JUKWAA LA KIKRISTO NA KIJAMII AMBALO LINATOA FURSA KWA JAMII KUJADILI NA KUELIMISHANA JUU YA MAADILI NA MAISHA KWA UJUMLA
Ijumaa, 1 Agosti 2014
Jumamosi, 26 Julai 2014
NAMNA YA KUISIKIA SAUTI YA MUNGU YA NDANI KWA URAHISI ZAIDI SEHEMU YA TATU
Mungu huzugumza na watu wake,kwa njia mblimbali kama vile ndoto,
maono,sauti ya dhahiri masikioni, au sauti ya ndani kama mawazo ambayo
tunajifunza n.k. vyovyote itakavyokuwa lakini Mungu huhakikisha kuwa anaongea
na watu wake.
Njia
ya Mungu kuongea na mtu mmoja inaweza ikatofautiana na mwingine lakini Mungu
anahakikisha ameongea na watu wake.
Wakristo
wengi husikia sauti ya Mungu kutokana na uzoefu wa kuishi na Mungu, lakini kwa
kupewa mafundisho inakuwa ni nadra sana.
Hii inawafanya wakristo hata wanaposikia
sauti ya Mungu wanakuwa na mashaka mashaka kuitekeleza. Hivyo wanaisikia kwa
kubahatisha. Hawajui kanuni kamili ya jinsi kuisikia sauti ya Mungu.
Biblia
inasema;
“Basi imani,
chanzo chake ni kusikia: na kusikia huja kwa neno la Kristo” (Warumi 10:17).
Kwa
kigriki maandiko yanaitwa grapha. Hii ni andiko la aina yoyote ile, liwe na
maana au lisiwe na maana. Wagiriki wakatofautisha maandiko ya kawaida na
maandiko ya neon la Mungu.
Maandiko ya neno la Mungu wakaita Logos. Logos ni neno la Mungu
ambalo tayari lipo tumepewa kama vile Biblia na vitabu mbalimbali vya neno la
Mungu vinavyoandikwa na watumishi wa
Mungu mbalimbali.
Wagiriki
wakaona neno la Mungu ni pan asana. Hivyo wakaona watofautishe Logos na neno la
Mungu linguine wakaita Rhema. Rhema ni neno la Mungu ambalo Mungu anazungumza
na mtu moja kwa moja saa hiyo (live).
Unaweza ukawa unasoma
andiko katika Biblia msitari fulani,ukawa unaendelea kusoma kila siku.
Huo msitari utaendelea kuwa Logos lakini siku moja unaweza ukausoma mstari huo
na Mungu akazungumza na wewe moja kwa moja kupitia mstari huo akakupa ujumbe
fulani. Siku hiyo huo mstari utakuwa Rhema.
Rhema
ni sauti ya Mungu au ni neno la Mungu analozungumza na mtu moja kwa moja.
Inaweza kuwa wazo fulani,hata kama Mungu atazungumza na wewe kwa njia nyingine
ya ndoto,maono, nk.
Baada ya maelezo hayo, hebu turudi kwenye andiko letu Basi imani,
chanzo chake ni kusikia: na kusikia huja kwa neno la Kristo (Warumi 10:17).
Sasa tujiulize swali je tusikie neno lipi kati ya Logos na Rhema ambalo
ukilisikia litazaa imani?.
Neno
ambalo ukilisikia huzaa imani ni Rhema siyo Logos, Logos haizai imani. Hii ndio
maana watu wengi wanasoma Biblia lakini haijawasaidia wala kuwafanya waokoke.
Wakristo wengi wameshindwa kuwa na imani ya kutenda miujiza kwa
sababu hawajui kanuni hii ya miujiza kutendeka. Kwa maana hiyo tumeona ili uwe
na imani yenye kutenda miujiza ni lazima usikie Rhema (usikie kutoka kwa Mungu
anakuagiza kutenda jambo).
Hakuna
mtu wa Mungu yeyote ambaye Mungu hazugumzi naye, tatizo ni uhakika wa kujua
kuwa hii ndiyo sauti ya Mungu, kwa sababu neno la Mungu linasema kondoo wanaijua
sauti ya mchungaji wao.
Mungu huongea na watu wake na kuwongoza
na kuwaelekeza nini wafanye. Lakini wakristo huwa hawatii hiyo sauti ya Mungu.
Kwa hiyo Mungu huamua kutoendelea kuongea nao tena.
Unapokuwa
mtii Kwa sauti ya Mungu ndipo Mungu anakuwa anazungumza na wewe na baadae
unaizowea sauti na inakuwa dhahiri kabisa kwako bila mashaka mashaka. Mkristo
ambaye sio mwombaji wa kuomba maombi marefu sauti ya Mungu itampa shida kidogo
kuitambua.
Mungu anazo njia nyingi za kuongea na watu wake, anaweza kuongea kwa
ndoto, maono,sauti ya masikioni na sauti ya ndani kama wazo, nk. Hata kama
Mungu amezungumza na wewe kwa njia kati ya hizo, hiyo ndio rehma.
Wakristo wengi wanafikiri kuwa ktika agano
la kale, manabii huenda Mungu alikuwa na njia maalumu sana ya kuongea nao
tofauti na sisi. Hao watu walikuwa kama sisi,waliishi hapahapa,walikula chakula
hikihiki n,k. hawakutofautiana na sisi. Mungu alizungumza nao kwa njia hii hii
ambayo ndiyo anazungumza na sisi leo,hakuna tofauti.
Kwa
hiyo ndugu yangu usipoweza kumtii Mungu katika mambo ya kila siku ya kawaida na
hata katika mambo madogomadogo, Mungu hawezi kuendelea kuongea na wewe, Mungu
anaposema tuishi kwa imani yaani maana yake tuishi kwa kumsikiliza yeye.
Biblia
inasema,
“Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani:
naye akisita sita Roho yangu haina furaha naye” (Waebrania 10:38).
Tumeona kuwa, imani chanzo chake ni kusikia. Sasa andiko hili
linasema Ataishi kwa imani. Maana yake ni kwamba, ataishi kwa kusikia kutoka
kwa Mungu (kwa sababu imani chanzo chake ni kusikia).
Kuishi
ni nini?
Kuishi
ni kule kuwa hai kila sekunde inayopita. Uhai ukisimama sekunde moja mtu
atakufa. Hivyo kila sekunde,dakika,saa,siku,wiki,mwaka, unapokuwa bado uko hai
huko ndiko kuishi.
Mungu anataka uishi kwa kumsikiliza yeye. Mungu anataka yeye ndiye
akuongoze akuagize nini cha kufanya kila sekunde katika maisha yako ya kimwili
na kiroho.
Wakristo
wengi wanajiendea tu na kujifanyia mambo yao wenyewe bila ya kuongozwa na
Mungu. Hii imekuwa hivi kwa sababu hawajui nini maana ya kuishi kwa imani.
Kuishi kwa imani wanafikiri ni kuishi maisha ya shida, kubahatisha
kupata riziki, maisha ya kubangaiza yasiyokuwa na uhakika. Kuishi kwa imani ni
kuishi maisha ya kumsikiliza Mungu anakuagiza kufanya nini.
Wakristo wengi wanaishi kwa kujionoa wenyewe,ndio maana wamejaa
shida,dhiki na kukosa mafanikio. Wengi wanafanya mambo ambayo Mungu haja
waagiza na wengi wapo mahali ambapo Mungu hajawaagiza kuwa pale. Wanafanya na
wapo pale kwa mapenzi yao wenyewe si kwa mapenzi ya Mungu.
Watumishi
wa Mungu wengi wana wito lakini wanafanya wito ambao hawakuitiwa. Ni sawa
wameitwa kumtumikia Mungu, lakini je ni Mitume, nabii, mwinjilisti, mchungaji
au mwalimu na je kituo au mji walipo ndipo Mungu anataka wawepo? Shida ni
kwamba wengi hawajui kuisikia sauti ya Mungu
Sauti
ya Mungu inapokuja kwako inakuwa ina mambo mawili. Ni kama kifurushi chenye
vitu viwili ndan yake ambayo ni maagizo
ya kufanya na nguvu ya Mungu ya kuyatekeleza maagizo hayo. Hivyo ukitenda
uliyoagizwa na Mungu unafanikiwa.
Ukitenda
maagizo ya shetani kunatokea uharibifu. Hakikisha unatenda maagizo ya Mungu na
pia hakikisha uko mahali ambapo Mungu amekuagiza uwe.
Sisemi uache kufanya lolot sababu Mungu hajazungumza na wewe, wewe
endelea kufanya mambo kama kawaida yako,hata kama Mungu hajazungumza na wewe,
na wakati huouo ukimsikiliza Mungu, endapo Mungu atasema na wewe basi fanya
lile aliloguagiza.
SAUTI
YA MUNGU KATIKA KUTENDA MIUJIZA.
Hakuna
mtu yeyote anayeweza kutenda muujiza kwa maamuzi yake mwenyewe, hata kama ni
mtumishi wa Mungu anayetumiwa kwa kiwango cha juu sana. Miujiza yote
inayotendwa, Mungu huzungumza na watakaotenda huzungumza nao kwa njia ya Rhema.
Katika kitabu cha waebrania sura ya kumi na moja yote inazungumzia
watumishi wa Mungu waliotenda miujiza mukubwa enzi za agano la kale,wakristo
wamezowea kuwaita watu hao mashujaa wa imani. Mambo hayo hawakuamua yatendeke
kwa mawazo yao wenyewe, bali Mungu aliwaagiza kuitenda miujiza hiyo.
Tofautisha
mawazo yako na imani. Mawazo yako hayawezi kutenda miujiza hata siku moja. Bali
kama Mungu akikuagiza kutenda kwa
kutumia sauti ya ndani. Wakristo wengi hawalijui jambo hili,hivyo wanapokuwa
wanapenda jambo fulani litendeke hufikiri imani itakuja kutokana na kutamani
kwao.
Baada ya hapo mawazo hayo huamua kuyakiri kwamba yamekuwepo. Baada
ya hapo wanayangojea yatokee wakisema wanayangoja kwa imani huku wakisema kuwa
maana imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo.
Kwa
maana hiyo hata wao wako katika kuyatarajia. Pia wanaendelea kusema kuwa imani
ni bayana na mambo yasiyoonekana, hivyo wanayatamani yatokee
MUNGU
AKUBARIKI TUKUTANE KATIKA SEHEMU YA TATU
Mob:
Furaha Amon 0713 461593.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)