Ijumaa, 7 Juni 2013

USHUHUDA MKUBWA WA DINI

Dini

Dini alikuwa mtoto mkubwa aliyetangulia kuzaliwa katika familia yake. Kwa miaka kumi na mbili Dini mara nyingi alikuwa ni mtoto aliyependwa na kuwa karibu zaidi na baba yake, mpaka pale alipokufa ghafla. Akajisikia vibaya sana hali iliyomfanya kuhisia hasira hasa pale alipogundua kwamba marehemu baba yake wakati wa uhai wake alikuwa akitembea na mama yake mdogo na alimwacha akiwa mja mzito. Na wakati huo huo akagundua ya kuwa mama yake pia alikuwa na ujauzito wa baba yake.
Mama yake Dini akiwa mjane mwenye mahangaiko mengi aliamua kuwapeleka watoto wake watatu wa mwisho katika kituo cha watoto yatima. Mama huyu pia alilazimika kuuza vitu vyake vya thamani ili familia walau iweze kupata fedha ya kununulia chakula. Baada ya miaka minne ndugu wa kifamilia alimwambia kuwa mama yake Dini angeolewa katika siku za karibuni. Dini aliumizwa sana na jambo lile na hakuweza kuelewa kabisa kwa nini mama yake hakuwa amemwambia mwenyewe kuhusu jambo lile. Alijihisi kuwa hakuwa na mtu yeyote ambaye angeweza kumtegemea tena tangu baba yake alipomvunja moyo, na sasa mama yake amefanya jambo lile lile la kumkatisha tamaa.
Dini akawa rafiki wa wafanya fujo shuleni kwake na hivyo akawa mkaidi bila utiifu pale shuleni. Alitoroka shule, hakuvaa sare ya shule, na alipenda sana kupigana pigana ovyo. Baada ya marafiki zake wachache kukutana na matatizo mengi, Dini akaanza kujiuliza maswali: “Je, mimi ninatafuta nini maishani mwangu? Je maisha ni nini kwangu? Sheria za dini hazijanifanya niwe na furaha. Hata hivyo, maisha huru bila ya sheria za kidini si kitu ambacho ninakitaka pia.”
Mwezi wa Ramadhani ulipofika Dini akafanya bidii na kuwa na juhudi na matendo ya kidini ili kuweza kuitimiliza saumu ya Ramadhani vema kama vile kufunga na kuomba. Usiku mmoja, wakati wa Ramadhani, aliamua kuomba ombi la TAHAJUDI. Ombi hili la TAHAJUDI halimo miongoni mwa zile sala tano zinazotakiwa kila siku. Sala hii inatakiwa kufanyika usiku wa manane tu, na hasa ni dua ya kumwomba Mungu akupe ishara fulani. Dini alitega saa yake ili iweze kumwamsha wakati alipotaka aamke ili aombe. Akasema: “Nilikuwa na imani kubwa kiasi kwamba chochote kile ambacho ningelimwomba Mungu usiku ule, Mungu angeliweza kunisikiliza na kunipatia jibu.” Mwishoni mwa sala yake ya kukaririwa, alilia sana na kumlilia Mungu na kusema: “Mungu, nimechanganyikiwa, nasema nimechanganyikiwa kweli kuhusu njia yangu ya kupendeza mapenzi yako. ” Akaendelea tena: “Mungu, kama ukipenda mimi niishi katika sheria zako, basi naomba sana usiku wa leo nioneshe njia sahihi ya kuifuata nia yako. Ila Mungu, usiponionesha niache mimi niishe katika maisha yale niyapendayo mimi. Na wakati huo sitajali tena sheria zile za kidini. Na kama nitakufa usinipeleke jahanamu. Kwa sababu wewe hukunionesha njia ya kweli! Si haki niende jahanamu, Mungu. Kwa kuwa hujawahi kunionesha njia sahihi. Mungu, ninachotaka ni kuoneshwa njia sahihi usiku huu. Nitaishi maisha utakayonionesha.”
Mara mwanga ulitokea na Dini akamwona mtu akisimama mbele yake. Mtu huyo alikuwa amevaa kanzu nyeupe lakini hata hivyo hakuweza kuiona sura yake vizuri. Hajui ni kwa vipi lakini alimtambua kuwa mtu yule ni Isa. Mtu huyo akasema: “Nifuate,” akachanganyikiwa na kuwaza, kisha akasema: “Bwana, mimi ni Mwislamu. Je nitawezaje kukufuata wewe?” Aliweza pia kuuliza maswali kadhaa kwani alishangaa sana ni kwa jinsi gani yeye Mwislamu angeweza kumfuata Mungu wa Wakristo. Akasikia sauti nyingine ikisema: “Huwezi kabisa kumfuata huyo! Achana kabisa na maombi yako! Sahau nia yako ya kupata maisha mazuri!” Lakini alipomtazama yule mtu aliyevaa kanzu nyeupe, alijisikia mwenye amani na utulivu mwingi. Yesu aliendelea na kusema: “Nifuate,” huku akimnyoshea mikono yake. Dini alihangaika juu ya uamuzi wake lakini hatimaye akasema: “Mungu ikiwa hii ndiyo njia ya kweli, sawa. Ninataka kukufuata wewe.” Mara tu alipomaliza kusema hivyo, alijisikia kuwa na baridi kama vile barafu kifuani mwake. Na ni wakati uleule aliposikia amani ambayo hakuwa amewahi kuwa nayo maishani mwake kabisa. Alisema: “Nilihisi kitu fulani kisichokuwa cha kawaida moyoni mwangu.” Baada ya Dini kuwa Mkristo, alikumbana na mateso mengi kutoka kwenye familia yake. Wakati huo alikuwa na umri wa miaka 17 tu walipomfukuza na kumwambia aondoke nyumbani. Alienda kwenye shule yenye hostel na hivyo aliweza kujitafutia mwenyewe mahitaji yote kwa kufanya kazi katika muda ambao hakutakiwa kuwa darasani. Pia alitafuta kupatana tena na familia yake. Alionesha kuheshimu mila na desturi za kabila lao la Kijava lakini hakukurudi nyuma au kuyumba katika imani yake thabiti kumfuata Kristo. Jaribu kubwa kwake lilikuwa ni kumsamehe marehemu baba yake na kumpokea mdogo wake aliyezaliwa na mama yake mdogo nje ya ndoa! Hata wakati mama yake hakuweza tena kumtunza, Dini alimlea mdogo wake kama mwanawe.
Dini anaendelea kuishi maisha ya kielezo wa “kufanya mambo yote kupitia Kristo anayemtia nguvu”.
















Hakuna maoni:

Chapisha Maoni