Yesu
alitoa ibada maalum mbili tu kwa kanisa:
ubatizo wa maji (ona Mathayo 28:19) na
Meza ya Bwana (ona 1Wakor. 11:23-26).
Tujifunze kuhusu ubatizo wa maji kwanza.
Katika agano jipya, kila aaminiye
anapaswa kubatizwa mara tatu tofauti, kama ifuatavyo: ubatizo wa kuingia katika
mwili wa Kristo; ubatizo wa maji, na ubatizo wa Roho Mtakatifu.
Mtu anapozaliwa mara ya pili,
anabatizwa ili kuingia katika mwili wa Kristo. Yaani, anafanyika kiungo katika
mwili wa Kristo ambao ni kanisa. Kwa maana katika Roho mmoja sisi
sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja (1Wakor. 12:13. Ona pia Warumi 6:3; Waefeso
1:22, 23; Wakolosai 1:18, 24).
Kubatizwa katika Roho Mtakatifu ni
kitu kinachofuata wokovu, na ubatizo huu ni kwa ajili ya kila aaminiye.
Mwisho – kila mwamini anapaswa
kubatizwa katika maji mara tu inapowezekana, baada ya kutubu na kumwamini Bwana
Yesu.
Ubatizo unapaswa kuwa tendo la kwanza la utii katika maisha ya mwamini
mpya.
[Yesu] Akawaambia, Enendeni
ulimwengu mwote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa
ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa (Marko 16:15, 16. Maneno mepesi
kukazia).
Kanisa la kwanza lilihesabu amri ya Yesu kuhusu kubatiza kuwa ya muhimu sana. Karibu kila mara, waamini wapya walibatizwa mara moja baada ya kuokoka kwao (ona Matendo 2:37-41; 8:12-16; 36-39; 9:17-19; 10:44-48; 16:31-33; 18:5-8; 19:1-5).
Mawazo
Kinyume Cha Biblia Kuhusu Ubatizo
Kuna wanaobatiza kwa kumnyunyuzia mwamini mpya matone kidogo tu ya maji. Je, ni sahihi?
batiza katika
Agano Jipya linatokana na neno la Kiyunani baptize, ambalo maana yake
halisi ni “kufunika kwa maji, kuzamisha.” Basi, wale wanaobatizwa kw amaji
wanatakiwa kuzamishwa ndani ya mani, si kudondoshewa matone machache tu. Maana
ya ubatizo wa Kikristo ambayo tutajifunza punde tu, inaunga mkono pia wazo la
kuzamishwa katika maji.
Kuna wengine wanaobatiza watoto
wachanga. Hakuna mifano ya maandiko kuhusu kubatizwa kwa watoto katika Biblia.
Desturi hiyo inatokana na mafundisho ya uongo kuhusu “ubatizo kuokoa” – wazo
kwamba mtu huzaliwa mara ya pili anapobatizwa.
yanafundisha wazi
kabisa kwamba watu wanapaswa kumwamini Yesu kwanza kabla ya kubatizwa. Hivyo,
watoto wakubwa kidogo, na wenye uwezo wa kutubu na kumfuata Yesu wanastahili
kubatizwa – si watoto wachanga au hata wadogo.
Kuna wanaofundisha kwamba, ingawa
mtu anaweza kumwamini Yesu, hajaokoka mpaka abatizwe. Kulingana na Maandiko,
hiyo si kweli. Katika Matendo 10:44-48 na 11:17, tunasoma kwamba watu wa
nyumbani mwake Kornelio waliokolewa na kubatizwa kwa Roho Mtakatifu kabla hawajabatizwa
katika maji. Ni kwamba haiwezekani yeyote abatizwe kwa Roho Mtakatifu kama
hajaokoka kwanza (ona Yohana 14:17).
Kuna wanaofundisha kwamba kama mtu
asipobatizwa kulingana na utaratibu wao, hajaokoka. Maandiko hayatoi utaratibu
fulani kiibada ambao unapaswa kufuatwa, ili uwe ubatizo sahihi au halali. Kwa
mfano:
Kuna wanaosema mwamini anatakiwa kubatizwa “katika jina la Yesu” (Matendo 8:16). Wanadai kwamba mtu akibatizwa “kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu” (Mathayo 28:19) hajaokoka.
Watu hao wanaonyesha roho ile ile ambayo iliwatawala Mafarisayo – wanachuja mbu na kumeza ngamia. Ni huzuni ilioje kwamba Wakristo wanahojiana kuhusu maneno yanayofaa kusemwa wakati wa ubatizo, huku dunia inasubiri kusikiliza Injili.
Kuna wanaosema mwamini anatakiwa kubatizwa “katika jina la Yesu” (Matendo 8:16). Wanadai kwamba mtu akibatizwa “kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu” (Mathayo 28:19) hajaokoka.
Watu hao wanaonyesha roho ile ile ambayo iliwatawala Mafarisayo – wanachuja mbu na kumeza ngamia. Ni huzuni ilioje kwamba Wakristo wanahojiana kuhusu maneno yanayofaa kusemwa wakati wa ubatizo, huku dunia inasubiri kusikiliza Injili.
Maana
Ya Ubatizo Kimaandiko
Ubatizo wa maji ni mfano wa vitu
vingi ambavyo vinakuwa vimekwisha tokea katika maisha ya mwamini. Kimsingi, ni
mfano kwamba tumesafishwa dhambi zetu, na sasa tunasimama mbele za Mungu tukiwa
safi. Wakati Anania alipotumwa kwa Sauli (au Paulo) mara tu alipo-okoka,
alimwambia hivi:
Basi sasa, unakawilia nini? Simama ubatizwe, ukaoshwe dhambi zako, ukiliitia jina lake (Matendo 22:16. Maneno mepesi kukazia).
Pili – Ubatizo wa maji ni mfano wa
sisi kujitambulisha na Kristo katika kufa Kwake, kuzikwa na kufufuka. Tukiisha
zaliwa mara ya pili na kuwekwa katika mwili wa Kristo, tunaanza kuhesabiwa kuwa
“katika Kristo” tangu wakati huo na kuendelea. Kwa sababu Yesu alituwakilisha,
Mungu anatuhesabia yote aliyofanya Yesu.
Basi, “katika Kristo” tumekufa, tumezikwa na tumefufuliwa ili kuishi kama watu wapya kabisa.
Basi, “katika Kristo” tumekufa, tumezikwa na tumefufuliwa ili kuishi kama watu wapya kabisa.
Hamfahamu ya kuwa sisi sote
tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti Yake? Basi tulizikwa
pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo
alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi
tuenende katika upya wa uzima (Warumi 6:3, 4).
Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo;
na katika huo mkafufuliwa pamoja naye kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua
katika wafu (Wakolosai 2:12).
Kila mwamini mpya anapaswa
kufundishwa kweli hizi muhimu sana wakati anapobatizwa kwa maji, naye anapaswa
kubatizwa mara moja baada ya kumwamini Yesu.
Meza
Ya Bwana
Meza ya Bwana asili yake ni katika
Sikukuu ya Pasaka ya Agano la Kale. Usiku ule Mungu alipowakomboa Israeli kutoka
utumwani Misri, aliagiza kila nyumba kuchinja mwana-kondoo wa umri wa mwaka
mmoja na kuinyunyiza damu yake kwenye miimo ya milango ya nyumba zao. Wakati
“malaika wa kifo” alipopita katika taifa hilo usiku ule, akiua wazaliwa wa
kwanza wote katika Misri, angeiona damu kwenye nyumba za Waisraeli, na “kupita
juu yake.”
Tena, Waisraeli walitakiwa
kusherehekea sikukuu usiku huo kwa kumla mwanakondoo wao wa Pasaka na pia kwa
kula mkate usiotiwa chachu kwa siku saba. Hili lilikuwa agizo la kudumu kwa
Waisraeli, na ni kitu cha kufanyika kila mwaka wakati huo huo (ona Kutoka
12:1-28). Ni dhahiri kwamba mwana-kondoo wa Pasaka alikuwa mfano wa Kristo,
anayeitwa “Pasaka wetu” katika 1Wakoirntho 5:7.
Wakati Yesu alipoanzisha Meza ya
Bwana, Yeye na wanafunzi Wake walikuwa kwenye Sherehe ya Pasaka. Yesu
alisulubiwa wakati wa Pasaka, na kwa njia hiyo kutimiza kikamilifu wito Wake
kama “Mwanakondoo wa Mungu, azichukuaye dhambi za dunia” (Yohana 1:29).
Ule mkate tunaokula na maji ya
matunda tunayokunywa ni mfano wa mwili wa Yesu, uliovunjwa kwa ajili yetu, na
damu yake, iliyomwagika kwa ajili ya ondoleo la dhambi zetu.
Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa
mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake akasema, Twaeni mle, huu
ndio mwili wangu. Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa akisema, Nyweni nyote
katika hiki; kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya
wengi kwa ondoleo la dhambi. Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa
uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika
ufalme wa Baba yangu (Mathayo 26:26-29).
Mtume Paulo anasimulia kisa hicho
hicho kwa njia tofauti, kama ifuatavyo:
Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana
niliyowapa nanyi, ya kuwa, Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, naye
akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu;
fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe
akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila
mnywapo, kwa ukumbusho wangu. Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe
hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo (1Wakor. 11:23-26).
Lini,
Namna Gani?
Maandiko hayasemi tushiriki Meza ya
Bwana mara kwa mara kiasi gani, lakini ni dhahiri kwamba katika Kanisa la
Kwanza ilifanyika mara kwa mara katika mikutano ya makanisa ya nyumbani, kama
mlo kamili (ona 1Wakor. 11:20-34). Kuwa kuwa Meza ya Bwana asili yake ni katika
Mlo wa Pasaka, ilikuwa ni mlo kamili ilipoanzishwa na Kristo, na ilikuwa sehemu
ya chakula kamili katika kanisa la kwanza. Hivyo ndivyo inavyotakiwa kuwa hata
siku hizi.
Kwa sehemu kubwa, makanisa mengi yanafuata “mapokeo ya wanadamu.”
Kwa sehemu kubwa, makanisa mengi yanafuata “mapokeo ya wanadamu.”
Tunapaswa kuikaribia Meza ya Bwana
kwa kicho na heshima. Mtume Paulo alifundisha kwamba ilikuwa kosa kubwa
kushiriki Meza ya Bwana kwa jinsi isivyostahili.
Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana. Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate na kukinywea kikombe.
Maana alaye na kunywa hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua ule mwili. Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadha wa kadha wamelala. Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwa. Ila tuhukumiwapo, twarudiwa na Bwana, isije ikatupasa adhabu pamoja na dunia (1Wakor. 11:27-32).
Tunashauriwa kujichunguza na
kujihukumu wenyewe kabla ya kushiriki Meza ya Bwana, na tukigundua dhambi
yoyote ile, tunahitaji kuungama na kuitubu. Vinginevyo, tunaweza kuwa “na hatia
ya mwili na damu ya Bwana.”
Kwa sababu Yesu alikufa na kumwaga
damu yake ili kutuweka huru kutokana na dhambi, kwa kweli hatutaki kushiriki
Meza yenye vitu vinavyowakilisha mwili na damu Yake, tukiwa na dhambi yoyote
ile tunayoijua, isiyotubiwa. Tukifanya hivyo, tunaweza kula na kunywa hukumu
juu yetu wenyewe katika ugonjwa na hata kifo kabla ya wakati, kama ilivyokuwa
kwa Wakristo Wakorintho. Njia ya kuepukana na adhabu ya Mungu ni “kujihukumu
wenyewe” – yaani, kukiri na kutubu dhambi zetu.
Dhambi kuu ya Wakristo Wakorintho
ilikuwa kutokuwa na upendo.
Walikuwa wanagombana wao kwa wao. Ukweli ni kwamba,
kutokujaliana kwao kulijidhihirisha hata wakati wa Meza ya Bwana, wakati
wengine walikula chakula na wengine wanakaa na njaa, na wengine hata walikuwa
wanalewa (1Wakor. 11:20-22).
Mkate tunaokula ni mfano wa mwili wa
Kristo, ambao sasa ndiyo kanisa.
Tunashiriki mkate mmoja, ambao ni mfano wa umoja wetu kama mwili mmoja (ona 1Wakor. 10:17). Ni kosa kubwa sana kushiriki kinachowakilisha mwili mmoja wa Kristo huku tuko katika mapigano na ugomvi na kutokuwa na ushirikiano na viungo wengine wa mwili huo! Kabla hatujashiriki Meza ya Bwana, tunahitaji kuhakikisha kwamba tuko katika mahusiano yaliyo sawa na ndugu zetu na dada zetu katika Kristo.
Tunashiriki mkate mmoja, ambao ni mfano wa umoja wetu kama mwili mmoja (ona 1Wakor. 10:17). Ni kosa kubwa sana kushiriki kinachowakilisha mwili mmoja wa Kristo huku tuko katika mapigano na ugomvi na kutokuwa na ushirikiano na viungo wengine wa mwili huo! Kabla hatujashiriki Meza ya Bwana, tunahitaji kuhakikisha kwamba tuko katika mahusiano yaliyo sawa na ndugu zetu na dada zetu katika Kristo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni