Jumamosi, 14 Januari 2017

SOMO: KUNENA KWA LUGHA SEHEMU YA TATU

Mwl : Furaha Amon







KUNENA KWA LUGHA NI KUJIJENGA NAFSI
Yeye anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake, bali ahutubuye hulijenga kanisa. Na mimi nataka ninyi nyote mnene kwa lugha lakini zaidi sana mpate kuhutubu maana yeye ahutubuye ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri ili kanisa lipate kujengwa (1Wakorinto 14:5)
Mkristo anayenena kwa lugha hujijenga nafsi yake na yeye ahutubuye ni mkuu kuliko anenaye kwa lugha kuhutubu maana yake ni kuhutubia au kuhubiri.
Tafsiri nyingine za Biblia neno kutabiri. Hapo ina maana kuwa wakorinto wakati huo baada ya kujazwa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha kama mkristo angesimama kuhubiri kusanyiko, badala ya kuhubiri kwa lugha inayoeleweka kwa wale anaowahubiria ili waelewe mahubiri anayohubiri au kama alikuwa anafundisha neno la Mungu wale wanaomsikiliza waelewe kilichofundishwa, wakorinto baada ya kuhubiri kwa lugha inayoeleweka wao walianza kunena kwa lugha.
Hili jambo huwa linatokea hata leo, tumeona wakristo wamejazwa Roho Mtakatifu wakafurika sana na wakati huo wakatoka kanisani wakaelekea majumbani kwao na walipokutana na watu njiani walishindwa kuongea lugha zinazoeleweka bali kila alipofungua midomo walianza kunena kwa lugha, lakini pia tumeona wakristo wamejazwa Roho Mtakatifu wakaanza kucheka, wengine wakaanza kuimba.
Wakristo wa jinsi hii wanahitaji mafundisho ili wajue kunena kwa lugha matumizi ya hadhara na matumizi ya faragha. Wasipofundishwa wanaweza kuendeleza unenaji wa lugha usiokuwa na utaratibu na hivyo kuleta makwazo.
Ni kweli kabisa Roho Mtakatifu wakati mwingine huwavuvia watu kwa nguvu sana kiasi analazimika kunena kwa lugha tumeona hata wahubiri mbalimbali wanapohubiri mikutano mikubwa ya injili, wakati mwingine wanajikuta wananena kwa lugha japokuwa huithibiti hali hiyo kutokana na kwamba wao wanajua matumizi ya kunena kwa lugha.
Tumeona hata viongozi wa sifa katika ibada mbalimbali wengine wameshindwa kuongoza sifa wakaanza kunena kwa lugha, tumeona hata waumini wanaochaguliwa kuomba sala mbalimbali kanisani kwa niaba yaw engine, wanaomba lakini lakini katikati ya sala zao wameshindwa kuendelea kuomba kwa lugha inayoeleweka badala yake wamenena kwa lugha.
Paulo ilibidi awafundishe wakorintho kwa sababu hali hii ilizidi sana huko korinto. Wakorinto wao waliona sawa tu kwa vile walikuwa hawajafundishwa matumizi ya kunena kwa lugha. Neno la Mungu linasema, yeye anenaye kwa lugha anajijenga nafsi yake, anayehutubu analijenga kanisa. Anayejenga kanisa analifundisha kanisa neno la Mungu, kwa maana hiyo anayehutubu ni mkuu kuliko yeye anayejijenga nafsi yake peke yake. Anayehutubu anafundisha watu wengi wamjue Mungu. Hapa ina maana kuwa wewe umetakiwa kuhutubia badala yake umenena kwa lugha.
Maandiko yamezungumza  vitu vitatu, kuhutubu,kuomba kwa akili na kunena kwa lugha. Maandiko yanaposema yeye AHUTUBUYE ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha. Haina maana kusema yeye AOMBAYE KWA AKILI ni mkuu kuliko anenaye kwa lugha. Maandiko yanasema ahutubuye ni mkuu kuliko anenaye kwa lugha, wakristo wengi wanachanganya sana eneo hili. Anayeomba kwa akili hawezi kuwa mkubwa kuliko anenaye kwa lugha. Anayenena kwa lugha anajijenga nafsi yake mwenyewe na anenaye kwa lugha anasema mambo ya siri kati yake na Mungu. Anayeomba kwa akili hawezi kunufaika na Baraka zinazopatikana katika kunena kwa lugha.
“Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha” (Wakorinto 14:5)
Kuna mafundisho potofu yasemayo kunena kwa lugha si muhimu kwa kila muumini kunena. Viongozi wengine wa dini wamekuwa wakiwazuwia wakristo wanapojazwa Roho Mtakatifu wasinene kwa lugha.
Maandiko yanawakataza wale wanaozuia wakristo kunena kwa lugha, wasizuwie kwa sababu kunena kwa lugha ni muhimu. Mkristo anayeomba kwa akili hawezi kujijenga nafsi yake, wala hawezi kusema mambo ya siri kati yake na Mungu. Hivyo maandiko yanasisitiza kuwa;-
“Wala msizuwie kunena kwa lugha” (1 Wakorinto 14:39)
Kunena kwa lugha ni muhimu sana kwa kila muumini, Wakristo ambao wamekataa kuliwekea kipaumbele jambo hili wana hasara kubwa. Biblia inasema
Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu,kusema Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu (1 Wakorinto 12:3)
Kwa maana hiyo katika kunena kwa lugha hakuwezi kumfanya mnenaji kulaani badala ya kubariki.
HATUJUI KUOMBA
“Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo: lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa” (Warumi 8:26).
Kama tulivyotangulia kusema kwamba Roho Mtakatifu anazifanya kazi zake zote kupitia karama tisa. Roho mtakatifu hutuombea kupitia karama hii ya kunena kwa lugha. Roho Mtakatifu hutuombea kwa sababu sisi hatujui hatujui kuomba, wakristo wengi husema kuwa wao wanajua kuomba sana. Lakini Mungu anajua kuwa sisi hatujui kuomba ndiyo maana Mungu akaweka kazi mojawapo ya Roho Mtakatifu iwe ni kutuombea. Paulo alijua hili ndiyo maana alikuwa ananena kwa lugha kuliko wengine maana yake alikuwa anampa Roho Mtakatifu muda mwingi wa kumwombea.
Wanadamu tuna mipaka ya kuelewa mambo yanayotukia hapa duniani. Huwezi kuelewa mambo yote yanayotokea hapa duniani kwa wakati huo; wanadamu tuna ukomo wa kuelewa. Huwezi kuelewa mambo yatakayotokea wakati ujao; huwezi kuelewa mambo yaliyotokea huko nyuma kabla ya kuzaliwa, huwezi kuelewa mambo yaliyoko katika ulimwengu war oho; huwezi ukaelewa mambo ambayo shetani amekupangia katika ulimwengu wa roho.
Ufahamu wa binadamu una mipaka kutokana na mwili. Mwili ndiyo unaotuwekea mipaka. Roho Mtakatifu yeye hana mipaka. Yeye ni Roho anao uwezo wa kujua mambo yajayo; yanayotendeka wakati huu duniani kote na anajua yaliyotendeka duniani huko nyuma. Kutokana na hili wewe ukiomba kwa ufahamu wako kwa akili zako. Hutaweza kuombea zile shida za muhimu kulingana na uhitaji wako.
Mfano unapoombea siku ya kesho unaombea mambo yaliyo katika ufahamu wako. Hivyo hutajua mambo mengine mengi ambayo shetani ameyapanga kukufanyia siku hiyo ya kesho. Lakini Roho Mtakatifu anajua mitego yote ambayo shetani amepanga kukufanyia siku hiyo ya kesho. Lakini Roho mtakatifu anajua mitego yote ambayo shetani amekutegeshea, ukiomba katika Roho Mtakatifu, atakuombea kwa ajili ya mitego hiyo ya shetani ili Mungu atume Malaika wake ili aitegue mitego hiyo ya shetani. Biblia inasema;-
“Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu” (Warumi 8:27)
Maombi ya Roho Mtakatifu ndiyo maombi ambayo yanampendeza Mungu, Roho mtakatifu yeye anamjua Mungu,maana ametokana na Mungu, hivyo anajua ni jinsi gani Mungu anapenda. Ili maombi yako yawe na uhakika kwa asilimia mia 100% kwamba yamempendeza Mungu basi ni katika kuomba kwa Roho Mtakatifu. Najua unafahamu kwamba kuna aina saba za maombi kwa watakatifu ambayo ni
1.  Kuomba kwa imani
2.  Kuomba kwa jina la Yesu
3.  Kuomba kwa ahadi za Mungu
4.  Maombi ya mapatano
5.  Maombi ya Roho Mtakatifu
6.  Maombi ya kufunga
7.  Kuomba bila kukoma
Kila aina ya kuomba inatakiwa tuitumie, kwa sababu kuna shida nyingine haziwezekani katika aina fulani ya maombi bali inawezekana katika milango mingine. Hivyo kuna mahitaji mengi sana ambayo hayawezekani kwenye milango mingine isipokuwa kwenye mlango huu wa kuomba katika Roho.
KUTUBU DHAMBI
Hakuna dhambi kubwa wala dhambi ndogo, kwa Mungu dhambi ni dhambi zote ziko sawa. Wakristo wengi wanapofikiria kuhusu dhambi wao huzungumzia juu ya dhambi zinazoonekana wazi, ama zile amri kumi za Mungu. Yesu alipokuwa anawaosha wanafunzi wake miguu, Petro alikataa kuoshwa. Yesu akamwambia kama hutaki kuoshwa na mimi basi, basi wewe sio mwenzetu. Petro aliposikia hivyo alisema basi kama ni hvyo basi si miguu tu, nioshe mwili mzima. Aliyeoga si wa kurudiwa kuoga bali kuoshwa vumbi miguu.
Hatujui kuomba jinsi itupasavyo. Roho Mtakatifu hutuombea hata dhambi ambazo tumezitenda tukasahau kuzitubu. Hakuna dhambi ndogo wala kubwa, dhambi ni dhambi tu. Mtu akivaa nguo ya rangi nyeupe safi halafu abebe gunia la mkaa kwenye mabega yake, baada ya dakika tano alitue lile gunia, atajikuta ile nguo nyeupe safi sio safi tena, tena haitamaniki kuvaliwa tena, itakuwa imechafuka hadi ifuliwe. Huo ni uchafu umeingia mara moja, lakini kuna mtu mwingine anafanya kazi ofisini kwenye kiyoyozi naye pia ana nguo nyeupe akienda kazini kwa gari pia lenye kiyoyozi akirudi nyumbani ile nguo inakuwa bado iko safi na anweza kuivaa na siku nyingine, lakini baada ya siku chache inakuwa haiwezi kuvaliwa tena inakuwa imechafuka na kutoa harufu. Hi nguo inakuwa imechafuliwa na uchafu unaoingia kidogo kidogo lakini mwisho umeichafua nguo sawa na Yule aliyeichafua kwa mara moja kwa dakika tano tu. Wakristo wengi wanaona dhambi ni zile kubwa zinazoonekana na watu, dhambi ndogondogo hawazijali wala hawazitubu wanapozitenda. Pamoja na kuokoka kwao hizo dhambi ndogondogo ndizo zinzopeleka watu jehanumu. Dhamb ndogo ndogo ndizo zinaweka kutu kwenye nyaya za simu ya mawasiliano yako na Mungu. Ndipo unakuta mtu wa Mungu pamoja na kuomba sana kwake lakini hapati mpenyo wala hapati majibu. Mawasiliano na Mungu yalishakatika siku nyingi. Mtu wa Mungu unapokuwa unanena kwa lugha, Roho Mtakatifu anakuombea hata dhambi ambazo wewe hujui kuwa hii ni dhambi lakini unazitenda, Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya kukuombea hata hizo dhambi.
