|
Hizi picha haihusiani na tukio linalolipotiwa ila imewekwa hapa kwa sababu ya mahusiano na vitendo vya kishetani |
“Bado
huyu yumo ndani amefungiwa, lakini saa saba za usiku wa kuamkia leo (jana)
alitaka kutoka, aling’ang’ana sana ili atoke, akapiga sana mlango...wakamfanya
dawa ndipo akajaribu kutulia hadi sasa bado yumo ndani na usiku alipewa chakula
akala na asubuhi amepewa uji” alisema mtu wa karibu wa mwanamke huyo.
MAMIA ya wakazi wa Kijiji cha
Lamadi, wilayani Busega mkoani Simiyu, juzi walifurika katika Kitongoji cha
Mabulugu kumshuhudia mwanamke Ngulima Kilinga (30), aliyedaiwa kufufuka huku
mwili wake ukiwa umehifadhiwa katika hospitali ya Mkula iliyopo mkoani humo.
Inadaiwa kuwa mwanamke huyo aliyefariki dunia tangu juzi, alionekana saa chache
baadaye akiwa mzima wa afya na kuingia nyumbani kwake.
Habari zaidi kutoka katika kitongoji hicho zinasema mwanamke
huyo bado amefungiwa ndani ya nyumba yake akifanyiwa dawa za kienyeji ili
arudie katika hali yake ya kawaida, kwani kwa sasa anaonekana kama zezeta.
“Bado huyu yumo ndani amefungiwa, lakini saa saba za usiku wa
kuamkia leo (jana) alitaka kutoka, aling’ang’ana sana ili atoke, akapiga sana
mlango...wakamfanya dawa ndipo akajaribu kutulia hadi sasa bado yumo ndani na
usiku alipewa chakula akala na asubuhi amepewa uji” alisema mtu wa karibu wa
mwanamke huyo.
Pia inadaiwa kuwa tayari mganga wa kienyeji amekwisha kuja kwa
ajili ya kutengeneza mwanamke huyo ili aweze kurudia hali yake na kwamba
amewashukuru wananzengo hao kwa kuweka maiti kwenye nyumba ya mtuhumiwa huyo,
kwamba hiyo ndiyo njia sahihi.
Kamanda wa Polisi mkoani Simiyu, Salum Msangi alithibitisha
tukio hilo, lakini akabainisha hayo ni mambo ya imani za kishirikina.
Kamanda Msangi alisema polisi walipelekwa katika eneo la tukio
kuhakikisha usalama wa wananchi na hadi saa 9:00 jioni jana, maiti ya mwanamke
huyo iliyokuwa hospitali ilikuwa haijazikwa.
Jana umati mkubwa wa watu ulifurika katika Hospitali ya Mkula
kulikohifadhiwa mwili wa mwanamke huyo kuushuhudia.
Ndugu wa mwanamke huyo akiwamo mumewe
Ngitu Masisanga na mama yake mzazi, Mwashi Myeya walisema Ngulima aliugua
ghafla juzi baada ya kukwama na mfupa wa samaki wakati akila chakula nyumbani
kwake.
“Baada ya kuugua alipelekwa hospitali ambako alifariki ghafla na kuwekwa kwenye
nyumba ya kuhiofadhiwa maiti’’ alisema.
Alisema cha ajabu ni kwamba wakati wamelala nyumbani kwa
marehemu sambamba na waombolezaji wengine, saa 7 usiku marehemu alitokea akiwa
uchi.
Walisema marehemu huyo alimwita mtoto wake ampatie nguop na
kuchukua albamu ambapo aliangalia picha.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa mbali na kutazama picha
hizo na kutaka kupewa nguo zake, pia marehemu huyo alichukua tochi iliyokuwa
ikiwaka na kuizima.
Mama mzazi wa marehemu alisema, “Kabla ya kukimbia nje tulimzuia
yeye kutoka nje tulimfungia mlango na sisi ndio tukakimbilia nje, licha ya
kufunga mlango alikuwa akiupiga kwa nguvu ufunguke ila na yeye aweze kutoka
nje, kuna mtu amefanya dawa za kienyeji ndio tunasubiri majibu.”
CHANZO:GAZETI LA MWANANCHI