Jumatatu, 10 Juni 2013

AINA GANI YA MUZIKI WA INJILI UNAOFAA MAKANISANI?


Aina gani ya muziki wa injili unafaa makanisani?


Naomba nianze kwa kuwapongeza na kuwaombea baraka nyingi za Mungu watumishi woote ambao wanamtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji. Mungu azidi kuwainua na kuumba kitu kipya ndani yenu kila siku. Kazi yenu inatuinua na kutubariki sana na kwa kweli inachangia sana katika kulikuza kundi la Bwana.
Mara nyingi nimekutana na watu ambao wamesema kwamba muziki wa injili au muziki wa kanisani umeingiliwa na mamluki kibao na unakuwa hauna tena utukufu wa Mungu. Mimi sipingi na wala sikubali kirahisi pia!! Lakini ninaomba wapendwa tusaidiane katika jambo hili. Kwa kuwa huwa tunakuwa wepesi sana kusema kwamba baadhi ya midundo (beats) kama Taarab, Reggae, Rap, Rock n Roll n.k haifai kwenye injili basi ninaomba tujue ni aina gani ya mdundo(beat) inayofaa kwenye muziki wa Injili?
Kwamba ni slow Rock, jazz, ballad, March, zouk n.k Nadhani hii itakuwa ndio solution ya malumbano yooote. Tukumbuke kwamba hapa nimeongelea aina ya muziki nikitegemea kwamba mashairi katika muziki huu yaani lyrics ni za kumtukuza Mungu pekee. Naomba tusaidiane katika kuujenga mwili wa Kristo! Ndimi Mshirika,


1.   
Lameck
Mimi nadhani muziki wa injili hasa katika nchi yetu ya tanzania unaacha mwelekeo kwani wengi wanaimba kwa ajili ya biashara kiasi kwamba wanaugeuza muziki wa injili kama ni muziki wa dansi. Mungu alisema nisifuni kwa zeze na vinubi kwa kuimba na kucheza lakini sasa watu wanaiga beats za miziki ya dansi kiasi kwamba maana na ujumbe katika muziki wa injili unapotea. Tusimtukuze mungu kwa kutaka kuonekana kwenye luninga na kwingineko bali tumtukuze mungu kwa moyo na tulihimidi jina lake siku zote.watu wanaimba muziki kwa kutuma ujumbe wa masengenyo nadhani si mahali pake.muziki wa injili ni ujumbe kwa jamii kutoka katika biblia na si vinginevyo
2.   

Asante saana kwa mada hii njema. Naamini inagusa wengi na ni swali ambalo limekuwa likiulizwa na wengi.
Narejea niliyosema kwenye “post” ya MAKOMA miezi kadhaa iliyopita kuwa muziki ni asili, na suala la wapi unaonekana ni wa kimataifa yategemea wanapata na kutumia miziki hiyo kwa namna gani. Mfano ni kwamba ukienda Jamaica na kusema huwezi kumuimbia Mungu kwa midundo ya reggae hutaeleweka, kama ambavyo utaenda Congo ukasema midundo yao ni ya kimataifa. Lakini kwanini twaamini kuwa midundo kama ya kikongo ni ya kimataifa? Ni kwa kuwa kwetu ilianza kuja ikiambatana na mashairi yasiyo ya kiMungu na hilo (kama yalivyo mengine mengi) LIKARIRIWA kuwa ni muziki wa kiMataifa. Lakini sidhani kama ukiweka nyimbo zinazoheshimika na kupendwa na kukubalika zaidi Tanzani na kuzicheza Israeli, ama Marekani ama Carribean ama Amerika ya Kusini utapata jibu la huo ndio muziki wa injili.
Narejea tena kuwa TUMEKARIRISHWA VIBAYA kuwa kuna midundo ya kumtukuza Mungu. Hili si sahihi, maana midundo mingi ina asili na kote wanaitumia kumtukuza Mungu. Hivi mmeshaona wasanii nyota na wanaoheshimika kwa muziki wa Injili hapa Marekani wanatumia midundo gani? Ingia you tube utafute kina Kirk Franklin ama Yolanda Adams ama Bobby Jones ama familia nzima ya kina Winans (kwa pamoja ama mmoja mmoja) uone wanatumia midundo gani. Kuanzia Mdumange, Chakacha, Taarab, Hip Hop mpaka REGGAE ni midundo inayokubalika katika kueneza injili. Matumizi kuendana na jamii ni muhimu lakini si makosa kuitumia.
Blessings
3.
   

Kitu chochote tunachofanya watu wa Mungu ikiwa ni pamoja na kwaya, lazima kimtukuze Mungu, na pia hata wasioamini wasiwe na neno kwacho tunachokifanya. Maandiko yanasema, “Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni”, Mathayo 5:20.
Iwapo watu wasioamini, wanaweza kufanya mambo mazuri yanayohusiana na imani zao kwa kukwepa kukwaza wengine, si zaidi sana sisi tunaosema kuwa tunamjua Mungu? Iwapo hatutaweza kuwazidi hao, maandiko yanasema hatutaurithi kwamwe ufalma wa Mungu. Kama watu wa Mungu tunapaswa kuliangalia hilo.
Watu wengi wenye nia ya kumtafuta Mungu, wanashindwa kuuamini wokovu, kwa sababu tu ya mambo yetu mengi tunayoyafanya katika ucha Mungu wetu ambayo hayana ushuhuda. Mambo hayo ni pamoja na hizo kwaya zinazoimbwa nyakati hizi n.k. Siku hizi nyimbo za kwaya tunazozitunga tunazitunga kwa kutazama tu jinsi sisi tutakavyopendezwa kwazo, hatutazami jinsi wasioamini watakavyoziona na kutuelewa!. Hatuangalii upande wa pili, na hiyo ndiyo sehemu ambayo shetani anapata goli kwetu.
Kuna namna nyingi tu na nzuri za kumwimbia Mungu, na kila mtu hata asiyeamini akaweza kusema kweli kuna Mungu eneo hilo. Namna hizo si lazima ziigizwe kwa mtindo wa tamaduni yoyote duniani. Tukiwa katika Roho katika kuimba, tunaweza kufanya namna zetu za kuimba zikawa moja duniani kote. Kinachotatiza sasa hivi ni kwa sababu, watu wanampenda Mungu na hapo hapo bado wanaipenda dunia, namna hiyo lazima tutachanganya tu, dunia na ya Mungu.
Nakumbuka kuanzia katikati ya miaka ya themanini na kuendelea, kulikuwa na kwaya moja ya Ulyankurlu Tabora, nyakati hizo nilikuwa sijaokoka bado, niliipenda sana ile kwaya, na niliinunua kanda yake ya kaseti.
Kununua kwangu kwa ile kanda hakukuwa kwa sababu ya kuburidika, bali kwa sababu ya ujumbe na umakini wa kiroho uliokuwemo katika kanda ile. Japo mimi nilikuwa si mtu wa Rohoni nyakati hizo, lakini kila nilipokuwa nasikia nilikuwa naguswa! Kutokana na jinsi nilivyokuwa mtu wa dini, ilikuwa si rahisi kuikubali kanda ile na nyimbo zake kama ingekuwa kama zilivyo kanda za nyimbo za nyakati hizi zenye vionjo vya miziki ya kidunia.
Kwaya ile kwa kweli kwa wale wanaoifahamu, watanielewa ninachokielezea, ilikuwa ni kwaya ambayo haikuwa na vionjo wala utamaduni wowote wa kidunia, lakini ilipendeza na iliweza kuliza watu, hasa kwa wimbo moja uliokuwa unajulikana kwa jina la, “Wakati ule wa Nuhu, watu walimwasi Bwana”. Je, nyakati hizi ndiyo haiwezekani kuwa na kwaya kama zile? Je hatuoni kuwa tunazidi kuporomoka na kuingia anga jingine kiroho?
Ukiangalia hali halisi, inaonesha kuwa watu wasioamini wanaufahamu sana wa mambo ya Mungu kuliko sisi tunaosema tumeokolewa. Tunapingana na kila Neno jema la Mungu na kuweka ya kwetu wenyewe.
Ninavyofahamu mimi kuimba, ni kwa ajili ya kumtukuza Mungu, na wala si kwa ajili ya kuwafurahisha wanadamu wanokuwa wanasikiliza au kuona kimwili. Kama ni kuwafurahisha hao wanadamu, basi ni kuwafurahisha kwa kuwafanya kufikia toba kwa nyimbo tunazoziimba.
Nyimbo zinapaswa kuheshimiwa na kuogopwa na watu wasioamini kama wanavyoyaheshimu na kuyaogopa mahubiri ya watumishi wa Mungu. Iwapo watapata neema ya kusikiliza basi wafikie toba kama vile wamesikia mahubiri.
Mahubiri mengine ya watumishi wa Mungu, yanaheshimiwa na kuogopwa kusikilizwa hata na watu wanaodhaniwa kuwa wameokoka. Wanayaogopa wasije wakayasikia na kuelewa, na wakabadili misimamo yao ya mafundisho yao ya awali. Iwapo katika mahubiri ya Neno la Mungu kuna nguvu kiasi hicho, kwa nini nyimbo zetu za kwaya nazo zisiwe na nguvu ya Mungu kama ilivyo katika mahubiri hayo?. Bila shaka kwaya zetu zingekuwa hivyo, shetani asingekuwa na nafasi kabisa ya kulichezea Kanisa la Mungu?
Shalom watu wa Mungu, huo ni mtizamo wangu kuhusiana na mziki unaopaswa kuwa makanisani!. Tuendelee kuelimishana.
4.   

Wow! Nimependezwa na maelezo ya Kaka Bernard. Lakini bado nadhani swali linabaki lilelile kuwa AINA GANI YA MUZIKI WA INJILI UNAFAA? Ulyankulu ilikuwa kwaya bora na itaendelea kuwa kwenye historia. Lakini bado nasema kuwa muziki ni asili na unatokana na mahali ulipo. Unless kama Kaka Godlove angesema kanisani wapi (kama ni Tanzania ama Dar ama mahala fulani) siwezi kusema kuna aina ya muziki ambao ni kwa ajili ya injili.
Ninalomaanisha hapa ni kwamba ukienda nchi nyingine huo muziki wa Ulyankulu hautakuwa akilini mwao na kama muziki pekee toka Tanzania ma awa midundo hiyo wanaoufahamu ni wa kimataifa, basi na huo utakuwa wa kimataifa.
Kwa hiyo kama twazungumzia wa Injili duniani basi hakuna muziki maalum, labda muziki wa aina fulani kulingana na mazingira ya wananchi wa eneo hilo.
Amani kwenu
5.  
 

Mimi nafikiri Inategemea na mtu mwenyewe anavyoguswa ki imani, Mimi ninakisikiza nyimbo za kwaya za zamani ambazo zilikuwa hazitumii hii mitindo ya sasa naguswa sana , hizi zinazopigwa kama muziki wa dansi nafurahia ala zake lakini kiimani hazinigusi sana, kutokana na kwamba nimekuwa sana kwenye muziki wa dansi na ninashindwa kuzitofautisha kabisa kwenye mawazo yangu
Labda kutokana na umri au sababu sijajengeka sana kwenye wokovu, lakini nikiangalia kwa vijana wadogo wao kama wamekulia kwenye muziki tuu huu wa dansi sidhani kama wanaweza kuguswa na muziki usio wa mitindo ya dansi
Kitu kingine ni uvaaji na uchezaji ukishaafanana sana inakuwa vigumu sana kwa watu kutofautisha muziki wa dini na wa dansi
Hivyo Makanisani kwangu mimi ni kuangalia wana watu wa aina gani, ndiyo maana kwenye makanisa zamani(sijui kuhusu siku hizi niko nje kwa muda), kulikuwa na kwaya ya Vijana na Kwaya Kuu, kwaya ya vijana ilikuwa inatumia ala za kisasa na Kwanya kuu ilikuwa wanaaimba sana sana kutumia Kinanda
Huu ni mtizamo wangu tuu
6.   

Kwanza nizungumze kidogo kuhusu waimbaji, na waandishi wa nyimbo za injili. Kutokukuwa kiroho kwa waimbaji na waandishi wa nyimbo za injili kumefanya nyimbo za injlili zionekane tuu kama mdundo na sio injili kama tunavyodhania. Leo hii mtu anaokoka na kipaji chake cha kuimba, hapo hapo utamsikia ametangaza concerts, sasa unategemea mtu huyo afanye vitu gani jukwani ama kanisani? Si ni uzoefu wake tuu wakuwafurahisha watu, japo utasikia haleluya yuma yake!!! Ninapo zungumza hilo, ninauhakika maana na mimi pia ni muimbaji wa nyimbo za injli. Nimekuwa mwalimu wa kwaya miaka mingi na kwambia nimeona mengi sana. Siku ya kwanza mtu anafika kanisani, kinacho mvutia tuu ni kujiunga na kwaya na kuwa muimbaji maramoja, hata nikaweka sheria kwenye kwaya kwamba mtu atafanya mazoezi kwanza miezi sita kabla aanze kuimba mbele ya kanisa, nikaomba mchungaji wa kanisa aweke kwenye agenda kila week mafundisho yawaimbaji wanaotaka kujiunga na kwaya ili wafundishwe huduma ya uimbaji ni nini. Hayo yalifanya watu wasikimbilie sana kwenye kwaya maana uimbaji sio takataka. Ninapowasikiriza waimbaji wengine nchini Tanzania, hata sehemu zingine, nashindwa kuelewa kwamba wamefundishwa na wachungaji wao huduma ya uimbaji ni nini. Kama kwaya ya Ulyankulu iliweza kubariki watu kwa nyimbo zao miaka ile, ni kwasababu ya kanisa lao lilowaelekeza hata na kuwawekea mipaka ili huduma yao isiingiliwe na ibilisi. Sasa swali ninalo jiuliza, je wachungaji wa siku hizi wanayo mamlaka kwa waimbaji? Wengi hao waimbaji wameanguka na kurudi nyuma baada ya kufanikiwa katika huduma hiyo, yote hayo ni kwasababu hawajafundishwa vizuri kabla ya kujiingiza kwenye uimbaji. Mdundo wa nyimbo, hutokana na jinsi mtu amepata wimbo. Kama umefunuliwa maneno ya wimbo, hakika na beat ya wimbo huo itaenda sawa na maneno ulioyafunuliwa. Malanyingi sana unapofunuliwa wimbo, unafuliwa melody ya wimbo huo. Zipo nyimbo zingine zinazotungwa juu ya wazo fulani mtu amekuwa nalo, na hapo ndipo hatari ilipo sasa. Maana nyimbo hizo unakaa na kutafakari lipi la kufanya ili wazo lako liweze kufanikiwa. Ndio maana muimbaji anajikuta ametafuta kuiga midundo ya nyimbo alizowahi kuzisikia ama anazosikiriza zilizoleta mafanikio kwa watunzi na waimbaji hao. Mala nyingi nyimbo hizo zinakuwa za kidunia. Na wengi hao waimbaji hawanamda wa kukaa na wapigamziki wao ili wa buni kitu kipya, huwa wanaenda kununuwa beats hizohizo na wanaweka maneno yao. Hilo linasababisha mtu atakaposikiriza wimbo huwo hakiri yake yote itaishia kwa mtunzi wa mziki ule, na hataweza kusikiriza ujumbe uliomo.
Suala hili lizungumziwe ili tuweze kujifunza kwa undani, shetani asituweze kwa nyimbo tunazoziimba na kuzitunga kwa midundo tofauti.
Mziki ni mziki tu
hakuna chakusema kama miziki ya ki 80′s ina nguvu/upako wa roho sana kushinda yakileo. Hata iwe reggea na mingine midundo tofauti it doesn’t matter, what matters is
Watu wengi sasahivi wanaimba kwakupenda kujionyesha, wapenda sifa (kuabudiwa) watu hatujui tena maana ya uimbaji wa nyimbo za injili na tunapokua katika hali kama hii ni vigumu sana kwa kuongozwa na Roho wa Mungu, na nyimbo zetu zinakua hazina upako wa Roho mtakatifu, wala hazina Nguvu kama mahuri ya watu wa Mungu wengine
Haijalishi aina gani ya mziki/mdungo bali uhusiano wako na Roho wa Mungu.
Isaack:)
Kwa upande wangu mimi nafikiri uimbaji unatakiwa ufanyike kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu,haijalishi muziki utakuwa katika mahadhi ya Leggae,Rhumba,Rap n.k.Kama tukisema kwamba muziki uliopigwa katika mahadhi ya Leggae au Rhumba si wa ki – Mungu tutakuwa tunakosea.Mtu anaweza akaimba muziki ambao kwa kuusikiliza ukaonekana ni wa Ki – Mungu lakini hauna mguso wowote Kiroho.Kwa upande wangu naweza kutoa mfano wa nyimbo za Marehemu Angela Chibalonza,ni nyimbo zilizo katika mahadhi ya Kikongo.lakini nikizisikiliza kwa upande wangu naona zina nigusa ki – kwelikweli.Na pia kuna nyimbo nyingine inaweza kuimbwa kwa Taratibu (Nyimbo ya kuabudu) lakini isilete mguso wowote Kiroho.Kwa hiyo kwa upande wangu nafikiri inategemea na Jinsi Roho Mtakatifu atakavyopenda.Nakubaliana moja kwa moja na Mpendwa pale juu Mubelwa T.Bandio.
N:B.Hiyo ni kwa upande wangu jinsi nionavyo.Itategemea Roho Mtakatifu atakavyokuongoza wewe binafsi,Ndio maana kuna Makanisa mengi,mengine watu wanaimba wamesimama wima,yapo kwa ajili ya wasiopenda kurukaruka..MUNGU ATUTIE NGUVU..

Ndugu zangu naamini hakuna kanuni ya namna ya kumwimbia ama kumtukuza Mungu.Maswali yanakuja pale tunapoona kuwa mtu anaimba ama kutukuza asichokijua, anachoimba ni kinyume na maisha yake, wanaimba kwa ajili ya wanadamu na siyo Mungu maana wanafanya biashara.
Matunda ya kazi yao ni kuleta Babeli, yana kupotosha kweli.Uimbaji wa injili kwa sasa una malengo ya kutajirisha waimbaji wenyewe na siyo kumtukuza Mungu, utitiri wa waimbaji unazidi kuleta upotoshaji, hakika thawabu yao ipo tayari.
Kuguswa kwa wengi kunakoelezwa hakuhusiani na Mungu bali hisia zao ndiyo maana hakuna mabadiliko endelevu.
Ndugu zangu Mungu bado anatafuta watakao mwabudu Mungu katika roho na kweli, jihoji wenyewe ni nani anafanya hivyo.Ujisijidanganye.
Mtu yeyote anayeimba na kuuza anachoimba tayari amepotosha maana ya anachokiimba. Tena nawaonya waache upuuzi huu mara moja.
Ni wapi katika Biblia imeandikwa uimbaji ni huduma inayojitegemea? Ni wapi uimbaji unauzwa katika Biblia?
Tena tusijidanganye; hata mtu anayenunua nyimbo naye ameingia katika mchezo wa hujuma ya kweli ya Kristo na maana ya kumwimbia na kumwabudu Mungu.
Hii sumu ya kujinufaisha imeenea sana.Mtu anayeimba na kuuza nyimbo zake hamjui Mungu na haujui mwili wa Kristo.
Namna ya uimbaji na vyombo gani si la msingi zaidi ya maana na kusudi la uimbaji wenyewe.Huyu ni shetani mwenyewe!
Kadri uimbaji huu wa sumu unavyoendelea ndivyo hali ya maadili na hofu ya Mungu inavyopungua maana Mungu hayupo katika uimbaji huu.
Na siyo uimbaji tu bali hata mahubiri mengi.Sumu naweza kusema imeanzisha USA na kuenea kwa kasi sana duniani kote. Utungaji wa vitabu vya kiroho na kuuza, video na cd. Tunatengeneza mamilionea kwa kuupotosha ukweli na uhalisia wa Mwili wa Kristo.
Uchafu umehamia kanisani.Je, huoni? Mwahoji vyombo na namna ya uimbaji?
KAMA HATUTAITA DHAMBI KWA JINA LAKE BASI TUMEPOTEA.
LAZIMA TUKEMEE SUMU HII YA UTUMISHI WA MANUFAA BINAFSI NA KUWA BARAKA KWA WOTE.KAMWE TUSIUMEGE MWILI WA KRISTO.NDUGU ZANGU MAMBO YATAKUWA MAGUMU ZAIDI SIKU ZA USONI NA MTAONA USHAHIDI WA UOVU WA WAIMBAJI HAYA MAANA ITATHIBIKA JINSI WASIVYOMJUA MUNGU.
BWANA AWE NA ROHO YAKO
10. 

Amani, Heshima na Upendo kwenu nyote.
Nafurahia saana jamvi hili kwa kuwa linaelimisha na kutoa maoni mbalimbali kulingana na uamini wa mtu. Kaka Fred hapo juu amenikumbusha hadithi ya mtu ambaye alisema “KAMA HUTAKI WAKUONE WEWE FUMBA MACHO” akimaanisha kuwa kama huwaoni basi hawakuoni japo si sahihi. Nimefurahia na NINAHESHIMU mawazo ya ndugu Fred hapo juu lakini kusema kwamba “Mtu yeyote anayeimba na kuuza anachoimba tayari amepotosha maana ya anachokiimba. Tena nawaonya waache upuuzi huu mara moja.Ni wapi katika Biblia imeandikwa uimbaji ni huduma inayojitegemea? Ni wapi uimbaji unauzwa katika Biblia?” na kusema “Mtu yeyote anayeimba na kuuza anachoimba tayari amepotosha maana ya anachokiimba. Tena nawaonya waache upuuzi huu mara moja.” nina wasiwasi kama tafsiri yako si kwa kuwa umefumba macho. Si kila aimbaye na kuuza anakuwa na malengo ya kujinufaisha. Yaonekana ndugu yangu wafuatilia saana Biblia na pengine kama kuna unaweza ku-mention waliposema kuhusu kuwalipa wachungaji mishahara ama kuhusu watu kulipia huduma kama hizi unazotumia kuwasiliana na sote ulimwenguni ama kuchangia huduma za kusambaza injili kwa wasioijua huko kwenye kazi za kimisionari na mengine mengi yanayoendelea katika mzunguko mzima wa uenezaji injili sasa ungesaidia kuyataja. Unaposema kanda zisiuzwe kwa kuwa haijaandikwa kwenye biblia napata shaka na imani ama tafsiri yako ya BIBLIA. Kumbuka Biblia haisomwi kama kitabu cha Algebra na kutafsiri kila usomacho bila kukumbuka kuwa Yesu mwenyewe aliongea kwa mifano kunaweza kukuweka kwenye nafasi ambayo ukajikuta mkosolewa badala ya mkosoaji.
Ni kweli kuwa wapo watu wanaofanya BIASHARA ndani ya neno la Mungu. Na ni kweli kuwa hata baadhi ya wachungaji feki wanafanya hivyo na nina mifano kamili ambapo kuna kanisa niliwahi kuhudhuria tukaambiwa tutaombewa na urefu wa sala utategemea na kiasi cha dola unachoweka kwenye pesa ya maombi. Sikurejea tena. Kwa hiyo ni kweli kuwa wapo, lakini si kweli kuwa akishauza kanda basi ni “mpuuzi”
NO. NO. NO.
CHANGAMOTO YANGU KWAKO NDUGU FRED ni kutaja nyimbo tatu ama za wanamuziki angalau watatu unazoona ni za injili kwelikweli na kisha uniambie kama hawakugharamika kuzitengeneza na hawakurejesha gharama hizo.
Kama utataja za wasanii watatu basi ujue kuwa ulizisikia na zikakugusa kwa kuwa kuna mtu alilipia utengenezaji na usambazaji na ndio maana ukabarikiwa nazo na kama huna basi hauna cha kuchangia pia maana huna unalopenda katika muziki wa injili.
Nadhani unastahili kuwaomba watumishi msamaha kwa kuwaita wapuuzi


Of coz Ndg Fred hapo umesema chamaana
tusiende mbali. Nakumbuka mimi mara ya kwanza nimepewa kuongoza nyimbo ya kuabudu kanisani heheee, nakwambia ilikua balaa!! kwanini coz nilikua bado sijakamilika na nilikua sijui nini maana ya kuabudu. So it depends actually on who is singing
Mungu awe nanyi Ndg zangu:)
12. 

Ndugu zangu,
Bwana Yesu asifiwe!
Na mimi nimeona nitoe mchango katika hili. Kutokana na muda kuwa mfinyu, nitakuwa very brief, lakini nitajitahidi kufikisha kile Roho anatamani kiwafikie!
Moja, lazima tujue kuwa shetani alikuwa ni Kerubi Afunikaye: ambaye ni Muziki unaoishi! Lakini pia lazima tujue kuwa baada ya anguko shetani aliharibu hekima yake, ikiwemo pia uimbaji. So Lazima alitengeneza namna ya muziki wake. Baada ya hayo, ningependa niende kwenye Jibu la swali la brother Godlove kama ifuatavyo:
Kwanza lazima tukubaliane, muziki wa injili si jina sahihi, bali ni muziki wa kumsifu Mungu. Muziki huu wa kumsifu Mungu ni kwa ajili ya kumsifu Mungu. Pili lazima tukubaliane kuwa, Mwili wetu ni rafiki mkuu wa shetani. Hata Yesu mwenyewe alishindana na mwili wake kuelekea Kalvari. Tatu Lazima tukubali Mungu siku zote huweka tofauti namna anavyotaka tumwabudu, na siku zote huwa ni tofauti na mungu wa dunia hii. Na Mwisho lazima tukubaliane kuwa, tunaelekea katika siku za Babeli, Nuhu na Sodoma & Gomora; zikiwa ni dalili za kurudi mwana wa Adamu. Uamsho wa upagani sasa upo juu mno na unavamia kanisa kwa kasi ya ajabu!
1. Muziki wa kumsifu Mungu, lazima uiinue roho yako imsifu na kumwabudu Mungu. Muziki ambao utakufanya uanguke mbele za Mungu wako, na kujiona namna gani ulivyo mwanadamu asiye kitu na jinsi yeye alivyo Mungu mtakatifu. Ni muziki unaokufanya uone huruma na rehema za Mungu na kukufanya umsifu kwa aliyokutendea. Ni maelezo marefu lakini natumaini mmenielewa.
Muziki ambao unauamsha na kuutia mwili tashwishi ili ujifurahishe na kuruka na kumweka Mungu pembeni, huo ni wa dunia bila kujali mashairi yake. Muziki wa kumsifu Mungu ni kwa ajili ya Mungu na si vinginevyo. Muziki ambao kazi yake ni kuufanya mwili ujisikie vizuri, si muziki wa sifa kwa Mungu wetu.
2. Muziki wa kumsifu Mungu huimbwa kwa kicho cha hali ya juu. Ni muziki ambao wanaoimba wanajua ya kuwa Mungu wanayemwimbia ni Mungu mtakatifu. Kuna kipindi nilikuwa nasikiliza muziki fulani nyumbani, na kuna ustadhi mmoja akasema “mziki huu kweli ni wa Mungu na huyu jamaa anamwimbia Mungu. Huu mziki hauwezi kupigwa baa.” Imagine! Ni kwa sababu mwimbaji, vyombo vilivyopigwa na wimbo wenyewe, vilikuwa na kicho cha Mungu.
3. Muziki wa sifa una lengo la kumwinua Mungu pekee na si mwanadamu. Mungu hachangii utkufu na awaye yeyote. Kwa hiyo Muziki wa sifa ni kwa ajili ya kumwinua Mungu na si mwanadamu. Kila jambo linalofanyika, kila neno linalotamkwa lazima yawe na utukufu kwa Mungu. Muziki unaomwinua mwanadamu, awe mwimbaji au wasikilizaji, huo si muziki wa kumsifu Mungu
4. Balance ya vyombo vya Muziki. Wasomaji wa Biblia wanajua kuwa ngoma (Drum Kick) haipo katika Biblia. Hii inaleta maana unapojua kuwa ngoma ipo kwa ajili ya kuongoza vyombo vya muziki viende pamoja (sync.) Sasa pale ngoma (Drum kick/ryhthm) inapokuwa juu, huu unakuwa si muziki wa kumsifu Mungu bali ni Ngoma za kupandishia majini. Fikiria, kwa nini Mungu hakuweka kick ktk listi ya vyombo vya muziki kwenye Biblia? Ni kwa sababu ngoma ina nguvu ya kuuamsha mwili na kuusisimua. Ngoma ikiwa juu na ya kasi, mtu anaweza kuwa high, akafanya jambo lolote. Kama ingetokea mwimbaji yeyote /producer akafuata standards za Mungu, na kupanga vyombo ambavyo Biblia imeagiza, huo muziki utakaotoka utakuwa “heaven class” music! Ninachosema ni kuwa Biblia inautambua muziki katika melody na si rhythm.
4. Muziki wa kumsifu Mungu lazima uwe sahihi kibiblia. Nyimbo zote, lazima zipatane na Biblia kwa asilimia mia moja! Kinyume na hapo ni muziki wa shetani, maana utauita jina gani muziki unaoimbwa huku maneno yake yakipingana na Biblia?
5. Mwisho, kutokana na wakati, Muziki wa kumsifu Mungu lazima usiambatane wala ku-promote utamaduni mwingine wowote ule. Tafsiri ya utamaduni ni namna nzima ya maisha. Hii inajumlish namna ya kuvaa, kuongea, kuabudu n.k. Yesu alipokuja duniani, alianzisha namna mpya ya maisha, utamaduni wa Kikristo. Ndio maana mtu akimgeukia Kristo, anageuzwa kwa Roho wa Kristo, kufuata utaratibu huu wa maisha, wa raia wa mbinguni.
Baada ya kusema hayo, muziki wa kumsifu Mungu, ni lazima u-promote utamaduni wa Kikristo kama ambavyo umeainishwa ktk Biblia. Naomba nitaje kwa ufupi baadhi ya muziki na tamaduni zinazokuwa zinahubiriwa na aina husika ya Muziki ambazo haziwezi kuwa Muziki wa kumsifu Mungu, hata kama tutaongeza viambata kama Jesus.. au Gospel.. n.k:
–> Reggae —- Urastafari
–> Rap —- Hip Hop
–> Taarab — Utamaduni wa pwani(Samahani kama hujaishi pwani, sina muda wa kuelezea)
–> Rock n Roll — Ushetani na Uabudu Shetani(satanism & Devil worship)
–> Muziki wa kizazi kipya — Vuguvugu la enzi za zama mpya (The New Age Movement)
–> Ngoma za asili — dini za asili za kabila husika (Nyimbo za kutambika, za mavuno n.k)
Listi ni ndefu, lakini natumai kwa mwongozo mfupi sana hapo juu, unaweza kupata picha, muziki wa Kikristo unafananaje.
CHANGAMOTO:
(a) Hebu fikiria Yesu akiwa katikati ya kundi la makutano. Kabla ya kuanza kufundisha, Petro akasimama na kuchana mashairi kadhaa ya rap na kisha Mary magdalene akashusha gospel R n B la nguvu, kabla ya Yohana kuwanyanyua makutano wakatengeneza duara kisha wote kwa pamoja… vidole juu. Baada ya watu “kusifu na kuabudu” Yesu akaanza kufundisha…Think about that!
(b) Paulo na Sila walifungwa gerezani. Katikati ya usiku, ghafla Paulo akalianzisha Gospel reggae la nguvu, na alipomaliza Sila akadakia na Gospel Ragga Muffin, kabla Paulo hajarudi tena na Gospel Hip hop akichana verse na Sila akipiga Chorus. Wakati wafungwa wanashangaa shangaa, Sila akanzisha ngoma za kigiriki huku akihubiri kwa hayo mashairi, na kisha Gospel sebene la nguvu, kabla ya Paulo kumalizia session ya Sifa, huku akifuta jasho kwa taarabu la nguvu…hapo ndipo Mungu Yehovah akalitikisa gereza na kufanya jambo ambalo liliacha milango wazi, pingu zikaachia…..Think about that!
(c) Yehoshaphati alikabiliwa na vita ngumu na baada ya maombi alitakiwa atangulize vikosi vya waimbaji. Na hivi ndivyo mfalme alivyoamuru: Mstari wa mbele, Gospel Hip hop kisha Gospel sebene, halafu Gospel Rock n Roll na reggae. Walipoanza Ku-rock na Ku-roll, Bwana akaweka waviziaji na akawaua maadui zao wengi…blah blah…Think about this!
Bwana Yesu atusaidie, maana la sivyo; siku hiyo tutakuwa na kesi nyingi za kujibu mbele yake!
Neema ya Mungu na izidi kwenu watakatifu wake


Ndugu zangu naomba tusiingie kwenye hukumu bila sababu, narejea tena kusema kwamba lazima tutambue majira tuliyo nayo na kwamba ikiwa hatuna amani juu ya kitu tutulie na kutafakari na Bwana kabla ya kupiga hatua.
Kwamba nimeandika haimaanishi natoa maoni kwa kuwa naamini kuwa nami nina roho.
Theolojia ndiyo imezaa haya yaliyoleta mada hii nami huko siko bali katika kweli yote.
Ndugu zangu hapa tujikumbushe NAMNA YA KUMWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI.Ukiona unahisi kumtumikia Mungu na huna zana za kumtumikia ujue saa bado, ukitumia nguvu zako kutimiza unayodhani ni maelekezo ya Mungu utaishia pengine.
Dhamira yangu iko huru na sijahukumiwa kwa niliyoandika. Nina ujasiri kwa kilichoandikwa.
Ndugu zangu kuna mengi yanayohitaji uharaka katika utekelezaji, machache niliyataja katika mada iliyopita. Ushahidi wa kutotambua majira ni mwendelezo wa maelezo yanayompa ibilisi nafasi.
Mtumishi wa Mungu atakayehisi ametukanwa na ujumbe nilioandika na atafakari vema kuhusu kazi yake na amhoji Mungu kwa kina kisha atatambua ikiwa amesimama katika huduma hiyo kwa uaminifu wote. Vita si vyetu ila vya Bwana.
Saa yaja na hakika mambo yatakuwa magumu, tutahitajiana kuliko mwanzo.
Mwenye kusikia na ayasikie haya.



Natumaini hamjambo katika jina la Yesu.
ninavyo ona hapa kwanza watu tuna shindwa kujibu swali lililo ulizwa nakuanza kuzungumzia ujumbe unao takiwa kubebwa katika nyimbo.
swali limeuliza, ni aina gani ya muziki wa injili unafaa makanisani?
tukitaka kuorodhesha aina ya miziki iliyopo ni mingi sana hasa inayofahamika sana inaweza kuwani;reggae,hip hop,ragga, taarabu, ngoma za asili lumba, zuku nk aina za miziki hii ukisikia tu muziki au ala zake bila kusikia ujumbe uliomo utagundua kwamba muziki huu niaina fulani ya muziki. Nadhani hapo ndipo swali limelala sio ujumbe kama baadhi ya wachangiaji walivyo sema hasa Bw, Steve kama ukisema miziki ya taratibu ndio inavuta uwepo wa Mungu mbona kuna nyimbo za taratibu zinaimbwa watu wasio okoka na zina captvate yaani zina uwepo au mvuto wa aina yake ndio maana miziki yao haikosi mashabiki.
Ukitaka kutafuta aina ya muziki wa kumuimbia Mungu inawezekana usipate kitu kipya na hata ukipata bado watu wa dunia wanaweza kuuchukua na wakautumia watakavyo kwahiyo siku zote utakuwa huna chako. Kwa kumalizia niseme mziki ni mziki tofaut ni mashairi au ujumbe uliobebwa kwenye huo muziki ndio unao ufanya mziki kutambulika kwa aina yake.
kuna mtu anaimba mziki anamsifia mpenzi wake namwingine anaimba mziki anamsifia Mungu wake,mwingine anafanya mziki anamtukana adui, mwingine anafanya muziki anapatanisha maadui nk.
so mziki ni mziki tafauti ni mashairi pokeeni baraka katika jina la Bwana,

Hili suala la muziki wa injili ni changamoto pia. Ndugu Pona mfano unasikia muziki wako unapigwa Bar! Je unajisikiaje? mtu anakunywa kilevi huku akitikisa mguu na kichwa akijiburudisha na muziki wa Injili? mi nadhani kila muziki kuna roho inayoenda nayo. Ndio maana wanamuziki wengine kama mfano Michal Jackson miziki yake inamfanana na wanaopenda miziki yake wana roho wanayopokea. Kwa sasa kuna muziki unaitwa mpenzi jini watu wanaufurahia na kuna roho ndani yake,
tukija kwa muziki wa injili ni tofauti inabidi iwepo roho ndani yake Roho wa MUngu ambaye itamfanya yule anayeusikiliza muziki huo kumuhamasisha kumuabudu Mungu na kubadilisha maisha yake. Kama anafanya dhambi au anafanya dhihaka ahisi kumkosea Mungu heshima na kuacha mara moja. Hapo sasa suala la midundo na muziki mi sielewe zaidi, ila ni ufahamu wangu tu kuhusu wasikilizaji wa Muziki wa injili,


Mimi nadhani, tukisema mziki ni mziki eti kinachotakiwa ni maneno yaliyomo katika muziki huo tutakuwa tunazidi kwenda mbali na mapenzi ya Mungu.
Sidhani kama tumeishiwa kabisa melody za miziki mpaka kufikia kuweka melody ya miziki ya kidunia, kama Raggae, Rap, Taarab, Mziki wa kizazi kipya, Bumping Twist Rumba n.k.
Naomba moja aniambie, hivi zile nyimbo za Urlyankulu Tabora za miaka ile ya themanini themanini na nyingine zinazofanana na hizo, ambazo zilifanya baadhi ya watu kukabidhi maisha yao kwa Yesu, zilikuwa za mahadhi gani? Ni Rock? Rumba?, Raggae? Rap? au ni nini?.
Niwaeleze ndugu zanguni, ni kwamba nyimbo za zamani hakuna mpagani aliyethubutu kuzisikiliza kama Mungu hakumkusudia. Zilikuwa zina upako usio wa kawaida na zilikuwa hazina mahadhi yoyote ya dunia hii ya sasa. Ukisikia zinaimbwa katika mtaa ujue kuna mlokole eneo hilo!
Nyimbo za sasa hivi? Kila mtu anazo, wengine mpaka wameziweka kwenye simu zao, lakini wapagani, wanasema hakuna kuokoka duniani, lakini nyimbo za walokole wa kizazi kipya wanazo ukiwauliza wanasema zinaburudisha sana! Jamani, tumekuja kuburudisha watu au kuwafanya waokoke? Ashamed upon us!
Tunapotea, Tunapotea, Tunapotea.
Amani ya Kristo iwe nanyi nyote.
  

Amani, Heshima na Upendo kwenu.
Nianze na kuchangia maoni ya ndugu Steve M. YAONESHA WAJIKIMBIA KATIKA KUJITAFUTA. Yaani wewe wataka mtu aamini kuwa akiimba muziki kwa mahadhi ya asili anakuwa anaabudu miungu ya asili? AM SORRY kwa hilo nadhani umekosea. Kusema kuwa Reggae ni U-Rastafari nakupinga maana nautambua vema muziki wa Reggae, natambua u-rasta na imani zao maana nimezisoma na hakuna uhusiano wa moja kwa moja. Kuna imani, kuna muziki na kuna wenye vyote, wenye kimoja na wasio na vyote. Kwa hilo nikuweke sawa. Pengine nikupongeze kwa kuweka uhusiano wa miziki na muonekano wa watu wengi na namna waaminivyo lakini hilo ni kwa mujibu wa mapokeo yetu. Miaka ya nyuma hatukujua kama kuna wa-Kongo waimbao injili na muziki wa Kongo uliokuja kwetu ulikuwa wa ki-dunia na kutufanya tuamini kuwa aina ya muziki ndio ya kidunia ilhali ni muziki wao wa asili na wapo wanaoutumia kumsifu Mungu.Tatizo linabaki kwenye ku-kariri kuwa HYMS ndio nyimbo za MUNGU jambo ambalo si sahihi. Usijikimbie, kuikimbia asili yako na kutukuza isiyo sahihi. Na ninalosema hapa ni kwamba hata kama nyingi za nyimbo ulizosikia wewe za asili ni za kitamaduni na kutukuza miungui yao, haimaanishi kuwa ndivyo ilivyo. Kuna haja ya kuwa makini tunapochangia.
Kaka Bernard. Wasioamini wanapoburudika na yaimbwayo na wenye imani haimaanishi kuwa waimbaji ndio wana makosa. Wewe mwenyewe ulisema ulivyokuwa ukifurahia na kuburudishwa na nyimbo za ulyankulu na wakati huo hukuwa na imani. Mbona huwalaumu Ulyankulu kwa uimbaji uliokugusa wakati ukiwa si mlokole? Tuache mambo ya MY WAY OR NO WAY katika kutangaza injili. Asiyeamini ana haki ya kupenda ama kutopenda muziki na hilo halimfanyi muimbaji kuwa na makosa kama hakutoka katika njia sahii ya kumuimbia Mungu kum’burudisha asityeamini.
Kuhusu nyimbo za Ulyankulu, haimaanishi kwamba kwa kuwa hujui ama nami sijui mahadhi yake basi ni mahadhi ya dini. Na nashukuru umemalizia kwa kusema na hapa nanukuu (japo sina hakika na usahihi wa sentensi) “ASHAMED UPON US” Ni kweli kuwa shame upon all those who try to think and force things to be only their way. Kama kuna dhehebu lililojitahidi kutunza midundo ni wa-Katoliki lakini hata wao hawataweza kuwa na ujasiri wa kusimama na kusema kuwa nyimbo zao ndio midundo ya dini. Haijalishi mahadhi ya ulyankulu yalikuwa yapi, lakini kama yalikufaa haimaanishi kuwa ndio ya dini. Tuanche hii selfishness ya kudhani tuko sahihi na wengine wako wrong kwa kuwa tunajua tujuavyo hata kama tujuavyo si sahihi.
Steve M. Changamoto zako sijui zimelenga nini. Sijui ni kwa ajili ya kuonesha nini na sijui unaweza kudhihirisha vipi kuwa hao walioimba enzi hizo hawakutumia mahadhi yoyote ambayo sasa wapo wayatumiayo kwa muziki wa aina nyingine?
Umesema ngoma (drum) haijatajwa kwenye Biblia lakini hujaonesha palipoandikwa Blogs, Websites, Microphones na hata Tai na suti ambazo pengine wapenda kuvaa.
Kumbuka kuwa hasira hupunguza busara hivyo kama una hasira usiandike maoni
Pleasee


Amani kwenu,
BADO TUNACHANGANYA MADA HUO MZIKI WA ZAMANI UKIUFUATILIA KILA KITU KILICHOMO UTAGUNDUA AIDHA NI MCHANGANYIKO WA MIZIKI YA KISASA NA ILE YA ASILI NDIO MAANA UNAKUWA UNASHIDWA KUUWEKA KWENYE GROUP LOLOTE.
TAFADHALI BW, BERNARD ELEKEZA MOJA KWA MOJA NI AINA GANI YA MUZIKI WA INJILI UNAOTAKIWA UNAOPASWA KUIMBWA MAKANISANI,MAANA HATA MIZIKI YA DUNIA KUNA ZILIPENDWA NAHII UTASEMA INAOKOA. PLEASE BE SPECIFIC.


Asante sana wapendwa, Bw. Bubelwa Bandio na Bw. Pona. Hii ni changamoto kwenu na kwetu sote kama wa-Kristo kuhusiana na suala la miziki ya Injili.
Nadhani unapoona baadhi ya watu wakisema kuwa, kitu chako ni kizuri, lakini kina kasoro za hapa na pale na pale, kama ni mwenye busara utashukuru na kuchukua hatua za kurekebisha maeneo yanayodhaniwa au kusemwa kuwa na kasoro. Lakini kama utazidi kung`ang`ania tu na kusema kuwa, hakuna tatizo, hakuna tatizo, ni mtazamo tu wa kimadhehebu itakuwa siyo busara. Hapa mjue kuwa tunaochangia ni watu wa kutoka madhehebu mbalimbali, na kama ni hivyo ilikuwa ni wakati wenu mzuri wa kurekebisha kasoro zinazosemwa hapa, maana hapa tupo katika kuujenga mwili wa Kristo na wala si vinginevyo.
Ni ukweli usiopingika kuwa miziki ya kwaya ya nyakati hizi, hata mataifa wanatushangaa, kwamba ni kitu gani tunafanya. Sasa kama wapendwa wenzangu mnaona hakuna tatizo, basi muendelee kwani ukweli ndio huo.
Mtu anayepinga kuwa hakuna kuokoka duniani, tunajua wazi kuwa mtu huyo hajakutana na Yesu. Watu tuliookoka haitarajiwi kuwa tutapingana kuwa hakuna kuokoka duniani, kwa sababu tayari wote tumekutana na Yesu, yaani ametuokoa.
Tunapopingana juu ya swala hili la kwaya/miziki ya Injili juu ya namna ya uimbaji wakati wote tunasema kuwa tumeokolewa na Yesu, basi kuna kasoro kubwa katika wokovu wetu, katika hili inatubidi tuogope.
Bw. Bandio amesema mbona mimi nilisikiliza nyimbo za ulyankuru na nikaburudika wakati nilikuwa sijaokoka na je, niwalaumu Ulyankurlu? Kama utakuwa umesoma vizuri katika meseji yangu hapo juu, niliandika hivi; “Niwaeleze ndugu zangu,ni kwamba nyimbo za zamani hakuna mpagani aliyethubutu kuzisikiliza KAMA MUNGU HAKUMKUSUDIA. Kwa hiyo hapa ni Mungu mwenyewe kwa neema yake hakikuwa kitu cha kawaida. Kama mimi nilisikiliza nyimbo hizo ni Mungu tu alinikusudia. Nakumbuka wakati huo, waliokuwa wanasikia nyimbo zile nyumbani kwangu walikuwa wananiuliza iwapo ni mlokole! Kama mmepata kufuatilia moja ya maelezo yangu huko nyuma katika blog , mimi kabla ya wokovu nilikuwa na magonjwa. Hivyo katika kusikiliza nyimbo hizo ilikuwa ni sehemu ya kuona kama ningeweza kupata uponyaji. Ilikuwa si kitu cha kawaida kusikia nyimbo za mlokole kama hujaokoka.
Bw. Pona ameniambiwa niwe specific, ni mziki gani wa injili ninaoona unafaa. Kwa kifupi ni kwamba mziki wa injili unaofaa ni ule usio na makwazo wala maswali kwa wasikilizaji. Tunapoimba tuangalie pande zote, kwetu waimbaji na wasikilizaji, kwamba watakaposikiliza watatuchukuliaje. Kama hivi tunapoona wengine wanapinga juu ya uimbaji wetu, tujue kuwa tunazo kasoro katika uimbaji wetu. Kana ni wenye busara tutatafuta namna ya kurekebisha kasoro hizo, ili hata watu walio wa aina ya Bw. Bernard na Bw. Steve waridhike, huko ndiko kuboresha kazi ya Mungu! Najua hawataridhika wote, lakini angalau kile tunachokisikia kutoka kwa wapendwa walio wengi kama hivi , tukitilie maanani na kukifanyia kazi!
Wewe unataka nitaje specific kwamba ni aina mf. RAGAE ndiyo inayofaa! Hapana, hatuna specific lakini kutokuwa na specific, kusitufanye tuchukue aina ya ragae. Kwa nini tuchukue makombo ya shetani na kuanza kuyaboresha? Je, sisi hatuna Roho Mtakatifu wa kutuwezesha kubuni mtindo wa Mungu?.
Mimi binafsi niwaeleze ukweli leo, ni kwamba baadhi ya nyimbo za kwaya hata katika TV za Kikristo zikiimbwa tu, huwa nahama `station` siwezi kuzivumilia kuangalia!
BWANA WA AMANI ATUFUNIKE!
S H A L O M !


Kweli tuko watu wa aina nne.
Wenye kujua na wanajua kuwa wanajua
Wenye kujua lakini hawajui kuwa wanajua
Wenye kutojua na wanajua kuwa hawajui
na mbaya zaidi ni wale
Wenye kutojua na hawajui kuwa hawajui.
Narudia tena. Si lazima kuchangia kila mada kwa kuwa si kila mtu ana ujuzi na uelewa wa kila mada. Nyakati nyingine tunajishushia hadhi kwa kung’ang’ania kufafanua kile ambacho wanaokijua wanatambua kuwa hatujui.
Sijui tunakaririshwa huko tuendako, ama tunakaririshwa na hawa tunaoshirikiana nao ama ni elimu yetu ya kusoma Biblia kama kitabu cha Algebra kwamba kila 1+1=2 ama ni kuchanganya kukaririshwa na watu na elimu yetu ama kukosa vyote kunakosababisha haya.
Lakini ndhani tuwe makini katika kuchagua kipi cha kuchangia maana kuna mada ambazo nakubaliana na wapendwa humu kwa kuwa wanajua wanachosema na wanachangia kwa ufasaha, lakini unapokmkuta mpendwa huyohuyo kwenye mada nyingine akijitumbuatumbua unaweza kutilia shaka hata zile BARAKA ulizopata kwenye mada ambazo anazifahamu.
Ni ushauri tu na yeyote anaweza kuutumia kama kioo kujiangalia.
Amani Kwenu


Huu muziki wa kufokafoka (rap) nao unaweza kuwa wa dini?
Nimeweka hii clip katika blogu yangu na sijui nyie wataalamu wa mambo ya wokovu mna maoni gani. Kwa maoni yangu nadhani hiki ni kizazi kipya kinajaribu kujitambulisha na kumsifu Mungu. Tembelea link ifuatayo:
22. 

Baraka kwenu
Nadhani wakati mwingine kukubaliana na ukweli au halisi pia ni jambo la muhimu na linaweza kuondoa mlolongo mrefu wa mjadala, kuliko kuendelea na nadhalia ambazo zinakuwa hazina mwisho na hazileti suluhu katika jambo ambalo tunaliona ni tatizo wakati si tatizo kwa Mungu, isipokuwa ni tatizo letu.
kuwa na msimamo si jambo baya ila msimamo huo ukiwa umejengwa kwenye msingi ambao sio imara yaani kinyume na neno la Mungu huo msimamo ni batili.
Jambo lakuzingatia mara zote nipale tunapo kosoa jambo basi tuwe na njia mbadala, au kama jambo hilo ni dhambi kuwe na namana ya kumfanya mhusika atambue kwamba anamkosea Mungu ikwezekana atubu na sio kuhukumu kama baadhi yetu tunavyo fanya japo ukimwambia furani unahukumu hatukubali kwakuwa neno linamhukumu nae pia lakini ukichunguza kwa kina maelezo yaliyo tolewa utagundua yanalenga hukumu.
kama hatuwezi kuorodhesha aina gani ya miziki ya injili itumike makanisani.
basi miziki iliyopo Mungu ameiruhusu.kama sio tupate huo ufunuo wa ni aina gani ya miziki ya injili itumike makanisani.
MUNGU NI MWEMA SAAAAAAAAAAAAAAANA HUWEZI JUA
  

Asante Ndg Pona kwa maoni yako. Ni vema kutohukumu.
Na kwa yeyote anayeweza kunijibu hili na naamini tunajua kuwa TWASTAHILI KUSEMA KWELI NA KWELI HIYO NDIYO ITAKAYOTUWEKA HURU. Maswali yangu ni haya.
1:Je! nyimbo za wanamuziki kama Cosmas Chidumule, Remmy Ongala na hata Mzee Makassy si za injili na hazifai kutumika makanisani kwa kuwa tu walikuwa wakitumia mirindimo iendanayo na hii ya sasa walipokuwa hawajaokoka?
2:Je wasanii kama Beatrice Muhone, Bahati Bukuku, Rose Mhando, Kijitonyama na wengine wengi wanaoimba na kugusa watu sasa hazifai kwa kuwa tu zina mirindimo iendanayo na baadhi ya hiyo mnayoiita ya kidunia?
3:Kwani muziki asili yake wapi na muziki wa dini asili yake wapi?
Kaka Bernard umesema na hapa nakunukuu kuwa “Hapana, hatuna specific lakini kutokuwa na specific, kusitufanye tuchukue aina ya ragae. Kwa nini tuchukue makombo ya shetani na kuanza kuyaboresha? Je, sisi hatuna Roho Mtakatifu wa kutuwezesha kubuni mtindo wa Mungu?.” Ina maana unakubali kuwa hakuna muziki wa Injili lakini unasema kuwa kuna unayosikiliza na mingine unahama “station”. Sasa kama hakuna wa injili huoni kuwa wowote unaosikiliza ni wa kidunia?
Anyway, maswali mawili ya mwanzo ndiyo ya muhimu zaidi.
Baraka kwenu


wapendwa,
mnapoendelea na hii mijadala mkumbuke na kuzingatia maonya haya: “Lakini maswali ya upuuzi ujiepushe nayo,na nasaba,na magomvi, na mashidano ya sheria. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana. Mtu alie mzushi, baada ya kumuonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae, ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi, maana amejihukumu hatia yeye mwenyewe.” Tito 3:9-11.
“Ee Timotheo, ilinde hiyo amana, ujiepushe na maneno yasiyo ya dini, yasiyo na maana, na mashidano ya elimu, iitwayo elimu ya uongo..” 1 Tim. 6:20

  

Mch. Malisa, nimependezwa sana na kauli yako pamoja na hilo andiko. Blog hili nadhani kama ilivyo, iwe ya kuelimishana na kuonyana kadiri tuonavyo siku zile zinakaribia.
Maandiko yanatukumbusha juu ya kulihubiri Neno, kukemea, kuonyana kwa uvumilivu wote. Katika 2Timotheo 4:2 maandiko yanasema [lihubiri Neno, uwe tayari wakati ukufaao na wakati usiofaa, karipia kemea na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ILA KWA KUZIFUATA NIA ZAO WENYEWE, watajipatia walimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti, nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na watazigeukia hadithi za uwongo]. Pia pamoja na kuonyana, maandiko mengine yanatukumbusha kama alivyosema Mch Malisa kuwa tuyakatae maswali ya upumbavu yasiyo na elimu tukijua kuwa huzaa magonvi [2Timotheo 2:23], asante sana, na Mungu azidi kutusaidia tusiingie katika mitego hii.
Amen!


I knew this was coming. It’s what i say everyday that “THE WAY YOU SEE THE PROBLEM IS THE PROBLEM”.
Ok. Let it be “someone’s way” to be educative for you


Kwa kweli hii mada ina changamoto kubwa.
Nami natamani kuchangia kutokana na ambavyo ninalielewa suala hili la muziki huu unaoitwa wa injili.
Lakini kabla sijachangia, ninakuomba radhi ndugu Pona kwamba ninatamani sana kama swali ambalo dada Miriam Joseph aliuliza tarehe 6/03/2009 ungelijibu. Ninategemea kujifunza kitu kutokana na jibu utakalotoa. Lakini hii haimaanishi mchango wangu unategemea jinsi jibu la swali hili litakavyokuwa!
Swali lenyewe liko hivi:
“Ndugu Pona mfano unasikia muziki wako unapigwa Bar! Je unajisikiaje? mtu anakunywa kilevi huku akitikisa mguu na kichwa akijiburudisha na muziki wa Injili?”
Narudia tena kwamba ninakuomba msamaha ndugu Pona kama kwa namna yoyote ninaweza kuwa nimemkwaza kwa kuhitaji majibu ya swali hili. Lakini ninaamini katika kujibu kwako swali hili kunaweza kupatikana point muhimu sana katika kuliweka sawa jambo hili.
Nasubiri kwa hamu kusoma jibu la swali hilo.
Amani!


Amani kwenu
asante sana Bw.John Paul kwakukazia swali lililo ulizwa na dada Miriam Joseph swali lenyewe lina sema; Ndugu Pona mfano unasikia mziki wako unapigwa Bar ungejisikiaje? mtu anakunywa kilevi huku akitikisa mguu na kichwa akijiburudisha na muziki wa injili.
JIBU
Ningejisikia vizuri tu tena kawaida SAANA maana hata mimi sifahamu huyo mlevi baada ya kutoka hapo atatubu au hata tubu kama atakufa au hata kufa lakini ninacho fahamu akili yake inajua kwamba anakunywa kilevi huku anajiburudisha na muziki wa injili na hata Mungu anakuwa na taarifa hiyo wakati huo hata baada ya hapo,
Mimi mwenyewe sikuokoka kwasababu nilihubiliwa na wainjilisti, au wachungaji siku niliyookoka nilikuwa nimevuta mmea yaani nililewa lakini nilifanya maamuzi sahihi ambayo ni matokeo ya Pona wa leo. Hata hivyo sikutaka nijibu swali la huyo dada kwa sababu asilimia kubwa ya swali lake linataka majibu ya ku-assume na mimi siishi kwaku assume mimi niko REAL ndio maana nimetoa huo ushuhuda mfupi kwa ajili ya kuona jinsi gani wakati mwingine mipango ya Mungu inavyokuwa tofauti kabisa na mitazamo yetu.
SWALI LINGINE TAFADHALI
MBARIKIWE

Asante ndugu Pona kwa jibu lako. Mimi sina swali jingine bali hilo ndilo lilikuwa swali pekee. Na wala kwa kukuuliza hivyo sikuwa na maana ya kuanza mlolongo mwingine wa maswali na majibu.
Asante


ni muhimu kuangalia kwa makini na kwa undani kile Biblia inafundisha kuhusu uimbaji na muziki kwa jumla, msipofanya hivyo sioni jibu sahihi katika swali hili. mengi yaliyotolewa mpaka sasa ni maoni binafsi ya wachangiaji yakiwa na mafundisho kidogo toka kwenye Biblia.
Pona amejibu, nanyi mnasemaje?
  

Nimebarikiwa sana na jibu lako kaka Pona na hasa sentesi ya mwisho “…jinsi gani wakati mwingine mipango ya Mungu invyokuwa tofauti kabisa na mitazamo yetu.”
Mara nyingine nadhani huwa sisi wanadamu tena ambao Mungu ametusaidia kuijua kweli tunapenda sana kumpangia Mungu jambo la kufanya. Kama watu wanaokoka wakiwa “high” na mmea then hata Muziki wa Injili ukipigwa Bar kuna mtu kati ya wengi ambao Mungu amemkusudia kukutana naye!!
Sisi inatupasa kuifanya kazi ya Bwana na hata katika kumsifu inatupasa kumsifu katika roho na kweli na hayo mengine tumwachie yeye kuyashughulikia. Tusiwe kama Yona ambaye baada ya kuihubiria Ninawi na kuona Mungu ameghairi kuiangamiza yeye akachukia. Najua kuna watu wanatamani waimbaji fulani wa sifa wapigwe radi na Mungu wakiwa madhabahuni! Jamani Mungu hayuko hivyo!!
Barikiwa kaka Pona na Amani ya Bwana ikae nayi nyote!!


Nami naungana nanyi nyote kumshukuru Ndg Pona kwa jibu lako. Ni zaidi ya ushuhuda. Ni utimilisho wa mipango ya MUNGU na ni lazima tujue kuwa kwa namna yoyote ile itatimia. TUTAKE TUSITAKE.
Kwa Mch Malissa nafurahi kuona unaendelea kufuatilia mjadala huu. Ningependa kujua hilo ulilosema kuwa Biblia inafundisha juu ya uimbaji na muziki kwa ujumla.
Ndg Godlove nimependa saana maelezo yako hasa uliposema “tunapenda kumpangia Mungu jambo la kufanya”. Na huo kwangu ndio ukweli. Kuwa watu wanadhani kwa kuwa wameokoka kwa njia hii ama wamelelewa kwa imani na mafundisho haya basi ni hayo pekee yaliyo na nguvu za kumuokoa mwingine ama ni mwendo na namna hiyo pekee yenye wokovu.
Tunakimbia uwezo wa Mungu. Tunataka kuwa tutakavyo kwa namna tutakavyo na tuwezavyo ilhali Mungu anataka tuwe alivyopanga tuwe. Na ili hili litimie kuna njia mbalimbali. Tatizo ni kuwa wapo tunaoona maisha yao lakini si kamili na tunadhani ndiko walikoishia. Kujua kilichomsibu Ayubu bila kusoma hitimisho lake kutakufanya usitambue mpango wa Mungu kwake. Hivyohivyo tumeona watu wakiokokea magerezani na sehemu nyingine zijumuishazo wahalifu na wakitoka huko wanakuwa nuru halisi. Kama alivyosema ndg Pona kuwa aliokoka akiwa “high” na sasa ni Pona mwenye ushuhuda wa nguvu, unadhani aliokoka bila kuijua hiyo njia ya wokovu akiwa high? Ina maana kuna wakati ambao kuwafikia wenye uhitaji ni wakati muafaka wa kuyageyuza na kuyashuhudia maisha ya wengi ambao watabadilika na kuwa nuru ya jamii.
Kwangu muziki bado utaendelea kuwa wenye kumsifu MUNGU na usioenda nje ya maandiko kuiridhisha hadhira.
Aina na midundo wala si tatizo kwangu maana vyote vina asili.
Blessings



Nimesikitika nimekuta huu mjadala kama unaenda mwisho hivi, anyway na mimi nichangie hivohivo.
Nadhani wengi wa wakristo wa sasa tuna mapokeo ya zamani(ambayo yalikua mema wakati huo)lakini hayafaidii u-kiroho wa mtu leo. kabla hujazungumzia muziki wa injili lazima ujue muziki ni nini. Ni mada ndefu kidogo lakini kuzalishwa kokote kwa sauti kunaweza fanywa muziki(kulingana na mtumiaji anavyotaka). Genre(sijui nikiita aina napatia au vipi) inaweza tumiwa kwa injili bila matatizo mradi kinachozungumziwa ndani kiwe injili sababu hakuna aina maalum ya muziki ambao umekua certified(sijui na nani!)kua utumike kwa injili.hao ulyankulu waliotolewa mfano ni watumishi wazuri wa Mungu kwa uimbaji lakini pia wamepiga reggae,country,bosa nk.nyingi ya kwaya za zamani zilipiga hizihizi chakacha na aina zingine za muziki ambazo ungezisikia zikipigwa na bendi za kidunia lakini zikiwa zimeboreshwa. Cha msingi kwa muimbaji na wakristo kwa ujumla ni kujua UHODARI WAKO KISANAA peke yake, japo ni mzuri, haupelekei watu kuguswa maisha yao na Yesu unaemuimba kama maisha yako si safi lakini pia zaidi sana kama huna ufahamu wa unachokifanya! maana hata ibada ya sifa kwa makanisa mengi siku hizi ni ka-ratiba tu au ‘kutifua mioyo’kabla hajaja muhubiri ambayo si sahihi ndugu zangu! Muziki kama muziki hauna shida kabisa maana kwanza hutofautiana kulingana na tamaduni na mambo kama hayo. Kama ambavyo mbwembwe na uhodari wa kutunga hotuba wa muhubiri haubadilishi maisha ya mtu zaidi ya kumsisimua,vivyohivyo aina ya muziki haina tatizo ila hali ya rohoni na ufahamu wa mwanamuziki kwa anachokifanya ndo hupelekea mguso wa Mungu kwa watu,sio msisimko wapendwa. blesses
34. 

Shalom wapendwa,
Nimekuwa nikitafakari juu ya hii mijadala ya Neno la Mungu katika blog hii, nimegundua kuwa kila mtu anatamani mwingine aandike kila ambacho yeye anakiona kinafaa. Akiandika tofauti anaambiwa kuwa anamtizamo wa kibinafsi au wa kidhehebu.
Nadhami blog hii ni kwa ajili ya kufundishana kuelimishana na kubadilishana uzoefu wa kiimani. Iwapo mwingine atakuwa yupo kinyume na mwingine, yule aliye kinyume asilaumiwe na kuonekana kama hana ufahamu wa Neno la Mungu. Iwapo mwingine atakuwa na msimamo mkali juu ya kile anachokiamini, basi nayo yachukuliwe kuwa ni mafundisho kwa wengine wenye kuyapokea, kwamba kuna watu wa aina hiyo katika imani.
Iwapo tutataka kuwa kila mtu ajihadhali na msimamo wa wengine ili kwenda sambamba, hakuna tutakachokuwa tunajifunza hapa, sana sana tutakuwa tumebaki katika KUFARIJIANA.
Tuelezane ukweli, kila mtu aeleze kile anachokiamini kuhusiana na Neno la Mungu, ili mwenye kuamini kile kinachoelezwa akifuate, na asiyeamini asishutumu. Iwapo atataka kutoa hoja, atoe kwa uwazi bila kuingiza misemo, mafumbo na nahau!
Hili ni eneo la kuelimishana mambo ya rohoni, mambo ya kutufikisha mbinguni. Shetani hawezi kukaa mbali na maeneo kama haya, anaweza akamtumia mtu moja na wote wakajikuta wanakwazika kwa huyo, pasipokujua hata wao kuwa wamekwazika.
Hivyo wapendwa katika Kristo, tuliangalie sana hili. Maandiko yanasema mwenye hekima huvuta roho za watu [Mithali 11:30]. Tumwombe Mungu atupe ufahamu wa yepi ya kuandika na iwapo mwingine ataonekana ameandika tunayoona hayafai bado tujue ni sehemu ya kujifunza, tumtie moyo kwa upole na uvumilivu wote. Tusitoe lawama na kumwona kuwa anakengeuka, tutafute hekima ya kumweleza ili naye ajione anasehemu katika mchango wake.
Tukifanya hivyo, bila shaka mada katika blog hii zitakuwa haziishi kabisa, kila siku itakuwa ni mpya kwetu. Lawama zinawafanya wengine kuanza kuwa waoga, kuwa wasije wakachangia kitu ambacho kitawaudhi wengine na wakaonekana kuwa hawana ufahamu juu ya Neno la Mungu.
S H A L O M !
35. 

Asante saana King kwa maelezo mwanana. Nadhani hapo umedhihirisha kuwa hata watu wenye mtazamo mmoja wanaweza kuwa na maelezo yanayomaanisha kitu kimoja lakini kukawa na UBORA wa kuyafupisha na kuyaeleza. Naamini ulichosema umewakilisha asilimia mia moja ya niliyokuwa nayawaza.
Labda kwa kuongeza tu ndugu zanguni ni kuwa MUZIKI kwa maana ya midundo hauna tatizo. Ntatoa mfano wa kompyuta ambazo asilimia zaidi ya 50 ya search inahusisha masuala ya ngono (kwa mujibu wa taarifa) lakini wewe usomaye hapa umeamua kuingia na kuitumia ipasavyo kujijenga mna kujenga nyoyo za wengine kuelekea mbinguni. Vivyo hivyo na muziki. Muziki una upana mkubwa saaana. Ni “silaha” pekee inayotumika kotekote. Kwenye sherehe na huzuni, makanisani na clubs. Kwenye kukusanya watu kumsikiliza mtumishi wa Mungu na kinyume chake. Kwa hiyo kama ambavyo huwezi kusema kompyuta zote ni haramu kwa kuwa wengi wanazitumia visivyo, vivyo hivyo huwezi kusema hilo kwa muziki na hata wanamuziki.
Mimi napenda saana muziki wa asili na Reggae. Na hata katika blog yangu nimekuwa nikisindikiza mambo mengi kwa muziki huu. Na hata Jumapili pia nimekuwa nikiweka muziki wa mahadhi haya kusindikiza siku yangu hiyo. Na wiki iliyopita nilikuwa na “somo” toka Math 5:3-12 na hata kabla ya hapo nimeshakuwa na mengi kuhusu Mungu (japo waweza kutofautiana namna umuitavyo) lakini bado kuna watu wengi wanaofuatilia kila Jumapili na nisipoweka (kutokana na sababu mbalimbali) huwa napata emails kuuliza kulikoni.
Pengine wanaobisha kuhusu nguvu ya mahadhi hayo (kama ndugu Steve M ambaye KIMAKOSA alichambua miziki kulingana na mtazamo wake na si maudhui yake)wanaweza kusikiliza japo wimbo wa jumapili iliyopita ama wa Jumapili ijayo kisha wanieleze kama kuna kasoro ya kuimba muziki wa injili ama dini katika mahadhi ya reggae.
Bofya
 h


Ubarikiwe saana!! na wachangiaji wote.
37. 

Ninakubaliana na aliyoyaandika ndugu Bernad juu ya namna watu wengine wanavyoyachukulia baadhi ya maoni ya watu wengine kwa sababu tu yanatofautiana na ufahamu au mtazamo wa mtu huyo. Ni kweli hapa ni mahali pa kujifunza Neno la Mungu. Ninaamini kila mmoja [anayemwamini Yesu] ni mwanafunzi wa Bwana Yesu hapa, kwa hiyo lugha yetu inatakiwa kuwa ni ya amani, heshima, upendo na kuvumiliana. Mimi ninatambuwa kwamba tunaufahamu na ujuzi tofauti wa mambo mbali mbali , kama alivyoandika ndugu Mubelwa tarehe 7/3/2009. Kinachotuunganisha hapa ni Neno la Mungu tu. Hivyo mimi naona ni vema sana tunapochangia maoni hapa {mada hii na nyinginezo} TUZINGATIE sana Neno la Mungu linasemaje. Elimu za duniani ziko nyingi, imani mbali mbali ziko nyingi sana pia, bila kutazama Neno la Mungu linavyosema tunaweza tukajikuta tumepoteza mwelekeo na kuanza kufuata mawazo na mitazamo ya watu na mwisho wake tukajikuta tumepoteza kujifunza na kubaki TUNAFARIJIANA kutokana na makundi ya ki-mtazamo.
Tukifanikiwa kuwa na lugha ya upendo na kuthaminiana ni kweli kabisa mada zitakuwa haziishi. Kila siku zitakuwa ni mpya. Na ninaamini kadri tunavyoendelea kujadiliana kwa upendo ndipo vipengere vipya vitavyozidi kuibuka. Kuibuka kwa vipengere vipya kutafanya mada zizidi kueleweka zaidi. Kwa mfano mada hii inavyozidi kupanuka tunaweza kujikuta pande zote zimeelimika. Watu wanaosema muziki ni muziki tu wanaweza jikuta wameelewa kwamba kumbe kuna mipaka [kama ipo] na wale wanaosema kwamba muziki fulani una matatizo wanaweza nao wakajikuta wameelewa ni kwa vipi muziki peke yake unaweza usiwe tatizo. [kama ni ndivyo ilivyo]. Na wale ambao hawako upande wowote wakajikuta nao wameielewa kweli kwa kuchanganya maoni toka pande zote mbili. Na mwisho wa siku kila mtu akafurahia kwa kukutana na mjadala huu. Lakini katika yote dira yetu ni Neno la Mungu.
Huku nikizingatia kwa makini aliyoyaandika ndugu Bernad Mwenda na niliyoyaandika nami pia ninaomba kupata ufafanuzi wa mambo fulani ambayo yamejitokeza kutokana na uchambuzi aliouandika ndugu Mubelwa T. Bandio:
1. Ndugu Mubelwa umeandika kwamba MUZIKI kwa maana ya MIDUNDO hauna tatizo. Mimi naona kama vile unatafsiri nyingine ya MUZIKI ambayo maana yake ni tofauti na MIDUNDO. Maana hiyo ya muziki iliyotofauti na maana ya “Muziki kama MIDUNDO” labda ndipo panaweza kuwa pana Tatizo. Tafadhali fafanua hapa kidogo. [Katika kufafanua hili unaweza kujibu pia swali hili: Je, Muziki ni MIDUNDO?]
2. Pia ndugu Mubelwa umeandika jinsi muziki unaweza KUTUMIKA kwenye sherehe na huzuni, makanisani na clubs, kwenye kukusanya watu kumsikiliza mtumishi wa Mungu na kinyume chake. Natumaini kuna mengi ungeyaandika lakini umefupisha kwa sababu ya nafasi na muda pia.
Mimi nafikiri hapa pia pana swali muhimu lililojitokeza. Swali lenyewe ni kwamba:
a). Je, muziki uliotumika kwenye CLUBS ni huo huo unaweza kutumika KANISANI? au Muziki unaotumika kwenye SHEREHE ni huo huo unaweza kutumika kwenye HUZUNI?]
b). Kutokana na hoja kwamba muziki ni muziki tu tofauti ni maneno, nauliza Je, kubadilisha maneno peke yake kutoka katika muziki fulani uliotumika kwenye tukio moja kunaweza kuufanya muziki huo huo UFAE KIKAMILIFU kutumika kwenye tukio jingine lolote tofauti? [mfano kubadilisha MANENO peke yake kwa muziki uliotumika kwenye SHEREHE zilizojaa vifijo na nderemo kunaweza kuufanya muziki HUO HUO ukatumika kwenye HUZUNI palipojaa vilio na machozi?]
c). Baadaye ukaandika maneno haya:
“Kwa hiyo kama ambavyo huwezi kusema kompyuta zote ni haramu kwa kuwa wengi wanazitumia visivyo, vivyo hivyo huwezi kusema hilo kwa muziki na hata wanamuziki.”
Kama ulivyoandika hukukosea chochote mimi naona maneno yako haya yanakubaliana na maoni ya watu wanaosema kwamba kunatakiwa kufanyika umakini katika kuchagua aina gani ya muziki [kama swali lilivyouliza] utumike makanisani. Sijasoma popote ambapo kuna maoni kwamba muziki wote ni haramu au kwamba wanamuziki [natumaini unamaanisha wanaoimba habari za Neno la Mungu] wote wanafanya vibaya [ingawa inawezekana ikawepo sehemu iliyoandikwa hivyo]. Maana niliyoipata mimi ni kwamba muziki uchambuliwe na kupata aina inayofaa kutumika kanisani na wanamuziki nao wajichunguze na kujipima na Neno la Mungu ili wasiweze kulaumiwa kwa aina yoyote [iliyo kinyume na mwenendo wa waaminio] katika utumishi wao. Kama ilivyoandikwa katika 2Korintho 6:3-10.
Natumaini tunavyoendelea kujadili hapa tunaweza kufikia mahali ambapo tunaweza kupata [kama vipo] VIGEZO vya kuzingatia juu ya AINA GANI YA MUZIKI UNAOFAA KUIMBWA MAKANISANI.
Tuendelee kujifunza!
38. 

Suala la uimbaji na aina ya muziki katika makanisa ni changamoto kwetu sote tuliokombolewa na Kristo. Kanisa limevamiwa na mamluki wa muziki wa injili. Kama ilivyo kawaida yake Lucifer amejigeuza kama malaika wa nuru katika eneo hili la muziki kanisani.
Nitaelezea baadae ninacho maanisha, lakini kwanza nataka tuangalie “neno” linasemaje kuhusu muziki na injili.
Muziki katika Biblia umegawanyika katika maeneo yafuatayo:
• Uimbaji kwa sauti tu bila vyombo ( Vocal Praise) Tunasoma katika Kut. 15:1-18, Waamuzi 5:1-, Mat. 26:30. Kuna vifungu vingi lakini hivi vinatosha , unaweza kusoma vifungu zaidi wewe mwenyewe.
• Uimbaji pamoja na ala (Instrumental Praise) aina hii ya uimbaji ilikuwa ya kawaida sana haswa katika Agano la Kale, tunasoma katika Kut. 15:20-21, 1 Sam.10:5, pia katika Agano Jipya kwa kiasi kama Ufu. 5:8-9, etc.
• Uimbaji wakati wa furaha au huzuni . Kwenye huzuni Mat.9:23, 1 Sam.16:15, kwenye furaha Muhubiri 2:8, n.k.
Mwanzoni kabisa mwa uumbaji tunaona suala la uimbaji kwa kutumia vyombo katika maisha ya kawaida ya wanadamu linatajwa katika Mwa. 4:21, huyu Yubali hakutumia vyombo hivi kumsifu Mungu kwani wakati huo tayari uasi ulikuwa mwingi.
Mungu Baba alipowaumba malaika mmoja wao aliitwa Lucifer ambae baada ya kuasi anajulikana kama shetani. Mungu aliweka ndani yake karama ya uimbaji na muziki kama tunavyosoma katika Ezekieli 28:13-15. Lucifer alipoasi aliamua kuharibu kila kitu chema alichokifanya Mungu Baba ikiwa ni pamoja na muziki. Kwa hiyo ni sahihi kabisa kusema kuwa leo hii kuna muziki wa kiroho na wa kidunia, kama vile kulivyo na mambo ya kiroho na ya kidunia. Kila alieokolewa na Kristo ni muhimu tena ni lazima kutambua tofauti hii.
Utatambuaje tofauti katika ya muziki wa kiroho na wakidunia? Nadhani hili ndio swali kubwa hapa. Wengine wameona tofauti ni maneno tu, yaani kama maneno ni ya kimungu haijalishi mudundo ni wa namna gani, kwao huo ni muziki wa kiroho (injili), wengine wameona ni lazima hata mdundo nao ufanane kiroho. Hili linawachanganya wengi kwa sababu hakuna mahali po pote kwenye Biblia pana sema mdundo wa aina Fulani ndio unaokubalika mbele za Mungu. Kwa sababu ni kweli kuwa shetani amechafua hata uimbaji, ni lazima kuwa na tahadhari katika aina ya muziki wa injili.
Ukisoma neno kwa makini, utaona kuwa watoto wa Mungu hawapaswi kuenenda kama watu wa dunia katika maeneo yote ya maisha yao, na je! Sio zaidi sana katika eneo la kumsifu na kumwabudu Mungu kwa uimbaji wetu? Warumi 12:2 “Wala msiifuatishe namna ya dunia hii, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu…”
Mt. Paulo anasema, “Lakini sisi hatukupokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.” 1 kor. 2:12.
Tujihadhari tusiilete dunia kanisani, bali tulipeleke kanisa duniani mwote!
Tatizo la muziki wa injili ni pana zaidi ya aina ya muziki wenyewe. Leo imekuwa ni kawaida kuona waimbaji “nyota wa injili” wakidai kulipwa mamilioni ili kuimba, hivi sasa kuna biashara kubwa ya nyimbo za injili. Waimbaji hawa wa injili huwezi kuwapata mpaka uwasiliane na mameneja wao!!!! Hivi sasa mkazo mkubwa katika nyimbo za injili ni katika uwezo wa mwimbaji kunen’gua na kutawala jukwaa. Mambo ya ajabu kabisa haya! Hakuna tena tofauti kati ya Twanga Pepeta, Msondo Ngoma na hao waimbaji wa muziki wa injili. Ndio maana hata kampuni za Pombe zinawapa waimbaji wa injili tuzo za uimbaji bora, nasisi tumebaki kuulizana upi ndio muziki sahihi wa injili!
Sio waimbaji wote wa injili wako kama nilivyoeleza hapo juu, na kiri kuwa kuna wachache, tena wachache sana, wanaomwimbia Mungu wao katika roho na kweli ,na hawa wazidi kubarikiwa ili kutenganisha nuru na giza. Bwana Yesu asifiwe!
Hivi kanisa lisipoamka sasa, litaamka lini? Hivi waliookoka wasipoamka sasa wataamka lini? Shetani haji kushambulia kanisa akiwa amevaa pembe kichwani na moto ukimtoka mdomoni, bali huja kama malaika wa nuru.
39. 

Kwako ndugu king,
Wakati tukiendelea kutafakari ujumbe aliouandika hapa Mchungaji Malisa naomba kurejea kwenye mchango wako uliouandika tarehe 17/3/2009. Katika mchango wako huo uliandika maneno haya:
“Nadhani wengi wa wakristo wa sasa tuna mapokeo ya zamani(ambayo yalikua mema wakati huo)lakini hayafaidii u-kiroho wa mtu leo.”
Kutokana na maneno haya mimi nimepata tafsiri kwamba kwa upande wako u-kiroho wa mtu wa leo ni tofauti na u-kiroho wa mtu wa jana (wakati uliopita). Kwamba u-kiroho unabadilika kutokana na wakati! Au kwa kufupisha ni kwamba wokovu wa ZAMANI ni tofauti na wokovu wa SASA.
Kama maana yako ni hiyo ninaomba ufafanue zaidi suala hili katika Mada ya Swali kuhusu Wokovu wa Zamani na wa sasa ya terehe 27/1/2009. Lakini kama ni kwa sababu sijakuelewa unaweza kufafanua hapa hapa.
Tukirudi kwenye suala letu la aina gani ya muziki, umeandika pia maneno haya:
“hao ulyankulu waliotolewa mfano ni watumishi wazuri wa Mungu kwa uimbaji lakini pia wamepiga reggae,country,bosa nk.nyingi ya kwaya za zamani zilipiga hizihizi chakacha na aina zingine za muziki ambazo ungezisikia zikipigwa na bendi za kidunia lakini zikiwa zimeboreshwa.”
…kwamba Ulyankulu walipiga reggae na aina zingine za muziki lakini pia bendi za kidunia zikapiga aina hizo hizo za muziki. Lakini ili zikubalike kwa wasikilizaji wake bendi za kidunia inabidi ZIBORESHE aina hiyo ya miziki. [kutokana na ulivyoandika wewe].
Changamoto iliyoko hapa ni kwamba UBORESHAJI huu wa muziki unaofanywa na bendi za kidunia ndiyo unaotofautisha vionjo vya muziki.
Mimi naona hapa tunaweza kuwa tumepata kigezo kimoja kwamba UTOFAUTI WA UBORESHWAJI WA AINA YA MUZIKI KUNAWEZA KUFANYA MUZIKI HUO UFAE KUTUMIKA KATIKA MAZINGIRA TOFAUTI. Kwamba ‘Genre’ fulani ikipigwa kinamna fulani inaweza kufaa kutumika kanisani lakini isifae kwenye Clubs na aina hiyo hiyo ya genre ikipigwa kwa namna fulani kwenye Clubs inaweza isifae kutumika kanisani!
Ndugu king wewe unaonaje kuhusu hili?
40. 

Ubarikiwe sana mtumishi wa Mungu Dkt Malisa, mimi kama mimi ninakubaliana kabisa na maelezo yote uliyoyatoa. Hali kwa kweli ndivyo ilivyo.
Hata hivyo kwa wapendwa wote, naomba mwenye kufahamu maana halisi ya andiko la Wakolosai 3:15 atusaidie, nalo linalosema “Na AMANI ya Kristo iamue mioyoni mwenu”.
Ninaomba msaada huo kwa sababu mara nyinyi andiko hili, limekuwa likitumika na wapendwa wengi kuelezea kuwa amani ya Kristo ndicho kipimo chetu cha kuamua mambo, na ndivyo ilivyo. Ninaomba nifafanuliwe kwa sababu nashindwa kuelewa kwa nini tunatofautiana wakati Kristo ni moja? Katika jambo hilo hilo moja, wengine wanasema wanayo AMANI kulifanya na wengine wanasema hawana AMANI kulifanya, kwa nini?
Mwenye ufahamu atufafanulie kwa upole, unyenyekevu na uvumilivu wote, maana halisi ya neno AMANI kama Kristo alivyokusudia.
S H A L O M !
41. 

Amani, Heshima na Upendo kwenu nyote. Kwanza nikubaliane na Ndg Bernard katika kile alichoandika kuhusu michango ya wapendwa humu. Lakini kuna haja ya kujiuliza kinachowafanya hao wachangiaji wamcharukie mtu. Hapa ni vema kutoa maoni kulingana na mada na kama unapinga ama la, lakini si kuwaita uwapingao wapuuzi maana huna ushahidi wowote kuwa uaminivyo ndio sahihi. Kwa hiyo ni vema kutambua kuwa CHANZO CHA TATIZO NDILO TATIZO. Pengine hayo yasiposemwa ama mtu akijitahidi kutetea upande wake na si kudhalilisha ama kuponda upande mwingine na kuukashifu tutaendelea kuelimishana tuu.
Kwako Kaka John nashukuru kwa uchangiaji wako na pia maswali yako nami nitayajibu kama ifuatavyo.
1: Muziki una tafsiri nyingi na pana kulingana na jamii, lakini kwa namna yoyote ile UNAANGUKIA KWENYE TAFSIRI YA KUWA MPANGILIO WA SAUTI. Kwa maana hiyo kila midundo iliyopangiliwa ni muziki japo si kila muziki una midundo.
2: Maswali ya pili ntayajibu kama ifuatavyo. Unless unataka kupinga kuwa muziki hautumiki huko nilikosema, mimi nasema kuwa muziki katika matukio unaendana na mahadhi kulingana na mazingira. Na hili naamini unalijua vema. Tatizo nilionalo hapa ni kuwa wakati wengine tunazungumzia muziki wa injili ki-ulimwengu wapo wanaozungumzia muziki ndani ya mkoa kama si nchi. Na unajua kuwa bolingo waweza kuwa muziki wa asili huko Kongo na usiwe na tatizo kutumika kanisani wakati nyumbani wanautumia kwenye clubs. Sasa je unadhani hapo “mtego” ama “fumbo” liko wapi? Ama wakati wapo ambao wanadhani Reggae ni muziki wa ki-rasta ilhali si ijulikanavyo huko visiwani unadhani kuna mkanganyiko na mchanganyiko gani hapo?
Maswali haya ninayotaka ujiulize ndio majibu ya swali la pili kuwa ukiangalia muziki wa injili kwa nchi ama jimbo ama wilaya ama mkoa fulani inaweza kuwa na maana kuliko kuongelea muziki kidunia. Na mara zote tumekuwa tukitofautiana katika mambo mengi kiimani kwa kuwa wapo wanaoamini kuwa namna dini inavyoaminiwa na kuabudiwa Tanzania ndio njia pekee na sahihi jambo ambalo sina hakika nalo na ndio maana sijawahi kukubaliana nalo.
Kwa hiyo naomba nawe ujitahidi kufafanua maswali hayo katika dhana ya ki-dunia na si ki-Tanzania na hapo tutaendelea kuelimishana.
Kama kuna swali sijajibu na ama unapenda kuuliza basi kuwa huru kufanya hivyo.
Kwa upande wa Mch Malisa nashukuru kwa maelezo yako. Lakini pia nina maswali maana licha ya kunukuu Biblia juu ya kile inachosema kuhusu aina za muziki bado hujajibu swali lililoulizwa na ambalo hata wewe umelizungumza kwenye aya yako uliposema “Utatambuaje tofauti katika ya muziki wa kiroho na wakidunia? Nadhani hili ndio swali kubwa hapa. Wengine wameona tofauti ni maneno tu, yaani kama maneno ni ya kimungu haijalishi mudundo ni wa namna gani, kwao huo ni muziki wa kiroho (injili), wengine wameona ni lazima hata mdundo nao ufanane kiroho. Hili linawachanganya wengi kwa sababu hakuna mahali po pote kwenye Biblia pana sema mdundo wa aina Fulani ndio unaokubalika mbele za Mungu. Kwa sababu ni kweli kuwa shetani amechafua hata uimbaji, ni lazima kuwa na tahadhari katika aina ya muziki wa injili.”
Kwa hiyo licha ya maelezo mazuri ya aina za muziki kwa mujibu wa Biblia na historia ya Lucifer na alichokimbia nacho, bado swali la ndg Godlove halijajibiwa katika maelezo yako. Unapingana na sisi tusemao kuimba kwa roho na kweli bila kujali midundo lakini husemi sasa MIDUNDO GANI AMBAYO IKIENDANA NA UIMBAJI WA ROHO NA KWELI ITAKUWA YA KIDINI.
Na pengine niulize kama unadhani waimbaji kuwa na mameneja ni kosa. Maana natambua kuwa kama wewe ni Mchungaji mwenye kanisa lenye watu na thamani kubwa unahitaji UONGOZI na kadri linavyozidi kukua ndivyo linavyohitaji watu mbalimbali kuanzia mtunza hazina, mwongoza muziki, anayeshughulikia kupiga picha za video, ku-edit na hata kurusha matangazo kama kanisa linafikia wakati wa kupeleka huduma ulimwenguni kote. Na hapo ndipo utakapoanza kuhitaji mtu wa kushughulikia transmission zako katika Tv mbalimbali na hata safari zako. Unadhani hapo utakuwa si mtumishi kwa kuwa uko ORGANIZED na WELL MANAGED?
Unaonaje juu ya hili?
Kwa kumalizia na kwa masikitiko niseme kuwa nimefuatilia mijadala kadhaa humu na kilichoonenaka ni kuwa baadhi ya watu wanapoulizwa maswali mengi na ya undani zaidi na kisha kuonekana kutokuwa na uhakika ama uwezo wa kuyatetea vema wanakuja na nukuu za kwenye Biblia zinazozungumzia juu ya kuwa makini na mabishano na kujichunga na wasioamini. Hiyo ni dhana mbaya ambayo inataka kuifanya dini kuwa ya vitisho kila unapotaka kujua kitu kwa ufasaha zaidi. Nadhani hili ni la kuacha pia maana kuna haja ya kuwa wakweli pale tusipojua tunachotetea na inapobidi basi kutojiingiza katika mijadala ambayo huna ufahamu nayo .
Mwisho kabisa niseme kuwa kuna maswali yangu ambayo nyote mmeamua kutoyajibu na ningefurahi kama nayo yangejibiwa na kwa kufanya hivyo nayaweka hapa kuyakumbusha nikiamini kuwa kama msemacho ndicho muaminicho, mtakuwa huru kuusimamia huo ukweli. Nauliza hivi
1:Je! nyimbo za wanamuziki kama Cosmas Chidumule, Remmy Ongala na hata Mzee Makassy si za injili na hazifai kutumika makanisani kwa kuwa tu walikuwa wakitumia mirindimo iendanayo na hii ya sasa walipokuwa hawajaokoka?
2:Je wasanii kama Beatrice Muhone, Bahati Bukuku, Rose Mhando, Kijitonyama na wengine wengi wanaoimba na kugusa watu sasa hazifai kwa kuwa tu zina mirindimo iendanayo na baadhi ya hiyo mnayoiita ya kidunia?
3:Kwani muziki asili yake wapi na muziki wa dini asili yake wapi?
BARAKA KWENU
42. 

Ndugu Mubelwa, tuko pamoja!
Jambo moja ambalo nafikiri ni kwamba hapa HATUPINGANI bali tunajifunza Neno la Mungu. [Kupingana kutokana na kitu mtu anachokiamini hakutatufaidia kitu bali kila mtu kujipima na Neno la Mungu. Kuamini kitu fulani, hata kama ni kizuri namna gani kibinaadamu, kama kitu hicho ni tofauti na lisemavyo na kuonya Neno la Mungu basi kuamini huko ni bure]. Nimeshaandika jinsi ambavyo tunatakiwa kufanya hivi kwa lugha ya amani na upendo na heshima. Kama huyu anaamini hivi na mwingine anaamini tofauti TUNATAKIWA KULIANGALIA NENO LA MUNGU LINAVYOSEMA JUU YA JAMBO HILO na mwishoni ukweli kujulikana ili kwamba ANAYEKUBALI UKWELI aamuwe kuufuata na yule ambaye BADO ANASHIKILIA ANACHOKIAMINI, hata kama BIBLIA IMEWEKA WAZI UKWELI WAKE, aendelee kuamini kinyume na Neno la Mungu. [Hili ndilo aliloandika Mch. Malisa tarehe 12/3/2009 kwamba ni lazima tuangalie linavyosema Neno, naye tayari ameshaanza kuleta mafundisho haya kwa kuweka vipengere vya Biblia vinavyohusiana na jambo hilo]. Lakini NAAMINI lengo la mijadala hii ni kwamba YULE ASIYEIFAHAMU KWELI YA NENO LA MUNGU aifahamu na KUIFUATA ili awe mfuasi mkamilifu wa Yesu Kristo aliye katika safari ya kwenda Mbinguni.
Tuendelee kujadili:
Mimi najibu sehemu yangu na wengine uliowajumuisha hapa kila mtu ataandika kwa wakati wake.
Kutokana na tafsiri ya muziki uliyoiweka hapa kwamba ” kila midundo iliyopangiliwa ni muziki japo si kila muziki una midundo” naomba kuuliza tena kwamba:
1. Kutokana na ukweli kwamba muziki huwa unatengenezwa kwa kujumuisha milio mbali mbali zikiwemo ngoma, magitaa, vifaa vya kupuliza na vifaa vingine vyenye milio mbali mbali. Je, kwako wewe MIDUNDO inamaanisha nini katika mchanganuo wa muziki?
2: Swali la pili bado sijapata jibu, inawezekana hatukuelewana. Ulichofanya ni kufafanua ulichoandika mwanzo. kwa ufupi umeandika hivi” mimi nasema kuwa muziki katika matukio unaendana na mahadhi kulingana na mazingira.” Hiki ndicho ulichoandika kwamba muziki hutumika kwenye sherehe, kanisani, kwenye clubs, kwenye huzuni nk.
Mambo haya uliyoyaandika yanatokea duniani kote. Si Tanzania tu na wala si Kenya tu. Kongo, ulikotolea mfano nako kuna huzuni, sherehe, kanisa, clubs nk. Ninaamini hata huko Kongo wana nyimbo ambazo hutumika kwenye huzuni, sherehe, clubs nk.
Hata hivyo Bolingo ni ‘Mtindo wa muziki’ na si aina ya muziki kwa maana ya ‘Style’ kama Salsa, Waltz, Disco, March nk. [Kama nimekosea nisahihishe!]
Kwa kutumia mfano wa Bolingo ulioutoa naomba tena kuuliza swali la pili nililoliuliza kwamba:
Bolingo iliyotumika kwenye sherehe ikiimbiwa wimbo wa vifijo na nderemo, Bolingo hiyo hiyo IKIWEKEWA MANENO YA HUZUNI (bila kubadilisha kitu kingine chochote, maneno peke yake) inaweza kufanya Bolingo hiyo hiyo itumike kwenye mazingira ya huzuni?
Hata hivyo mimi natoa mchango wangu hapa kwa kuzingatia WOKOVU na Ukristo kwa ujumla. Sitowi maoni kwa kuzingatia utaifa, u-bara au utamaduni fulani!
3. Suala la tatu ni vema kwa kuwa umesema HUNA UHAKIKA nalo. Umezungumzia jinsi watu wanavyoabudu DINI Tanzania wakifikiri ndiyo ilivyo duniani kote.
Napenda kuweka wazi kwamba Ukishaingia kwenye masuala ya DINI lazima kuwe na utofauti. Na ninawapa pole watu WANAOABUDU DINI. Kuabudu DINI kunaweza kutofautiana lakini KUMWABUDU MUNGU ALIYE HAI, JEHOVA ni kule kule Duniani kote. Kwa maana MUNGU NI ROHO nao WAMWABUDUO imewapasa kumwabudu katika ROHO na KWELI.[Yohana 4:24]. Huu ni ujumbe kwa wanadamu wote ulimwenguni!
Neno la Mungu ndilo KIONGOZI wetu. Bila kuzingatia hili tunaweza kujikuta tunatofautiana katika mambo mengi kwa kuwa tu kumbe kuna wengine wanaweza kuwa wanachangia hoja hapa kwa kuzingatia mazingira wanayoishi, au kutokana na imani zao za dini, au kwamba wako nchi masikini, au labda nchi tajiri, au kwa sababu ya mila ya nchi fulani au kwa sababu ya utajiri alionao mtu binafsi. Bila kulitambuwa tatizo hili HATUWEZI KUFIKIA KUNIA MAMOJA kama Biblia inavyotufundisha. Yesu ni mmoja, Wokovu ni mmoja na Roho ni mmoja.[Efeso 4:4-6] Kwa hiyo sisi tunaomwamini na kumfuata Yesu MWELEKEO WETU unatakiwa kuwa mmoja. Ikija HATARI kila mtu aitambuwa kuwa ile ni HATARI. Likija jambo jema kila mtu atambuwa kwamba lile ni JAMBO JEMA. Bila kuufikia umoja huu katika Roho Hatari itakuja, wengine wakaiona kuwa ni hatari wakajiepusha nayo lakini wengine wakaiona kama ni jambo jema na hatimaye wakaangamia.
Kunapokuwa na utofauti wa mitazamo juu ya jambo fulani la Ki-Mungu SABABU ya tofauti hiyo ni SISI BINAADAMU na wala si NENO LA MUNGU. Ili kuondoa tofauti hizi ndiyo maana tunafundishana hapa tukionyana na kushauriana, kwa kuzingatia Neno la Mungu, ili tuweze KUUFIKIA UMOJA wa ROHO na msimamo wetu KINYUME na ADUI WA ROHO ZETU WOTE,[Ibilisi] uwe ni MMOJA bila kujali nchi atokayo mtu au tamaduni fulani au aina hali yoyote inayotofautisha watu wa jamii moja na nyingine!
4. Maswali yako uliyomalizia sijuwi sana kama yananihusu na mimi pia. Maana mimi bado sijasema lolote juu ya muziki wa injili au muziki wa kidunia na wa kiroho. Nilichoanza nacho ni kuwekana wazi kwanza juu ya ufahamu wa MUZIKI. Tukishapata vipengere fulani muhimu ndipo nitahitimisha. Kwa hiyo maswali yako hayo sitayajibu sasa hadi hapo nitakapokuwa tayari kufanya hivyo, lakini natumaini mtu yeyote mwenye majibu anaweza kuyajibu.
Lakini naomba kuuliza swali moja kwamba kwa kusema ‘MIRINDIMO’ una maana ni MIDUNDO au ni nini tena? nisaidie hapa tafadhali!
43. 

Wapendwa wachangiaji,
Bwana Yesu asifiwe,
kabla ya kujibu maswali niliyoulizwa, naomba kuambatanisha hapa article inayoelezea jinsi muziki wa kishetani ulivyopenya katika jumuia na hata kanisani. katika makala yangu hapo juu nilionyesha kuwa kuna muziki wa kiroho na wakidunia. Makala hii ni nzito hivyo inahitaji ukomavu katika kuisoma na kuielewa. Sisi tutaendelea kuulizana muziki upi unafaa, lakini shetani yeye yuko busy already!!!!
THE SATANIC ROOTS OF ROCK:
Today, at almost any “heavy-metal” rock concert one can hear the audience being exhorted to rape and murder in the name of Satan. Lyrics such as the following are typical:
“We come bursting through your bodies
Rape your helpless soul
Transform you into a creature
Merciless and cold
We force you to kill your brother
Eat his blood and brain
Shredding flesh and sucking bone
Till everyone’s insane
We are pestilent and contaminate
The world Demonic legions prevail”
Any loving parent today would be horrified and shocked to learn that their sons and daughters are eagerly listening to such evil. Perhaps though, some may think privately, “If only we could return to the ‘good old days,’ with the music of the Beatles.” Little do most people suspect that it was with those innocent-looking Beatles, that most of the trouble started.
Modern electronic-rock music, inaugurated in the early 1960s, is, and always has been, a joint enterprise of British military intelligence and Satanic cults. On the one side, the Satanists control the major rock groups through drugs, sex, threats of violence, and even murder. On the otherside, publicity, tours, and recordings are financed by record companies connected to British military intelligence circles. Both sides are intimately entwined with the biggest business in the world, the international drug trade.
The so-called “rock stars” are pathetic puppets caught in a much larger scheme. From the moment they receive their first recording royalties, the groups are heavily immersed in drugs. For example, much-admired “stars” such as John Lennon of the Beatles and Keith Richard of the Rolling Stones, were heroin addicts. Richard had to obtain blood transfusions, replacing his entire heroin-laced blood supply, in order to get a visa to enter the United States.
The “rock stars” are also totally artificial media creations. Their public image, as well as their music, is fabricated from behind the scenes by controllers. For example, when the Beatles first arrived in the United States in 1964, they were mobbed at the airport by hundreds of screaming teenage girls. The national press immediately announced that “Beatlemania” had besieged the U.S.A. But the girls had all been transported from a girl’s school in the Bronx, and paid for their screaming performance by the Beatles’ promoters.
The money of the 1960s rock groups, which in somes cases mounted to hundreds of millions of dollars, was also totally under the control of mob-connected promoters. From 1963 to 1970, the Rolling Stones made over $200 million, yet the group’s members were all nearly bankrupt. None of them had any idea of where their money went.
Between 1963 and 1964 the Beatles and the Rolling Stones laid siege to Western European and American culture. This two-pronged invasion from England was well-planned and well-timed. America had just suffered the shock of the assassination of President John Kennedy, while in the streets the mass-based civil rights movement had just held a Washington, D.C. rally, led by Martin Luther King, of 500,000 people. The rock counterculture would be used as a weapon to destroy such political movements.
Later in 1968 and 1969, years which saw a mass strike of students and workers in the United States and Europe, huge, open-air rock concerts were used to head off the growing discontent of the population. The rock concerts were devised as a means for mass recruitment to the drug-saturated, free-sex counterculture. For the millions who came to these concerts, thousands of tablets of the hallucinogenic drug, LSD, were made freely avaliable. These drugs were secretly placed in drinks such as Coca-Cola, turning thousands of unsuspecting victims into raving psychotics. Many committed suicide.
Less than a half century ago, our young children studied violin and piano, learning about the great classical composers such as Bach, Mozart, and Beethoven. As will be shown, the same record companies who today promote Satanic “heavy-metal” rock have run covert operations to destroy the musical heritage of these great classical composers.
For the past thirty years, Western society has been under the gun of a deliberate plan of cultural warfare, with the purpose of eliminating Judeo-Christian civilization as we know it. These plans must not succeed. So that the reader can better combat this evil, we’ll go back nearly thirty years, when those four innocent lads from Liverpool, England, the Beatles, were just starting out.
44. 
AMIN NGULUMA
Nimefurahi kuwa mjadala huu umerudishwa tena baada ya kusimamishwa miezi kadhaa iliyopita. Sijui ni kwa sababu niliuliza.
Hata hivyo napenda kuweka sawa hoja ya ndugu yangu mpendwa Fred juu ya kile anachoona kuwa USA ndio kiini cha kazi ya Mungu kuuzwa(Hapa namaanisha nyimbo na mahubiri ya injili)
Inavyoonekana bado tupo katika hatua ya chini kabisa katika kuifikia kweli ya Injili ya Kristo Yesu katika mambo kadhaa na ya kuwa karibu wengi tumefungwa na mipaka ya mafundisho na theolojia za madhehebu yetu.
Hata hivyo ndugu yangu Fred naomba utambue kuwa uimbaji wa nyimbo za injili si huduma ya kuokolea bali ni sehemu ya ibada kwa mkristo awaye yote. Unaweza kujifunza kwa kuangalia namna mwinjilisti Luka alivyoandika akionyesha hatua mbali mbali kabla ya mateso ya Yesu,na wakati wanafunzi wa Yesu wakisubiri ahadi ya Baba. Mara zote walikuwa akielezea kuwa waliimba(wakiwa bustanini,na siku zote walizokuwa wakidumu katika kumngojea Roho mtakatifu)-Soma kwa makini injili ya Luka na Matendo ya mitume.
Lakini kanisa limekuwa likitumia nyimbo katika ibada zake karibu karne zote za uhai wake na baadaye kuziweka nyimbo hizi katika vitabu mbali mbali za nyimbo kama vile (Hapa nitataja vitabu vya kiswahili) Nyimbo za dini,Tenzi za Rohoni,Nyimbo za wokovu,Nyimbo za kikristo n.k. vitabu hivi vinauzwa havitolewi bure. Teknolojia ya kutunza nyimbo kwa njia ya sauti yaani VHS,DVD na VCD inaelekea kuchukua nafasi ya vitabu katika karne hii.
Ndugu yangu Fredi je vitabu vya nyimbo ama hata Biblia inatolewa bure? na kama vinauzwa unasemaje sasa.
Je udhambi wa kuuza kanda za nyimbo za injili unazaliwa wapi endapo Biblia ambalo ndicho kitabu mama cha kikristo kinauzwa?
Tuache kuingiza cults kwenye imani ya kikristo tutaelekea kubaya.
Niendelee kuwashukuru ndugu wote ambao mmetia mioyo yenu katika kuelimisha kanisa la Mungu
AMANI IWE KWENU NYOTE.
45. 

Mumebarikiwa kujua yote hata hamhitaji mtu awafundishe kumjua Mungu.
Ndugu zangu naomba niwafahamisha kwamba mjadala huu haujaleta amani rohoni na ikiwa tunashindwa kutambua kwamba adui amekwishaingia hapa basi upofu umekwishashika mizizi.
Mti wa mema na mabaya huleta kifo na ndicho kinachoendelea hapa.Tukumbuke kwamba hata kama unaeleza ukweli na taarifa sahihi LAKINI kukawa hakuna amani juu ya unachosema basi kuna tatizo.Na ndicho ninachopata katika mjadala huu.
Maelezo yote haya yanayotolewa kimsingi yanapaswa kuzungumzia jinsi ya KUMWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI.Ikiwa tumeona kwamba huu ndio moyo wenyewe basi tungekuwa tumepiga hatua na kujua nini hasa kinapaswa kufanyika majira haya.
Kuna maswali yameelekezwa kwangu.Kimsingi ikiwa kuna mtu anaamini kwamba kuna mafunuo mapya juu ya kilichoandikwa kwenye Biblia na kwamba wengine hawawezi kujua kwa kuamini na kukitendea kazi kilichoandika hadi wamefunuliwa basi kuna kazi.
Kamwe usiitumainia akili zako.Jihoji kwanini umeambiwa umepokea bure utoe bure.Je, wajua maana yake? mipaka yake ikoje?
Hakuna orodha ya dhambi. Dhambi ni chochote kilicho kinyume na AMANI.Je, wajua kwamba kinachoendelea sasa katika mada hii hakileti AMANI?Na kwanini watu wanaendelea kuchangia? Kinatoka wapi wanachochangia?
Waefeso 4. Tunapata msingi wa namna tunapaswa kuishi.Je, unapata ukweli wa andiko hilo kwenye mada inayoendelea?
Ikiwa wajua maana ya kumwabudu Mungu katika roho na kweli.Unachochangia ni nini?
Kwa kuuliza yote hayo haimaanisha ninahitaji majibu bali nakusihi umhoji Mungu nini hasa anakitaka kwetu majira haya na ikiwa kuna maisha katika mada hii na mengine ambayo yamekuwa jakichangiwa.
Amani ikifundishe yote.Amen
46. 

Ninamshukuru Mungu wa mbinguni kuwa mawazo yangu yalipata kibali cha kuwemo katika blog hii kuhusiana na nilichochangia ambacho sina mashaka kuwa ni sehemu ya kile ambacho Mungu muumba mbingu na nchi amekipanda ndani yangu kwa neno lake lililo hai na lenye nguvu ya kutambua mawazo na makusudi ya moyo.
Niendelee kusisitiza kuwa tusipoangalia msingi wa imani yetu tutafikia mahala tutatoka katika mpango sahihi wa Mungu kama wana wa Israeli walivyojikuta wakikwazwa na sheria ambayo waliahidi mbele za Musa na hata Yoshua kuwa wataishika.
Naomba tufunguliwe macho yetu ya rohoni kujua kuwa msingi wa imani yetu ni katika NENO LA MUNGU na si kwa jinsi tulivyo na amani kwani amani ya kweli inapatikana kwa Yesu ambaye ndiye neno la MUNGU na ndiye Mungu mwenyewe. Hivyo amani yoyote isiyo na msingi na shina la neno la Mungu amani hiyo si ile iliyoachwa na Yesu.
Pili niweke sawa jambo hili kuwa kuabudu si kuimba pekee ila ni maisha halisi ya kiroho kwa kila anayemwani Bwana Yesu na aliyemkabidhi maisha yake huyo (YESU). Ni maisha yaliyo uhai kamili kwa kila aliyekombolewa na kufahamu thamani ya wokovu wake na katika hili kuimba kunakuwa sehemu tu ya kuonyesha maisha hayo. Hii ikiwa ni pamoja na kusifu na kumwadhimisha Bwana Yesu.
Pia niwe muwazi kusema jambo hili ambalo sasa linatumiwa kama njia ya kuwafanya watu waishi kwa woga na tahadhari inayowafanya kupoteza uhuru wao halisi uliotangazwa na Bwana Yesu (LUKA4:18). Shetani yupo wakati wote huu ambao tunasubiri siku ile kuu ya pambazuko la roho. Anatenda kazi kwa namna mbali mbali na pia kwa habari ya kulivamia kanisa amefanya hivi kwa karne nyingi sana tangu kanisa la kwanza (soma waraka wa kwanza wa Yohana:1-2). Ndio maana tuna utitiri wa madhehebu duniani kudhihirisha kuwa uvamizi ndani ya kanisa umekuwepo. Lakini Mungu anawajuwa watu wake kwani wameshapigwa muhuri tayari na Roho Mtakatifu na wao wanaijua sauti ya Mchungaji mwema. Kinachofuata sasa si kupiga kelele za shetani amelivamia kanisa bali tuinue macho yetu juu kumtazama Kristo alipo ameketi mkono wa kuume wa Mungu baba mwenyezi kwa kujua sana kweli yake ambayo ni neno lake. Pia kuomba kwa bidii mbele zake ili upate kuwafahamu ndugu sahihi walio na roho moja nawe (Efeso4:4). Na si kuogopa namna watu wanavyonengua kwenye uimbaji ama kubarikiwa na kundi fulani ambalo linapokutanika kuna kunena kwa lugha ama matendo ya miujiza.
Mungu awabariki sana ndugu wapendwa kwa moyo wenu wa kumtumikia Mungu kwa njia hii ya kubadilishana mawazo na si kurumbana kusiko na faida.
AMEN
47. 

Amani, heshima na upendo kwenu nyote. Na naendelea kushukuru kwa kila anayechangia.
Nilipotezwa na majukumu kiasi na namshukuru MUNGU kuwa nimerejea kujifunza zaidi na zaidi. Kwako kaka John
1: Midundo inaweza kuwa kiashiria cha utamaduni wa asili ya muziki. Mfani kuna midundo ambayo ikisikika watu watajua kuwa ni muziki wa Latin America, lakini pia muziki unakuwa na kama ilivyo kwa vitu vingine visivyo na mipaka” huwezi kuu-limit kuwa utakuwa umetokea ama umepigwa huko kwa kuwa tu ni asili yake. Na ndio maana leo hii tunasikiliza Gospel za midundo na mahadhi ya aina zote. Ninalomaanisha hapa ni kuwa MIDUNDO HAIBEBI UJUMBE BALI ASILI NA TAMADUNI.
2: Sina hakika na tofauti ya Bolingo na Salsa kiutendaji (zaidi ya kimatamshi na asili). Lakini kama unaamini kuwa Bolingo si aina basi naamini na salsa pia. Kwa hiyo nahisi ama niseme kuwa naamini kuwa vyote viko pamoja. Na kuhusu kubadili maneno “bila kubadili kitu kingine chochote” nadhani unaweza kufanya hivyo kwa dhamira ya kubishana tu na si katika uhalisia wa mambo. Ni sawa na kumwambia mtu ALIE KWA TABASAMU. Ninavyofahamu mimi ni kuwa nyimbo zitawekewa maneno ziendane na midundo na / mahadhi kama lengo ni kufikisha ujumbe sahihi. Kwa hiyo REALLISTICALLY sioni MANTIKI ya kubadili maneno na kuweka ya huzuni kwenye wimbo wa sherehe. Hiyo kwangu ni dhana ya kudhihirisha kitu ama kutengeneza parody na si kwa lengo kamili la muziki.
3: Hili nahisi umelielezea na kuweka utata zaidi. Umesema huabudu dini bali MUNGU ALIYE HAI. Natambua kuwa wewe ni MKRISTO na kama hauukani sasa basi unaabudu Mungu aliye hai kwa kuwa wewe ni mkristo na UKRISTO ni dini ya wale ambao wanamcha na kumfuata KRISTO (naamini wewe ni mmoja wapo labda useme vinginevyo). Na pia natambua kuwa kuna wengi wanaomuabudu Mungu japo kwa njia tofauti na Kristo na ndio maana si waKristo, kwa hiyo kusema huabudu dini bali wamwabudu Mungu unaweza kuwa na maelezo tofauti na nilivyoelewa mimi na niaendelea kutunza haki ya kukosea na kukosolewa. Kwa hiyo ukihisi sijakuelewa basi nikosoe tafadhali.
4: Kwa swali hili ningefurahi, kushukuru na kufarijika kama ungeeleza tofauti uliyonayo kati ya MIRINDIMO na MIDUNDO.
Kisha nami ningefurahi kuona upande uliopo katika hili, kujua una mtazamo gani na namna unavyoweza kutuelimisha kulingana na mtazamo wako.Na pia ningependa kujua nyimbo unazopenda kusikiliza ambazo unaamini NDIZO NYIMBO ZA DINI / ZIFAAZO MAKANISANI
Nikirejea kwa Dr Malisa, umeanza kwa kusema “kabla ya kujibu maswali niliyoulizwa, naomba kuambatanisha hapa article inayoelezea jinsi muziki wa kishetani ulivyopenya katika jumuia na hata kanisani.” Na baada ya hapo hujajibu maswali. Sijui ulikuwa ukimaanisha kuwa utayajibu wakati mwingine ama la!! Lakini katika maoni yako yote uliyotoa sijaona ukijaribu kujibu maswali yaliyoulizwa kuhusu Muziki ufaao. Na pia umetoa article ambayo hujaeleza umeitoa wapi na hao walioiandaa walifikia vipi katika takwimu walizotoa. Pengine work citations husaidia kusaka kwa undani umakini wa mtayarishaji maana kuna kazi nyingi huandikwa na kuonekana zafaa kwa wengine na baadae kuja kugundulika kuwa hazikuwa na ukweli. Ndio maana kwenye uandishi huzingatia “work citations” katika kila unakilicho. Lakini nawe pia ningependa kupata majibu hasa juu ya MUZIKI UFAAO MAKANISANI. Na ombi la ziada ni kujua nyimbo unazopenda zaidi kusikiliza ambazo unaamini NDIZO NYIMBO ZA DINI
Kwa Kaka Fred. Kwanza maswali yangu ya tarehe 2 hayakujibiwa na ningetamani saana kama ungefanya hivyo ili kujua hao ambao wewe unawasikiliza ukiamini kuwa wanaimba ama wana muziki wa injili ufaao makanisani. Na katika maoni yako ya tarehe 24 umesema “Mti wa mema na mabaya huleta kifo na ndicho kinachoendelea hapa.Tukumbuke kwamba hata kama unaeleza ukweli na taarifa sahihi LAKINI kukawa hakuna amani juu ya unachosema basi kuna tatizo.Na ndicho ninachopata katika mjadala huu.” Pengine ingependeza kama ungefafanua unachomaanisha. Maana unatambua fika kuwa si kila mtu ana uelewa mkubwa kama wako na bila ufafanuzi hakutakuwa na kutimilika kwa lengo la kuelimishana.
Mwisho narejesha maswali yangu kwa mara ya tatu na naamini ntajibiwa
Nauliza hivi
1:Je! nyimbo za wanamuziki kama Cosmas Chidumule, Remmy Ongala na hata Mzee Makassy si za injili na hazifai kutumika makanisani kwa kuwa tu walikuwa wakitumia mirindimo iendanayo na hii ya sasa walipokuwa hawajaokoka?
2:Je wasanii kama Beatrice Muhone, Bahati Bukuku, Rose Mhando, Kijitonyama na wengine wengi wanaoimba na kugusa watu sasa hazifai kwa kuwa tu zina mirindimo iendanayo na baadhi ya hiyo mnayoiita ya kidunia?
3:Kwani muziki asili yake wapi na muziki wa dini asili yake wapi?
BARAKA KWENU
48. 

Kwa ndugu Mubelwa,
Pole kwa majukumu! ..nayo ni baraka pia.
Nashukuru kwa majibu yako. Katika unayoyaandika kuna mambo ambayo najifunza pia.
1.Tafsiri yako ya MIDUNDO nitaiacha kama ilivyo kwa kuwa umeandika unavyoelewa wewe. Ni haki yako!
2.Jambo hili la pili ni moja ya mambo ambayo inabidi tuwekane sawa.
i). Suala la Bolingo kuwa ni mtindo na si aina ya muziki ni la kimuziki [taaluma] zaidi. Bolingo ni mtindo kama ilivyo kwa Taarabu. Bolingo hupigwa kwa kutumia [mara nyingi] mdundo wa Disco na Taarabu nayo hutengezwa kwa kutumia zaidi mdundo wa Slow Rock. Salsa ni ‘style’ kama zilivyo Disco na Slow Rock. Hata hivyo maelezo haya ni ya kitaaluma ya muziki kwa hiyo mtu kama hafanyi muziki ni vigumu kuyaelewa. Lakini maelezo haya machache nafikiri yanatosha kuweka ACBs.
ii). Kama ambavyo muziki uliopigwa kwenye ‘sherehe’ hauwezi kufaa ukipigwa kwenye ‘huzuni’ [kama ulivyo], hali kadhalika muziki uliopigwa kwenye ‘club’ hauwezi kufaa ukipigwa kanisani, [pasipo kuubadili chochote]. Unless hatukubali kwamba muziki hubadilika kutokana na mazingira na hali ya unapopigwa!.
Kwa hiyo hapa tunaona kwamba SI KWELI tukisema ‘muziki ni muziki tu’ bali ‘maneno ndiyo hubeba ujumbe’. Kama ingekuwa ni kweli basi muziki uliopigwa kwenye ‘sherehe’ tungebadili maneno tu na huo huo tukaupiga kwenye ‘huzuni’ muziki uliopigwa kwenye ‘club’ tungebadilisha maneno tu na tukatumia muziki huo huo kanisani. Lakini hili haliko hivyo kama ambavyo umeeleza kwamba ni sawa na kumwambia mtu ‘alie kwa tabasamu’.
Mazingira ya kwenye sherehe ni tofauti na mazingira ya kwenye huzuni. Mazingira ya kwenye sherehe za siku ya wafanya kazi duniani ni tofauti na mazingira ya kwenye mkutano wa Injili. Mazingira ya kwenye Vilabu vya pombe ni tofauti na mazingira ya makanisani. Furaha ya kanisani ni tofauti na furaha ya kwenye Club. Hivyo hata kama ni muziki wa ‘sherehe’ ukapigwa kwenye club, muziki huo haufai kuupiga kwenye ‘sherehe’ ya kanisani kwa kuwa mazingira ya sehemu hizi ni tofauti. Kwa hiyo basi muziki unaopigwa kwenye sehemu hizi lazima uwe UMEPANGWA VEMA KULINGANA NA HALI YA SEHEMU HUSIKA ili kufikisha ujumbe sahihi.
Tukisema ‘muziki ni muziki tu cha maana ni maneno’ tutasababisha muziki fulani, pasipokuzingatia ujumbe unaokusudiwa, upigwe sehemu isiyo yake na kwa njia hiyo tutakuwa tunatengeneza parody na si kwa lengo kamili la muziki.
3. Dini ziko nyingi na kila dini ina utaratibu wake wa kuabudu. Utaratibu huu waweza kubadilika toka sehemu moja hadi nyingine. Ndiyo maana hata Padri Privatus Karugendo alishawahi kulalamika kwamba jinsi dini yao inavyoendeshwa hapa Tanzania ni tofauti na jinsi inavyoendeshwa sehemu nyingine za ulimwengu. Watu wengi wana dini lakini si wote wanaommwamini na kumfuata Yesu Kristo. Hata baadhi ya wale wenye dini zinazoitwa za Kikristo wengine wao hawafuati mafundisho ya Bwana Yesu lakini ni wafuasi wazuri wa mafundisho ya dini zao. Ni waumini wazuri wa dini lakini si waumini wa Bwana Yesu. Watu hawa ndio wanaoabudu Dini.
Watu wanaomwamini na kumfuata Yesu hawa humwabudu Mungu. Huishi na kufuata mafundisho ya Bwana Yesu kama yalivyoandikwa kwenye Biblia. Utaratibu wao wa kuabudu ni kulingana na Biblia. Hawa ndio waabuduo halisi. Hawa ndio Yesu Kristo alisema kwamba Mungu Baba anawatafuta; wanaoabudu katika Roho na kweli. Ndiyo maana nikakuambia kwamba WATU WOTE WALIOOKOKA WANATAKIWA KUMWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI. Ni utaratibu wa ulimwengu wote.
4. i).Umenirudishia swali ambalo nilikuomba unisaidie. Nitalijibu ili tufupishe dialogue:
Kwa maana na tofauti niliyonayo mimi MRINDIMO ni Muungurumo. Ni mlio wa sauti nzito unaoendelea kwa muda fulani. Mlio wa sauti nzito ambao ni wa muda mfupi ni Kishindo. Mfano ni kama vile radi ikipiga ule muungurumo unaojitokeza pale ni mrindimo; na
MDUNDO ni mlio wa ngoma. Inaweza kuwa ‘electronic’ au ‘acaustic’ drum. Ni mlio unaosikika baada ya ngoma kupigwa.
ii. Nyimbo ninazopendelea kusikiliza ni zile ambazo muziki wake umepigwa kwa kuzingatia ujumbe wa Kikristo unaokusudiwa kuwafikia watu. Kwa upande wa pili sipendi kusikiliza nyimbo ambazo muziki wake umepigwa kwa kigezo cha muziki ni muziki tu pasipo kuzingatia ujumbe unaokusudiwa uwafikie watu. Hiyo ni vurugu.
Kwa hiyo mimi siko upande wowote, niko kati kati!
Ninaandaa maelezo, kama somo fulani, ambayo nitayaleta mwishoni baada ya kuwa tumekubaliana juu ya mambo kadhaa ya msingi.
Kama kuna mahali hujanielewa unaweza kuuliza swali maana mimi niko tayari kujibu kila swali linalojitokeza kutokana na ninachokiandika hapa. Huwa sina tabia ya mtu aniulize swali halafu nikamrudishia swali hilo.
Kwa sasa nitajibu kwa kiasi fulani maswali yako ambayo umeyauliza kwa mara ya tatu sasa:
1. Nyimbo za wanamuziki uliowataja, na wengine wengi, ni za injili na zinafaa kutumika makanisani kwa kuwa zina ujumbe unaohusu Injili na Neno la Mungu kwa ujumla.
Wengi wa watu ambao walikuwa wanapiga muziki secular halafu wakaokoka kuna badiliko kubwa sana kwenye muziki wanaoupiga baada ya kuokoka. Tofauti hii inaweza isieleweke kwa mtu ambaye hajuwi kutotofautisha ‘lugha’ ya muziki. Waimbaji kama Cosmas Chidumule, na wengine wengi, muziki wao wa sasa unatofauti kubwa sana na unastahili kabisa kubeba ujumbe wa Neno la Mungu. Wako baadhi ya wanamuziki ambao walipookoka hawakulijuwa hilo na kuendelea kupiga muziki kama ule ule wa zamani. Watu hawa hata ukisikiliza nyimbo zao haziko vizuri maana ni mchanganyiko wa mambo na wala hazidumu angani! Siwezi kutaja mmoja mmoja hapa kwa kuwa hapa hatuko mahakamani kuhukumiana lakini tunachoweka hapa ni kama kioo ili kila mtu ajiangalie yuko sehemu gani.
2. Wasanii kama Beatrice Muhone, Bahati Bukuku, Rose Muhando, Kitonyama na wengine wanaoimba na kugusa watu sasa nyimbo zao zinafaa. Waimbaji uliowataja ni baadhi ya waimbaji ambao nyimbo zao zimepigwa muziki kulingana na wimbo wenyewe. Msisitizo [emphasis] katika nyimbo zao ni ujumbe na sio muziki [intrumental]. Nyimbo nyingi za waimbaji uliowataja zimepigwa muziki rahisi ambao humfanya msikilizaji asikilize maneno zaidi kuliko muziki. Ingawa ziko baadhi ya nyimbo ambazo zingepigiwa muziki mbadala ujumbe wake ungemfikia zaidi msikilizaji kuliko zilivyo sasa. Hapa pia sitataja nyimbo hizo kwa sababu niliyoiandika hapo juu.
3. i).Muziki asili yake ni mbinguni.
ii). Kwangu mimi hakuna muziki wa dini kwa sababu ala za muziki zinazotumika ni hizo hizo kwenye nyimbo zinazohusu Neno la Mungu na nyimbo zisizohusu Neno la Mungu. Gitaa hilo hilo hupigwa kwenye muziki wa kidunia na muziki wa Neno la Mungu na vivyo hivyo kwa vyombo vingine vyote vya muziki. Kinachobadilika ni namna chombo hicho kinavyotumika.
Ninachoweza kujibu ni kwamba Muziki wa Injili asili yake ni kwa watu wanaoimba habari za Neno la Mungu. Watu ambao wanakusudia kuihubiri Injili kupitia nyimbo zao.
Kama kuna mahali popote ambapo sijaeleweka au sijajibu ipasavyo nakaribisha swali kwa moyo wa kujifunza!
Changamoto ninachokuachia ndugu yangu Mubelwa ni hii:
March 18 uliandika kwamba wewe hupendelea sana muziki wa Reggae. Swali ni kwamba Je,unaifahamu sababu inayokufanya upendelee muziki huo?
Utakapokuwa unalijibu swali hili [mimi sihitaji jibu lake hapa] zingatia yafuatayo:
i). Sababu hiyo si Ujumbe – Kwa sababu ujumbe wa Neno la Mungu unaimbwa katika muziki wa aina mbali mbali na kama lengo ni ujumbe basi ungependelea kila aina ya nyimbo ili uweke kupata ujumbe wake.
ii). Sababu hiyo siyo muziki wenyewe – Kwa sababu muziki hauna maneno. Milio ya gitaa na vinanda na ngoma haiwezi kutafsiriwa kwa maneno ambayo yanaweza kuwa na ujumbe kwa mtu. Kwa hiyo kama ni kwa sababu ya muziki wenyewe basi hakuna lolote unalojifunza kutokana na kupendelea muziki huo.
iii). Sababu hiyo si asili – Kwa sababu wewe asili yako si kule ambako muziki huo ulianzia.
Kwa hiyo nakuanchia changamoto hii ili ufahamu ni nini kinakufanya upendelee muziki aina ya Reggae.
Tuendelee kujifunza.
49. 

Ndugu zangu neema iwe nanyi. Namshukuru Mungu kwa yote.
Niweke wazi mapema kuwa huu mjadala haujengi na kwa kiwango kikubwa umeruhusu Babeli kupata nafasi zaidi.
Ndugu Mubelwa T Bandio usimpe ibilisi nafasi, acha ubishi, una roho udadisi usio na msingi(critical spirit) wa kujenga, uwe makini, tubu na umtii Bwana.Hali hiyo lazima ikome mara moja.
Kuna watu humu ndani lazima vinywa vyao vizibwe.
Wakolosai 3:15.
Hatuwezi kufika kwa utaratibu huu.
Mwenye masikio ya kusikia na ayasikie haya.
Amani iwe nanyi.
50. 

Wow!
Mwenye macho na asome maoni yako yote Fred
Amani iwe nawe pia.
51. 

Hello watakatifu wa Bwana,
Nashukuru Mungu kwa kunipa nafasi hii tena ya kushirikiana nanyi mambo ambayo ameweka katika moyo wangu. Ni muda kidogo nimepotea, na hii ni kutokana na majukumu ya hapa na pale. Nashukuru kuona mijadala inaendelea hapa SG, lengo likiwa ni kujifunza na kukua kiroho, katika safari yetu ya kwenda mbinguni!
Ningependa nianze kusema kuwa sitaweza kujibu baadhi ya maswali kwa leo, maana siajapata muda wa kuyapitia. Lakini wakati ninaendelea kupitia maswali, nimeona niseme machache juu ya mjadala huu.
Kwanza lazima ifike mahali tuone kwa namna sahihi maisha ya kikristo na wokovu. Tunapomkubali Yesu Kristo, na damu yake iliyolipa gharama za makosa yetu, tu watakatifu mbele za Mungu, na toka hapo tunakuwa tumeokolewa na kama ukifa, unaenda mbinguni. Lakini Mungu kwa makusudi kabisa, hatuondoi duniani tukiisha kuokolewa, KWA NINI? Kwa sababu anataka tuishi maisha yanayoonyesha kuna kitu kisicho cha kawaida kimefanyika. Anataka tuwe nuru na chumvi ya ulimwengu. Hapa ndipo wapendwa wengi wanakwazika.
Maisha ya Kikristo ni maisha ya kujitenga na ulimwengu. Waefeso 5:11 inasema tusiwe na shirika na kazi za giza bali tuzikemee. Kwa hiyo ulimwengu unatakiwa kujifunza toka kwa Kanisa na si kinyume! Haya ndiyo matendo ya nuru.
Wapi ninaelekea? Ni kwenye Muziki unaofaa mbele za macho ya Mungu. Biblia iko wazi ya kuwa Mungu hajengi juu ya kitu ambacho msingi wake hakuuweka. Mambo ya walawi 10 tunasoma jinsi Mungu alivyo makini kuliko tunavyotaka awe. Hiyo imekuwa kanuni ya Mungu. Wakati shetani anaweza kutumia chochote kutimiza matakwa yake, kwa Mungu wetu ni tofauti. Hatumii chochote ambacho hajakiwekea msingi.
Tatizo lililopo sasa ni kuwa wapendwa wana miungu yao waliyoijenga kwenye fahamu zao ambao kwa hakika hawapo! Mathalani mtu atasema mungu wangu hafanyi hiki au kile. Lakini utakuta jambo analosema haliko katika Neno la Mungu. Huyo Mungu anayemsema ni mazao ya mafikirio yake. ni sanamu!
Nikifika kwenye suala la muziki, kumekuwa na maoni mbalimbali, lakini je ukweli ni upi? Kwa msingi nilioujenga hapo juu utajua kuwa Muziki wowote ambao asili yake haikuwa kumtukuza Mungu, yaani ambao Mungu hakuweka Msingi, haufai kanisani! Hapa nitatoa baadhi ya mifano kuonesha ninachomaanisha.
Lakini kabla sijatoa mifano hiyo ni lazima tufahamu tofauti ya utamaduni na muziki. Mfano, kuna utamaduni wa kinyaturu(utaratibu wa maisha wa wanyaturu). Hii inajumuisha ngoma zao, ibada zao, nk. Utaona muziki ni kasehemu ka utamaduni wao. Pia Lazima tujue kuwa ukristo,tangu misingi yake, ni utamaduni uliowekwa na Yehova. Kuna namna ya kuabudu, miiko, nk.
Sasa turudi kwenye mifano. Nitaanza na hip hop. Wapendwa wengi wamekosea kuita Hip hop muziki! Kwa wanaoufahamu, ni utamaduni(namna ya maisha). Akihojiwa na mtangazaji mmoja, Kirk Franklin alikiri kuwa Hip hop ni utamaduni na kanisa ni lazima likumbatie utamaduni huu ili kuwafikia walio katika utamaduni huu. Hii ni kinyume kabisa na waefeso 5:11. Aina ya muziki ambayo inatumika kama mashua ya kubeba utamaduni wa hip hop ni rap. Kwa msingi huo, rap haiwezi kutumika kanisani kwani ikiruhusiwa kanisani kama ambavyo ilivyo sasa, tutashuhudia (kama tunavyooona sasa) vijana wakiukumbatia utamaduni huu ambao misingi yake ni kuzimu! Mungu, kama ambavyo hakukubaliana na Nadabu na Abihu, hakubaliani na Hip hop! nani ana ujasiri wa kusema kuwa mbinguni tutamwimbia Baba kwa kufoka-foka?
Mfano mwingine ni Sebene! Kwa bahati tangu utotoni nimekuwa mfuatiliaji wa Muziki huu toka Kongo. Wengi tunafahamu namna muziki huu usivyofaa kutazama hata katika macho, lakini hata leo nashangaa jinsi ulivyoingizwa kanisani. Lengo la sebene ni kuwaburudisha watazamaji kwa viuno na mavazi machafu. Kwa hakika, mara nyingi baada ya kutoka jukwaani, wanenguaji hupata ofa mbalimbali toka kwa wanaume wazinzi. Sasa ilikuwaje na inakuwaje tunakuwa na muziki wa namna hii kanisani? Jibu ni kuwa, haya yote yamepata mlango pale tulipogeuza muziki toka kumsifu Mungu hadi kuwa starehe! Ni pale tulipogeuza makanisa kuwa Klabuza jamii!
Mfano mwingine ni taarabu. Watu wa pwani wanafahamu kuwa taarabu ni sehemu ya utamaduni huu. Mambo yanayofanyika ktk taarabu hayafai kuyaandika. Kwa hakika, taarabu ni moja ya miziki inayochochea uzinzi na uasherati. Sasa kwa msingi huu, ilikuwaje taarabu ikaingia kanisani? Je Mungu amebadili misingi ya utendaji wake? Jibu ni hapana, ila sisi tumetengeneza mungu mwingine ambaye kwake taarabu, hip hop au chochote kile ni sawa, maadamu tu kibadilishiwe lebo kiwe gospel XXX na mashairi pia yafanane na ukristo. Huyo si Jehova, bali ni baali, ndama tuliyojitengenezea.
Kuna mifano mingi tu, lakini hii inatosha kuonesha ambayo Mungu ameweka katika moyo wangu. Kama ambavyo ndugu G. Craige Lewis aliuliza ningependa pia niulize, lebo ya 666 ikibadilika na kuitwa Gospel 666 utakubali kuipokea? Bila kujali lebo 666 ni 666 tu!
Ni muda wa kuacha kung’ang’ania mambo mafu na yenye misingi ya giza, turudi katika misingi halisi ya Imani yetu. Moja kati ya sifa za Mkrsto aliyekua ni kukubali kugeuka, pale anapokosea. Kung’ang’ania mambo ya dunia ni utoto wa kiroho, lazima ifike mahali tukue!
Je hii ina maana kuwa wanaoimba Hip hop, taarabu, reggae sebene n.k ni wabaya? Siyo lazima iwe hivyo! Ni naamini ni kwa kuwa wamedanganywa kuwa shetan aliiba muziki wetu hivyo lazima tuurudishe. Wanahitaji tu kujua matatizo yaliyo katika miziki hiyo!
Mwisho ningeomba tujadili kwa kufuata Neno la Mungu badala ya mawazo binafsi! Mimi naweza kuamini kwa mawazo yangu kuwa hakuna mji wa Kericho, na Jirani yangu akaamini upo lakini ni sayari ya Mars na mwingine akasema Uko phillipines! Bila kuweka Ramani na kuangalia tutapotea. Mwongozo wetu ni Biblia. Hivyo mijadala yetu iwe na mipaka ndani ya Biblia.
Neema na amani ya Kristo iwe nanyi!
Amina
52. 

Hapa nimejifunza. Na nimejifunza kwenu nyote. Nawashukru Kaka Steve M na John Paul kwa haya. Naamini kutakuwa na uwanja wa hili maana nahisi linaelekea kwenye uhitaji wa ufafanuzi.
Amani kwenu
53. 

It doesn’t matter what style music it is as long as the music gives glory to God. God likes any style of music that glorifies Him.
54. 

Kwa ndugu Bernad Mwenda,
Mimi naomba kuchangia katika swali lako kuhusu AMANI YA KRISTO, ulilouliza tarehe 20/3/2009, kama ifuatavyo:
Katika Wakolosai 3:15 tunapata andiko muhimu kuhusu suala hili kwamba “Na amani ya Kristo iamuwe mioyoni mwenu”
Lakini tukisoma sura hiyo ya 3 kuanzia mwanzo na kuendelea tunapata mambo muhimu sana juu ya mtu mwenye MOYO au TABIA AMBAYO KWAKE AMANI YA KRISTO INAWEZA KUFANYA KAZI. Baadhi ya mambo yaliyoandikwa hapo ni yafuatavyo:
i). Mtu aliyefufuka pamoja na Kristo (kuzaliwa mara ya pili)
ii). Mtu anayetafuta mambo ya mbinguni
iii). Mtu aliyevifisha viungo vya mwili asienende kwa kufuata ulimwengu huu
iv). Mtu asiyesema uongo
v). Mtu aliyefanywa upya fahamu zake ili awe na ufahamu sahihi
vi). Mtu ambaye katika maisha yake Kristo ndiyo kila kitu
vii). Mtu mwenye moyo wa rehema, unyenyekevu, upole uvumilivu na mambo yafananayo na hayo
viii). Mtu ambaye amejaa upendo,
ix). Mtu mwenye neno la Kristo kwa wingi ndani yake
x). Mtu ambaye kila analolifanya anafanya kwa jina la Bwana Yesu.
Hayo ni baadhi ya mambo yaliyoandikwa katika sura hiyo ya kitabu cha Wakolosai.
Kwa hiyo tunaweza kuona kwamba ili AMANI YA KRISTO iweze kutenda kazi ndani ya mtu, mtu huyo anatakiwa awe mkamilifu kweli kweli katika Kristo. Mtu ambaye ana uwezo wa kuisikia sauti ya Mungu ndani yake kupitia Roho mtakatifu.
Mtu aliyeokoka dhamiri yake huwa ni hai. [Ebrania 9:14] Uhai huu hufanywa katika Roho wa Mungu. Roho wa Mungu huzungumza ndani ya mtu aliyeokoka kwa kumjulisha kila kitu anachofanya kuwa ni sawa au si sawa; kwamba ni salama au ni hatari. Ni kama kipimo fulani cha kiroho ndani ya mcha Mungu. Mambo yanapokuwa ni shwari Amani hii huwepo moyoni. Amani hii humuongoza mtu kwa masuala yote, yaani mambo yahusuyo Mungu na mambo yahusuyo binaadamu.
Suala linalotofautisha utendaji wa Amani hii ndani ya mtu mmoja na mwingine ni mifumo ya maisha inayotofautiana. [Hapa ni kwa mambo yanayotuhusu sisi binaadamu]. Tofauti hii yaweza kusabishwa na mambo kama Huduma ambayo mtu huyo ameitiwa katika mwili wa Kristo; Umri; Mazingira anayoishi mtu na jamii inayomzunguka; Hali ya kiuchumi ya mtu na mambo mengine ambayo yanaweza kusabisha jambo fulani la kibinaadamu lifanyike kutokana na utofati huo.
Amani ya Kristo huamuwa katika mambo mengi. Jambo fulani laweza kuwa si sahihi kufanywa na mtu fulani au kufanyika kwa mtu fulani wakati jambo hilo hilo likawa si tatizo kama litafanywa na mtu mwingine. Amani ya Kristo HUONGOZA KATIKA MAMBO MENGINE PIA AMBAYO SI LAZIMA YAWE NI DHAMBI.
Nitatoa mifano kadhaa:
a). Kazi fulani yaweza sababisha kukosekana kwa amani ya kristo ndani ya moyo wa mtu ambaye kazi hiyo inaweza kukwamisha huduma yake aliyoitiwa katika mwili wa kristo lakini kazi hiyo hiyo inaweza isiwe tatizo moyoni mwa mtu asiye na huduma hiyo husika.
b). Mtu fulani anaweza asipate amani moyoni kwenda kwa mtu fulani kwa sababu kumbe kama angeenda asingemkuta
c). Mtu anaweza asipate amani kusafiri na gari fulani halafu baadaye akasikia gari lile alilokuwa asafiri nalo lilikwenda akupata ajali.
KUTOFAUTIANA KATIKA BAADHI YA MAMBO
Kuna mambo ambayo mtu mmoja anaweza asipate Amani lakini mwingine akasema ana Amani. Kwa mambo yanayotuhusu sisi wenyewe binaadamu inawezekana kabisa, binaadamu tuna mifumo tofauti ya maisha. Kama nilivyoandika juu kwamba tuna mambo mengi yanayotutofautisha. Na haya yanayotutofautisha ni ya kwetu wenyewe binaadamu. Katika Mambo yanayohusu Mungu huwa hakuna tofauti kwa sababu Kristo ni mmoja na Roho Mtakatifu ni mmoja.
Huwa inatokea watu wakatofautiana katika jambo fulani linalohusu maisha ya Kiroho huku kila mmoja akisema anajisikia Amani. Katika hali kama hii ni lazima upande mmoja uwe na matatizo. Haiwezekani jambo fulani likawa ni uovu kwa mtu mmoja halafu kwa mwingine likawa si uovu. Tofauti hii inapokuwa imetokea yaweza kusababishwa na moja ya sababu zifuatazo:
i). Kuchanganya Amani ya Kristo na Hisia za kibinaadamu
ii). Kuizimisha kwa makusudi Sauti ya Roho mtakatifu
iii). Kutokufahamu kabisa amani ya Kristo na utendaji kazi wake.
Maelezo kwa ufupi:
i). Kuchanganya Amani ya Kristo na Hisia za kibinaadamu
Kuna mtu ambaye anaweza kuwa ameokoka kabisa na dhamiri yake ikawa hai kwa kutambuwa uongozi wa Amani ya Kristo katika kujiepusha na mambo mbali mbali ambayo ni machukizo mbele za Mungu. Lakini katika mwendo wa maisha inaweza ikafika mahali mtu huyo asiweze kutofautisha kwa usahihi Uongozi wa amani ya Kristo na Hisia zake mwenyewe. Hii inaweza kusababisha MSISIMKO uchukuliwe kama ndio amani ya Kristo yenyewe. Hali inapokuwa namna hii lazima kuwe na utofauti kati ya mtu mwenye tatizo hili na mtu asiyenalo.
Mfano tunaoweza kuutumia hapa ni kama vile unaweza kuta mkaka ameokoka kabisa lakini katika pilika za kutafuta mchumba akakutana na mdada ambaye kutokana na umbile lake lilivyo mkaka huyo akasisimuka na kuona kama huyo ndiye mke wake halisi. Lakini inaweza kutokea rafiki yake wa karibu akamwambia kwamba hajisikii Amani moyoni na kumuomba waombe Mungu ili kupata uthibitisho wa suala hili. Lakini mkaka huyo atabisha na hatimaye kumuoa mdada huyo ambaye baada ya muda utasikia kuna matatizo mengi sana katika ndoa hiyo.
ii). Kumzimisha kwa makusudi Roho mtakatifu.
Mtu mmoja anaweza kuwa anasikia kabisa moyoni mwake kwamba hakuna Amani moyoni juu ya jambo fulani lakini mtu huyu akang’ang’ana na jambo hilo tofauti na wapendwa wengine wanavyojisikia. Mtu huyu huwa anakaidi tu kwa makusudi. Ndiyo maana Andiko la “Msimzimishe Roho” likaandikwa. [1Thesalonia 5:19]. Andiko hili ni kwa mtu anayefahamu utendaji kazi wa Roho Mtakatifu.
iii). Kutokufahamu kabisa Amani ya Kristo na utendaji kazi wake.
Kuna watu wengi ambao huwa wanaiga mwenendo wa watu waliookoka. Ni wakristo waungwana lakini hawajaokoka kwa hiyo mambo ya rohoni kwao hayaeleweki. Waigaji hawa huweza kubainika wazi linapotokea suala linalotakiwa litatuliwe kwa mtazamo wa Rohoni na si mwilini. Waigaji hawa, kwa kutokulipambanua jambo hilo katika Roho, hulazimisha kwa mtazamo wa kibinaadamu kwamba suala hilo si Tatizo wakati katika mtazamo wa rohoni suala hilo ni ugonjwa wa kufisha. Wakati mwingine watu wa namna hii hufikiri pia mafundisho ya mapokeo wanayofundishwa kwenye makanisa yao ndiyo kipimo pia cha Amani ndani yao.
Katika hali ya namna hii lazima kuwe na tofauti katika jambo hilo hilo moja.
Si kila mtu aliye Mkristo huwa ameokoka na mbaya zaidi Si kila mtu anayesema kuwa ameokoka huwa ameokoka kweli. Kwa hiyo linapokuwa limetokea jambo fulani la Kiroho ni lazima tofauti hii ionekane hata kwa watu ambao wote wanasema wameokoka.
HITIMISHO
Amani ya Kristo hufanya kazi ndani ya moyo wa mtu ambaye ameokoka kikamilifu na anaishi maisha matakatifu. Amani ya Kristo kwa maneno mengine ni chombo ambacho Roho mtakatifu hutumia kuwasiliana na wana wa Mungu, watakatifu walioko duniani ambao Mungu hupendezwa nao, katika kuwaongoza kwenye mapito mbali mbali ya mambo ya rohoni na hata ya mwilini pia.
Hivi ndivyo nilivyoweza kuchangia kwa sasa. Kama sijaeleweka mahali fulani au nimekosea, maswali yanakaribishwa ili kwa pamoja tuendelee kujifunza.
55. 

Asante saana mtakatifu wa Bwana John Paul!.
Mimi binafsi nimeshiba na kuridhika kabisa kwa maelezo na ufafanuzi wa kina, uliojaa nguvu ya Roho Mtakatifu, kuhusiana na maana ya `AMANI YA KRISTO` Bwana akuzidishie na azidi kukutumia,
Amin!.
56. 

Ndugu Bernad,
Namshukuru Mungu pia kama umeridhika kwa maelezo na ufafanuzi nilioutoa kuhusu AMANI YA KRISTO.
Tuzidi kuombeana katika safari hii ya mbinguni.
57. 

Bwana wetu Yesu apewe sifa,Asante sana kwa kuweka mjadala huu Mungu awabariki sana.Wapo watu wengi hujiuliza na kuuliza wenzao hata kulaumu kuhusu jinsi wakristo wanavyo msifu na kumtukuza Mungu wao kwa nyimbo.Mimi kwa maoni yangu MUZIKI AU BEATS ZOTE KWA LUGHA ZOTE KWA NCHI ZOTE HAZINA MIPAKA WA KUMSIFU NA KUMTUZA MUNGU.Hakuna asili ya miziki wa Injili, wakristo wanaimba kulingana na utamaduni wa nchi zao,mfano watu wa Jamaica wanaimba kwa mtindo wa reggae au wafrika ya kusini wanaimba kulingana na utamaduni wao,hapo huwezi kumkosoa mtu eti ametumia mdundo usiofaa au unafaa.Wakati Bwana wetu Yesu Kristo alikua hapa duniani hakusema kwamba eti kwenye masinagogi mtakua mukimsifu kwa kumwimbia Mungu kwa mdundo huu…kama tunavyo soma katika Maandiko Matakatifu kwamba Mfalme Daudi alimuimbia na kumchezea Mungu hapo hatujui ni mdundo wa aina gani alioutumia. Kwa hiyo wakristo tusiende mbali kama sisi wanadamu tunayo mambo mengi yanayo tutofautisha na mifumo tofauti,nilazima tuseme hawa au wale hawafae kumsifu au kumtukuza Mungu hivo.Asanteni sana, mubarikiwe…
58. 

Baraka kwenu
Ningefurahi saana kama Bw Stev angeorodhesha kabisa ni aina gani ya miziki inatakiwa itumike makanisani kuliko kuunyesha tu ninamna gani miziki haifai,
Mwishoni umesema tujitahidi kujadili kwakuzingatia Neno au Biblia lakini wewe umezungumza sana kutokana na mtizamo wako uzoefu wako huoni kwamba unajaribu kuwa selfish na kutoa miongozo ambayo wewe mwenyewe huifuati???
Unapo weka mfano wa Kirk franklin na majibu yake huoni kwamba unaulekeza umma sehemu yakujitizama ambayo sio sahihi kwakuwa Kirk naye ni binadamu kama wewe?
Bw Steve unaweza saana kukosoa sidhani na sina hakika kama unaweza kujikosoa.
Wapendwa kama tungekuwa tunaweza kuwa safi au watakatifu kwanguvu zetu wenyewe ingekuwa haina haja ya Mungu kumtuma Yesu, au Kupata wokovu kwa Neema,simaanishi kwasababu ya hayo tutende dhambi la hasha ila kwa sababu hatuwezi kuwa watakatifu kwanguvu zetu wenyewe ndio maana Yesu akaja Neema ikaja na Roho Mtakatifu yote haya ni kwa ajili ya kutukamilisha.
59. 

Amani, Heshima na Upendo kwenu nyote.
Jinsi ninavyorejea maoni na mafunzo ya wengi ndivyo ninavyojifunza zaidi na zaidi na kisha kujiuliza mengi katika nia ya kutaka kujifunza zaidi na zaidi.
Katika baadhi ya maoni nimeelewa (na kama nimekosea nitaomba kukosolewa na / kuelimishwa) kuwa suala kuu si mahadhi tu, wala ujumbe, bali msanii mwenyewe. Anamaanisha vipi katika analoimba na ni vipi amejitolea kumtumikia MUNGU na si kutengeneza pesa kwa kutumia kivuli cha Nyimbo za Injili.
Swali langu ni kuwa tunapozungumzia msanii tunajumuisha “mfumo” mzima wa utayarishaji mpaka utoaji na upatikanaji wa muziki ama? Ninalomaanisha ni kuwa Je! ni sahihi kwa msanii wa nyimbo za injili kumtumia yeyote asiye MKRISTO katika kuitayarisha na hata kuisambaza kazi yake? (Tukumbuke yaliyoandikwa humu kwenye web hii juu ya kutochangamana na wasioamini). Sasa je! wanamuziki wacheza ala wakiwa si waamini ama mtayarishaji, ama mmiliki wa studio, ama msambazaji, hilo litaweza kuharibu utumishi wa nyimbo hizo za injili? Na kama ndio, kuna yeyote anayeweza kusema kuwa anafanya kazi zake na waamini pekee?
Naendelea kujifunza
60. 

Mungu ni mwema
Asante sana kaka Mubelwa T Bandio kwa maswali,kabla sijajibu nikubaliane nawe kwamba jambo la msingi si mahadhi ya mziki tu bali inategemea ninamna gani msanii amejitoa kwa Mungu nasio kutumia kivuli cha muziki au nyimbo za injili kwa maslahi binafsi,
Msanii anaye muishia Mungu na kumtanguliza katika mambo yake yote Mungu atamuongoza Msanii huyo katika maandalizi ya muziki wake.
Haijalishi atampeleka kwa wapagani au walio okoka ilimladi Mungu anaongoza kokote kule ni sahihi.
Mfano mziki wangu nimerekodia katika studio ya Mchungaji John Said inatambulika kama Hosana Production,Pruducers ni Ozzeey, Norbert na Amour wote wameokoka,
kuna watu wanaukubali mziki wangu nawengine hawaukubali,
kuna wasanii wa injili wamerekodi kwenye Studio za watu ambao hawajaokoka na bado nyimbo zina nguvu ya Mungu ile ile nanyi mnabarikiwa mkisikiliza nyimbo zao hata kujazwa Roho mara watumishi hawa wanapo hudumu.
Msanii ni mtu yeyote anae weza fanya kitu chochote kwakutumia ujuzi, akili, maarifa,kipaji,ubunifu nakazalika.
Mwanzilishi wa sanaa ni Mungu mwenyewe maana anaujuzi wote akili zote, ubunifu wote, vipaji vyote,maarifa yote ndio maana ameumba vyote lakini kwa makusudi mema.
Wanadamu tumepewa sehemu ndogo yakufanya yale tunayo fanya kamwe hatuwezi kufanana na Mungu.
Msanii anaweza kuwa mtu mbaya yaani muovu au mtu mwema ilimladi anasifa nilizozitaja hapo juu huyo ni msanii ndio maana hata matapeli tunawaita wasanii kwasababu wametumia akili, ubunifu,ujuzi,maarifa hadi waka fanikiwa azima yao.
Nisahihi kabisa kwa msanii wa injili kufanya kazi na mtu yeyote awe mkristo au la. MLADI TU MUNGU ANAMUONGOZA KUFANYA HIVYO.
MBARIKIWE NA MNAZARETI ALIYE FUFUKA TOKA KWA WAFU.
61. 

Asante saana Ndg Pona. Nafurahia maelezo ya mtu anayefanya kinachozungumziwa na ama anayekitambua vema. Huu ni uelimishaji ambao nimekuwa nikitafuta kuweka bayana dhana hii. Nakumbuka kuna walioandika kuwa “tusichangamane na wenye dhambi/ ambao hawajaokoka” nami nikajiuliza kama nikimualika ambaye hajaokoka anipigie bass guitar naweza kuwa nimetengua wokovu wa kazi yangu? Nashukuru kwa majibu yako na NAENDELEA KUJIFUNZA ZAIDI
62. 

ninapenda kuwashukuru woote mlisema chochote katika mada hii Mungu awabariki. mimi ninadhani kwamba Roho Mtakatifu ndo wa muhimu maana , nikiwa na maana kuwa mahusiano na Mungu yakoje yeye ndiye aongozaye mambo yoote, kwa hiyo haijalishi beat ikoje , wimbo ukiimbwa na mtu aliye jaa roho watu watabarikiwa na mtu asiyeongozwa na roho aimbe kwa beat tunayodhani kuwa ni ya kitakatifu nadhani watu wataguna . la msingi ni maisha matakatifu siyo beat . nimeona wahindi waliookoka wakimwinua Mungu kwa beat za kihindi , je hao tutasema hawajaokoka ? si hao tu. nimeona pia waarabu. n.k
mbarikiwe.
63. 
Tarehe 29/3/2009, niliahidi kwamba ningeandaa maelezo/somo fulani juu ya mada hii. Na sasa wakati tunaendelea kusubiri jibu kutoka kwa ndugu Pona kwenye swali aliloulizwa na ndugu Mubelwa, ninaomba tutafakari yafuatayo ambayo ndiyo mwanzo wa maelezo ambayo niliahidi ningeyaandaa.
Tuendelee…..
Binaadamu ana milango mitano [5] ya fahamu katika ulimwengu wa vitu vinavyoonekana. Milango hii ni KUONA, KUONJA, KUNUSA, KUGUSA na KUSIKIA. Na kila mlango wa fahamu hutafsiri vionjo wa kitu husika katika mlango huo:
Kwa macho tunaweza kuona kitu na kutoa maamuzi kwamba kitu hicho ni kizuri au kibaya, kwamba hakifai au kinafaa kwa namna moja au nyingine, kutokana na mazingira, wakati, umri nk.
Kwa ulimi tunaweza kuonja kitu na kutambuwa kuwa ladha yake ni mbaya au nzuri kwamba inafaa au haifai kwa namna moja au nyingine.
Kwa pua tunaweza kunusa harufu fulani na kutambuwa kabisa kwamba harufu hii ni nzuri au mbaya, ni ya kitu chema au ni ya kitu kilichooza au kuharibika nk.
Kwa kugusa tunaweza kupambanua kama kitu tulichogusa kina hali gani; kwamba ni cha baridi,ni cha moto, ni kikavu, ni laini,ni smooth au rough na hivyo kukifanya kifae au kisifae katika matumizi fulani na fulani.
Kutokana na ukweli huo kwa milango hiyo minne ya fahamu, mimi naamini huo ndio ukweli pia hata kwa mlango wa tano wa fahamu ambao ni KUSIKIA:
Kwa masikio tunaweza kusikia na kutambuwa kwamba sauti/mlio tunaosikia ni wa furaha, ni wa huzuni, ni wa kanisani, ni wa msikitini, ni wa gari, ni wa pikipiki, ni wa kihuni, ni wa kiungwana, ni wa vitani, ni wa maombolezo nk.
Musa, mtumishi wa Mungu alipokuwa akishuka kutoka mlimani alisikia sauti/mlio ambao ulikuwa ukitoka kwa wana wa Israel baada ya kutengeneza yule ndama kuwa kama ndiye mungu wao. Aliposikia sauti hiyo alijiuliza uliza kuhusu sauti hiyo kama ifuatavyo: “Hiyo si sauti ya watu wapigao kelele kwa sababu ya kushinda vitani, wala si sauti ya watu wapigao kelele kwa sababu ya kushindwa, bali kelele za watu waimbao ndizo nazisikia mimi” [Kutoka 32:18]. Si maneno yaliyomfanya atambuwe hilo bali ni sauti tu! Hivi ndivyo masikio yanatakiwa yafanye kazi, yaweze kupambanua kwamba sauti/mlio unaosikika unaashiria jambo fulani. Kwa maana hiyo sauti/mlio wenyewe unatosha kufanya mtu atambuwe sauti/mlio huo unahusiana na kitu gani. Masikio ambayo hayawezi kupambanua sauti/mlio yatakuwa na tatizo.
Muziki hutoa sauti/mlio ambao huweza kuwa na maana fulani. Mfano, Kuna muziki wa ala tupu [intrumental] ambao huweza kupigwa maeneo fulani kutokana na jinsi muziki huo ulivyotengenezwa. Ni mara nyingi hutokea kukuta watu wanapiga muziki fulani wa ala ambao huwachanganya wasikilizaji kwa kuwa hauendani na sehemu hiyo. Ambacho hutakiwa kufanyika ni kubadilisha na kupiga muziki unaoendana na sehemu/function hiyo.
Linapokuja suala la kanisani hatutakiwi kuupinga ukweli huu. Kwamba kwa kuwa ni kanisani basi piga muziki wowote, pasipo kujali! Ikitokea hivi hapa kutakuwa na mambo mawili: Yawezekana
1. Masiko yetu hayawezi kupambanua vionjo vya muziki, au
2. Tunalazimisha muziki wowote upigwe kanisani kwa maslahi binafsi, kama vile kutimiza tamaa zetu wenyewe!
Suala la kuzingatia katika mada hii ni kwamba muziki ni zaidi ya beat. Beat beat ni MDUNDO. Na hili tulishalizungumzia na ndg Mubelwa, tukakubaliana.
Kama vile kuona, kugusa, kuonja na kunusa vina vionjo vyake na tunaviheshimu vionjo hivyo, vivyo hivyo inatakiwa kuviheshimu vionjo vya kusikia. Macho hutuogonza tusije jikwaa au kugonga vitu na faida zingine nyingi, Ulimi hutuepusha tusile vitu vibaya na mambo mengine mengi, Pua hutuelekeza inapotokea kuna harufu mbaya na kwa sababu hiyo, kwa mfano, tunaweza kusafisha mazingira yetu yakawa safi na faida zingine, Ngozi hututahadharisha kwamba tulishogusa si kitu chema ili tukiepuke na mambo mengine mengi. Hali kadhalika Maskio yetu yana uwezo wa kutuongoza kutokana na sauti tunazisikia kwamba zinahusiana na kanisani au kilabuni kwenye pombe, zinahusiana na msibani au kwenye sherehe na mambo mengine mengi, kwamba zinahusiana na Mungu au Shetani ili tuweze kukimbia toka kwa Shetani na kuelekea kwa Mungu, kwenye usalama wetu!
Kwa leo naishia hapa. Maelezo haya yataendelea. Lakini kabla ya kuendelea kama kuna swali linakaribiswa ili tuweze kwenda wote pamoja!
Tuendelee kujifunza.
64. 

Nianze kwa kuwashukuru na kuwapongeza wapendwa waliojadili mada hii kwa kina sana hapo juu.
Ingawa ni mgeni kidogo katika blog hii, nasukumwa kusema kitu kuhusiana na mada hii ambayo kwa kweli ni mhimu na inagusa sana mrengo wa imani na matendo ya dini ya Kikristo. Nimekuwa nikifanya uchunguzi (Research) kwa muda sasa nikilenga kugundua ni gani hasa ya mziki upigwe kanisani?
Na pengine niwakumbushe wapendwa waliotangulia kujadili kuwa tunapojiuliza swali hili ni vema pia kujiuliza kuwa: Ni nini chanzo (nature) ya miziki ambayo inapigwa makanisani ambayo tunaitilia shaka?
Haya ni baadhi ya matokeo au majibu ya uchunguzi wangu:
- Hakuna identity ya mziki wa kanisani tangu zama za mababu na hata leo.Hii ni kutokana na ukweli kwamba kila ametokana na kabila lake, taifa au nchi yake kwanza kabla hajawa mkristo. Mfano: Sisi tumekuwa wa Tanzania kwanza kabla hatujawa Wakristo; na zaidi ya hapa tumekuwa na makabila yetu kwanza kabla hatujawa wa Tanzania. Kwa hali hii, maisha tunayoishi, na mambo tunayoyafanya hayatokani na new identity yetu baada ya kuamini, bali na utu wetu wa asili kama wa Tanzania na watu wa kabila mbalimbali.
Ikumbukwe kwamba: mziki haujaanzia kanisani, ulianza zamani sana katika jamii zetu. Katika Biblia tunasoma mziki ulianza na Yubali aliyekuwa baba wa wapiga vinubi katika Mwanzo 4:21. Lakini hata hivyo historia inaonyesha kuwa Yubali pia hakupiga mziki ambao tungeweza kuuita mziki wa kiMungu pengine! Bali alipiga mziki wa kitaifa/kiukoo na kabila la Israeli japokuwa alimtaja Yahweh/Mungu katika lyrics/mashairi yake.
Kila mwimbaji wa nyimbo za injili anafanya sawa na Yubali. Wote huimba nyimbo za Injili lakini kwa kuongozwa na Haiba ya kabila au utamaduni fulani. Na zaidi kwa waimbaji wa Tanzania huvutiwa na styles za nchi za magharibi kama rock n roll, reggae n.k.Lakini pia hata wasipoiga miziki hiyo bado wataimba kutokana na tamaduni za makabila yao ambazo sio lazima kuwa zinakubalika na Mungu.
Sasa basi: Wito wangu ni kwamba tunapofikiri juu ya mziki wa kanisani na wakidunia, tufikiri juu ya namna ambayo tunaweza ku- CONTEXTUALIZE neno la Mungu na kuli- articulate katika context yetu ya Kitanzania kupitia mziki ili tupate Haiba ya mziki halisi wa kanisani. (samahani kwa kutumia maneno ya Kiingereza, sijaweza kupata kwa haraka maneno mazuri ya kiswahili: unaweza kufasiri). Ninadhani kosa wanalolifanya waimbaji wetu wa mziki wa Injili ni KULE KUIGA (KU- PHOTOCOPY) mziki au styles za waimbaji maarufu na kuziingiza kanisani.Waimbaji wengine hawamjui Mungu lakini styles za miziki yao ipo kanisani, na inawakera sana Wakristo, hasa mimi. Kwa mfano Miziki ya Rock & Roll asili yake ni miziki ya kishetani maana watunzi wake walipata uwezo wa kutunga na kucheza kupitia nguvu za kishetani (Devil worshippers).
Na ukweli ni kwamba, hata kama waimbaji wetu watabadilisha maneno katika miziki yao, bado wataendelea kumtukuza na kumuenzi mwanzilishi wa style hiyo. Na kwa kesi kama hii ni kutukuza shetani aliyewapa uwezo wa kubuni style hizo. Ni hatari na tunapaswa kuwa makini sana.
Ninaamini kuwa Mungu amempa kila mwanadamu uwezo wa kufanya jambo la msingi na la kipekee tofauti kabisa na mwanadamu mwingine. Waimbaji wa mziki wa Injili wanapaswa kumwomba Mungu awasaidie kutunga mziki ambao yeye Mungu mwenyewe atauanzisha kwao na sio kuiga.
Kama ambavyo wengine husema, leo niishie hapa. Asante sana wanablog hii Mungu awabariki sana. Nitafurahi sana kupokea maswali kuhusiana na nilichokisema. Na pia kukosolewa…
Tubarikiwe:)
65. 

Asante saana Cloud.
Labda nami nisubiri wale wenye kuamini kuwa kuna AINA YA MUZIKI UNAOFAA MAKANISANI waorodheshe aina hizo hapa ili kuwekana bayana kwani wapo wanaopinga matumizi kama Reggae (ambayo ni asili ya Carribbean) ama midundo ya asili ya Kikongo, ama Hip Hop ambayo yote ina asili lakini kwetu (Tanzania) yachukuliwa kama ya ki-Dunia.
Blessings
66. 

Ndugu Cloud,
Binafsi nimefurahia uchambuzi ulioufanya. Na hasa nimefurahishwa na maneno yafuatayo:
“Waimbaji wengine hawamjui Mungu lakini styles za miziki yao ipo kanisani, na inawakera sana Wakristo, hasa mimi. Kwa mfano Miziki ya Rock & Roll asili yake ni miziki ya kishetani maana watunzi wake walipata uwezo wa kutunga na kucheza kupitia nguvu za kishetani (Devil worshippers).”
Kwa maneno yako hayo naona unaweka wazo kwamba kuna aina ya muziki ambayo haifai kuwepo makanisani kutokana na namna ilivyopatikana. Katika kuelezea hilo umetoa mfano wa Rock & Roll ambayo ilipatikana kwa kutumia nguvu za shetani. Na hapo ndipo kwenye shina la mjadala: kuzianisha aina hizo za muziki, kama inawezekana, ambazo kwa sababu moja au nyingine hazifai kutumiwa kwenye muziki wa injili.
Lakini kabla ya kuendelea ninaomba ufafanue kidogo unamaanisha nini unaposema muziki haukuanzia kanisani?…yaani kanisa umelichukulia kama kitu gani? Nitafurahi sana kupata ufafanuzi huo ili niweze kukupata vizuri.
Kuna mengine kadhaa ambayo ningependa tujadiliane. Lakini naona tukianza na hili moja itakuwa vizuri tu ili twende hatua kwa hatua. Na kwa kuwa umesema utafurahi kuulizwa maswali na hata kukosolewa ninaamini utakuwepo kwa ajili ya kujibu maswali yote yatakaojitokeza kutokana na maelezo yako. Ukiingia mitini haitaleta maana yoyote!
67. 

Naona majibu ya aina mbili hapa. Binafsi nasema AINA ZOTE ZINAFAA KUTUMIKA KANISANI na kuna ambao wanasema SI AINA ZOTE ZINAZOFAA KUTUMIKA KANISANI.
Bado nawakilisha ombi langu kuwa TUREJEE KWENYE SWALI LINALOULIZA “AINA GANI YA MUZIKI WAINJILI UNAFAA MAKANISANI?”
Na kwa wale wanaopinga kutumika kwa aina zote ama nyingi, basi waorodheshe aina wanazoamini ZINAFAA na watuelimishe ni kwanini wanaamini zinafaa. Binafsi litanisaidia zaidi kuliko maelezo ya kuwa si miziki yote inafaa ilhali hawasemi ni miziki gani inayofaa.
Blessings
68. 

Ninavyofahamu mimi maswali magumu hayana majibu rahisi. Suala hili na muziki ni moja ya mambo magumu kwa hiyo jibu lake haliwezi kuwa rahisi kama, kwa mfano, jibu la swali la mtu kuulizwa utaje jina lako. Suala la muziki ni suala la vizazi na vizazi na limechanganyikana na mambo mengi. Imani, Utamaduni, mapokeo, ustaarabu nk. Kwa hiyo linahitaji mjadala mrefu na katika kujadili huko naamini tunaweza kupata vigezo vinavyoweza kusaidia kuanisha aina hizo.
Kadri mjadala unavyoendelea yawezekana tukaja gundua labda aina zote za muziki zinafaa; au baadhi tu ndiyo zinafaa au pengine muziki wowote haufai makanisani. Ninasema hivi kwa sababu kuna baadhi ya watu wanaamini kwamba kanisani hapatakiwi kupigwa muziki wowote bali ni kuimba tu! Kwa hiyo nafikiri kinachotakiwa ni kuwa na uvumulivu, huku kila mtu akijitahidi kuweka aliyo nayo kwa ajili ya kuchangia mada hii, kwa upole kabisa na kwa kutambua kwamba mada hii ni nzito kwa hiyo inahitaji mchanganuo wa mambo mengi.
Natumaini kwa pamoja tunaweza kupata jibu linalofaa!
Ninasubiri majibu kutoka kwa ndugu Cloud ili niendelee kumuuliza niliyonayo kutokana na mchango wake!
69. 

That’s what i thought.
70. 

Ni kweli Ndg John kuwa yawezekana kuna ugumu hapa (kulingana na tafsiri yako).
Lakini haimaanishi kuwa mpaka sasa huna hata aina moja ya muziki unayoamini inafaa. Ningependa u-mention hiyo ama hizo ambazo so far unadhani zinafaa na kisha utuambie ni kwanini (KWA NUKUU ZA BIBLIA) unaamini zinafaa na kama huna aina unayoamini inafaa nalo pia liweke wazi.
NASUBIRI MAJIBU TOKA KWAKO KAMA USUBIRIVYO YA CLOUD
71. 

Mungu ni mkuu sana na tena anastahikhi heshima. Kwa hali hiyo kuimba ni vyema waimbaji wakajua wajibu wao wa kutimiza kusudi la Mungu kwa kuimba yaani MAPENZI YA MUNGU YATIMIZWE KAMA ILIVYO MBINGUNI NA HAPA DUNIANI.
kinacho nisikitisha ni pale waimbaji wanapoingia katika mtindo wa Bongo beat uwepo wa Mungu unaondoka kabisa haswa pale waimbaji nyimbo zao zinageukia katika usanii na rusha roho.
najua kama waimbaji watajipanga vyema watu wote wataokolewa na nchi yetu itakuwa na amani. WAIMBAJI NI WAHUBIRI WAKUBWA SANA LAKINI KWA LEO HAWAIMBI KUMTUKUZA MUNGU AU KUPELLEKA UJUMBE BALI WANAJIWAKILISHA WENYEWE HASWA NYIMBO ZA VIDEO SIKU HIZI HAKUNA TENA KUSIFU NA KUABUDU BALI KUNA KUCHEZA NA KUIMBA TUU
KWA HALI HIYO WENGI TUNASHABIKIA MINENGUO NA SURA ZILIZO CHUBULIWA NA KUWEKWA RANGI ZA AJABU NA NYWELE ZA BANDIA NA MAVAZI YA MITINDO.
WAPAGANI WASIO MJUA MUNGU WETU HAWATA BADILIKA TENA. INJILI INAKUWA NGUMU SANA TUNAPO SHUHUDIA MITAANI
NADHANI WAIMBAJI WANATAKIWA WAJUE KUWA LuCIFER ALIKUWA KIONGOZI WA SIFA MBINGUNI NA NDO MAANA ALIPO JIINUA AKATUPWA CHINI MPAKA SASA ULIMWENGU UNATESEKA NA WAIMBAJI WANACHEZA KWENYE FANI YA LUCIFER
NAOMBA WATENGENEZE MIOYO YAO NA KUMPA MUNGU UTUKUFU. NASHANGAA MPAKA SASA NYIMBO ZA SIFA ZINAWEKEWA HAKI MILIKI. WATU WANAPELEKANA MAHAKAMANI KWA KUIBIANA NYIMBO MH TUNAKWENDA WAPI WAPENDWA? MWIMBIENI BWANA KWA MIOYO YENU YOTE.
AAAAAAAACHA BWANA AKUINUE UTAPEWA HAKI YAKO TUU UKIMWINUA BWANA
72. 

Shalom watumishi wa Mungu.
Kimsingi ninapenda kumshukuru Mungu kwa Mwanzilishi wa Mada hii, maana nimekuwa nikitaabishwa sana Moyoni Mwangu na jinsi huo unaoitwa Muziki wa Injili ulivyo. Namshukuru Mungu pia kwa ajili ya kaka Steve M. ambaye amechambua vizuri na kuweka mifano ambayo imenifundisha na kunichekesha pia..
Nikirudi kwenye Mada Husika, nadhani hapa kuna mambo kadhaa ya kuyatazama.
1. kwanza ninapenda kukubaliana na kaka Steve Kuuita muziki huu Muziki wa Kumsifu Mungu na si Muziki wa Injili.
2. Pili, Muziki wowote wa kumsifu Mungu msingi wake
ni hali ya kiroho ya Muimbaji mwenyewe, nikimaanisha kuanzia mpiga vyombo na yule anayeimba. Kimsingi biblia imetuwekea wazi kuwa waabuduo wanapaswa kumwabudu mungu katika Roho na kweli. Maana yake ni kwamba watu hawa ni lazima wawe na Spiritual connection na Mungu wanayemuabudu, Wakiutambua ukuu na utukufu alionao kwa kiwango cha kuvutwa na kumwabudu katika roho na kweli.
3. Muziki wa kumsifu Mungu unajengwa pia katika msingi wa neno la Mungu. Kiasi cha neno la Mungu kilicho ndani ya Mtu ndicho kinachojenga msingi wa Imani ya Mtu na imani hiyo ndiyo inamsukuma mtu kumsifu Mungu kwa jinsi anavyoamini.
3 Biblia pia katika 1wakorintho 10:31 imeweka wazi kuwa,Watoto wa Mungu wanapaswa kufanya kila jambo KWA UTUKUFU WA MUNGU. maana rahisi ya hili ni kwamba, kama mtoto wa mungu ni lazima uweze kufanya judgement ya Motives zako, unafanya muziki huo kwa sababu gani? is it for the glory of God?
4. Mwanadamu ni Roho iliyo na nafsi, inayoishi katika mwili. kupitia Nafsi, roho ya mwanadamu inakuwa na connection na ulimwengu pale mtu anapokuwa self centered, akiishi katika tamaa za mwili. lakini pia kupitia nafsi roho ya mwanadamu inakuwa na connection na Mungu pale Yesu anapokuwa the center of your life. kwa jinsi hii roho ya mtu inakuwa na connection na Mungu na mtu anaishi katika Roho.Whether JESUS is the Center of Your Life or YOURSELF is the center of your life matters a lot katika uimbaji wa nyimbo za kumsifu Mungu pamoja na ala zake.
5.Uzuri wa nyimbo za kumsifu Mungu hauwezi kupimwa kwa vile ulivyopigwa, ila unapimwa kwa ile Nguvu ya Mungu na utiisho unaoambatana na wimbo ule kwa kiasi cha kuwavuta watu kunyenyekea mbele za Mungu na Kumwabudu katika Roho na kweli, au kuzijutia dhambi na kumtafuta Mungu kwa upya.
MATATIZO YALIYPO KATIKA NYIMBO ZINAZOITWA ZA INJILI.
Si kusudi langu Kuhukumu uimbaji wa watumishi wa Mungu, ila ninataka kuweka wazi yale ambayo ninayaona kutokana na aina ya Muziki uliopo na jinsi unavyopigwa.
1. Muziki wa sasa umekosa nguvu ya Mungu na wala hauwavuti watu tena kumrudia wala kumwabudu mungu. hii ni kutokana na waimbaji wenyewe kutokuwa sawa kiroho, pia ala/midundo ya Muziki kupigwa na watu wasiomjua Mungu na hivyo ndani yao hakuna uchaji. wanatoa kile nafsi zao zilichonacho ambacho ni tamaa zao binafsi. hii ndio sababu ni kawaida sana sasahivi kusikia wimbo wa injili ukipigwa kwenye baa na watu wakiendelea kulewa na matendo mengine ya anasa pasipo kushituka.
2. Wasanii wengi hawajui neno la Mungu, na kama wanajua, hawachukui muda wa kutosha kutafakari maana halisi ya wanachojua katika maisha ya watu. ikumbukwe, uimbaji, kama uinjilisti, ualimu na uchungaji ni huduma inayohitaji maandalizi binafsi, mtu anatakiwa kujifunza neno, kukaa na kutafakari, kumwomba Mungu ampe nyimbo za kweli zitokazo kwake, zenye nguvu ya kuwavuta watu kwa Mungu.
Wasanii wengi hawafanyi hili, wanakurupuka na kuimba nyimbo zitokazo katika akili zao na si katika msingi wa kujua neno la Mungu. unasikia mtu anaimba “acha tuteseke, ulimwengu ututese, watu watusimange, watunenee mabaya,……… tutaendelea kumfuata Yesu” Maneno ambayo yanaleta Negative Faith kwa watu wachanga, inawafanya waone kama kumtumikia Mungu ni mateso juu ya mateso, Biblia imeweka wazi kuwa “Njia za mtu zikimpendeza Mungu, hata adui zake Humpatanisha nao”, tena inasema “uzima na mauti vimo katika uweza wa ulimi”. You dont need to confess any negative thing in your life, kwa nini uconfess kuteseka na kusengenywa?.
Mtu wa jinsi hii akiteseka na kusimangwa atakwenda analia kwa Mungu? sasa watu wengi wanavutwa na midundo, lakini msingi mzima upo katika neno la Mungu na nguvu ya Mungu inayoambatana na wimbo Husika. Nyimbo za kumsifu Mungu si za kufanyia ushabiki na kuhangaika na midundo, zinahitaji hekima ya Mungu kutambua usikilize nini, kwa kuwa tumeshaambiwa “Imani chanzo chake ni kusikia” Warumi 10:17.
3. Kimsingi ninachojua ni kwamba, Kuanzia uimbaji hadi upigaji wa vyombo vya Muziki wa kumsifu Mungu kunahitaji watu wanaomjua Mungu na wenye kicho cha kweli, haiwezekani Muimbaji akawa ni mtu aliyeokoka mwenye kicho cha kweli, akapigiwa ala na Mtu asiyemjua Mungu asiye na kicho cha kweli na mwenye kuongozwa na tamaa za mwili wake, hapa kuna conflict Kubwa na ndipo matatizo mengi katika muziki wa ijili yalipotokea. Biblia imeweka wazi kabisa kwamba “Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya Roho”I Wakorintho 2:14. anawezaje mtu wa jinsi hii kukupigia ala za Muziki utakaOumsifu Mungu? Motives zake si sahihi na wala ndani yake hamna hofu ya Mungu.
Kimsingi naguswa sana na uimbaji wa Marehemu Fanuel Sedekia. haiwezekani ukapita kwenye Baa ukasikia wanapiga nyimbo kama Manukato, na nyimbo zake nyingine katika album ile, the same applies katika album yake inayoitwa “katika ibada”
Kioo cha kupima Muziki wa Kumsifu Mungu ni neno la Mungu lakini pia ni nguvu ya Mungu inayoambatana na Muziki huo, Mungu atupe hekima ya kujua kinachoendelea katika Muziki uliopo nyakati zetu.
Mungu awabariki.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni