Ijumaa, 13 Mei 2016

NAMNA YA KUISIKIA SAUTI YA MUNGU YA NDANI KWA URAHISI ZAIDI SEHEMU YA PILI




Jambo likifika hatua hii ni vigumu kulizuwia kutendeka. Huwa vigumu sana kwa mtu aliyeokoka afike hatua ya kutenda dhambi, kwa sababu kuna hatua ndefu sana tangu ulipoingiwa na wazo chafu hadi ufikie hatua ya kutenda dhambi.
Hivyo unayo nafasi kupingana na hilo wazo chafu kabla halijaingia katika mlango fahamu wa mawazo, ikishindikana hapo bado kuna mlango wa fahamu wa maamuzi.
Pigana naye hapo hasa wakati unaposikia sauti mbili zinabishana kuwa fanya nyingine inasema usifanye, usingoje hadi jambo lifike kwenye hisia,hapo itakuwa kazi kubwa sana kuchomoa.
Biblia inasema;
maana ingawa tunaenenda katika mwili,hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili,maana silaha zetu si za mwili,bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome; tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka,kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii kristo.” (2Korintho 10: 3,5).
Iwapo mtu hajaokoka nafsi yake inatawaliwa na roho waovu hivyo wazo la kutoka kwa Mungu haliwezi kupita na kupata kibali. Mambo ambayo yatapata kibali ni yale ya shetani. Hivyo hivyo hata kwa mtu aliyeokoka,nafsi yake inatawaliwa na Mungu,hivyo wazo kutoka kwa shetani halitapata kibali.
Kwa kifupi kitu ambacho nilitaka ufahamu hapa ni kwamba mawao ndiyo masikio ya rohoni. Mungu au Shetani akiongea na wewe utasikia wazo. Wazo la Mungu au la shetani husikika kama mtu mwingine ambaye si wewe akikuongelesha, hili ndio ujue ni wazo kutoka kwa Mungu au kwa shetani. Wazo la shetani liko kinyume na Mungu, wazo kutoka kwa Mungu linakubaliana na neon la Mungu.
Iwapo wazo ni lako mwenyewe hutalisikia kama mtu wa pili akikuongelesha, bali nafsi yako itakuwa inajiongelesha yenyewe (nia). Hivyo, iwapo sauti ya shetani utaisikia kama mtu wa pili akikuongelesha katika mawazo yako. Pia iwapo ni sauti ya Mungu utasikia kama mtu wa pili akikuongelesha katika mawazo yako.
Mfano
1.  Unaweza kusikia sauti ikikushauri unaonaje kama ukiiba. (hii ni sauti ya shetani).
2.  Unaweza kusikia sauti ikikushauri usiibe (sauti ya Mungu)
3.  Ninatamani kuiba (Nia)
Hizi sauti ya kwanza na ya pili zote unazisikia kama mtu wa pili akikuongelesha. Lakini sauti ya tatu wewe mwenyewe ukijiongelesha,yaani unasikia unajiongelesha wewe mwenyewe.
Sauti ya Mungu au yako mwenyewe inasikika kwenye mawazo. Pepo anakuja kwa njia yeyote ile lakini kituo cha kwanza kabisa ni kwenye mawazo,baada ya hapo ni kwenye maamuzi na baadae hisia,tayari kwa utekelezaji.
Utendaji kazi wa milango ya fahamu ya Roho
Kama tulivyojifunza kwamba roho inayo milango mitatu ya fahamu,mawasiliano na Mungu,kujulishwa na dhamiri. Hebu tuangalie utendaji wa mlango mmojammoja.
Uhusiano kati ya mtu na Mungu unajengwa katika kuwasiliana naye. Mawasiliano ya kawaida katika maeneo yote ya kiroho yanapitia mlango huu wa fahamu wa mawasiliano.
Mfano
Unapohubiriwa na kufikia kulikubali neno la Mungu unapolielewa na kukubaliana nalo,huwa ni Mungu ndiye anayezungumza na wewe kupitia njia hii.
Unapotafakari neon la Mungu huwa ni mlango huu wa mawasiliano.
 hutumika.
Mahusiano ya kila siku ya kawaida kati ya mtu na Mungu, Mungu anapozungumza ujumbe maalumu kwa mtu,huzungumza kupitia mlango huu, kama vile ufunuo fulani, neno la maarifa, neno la hekima,kupambanua roho n.k.
Ni hali ya kutojisikia amani wakati ukiwa katika hali ambayo Mungu hataki  uwepo mahali hapo au hali ya kujisikia amani iwapo utakuwa katika hali inayompendeza Mungu.
Mfano
Umepanda gari ukiwa kwenye gari hilo unakosa amani rohoni, hapo ina maana kuwa Mungu hataki upande gari hilo. Mungu amezungumza na wewe kwa njia ya dhamiri yako kukushuhudia kuwa uko mahali ambako Mungu hataki uwepo hivyo unatakiwa kushuka kwenye hilo gari. Tafuta gari linguine na usiulize kwa nini. Mungu ndio anajua ni kwa nini hakutaka upande hilo gari, na linaweza kwenda na kufika salama lakini pengine uwepo wako ndani ya hilo gari Mungu aliona mitego ya adui.
Roho ilitoka kwa Mungu, hivyo inazo tabia ya Mungu, Mungu anapokuja kwa mtu hufikia kwenye roho, hivyo roho daima inatawaliwa na Mungu Hivyo hata milango ya fahamu yote ya fahamu ya roho hutumiwa na Mungu peke yake. Hapa tunaona kwamba sauti ya Mungu hufika kwenye mawazo ikitokea rohoni na sauti ya shetani hufika kwenye mawazo ikitokea mwilini.
Mtu ambaye hajaokoka roho yake imekufa, hivyo milango ya fahamu ya roho haiwezi kufanya kazi kwa sababu roho yake imekufa. Hivyo mtu huyu hatakuwa na mawasiliano na Mungu. Hata kama sauti ya Mungu itazungumza naye kwenye mawazo yake,hiyo sauti ya Mungu haitakuwa na nguvu, wala haitapata kibali maana nafsi na milango yote ya fahamu ya nafsi itakuwa inatawaliwa na shetani
Hapo tulipofika sasa tunaweza kuielewa sauti ya Mungu bila matatizo. Sauti ya Mungu bila kujali ni mlango gani wa fahamu war oho uliotumika ndio inamwongoza mkristo katika kila kitu cha ki Mungu. Mungu huongoza na kusimamia kila kitu katika maeneo mbalimbali ya maisha ya maisha ya mkristo. Hivyo mkristo ambaye hataisikia sauti ya Mungu hawezi kufanikiwa kiroho na kimwili. Katika mambo yot tunayoyafanya Mungu anataka azungumze nasi na kutuongoza na kutuelekeza nini cha kufanya. Mambo kama kuomba, kuhubiri, utoaji, kutenda miujiza, kazi, biashara, kilimo, masomo,nk

MUNGU AKUBARIKI TUKUTANE KATIKA SEHEMU YA TATU
Mob: Furaha Amon 0713 461593.




NAMNA YA KUISIKIA SAUTI YA MUNGU YA NDANI KWA URAHISI ZAIDI

NAMNA YA KUISIKIA SAUTI YA MUNGU YA NDANI KWA URAHISI ZAIDI SEHEMU YA KWANZA



Utangulizi:
Kwa mtu mbaye haelewi mambo ya kiroho unaposema kwamba Mungu ameniambia jambo fulani huwa ni kama kituko kwake, hawezi kuamini na anaweza kukuona kama unafanya mzaha vile au unajifanya unajua sana. Lakini ukweli ni kwamba sauti ya Mungu iko kila sekunde unayoishi na ipo tayari kwa ajili ya kukuongoza kukushauri na kukuelekeza kitu ambacho Mungu anataka ukifanye kwa wakati huo.

Kwa nini tunajifunza somo:
Tunajifunza somo hili kwa sababu nyakati tulizonazo tunao walimu wengi na watumishi wengi wa ukweli na wa uongo na kufanya kuwe na sauti nyingi katika mafundisho ambapo kama watu hawajafundishwa sawasawa kuisikia sauti ya Mungu ni rahisi kuchukuliwa na upepo wa kila elimu. Lakini watakapojifunza sauti ya Mungu itawasaidia sana kuwa na msingi imara kiasi kwamba watajua kutofautisha sauti ya Mungu,shetani na yao wnyewe katika kumua mambo yanayohusu maisha yao ya kimwili na kiroho.
Niliwauliza wanafunzi wangu wa kanisa la vijana ni kwa nini wanapofanya makosa ya kiroho (dhambi) haraka sana wanaamini kwamba Mungu ameshaona na kusikia, na kwa nini wanapofanya maombi hawaamini kuwa Mungu amesikia. Sasa hili ni somo jingine lakini katika somo hili nataka kukupa njia nyepesi kabisa za kusikia sauti ya Mungu kwa mfano.


Kwa mfano:
 Mimi niko kurasini hapo Dar na ninataka kumtembelea rafiki yangu Elie chansa ambaye anaishi Mbagala na labda sina mawasiliano naye ya simu. Wakati nasubiri usafiri wa kwenda Mbagala linakuja wazo ndani yangu kwamba nenda kwanza kariakoo ambako hukupanga kwenda na mimi naamua kutii lile wazo na kupanda gari la kariakoo ambako labda sikuwa na umuhimu sana wa kwenda huko. Lakini ninaposhuka kwenye gari Kariakoo namuona Elie yuko pale kituoni anasubiri usafiri.
Hapo inakuwa lile wazo la kwenda kariakoo halikuwa wazo la kawaida bali ilikuwa ni sauti ya Mungu halisi na kwa sababu nilitii ndio maana sikulazimika kupoteza muda na nauli kwenda Mbagala.
Mtu ni nini
Ili tuanze vizuri kujenga msingi wa somo hili ni muhimu kwanza kujua mtu ni nini,kwa mujibu wa Biblia tunajifunza kwamba Mungu alisema na tumfanye Mtu kwa mfano wetu na sura yetu, (Mwanzo 1: 26a) kwa hiyo Mungu aliumba roho kwanza. Ni katika roho tu ndiko ambako wanadamu wote tunafanana na Mungu, kwa maana nyingine hatufanani na Mungu katika mwili ndio maana kuna sisi weusi kama mimi, kuna wahindi wekundu, wajapani na wakorea wanjano kuna wazungu weupe. Biblia inaeleza kuwa baadae Mungu akachukua mavumbi akaufanya mwili na kisha akapuliza pumzi yake na mwanadamu akawa nafsi hai. Kwa kifupi tunajifunza kwamba mtu ni roho, anayo nafsi na anaishi katika mwili.
Kwa hiyo nafsi na roho zimeunganishwa pamoja ambayo ndio wewe Tunajifunza kwamba baada ya mtu kufa mwili hurudia hali yake ya kuwa udongo, Nafsi na roho ndio mwanadamu mwenyewe atakayeishi milele, aidha mbinguni ama jehanamu kutegemeana na mwenyewe alivyoishi hapa duniani.
Kwa sababu hiyo ni muhimu kuifahamu milango ya fahamu ambayo iko kwenye mwili, nafsi na kwenye roho hiyo itatusaidia sana kuelewa sauti ya Mungu na umuhimu wake.

Milango ya fahamu ya mwili
Mwili unao milango mitano ya fahamu, ambayo ni;
1.  kuona,
2.  kugusa,
3.  kuonja,
4.  kusikia na
5.  kunusa.

Milango ya fahamu ya roho

Roho nayo inayo milango mitatu ya fahamu ambayo ni
1.  mawasiliano na Mungu,
2.  uwezo wa kujulishwa (ituition)
3.  na dhamiri (Consious).

Milango ya fahamu ya nafsi
Nafsi nayo inayo milango mitatu ya fahamu ambayo ni
1.  KUAMUA (willing).
2.   KUJISIKIA au hisia (emotion) na
3.   MAWAZO.


Mapambano yasiyo na mwisho
Ili tuweze kuijua sauti ya Mungu ni lazima tufahamu kwanza kwamba yapo mpambano yasiyoisha tangu mwanadamu anapotungwa mimba mpaka siku anapolala mauti, ni muhimu kukumbuka kwamba uumbaji wa Mungu bado unaendelea hadi sasa kwa maana ya kwamba mbegu ya baba inapokutana na yai la mama Mungu hutia pumzi yake na hapo ndio  mwanzo wa binadamu kuja duniani ambako anakuta tayari kuna mitego ambayo imetokana na maagano ya kimila na laana za kifamilia kutoka kwenye koo na mababu, lakini pia anakuwa anawindwa na roho ya kukataliwa kutokana na jinsi wazazi wake walivyokuwa wamejiandaa kumpokea pamoja na madhira mengine mbalimbali. Kwa sababu hiyo ni lazima tuangalie mbinu ambazo shetani anatumia katika kumshambulia binadamu tukianzia na jinsi anavyoitumia milango ya fahamu ya kwenye mwili nafsi na roho.

Mawazo ni nini?
Kwa sababu nia ya somo hili ni kutaka ufahamu kusikia sauti ya Mungu kwa urahisi zaidi, nimeshawishika kuanza na mmojawapo wa milango ya fahamu uliopo kwenye nafsi ambao unaitwa mawazo.
Mawazo ni njia mojawapo ya mawasiliano kati ya mtu na ulimwengu wa roho, na viumbe ambavyo viko katika ulimwengu wa roho, mawazo ndio chombo kikuu cha mawasiliano kati ya ulimwengu wa Roho na Mtu. Mungu na shetani wanaishi katika ulimwengu wa roho, njia ambayo huwasilian na watu ni kupitia katika mawazo.
Mungu anapokuja kwa mtu hukaa kwenye roho, lakini anapoongea na mtu,huongea kupitia mawazo. Shetani anapokuja ndani ya mtu hupitia kwenye mwili na kufika kwenye nafsi na anapoongea na mtu huongea kupitia mawazo. Mtu mwenyewe pia huwa na matakwa yake,hivyo naye anayo mawazo yake. Matakwa ya mtu huitwa nia.
Baada ya wazo kumfikia mtu hilo wazo likipata kibali kwake linahamia kwenye mlango fahamu wa maamuzi ili likaamriwe kufanyika au hapana. Wazo likifika kwenye mlango fahamu wa maamuzi hapo huamriwa litendeke au lisitendeke. Iwapo wazo likikubalika kutendeka linapelekwa kwenye mlango fahamu wa hisia.
Mlango wa hisia ndio mlango wa utekelezaji wa jambo. Hapo mwili huwa unaamriwa kutenda wazo ambalo limeruhusiwa kutendeka. Kama ni zinaa hapo mwili wote unawake tama ya kuitenda dhambi hiyo. Iwapo ni jambo la ki Mungu,basi mwili wote utakuwa na shauku au hamu ya kulitenda hilo jambo. Daudi mfalme anasema mwili wangu wakuonea shauku (Zaburi 63:1).Eee Mungu wangu,nitakutafuta mapema,Nafsi yangu inakuonea kiu, mwili wangu wakuonea shauku,katika nchi kame na uchovu,isiyo na maji.

MUNGU AKUBARIKI TUKUTANE KATIKA SEHEMU YA PILI
Mob: Furaha Amon 0713 461593.

Jumatano, 11 Mei 2016

SOMO: ALICHOKIUNGANISHA MUNGU (8)


Mwl Furaha Amon


Pingamizi
Watu mara nyingi wamesema hivi: “Kama watu wataambiwa ni halali kwao kuoa tena baada ya kuachana kwa sababu yoyote, itawatia moyo wao kuachana kwa sababu zisizo halali.” Yawezekana ikawa kweli kiasi fulani kwa watu wa dini ambao hawajitahidi kumpendeza Mungu. Lakini, kujaribu kuwazuia watu ambao hawajajitoa kwa Mungu kabisa wasitende dhambi ni swala gumu. Ila, watu waliojitoa kwa Mungu kabisa hawatafuti njia za kutenda dhambi. Wanajaribu kumpendeza Mungu.
Na watu aina hiyo kwa kawaida wana ndoa zenye nguvu. Tena, Mungu hakusumbuka sana kwamba watu katika agano la kale wataachana kwa sababu zisizo halali kwa sababu ya kuwapa sheria nyepesi ya kuoa au kuolewa tena, maana sheria aliyotoa kwa Israeli kuhusu jambo hilo ilikuwa nyepesi kabisa.
Je, tuepuke kuwaambia watu kwamba Mungu yuko tayari kuwasamehe dhambi yoyote, wasije wakatiwa moyo kutenda dhambi kwa sababu wanajua msamaha unapatikana? Kama ndivyo, itabidi tuache kuhubiri Injili. Kila kitu kinategemea hali ya moyo ya wanadamu. Wale wanaompenda Mungu wanataka kumtii. Ninajua vizuri sana kwamba msamaha wa dhambi unapatikana kwangu nikiomba, hata kama nitatenda dhambi ya aina gani. Lakini hali hiyo haijawahi kunisukuma kufanya dhambi hata kidogo, kwa sababu nampenda Mungu na nimeokoka na ninajua Mungu anataka nimtumikie kwa uaminifu. Nimebadilishwa kwa neema ya Mungu. Ninataka kumpendeza yeye.

Mungu anajua hakuna haja ya kuongeza tokeo lingine baya kwenye matokeo mabaya mengi yasiyoepukika ya talaka, kwa matumaini ya kuwahamasisha watu wakae katika ndoa. Kuwaambia watu wenye ndoa zenye shida kwamba wasiachane kwa sababu hawataruhusiwa kuoa au kuolewa tena hakutoi hamasa kwa watu kuendelea katika ndoa. Hata kama atakuamini, uwezekano wa kuishi peke yake ukilinganisha na maisha ya mateso ya ndoa daima utasikika kama paradiso kwa mtu mwenye ndoa mbaya.
Asemavyo Paulo Kuhusu Kuoa Tena
Kabla ya kupambana na tatizo la kulinganisha maneno ya Yesu na ya Musa kuhusu kuoa tena, tunahitaji kutambua kwamba yupo mwandishi mwingine mmoja wa Biblia anayekubaliana na Musa, naye ni Paulo Mtume. Paulo aliandika waziwazi kabisa kwamba kuoa au kuolewa tena kwa walioachika si dhambi, na kukubaliana na kinachosemwa na Agano la Kale.
Kwa habari za wanawali sina amri ya Bwana, lakini natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kwa rehema za Bwana kuwa mwaminifu. Basi naona hili kuwa jema kwa ajili ya shida iliyopo, kwamba ni vema mtu akae kama alivyo. Je, umefungwa kwa mke? Usitake kufunguliwa. Umefunguliwa? Usitafute mke. Lakini kama ukioa, huna hatia; wala mwanamwali akiolewa, hana hatia. Lakini watu kama hao watakuwa na dhiki katika mwili nami nataka kuwazuilia hayo (1Wakor. 7:25-28).
Bila shaka Paulo alikuwa anasema na watu walioachika katika fungu hili. Anawashauri walio na ndoa, wasio na ndoa na walioachika wabaki katika hali zao kwa sababu ya mateso ambayo Wakristo walikuwa wanapitia wakati huo. Ila, Paulo alisema wazi wazi kwamba watu walioachika na wanawali hawatatenda dhambi wakiingia katika ndoa.
Ona kwamba Paulo hafafanui uhalali wa kuoa au kuolewa tena kwa walioachika. Hakusema kwamba kuoa au kuolewa tena kunaruhusiwa kama walioachika hawana lawama yoyote katika talaka ya ndoa iliyopita. (Kwani, nani mwenye sifa za kutosha kuhukumu kitu kama hicho, zaidi ya Mungu?) Hakusema kwamba kuoa au kuolewa tena kunaruhusiwa tu kwa wale ambao waliachana kabla ya kuokoka. Hapana! Yeye alisema tu kwamba kuoa au kuolewa tena si dhambi, kwa walioachika.
Je, Paulo Alilegeza Masharti Kuhusu Talaka?
Je, ina maana Paulo alilegeza masharti kuhusu talaka kwa kuwa aliruhusu kanuni ya neema kwa habari ya kuoa na kuolewa tena? Hapana! Paulo alikuwa anapingana na talaka kwa ujumla. Katika mistari ya mwanzoni ya sura hiyo hiyo ya barua ya kwanza kwa Wakorintho, aliweka sheria kuhusu talaka ambayo inalingana na chuki ya Mungu kwa talaka.
Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi ila Bwana; mke asiachane na mumewe. Lakini ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe. Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye, asimwache. Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe. Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi, bali sasa ni watakatifu. Lakini, yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyu ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani. Kwa maana wajuaje wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje wewe mwanamume, kama utamwokoa mkeo? Lakini kama Bwana alivyomgawia kila mtu, kama Mungualivyomwita kila mtu, na aenende vivyo hivyo. Ndivyo ninavyoagiza katika makanisa yote (1Wakor. 7:10-17).
Angalia kwamba Paulo anasema na waamini kwanza, ambao wana ndoa na waamini wenzao. Hawapaswi kuachana, na Paulo anasema hayo si maagizo yake, bali ya Bwana. Bila shaka hayo yanakubaliana kabisa na kila kitu tulichotazama katika Biblia mpaka hapa.

Yanayofuata yanasisimua. Paulo alikuwa mkweli wa kutosha kutambua kwamba hata waamini wanaweza kuachana, japo kwa nadra. Hayo yakitokea, Paulo anasema kwamba yule aliyemwacha mwenzake akae bila ndoa au wapatane. (Japo ushauri wa Paulo unawalenga zaidi wake, kanuni hiyo bila shaka inawahusu hata waume.)
Hapa tena – alichoandika Paulo kisitushangaze. Anatangulia kuweka sheria ya Mungu kwanza kuhusu talaka, lakini ana akili ya kutosha kutambua kwamba kutii sheria ya Mungu si kitu kinachofanyika kila wakati. Hivyo, dhambi ya kuachana inapotokea kati ya waamini wawili, anatoa maagizo zaidi. Yule aliyemwacha mwenzake abaki bila kuoa au apatane na mwenzake. Hicho ndicho kinachofaa endapo waamini wawili wataachana. Muda wote watakaobaki hawana ndoa, kuna tumaini la wao kupatana, na hilo ndiyo bora. Kama mmoja wao akioa tena, hapo ndiyo mwisho wa matumaini na uwezekano wa kupatana. (Tena, kama wametenda dhambi isiyosameheka kwa kuachana, isingekuwepo sababu ya Paulo kuwaaambia wabaki bila ndoa au wapatane.)
Unaonaje? Paulo alikuwa na akili za kutosha kujua kwamba agizo lake la pili kwa waamini walioachana halitafuatwa? Bila shaka! Labda ndiyo sababu hakutoa ushauri zaidi kwa waamini walioachana kwa sababu alitazamia kwamba waamini wa kweli wangefuata agizo lake la kwanza la kutoachana, na kwamba katika mazingira adimu sana, agizo lake la pili lingehitajika. Kwa hakika, wafuasi wa kweli wa Kristo wangefanya kila kinachowezekana ili kuhifadhi ndoa yao, kama walikuwa na matatizo ya ndoa. Na kwa hakika, mwamini ambaye, baada ya juhudi zote za kuhifadhi ndoa angejisikia kwamba hana jinsi isipokuwa kuachana, kutokana na aibu yake binafsi na shauku ya kumheshimu Kristo asingefikiri kuwa na ndoa nyingine, na bado angetumainia mapatano. Inaonekana kwamba tatizo halisi katika kanisa la kisasa kuhusu talaka ni kwamba kuna waamini bandia wengi sana – watu ambao hawajawahi kumwamini Bwana Yesu kweli, na kujitoa kwake.

Ni dhahiri basi kutokana na yale Paulo anayoandika katika 1Wakorinto 7 kwamba, Mungu ana matazamio makubwa sana kwa waamini – watu waliojazwa na Roho Mtakatifu – kuliko aliyo nayo kwa wasioamini. Kama tulivyosoma, Paulo aliandika kwamba waamini wasiwaache hata wenzao wasioamini mradi wako tayari kuishi nao. Hapo tena, agizo hili halitushangazi kwa sababu linakubaliana kabisa na kila kitu tulichosoma katika Maandiko kuhusu jambo hilo hadi sasa. Mungu anapinga talaka. Lakini Paulo anaendelea kusema kwamba, kama yule asiyeamini anataka talaka, mwamini aruhusu hiyo. Paulo anajua kwamba asiyeamini hajajitolea kwa Mungu, na hivyo hamtazamii asiyeamini kutenda kama anayeamini. Nyongeza ndogo hapo: Asiyeamini anapokubali kuishi na aaminiye, ni ushuhuda mzuri kwamba, pengine asiyeamini ana mwelekeo wa kupokea Injili, au yule anayeamini amerudi nyuma au ni Mkristo bandia.

Sasa, nani atakayesema kwamba mwamini aliyeachwa na asiyeamini hayuko huru kuoa tena? Paulo hasemi hivyo kamwe, kama alivyosema kwa habari ya waamini wawili walioachana. Itabidi kushangaa ni kwa nini Mungu apinge mwamini aliyeachwa na asiyeamini kuoa au kuolewa tena. Hilo lingetimiza kusudi gani? Lakini, ruhusa hiyo inaonekana inapingana na maelezo ya Yesu kuhusu kuoa tena, kwamba, “Yeyote amwoaye mwanamke aliyeachwa, azini” (Mathayo 5:32 ). Hapo tena, kuna mashaka kwamba pengine tumefasiri vibaya yale ambayo Yesu anasema.





MAPAMBANO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO SEHEMU YA TATU Watu wasiomjua Mungu unajimu unaweza kuwasaidia kujua wakati unaofaa wa kushiriki katika utendaji fulani au kuanza kufanya mambo fulani. Inasemekana kwamba habari hizi zinaweza kujulikana kwa kutazama mpangilio wa nyota au sayari fulani na kuchunguza uhusiano kati ya nyota na sayari hizo, na pia uhusiano wake na dunia. Inasemekana kuwa uvutano wa nyota na sayari juu ya maisha ya mtu binafsi unategemea mpangilio wake wakati wa kuzaliwa kwa mtu huyo. Wanajimu wa kale walifikiri kuwa dunia ndiyo kitovu cha ulimwengu, na kwamba sayari na nyota zilikuwa zimefungiwa katika miviringo ya kimbingu ambayo iliizunguka dunia. Lakini pia walifikiri kwamba jua linasafiri angani likiwa kati ya makundi ya nyota likifuata njia fulani hususa katika mzunguko wa kila mwaka. Waliigawanya njia hii ya jua ya kila mwaka katika sehemu au maeneo 12. Sehemu hizo zote zilikuwa na makundi ya nyota, na kila sehemu ilipewa jina kulingana na kundi la nyota ambamo jua lilipitia. Sehemu hizo zikawa zile ishara 12 za nyota na kuitwa “nyumba za mbinguni,” kwa sababu zilionwa kuwa makao ya miungu ya kipagani. Hata hivyo, wanasayansi waligundua baadaye kuwa jua haliizunguki dunia bali dunia ndiyo inayozunguka jua. Uvumbuzi huo mpya ulithibitisha kuwa unajimu si sayansi yenye kutegemeka bali ni uchawi sawa na kupiga ramri. Bado hata sasa katika nchi nyingi duniani watu hawatoki majumbani kwao bila kujua nyota yake inasemaje kuhusu siku hiyo, kwa hiyo ni lazima wapate magazeti yenye kurasa maalumu za watabiri wa nyota. UNAJIMU HAUWEZI KUFUNUA SIRI ZA MUNGU Wakati wa utawala wa Mfalme Nebukadneza wa Babiloni, makuhani na wanajimu walishindwa kufasiri ndoto ya mfalme. Danieli, nabii wa Mungu wa kweli, alionyesha sababu zilizofanya washindwe kufasiri ndoto hiyo aliposema: “Siri ambayo mfalme anauliza, watu wenye hekima, wala wafanya-mazingaombwe, wala makuhani wenye kufanya uchawi wala wanajimu hawawezi kumwonyesha mfalme. Hata hivyo, kuna Mungu mbinguni ambaye Ni Mfunuaji WA siri, naye amemjulisha Mfalme Nebukadneza mambo yatakayotokea katika siku za mwisho.” (Danieli 2:27, 28) Danieli alimtumaini Mungu ambaye ni “Mfunuaji wa siri” bali si katika jua, mwezi, au nyota, na akamweleza mfalme maana ya kweli ya ndoto yake. Danieli 2:36-45. Kwa maana nyingine ni kwamba Mamlaka ya Mungu katika ulimwengu wa roho ilikwisha kaa kikao na kuamua juu ya hatma ya ufalme wa Nebukadneza, kwa hiyo Nebukadneza hata angejitahidi kupambana wakati anguko lake linatokea angekuwa anapigana katika damu na nyama. Hapo ndipo mtume Paulo anakataa kwamba hatutaki



na Mwl Furaha Amon

 

Watu wasiomjua Mungu unajimu unaweza kuwasaidia kujua wakati unaofaa wa kushiriki katika utendaji fulani au kuanza kufanya mambo fulani.

Inasemekana kwamba habari hizi zinaweza kujulikana kwa kutazama mpangilio wa nyota au sayari fulani na kuchunguza uhusiano kati ya nyota na sayari hizo, na pia uhusiano wake na dunia.

Inasemekana kuwa uvutano wa nyota na sayari juu ya maisha ya mtu binafsi unategemea mpangilio wake wakati wa kuzaliwa kwa mtu huyo.

Wanajimu wa kale walifikiri kuwa dunia ndiyo kitovu cha ulimwengu, na kwamba sayari na nyota zilikuwa zimefungiwa katika miviringo ya kimbingu ambayo iliizunguka dunia.

Lakini pia walifikiri kwamba jua linasafiri angani likiwa kati ya makundi ya nyota likifuata njia fulani hususa katika mzunguko wa kila mwaka.

Waliigawanya njia hii ya jua ya kila mwaka katika sehemu au maeneo 12. Sehemu hizo zote zilikuwa na makundi ya nyota, na kila sehemu ilipewa jina kulingana na kundi la nyota ambamo jua lilipitia.

Sehemu hizo zikawa zile ishara 12 za nyota na kuitwa “nyumba za mbinguni,” kwa sababu zilionwa kuwa makao ya miungu ya kipagani. Hata hivyo, wanasayansi waligundua baadaye kuwa jua haliizunguki dunia bali dunia ndiyo inayozunguka jua.

Uvumbuzi huo mpya ulithibitisha kuwa unajimu si sayansi yenye kutegemeka bali ni uchawi sawa na kupiga ramri.

Bado hata sasa  katika nchi nyingi duniani watu hawatoki majumbani kwao bila kujua nyota yake inasemaje kuhusu siku hiyo, kwa hiyo ni lazima wapate magazeti yenye kurasa maalumu za watabiri wa nyota.

UNAJIMU HAUWEZI KUFUNUA SIRI ZA MUNGU

Wakati wa utawala wa Mfalme Nebukadneza wa Babiloni, makuhani na wanajimu walishindwa kufasiri ndoto ya mfalme. Danieli, nabii wa Mungu wa kweli, alionyesha sababu zilizofanya washindwe kufasiri ndoto hiyo aliposema:

“Siri ambayo mfalme anauliza, watu wenye hekima, wala wafanya-mazingaombwe, wala makuhani wenye kufanya uchawi wala wanajimu hawawezi kumwonyesha mfalme. Hata hivyo, kuna Mungu mbinguni ambaye Ni Mfunuaji WA siri, naye amemjulisha Mfalme Nebukadneza mambo yatakayotokea katika siku za mwisho.” (Danieli 2:27, 28)

Danieli alimtumaini Mungu ambaye ni “Mfunuaji wa siri” bali si katika jua, mwezi, au nyota, na akamweleza mfalme maana ya kweli ya ndoto yake.

Danieli 2:36-45. Kwa maana nyingine ni kwamba Mamlaka ya Mungu katika ulimwengu wa roho ilikwisha kaa kikao na  kuamua juu ya hatma ya ufalme wa Nebukadneza, kwa hiyo Nebukadneza hata angejitahidi kupambana wakati anguko lake linatokea angekuwa anapigana katika damu na nyama.

Hapo ndipo mtume Paulo anakataa kwamba hatutakiwi kupigana katika damu na nyama, kwa kufanya hivyo ni sawa na kutapatapa kwa sababu, watu wameshamaliza katika ulimwengu wa roho.

Baada ya kujua machache kuhusu ulimwengu wa roho naamini utakuwa umepata ufahamu kidogo utakaokusaidia kwenda sambamba na somo hili. Mtume Paulo bado anaendelea na kutuingiza katika chumba cha silaha na kutushauri katika mstari wa kwamba;

SOMO LITAENDELEA

Tunaweza kuwasiliana

Furaha Amon Mob: 0713 461593