Kuna msemo ambao unapenda kutumiwa na Wakristo ambao hawaamini katika kujazwa Roho Mtakatifu na ishara ya kunena kwa lugha kuonekana, kabla ya kuomba hupenda kusema kuwa tujitakase, kwa mtu anayemjua Mungu kujitakasa ni kugeuka na kuacha njia mbaya. Sawa Mungu aliwaambia wana wa Israeli katika mlima wa Sinai kuwa jitakase siku tatu; lakini tunakuta kwenye agano jipya maandiko yanatuambia kuwa sisi baada ya kumpokea Yesu tunakuwa watakatifu.
“Watakatifu walioko dunian ndio walio bora. Hao ndio niliopendezwa nao” (Zaburi 16:2)
Neno la Mungu halisemi tujitakase bali linasema tuzidi kutakaswa. Wakristo wengi msemo huu umewapotosha hivyo wanakuwa bado wanaendelea kutenda dhambi wakitegemea kujitakasa. Haya ni mapokeo yanayotoka kwenye dini yakimtaka mkristo baada ya kutenda dhambi aende kwenye chumba cha kitubio akatubu dhambi mbele ya kasisi, baada ya hapo dhambi zinaondolewa na anapewa malipizi ya kufanya hapo hapo. Sasa mtindo huu umeingizwa kwenye wokovu na baadhi ya watu wasiojua vizuri neno la Mungu. Sasa kwenye wokovu kwa kuwa hakuna kutubu mbele ya wakuu wa dini, bali kwenye wokovu kila mtu anatubu mbele za Mungu, wakristo ambao hawataki kubadili njia zao, hata baada ya kuokoka wamen’gang’ania madhaifu fulani fulani ambayo wanayatenda kila siku, hivyo wanapofikia suala la kumwomba Mungu wanaanza na kujitakasa. Sisemi kwamba kutubu kabla ya maombi hakutakiwi, bali toba hiyo haitakusaidia kama huwezi kugeuka na kuacha kabisa.
Hapa kinachofundishwa hapa ni kukuondoa kwenye wazo la kuendekeza kuwa hata nikitende  dhambi nitajitakasa, hata nikitenda dhambi nitatubu. Inatakiwa kujitakasa kwako kuendane na tendo la kugeuka na kuacha hilo kosa ndipo kujitakasa kwako kutakapokuwa na maana, kujitakasa au kutubu lakini huku unaendelea kuishi kwenye kosa hakutakusaidia. Baada ya kuokoka unatakiwa ujifunze kwa bidii sana neno la Mungu, neno ndilo litakuchonga na kukubadilisha uishi sawa na ulivyojifunza na kutenda sawa na mafundisho siyo kuhusiana na dhambi tu, lakini kuhusiana na maeneo yote ya wokovu, kama kuomba, kushuhudia, kumtolea Mungu, upendo, utakatifu, n.k. mtu akijua neno asipotenda kwake hiyo ni dhambi. Hivyo neno la Mungu ndiyo linalotutakasa, basi kama ni neno la Mungu basi Mungu mwenyewe ndiye anayetutakasa.
“Mtakatifu na azidi kutakaswa” (ufunuo wa Yohana 22:11)
Inatakiwa tujitakase; tutubu lakini huku kusitufanye tukavunja uwezo wa kupambana na dhambi, hivyo tukawa hatuna juhudi katika kuacha kutenda dhambi kwa sababu tunatumainia kuwa tutajitakasa.
Hata hivyo kujitakasa kwa kuomba kwa akili hakutoshelezi, makosa tuliyoyafanya bila ya sisi kujua hatuwezi kuyaombea kwa akili maana akili zetu tayari haiyajui. Kunena kwa lugha ndiyo njia pekee ya kutakaswa. Unajijenga nafsi, mtu anayenena kwa lugha hutakaswa kwa kiwango kikamilifu.
“Unikumbushe; na tuhojiane; eleza mambo yako upate kupewa haki yako” (Isaya 43: 26)
Biblia inasema, nikumbusheni mpate kupewa haki zenu. Mungu amechagua mwenyewe njia ya sisi kumkumbusha ili tuweze kupewa haki zetu. Kuna maombi ambayo umeomba miaka mingi iliyopita lakini maombi hayo hadi 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni