Lakini pasipo imani haiwezekani
kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aaini kwamba yeye yuko, na
kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao (Waebrania 11:6).
Kama waaminio, imani yetu imejengwa
kwenye msingi kwamba Mungu yupo, naye huwatendea watu wanaomtafuta kitofauti na
wale wasiomtafuta. Tukiamini kweli kweli mambo hayo, tunaanza kumpendeza
Mungu, kwa sababu mara moja tunaanza kumtafuta. Kumtafuta Mungu ni pamoja na
(1) Kujifunza mapenzi Yake, (2) Kumtii, na (3) Kutumainia ahadi Zake.
Hayo yote
matatu yanapaswa kuwa sehemu ya mwenendo wetu wa kila siku.
Sura hii inatazama mwendo wetu wa
imani. Ni bahati mbaya kwamba wengi wamekazia imani mpaka ikapita mipaka ya
KiBiblia – hasa mkazo kuhusu mafanikio kimwili. Kwa sababu hiyo, kuna watu
ambao wana hofu kulishughulikia swala hili kabisa. Lakini, kwa kuwa kuna watu
wanaozama katika madimbwi yao ya kuogelea, si sababu kwetu kuacha kunywa maji.
Tunaweza kuwa na msimamo na ukweli wa Maandiko. Biblia ina mengi sana
inayofundisha kuhusu mada hiyo, na Mungu anataka tuitumie imani yetu kwa habari
ya ahadi Zake nyingi sana.
Yesu aliweka mfano wa mwenye kuwa na
imani katika Mungu, Naye anatazamia wanafunzi Wake kufuata mfano Wake.
Vivyo
hivyo, mtumishi anayefanya wengine kuwa wanafunzi hujitahidi kuweka mfano wa
kumtumaini Mungu, naye huwafundisha wanafunzi wake kuziamini ahadi za Mungu.
Hii ni muhimu sana sana. Sit u kwamba haiwezekani kumpendeza Mungu pasipo
imani, ni kwamba haiwezekani kupokea majibu ya maombi yetu pasipo imani (ona
Mathayo 21:22; Yakobo 1:5-8). Maandiko yanafundisha wazi wazi kabisa kwamba
wenye mashaka wanakosa baraka ambazo waamini hupokea. Yesu alisema hivi: “Yote
yanawezekana kwake yeye aaminiye” (Marko 9:23, ).
Tafsiri ya KiBiblia ya imani
inapatikana katika Waebrania 11:1, kama ifuatavyo:
Basi imani ni kuwa na hakika ya
mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyo-onekana.
Kutokana na tasiri hii, tunapata
sifa kadhaa za imani. Kwanza – mtu mwenye imani ana uhakika. Hii ni
tofauti na tumaini, kwa sababu imani ni “uhakika wa mambo yatarajiwayo.”
Tumaini hutoa nafasi kwa mashaka. Tumaini kila wakati linasema, “labda”. Mfano:
Ninaweza kusema hivi: “Natumaini leo mvua itanyesha ili shamba langu
lipate maji.” Ni kwamba natamani mvua, lakini sina hakika kama itanyesha.
Lakini imani ina uhakika wakati wote, “wa mambo yatarajiwayo.”
Kile ambacho watu wanaita imani
mara nyingi si imani kwa tafsiri ya Biblia.
Wanaweza kutazama mawingu meusi juu
na kusema, “Naamini mvua itanyesha.” Ila, hawana hakika kwamba itanyesha
– wao wanafikiri tu kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba pengine
itanyesha. Hiyo si imani ya KiBiblia. Imani ya Biblia haina sehemu ya mashaka.
Haitoi nafasi yoyote kwa chochote kingine isipokuwa kile ambacho Mungu
ameahidi.
Imani
Ni Uhakika Wa Mambo Yasiyo-onekana
Tafsiri ipatikanayo katika Waebrania
11:1 pia inasema kwamba imani ni “bayana ya mambo yasiyo-onekana.” Basi, kama
tunaweza kuona kitu au kukitambua kwa hisia zetu tano, imani haitakiwi.
Hebu fikiri kwamba mtu hivi: “Kwa
sababu ambayo siwezi kueleza, nina imani kwmaba kuna kitabu mikononi mwako.”
Bila shaka ungedhani kwamba ana matatizo fulani. Ungemwambia hivi: “Ha! Huna
haja ya kuamini kwamba nina kitabu mikono mwangu, maana unaweza kuona
dhahiri kabisa kwamba nimeshika kitabu.”
Imani ni ya dunia isiyo-onekana na
macho. Kwa mfano: Ninapoandika maneno
haya, ninaamini kwamba kuna malaika karibu na mimi. Yaani, nina hakika kabisa.
Ninawezaje kuw ana uhakika kiasi hicho? Je, nimemwona? Hapana. Je, nimehisi au
kusikia malaika akiruka karibu? Hapana. Kama ningekuwa nimemwona au kumsikia au
kuguswa na mmoja, nisingekuwa na haja ya kuamini kwamba kuna malaika karibu
nami – ningejua kwamba yupo.
Basi, ni kitu gani kinachonifanya kuwa
na hakika kwamba malaika yupo? Uhakika wangu unatokana na ahadi moja ya Mungu.
Katika Zaburi 34:7, aliahidi hivi: “Malaika wa Bwana hufanya kituo karibu na
wale wamchao, na kuwaokoa”
. Sina ushahidi wa kile ninachoamini isiokuwa
Neno la Mungu. Hiyo ndiyo imani ya kweli ya Biblia – ‘bayana ya mambo
yasiyo-onekana’. Watu wa dunia mara nyingi wanatumia msemo huu: “Kuona ni
kuamini.” Katika ufalme wa Mungu ukweli ni kinyume: “Kuamini ni kuona.”
Tunapofanyia kazi imani yetu kuhusu
ahadi mojawapo ya Mungu, mara nyingi tunakabiliana na mazingira
yatakayotujaribu kuwa na mashaka, au kupitia kipindi ambapo inaonekana kana
kwamba Mungu hatimizi ahadi yake kwa sababu mazingira yetu hayabadiliki. Kwa
hali hiyo, tunachohitaji kufanya ni kupinga mashaka, kudumu katika imani, na
kuendelea kuamini mioyoni mwetu kwamba Mungu siku zote hutimiza Neno Lake. Yeye
hawezi kudanganya kamwe (ona Tito 1:2).
Tunapataje
Imani?
Kwa kuwa imani imejengwa kwenye
ahadi za Mungu tu, kuna mahali pamoja tu pa kupata imani ya KiBiblia – Neno la
Mungu. Warumi 10:17 inasema hivi: “Basi, imani huja kwa kusikia, Neno la
Kristo (TLR, maneno mepesi kutilia mkazo). Neno la Mungu hufunua mapenzi Yake.
Tunapoyajua mapenzi ya Mungu ndipo tunapoweza kuyaamini.
Basi, ukitaka kuwa na imani, lazima
usikie (au usome) ahadi za Mungu. Imani haiji kwa maombi, kwa kufunga, au kwa
mtu kukuwekea mikono ili uipate. Inakuja kwa kusikia Neno la Mungu. Na, ukiisha
kulisikia, bado inakubidi ufanye uamuzi kuliamini.
Zaidi ya kupata imani, imani yetu
pia inaweza kuwa na nguvu. Biblia inataja viwango kadhaa vya imani – kutoka
imani ndogo hadi imani yenye kuhamisha milima. Imani hukua na kupata nguvu sana
inapolishwa na kufanyiwa kazi, sawa tu na musuli ya kibinadamu. Tunapaswa
kuendelea kuilisha imani yetu kwa kutafakari Neno la Mungu. Tunapaswa
kuifanyisha kazi kwa kutenda na kuitikia kila kitu kulingana na Neno la Mungu.
Hata nyakati zile tunapokabiliana na matatizo, wasiwasi na mambo
yanayotusumbua.
Mungu hataki watoto Wake kuwa na wasiwasi kuhusu lolote, bali
kumtumaini katika kila hali (ona Mathayo 6:25-34; Wafilipi 4:6-8; 1Petro 5:7).
Kukataa kuwa na wasiwasi ni njia moja ya kufanyia kazi imani yetu.
Kama kweli tunaamini aliyosema
Mungu, tutatenda na kusema kana kwamba ni kweli. Ukiamini kwamba Yesu ni Mwana
wa Mungu, utasema na kutenda kama mtu anayeamini hayo. Kama unaamini kwamba
Mungu atakupa mahitaji yako yote, utasema na kutenda hivyo. Ukiamini kwamba
Mungu anataka uwe mwenye afya, utatenda nakuzungumza hivyo.
Biblia imejaa
mifano ya watu ambao wakiwa katikati ya mazingira magumu, walifanyia kazi imani
yao katika Mungu na wakapata miujiza. Tutawatazama baadhi yao katika sura hii
baadaye, na katika sura inayofuata kuhusu uponyaji wa Mungu. (Ukitaka mifano
mingine mizuri, tazama 2Wafalme 4:1-7; Marko 5:25-34; Luka 19:1-10 na Matendo
14:7-10).
Imani
Ni Kitu Cha Moyo
Imani ya KiBiblia haifanyi kazi
katika akili zetu – ni moyoni. Paulo aliandika hivi: “Maana kwa moyo mtu
huamini” (Warumi 10:10a). Yesu naye alisema hivi:
Yeyote atakayeuambia mlima huu,
‘Ng’oka ukatupwe baharini’, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini
kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake (Marko 11:23..
Yawezekana kabisa kuwa na mashaka
kichwani mwako na ukawa bado na imani moyoni mwako na kupokea kile ambacho
Mungu ameahidi. Ukweli ni kwamba mara nyingi tunapojaribu kuamini ahadi za
Mungu, aili zetu, zikishawishiwa na hisia zetu za kimwili na uongo wa Shetani,
hushambuliwa na mashaka. Katika nyakati hizo tunahitaji kuondoa mawazo yenye
mashaka na kutia ahadi za Mungu mahali pake, na kudumu katika imani bila ya
kusita au kuyumba.
Makosa
Ya Kawaida Kuhusu Imani
Tunapojaribu kuwa na imani katika
Mungu, wakati mwingine tunashindwa kupokea tunachotaka kwa sababu hatufanyi
kulingana na Neno la Mungu. Kosa moja la kawaida sana hutokea wakati
tunapojaribu kuamini kupata kitu ambacho Mungu hajatuahidi.
Kwa mfano: Ni halali KiMaandiko kwa
wenye ndoa kumwamini Mungu kupata watoto kwa sababu Neno la Mungu lina ahadi
ambayo wanaweza kuisimamia. Ninajua wana ndoa ambao wameambiwa na daktari
kwamba hawatapata watoto. Wao waliamua kumwamini Mungu, wakisimama kwenye ahadi
mbili zinazofuata hapo chini, na leo hii ni wazazi wa watoto wenye afya nzuri
sana.
Nanyi mtamtumikia BWANA Mungu wenu,
naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati
yako. Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba wala aliye tasa katika nchi yako; na
hesabu ya siku zao nitaitimiza (Kutoka 23:25-26).
Utabarikiwa kuliko mataifa yote;
hakutakuwa na mtu mume wala mke aliye tasa kati yenu; wala kati ya wanyama wenu
wa mifugo (Kumbu. 7:14).
Ahadi hizi ziwatie moyo wana ndoa
wasiokuwa na watoto! Lakini, kujaribu kuamini kwamba lazima mtoto awe mvulana
au msichana ni jambo lingine. Katika Biblia hakuna ahadi zinazosema tutachagua
jinsia ya watoto tutakaozaa. Lazima tukae katika mipaka ya Neno la Mungu kama
tunataka imani yetu itende kazi. Tunaweza kumwamini Mungu kwa kile
alichotuahidi tu.
Hebu tuone ahadi nyingine ya Neno la
Mungu, kisha tuamue tunachoweza kuamini kutokana na ahadi hiyo.
Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka
kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya
Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza (1Wathes. 4:16).
Kutokana na andiko hilo, tunaweza
kuamini kabisa kwamba Yesu atarudi. Lakini je, tuombe na kuamini kwamba Yesu
atarudi kesho? Hapana, kwa sababu andiko hili halituahidi hivyo, wala lingine
lolote. Tena, Yesu mwenyewe alisema hakuna ajuaye saa wala siku ya kurudi
Kwake.
Ila, tunaweza kuomba tukitumaini
kwamba Yesu anaweza kurudi kesho, lakini hatuna uhakika kwamba itatokea kama
tunavyoomba. Tunapoomba kwa imani, tuna hakika kwamba kile tunachokiomba
kitatokea kwa sababu tuna ahadi ya Mungu kuhusiana nacho.
Kwa andiko hilo hilo, tunaweza
kuamini kwamba miili ya wale waaminio waliokufa itafufuliwa wakati Yesu
atakaporudi. Lakini je, sisi tulio hai wakati wa kurudi kwa Kristo tuamini
kwamba tutapokea miili ya ufufuo wakati huo huo kama “waliokufa katika Kristo”,
au hata kabla yao? Hapana, maana andiko hili linatuambia tofauti kabisa,
kwamba: Wale “waliokufa katika Kristo” watafufuliwa kwanza.” Mstari unaofuata
unaendelea hivi: “Kisha sisi tulio hai tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu”
(1Wathes. 4:17). Basi, hakuna uwezekano kwamba “waliokufa katika Kristo”
hawatakuwa wa kwanza kupokea miili yao ya ufufuo wakati Yesu atakaporudi. Neno
la Mungu limeahidi kwamba watakuwa wa kwanza.
Hivyo – kama tunatakiwa kumwamini
Mungu kwa habari ya kitu fulani, lazima tuwe na uhakika kwamba ni mapenzi ya
Mungu kwa ajili yetu kupokea tunachotaka. Mapenzi ya Mungu yanaweza kujulikana
vizuri sana kwa kutazama ahadi Zake zilizoandikwa katika Biblia.
Imani inafanya kazi hivyo hivyo
katika dunia ya kawaida. Utakuwa mjinga kuamini kwamba nitakutembelea nyumbani
kesho mchana kama sikuwa nimekuahidi hivyo.
Imani bila ahadi ya kuisimamia, si
imani kweli – ni upumbavu. Kwa hiyo – kabla hujamwomba Mungu chochote, kwanza
jiulize swali hili – ni andiko gani katika Biblia linaloniahidi kile
ninachotaka? Kama huna ahadi, huna msingi wa imani yako.
Kosa
La Pili La Kawaida
Mara nyingi Wakristo hujaribu
kutegemea ahadi moja ya Mungu kutimizwa maishani mwao bila ya kutimiza masharti
yote yenye kuambatana na ahadi yenyewe. Kwa mfano: Nimesikia Wakristo wengi
wakirejea maneno ya Zaburi 37 na kusema hivi: “Biblia inasema Mungu atanipa
matakwa ya moyo wangu. Ninamwamini kwa hilo.”
Tatizo ni kwamba, Biblia haisemi tu
kwamba Mungu atatupa matakwa ya mioyo yetu. Angalia inachosema:
Usikasirike kwa sababu ya watenda
mabaya, usiwahusudu wafanyao ubatili. Maana kama majani watakatika mara, kama
miche mibichi watanyauka. Umtumaini BWANA ukatende mema, ukae katika nchi,
upendezwe na uaminifu. Nawe utajifurahisha kwa BWANA, naye atakupa haja za moyo
wako. Umkabidhi BWANA njia yako, pia umtumaini, naye atafanya (Zaburi 37:1-5).
Kuna masharti kadha ambayo lazima
tutumize ikiwa tunataka kumwamini Mungu atupe matakwa ya moyo. Ukihesabu utaona
masharti nane katika ahadi hiyo. Tusipotimiza masharti hayo, hatuna haki ya
kupokea baraka zilizoahidiwa. Imani yetu inakuwa haina msingi.
Pia, Wakristo wanapenda kureje ahadi
inayopatikana katika Wafilipi 4:19, kwamba “Mungu wangu atanipa mahitaji yangu
yote kulingana na utajiri Wake katika utukufu.” Sawa – je, kuna masharti katika
ahadi hiyo? Bila shaka.
Ukichunguza mantiki ya ahadi ya
Wafilipi 4:19, utaona kwamba si ahadi itolewayo kwa Wakristo wote. Ila ni ahadi
itolewayo kwa Wakristo ambao ni watoaji. Paulo alijua Mungu angewapa Wafilipi
mahitaji yao yote kwa sababu walikuwa wamemtumia sadaka. Kwa kuwa walitafuta
kwanza ufalme wa Mungu kama Yesu alivyoagiza, Mungu angewapa mahitaji yao yoe,
kama Yesu alivyoahidi (Mathayo 6:33). Ahadi nyingi katika Biblia zinazohusu
Mungu kutupa mahitaji yetu ya kawiada zina sharti kwamba sisi tuwe watoaji
kwanza.
Kweli hatuna haki ya kumtumaini
Mungua kutane na mahitaji yetu kama hatutii amri Zake kuhusu fedha yetu. Katika
agano la kale, Mungualiwaambia watu Wake kwamba walikuwa wamelaaniwa maana
hawakuwa wanatoa zaka zao. Ila, aliahidi kuwabariki kama wangetoa zaka na
sadaka zao kwa uaminifu na kwa utii (ona Malaki 3:8-12).
Baraka nyingi zilizoahidiwa kwetu
katika Biblia zinategemeana na sisi kumtii Mungu. Basi, kabla ya kujaribu
kumwamini Mungu kwa kitu fulani, tujiulize kwanza hivi: “Je, ninatimiza
masharti yanayoambatana na ahadi hiyo?”
Kosa
La Kawaida La Tatu
Katika Agano Jipya, Yesu aliweka
sharti ambalo linafanya kazi kila wakati tunapo-omba kuhusu kitu.
Mwaminini Mungu. Amin nawaambia,
‘Yeyote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka
moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Kwa
sababu hiyo nawaambia, Yoyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba
mnayapokea, nayo yatakuwa yenu (Marko 11:22-24, maneno mepesi kutilia
mkazo).
Sharti ambalo Yesu alitaja ni
kuamini kwamba tumekwisha pkea tunapoomba. Wakristo wengi hukosea kwa kujaribu
kufanyia kazi imani yao kwa kuamini kwamba wamepokea wanapo-ona jibu la
maombi yao. Wanaamini kwamba watapokea, si kwamba wamekwisha pokea.
Tunapomwomba Mungu kitu ambacho
ametuahidi, tunatakiwa kuamini kwamba tunapoikea jibu wakati tunapo-omba,
kisha tuanze kumshukuru Mungu kwa jibu wakati huo. Lazima tuamini kwamba
tumejibiwa kabla ya kuona, si baada ya kuona. Tunatakiwa
kumjulisha Mungu haja zetu pamoja na shukrani, kama anavyoandika Paulo.
Msijisumbue kwa neno lolote; bali
katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na
zijulikane na Mungu (Wafilipi 4:6).
Kama tulivyokwisha ona, tukiwa na
imani mioyoni mwetu, maneno yetu na matendo yetu vitalingana na kile
tunachoamini. Yesu alisema hivi: “Mdomo hunena yale yaujayazo moyo” (Mathayo
12:34).
Kuna Wakristo wengine wanaofanya
kosa la kurudia kuomba kitu kile kile. Hiyo inadhihrisha kwamba hawajaamini
bado kwamba wamekipokea. Kama tunaamini kwamba tunapokea tunapoomba, hakuna
haja ya kurudia kuomba ombi lile lile. Kurudia kuomba kitu kile kile ni
kuonyesha mashaka kwamba Mungu hakutusikia tulipomwomba mara ya kwanza.
Je,
Yesu Hakurudia Ombi Zaidi Ya Mara Moja?
Yesu alirudia ombi moja mara tatu,
alipokuwa anaomba katika Bustani ya Getsemane (ona Mathayo 26:39-44). Lakini
kumbuka hakuwa anaomba kwa imani kulingana na mapenzi ya Mungu. Alipoomba mara
hizo tatu ili ikiwezekana asiende msalabani, alijua kwamba ombi Lake lilikuwa
kinyume na mapenzi ya Mungu. Ndiyo sababu alijinyenyekeza kwa mapenzi ya Baba
Yake mara tatu pia katika sala hiyo hiyo.
Hiyo sala mara nyingi hutumiwa
kimakosa kwamba ni mfano wa maombi yote, maana kuna wengine
wanaofundisha kwamba kila sala inapaswa kumalizika kwa kusema hivi: “Kama ni
mapenzi Yako” au “Si kama nitakavyo mimi, bali mapenzi Yako yatendeke.”
Hapa tena tunapaswa kukumbuka kwamba
Yesu alikuwa anaomba kitu alichojua kwamba si mapenzi ya Mungu. Kufuata mfano
Wake wakati sisi tunaomba kitu kulingana na mapenzi ya Mungu ni kosa, na
kutokuwa na imani. Kwa mfano: Kuomba hivi: “Bwana! Naungama dhambi yangu kwako,
nami naomba unisamehe ikiwa ni mapenzi Yako” ni kuonyesha kwamba yawezekana si
mapenzi ya Mungu kusamehe dhambi yangu. Tunajua kwamba Biblia inaahidi Mungu
atatusamehe tunapoziungama dhambi zetu (ona 1Yohana 1:9). Hivyo, sala kama hiyo
itadhihrisha kutokuwa na imani kwa mtu, kuhusu mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa
wazi.
Yesu hakumaliza kila sala kwa
kusema, “Si kama nitakavyo mimi, bali mapenzi Yako yatimizwe.” Kuna mfano mmoja
tu wa Yeye kuomba hivyo, na ni wakati alipokuwa anajitolea kufanya mapenzi ya
Baba Yake, akijua mateso ambayo angepitia kwa sababu hiyo.
Kwa upande mwingine, kama hatujui
mapenzi ya Mungu katika hali fulani kwa sababu hajayafunua, basi inafaa
kumalizia maombi yetu kwa maneno haya: “Kama ni mapenzi yako.” Yakobo aliandika
hivi:
Haya basi ninyi msemao, Leo au kesho
tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima na kufanya biashara na
kupata faida; walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana
ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka. Badala ya kusema, Bwana
akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi. Lakini sasa mwajisifu katika
majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya (Yakobo 4:13-16).
Tufanye nini tukiisha omba kulingana
na ahadi ya Mungu, na kutimiza masharti yote? Tuendelee kumshukuru Mungu kwa
majibu ambayo tumeamini kwamba tumeyapokea mpaka tupokee tulichokiomba.
Tunapokea na kurithi ahadi za Mungu kwa imani na subira (Waebrania 6:12).
Shetani atajaribu kutushinda kwa kuleta mashaka, nasi lazima tutambue kwamba
akili zetu ndiyo uwanja wa mapambano. Wakati mawazo ya mashaka yanaposhambulia
akili zetu, tunahitaji kuyabadilisha kwa mawazo yenye msingi kwenye ahadi za Mungu
na kulitamka Neno la Mungu kwa imani. Tukifanya hivyo, Shetani lazima akimbie
(ona Yakobo 4:7; 1Petro 5:8-9).
Mfano
Wa Imani Katika Matendo
Mfano mmoja maarufu sana katika
Biblia kuhusu imani katika matendo ni habari ya Petro akitembea juu ya maji. Hebu
tusome habari yenyewe, tuone tutajifunza nini.
Mara [Yesu] akawalazimisha wanafunzi
wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng’ambo, wakati yeye
alipokuwa akiwaaga mkutano. Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani
faraghani kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake. Na kile
chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi, maana
upepo ulikuwa wa mbisho. Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea,
akienda kwa miguu juu ya bahari. Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari
wakafadhaika wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu. Mara Yesu alinena
akawaambia, Jipeni moyo, ni mimi, msiogope. Petro akamjibu akasema, Bwana!
Ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. Akasema, Njoo. Petro akashuka
chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu. Lakini alipouona
upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe akisema, Bwana, niokoe. Mara Yesu
akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona
shaka? Nao walipopanda chomboni, upepo ulikoma. Nao waliokuwamo ndani ya chombo
wakamsujudia wakisema, Hakika wewe u Mwana wa Mungu! (Mathayo 14:22-33).
Kabla ya hapa, wanafunzi wa Yesu
walikuwa wamenaswa katika dhoruba nyingine kali wakiwa mtumbwini katika Bahari
ya Galilaya (ona Mathayo 8:23-27). Wakati wa tukio hilo, Yesu alikuwa nao, na
baada ya kutuliza dhoruba kwa neno lake, aliwakemea wanafunzi Wake kwa kutokuwa
na imani kwao. Kabla ya kuanza safari alikuwa amewaambia kwamba ni mapenzi Yake
wavuke hadi ng’ambo ya pili ya ziwa (Marko 4:35). Lakini, dhoruba ilipotokea,
walishawishika zaidi na mazingira yao, na kuna wakati waliamini watakufa wote.
Yesu alitazamia haidhuru wasiogope basi.
Safari hii, Yesu aliwatuma wavuke
ng’ambo ya ziwa wakiwa peke yao. Hakika aliongozwa na Roho kufanya hivyo, na
hakika Mungu alijua kwamba upepo wa mbisho ungetokea usiku huo. Kwa hiyo Bwana
aliwaruhusu wakabiliwe na changamoto ndogo tu kwa imani yao. Kwa sababu ya hizo
pepo za mbisho, safari ambayo ingechukua masaa machache tu ilichukua usiku
kucha. Kweli tunastahili kuwasifu wanafunzi kwa jitihada zao, lakini hatuachi
kushangaa ikiwa kuna mmoja wao aliyejaribu hata kuwa na imani kwamba hizo pepo
zitulie – kitu ambacho walikuwa wamemwona Yesu akifanya siku chache kabla ya
hapo. Cha ajabu ni kwamba, katika Injili ya Marko, tunasoma kwamba wakati Yesu
alipowaendea akitembea juu ya maji, “akataka kuwapita” (Marko 6:48). Alikuwa
anataka awaache wakabiliane na tatizo lao peke yao, huku yeye anapita hapo
kimuujiza! Hii inaonyesha kwamba hawakuwa wanaomba au kumtazama Mungu.
Changamoto kwetu ni kwamba Mtenda Miujiza hutupita mara ngapi tunapong’ang’ana
na maisha dhidi ya upepo wa matatizo.
Kanuni
Za Imani
Yesu aliitikia wito wa Petro kwa
neno moja tu: “Njoo.” Kama Petro angejaribu kutembea juu ya maji kabla ya neno
hilo, angezama mara moja, maana asingekuwa na ahadi ya kutegemeza imani yake.
Angekuwa anajitokeza kwa kudhania badala ya imani. Vile vile hata baada
ya Yesu kusema neno Lake, kama mwanafunzi mwingine yeyote angejaribu kutembea
juu ya maji, angezama mara moja, kwa sababu Yesu alimpa Petro tu ahadi. Hakuna
mwingine ambaye angeweza kutimiza masharti ya ahadi hiyo, maana hawakuwa Petro.
Basi, kabla yeyote kati yetu hajajaribu kutegemea ahadi moja ya Mungu, lazima
kuhakikisha kwamba ahadi hiyo ni yetu na kwamba tunatimiza masharti yake.
Petro akaweka mguu kwenye maji. Hapo
ndipo alipoamini, japo hakuna shaka kwamba yeye aliyekuwa anapiga kelele kwa
kuogopa mzuka muda mfupi kabla ya hapo, pia alikuwa na mashaka ichwani mwake alipopiga
hatua ya kwanza. Lakini ili aweze kupokea muujiza, ilibidi afanyie kazi imani
yake. Kama angeshikilia mlingoti wa mtumbwi na kutia dole gumba la mguu ndani
ya maji aone kama maji yana uwezo wa kumbeba, asingepata muujiza. Vivyo hivyo
na sisi – kabla ya kupokea muujiza wowote, lazima tujitolee kuamini ahadi ya
Mungu, kisha tutende kama tunavyoamini. Kila mara kuna wakati ambapo imani yetu
lazima ipimwe. Wakati mwingine kipindi ni kifupi, wakati mwingine kirefu.
Lakini kuna muda ambapo itabidi tupuuze ushahidi wa hisia zetu na kutenda
kulingana na Neno la Mungu.
Petro aliendelea vizuri mwanzoni.
Lakini alipotafakari jinsi hicho alichokifanya kisivyowezekana, akikumbuka
upepo na mawimbi, aliogopa. Pengine aliacha kutembea, akihofia hatua
inayofuata. Sasa – yeye aliyekuwa anapokea muujiza akajikuta anazama. Twahitaji
kuendelea katika imani tukiisha anza – kuendelea kutenda kulingana na imani
yetu. Tuzidi kusonga mbele.
Petro alizama kwa sababu alikuwa na
mashaka. Mara nyingi watu hawapendi kujilaumu wenyewe kwa kukosa imani kwao.
Wanaona ni afadhali kumlaumu Mungu. Lakini, unadhani Yesu angeitikiaje kama
angemsikia Petro, baada ya kurudi mtumbwini salama, akiwaambia wanafunzi
wenzake hivi: “Kweli, mpango wa Mungu kwa ajili yangu ilikuwa kufika hapo nilipofika?”
Petro alishindwa kwa sababu
aliogopa, akapoteza imani. Huo ndiyo ukweli. Yesu hakumlaumu, bali alinyosha
mkono wake mara moja kumpa Petro kitu thabiti zaidi cha kushika. Na mara moja
akamhoji Petro kwa nini aliona shaka. Petro hakuwa na sababu yoyote nzuri ya
kuwa na shaka, kwa sababu neno la Mwana wa Mungu ni thabiti kuliko kitu
chochote. Hakuna yeyote kati yetu mwenye sababu nzuri ya kutilia shaka Neno
la Mungu, au kuogopa, au kuwa na wasiwasi.
Maandiko yamejaa ushindi ambao
ulitokana na imani, na kushindwa kulikotokana na mashaka. Yoshua na Kalebu
waliingia Nchi ya Ahadi kwa sababu ya imani yao. Wenzao wengi walikufa jangwani
kwa sababu ya mashaka yao (ona Hesabu 14:26-30). Wanafunzi wa Yesu walipata
mahitaji yao waliposafiri wawili wawili kuhubiri Injili (Luka 22:35), lakini
waliwahi kushindwa kutoa pepo kwa sababu ya kutokuamini kwao (ona Mathayo
17:19-20). Wengi walipokea miujiza ya uponyaji katika huduma ya Kristo, lakini
wagonjwa wengi katika mji wa Nazareti – nyumbani Kwake – walibakia wagonjwa kwa
sababu ya kutoamini kwao (Marko 6:5-6).
Kama wote, hata mimi nimepata
mafanikio na kushindwa kulingana na imani yangu au mashaka yangu. Lakini
sitaskia uchungu kwa kushindwa kwangu au kumlaumu Mungu. Sitajihesabia haki kwa
kumlaumu Yeye. Sitatafuta maelezo yasiyoeleweka kirahisi, yenye kutengeneza
upya mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa wazi. Najua Mungu hawezi kusema uongo. Kwa
hiyo, ninaposhindwa, ninatubu kutokuamini kwangu na kuanza kutembea juu ya maji
tena. Nimeona kwamba Yesu kila mara ananisamehe na kuniokoa nisizame!
Tunamalizia hivi: Waamini
hubarikiwa; wenye mashaka hawabarikiwi! Mtumishi anayefanya watu kuwa wanafunzi
hufuata mfano wa Yesu. Yeye mwenyewe amejaa imani, na anawashauri wanafunzi
wake hivi:
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni