na Mwl Furaha Amon
JUKWAA LA KIKRISTO NA KIJAMII AMBALO LINATOA FURSA KWA JAMII KUJADILI NA KUELIMISHANA JUU YA MAADILI NA MAISHA KWA UJUMLA
Jumatano, 11 Mei 2016
MAPAMBANO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO SEHEMU YA TATU Watu wasiomjua Mungu unajimu unaweza kuwasaidia kujua wakati unaofaa wa kushiriki katika utendaji fulani au kuanza kufanya mambo fulani. Inasemekana kwamba habari hizi zinaweza kujulikana kwa kutazama mpangilio wa nyota au sayari fulani na kuchunguza uhusiano kati ya nyota na sayari hizo, na pia uhusiano wake na dunia. Inasemekana kuwa uvutano wa nyota na sayari juu ya maisha ya mtu binafsi unategemea mpangilio wake wakati wa kuzaliwa kwa mtu huyo. Wanajimu wa kale walifikiri kuwa dunia ndiyo kitovu cha ulimwengu, na kwamba sayari na nyota zilikuwa zimefungiwa katika miviringo ya kimbingu ambayo iliizunguka dunia. Lakini pia walifikiri kwamba jua linasafiri angani likiwa kati ya makundi ya nyota likifuata njia fulani hususa katika mzunguko wa kila mwaka. Waliigawanya njia hii ya jua ya kila mwaka katika sehemu au maeneo 12. Sehemu hizo zote zilikuwa na makundi ya nyota, na kila sehemu ilipewa jina kulingana na kundi la nyota ambamo jua lilipitia. Sehemu hizo zikawa zile ishara 12 za nyota na kuitwa “nyumba za mbinguni,” kwa sababu zilionwa kuwa makao ya miungu ya kipagani. Hata hivyo, wanasayansi waligundua baadaye kuwa jua haliizunguki dunia bali dunia ndiyo inayozunguka jua. Uvumbuzi huo mpya ulithibitisha kuwa unajimu si sayansi yenye kutegemeka bali ni uchawi sawa na kupiga ramri. Bado hata sasa katika nchi nyingi duniani watu hawatoki majumbani kwao bila kujua nyota yake inasemaje kuhusu siku hiyo, kwa hiyo ni lazima wapate magazeti yenye kurasa maalumu za watabiri wa nyota. UNAJIMU HAUWEZI KUFUNUA SIRI ZA MUNGU Wakati wa utawala wa Mfalme Nebukadneza wa Babiloni, makuhani na wanajimu walishindwa kufasiri ndoto ya mfalme. Danieli, nabii wa Mungu wa kweli, alionyesha sababu zilizofanya washindwe kufasiri ndoto hiyo aliposema: “Siri ambayo mfalme anauliza, watu wenye hekima, wala wafanya-mazingaombwe, wala makuhani wenye kufanya uchawi wala wanajimu hawawezi kumwonyesha mfalme. Hata hivyo, kuna Mungu mbinguni ambaye Ni Mfunuaji WA siri, naye amemjulisha Mfalme Nebukadneza mambo yatakayotokea katika siku za mwisho.” (Danieli 2:27, 28) Danieli alimtumaini Mungu ambaye ni “Mfunuaji wa siri” bali si katika jua, mwezi, au nyota, na akamweleza mfalme maana ya kweli ya ndoto yake. Danieli 2:36-45. Kwa maana nyingine ni kwamba Mamlaka ya Mungu katika ulimwengu wa roho ilikwisha kaa kikao na kuamua juu ya hatma ya ufalme wa Nebukadneza, kwa hiyo Nebukadneza hata angejitahidi kupambana wakati anguko lake linatokea angekuwa anapigana katika damu na nyama. Hapo ndipo mtume Paulo anakataa kwamba hatutaki
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni