Alhamisi, 3 Januari 2013

MIKUTANO YA INJILI KWA SIKU HIZI HAINA MATUNDA WALA HAMASA KAMA ZAMANI



Wakati naanza kupata akili ya kuelewa kuhusu mambo ya imani yangu,nilikuta mikutano ya injili ikiwa ndio njia kuu ya kuwaleta watu kwa Yesu. Lakini waliotutangulia katika imani hii wanatusimulia kuwa Mwishoni mwa Miaka ya 1970 na Mwishoni mwa Miaka ya 1980 bado njia kuu iliyokuwa ikitumika kuwaleta watu kwa Yesu ilikuwa ni Mikutano Ya Injili ya hadhara ambapo watu wengi walimpokea Yesu kupitia mikutano hiyo. Wahubiri wa kizazi hicho, Mzee Emmanuel Lazaro, Mzee Moses Kulola,  Mzee Ayoub Mgweno na Wengineo
walikuwa na kazi kubwa ya kueneza neno la Mungu na asilimia kubwa ya watu waliookoka katika zama hizo waliokoka kwenye mikutano ya wahubiri hawa.

Miaka ya 80, ikaanzishwa huduma inaitwa “The Big November Crusades” chini ya Mzee Lutembeka na Mzee Kisondo. Mikutano hii ilikuwa na nguvu sana miaka hiyo. Nakumbuka ilifanyika katika maeneo ya Mnazi Mmoja na Jangwani kwa wakazi wa Dar, Wagonjwa walikuwa wanaletwa kutoka Muhimbili na walikuwa wakirudi wamepona. 
George Gichana kutoka Kenya ali maarufu “GG”  nakumbuka enzi hizo pamoja na Mzee Roy Daman walikuwa wakija Dar-es-Salaam, kila shughuli ilikuwa inasimama na kila mtu akisubiria “The Big November” ili kuona miujiza lakini pia kuona kwaya kuu zilizokuwa zikitamba enzi hizo, Mtoni Lutheran, na wimbo wao wa Lulu, Chini ya Mwl. George Victory Singers na Wimbo wao wa Mchakamchaka, Chini ya Mwalimu Mwalubalile na Revival Singers na wimbo wao uko wapi, chini ya Mwalimu Mackenzie

Miaka ya 90 na Mpaka sasa nimeona kama hii mikutano ya injili ya hadhara imekuwa kama haina matokeo mazuri ama makubwa kuliko katika kizazi kile cha Mwishoni    mwa , 2010 niliamua kutembelea katika baadhi ya mikutano ya injili iliyokuwa inafanyika Tanga, nilitembelea pale kanisa la TAG Mwembe wa Yesu pale Kisha nikashiriki mkutano wa injili tuliouandaa kanisani kwetu KLPT Majani mapana , kinanisukuma kutazama mikutano hii ni kuamini pia kuona mikutano hii inavyoendeshwa, mwitikio wa waumini wenyewe kwenye mikutano hii, na pia mpango mkakati wa kuwatunza hawa wanaoamua kumpa Yesu Maisha yao.
            
Mbali na mikutano ya injili, pia nimekuwa nikiwasikiliza watumishi wa Mungu wale wanaohubiri kwenye vituo vya mabasi, pale Posta kuna rafiki yangu huwa anahubiri, mwenge kituoni kuna mpendwa huwa anahubiri, stendi ya mkoa kuwa wanaohubiri na kuna wengine wanakusanya sadaka kabisaaaa kwa ajili ya kupata maomb meona kwenye kuangalia kwangu nikama ifuatavyo   



Mbali na mikutano ya injili, pia nimekuwa nikiwasikiliza watumishi wa Mungu wale wanaohubiri kwenye vituo vya mabasi, pale Posta kuna rafiki yangu huwa anahubiri, mwenge kituoni kuna mpendwa huwa anahubiri, stendi ya mkoa kuwa wanaohubiri na kuna wengine wanakusanya sadaka kabisaaaa kwa ajili ya kupata maomb meona kwenye kuangalia kwangu nikama ifuatavyo.

                                                                       
 Mikutano Ya Injili.

1. Waumini wengi (wenyeji) wa mikutano wanapatika siku za Jumamosi na Jumapili, siku za kawaida mikutano huwa na watu wachache na kukosa hamasa ya watu.

2. Mkutano Mingi inayowekwa kwenye viwanja vya makanisa huwa na washirika zaidi kuliko wenye dhambi katika kuhudhuria. Ikifika saa ya kukata shauri muhubiri hutumia muda mrefu wa kuamua kuimba pambiodent:-

3. Wahudumu wengi wa Mikutano wanakuwa hawako well trained kwa ajili ya hiyo kazi, Mfn. Namna ya kukaribisha watu, namna ya kubeba wagonjwa, namna ya kukemea mapepo na pia namna ya kusimama katika kuombea watu, kila Muhubiri ana style yake ya wahudumu kusimama.

4. Mikutano inayofanyikia kama Jangwani, Biafra, Kawe au katika viwanja vya wazi ni ngumu kuwapata wale kondoo wapya kutokana na umbali wa viwanja na makazi ya watu pia.

Wengi wanaohudhuria mikutano hii ni watu wa hali ya chini, wale wasiokuwa na kazi, wafanyakazi wa ndani na wanafunzi. Watu ambao ni wafanyakazi wengi wanatingwa na shughuli nyingi za kutafuta kipato.

6. Waongofu wapya wengi huwa hawadumu, unaweza kuta waliookoka jumla ni 100, wanaoendelea mpaka sasa ni wawili.

7. Wahubiri wengi wa nje wanaongea vizuri  lakini ile nguvu ya udhihirisho ni ndogo sana, yaani wagonjwa kupona wengi ni wale wa tumbo, kichwa na maumivu tu. Ila vipofu, vilema na viziwi bado imekuwa utata kuwapata waliofunguka

8. Ile tabia ya watu kukata shauri na kuhamia kwenye “dhehebu” wenye kuhost mkutano imepitwa na wakati. Wengi wanaokoka na kubaki huko huko waliko ambapo imepelekea kupunguza morale ya “kuwavunia” wengine na makanisa kuamua ku-opt “Semina Za Ndani”.

9. Waumini wengi si wepesi wa kwenda nao zaidi ya wenyeweji kujazana wenyewe uwanjani

1. Wengi wa wahubiri hawa hawajaribu kuonesha upendo wa Mungu, ila kuwatuhumu abiria na kuwaogopesha na siku ya mwisho. Nimewahi kumsikia Muhubiri pale Posta akiongelea mavazi na wakati mwingine hata Dowans katikati ya Mahubiri.

2. Muhubiri anapokanza kuhubiri wanaomsikia ni wengine, mpaka ikifik kata shauri ni mara chache mtu akakaa kituo cha basi zaidi ya nusu saa kusikiliza mahubiri kuliko mtu kusikiliza sauti ya konda anapoita abiria

3. Mpango Mzima wa sadaka sijajua kama wale watumishi wanakumbuka kutoa kikumi, maana akichukua kila basi per day ana make inaweza kumfanya akaona ile ndo ajira yake ya kila siku, kuhubiri na kukusanya sadaka

Lazima nikiri kuwa kuhubiri katika hadhara pia ina faida sana kwenye maisha ya waamini, inakujenga na kukupa ujasiri. Kwa sisi ambao tumekuwa bega kwa bega na wazee wetu kwenye mikutano ya injili, lazima tukiri mikutano ya injili ya nje inakujenga kimwili na kiroho na kisaikolojia pia.

Kwa changamoto nilizozitaja kwangu naona mikutano ya injili inahitaji kutazamwa upya kwa maana ya namna tunavyotumia rasilimali tulizonazo, muda, fedha, watu na kila kilichopo. Semina za Kiroho ambazo zimekuwa zikijenga hata wapendwa nimebaini zimekuwa natokeo makubwa kuliko mikutano ambayo Kanisa linatumia gharama kubwa kuliko matunda ya mikutano hii. Nadhani ipo haja ya sisi wadau kusaidia kuliona hili na pia kushauri pale tunapopaswa kushauri                                                                                                                      
Wasalaam,
Samuel Sasali Papaa


Kweli mikutano ya nje imepungua na hii mi naona ni kusababishwa na mazingira nikimaanisha mikutano mingi ya zamani ilibase kwenye injili haswa na watu kuokoa, kwasasa mingiimeamiakwenye semina na semina nyingi kufanya na wenyehudumaya kialimu na mitume,pia naona imeamia kwenye majengo ya ndani nikimaanisha makanisa na mahema. 

Kingine naona ni wale wainjilisti wa zamani waliokuwakwenye majukwaa na viwanjani hawakuandaa watu kipindi walichokuwepo ili ikitokea hawapo au kipindi chao cha kazi kumalizika basi gurudumu litabebwa na hao walioachiwa. 

Finally kwangumimi naona ni swala la season kwa sasa Mungu anatumia huduma ya kialimu sana kuwafundisha watu neno badala ya forces za wainjilisti. 

Lakiniinabidi kukutana na wainjilisti hawa wa zamani ni rahisikupata views zao katikahili na pia tazama vijana wa sasa nguvu na upako wakiinjilisti umepoa sana kwao wote wanabase kwenye miracles,unabii na n.k


Kwa mimi nahisî msukumo wa kuendelea na mikutano pia umepungua.
yawezekana ni :
1. kuongezeka waumini makanisa ya wale waliokuwa wanafanya mikutano hii ya injili ya nje.

2. mafundisho ya kiinjilisti yamepungua na hivyo kukosekana kwa wainjilisti wapya kuendeleza kazi.

3. Maendeleo ya kiteknolojia yanayofanya matumizi ya redio na tv kuwa makubwa na hivyo kuwafikia watu wengi zaidi kama vile afanyavyo mzee wa upako, mama lwakatare na kakobe. Hata miziki ya injili inavyozidi kuimarika na kuwafikia watu wengi kubadilisha maisha yao.


                 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni