Ibada ni kumshangaa Mungu. Kwa ufahamu tulio nao na akili
ya kibinadamu tuliyo nayo hatuwezi kumwelewa Mungu kikamilifu tukamfahamu.
Isaya 55:8-9:,
“Maana mawazo yangu si mawazo yenu,
wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo
juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na
mawazo yangu kuliko mawazo yenu.”
- Mungu ni mkuu kuliko uwezo wa ufahamu wa mwanadamu
- na yuko juu sana kuliko mawazo ya mwanadamu.
- na yuko juu sana kuliko njia za mwanadamu
kwahiyo hatuwezi kumfahamu vyema. Hivyo basi siku zote
tutakapokusanyika pamoja au mtu akiwa peke yake kumwabudu na kukutana naye
atamshangaa (tutamshangaa).
- Hutaweza kukaa mbele za Mungu ukimwabudu katika Roho na
Kweli ikawa jambo la kawaida,
- maana Mungu huyo ni Mfalme Mkuu lazima utamshangaa Mfalme
huyo.
- Utukufu wake utakushangaza na kutamani kumwangalia.
Wafalme wa dunia japokuwa ni wanadamu, raia wao
hutetemeka na kuwaheshimu wanapojitokeza mbele na kila mtu hutamani kumwona na
kumshangaa, na kukusanyika mahali pamoja ili wamsikilize Mfalme wao. Mungu ni
Mfalme wa ajabu anayejihudhurisha kati ya watu wake wanapomfanyia ibada kwa
kumwabudu na kuwashangaza waabuduo ambapo na wao wanazama katika mshangao. Zab.
47:7, 66:3, 68:35, 71:16, 89:7
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni