UIMBAJI NI TAALUMA
Mwimbaji asiyejua kuimba hawezi kuwa huru kuhudumu ni
muhimu afahamu uimbaji, ili aimbe kwa uhuru na kwa ufanisi. Ufanisi unahitaji
muda wa mazoezi yakutosha pamoja na mwalimu mwenye uwezo wakukuelekeza jinsi ya
kuimba Muziki (uimbaji) upo katika mafungu makuu mawili:
1.
Vocal
2.
Instrumentals
VOCAL:
- Ni sauti ya wanadamu. Sauti isiyochanganywa kitu
chochote. Sauti asilia ya mtu (Natural voice)
INSTRUMENTALS:
- Ni sauti zitokanazo na vyombo. Sauti pasipo kuchanganywa
na kitu chochote yaani ala za muziki.
Sehemu hizi mbili zikichanganywa pamoja hufanya kitu
kinachoitwa muziki (uimbaji) na kukamilisha maana ya neno muziki.
SAUTI.
Ni hisia inayonaswa na masikio na (hutengenezwa) na
msuguano wa hewa katika mzunguko, mgongano wa vitu au mkwaruzo kiasi cha kutoa
mlio (sauti).
SAUTI –MLIO (AUDIBLE, SOUND)
Kitaalamu Sauti ina misingi au kanuni. Misingi hiyo ni
Miwili. Ni kwa misingi ya sehemu hizo mbili kuu- Sauti
hujengwa/huumbika, tutaelewa misingi hiyo vizuri kwa
kuziangalia tabia za sauti
(Characteristics of Musical Sound) Au tabia za milio.
- Msingi wa
kwanza:
Sauti ina tabia ya –
Melody – Yaani kwa Kiswahili – Ghani
Melody – Ghani – Ni mistari ya sauti ya muziki inayotambulisha chanzo (tone) cha wimbo
Melody – Ghani – Ni mistari ya sauti ya muziki inayotambulisha chanzo (tone) cha wimbo
ni sauti yenye
kuelekeza ubora wa mtiririko wa ghani (melody)
unaokupa hisia ya mlio unaohusika au unaousikia.
Rhythm – Ni utaratibu au mfumo wa aina ya mwendo wa sauti katika wakati au mfululizo wa sauti katika muda, mwendo, pigo, mdundo au msisimko. Uwezo wa sauti wa kutembea katika wakati usiobadilika.
Harmony –
Mkusanyiko wa sauti unaopendeza, utaratibu au mfumo wa ulinganifu wa sauti,
usawa, muafaka, kusikilizana pasipokuachana kwa sauti au kuwa nje ya tune hasa
wakati kuna watu wengi wanaimba, katika ngazi tofauti yaani sauti ya msitari wa
1, 2, 3 na 4 pamoja.
Unison—Ni sauti ya aina moja inayoimbwa na watu wengi bila ya kutofautisha ngazi za sauti ya kwanza, pili, tatu na nne. Na kwa kawaida sauti ya unison hutumia sauti ya kwanza.
Unison—Ni sauti ya aina moja inayoimbwa na watu wengi bila ya kutofautisha ngazi za sauti ya kwanza, pili, tatu na nne. Na kwa kawaida sauti ya unison hutumia sauti ya kwanza.
Form – Ni
mwonekano wa kipekee, utaratibu au mfumo wa kuweka uimbaji katika aina ya mfumo
unaojitambulisha katika mtindo wake wenyewe kama vile mtindo wa kizungu, wa
kiafrika, kinyakyusa, kibena nakadhalika.
Tone Color – Aina
mbalimbali za sauti kufuatana na chombo au mtu anayeimba
– kwa mwanadamu sauti
hutegemea mapafu yake na mishipa ya fahamu ya kichwani.
Yaani sauti kavu, sauti
laini, yenye mikwaruzo, yenye mawimbi nakadhalika,
kusikika kwa sauti
kipeke, kivyake kwa kadri ya mtu anavyotoa sauti au chombo kinavyo toa sauti
kwa namna ya mlio wake
Msingi wa
Pili:
Sehemu ya kwanza Nimetaja nadharia ya tabia za sauti,
tabia hizi huwezi kuziona wala kuzihisi, ama kuzisikia, ila unaweza kuzifikiria
katika mawazo.
- Kuimba sio nadharia wala mawazo ni matendo halisi.
- Nadharia hiyo lazima itafsiriwa katika vitendo
tunavyoweza kuviona, kuhisi, kusikia tabia za sauti au milio hiyo.
- Haya yanawezekana kwa kutumia nyenzo, njia za muziki za
kiufundi zinazotuwesha kutenda.
(Musical Skills Performance Methods)
(Musical Skills Performance Methods)
Nyenzo au njia hizo ni:
(a) Kuimba –
(Singing – Melody) Unapoimba ndipo Ghani
itajitokeza katika mpangilio wa sauti kwa njia inayopendeza na kwa utaratibu,
hapo Tone Color itasikika yaani kwa kuimba wimbo, ghani na aina za sauti katika
ubora wake utasikika.
(b) Kupiga
vyombo vya muziki Accompanyments vikolezo.
Melody ambayo ni Ghani itasikika – Tone color pia itasikika.
(c) Form,
Kutenda vitendo – (Moving Movement Steps) Rhythm Na Form itaonekana yaani kucheza kwa mwendo wa mapigo. Yaani sauti na maneno
unayoimba yataenda kwa kufuata mapigo
na midundo ya wimbo na kuwa na muonekano wa kipekee.
(d) Harmony. Kusikiliza ndiko kutakuwezesha kuleta ulinganifu katika
mkusanyiko wa sauti za kupendeza na kukuwezesha uimbe sawasawa na sauti
nyingine bila kuhitilafiana wala kuachana au kuwa nje ya ghani.
(e) Kuunda au Ubunifu (Creation
– Form, Rhythm na melody) Wimbo
utakamilishwa kwa kuunganisha nyenzo hizo nakuwa halisi yaani wimbo halisi
wenye kusikika vizuri.
Katika msingi huu wa
pili tunafika katika kukamilisha muziki na ndiyo uimbaji. Muziki ni sayansi
lakini kila mmoja wetu anayo na anaweza kuitendea kazi kwa kujifunza na
kujizoeza.
SIFA ZA
MWIMBAJI.
Kazi ya kumwimbia na kumsifu Mungu ni huduma inayodai
maisha ya mtu kujitoa kikamilifu na kuwa na mwenendo ulio safi.
- Mungu aliwaweka waimbaji katika hekalu waifanye huduma
hiyo maalumu.
- Kwa hiyo ni lazima pawepo na sifa za kutosha na mchakato
yakinifu kuhusu mwimbaji anayefaa kuifanya huduma hii kubwa.
- Mwimbaji ni chombo cha sifa za Mungu ni lazima chombo
hicho kiwe na sifa zinazoendana na sifa za Mungu na heshima kimfaacho Bwana kwa
kazi hiyo.
“Mpigieni BWANA vigelegele enyi wenyi
haki, Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo (Zaburi 33:1 1)
ROHO YA UIMBAJI
Ni kujaa Neno, kusemezana, kushangilia, kuimba
kufundishana, kuonyana, kujaliana, umoja na shukrani,
“Tena
msilewe kwa mvinyo ambamo mna ufisadi ;bali mjazwe roho, mkisemezana kwa zaburi
natenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;
na kumshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu
Yesu Kristo” (Waefeso 5:18-20)
“Neno la Kristo na
likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa
zaburi na nyimbo, na tenzi za rohoni, huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni
mwenu”. (Wakolosai 3:16-17)
hii ndiyo Roho ya uimbaji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni