Baadhi ya waamuzi wa shindano la kutafuta vipaji vya waimbaji wa nyimbo za injili Tanga wakiongoza nyimbo za utangulizi wa Tamasha hilo jukwaani. aliye mbele ni Sister Meclin Ludamila akishirikiana na Hellen Kijazi na Devota Mkanumkole
mara nyingi sana ninapokutana na watu mbalimbali wanaopenda nyimbo za injili wa hapa kwetu Tanga au sehemu nyingine, huwa najisikia mzigo ambao kama sijaongea nao kuhusu namna ya kuinua uimbaji wa nyimbo za injili katika jiji letu la Tanga sijisikii vizuri. najua hali hii imeniletea shida na lawama kutoka kwa waimbaji wa nyimbo za injili hapa Tanga, nimepata ujumbe kwamba wakija waimbaji kutoka nje ya Tanga ninawambia kwamba Tanga hakuna watu wenye vipaji. nimekanusha mara nyingi na hata nilipopata nafasi kwenye Tv nilifafanua sana jambo hili. ninachosema na ninachoamini ni kwamba Tanga kuna waimbaji wengi wenye vipawa vikubwa lakini wamekosa
Fainali zilifanyika katika ukumbi huu wa kanisa la Agape ministry zamani ulikuwa ukumbi wa kuangalia picha za senema uliokuwa ukijulikana kwa jina la Legali hall. |
Kwaya ya kanisa la sabato Nguvumali waliimba kwa ustadi mkubwa siku ya fainali za kusaka vipaji Tanga.
kutangazwa. na hii imetokana na tabia ya viongozi wetu kuwa na tabia ya changu ni changu. na kwa jinsi wanavyotiliana shaka na kutokushirikiana, ndivyo na waimbaji wanavyoshindwa kushirikiana na matokeo yake tuna kwaya nzuri zina nyimbo nzuri na tuna waimbaji wazuri lakini hawajulikani kwa watu wa Tanga bali wanajulikana kanisani kwao na kwa wachungaji wao. na hata wakipata nafasi ya kwenda katika sehemu ambayo wataonekana na kukuza vipaji vyao mara nyingi huwa ni vita kutoka kwa wakuu wao wa dini. kwa kweli Tanga ina watu wengi wanaopenda nyimbo za injili lakini sisi waimbaji hatujiamini ukiona mtu ameandaa tamasha basi ujue kuna waimbaji wenye majina kutoka nje ya mkoa ili kuja kusaidia kuvuta watu na wenyewe wameshagundua hili,siku hizi kuwapata ni biashara kubwa sana. mimi niliwashauri marafiki zangu waimbaji kwamba ni lazima sisi wenyewe tuanze kuandaa matamasha yanayotuhusu sisi wenyewe. tutafute marafiki tutengeneze familia yetu ambayo itatusaidia kuandaa matamasha bila kiingilio au kwa kiingilio kidogo sana ili tuwazoeshe watu kuupenda muziki wa injili na kuacha tabia ya kwenda kushangaa maji ya bahari ya hindi ufukweni. lakini pamoja na hayo tuanze na kuwatayarisha vijana wadogo ili kuwaandaa katika misingi ambayo nao watawarithisha wengine. Watoto wanahitaji kulelewa katika malezi yatakayowazesha kuishi katika mapenzi ya Mungu na kukua katika kicho. Ni muhimu sana kwa kanisa kutambua uwepo na mahitaji ya kuandaa watoto katika kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji. Najua kwa hakika kabisa
jukumu hili ni la Kanisa kwa ujumla hapa nina maana ya mwili wa Kristo na sio kanisa kama jengo la mahali fulani. sasa kama kanisa limepoteza hamu au limejisahau kuchukua jukumu lake ni muhimu kuzidi kumuomba Mungu ainue watu wengine wenye uwezo na ama Mungu awape uwezo wa kuisimamia huduma hii ambayo kwa kweli inalegalega. ukipata bahati ya kuangalia kalenda za makanisa mengi yaliyopo hapa Tanga huwezi kupata ratiba ya tamasha lolote la waimbaji kwa mwaka mzima. ndio maana ninadiriki kusema sisi tulithubutu na tumeona kwamba inawezekana tumeandaa
Mchungaji Bright Mashauri akimkabidhi zawadi ya kumtambua mshindi wa pili wa shindano hilo Earnest Daffa |
Kwaya ya vijana wa kanisa la KKKT mikanjuni wakitoa burudani kwa washiriki na waalikwa wa fainali.za shindano la kusaka vipaji Tanga 2012. |
matamasha matatu kwa mwaka huu 2012,tumeendesha zoezi la kusaka vipaji na washindi wamepatikana. tunawashukuru sana Novelty Youth Centre,Dr Kijazi na marafiki wengine ambao walitusaidia kufikia malengo. na neno litasimama.
Kwanini wao watamani tu kuona na kushiriki vitu kama kili music award au Bongo star search pasipo kuwapa hamasa katika kuinua vipaji vitakavyo mpa mungu utukufu?
Mkurugenzi wa kituo cha kulea vijana Tanga Nolverty Youth Centre akitoa cheti cha utambulisho kwa mshindi wa tatu wa shindano hilo Yohana Kuziwa ambaye alifanya vizuri sana. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni