MAPAMBANO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO
SEHEMU YA KWANZA
Biblia inasema.
10 Hatimaye,
mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
11 Vaeni
silaha zote za Mungu,mpate kuweza kuzipinga hila za shetani
12 kwa maana kushindana
kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka,juu ya
wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
13 kwa sababu
hiyo twaeni silaha zote za Mungu,mpate kuweza kushindana siku ya uovu,na
mkiisha kuyatimia yote kusimama.
14 Basi
simameni hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa darii ya haki kifuani,
15 nakufungiwa
miguu utayari wa injili ya amani.
16 Zaidi ya yote mkitwaa
ngao ya imani ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya Yule
mwovu
17 tena ipokeeni chepeo ya wokovu, na upanga wa r oho ambao ni neno la
Mungu
18 kwa sala zote na maombi
mkisali kila wakati katika roho.
ili tuweze kulewa vizuri na kwa
urahisi somo hili ni muhimu kuanza na mistari hii ya Biblia ili kujenga msingi
wa somo hili.
Tunasoma hapa mtume Paulo anawaelezea Waefeso
mistari michache lakini muhimu sana juu ya aina ya vita tunayopigana, na namna
ambavyo tunatakiwa kupigana.
Kwa kawaida
vita huwa inapiganwa kwa mbinu na mipango, maana kama umewahi kusikia watu
wakisema kwamba vita si lelemama kwa hiyo ili tuweze kushinda vita ya aina
yeyote ile tunahitaji kujifunza mbinu za kivita.
Maisha ya wokovu sio maisha
mepesi kama tunavyoaminishwa na baadhi ya wainjilisti kwamba kwa Yesu ni
tambarare, hakuna milima wala mabonde!. Hiyo sio kweli, ukishaambiwa kuna vita
na unatakiwa kupigana basi ni lazima ujue kwamba wewe sio raia tena bali ni askari.
Na kwa
kawaida askari ni raia aliyepewa mafunzo maalumu ya kupigana vita, kwa kutumia
zana mbalimbali za kivita. Ndio maana inakuwa muhimu sana kujifunza aina ya
vita na mbinu ambazo zitatusaidia kupata ushindi.
katika mstari wa 12 Mtume Paulo analiambia
kanisa;-
” 12 kwa maana kushindana kwetu
sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa
giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”
Katika mstari huu Biblia
inatujulisha wazi kuhusu aina ya vita tunayopigana, tunapigana na nani, lakini
pia ni katika mstari huu anatufahamisha kuhusu aina mbili za ulimwengu, kwamba
kumbe kuna ulimwengu wa damu na nyama ambao ndio dunia hii ambayo sisi
tunayoishi, Lakini pia kuna ulimwengu wa roho ambao sisi kwa macho na kwa akili
za kawaida hatuwezi kuuona wala viumbe vinavyokaa katika ulimwengu huo hatuwezi
kuviona katika macho ya kawaida.
Ulimwengu huo ndio ambao nataka tuuangalie
kwa undani zaidi kwani katika sehemu ya pili ya somo hili, kwani inawezekana
tukawa tunajua mambo machache sana kuhusu ulimwengu huo wa roho.
SOMO LITAENDELEA
Tunaweza kuwasiliana
Furaha
Amon Mob: 0713 461593
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni