- Huleta hofu ya
Mungu katikati ya watakatifu.
- Huyeyusha mioyo
migumu katika kupokea mambo ya Mungu.
- Hulipua vizuizi
vya kuikulia neema ya Mungu
- Nguvu ya Mungu
huonekana.
- Utendaji wa Roho
Mtakatifu hujidhihirisha kwa karama kuchanua.
- Moto wa uamsho
hutembea na maelfu ya watu kuokoka.
Matokeo ya kusifu
na kuabudu kwa kanisa
(Yohana 4:1-23)
- Mungu hupewa sifa
na utukufu
- Ni ibada ya moyo
kwa moyo na Mungu (Yohana 4:24)
- Roho ya mtu au
yule mtu wa ndani ndiye awezaye kuabudu.
- Mungu ni Roho anawatafuta
watu kama hao wamwabudu.
- Watu hawa ni
wachache sana na adimu miongoni mwa wengi waziendeao nyumba za siku za
jumapili. Ndio maana Mungu anafanya kuwatafuta.
- Mungu wetu anayo
namna ya kuabudiwa kutoka katika roho ya mtu wa ndani, ni mtu wa ndani pekee
ndiye awezaye kumuabudu Mungu ipasavyo.
- Yeye ndiye mwenye
mahusiano na ushirika hai na Mungu.
- Mtu asiyeokoka
hawezi kuabudu Mungu kihalisi (Mt 15: 8-9)
- Asiye okoka
hawezi kuufikia ujuzi wa kweli katika kuabudu.
- Mtu aliyeokoka
ndiye pekee awezaye kuabudu halisi kwa kuwa mwelekeo wa kuabudu ni kutoka kwa
mwamini kwenda kwa Mungu
- Toka kwa mtu wa
ndani hadi mawazo kisha maneno.
- Maneno ni mawazo
yaliyovishwa sauti hatimaye kuingia kwenye vitendo (udhihirisho wa mwitikio wa
moyo)
- Twamsifu na
kumuabudu Mungu tukijieleza kwake.
- Upendo wetu,utii
wetu,kujitoa kwetu kwake twasema kuwa
§ Mungu ni nani
§ Amesema nini
§ Anafanya nini na
alifanya nini
- Asiyeamini mtu wa
litulgia hawezi kufanya yote haya yeye binafsi toka katika vilindi vya moyo
wake.
- Mungu hana
ushirika na kiumbe katika kuabudiwa.
- Katika maandiko
(Mt 4: 9-10) majibu ya Bwana Yesu kwa shetani yanaonyesha kuwa Mungu hana
mshirika katika kupokea ibada na kiumbe yeyote duniani, mbinguni au kuzimu
(kutoka 34:14) Mungu anasema kuwa yeye ni Mungu mwenye wivu.
Wafilisti katika kitabu cha
(1Samweli 5:1-5) waliliteka sanduku la Mungu na kulitia katika nyumba ya dagoni
mungu wao. Wakaliweka sanduku la Mungu karibu na dagoni mungu wao,
- hii ilikuwa ni sawa na
kumlinganisha Mungu YEHOVA na dagoni.
- Kwa waisraeli lilipokuwa
sanduku la Mungu ilikuwa ni ishara kuwa YEHOVA yuko mahali hapo.
- Wafilisti walipoamka
asubuhi siku ya pili, kumbe sanamu lao dagoni limeanguka kifudifudi mbele ya
Mungu wa Israeli.
- Huku kichwa cha dagoni na
vitanga vya mikononi vimekatika vipo vimelala kizingitini dagoni imebaki
kiwiliwili.
YEHOVA Mungu wetu ni Mungu
mwenye wivu, na hatalinganishwa na chochote, maana yeye ndiye muumbaji.
- Iwe binadamu, malaika au
shetani na mapepo yake ambao awali walikuwa ni sehemu ya malaika wa Mungu kisha
wakaasi, hapo ndipo walipopoteza nafasi zao katika ufalme wa Mungu mbinguni.
- Kumbuka kwamba tumeumbwa
ili tumuabudu Mungu. Hii ndio moja ya sababu kubwa ya kuumbwa kwa jinsi
tulivyo. (Zab 103:1).
Kama vile wanadamu waundapo
magari na mitambo mbalimbali, wanaunda wakilenga kutosheleza uwezo wa kutendea
kazi iliyokusudiwa.
- Hali kadhalika ndivyo
ilivyo hata tunapoamua kujenga nyumba, barabara, n.k.
- vivyo hivyo kwa wanadamu
kila kiungo chetu kimekuwepo pia kutuwezesha kufikia makusudi ya Mungu ya
kumwabudu tuwapo katika dunia tuliyoumbiwa. (Tazama Isaya 45:12).
Viungo vyetu pia
hutuwezesha kuwa na mahusiano na dunia lakini tukishatoka duniani na kuvishwa
mwili mpya (1Wakorinto 15:40) tujapokuwa katika mwili mpya lakini katika umbo
la kibinadamu tutakuwa na;-
- Miguu inayoweza kucheza kwa
urahisi
- Magoti yanayoweza kujikunja
tuabudupo
- Kiuno na mgongo uwezao
kuinama na kuinuka
- Mabega yawezayo kucheza
- Mikono iwezayo kupiga
makofi kunyanyuliwa juu
- Kichwa kiwezacho kucheza
- Kinywa chenye kutoa sauti
zenye tuni mbalimbali.
Hakuna kiumbe aliyeumbwa
huru kutenda vitendo vingi kama binadamu tazama (Zaburi 139:15).
Sifa
za Bwana ni bubujiko la moyo (Yoh 4:10)
- Bwana alimfananisha Roho
Mtakatifu na maji yabubujikayo, ampokeaye humuondolea kiu milele.
- Maji hayo hububujika kutoka
utu wa ndani wa mtu hadi kudhihirika katika utu wan je (utu wa asili)
- Hali ya ukame kiu
haitakuwapo tena, hutasifu na kuabudu kwa dakika 2 na kujisikia kuchoka.
- Hutakuwa na moyo unaokerwa
na bubujiko la Roho Mtakatifu.
- Hutazuwia kunena kwa lugha
(1Wakorinto 14:39)
Kuna watu wanaodhani kuwa
utaratibu wao wa ibada ni sahihi,
- Watu hao hupanga kusifu na
kuabudu kwa dakika zisizozidi 10.
- Lakini matengenezo na
mipango yao ya kanisa hupangwa husemwa kwa dakika zaidi ya 30.
- Poroja za kusalimiana na
kutambulishana huchukua zaidi ya saa.
- Hapo wakisahau makusudi ya
Mungu kwa wanadamu.
Napenda kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuandika kitabu
hiki kuhusu ibada.
Naamini kwamba bila ya himizo la Roho Mtakatifu ndani
yangu nisingeweza kukamilisha kazi hii.
Ni matumaini yangu kwamba kila atakayesoma atapata msaada
na kukua kiroho.
Wito wake kwa Kanisa la Kristo ni kuwataka waamini waijue
ibada ya Kiroho na ya Kweli yenye upako wa Roho Mtakatifu. Ambapo waabuduo
watamwabudu Mungu katika Roho na Kweli, na kurejesha maana ya sifa, ibada na
kuabudu kulikopotea hekaluni mwa Bwana. Ibada ya kweli italeta furaha ya Roho
Mtakatifu maishani mwa waamini na kurejesha tumaini la utukufu mioyoni mwao
maana tayari wameona uwepo wa Mungu katikati yao, kisha kujenga imani zao, na
shauku yao kwenda kuwa pamoja na Bwana Mbinguni.
IBADA NI NINI?
Ibada ni tendo la heshima ya hali ya juu linalofanywa na
mtu kwa kiumbe aliye mkuu katika mazingira yake yote, kiroho na kimwili na
kiumbe huyo akaaminiwa kuwa ni MWENYE ENZI asiyefananishwa na kiumbe kingine
mkamilifu katika matendo yake.
Kuabudu Mungu katika Roho na Kweli kunaweza kukafanywa
wakati wowote na mahali popote mradi lengo ni kumfanyia Mungu IBADA.
- Jambo la
muhimu ni yule tunayemwabudu kuliko mahali tunapofanyia ibada
- ingawa mahali tunafanyia ibada ni kitu chema ,lakini
pasipewe nafasi mioyoni mwetu na kuheshimiwa kama sehemu ya ibada.
- Pamoja na hoja hiyo mahali pa ibada pasipuzwe na
kudharauliwa maana pamewekwa wakfu kwa huduma ya Mungu pametakaswa.
- Mtu akionyesha dharau au kuto paheshimu anaweza kupata
madhara,
- hivyo ni muhimu kila mtu ajue jambo hili na kuenenda kwa
utaratibu na kwa heshima mahali hapo.
Kwa vile Ibada ni shughuli ambayo inashikamana sana na
mfumo wa maisha ya mwanadamu, na kwamba ibada hutofautiana sana katika maana na
mitazamo kulingana na imani ya mtu juu ya Mungu anayemwabudu, ni vema tukaelewa
kwa usahihi ibada ninini kwa mujibu wa Biblia ifundishavyo.
“Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa
huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya
kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msifuatishe namna ya dunia
hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya
Mungu yaliyo mema , ya kupendeza, na ukamilifu”. (Rumi 12:1-2)
Tendo la Ibada ni tendo la kujitoa kama dhabihu, lakini
ibada ya kweli lazima dhabihu hiyo iwe hai na takatifu, Mwili, Roho na ufahamu
viwe na lengo moja lakumfanyia Mungu Ibada takatifu basi, ambapo ibada nje ya
utakatifu si ibada inayompendeza.