rr
Fahamu
ndege kubwa duniani;Boeing kuwasilisha 787 ya kwanza kabisa
Kampuni ya utengenezaji ndege ya Marekani - Boeing - itawasilisha rasmi ndege ya kwanza aina ya 787 Dreamliner kwa shirika la ndege la All Nippon Airways (ANA) la Japan.
Dreamliner
Awali Dreamliner
ilipangwa kuwa tayari mwaka 2008, lakini Boeing imekumbwa na mfululizo wa
vikwazo, ambapo hivi karibuni moto uliwaka ndani ya ndege za majaribio mwezi
Januari.
Ndege hiyo isiyotumia
mafuta mengi imetengenezwa kwa kutumia malighafi nyepesi.
Boeing inapanga
kutengeneza ndege 10 kwa mwezi kuanzia mwaka 2013.
Ndege hiyo itakabidhiwa
kwa ANA katika kitongoji cha Everett, Washington kabla ya kuruka na kwenda
Tokyo ambapo itawasili siku ya Jumatano.
Dreamliner
Boeing imesema ndege
hiyo yenye safu mbili na ukubwa wa kati ina madirisha makubwa na hali nzuri ya
unyevunyevu ndani ya ndege na hewa safi hali ambayo itaruhusu abiria kuwasili
wanapokwenda wakiwa katika njema zaidi.
Lakini matatizo ya
Dreamliner yameharibu sifa ya Boeing, na kampuni hiyo ina matumaini kuwa
uzinduzi wenye mafanikio utasaidia kufuta ucheleweshwaji uliotokea.
Mashaka
Makamu wa rais wa
masuala ya masoko wa Boeing, Randy Tinseth ameiambia BBC: "Huu ni mradi
ambao umetoka mbali. Tunaamini itakuwa ndege nzuri.
"Hatimaye tunaona
matumaini ya maelfu ya 787 katika siku za mbele."
Alipoulizwa sababu za
kuchelewa kutoka kwa ndege ya Boeing 787 Bw Tinseth amesema "kuna mashaka
katika kila ndege mpya".
Amesema:
"Tumetumia fedha zaidi katika ndege hii kuliko tuliyotarajia, lakini kwa
mara nyingine tena bado tupo katika nafasi nzuri, tunaamini mradi huu
utaendelea kuwa na faida."
Uzalishaji
Uzalishaji wa
Dreamliner kwa sasa unatoa takriban ndege 2.5 kwa mwezi.
Mpaka sasa ndege
zipatazo 821 aina ya 787 zinatakiwa kununuliwa kutoka Boeing, ambayo inasema
inatumia 20% pungufu ya mafuta yanayotumiwa na ndege za kawaida za ukubwa huo.
Boeing na Airbus
Ikiwa na uwezo wa
kubeba abiria 290 katika ndege yake kubwa ya 787-9, lakini 787 ni ndogo kuliko
jumbo jet 747 ya Boeing.
Hata hivyo, Boeing
inadhani kuwa 787 itakuwa maarufu katika makampuni ya ndege, kwa kuwa itakuwa
na uwezo wa kuruka moja kwa moja kwenda katika viwanja vidogo vya ndege.
Mahasimu
Mahasimu wa Boeing wa
Ulaya, Airbus, kwa sasa inatengeneza mshindani wa moja kwa moja wa 787, iitwayo
Airbus A350 XWB.
Airbus imepokea maombi
ya ununuzi yanayozidi ndege 550 ya A350 XWB, lakini ndege hiyo haitakuwa tayari
hadi mwaka 2013.
ANA inatazamia kuanza
kutumia ndege ya kwanza aina ya 787 katika safari kutoka Tokyo kwenda
Okayama-Hiroshima tarehe 11 Novemba.
Baadaye itaruisha ndege
hiyo kimataifa kutoka Tokyo kwenda Frankfurt Ujerumani, mwezi Januari.
"Watu wengi
wanasema kuwa ndege hii [787] itakuwa maarufu sana," amesema George
Hamlin, rais wa taasisi ya washauri wa usafirishaji ya Hamlin.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni