri au mbaya, ni ya
kitu chema au ni ya kitu kilichooza au kuharibika nk.
Kwa kugusa tunaweza
kupambanua kama kitu tulichogusa kina hali gani; kwamba ni cha baridi,ni cha
moto, ni kikavu, ni laini,ni smooth au rough na hivyo kukifanya kifae au
kisifae katika matumizi fulani na fulani.
Kutokana na ukweli huo
kwa milango hiyo minne ya fahamu, mimi naamini huo ndio ukweli pia hata kwa
mlango wa tano wa fahamu ambao ni KUSIKIA:
Kwa masikio tunaweza
kusikia na kutambuwa kwamba sauti/mlio tunaosikia ni wa furaha, ni wa huzuni,
ni wa kanisani, ni wa msikitini, ni wa gari, ni wa pikipiki, ni wa kihuni, ni
wa kiungwana, ni wa vitani, ni wa maombolezo nk.
Musa, mtumishi wa Mungu
alipokuwa akishuka kutoka mlimani alisikia sauti/mlio ambao ulikuwa ukitoka kwa
wana wa Israel baada ya kutengeneza yule ndama kuwa kama ndiye mungu wao.
Aliposikia sauti hiyo alijiuliza uliza kuhusu sauti hiyo kama ifuatavyo: “Hiyo
si sauti ya watu wapigao kelele kwa sababu ya kushinda vitani, wala si sauti ya
watu wapigao kelele kwa sababu ya kushindwa, bali kelele za watu waimbao ndizo
nazisikia mimi” [Kutoka 32:18]. Si maneno yaliyomfanya atambuwe hilo bali ni sauti
tu! Hivi ndivyo masikio yanatakiwa yafanye kazi, yaweze kupambanua kwamba
sauti/mlio unaosikika unaashiria jambo fulani. Kwa maana hiyo sauti/mlio
wenyewe unatosha kufanya mtu atambuwe sauti/mlio huo unahusiana na kitu gani.
Masikio ambayo hayawezi kupambanua sauti/mlio yatakuwa na tatizo.
Muziki hutoa sauti/mlio
ambao huweza kuwa na maana fulani. Mfano, Kuna muziki wa ala tupu [intrumental]
ambao huweza kupigwa maeneo fulani kutokana na jinsi muziki huo
ulivyotengenezwa. Ni mara nyingi hutokea kukuta watu wanapiga muziki fulani wa
ala ambao huwachanganya wasikilizaji kwa kuwa hauendani na sehemu hiyo. Ambacho
hutakiwa kufanyika ni kubadilisha na kupiga muziki unaoendana na
sehemu/function hiyo.
Linapokuja suala la
kanisani hatutakiwi kuupinga ukweli huu. Kwamba kwa kuwa ni kanisani basi piga
muziki wowote, pasipo kujali! Ikitokea hivi hapa kutakuwa na mambo mawili:
Yawezekana
1. Masiko yetu hayawezi kupambanua vionjo vya muziki, au
2. Tunalazimisha muziki wowote upigwe kanisani kwa maslahi binafsi, kama vile kutimiza tamaa zetu wenyewe!
2. Tunalazimisha muziki wowote upigwe kanisani kwa maslahi binafsi, kama vile kutimiza tamaa zetu wenyewe!
Suala la kuzingatia
katika mada hii ni kwamba muziki ni zaidi ya beat. Beat beat ni MDUNDO. Na hili
tulishalizungumzia na ndg Mubelwa, tukakubaliana.
Kama vile kuona, kugusa,
kuonja na kunusa vina vionjo vyake na tunaviheshimu vionjo hivyo, vivyo hivyo
inatakiwa kuviheshimu vionjo vya kusikia. Macho hutuogonza tusije jikwaa au
kugonga vitu na faida zingine nyingi, Ulimi hutuepusha tusile vitu vibaya na
mambo mengine mengi, Pua hutuelekeza inapotokea kuna harufu mbaya na kwa sababu
hiyo, kwa mfano, tunaweza kusafisha mazingira yetu yakawa safi na faida
zingine, Ngozi hututahadharisha kwamba tulishogusa si kitu chema ili tukiepuke
na mambo mengine mengi. Hali kadhalika Maskio yetu yana uwezo wa kutuongoza
kutokana na sauti tunazisikia kwamba zinahusiana na kanisani au kilabuni kwenye
pombe, zinahusiana na msibani au kwenye sherehe na mambo mengine mengi, kwamba
zinahusiana na Mungu au Shetani ili tuweze kukimbia toka kwa Shetani na
kuelekea kwa Mungu, kwenye usalama wetu!
Kwa leo naishia hapa.
Maelezo haya yataendelea. Lakini kabla ya kuendelea kama kuna swali
linakaribiswa ili tuweze kwenda wote pamoja!
Tuendelee kujifunza.
64.
Nianze kwa kuwashukuru
na kuwapongeza wapendwa waliojadili mada hii kwa kina sana hapo juu.
Ingawa ni mgeni kidogo
katika blog hii, nasukumwa kusema kitu kuhusiana na mada hii ambayo kwa kweli
ni mhimu na inagusa sana mrengo wa imani na matendo ya dini ya Kikristo.
Nimekuwa nikifanya uchunguzi (Research) kwa muda sasa nikilenga kugundua ni
gani hasa ya mziki upigwe kanisani?
Na pengine niwakumbushe
wapendwa waliotangulia kujadili kuwa tunapojiuliza swali hili ni vema pia
kujiuliza kuwa: Ni nini chanzo (nature) ya miziki ambayo inapigwa makanisani
ambayo tunaitilia shaka?
Haya ni baadhi ya
matokeo au majibu ya uchunguzi wangu:
- Hakuna identity ya
mziki wa kanisani tangu zama za mababu na hata leo.Hii ni kutokana na ukweli
kwamba kila ametokana na kabila lake, taifa au nchi yake kwanza kabla hajawa
mkristo. Mfano: Sisi tumekuwa wa Tanzania kwanza kabla hatujawa Wakristo; na
zaidi ya hapa tumekuwa na makabila yetu kwanza kabla hatujawa wa Tanzania. Kwa
hali hii, maisha tunayoishi, na mambo tunayoyafanya hayatokani na new identity
yetu baada ya kuamini, bali na utu wetu wa asili kama wa Tanzania na watu wa
kabila mbalimbali.
Ikumbukwe kwamba: mziki
haujaanzia kanisani, ulianza zamani sana katika jamii zetu. Katika Biblia
tunasoma mziki ulianza na Yubali aliyekuwa baba wa wapiga vinubi katika Mwanzo
4:21. Lakini hata hivyo historia inaonyesha kuwa Yubali pia hakupiga mziki
ambao tungeweza kuuita mziki wa kiMungu pengine! Bali alipiga mziki wa
kitaifa/kiukoo na kabila la Israeli japokuwa alimtaja Yahweh/Mungu katika
lyrics/mashairi yake.
Kila mwimbaji wa nyimbo
za injili anafanya sawa na Yubali. Wote huimba nyimbo za Injili lakini kwa
kuongozwa na Haiba ya kabila au utamaduni fulani. Na zaidi kwa waimbaji wa
Tanzania huvutiwa na styles za nchi za magharibi kama rock n roll, reggae
n.k.Lakini pia hata wasipoiga miziki hiyo bado wataimba kutokana na tamaduni za
makabila yao ambazo sio lazima kuwa zinakubalika na Mungu.
Sasa basi: Wito wangu ni
kwamba tunapofikiri juu ya mziki wa kanisani na wakidunia, tufikiri juu ya
namna ambayo tunaweza ku- CONTEXTUALIZE neno la Mungu na kuli- articulate
katika context yetu ya Kitanzania kupitia mziki ili tupate Haiba ya mziki
halisi wa kanisani. (samahani kwa kutumia maneno ya Kiingereza, sijaweza kupata
kwa haraka maneno mazuri ya kiswahili: unaweza kufasiri). Ninadhani kosa
wanalolifanya waimbaji wetu wa mziki wa Injili ni KULE KUIGA (KU- PHOTOCOPY)
mziki au styles za waimbaji maarufu na kuziingiza kanisani.Waimbaji wengine
hawamjui Mungu lakini styles za miziki yao ipo kanisani, na inawakera sana
Wakristo, hasa mimi. Kwa mfano Miziki ya Rock & Roll asili yake ni miziki
ya kishetani maana watunzi wake walipata uwezo wa kutunga na kucheza kupitia
nguvu za kishetani (Devil worshippers).
Na ukweli ni kwamba,
hata kama waimbaji wetu watabadilisha maneno katika miziki yao, bado
wataendelea kumtukuza na kumuenzi mwanzilishi wa style hiyo. Na kwa kesi kama
hii ni kutukuza shetani aliyewapa uwezo wa kubuni style hizo. Ni hatari na
tunapaswa kuwa makini sana.
Ninaamini kuwa Mungu
amempa kila mwanadamu uwezo wa kufanya jambo la msingi na la kipekee tofauti
kabisa na mwanadamu mwingine. Waimbaji wa mziki wa Injili wanapaswa kumwomba
Mungu awasaidie kutunga mziki ambao yeye Mungu mwenyewe atauanzisha kwao na sio
kuiga.
Kama ambavyo wengine
husema, leo niishie hapa. Asante sana wanablog hii Mungu awabariki sana.
Nitafurahi sana kupokea maswali kuhusiana na nilichokisema. Na pia kukosolewa…
Tubarikiwe:)
65.
Asante saana Cloud.
Labda nami nisubiri wale wenye kuamini kuwa kuna AINA YA MUZIKI UNAOFAA MAKANISANI waorodheshe aina hizo hapa ili kuwekana bayana kwani wapo wanaopinga matumizi kama Reggae (ambayo ni asili ya Carribbean) ama midundo ya asili ya Kikongo, ama Hip Hop ambayo yote ina asili lakini kwetu (Tanzania) yachukuliwa kama ya ki-Dunia.

66.
Ndugu Cloud,
Binafsi nimefurahia
uchambuzi ulioufanya. Na hasa nimefurahishwa na maneno yafuatayo:
“Waimbaji wengine
hawamjui Mungu lakini styles za miziki yao ipo kanisani, na inawakera sana
Wakristo, hasa mimi. Kwa mfano Miziki ya Rock & Roll asili yake ni miziki
ya kishetani maana watunzi wake walipata uwezo wa kutunga na kucheza kupitia
nguvu za kishetani (Devil worshippers).”
Kwa maneno yako hayo
naona unaweka wazo kwamba kuna aina ya muziki ambayo haifai kuwepo makanisani
kutokana na namna ilivyopatikana. Katika kuelezea hilo umetoa mfano wa Rock
& Roll ambayo ilipatikana kwa kutumia nguvu za shetani. Na hapo ndipo
kwenye shina la mjadala: kuzianisha aina hizo za muziki, kama inawezekana,
ambazo kwa sababu moja au nyingine hazifai kutumiwa kwenye muziki wa injili.
Lakini kabla ya
kuendelea ninaomba ufafanue kidogo unamaanisha nini unaposema muziki haukuanzia
kanisani?…yaani kanisa umelichukulia kama kitu gani? Nitafurahi sana kupata
ufafanuzi huo ili niweze kukupata vizuri.
Kuna mengine kadhaa
ambayo ningependa tujadiliane. Lakini naona tukianza na hili moja itakuwa
vizuri tu ili twende hatua kwa hatua. Na kwa kuwa umesema utafurahi kuulizwa
maswali na hata kukosolewa ninaamini utakuwepo kwa ajili ya kujibu maswali yote
yatakaojitokeza kutokana na maelezo yako. Ukiingia mitini haitaleta maana
yoyote!
67.
Naona majibu ya aina mbili hapa. Binafsi nasema AINA ZOTE
ZINAFAA KUTUMIKA KANISANI na kuna ambao wanasema SI AINA ZOTE ZINAZOFAA
KUTUMIKA KANISANI.
Bado nawakilisha ombi langu kuwa TUREJEE KWENYE SWALI LINALOULIZA “AINA GANI YA MUZIKI WAINJILI UNAFAA MAKANISANI?”
Bado nawakilisha ombi langu kuwa TUREJEE KWENYE SWALI LINALOULIZA “AINA GANI YA MUZIKI WAINJILI UNAFAA MAKANISANI?”
Na kwa wale wanaopinga
kutumika kwa aina zote ama nyingi, basi waorodheshe aina wanazoamini ZINAFAA na
watuelimishe ni kwanini wanaamini zinafaa. Binafsi litanisaidia zaidi kuliko
maelezo ya kuwa si miziki yote inafaa ilhali hawasemi ni miziki gani inayofaa.
Blessings
68.
Ninavyofahamu mimi
maswali magumu hayana majibu rahisi. Suala hili na muziki ni moja ya mambo
magumu kwa hiyo jibu lake haliwezi kuwa rahisi kama, kwa mfano, jibu la swali
la mtu kuulizwa utaje jina lako. Suala la muziki ni suala la vizazi na vizazi
na limechanganyikana na mambo mengi. Imani, Utamaduni, mapokeo, ustaarabu nk.
Kwa hiyo linahitaji mjadala mrefu na katika kujadili huko naamini tunaweza
kupata vigezo vinavyoweza kusaidia kuanisha aina hizo.
Kadri mjadala
unavyoendelea yawezekana tukaja gundua labda aina zote za muziki zinafaa; au
baadhi tu ndiyo zinafaa au pengine muziki wowote haufai makanisani. Ninasema
hivi kwa sababu kuna baadhi ya watu wanaamini kwamba kanisani hapatakiwi
kupigwa muziki wowote bali ni kuimba tu! Kwa hiyo nafikiri kinachotakiwa ni
kuwa na uvumulivu, huku kila mtu akijitahidi kuweka aliyo nayo kwa ajili ya
kuchangia mada hii, kwa upole kabisa na kwa kutambua kwamba mada hii ni nzito
kwa hiyo inahitaji mchanganuo wa mambo mengi.
Natumaini kwa pamoja
tunaweza kupata jibu linalofaa!
Ninasubiri majibu kutoka
kwa ndugu Cloud ili niendelee kumuuliza niliyonayo kutokana na mchango wake!
69.
That’s what i thought.
70.
Ni kweli Ndg John kuwa yawezekana kuna ugumu hapa (kulingana na
tafsiri yako).
Lakini haimaanishi kuwa mpaka sasa huna hata aina moja ya muziki unayoamini inafaa. Ningependa u-mention hiyo ama hizo ambazo so far unadhani zinafaa na kisha utuambie ni kwanini (KWA NUKUU ZA BIBLIA) unaamini zinafaa na kama huna aina unayoamini inafaa nalo pia liweke wazi.
NASUBIRI MAJIBU TOKA KWAKO KAMA USUBIRIVYO YA CLOUD

71.
Mungu ni mkuu sana na tena anastahikhi heshima. Kwa hali hiyo
kuimba ni vyema waimbaji wakajua wajibu wao wa kutimiza kusudi la Mungu kwa
kuimba yaani MAPENZI YA MUNGU YATIMIZWE KAMA ILIVYO MBINGUNI NA HAPA DUNIANI.
kinacho nisikitisha ni pale waimbaji wanapoingia katika mtindo wa Bongo beat uwepo wa Mungu unaondoka kabisa haswa pale waimbaji nyimbo zao zinageukia katika usanii na rusha roho.
kinacho nisikitisha ni pale waimbaji wanapoingia katika mtindo wa Bongo beat uwepo wa Mungu unaondoka kabisa haswa pale waimbaji nyimbo zao zinageukia katika usanii na rusha roho.
najua kama waimbaji
watajipanga vyema watu wote wataokolewa na nchi yetu itakuwa na amani. WAIMBAJI
NI WAHUBIRI WAKUBWA SANA LAKINI KWA LEO HAWAIMBI KUMTUKUZA MUNGU AU KUPELLEKA
UJUMBE BALI WANAJIWAKILISHA WENYEWE HASWA NYIMBO ZA VIDEO SIKU HIZI HAKUNA TENA
KUSIFU NA KUABUDU BALI KUNA KUCHEZA NA KUIMBA TUU
KWA HALI HIYO WENGI
TUNASHABIKIA MINENGUO NA SURA ZILIZO CHUBULIWA NA KUWEKWA RANGI ZA AJABU NA
NYWELE ZA BANDIA NA MAVAZI YA MITINDO.
WAPAGANI WASIO MJUA
MUNGU WETU HAWATA BADILIKA TENA. INJILI INAKUWA NGUMU SANA TUNAPO SHUHUDIA
MITAANI
NADHANI WAIMBAJI
WANATAKIWA WAJUE KUWA LuCIFER ALIKUWA KIONGOZI WA SIFA MBINGUNI NA NDO MAANA
ALIPO JIINUA AKATUPWA CHINI MPAKA SASA ULIMWENGU UNATESEKA NA WAIMBAJI
WANACHEZA KWENYE FANI YA LUCIFER
NAOMBA WATENGENEZE MIOYO
YAO NA KUMPA MUNGU UTUKUFU. NASHANGAA MPAKA SASA NYIMBO ZA SIFA ZINAWEKEWA HAKI
MILIKI. WATU WANAPELEKANA MAHAKAMANI KWA KUIBIANA NYIMBO MH TUNAKWENDA WAPI
WAPENDWA? MWIMBIENI BWANA KWA MIOYO YENU YOTE.
AAAAAAAACHA BWANA
AKUINUE UTAPEWA HAKI YAKO TUU UKIMWINUA BWANA
72.
Shalom watumishi wa
Mungu.
Kimsingi ninapenda
kumshukuru Mungu kwa Mwanzilishi wa Mada hii, maana nimekuwa nikitaabishwa sana
Moyoni Mwangu na jinsi huo unaoitwa Muziki wa Injili ulivyo. Namshukuru Mungu
pia kwa ajili ya kaka Steve M. ambaye amechambua vizuri na kuweka mifano ambayo
imenifundisha na kunichekesha pia..
Nikirudi kwenye Mada Husika, nadhani hapa kuna mambo kadhaa ya
kuyatazama.
1. kwanza ninapenda kukubaliana na kaka Steve Kuuita muziki huu Muziki wa Kumsifu Mungu na si Muziki wa Injili.
1. kwanza ninapenda kukubaliana na kaka Steve Kuuita muziki huu Muziki wa Kumsifu Mungu na si Muziki wa Injili.
2. Pili, Muziki wowote wa kumsifu Mungu msingi wake
ni hali ya kiroho ya Muimbaji mwenyewe, nikimaanisha kuanzia mpiga vyombo na yule anayeimba. Kimsingi biblia imetuwekea wazi kuwa waabuduo wanapaswa kumwabudu mungu katika Roho na kweli. Maana yake ni kwamba watu hawa ni lazima wawe na Spiritual connection na Mungu wanayemuabudu, Wakiutambua ukuu na utukufu alionao kwa kiwango cha kuvutwa na kumwabudu katika roho na kweli.

3. Muziki wa kumsifu Mungu unajengwa pia katika msingi wa neno
la Mungu. Kiasi cha neno la Mungu kilicho ndani ya Mtu ndicho kinachojenga
msingi wa Imani ya Mtu na imani hiyo ndiyo inamsukuma mtu kumsifu Mungu kwa
jinsi anavyoamini.
3 Biblia pia katika 1wakorintho 10:31 imeweka wazi kuwa,Watoto wa Mungu wanapaswa kufanya kila jambo KWA UTUKUFU WA MUNGU. maana rahisi ya hili ni kwamba, kama mtoto wa mungu ni lazima uweze kufanya judgement ya Motives zako, unafanya muziki huo kwa sababu gani? is it for the glory of God?

4. Mwanadamu ni Roho iliyo na nafsi, inayoishi katika mwili.
kupitia Nafsi, roho ya mwanadamu inakuwa na connection na ulimwengu pale mtu
anapokuwa self centered, akiishi katika tamaa za mwili. lakini pia kupitia
nafsi roho ya mwanadamu inakuwa na connection na Mungu pale Yesu anapokuwa the
center of your life. kwa jinsi hii roho ya mtu inakuwa na connection na Mungu
na mtu anaishi katika Roho.Whether JESUS is the Center of Your Life or YOURSELF
is the center of your life matters a lot katika uimbaji wa nyimbo za kumsifu
Mungu pamoja na ala zake.
5.Uzuri wa nyimbo za kumsifu Mungu hauwezi kupimwa kwa vile ulivyopigwa, ila unapimwa kwa ile Nguvu ya Mungu na utiisho unaoambatana na wimbo ule kwa kiasi cha kuwavuta watu kunyenyekea mbele za Mungu na Kumwabudu katika Roho na kweli, au kuzijutia dhambi na kumtafuta Mungu kwa upya.

MATATIZO YALIYPO KATIKA
NYIMBO ZINAZOITWA ZA INJILI.
Si kusudi langu Kuhukumu uimbaji wa watumishi wa Mungu, ila
ninataka kuweka wazi yale ambayo ninayaona kutokana na aina ya Muziki uliopo na
jinsi unavyopigwa.
1. Muziki wa sasa umekosa nguvu ya Mungu na wala hauwavuti watu tena kumrudia wala kumwabudu mungu. hii ni kutokana na waimbaji wenyewe kutokuwa sawa kiroho, pia ala/midundo ya Muziki kupigwa na watu wasiomjua Mungu na hivyo ndani yao hakuna uchaji. wanatoa kile nafsi zao zilichonacho ambacho ni tamaa zao binafsi. hii ndio sababu ni kawaida sana sasahivi kusikia wimbo wa injili ukipigwa kwenye baa na watu wakiendelea kulewa na matendo mengine ya anasa pasipo kushituka.

2. Wasanii wengi hawajui neno la Mungu, na kama wanajua,
hawachukui muda wa kutosha kutafakari maana halisi ya wanachojua katika maisha
ya watu. ikumbukwe, uimbaji, kama uinjilisti, ualimu na uchungaji ni huduma
inayohitaji maandalizi binafsi, mtu anatakiwa kujifunza neno, kukaa na
kutafakari, kumwomba Mungu ampe nyimbo za kweli zitokazo kwake, zenye nguvu ya
kuwavuta watu kwa Mungu.
Wasanii wengi hawafanyi hili, wanakurupuka na kuimba nyimbo zitokazo katika akili zao na si katika msingi wa kujua neno la Mungu. unasikia mtu anaimba “acha tuteseke, ulimwengu ututese, watu watusimange, watunenee mabaya,……… tutaendelea kumfuata Yesu” Maneno ambayo yanaleta Negative Faith kwa watu wachanga, inawafanya waone kama kumtumikia Mungu ni mateso juu ya mateso, Biblia imeweka wazi kuwa “Njia za mtu zikimpendeza Mungu, hata adui zake Humpatanisha nao”, tena inasema “uzima na mauti vimo katika uweza wa ulimi”. You dont need to confess any negative thing in your life, kwa nini uconfess kuteseka na kusengenywa?.
Mtu wa jinsi hii akiteseka na kusimangwa atakwenda analia kwa Mungu? sasa watu wengi wanavutwa na midundo, lakini msingi mzima upo katika neno la Mungu na nguvu ya Mungu inayoambatana na wimbo Husika. Nyimbo za kumsifu Mungu si za kufanyia ushabiki na kuhangaika na midundo, zinahitaji hekima ya Mungu kutambua usikilize nini, kwa kuwa tumeshaambiwa “Imani chanzo chake ni kusikia” Warumi 10:17.

3. Kimsingi ninachojua ni kwamba, Kuanzia uimbaji hadi upigaji
wa vyombo vya Muziki wa kumsifu Mungu kunahitaji watu wanaomjua Mungu na wenye
kicho cha kweli, haiwezekani Muimbaji akawa ni mtu aliyeokoka mwenye kicho cha
kweli, akapigiwa ala na Mtu asiyemjua Mungu asiye na kicho cha kweli na mwenye
kuongozwa na tamaa za mwili wake, hapa kuna conflict Kubwa na ndipo matatizo
mengi katika muziki wa ijili yalipotokea. Biblia imeweka wazi kabisa kwamba
“Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake
huyo ni upuuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya
Roho”I Wakorintho 2:14. anawezaje mtu wa jinsi hii kukupigia ala za Muziki
utakaOumsifu Mungu? Motives zake si sahihi na wala ndani yake hamna hofu ya
Mungu.
Kimsingi naguswa sana na uimbaji wa Marehemu Fanuel Sedekia. haiwezekani ukapita kwenye Baa ukasikia wanapiga nyimbo kama Manukato, na nyimbo zake nyingine katika album ile, the same applies katika album yake inayoitwa “katika ibada”
Kioo cha kupima Muziki wa Kumsifu Mungu ni neno la Mungu lakini pia ni nguvu ya Mungu inayoambatana na Muziki huo, Mungu atupe hekima ya kujua kinachoendelea katika Muziki uliopo nyakati zetu.

Mungu awabariki.