Utangulizi:
Kwa mtu mbaye haelewi mambo
ya kiroho unaposema kwamba Mungu ameniambia jambo fulani huwa ni kama kituko
kwake, hawezi kuamini na anaweza kukuona kama unafanya mzaha vile au unajifanya
unajua sana. Lakini ukweli ni kwamba sauti ya Mungu iko kila sekunde unayoishi
na ipo tayari kwa ajili ya kukuongoza kukushauri na kukuelekeza kitu ambacho
Mungu anataka ukifanye kwa wakati huo.
Kwa
nini tunajifunza somo:
Tunajifunza somo hili kwa
sababu nyakati tulizonazo tunao walimu wengi na watumishi wengi wa ukweli na wa
uongo na kufanya kuwe na sauti nyingi katika mafundisho ambapo kama watu
hawajafundishwa sawasawa kuisikia sauti ya Mungu ni rahisi kuchukuliwa na upepo
wa kila elimu. Lakini watakapojifunza sauti ya Mungu itawasaidia sana kuwa na
msingi imara kiasi kwamba watajua kutofautisha sauti ya Mungu,shetani na yao
wnyewe katika kumua mambo yanayohusu maisha yao ya kimwili na kiroho.
Niliwauliza wanafunzi wangu
wa kanisa la vijana ni kwa nini wanapofanya makosa ya kiroho (dhambi) haraka
sana wanaamini kwamba Mungu ameshaona na kusikia, na kwa nini wanapofanya
maombi hawaamini kuwa Mungu amesikia. Sasa hili ni somo jingine lakini katika
somo hili nataka kukupa njia nyepesi kabisa za kusikia sauti ya Mungu kwa
mfano.
Kwa
mfano:
Mimi niko kurasini hapo Dar na ninataka
kumtembelea rafiki yangu Elie chansa ambaye anaishi Mbagala na labda sina mawasiliano
naye ya simu. Wakati nasubiri usafiri wa kwenda Mbagala linakuja wazo ndani
yangu kwamba nenda kwanza kariakoo ambako hukupanga kwenda na mimi naamua kutii
lile wazo na kupanda gari la kariakoo ambako labda sikuwa na umuhimu sana wa
kwenda huko. Lakini ninaposhuka kwenye gari Kariakoo namuona Elie yuko pale
kituoni anasubiri usafiri.
Hapo inakuwa lile wazo la
kwenda kariakoo halikuwa wazo la kawaida bali ilikuwa ni sauti ya Mungu halisi
na kwa sababu nilitii ndio maana sikulazimika kupoteza muda na nauli kwenda
Mbagala.
Mtu
ni nini
Ili tuanze vizuri kujenga
msingi wa somo hili ni muhimu kwanza kujua mtu ni nini,kwa mujibu wa Biblia
tunajifunza kwamba Mungu alisema na tumfanye Mtu kwa mfano wetu na sura yetu,
(Mwanzo 1: 26a) kwa hiyo Mungu aliumba roho kwanza. Ni katika roho tu ndiko
ambako wanadamu wote tunafanana na Mungu, kwa maana nyingine hatufanani na
Mungu katika mwili ndio maana kuna sisi weusi kama mimi, kuna wahindi wekundu,
wajapani na wakorea wanjano kuna wazungu weupe. Biblia inaeleza kuwa baadae
Mungu akachukua mavumbi akaufanya mwili na kisha akapuliza pumzi yake na
mwanadamu akawa nafsi hai. Kwa kifupi tunajifunza kwamba mtu ni roho, anayo
nafsi na anaishi katika mwili.
Kwa hiyo nafsi na roho
zimeunganishwa pamoja ambayo ndio wewe Tunajifunza kwamba baada ya mtu kufa
mwili hurudia hali yake ya kuwa udongo, Nafsi na roho ndio mwanadamu mwenyewe
atakayeishi milele, aidha mbinguni ama jehanamu kutegemeana na mwenyewe
alivyoishi hapa duniani.
Kwa sababu hiyo ni muhimu
kuifahamu milango ya fahamu ambayo iko kwenye mwili, nafsi na kwenye roho hiyo
itatusaidia sana kuelewa sauti ya Mungu na umuhimu wake.
Milango ya fahamu ya
mwili
Mwili
unao milango mitano ya fahamu, ambayo ni;
1. kuona,
2.
kugusa,
3.
kuonja,
4.
kusikia
na
5.
kunusa.
Milango
ya fahamu ya roho
Roho nayo inayo milango
mitatu ya fahamu ambayo ni
1. mawasiliano
na Mungu,
2. uwezo
wa kujulishwa (ituition)
3. na dhamiri
(Consious).
Milango
ya fahamu ya nafsi
Nafsi
nayo inayo milango mitatu ya fahamu ambayo ni
1.
KUAMUA
(willing).
2.
KUJISIKIA au hisia (emotion) na
3.
MAWAZO.
Mapambano
yasiyo na mwisho
Ili tuweze kuijua sauti ya
Mungu ni lazima tufahamu kwanza kwamba yapo mpambano yasiyoisha tangu mwanadamu
anapotungwa mimba mpaka siku anapolala mauti, ni muhimu kukumbuka kwamba uumbaji
wa Mungu bado unaendelea hadi sasa kwa maana ya kwamba mbegu ya baba
inapokutana na yai la mama Mungu hutia pumzi yake na hapo ndio mwanzo wa binadamu kuja duniani ambako
anakuta tayari kuna mitego ambayo imetokana na maagano ya kimila na laana za
kifamilia kutoka kwenye koo na mababu, lakini pia anakuwa anawindwa na roho ya
kukataliwa kutokana na jinsi wazazi wake walivyokuwa wamejiandaa kumpokea
pamoja na madhira mengine mbalimbali. Kwa sababu hiyo ni lazima tuangalie mbinu
ambazo shetani anatumia katika kumshambulia binadamu tukianzia na jinsi
anavyoitumia milango ya fahamu ya kwenye mwili nafsi na roho.
Mawazo
ni nini?
Kwa sababu nia ya somo hili
ni kutaka ufahamu kusikia sauti ya Mungu kwa urahisi zaidi, nimeshawishika
kuanza na mmojawapo wa milango ya fahamu uliopo kwenye nafsi ambao unaitwa
mawazo.
Mawazo ni njia mojawapo ya
mawasiliano kati ya mtu na ulimwengu wa roho, na viumbe ambavyo viko katika
ulimwengu wa roho, mawazo ndio chombo kikuu cha mawasiliano kati ya ulimwengu
wa Roho na Mtu. Mungu na shetani wanaishi katika ulimwengu wa roho, njia ambayo
huwasilian na watu ni kupitia katika mawazo.
Mungu anapokuja kwa mtu
hukaa kwenye roho, lakini anapoongea na mtu,huongea kupitia mawazo. Shetani
anapokuja ndani ya mtu hupitia kwenye mwili na kufika kwenye nafsi na
anapoongea na mtu huongea kupitia mawazo. Mtu mwenyewe pia huwa na matakwa
yake,hivyo naye anayo mawazo yake. Matakwa ya mtu huitwa nia.
Baada ya wazo kumfikia mtu
hilo wazo likipata kibali kwake linahamia kwenye mlango fahamu wa maamuzi ili
likaamriwe kufanyika au hapana. Wazo likifika kwenye mlango fahamu wa maamuzi
hapo huamriwa litendeke au lisitendeke. Iwapo wazo likikubalika kutendeka
linapelekwa kwenye mlango fahamu wa hisia.
Mlango wa hisia ndio mlango
wa utekelezaji wa jambo. Hapo mwili huwa unaamriwa kutenda wazo ambalo
limeruhusiwa kutendeka. Kama ni zinaa hapo mwili wote unawake tama ya kuitenda
dhambi hiyo. Iwapo ni jambo la ki Mungu,basi mwili wote utakuwa na shauku au
hamu ya kulitenda hilo jambo. Daudi mfalme anasema mwili wangu wakuonea shauku
(Zaburi 63:1).Eee Mungu
wangu,nitakutafuta mapema,Nafsi yangu inakuonea kiu, mwili wangu wakuonea
shauku,katika nchi kame na uchovu,isiyo na maji.
MUNGU
AKUBARIKI TUKUTANE KATIKA SEHEMU YA PILI
Mob:
Furaha Amon 0713 461593.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni