Si kila Ibada inayofanywa na mwanadamu ni halali na
kukubalika na Mungu, hapana. Mungu ni Mungu wa utaratibu na mipango mikamilifu.
Mungu amesema wazi ni ibada ipi anaikubali na kuipokea
akaisikiliza. Lakini kwa kuwa ulimwengu ni mpana na wenye tofauti za watu walio
na itikadi tofauti na ibada za walimwengu pia ni tofauti.
- Mungu wa kweli ni mmoja na njia ni moja ya kumfikia
ambayo ni Yesu. Yohana 14:1-6, ITim 2:15.
- Ni katika Yesu ambaye ni mpatanishi wetu na Mungu na
ambaye ni kweli, njia na uzima tutasikilizwa na kukubaliwa,
Yesu anasema mtu yeyote hawezi kwenda kwa Mungu isipokuwa
kwa njia yake, hakuna njia ya mkato kwenda kwa Mungu, bali ni kwa njia ya Yesu
tu. Kwa hiyo ibada lazima iwe,
a. Ibada katika Roho na Kweli yenye kumtambua Yesu kuwa
kiini na mlengwa wa Ibada hiyo Mdo 4:11-12 Waef 2:4-8
b) Si ibada ya mdomoni wala makusanyiko ya kidini na taratibu za kibinadamu zilizobuniwa kwa umahiri na wala si mapokeo ya mila na desturi za watu. Mdo17:22-27
c) Ibada ambayo haimchanganyi Mungu aliyejifunua katika maandiko na miungu mingine, japokuwa miungu hiyo inaabudiwa na mamilioni ya watu pamoja na vitu vilivyotukuzwa kiasi cha kukubalika kuwa Mungu. Zab 115:4-8
Sanamu zao ni fedha na dhahabu, kazi ya mikono ya
wanadmu. Zina vinywa lakini havisemi, zina macho lakini haioni. Zina masikio
lakini hazisikii, zina pua lakini hazisikii harufu. Mikono lakini hazishiki,
miguu lakini haziendi, wala hazitoi sauti kwa koo zake. Wazifanyao watafanana nao,
kila mmoja anayezitumainia.
Sasa ili tujiridhishe na ibada ya kweli inayokubaliwa na
Mungu hebu tuangalie ibada ya mbinguni ilivyo, na jinsi viumbe wa mbinguni
wanavyomwabudu Mungu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni