Zab: 100:1-4, 95:1-7
Mungu yuko mahali palipotukuka sana na kuinuliwa:
Hili linanipa wazo kwamba kuabudu na kusifu ni stahili ya
MUNGU, Biblia inasema.
“Maana yeye aliye juu aliyetukuka akaaye
milele ambaye jina lake ni Mtakatifu – anasema hivi; Nakaa mimi mahali
palipoinuka palipo patakatifu tena pamoja na yeye aliye na Roho iliyotubu na
kunyenyekea na kuifufua mioyo yao waliotubu.” (Isaya 57:15-16).
Hii ndiyo sifa na ufunguo unaotakiwa na Mungu.
Tutamkaribiaje Mungu kama huyu aliyeinuliwa na kutukuka sana?
1. Jibu linapatikana katika maandiko haya Zab 95:1-5
“Njoo tumwimbie Bwana Tuje mbele zake
kwa shukrani Kwakuwa Bwana ni Mungu Mkuu na mfalme mkuu juu ya miungu yote”. Mikononi
mwake zimo bonde za dunia , mikono yake iliumba bahari na nchi kavu
Katika mstari wa 6 mwaliko unatolewa
kwenda kumwabudu, kumsujudia kwa kumpigia magoti (kupiga magoti ni tendo la
kumkiri na kumtambua kuwa ni Mungu) Bwana aliyetuumba- Mungu wetu ambapo sisi
tu malisho yake na kondoo wa mkono wake (yeye ni Mchungaji).
Mungu hukaa na mtu aliyetubu na kunyenyekea, kamwe hawezi kukaa na
mwenye dhambi ingawa anampenda. Ibada ya mtu huyu itakubaliwa na Mungu Zab 96:9
Huu ni wito mwingine:
Mwabuduni Bwana kwa uzuri, na hofu ya utisho ndani ya moyo wa utakatifu
– tetemekeni mbele zake nchi yote. Utakatifu na hofu ni funguo za mlango wa
sifa na ibada ya kweli. Njia kuu kwa mwanadamu kumfikia Mungu katika enzi yake
ni kumpa shukrani na sifa anazostahili – tukishajitakasa kwa Toba
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni