Alhamisi, 25 Oktoba 2012

KUNDI LA TATU LA VIJANA WADOGO LASONGA MBELE

Mcheza kinanda wa kanisa la SDA Gofu juu Tanga akiwapigia kinanda wanakwaya wa kwaya hiyo ambao walishiriki katika tamasha la kuwasogeza mbele vijana wa kanisa la KLPT Parishi ya Tanga ambao ndio wanafikisha umri wa miaka 18 kwa sheria za kanisa la KLPT majani mapana vijana hawa wanahesabika kuwa wapiganaji hodari wa vita vya kiroho.
Hawa ndio vijana kumi (10) waliopasishwa na kupewa vyeti na Mgeni Rasmi Mchungaji George Nywage wa kanisa la KLPT majani mapana ukipenda unaweza ukaita Shalom tarbenacle
Mchungaji wa vijana Eva Masongo akiwa katika shughuli zake za kuwafundisha vijana mambo mbalimbali yanayohusu maisha yao ya kiroho.
Kwaya ya SDA gofu juu wakiimba katika tamasha la siku hiyo.
Huyu ni Mama Maombi akiimba katika na vijana wa kwaya ya EAGT mikanjuni.

Jumanne, 23 Oktoba 2012

ILIKUWA NI SIKU YA HUZUNI SANA


IJUMAA  YA TAREHE 19 October 2012 ILIKUWA NI SIKU YA HUZUNI SANA KLPT MAJANI MAPANA TANGA.
Marehemu Austeria Deo wa pili kulia akiwa na wanakwaya wenzake wakiimba nyimbo za maombolezo katika msiba wa mzee Elias Ludamila

Lakini ndugu hatutaki msijue habari zao waliolala mauti,msije mkahuzunika kama wengine wasio na matumaini. Maana ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka,vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu,Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana,kwamba sisi tulio hai,tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana,hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko,na sauti ya malaika mkuu,na parapanda ya Mungu,nao waliokufa katika kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai  tuliosalia tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu,ili tumlaki Bwana hewani na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Farijianeni kwa maneno hayo. (Wathesalonike 4:13   17).
Mchungaji George Nywage akiwa pamoja na waombolezaji nyumbani kwa marehemu wakisubiri kufanya ibada ya kuaga mwili wa marehemu ambao ulisafirishwa kwenda kuzikwa nje kidogo ya mji wa Mbeya.

Nimetanguliza maneno hayo ili kukupa nguvu  msomaji wangu ambaye uliguswa na msiba wa ndugu yetu Austeria Deo (mama Suzi) habari za msiba wa dada yetu huyu zilimshitua kila mtu aliyezisikia. Ninaamini Mungu wetu alifanya siri kubwa sana kwa namna alivyoweza kumpumzisha dada yetu huyu,hakuna mtu wa karibu ambaye ameshasema kwamba Mungu alimuonyesha kwamba kuna mtu mmoja muhimu sana anaweza akaondoka katika familia ya wana Shalom Tarbenacle KLPT majani mapana. Siwezi kusema kwamba ninamfahamu sana marehemu kwa maana ya kwamba labda nimefanya naye huduma katika idara moja ndani ya kanisa,hapana  ninamfahamu kama mshirika mwenzangu ndani ya kanisa, kwa hiyo nitamuelezea kwa kiwango ninachomfahamu. Nianze kwa kusema kwamba ndani ya kanisa kuna wapambanaji wanaoonekana katika mstari wa mbele kwa ajili ya kuhamasisha watu katika mapambano, na hawa mara nyingi wanakuwa na nafasi za uongozi zinazoheshimika. Lakini wapo wapambanaji wengine ambao hawajulikani sana na watu lakini Mungu anawafahamu na shetani pia anajua kazi yao. Hawa ni watu ambao ukiwaona kwa macho ya kawaida unaweza ukadhani kuwa si lolote lakini ni watu wanaoweza kuutetemeha ufalme wa shetani,nilimuona dada huyu kila kitu alichoamriwa kukifanya,iwe kufundisha wakristo wachanga,kuongoza maombi,kuongoza ibada n.k. alifanya kwa bidii kutoka ndani ya moyo wake kabisa,hakupenda kufanya mambo kinafiki ili kwamba watu wamuone. Bali alifanya kile alichoamini kwamba kina manufaa kwa Bwana Mungu wetu. Alikuwa ni mtu anayejituma katika mambo ya Mungu na kuna ushahidi wa kutosha kwamba hata mauti yanamkuta alikuwa amemaliza maombi siku chache kabla ya kifo chake. Pamoja na kwamba sikuwa karibu naye sana ,lakini nakumbuka maongezi yetu ya mwisho mwezi mmoja kabla ya msiba. Kuna tukio nilikuwa nimelifanya mimi katika ibada ya jioni ambalo yeye
Marehemu Austeria Deo akiwa na washirika wengine wakifuatilia mahubiri kwa makini.

 halikumpendeza, nilikuwa nimetoka na mtu mmoja nje kwa mazungumzo ya dharura wakati ibada ya maombi inaendelea. Yeye binafsi hakutukasirikia ila alihisi kwamba kuna watu tumewakwaza kwa kitendo chetu. Mimi nilijitetea na kumwambia kwamba wokovu sio ndani ya ibada peke yake ndio uwe na nidhamu kama watu wa dini nyingine wanavyonyenyekea. Nilimwambia wokovu ni kumcha Mungu, na kumcha Mungu ni mfumo wa maisha ambayo huyo Mungu unayemcha anakutaka uishi,haijalishi uko nyumbani,kanisani, kazini,n.k. na kwa pamoja tulikataa dhana ya watu wengine wanaotaka kuonyesha unyenyekevu kanisani tu na nje ya hapo hawako hivyo. Dada yetu ametutoka ghafla sana,hakuna aliyejua na ninaamini manabii walioko kanisani wangejua
Suzi mtoto mkubwa wa marehemu na mshirika wangu wa kanisa la vijana la KLPT majani mapana napenda kumkumbusha tena maneno tuliyoongea siku ya msiba. nilimwambia maisha ni kama ndoto ambayo mtu anaiota usiku halafu akiamka asubuhi anakuta hakuna kitu. kwa tukio lililompata anatakiwa ajione kama alikuwa kwenye ndoto akiwa na mama mmoja mzuri sana,anampenda na kumwelekeza anataka awe na maisha gani siku zake za usoni,mama sasa hayupo lakini maisha bado yanaendelea. kwa hiyo ni muhimu kwake kukumbuka yale mazuri yote ambayo mama alikuwa anataka ayafuate.

 jambo hili mapema pengine wangemsihi sana Mungu ahairishe au asogeze mbele msiba huu,na wangetoa sababu na Mungu angekubali. Lakini inaonekana Mungu mwenyewe alimuandaa kimya kimya hakuna aliyejua hata yeye mwenyewe hakujua. Ameamka vizuri asubuhi kawatayarisha watoto wake kwenda shule na wakati anapiga mswaki ili naye ajiandae kwenda katika shughuli zake,ndipo alianguka na kupoteza fahamu na ndio ukawa mwisho wa maisha yake,tumeumizwa sana na tukio hili,lakini Mungu anabaki kuwa Mungu na sisi ataendelea kuwa Baba na rafiki yetu. TUTAKUKUMBUKA DAIMA MILELE NDUGU YETU NA BWANA ATAKUFUFUA SIKU YA MWISHO TUTAFURAHI PAMOJA NA BWANA.