Alhamisi, 2 Agosti 2012

NAMNA YA KUINUA IMANI ILIYOSHUKA

NAMNA YA KUINUA IMANI ILIYOSHUKA (Rum 11.6
Huwezi kusema kuwa wewe ni mkristo bila kusimama kwenye imani. Kwa sababu Imani ndiyo uti wa mgongo wa maisha ya mwamini kwa sababu huwezi kupata kitu unachokitaka bila kupigana vita. Biblia inasema
"Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu." 1Yohana 5.4 

Israel walipewa nchi lakini ilibidi wapigane vita ili hatimaye kuikalia nchi ambayo ki msingi walishapewa na Mungu. Tunahitaji kuwa na imani iliyokamilika ili kuweza kushinda katika vita vya kiroho na kukamata mateka. Biblia inasema Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka ,juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kushindana siku ya uovu. Na mkiisha kuyatimiza yote kusimama. Waefeso 6.12,13 

 

Imani ni silaha ya vita kwa mkristo, kwa imani vinywa vya simba vilifungwa dhidi ya shujaa Daniel. Kwa imani moto haukuwa na nguvu kwa shadraka Meshaki na Abednego. Ukizimia siku ya taabu nguvu zako ni chache  Mithali 24.10 Huyu imani yake ni ndogo ndio maana na nguvu yake ni ndogo. 

Imani inapatikana kwa kufundishwa neno la Mungu, imani ni kitu kinachoshuka na kupanda na katika hali hiyo ya kupanda na kushuka kwa imani  sio kwamba umetenda dhambi. Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka kwa kukosa kuwa na maarifa Isaya 5.13. Roho Mtakatifu anatembea katika neno la Mungu hivyo ni muhimu sana kujua neno la Mungu. Na walio na hekima watangaa kama mwangaza wa anga,na hao waongozao wengi kutenda mema watangaa kama nyota milele na milele. Danieli 12.3
KILA MTU ALIYEOKOKA IMANI YAKE INAWEZA KUSHUKA NA WALA SIO DHAMBI IMANI IKISHUKA.
Katika biblia baba yetu Ibrahimu anasifiwa kuwa ndiye baba wa imani lakini biblia hiyo hiyo inatuhabarisha kwamba alizaa na binti yake wa kazi pamoja na kwamba Mungu alimuahidi kuwa atakuwa na watoto wengi wasiohesabika kama mchanga na wengine kama nyota kupitia kwa mkewe kikongwe Sara. Ni rahisi kusema kwamba alikubaliana na mkewe Sara,lakini bado akili haiwezi kushawishika kukubali kwamba imani yake haikushuka na matokeo yake ndio vurugu tunazoziona mashariki ya kati baina ya mtoto wa Hajiri anayeitwa Ismael na mtoto wa Sara Isaka. 


Ibrahimu alikuwa ni rafiki wa Mungu na Mungu ndiye aliyekuwa akimwonyesha mchanga na kumwambia auhesabu na aliposhindwa akamueleza ndivyo utakavyokuwa wingi wa uzao wake akiwa na maana ya watoto wa kimwili lakini pia alimwambia ajaribu kuhesabu nyota ambazo zilikuwa zinawakilisha watoto wa kiroho waliookoka ikiwepo mimi na wewe msomaji wangu.

Mwingine ni nabii Eliya pamoja na kufanya mambo makubwa ya kutisha ya Mungu katika mlima wa Karmeli hii ilikuwa ni baada ya kutoa sadaka ya kuteketezwa kwa kuamuru moto kutoka mbinguni na kisha kuwachinja makuhani wa baali mbele ya macho ya wana wa Israel huku mfalme Ahabu akijua. lakini baada ya hapo alimkimbia msichana Yesebeli mke wa mfalme Ahabu hapo imani yake ilishuka.


Petro ni binadamu mwenye rekodi ya pekee ya kutembea juu ya maji rekodi ambayo haijavunjwa,ni mtu aliyeona miujiza mingi kuliko mitume wote katika wanafunzi 12 wa yesu walikuwa wamegawanyika kwa kuwa karibu na Yesu kuna sehemu nyingine Bwana Yesu alikuwa anaenda na wanafunzi wachache sana mfano ni pale penye mlima wa ugeuko na maeneo mengine mengi sana utaona Petro yupo, na ndiye aliyeombewa maombi maalumu na Yesu kwamba imani yake isitindike lakini baada ya Yesu kufa ndiye ambaye imani yake ilishuka na akawaongoza wenzake kurudi kwenye kazi yao ya zamani ya kuvua samaki ambako pia hawakuambulia kitu mpaka walipokutana na Yesu asubuhi bila wao kujua na akawaelekeza watupe jarife upande wa pili na ndipo walipogundua kwamba ni Bwana. Kuna wakati hata taifa linaweza kushuka imani, biblia inatukumbusha kwamba baada ya Yesu kufa Taifa zima lilishuka imani na Bwana Yesu mwenyewe akashuka katika mji wa Emau ambako akaongozana na watu waliokuwa wakisimuliana mambo yaliyotokea mjini,nay eye akajifanya kuwauliza ili ajue wameshuka imani kwa kiasi gani,Biblia inasema wakamkazia macho,na kumshangaa kwamba kwa nini hajui yaliyomtokea mtu ambaye walitegemea awaletee tumaini.

Biblia inasema kwamba sisi tutamiliki hapa duniani na sio mbinguni. Mbinguni anamiliki Mungu na sio mwingine kwani shetani alishafukuzwa. Kama ni utajiri tunatakiwa tuupate hapahapa duniani na kumiliki.  baada ya kifo ni hukumu
JINSI YA KUINUA IMANI ILIYOSHUKA
1.     Amua kulala usingizi ,sio kiroho bali usingizi wa kawaida  angalia Biblia yako Matendo 12.1 , 9 Petro alikuwa kwenye jaribu gumu kuliko wakati wowote katika maisha yake ya utumishi Yakobo ndugu yake Yohana alikuwa tayari ameisha uawa kwa upanga,na mfalme Herode akaona hilo jambo limewafurahisha wayahudi akamkamata na Petro na kumuweka kwenye gereza lenye ulinzi mkali usio wa kawaida, walikuwa wanangoja pasaka ipite naye akatwe kichwa kwa maana hiyo alikuwa anajua hakika kwamba atakufa kifo kibaya sana,sasa ili asiwaze na kuingia katika jaribu la kumlaumu Mungu aliamua kulala usingizi wa kawaida. Shetani anatumia sana kuwaza kwako ili kushusha imani yako.
2.                                                                                                           AMUA KUSIFU NA KUABUDU,  
hHapa inatakiwa sifa za ukweli ukweli sio zile nyimbo za sifa za kidini ati vijana wengi wamemuasi Bwana au ule wa kwenye kitabu atujua tu dhaifu maombi asikia. hapo sio sifa hizo. Tatizo ni kwamba viongozi wengi wa sifa huwa hawaombi Mungu ili kupata ili kupata nyimbo zinazotakiwa, wakati muhubiri ni lazima aombe Mungu ili kupata ujumbe. Soma Matendo 16:22,26 hizi ni sifa zinazoweza kuchanganya akili ya mtu,Paulo na Sila walimsifu Mungu na kupandisha imani yao.

3.     KUOMBA MAOMBI YA KINABII
(prophetic Prayer. 
Haya ni tofauti na maombi ya kawaida,ni maombi ya kusemelea au kutabiri ushindi kwa kutumia maneno ya Biblia,huku unamkumbusha Mungu ahadi zake. Maombi ya namna hii husababisha imani kuja juu ghafla na kukamata muujiza wako, je nitaishawishije akili yangu isiwaze wakati kuna hali ya hatari na kifo? hapo ni lazima kunena kwa lugha sana mpaka kieleweke kwa sababu akili haiwezi kukusaidia kuibeba imani yako,kunena kwa lugha ni sawa na kutema moto wa kiroho.
4.     Kumbuka miujiza ambayo Mungu aliwafanya watu wengine kama vile mama mwenye kutoka damu kwa muda mrefu,Binti mfu wa Yairo. Yesu alitaka ushuhuda kwa lazima ili kuinua imani yake huyu mama alikuwa  sawasawa na matatizo ya mtoto wa Yairo,Yesu alitaka Yairo asikie ili imani yake ipande.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni