Jambo likifika hatua hii ni vigumu kulizuwia kutendeka. Huwa vigumu
sana kwa mtu aliyeokoka afike hatua ya kutenda dhambi, kwa sababu kuna hatua
ndefu sana tangu ulipoingiwa na wazo chafu hadi ufikie hatua ya kutenda dhambi.
Hivyo unayo nafasi kupingana na hilo wazo
chafu kabla halijaingia katika mlango fahamu wa mawazo, ikishindikana hapo bado
kuna mlango wa fahamu wa maamuzi.
Pigana naye hapo hasa wakati unaposikia sauti mbili zinabishana
kuwa fanya nyingine inasema usifanye, usingoje hadi jambo lifike kwenye
hisia,hapo itakuwa kazi kubwa sana kuchomoa.
Biblia inasema;
“maana ingawa tunaenenda katika mwili,hatufanyi vita kwa jinsi ya
mwili,maana silaha zetu si za mwili,bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha
ngome; tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka,kijiinuacho juu ya elimu ya
Mungu; na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii kristo.” (2Korintho
10: 3,5).
Iwapo mtu hajaokoka nafsi yake inatawaliwa na roho waovu hivyo wazo
la kutoka kwa Mungu haliwezi kupita na kupata kibali. Mambo ambayo yatapata
kibali ni yale ya shetani. Hivyo hivyo hata kwa mtu aliyeokoka,nafsi yake
inatawaliwa na Mungu,hivyo wazo kutoka kwa shetani halitapata kibali.
Kwa kifupi kitu ambacho nilitaka ufahamu
hapa ni kwamba mawao ndiyo masikio ya rohoni. Mungu au Shetani akiongea na wewe
utasikia wazo. Wazo la Mungu au la shetani husikika kama mtu mwingine ambaye si
wewe akikuongelesha, hili ndio ujue ni wazo kutoka kwa Mungu au kwa shetani.
Wazo la shetani liko kinyume na Mungu, wazo kutoka kwa Mungu linakubaliana na
neon la Mungu.
Iwapo
wazo ni lako mwenyewe hutalisikia kama mtu wa pili akikuongelesha, bali nafsi
yako itakuwa inajiongelesha yenyewe (nia). Hivyo, iwapo sauti ya shetani
utaisikia kama mtu wa pili akikuongelesha katika mawazo yako. Pia iwapo ni
sauti ya Mungu utasikia kama mtu wa pili akikuongelesha katika mawazo yako.
Mfano
1. Unaweza
kusikia sauti ikikushauri unaonaje kama ukiiba. (hii ni sauti ya shetani).
2. Unaweza
kusikia sauti ikikushauri usiibe (sauti ya Mungu)
3. Ninatamani
kuiba (Nia)
Hizi sauti ya kwanza na ya pili zote
unazisikia kama mtu wa pili akikuongelesha. Lakini sauti ya tatu wewe mwenyewe
ukijiongelesha,yaani unasikia unajiongelesha wewe mwenyewe.
Sauti ya Mungu au yako mwenyewe inasikika kwenye mawazo. Pepo
anakuja kwa njia yeyote ile lakini kituo cha kwanza kabisa ni kwenye
mawazo,baada ya hapo ni kwenye maamuzi na baadae hisia,tayari kwa utekelezaji.
Kama tulivyojifunza kwamba roho inayo
milango mitatu ya fahamu,mawasiliano na Mungu,kujulishwa na dhamiri. Hebu
tuangalie utendaji wa mlango mmojammoja.
Uhusiano
kati ya mtu na Mungu unajengwa katika kuwasiliana naye. Mawasiliano ya kawaida
katika maeneo yote ya kiroho yanapitia mlango huu wa fahamu wa mawasiliano.
Mfano
Unapohubiriwa na kufikia kulikubali neno la
Mungu unapolielewa na kukubaliana nalo,huwa ni Mungu ndiye anayezungumza na
wewe kupitia njia hii.
Unapotafakari neon la Mungu huwa ni mlango
huu wa mawasiliano.
hutumika.
Mahusiano
ya kila siku ya kawaida kati ya mtu na Mungu, Mungu anapozungumza ujumbe
maalumu kwa mtu,huzungumza kupitia mlango huu, kama vile ufunuo fulani, neno la
maarifa, neno la hekima,kupambanua roho n.k.
Ni hali ya kutojisikia amani wakati ukiwa katika hali ambayo Mungu
hataki uwepo mahali hapo au hali ya
kujisikia amani iwapo utakuwa katika hali inayompendeza Mungu.
Mfano
Umepanda gari ukiwa kwenye gari hilo unakosa
amani rohoni, hapo ina maana kuwa Mungu hataki upande gari hilo. Mungu
amezungumza na wewe kwa njia ya dhamiri yako kukushuhudia kuwa uko mahali
ambako Mungu hataki uwepo hivyo unatakiwa kushuka kwenye hilo gari. Tafuta gari
linguine na usiulize kwa nini. Mungu ndio anajua ni kwa nini hakutaka upande
hilo gari, na linaweza kwenda na kufika salama lakini pengine uwepo wako ndani
ya hilo gari Mungu aliona mitego ya adui.
Roho ilitoka kwa Mungu, hivyo inazo tabia ya Mungu, Mungu anapokuja
kwa mtu hufikia kwenye roho, hivyo roho daima inatawaliwa na Mungu Hivyo hata
milango ya fahamu yote ya fahamu ya roho hutumiwa na Mungu peke yake. Hapa
tunaona kwamba sauti ya Mungu hufika kwenye mawazo ikitokea rohoni na sauti ya
shetani hufika kwenye mawazo ikitokea mwilini.
Mtu
ambaye hajaokoka roho yake imekufa, hivyo milango ya fahamu ya roho haiwezi
kufanya kazi kwa sababu roho yake imekufa. Hivyo mtu huyu hatakuwa na
mawasiliano na Mungu. Hata kama sauti ya Mungu itazungumza naye kwenye mawazo
yake,hiyo sauti ya Mungu haitakuwa na nguvu, wala haitapata kibali maana nafsi
na milango yote ya fahamu ya nafsi itakuwa inatawaliwa na shetani
Hapo tulipofika sasa tunaweza kuielewa
sauti ya Mungu bila matatizo. Sauti ya Mungu bila kujali ni mlango gani wa
fahamu war oho uliotumika ndio inamwongoza mkristo katika kila kitu cha ki
Mungu. Mungu huongoza na kusimamia kila kitu katika maeneo mbalimbali ya maisha
ya maisha ya mkristo. Hivyo mkristo ambaye hataisikia sauti ya Mungu hawezi kufanikiwa kiroho na kimwili.
Katika mambo yot tunayoyafanya Mungu anataka azungumze nasi na kutuongoza na
kutuelekeza nini cha kufanya. Mambo kama kuomba, kuhubiri, utoaji, kutenda
miujiza, kazi, biashara, kilimo, masomo,nk
MUNGU AKUBARIKI TUKUTANE KATIKA SEHEMU YA TATU
Mob:
Furaha Amon 0713 461593.
NAMNA
YA KUISIKIA SAUTI YA MUNGU YA NDANI KWA URAHISI ZAIDI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni