Faida za kufanya kazi au shughuli inayodharauliwa
Rais wa marekani Barack Obama akiwa na bibi mzazi wa baba yake husein Obama alipokuja kuwatembelea nyumbani kwa mababu zake Kenya |
nyumba,
miradi na biashara kubwa huku wafanyakazi maofisini wakigeuka wakopaji kwenye
maduka ya Wamachinga wanaotembeza nguo mikononi kwenye mitaa ya mijini? Naamini
ushahidi upo wa kutosha.
Maeneo mengi ya wakulima wa zao la tumbaku katika mkoa wa Tabora, kwa mfano, na vijana wanaomiliki maduka madogomadogo maarufu kama vioski ni wageni ambao walifika kwenye mkoa huo kama watumishi au wasaidizi wa mashambani, wakifanya kazi dhaifu ambazo wenyewe huzitafsiri kama shughuli zisizokuwa na heshima. Lakini pato la kazi hizohizo ndilo hatimaye huwapatia vioski ambavyo wenyeji huenda kukopa bidhaa.
Katika hali ya kawaida, kazi zinazoonekana dhaifu ni funzo kubwa sana katika maisha na mara nyingi hujenga ari ya aina yake katika uwajibikaji wenye lengo la kujikomboa na hiyo zana ya kudharaulika.
Watu wengi matajiri historia zao huanzia kwenye kazi dhaifu. Huko ndiko kulikowafunza nidhamu ya matumizi ya fedha. Kwenye dharau kumejaa maarifa na mbinu za ukombozi kuliko mahali penye maisha ya heshima ambako hupumbaza na kuwafanya wahusika wasipige mbio kuelekea kwenye mafanikio zaidi.
Wito wangu kwa vijana wenzangu, Watanzania wote, tusikubali kuishi na ufalme, heshima na utukufu usioweza kutusaidia, badala yake tukubali kufanya kazi hata zinazoonekana dhaifu kwa lengo la kujipatia kipato ili hatimaye tutafsri hali ya kudharauliwa kuwa heshima

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni