MWENDO WA KANISA WAKATI
LINAPOPITA KATIKA VIPINDI VYA MABADILIKO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA SISI JE
TUTAPATAJE KUPONA.
Dunia inapita katika kipindi cha mabadiliko
makubwa Sana katika Nyanja ya sayansi na teknolojia. Kasi ambayo dunia
inakwenda ni kubwa sana kuliko tunavyofikiri, Na inagusa karibu katika nyanja
zote za maisha ya kila siku ya binadamu ikiwemo hata na ndani ya kanisa. Biblia
inaposema kwamba katika nyakati za mwisho maarifa ya wanadamu yataongezeka,watu
wengi hudhani kwamba kanisa halitahusika na mabadiliko hayo lakini ukweli ni
kwamba kanisa ni mdau wa mabadiliko na kamwe haliwezi kujitenga na mabadiliko
yanayotokea duniani kisayansi,kiutamaduni,kijamii n.k.
Magarimoshi
ya mwanzo kabisa
gari
kwanza linalotumia mvuke haya ni Gari la
linalotumia umeme haya ni baadhi
mapinduzibaada ya kutoka kwenye ya
maendeleo makubwa ya teknolojia
magari yanayokokotwa na wanyama.
Mara nyingine wakati nchi yetu ambayo iko katika
kundi la nchi zilizoko katika dunia ya tatu inapojiandaa kuingia katika
mabadiliko fulani ambayo nchi zilizoendelea na zinazoendelea imefikia, inakuta
dunia ya kwanza na ya pili zimeshahama huko na kwenda hatua ya mbali zaidi.
Hali hii imesababisha kanisa kuburuzwa na mabadiliko haya na kuwa kama mchezaji
mlalamishi katika uwanja wenye mabadiliko ya sheria na kanuni za mchezo wa
maisha katika jamii. Wenzetu walioipigania injili walijitahidi sana kujaribu
kupingana na mabadiliko haya yasiingie ndani ya kanisa lakini walishindwa hii
ni kwa sababu waliotuletea dini hizi walileta bia na utamaduni wao ambao wao
wanauita ustaarabu na ndio maana dini za kikrito waliotuletea dini hii walitoka
ulaya na ndio waliotuletea ustaarabu wa kuvaa suruali na mashati na wakati
unahubiri ni vizuri uvae koti japo na tai tofauti na walioleta dini ya kiislamu
ambao wanatoka mashariki ya kati na ambao vazi lao la heshima ni kanzu na
vinginevyo hawakuelewi. Mtumishi mmoja aliniambia kwamba zamani ilikuwa ni
marufuku hata kutumia gitaa kwenye ibada, ile kukubali tu kutumia magitali
ndani ya kanisa lao ilikuwa ni mjadala mgumu sana na hata ilipokubaliwa
walikuwa na aina ya mapigo waliyotakiwa kupiga. siku moja walipiga wimbo mmoja
kwa mtindo wa regae ya Jamaika ambayo kwa wakati huo ilikuwa inavuma sana miaka
hiyo ya 1970. Baada ya ibada kwisha kwaya nzima walisimamishwa na wengine
wakatengwa. Lakini siku hizi hakuna kitu kama hicho na kanisa kama halina
magitaa watu ni vigumu sana kuhisi kama kweli wameabudu. Hapo tunaweza kusema utandawazi
umeingia mpaka kanisani.
Wengine walijaribu kuzuia kwa kufunga na
kuomba ili kwamba matumizi ya internet yasiingie Tanzania na hata yakiingia
yasiguse kanisani wakiamini kabisa kwamba ni mtandao wa mping Krito lakini
haikuwezekana hatimaye yaliingia na hatimaye wao wenyewe siku hizi wanayatumia
na wanaona yana faida kubwa sana katika kazi ya Mungu na makanisa ambayo
hayatumii mtandao yanajirudisha nyuma na kujiweka katika wakati mgumu kupambana
na mazingira yanayobadilika kila kunapokucha.
Hapa
ni mchanganyiko wa ndege za kizamani na ndege za kisasa kulingana na mabadiliko
ya teknolojia inavyokwenda kasi sana.
Sasa hivi wataalamu wanafikiria kutengeneza
memory card kama zinazotumika kwenye simu kwa ajili ya kuweka na kupata taarifa
za binadamu ambazo zitachomekwa ndani ya
miili ya watu,kama vile walivyokuwa wanapandikiza vijiti katika uzazi wa mpango
ambavyo
Vitawawezesha kila mtu anaposafiri hakutakuwa
na haja ya kuchukua pasiport ila
kutakuwa na mashine maalumu mipakani,kwenye viwanja vya ndege na kwenye ofisi
za uhamiaji ambazo mtu akipita zitasoma taarifa na kumbukumbu zake zote.
Viongozi wakuu wa duia Baraka Obama wa USA na rais
wa urusi hawa ni viongozi wanaoongoza dunia kama wanavyotaka.
Haya ndio maandalizi ya kuifanya dunia kuwa
kijiji kimoja, na kuivunjilia mbali kabisa mipaka ya mataifa. Jambo hili Biblia
ilishaliona na kwa kweli halikwepeki tutake ama tusitake ni lazima hatimaye
dunia itakuwa na kiongozi mmoja. Na tutatumia sarafu moja na watu hawataulizana
juu ya utaifa wa mtu, haya mabadiliko tunayoyaona ya jumuiya za kikanda kama
SADC, ECOWAS n.k. ni maandalizi ya huko tunakoelekea
.
UTANDAWAZI
NINI MAANA YAKE NA UNA NIA GANI.
Nia kubwa ya utandawazi ni kuvunjilia mbali
mipaka ya nchi na kuifanya dunia hatimaye kuwa kama kijiji kimoja katika nyanja
za elimu, mawasiliano, sayansi na Teknolojia.
Haya
ni baadhi ya mavazi ya vijana wa kisasa ni vigumu sana kuwatoa hapo na ndio
tunaowahubiri waje kanisani kama walivyo ili Yesu awabadilishe
Tangu zama za mawe dunia imekuwa ikipita
katika mabadiliko mbalimbali yenye lengo la kumsaidia mwanadamu na
kumrahisishia kukabiliana na maisha yake katika mazingira yake. Mtoto mmoja wa
kizungu alimwambia mtoto mwenzake wa kiafrika ambaye alimuona akihangaika
kujumlisha mahesabu kwa kuandika akiona aibu kutumia kikokoteo cha hesabu
(Caluculator) akamwambia sasa babu zetu walihangaikia nini kubuni chombo hiki
kama hutaki kukitumia, ilikuwa ni wajibu wao kuturahisishia sisi maisha ili na
sisi tuwarahisihie watoto wetu maisha. Na hii nikweli tunajua kwamba binadamu
alianza kusafiri kwa miguu, punda wenye
Wabunifu
wa mitindo ya mavazi nao wakiwa kazini kubuni mavazi ambayo wanaamini
yatawavutia vijana wa kizazi cha kisasa.
mikokoteni Na kila siku watu wamekuwa
wakibuni vitu mbalimbali kwa lengo la kurahisisha maisha ya mwanadamu, ndio
maana tunaweza kusema kwamba wale watu waliotajirika sana duniani ni wale
waliobuni vitu ambavyo vilikuja kuwasaidia sana wanadamu kutatua matatizo yao,
fikilia kwa mfano mtu aliyevumbua vyombo vya usafiri kama vile gari, ndege n.k.
DUNIA
KATIKA MABADILIKO MAKUBWA
Katika karne ya 21 dunia iliingia katika
mabadiliko makubwa Sana pamoja na kwamba watu wengi walihisi kwamba kompyuta
zingeshindwa kuusoma mwaka 2000 kwa sababu mwaka huo haukuingizwa kwenye
kompyuta lakini wataalamu wakabuni kitu kilichojulikana kama Y2K ili kuendeleza na kubuni mambo
mengine makubwa zaidi ambayo kwa kiasi kikubwa yameleta mabadiliko makubwa katika
ulmwengu wa sayansi kwa lengo la kumsaidia mwanadamu kukabiliana na maisha
yake.
Tangu wakati huo teknolojia ya habari na
mawasiliano (Teknohama)
imekuwa ni muhimili mkubwa sana unaobeba mabadiliko haya. Wakati Biblia inatoa
tahadhali kwamba katika nyakati za mwisho maarifa ya wanadamu yataongezeka Sana,
watu waliookoka ndani ya makanisa wanadhani kwamba andiko hilo haliwahusu wao
bali linawahusu watu wa dunia. Matokeo
yake kanisa linajikuta linaburuzwa na mabadiliko ya dunia bila kuwa na
maandalizi ya kimkakati ili kupambana na mabadiliko yanayoletwa na sayansi na
teknolojia kwa sababu hayana budi kuja na ni lazima yaje. Paulo mtumishi wa
Mungu aliwahi kuwaeleza wakorintho kwamba alipowaambia wajitenge na dunia,
hakuwa na maana kwamba waondoke kabisa hapa duniani. Bali aliwataka wajitenge
na tabia za kidunia.
TUNAWEZAJE
KUJITENGANISHA NA TABIA ZA KIDUNIA?
Lakini kwa hali yoyote ile ni vigumu sana
kuwatenganisha watu wanaoishi hapa duniani na watu waliopo kanisani kwa sababu
watu waliopo kanisani ni zao la jamii ya watu waliopo katika mazingira hayo na
kwa uhakika ni haohao, isipokuwa
wakiingia kanisani kuna mafunzo wanayoyapata
mafunzo yanayohusu namna ya kumjua Mungu na thamani ya wokovu na hali
halisi ya maisha ya dunia inavyokwenda,
kwa ujumla hakuna namna ya kujiepusha na mabadiliko ya hali ya dunia kwa sababu
hakuna sehemu inayoweza kusalimika au kuepuka mabadiliko haya kwa sababu hiyo
ni muhimu kuweka mikakati ya kueleweka bila ya hivyo kanisa linaweza kujikuta
linaingia katika mabishano ya vitu vidogovidogo kama mitindo ya mavazi,mapambo
ya akina mama na nywele mitindo inayoletwa na mabadiliko ya nyakati, kama
tunavyoona mambo yanayoendelea hivi sasa wakati nguvu kubwa ya fedha inatumika
kununua vipindi kwenye Televisheni kwa nia ya mabishano ambayo hayana faida
yoyote kwa kukuza kazi ya Mungu.
MTINDO
WA KUWAZUWIA NA KUWAFUKUZA WATU KANISANI
Hakuna
mwanadamu aliyekufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu na kanisa ni mali ya Bwana
Yesu ni makosa kumfukuza mtu kanisani wakati aliyemfia bado anamuhitaji.
Makanisa Mengine yamefikia hatua ya kuwazuwia
au kuwafukuza watu kuingia kanisani. Cha kusikitisha zaidi ni kwamba watu hao
ni jamii ya watu ambao bado hawajaamini ambao wamewasindikiza ndugu zao kwenda
kwenye maombezi kanisani. Lakini wakifika milangoni wanakuta kuna watu
wamewekwa na kanisa kwa nia ya kuwakagua na wakiwaona labda wamevaa au
wametengeneza nywele saluni, basi wanawalazimisha wafunge vilemba au wavae
kanga na magauni marefu.
Ukifikiria
sana utaona kwamba hapo kuna tatizo kubwa sana na kuna maswali mengi
sana ya kujiuliza na swali la muhimu sana hapo ni kuuliza ni jukumu la nani? Kumsaidia
mtu huyu aweze Kubadilika na kuwa mtu mwenye kiwango cha kufaa kuingia katika
majengo ya kanisa lenu?.
KANISA
NI MFANO WA MASHINE YA KUSAGA
Mtu anapokwenda mashine kusaga nafaka ili
kupata unga akiwa mashine ataona vitu vitatu muhimu. Kwanza ataona kinu hii ni sehemu ambayo
ukifika mashine unaweka nafaka na mara nyingi kuna mtu anayekuwa pale
kuhakikisha zile nafaka zote zinakwenda kwenye mkondo unaotakiwa na kuzielekeza
kwenda sehemu ya pili ambayo ni kwenye mashine yenyewe mortal. Kazi ya mortal ni kuisaga nafaka hii ili iwe unga na
kisha ataona kitu cha tatu ambacho mara
nyingi huwa ni mfano wa bomba ambalo limezungushiwa kitambaa cheupe na sehemu
hii ndiko unakotokea unga safi uliotokana na nafaka iliyosagwa na mortal. Kwa maana hiyo, kama itatokea
nafaka ambayo haikusagwa basi ujue kwamba haikupita katika mortal kwa mfano huu ni kwamba watu wa dunia ni mavuno (nafaka). Wakristo
waliookoka ni sawa na watenda kazi ya kwenda shamba na (kuvuna watu wa dunia na
kuwapeleka kwenye kanisa) kuleta nafaka mashine. Wakifika mashine kuna mtu
wanayemkabidhi nafaka hizo ili aziweke kwenye kinu, tayari kwa kuzisaga kuwa
unga ambapo kwa mfano huu kinu ni kanisa la Mungu ambapo watenda kazi (washirika wa kanisa) kazi yao ni
kuleta nafaka mashine na wakifika hapo mashine kuna mtu (Mchungaji), yupo hapo
kwa ajili kuziongoza hizo nafaka kuelekea kwenye mortal (Roho Mtakatifu). Kwa hali yoyote nafaka zikifika
kwenye kinu haziwezi kubadilika na kuwa unga bila kupita kwenye mortal ambayo ni mafundisho na maisha
ya kiroho yanayoletwa na Roho Mtakatifu, na kumbadilisha mtu taratibu hatua kwa
hatua hadi kuwa mtu anayetakiwa.
Kwa kutokulijua hili au kwa ghiliba za
shetani, watenda kazi wasiokuwa na ujuzi wa vita vya kiroho badala ya kufurahia
na kushukuru Mungu kwamba mavuno yamekuja yenyewe kwenye kinu bila
kuyafuatilia. Badala ya kutulia na hao watu na kuwaelekeza kwenye kinu kwa
upole na upendo mwingi.
Wao wanataka watu hao wageuke unga ghafla
bila kupitia kwenye mortal
kitu ambacho kwa kweli hakiwezekani. Nafaka ikiwa kwenye kinu hata ukemee mpaka
Mapovu ya damu yakutoke, Nafaka bila kupita kwenye mortal haiwezi kugeuka na kuwa
unga. Hata kama ukikemea na kuomba mpaka siku Yesu akirudi punje ya nafaka
itabaki kuwa punje, ni mpaka utakapofuata kanuni za Mungu, kwa sababu ni Mungu
anayetupa mabadiliko ya kweli katika wokovu. Inawezekana yule anayewazuwia watu
wasiingie kanisani wakati watu wanaotaka kukutana na Mungu wao aliyewanunua kwa
damu yake ya thamani. halafu yeye anawazuwia kana kwamba yeye aliokolewa kwa
sababu alikuwa mtakatifu sana. Mtu huyo nina mashaka naye sana kama sio wakala
wa shetani, basi hajui anachokifanya na ama hajui sababu ya kifo cha Bwana Yesu
pale kalvary.
KILA
MTU KANISANI NI MUHIMU NA ANAFAA KWA MUNGU.
Inawezekana mtu huyo akawa sio muhimu kwako
wala kwa kanisa lako lakini mbele za Mungu ni mtu muhimu sana na anajulikana
sana kwenye ufalme wa mbinguni.
Wakati fulani nilikwenda kutembelea kanisa
moja nje kidogo ya Mji wetu, na baada ya kumaliza kufanya huduma, Mchungaji wa
kanisa lile akaniongoza ofisini kwake kwa Mapumziko na mazungumzo mafupi.
Wakati tunaendelea na mazungumzo hayo
aliingia ofisini mshirika mmoja wa kike kwa shughuli za kiutumishi, na baadae
alipotoka nje ya ofisi mchungaji alitaka kupata mawazo yangu na maoni yangu
kuhusiana na muonekano na hasa mavazi aliyokuwa amevaa yule mwanadada.
Spika
wa Bunge la Tanzania Anne Makinda akiwa na watanzania wengine katika mavazi ya
kisasa na ya heshima yanayovaliwa na watanzania wenye umri wa makamo,lakini
hata vijana wakivaa mavazi kama haya huwa wanapendeza sana.
Wanakwaya
wa kisabato kutoka Rwanda mavazi yao huvutia sana watazamaji wanaowahudumia kwa
uvaaji wa mavazi nadhifu.
Wanakwaya
wa Ambasador wakiwa na mmoja wa wanakwaya wa kitanzania anayehudumu kwenye
kwaya hiyo
Kwanza sikuelewa mchungaji anataka kusema
nini juu yake, hata hivyo nilikuwa naamini kuna kitu anataka kunifundisha
kutokana na swali hilo hivyo ilinibidi niwe makini kueleza jinsi ninavyomuona
kwa hisia zangu mwenyewe. Nikamwambia mchungaji huyu dada amevaa vizuri sana na
ningependa wakina dada wote makanisani mwetu wavae mavazi ya heshima kama
aliyovaa yule dada, kwanza ni mavazi ya kisasa na unaweza ukaingia nayo mahali
popote kwenye hadhi kubwa.
Nikaona mchungaji anacheka kisha akaniambia
alitegemea majibu kama hayo kutoka kwangu ila akaniambia kuna kitu kikubwa sana
ambacho yeye binafsi Mungu amemfundisha kupitia katika maisha ya yule dada.
Akasema huyu dada alikutana na Bwana Yesu akiwa kwenye shughuli za ukahaba changudoa akiwa kwenye danguro (sehemu ambako
watu wanajiuza miili yao) na alikutana na Bwana Yesu akiwa huko na akamuongoza
kuja katika kanisa hili analolichunga na yeye akampokea. Anasema kama
unavyofahamu, Maisha ya watu wa aina hii hakuwa na nguo ya maana hata moja.
wa
Haya
ni baadhi ya mavazi ambayo tukijaribu kuyajadili tunaweza kuonekana kama vile
watu wa mashambani, lakini ukiyaangalia utaona kuwa yapo kibiashara zaidi. Na
hatutegemei kwamba siku moja yataingia kanisani.
Nguo zake nyingi zilikuwa ni zile alizokuwa
anazivaa kwenye shughuli zake za kujitafutia riziki kwa njia haramu. Anasema
alipofika kanisani washirika hawakumkubali na wengine walikuwa wakimtolea
maneno ya kashfa kwamba anawadhalilisha, wengine walitaka aondoke kabisa
kanisani. Hili jambo ni lazima watu walifahamu kwamba kanisa ni mali ya Yesu
mwenyewe na yeye ndiye anayejua nani ampeleke katika kanisa gani, si jukumu
letu kulalamika kwamba mbona kanisa ninalolichunga halina matajiri au
wafanyakazi wenye hadhi kubwa (waheshimiwa) kanisa lipo kwa ajili ya watu
wote.
Dunia ni kama bahari iliyochafuka na kanisa ni
kama meli ya usalama iliyoko juu ya bahari. Watu wanapookoka inakuwa ni sawa na
watu waliozama baharini wanategemea wakiokolewa na kuingia kwenye Meli (kanisa) watakuwa salama na
watafundishwa namna ya kuishi kwenye meli hiyo. Sasa hawawezi kujifunza kwa
siku moja au mbili wengine inaweza kuwachukua miaka kadhaa kuweza kujua namna
ya kuishi katika chombo hicho (kanisa) Mchungaji yule anasema mara nyingi yule
dada alikuwa anakwenda ofisini kwake akiwa analia na kueleza jinsi ambavyo
anabaguliwa na kusemwa vibaya na washirika wenzake ndani ya kanisa.
Mwaimbaji
Rebecca Malope toka Afrika Kusini akijiandaa kuingia kwenye jukwaa akiwa
amevalia mavazi ya asili kutoka kwao. Je watanzania tuna mavazi gani
yanayotutambulisha kama Taifa? Usinijibu jibu baki nalo mwenyewe.
Mchungaji alimwambia kwamba wala asisikilize
neno la mtu awaye yeyote kuhusu kitu chochote kama kuna kitu kibaya yeye
mchungaji ndio atamwambia. Kwa maana yeye ndio mchungaji wake. Maneno yale
yalikuwa yanamfariji sana yule dada na kumpa bidii ya kuhudhuria vipindi karibu
vyote vya kanisani. Baadae alianza kubadilika na akawa anavaa vizuri kushinda
hata wale waliokuwa wanataka kumfukuza kanisani. na kwa kweli ni mtu anayempenda sana Bwana
Yesu na hata wakati huo alikuwa ni msaada mkubwa sana kwa mchungaji wake na kanisa
lake kwa ujumla.
Muda mwingi Yule dada anautumia kanisani kwa kuombea
watu wanaofika kanisani na kufanya usafi wa kanisa.
Hii ilikuwa ni habari ya ajabu sana kuhusu
nguvu ya Roho mtakatifu inavyoweza kumbadilisha mtu kutoka katika shimo la giza
na kumfanya kuwa nuru na kielelezo kwa wengine. Mchungaji anasema katika
mafundisho aliyokuwa akipewa na Mungu kwa ajili ya kanisa kwa kipindi chote cha
mabadiliko ya yule dada hakukuwa na mafundisho kabisa yanayohusu mavazi au
mabadiliko ya tabia, mafundisho mengi yalihusu imani na nguvu za Mungu.
Kikundi
cha wanakwaya wakiwa nadhifu kabisa wakimtumikia Mungu.
Nimekupa ushuhuda huu makusudi ili uweze
kufahamu kwamba
Imani huwa inazaliwa na imani huwa inakuwa
ama inaongezeka kulingana na jinsi ambavyo unavyojitoa mbele ya Mungu, na jinsi
vile Mungu anavyoonekana kwako. Kwa sababu imani ni mchakato na maisha ya
wokovu ni kuzaliwa mara ya pili haitawezekana mtoto akazaliwa mara moja akaanza kuongea na kutembea
ni lazima tufahamu kwamba, mtoto kabla hajakuwa mtu mzima kuna hatua nyingi
anazopitia na anahitaji uangalizi wa hali ya juu sana . Kuna makosa mengine
mtoto akifanya wala huwezi kumlaumu bali utawalaumu walezi wake au wasimamizi
wake, lakini kuna kipindi ambacho mtoto anapoendelea kukua inabidi kumwelekeza
kwa bidii juu ya nini anachotakiwa kukifanya na kipi hatakiwi kukifanya na kuna
kipindi kinapofika huna haja tena ya kumwelekeza mtoto nini cha kufanya hapo
ndipo utakapoweza kumuadhibu lakini inapotokea mtoto amezaliwa tu na wewe
unaanza kumchapa hata kabla hajajua maisha yanakwenda vipi. Ukifanya hivyo wewe
mzazi watu watakulaumu na ikibidi serikali itakupokonya mtoto huyo alelewe na
mtu mwingine. Maana wewe utamuua mtoto (kwa maana wewe hujui kulea kuna kumwogesha
kumnawisha akijichavua na kumtunza kwa upendo,kama kuna mchungaji hajui jambo
hili basi ni hatari kwamba imani yetu itakuwa imevamiwa kwa kiasi cha kutisha
sana au huyo mchungaji atakuwa ama amechukua washirika kutoka kwa wachungaji
wengine au labda anachunga malaika kutoka mbinguni lakini kama ni wanadamu wa
kizazi cha leo ni lazima awe mpole na afanye kazi ya Mungu kwa uvumilivu sana,
kitendo chochote cha kumfukuza mshirika ama kumzuwia kuingia katika jengo la
dini yako ni kukwepa wajibu wa kiutumishi, kwa sababu watu hawawezi kufanana na
unaweza ukamuona wewe mtu Fulani hafai na matokeo yake akaja kuwa mtenda kazi
hodari kabisa nyumbani kwa Mungu na akawa msaada mkubwa kwa ufame wa Mungu na
ukashangaa kabisa, haya mambo yameshatokea sana kwa watumishi wengi waliwafukuza
watu na baadae wakaja kugundua kuwa ama hawakushauriwa vizuri au hawakutulia
vizuri kumsikiliza Mungu. Maisha ya Kiroho Sio Mepesi Kama Tunavyofikiri.
TUNAPAMBANA NA SHETANI YULEYULE WA KWENYE
BUSTANI YA EDEN LAKINI KATIKA MAZINGIRA YALIYOBADILIKA SANA.
Ni muhimu sana kufahamu kwamba tunapambana na
shetani yuleyule aliyemuangusha Adamu na mkewe Eva katika bustani ya eden
lakini tunapambana naye katika mazingira yaliyobadilika sana. Na ni lazima na
sisi tuhakikishe kwamba tunakwenda na kubadilisha mbinu mara kwa mara ili
kukabiliana na dunia inayobadilika kwa kasi kubwa.
Kama
kijidudu cha maralia tumekibadilishia dawa mara nyingi sana, lakini bado
kijidudu hiki kimeendelea kuua watu wengi zaidi kuliko ugonjwa wa aina yeyote
na kwa kweli dawa yake halisi ni quinen. Lakini tumekibadilishia dawa za aina
mbalimbali kama vile cloloquine maralaquin shelaquin n.k. na kama
unavyoona katika kila dawa ilipobadilishwa qunine ilikuwepo ndani yake.
Hapo ina maana kwamba kila walipokuwa
wakitibu kijidudu hiki kiliporudi kilikuja kikiwa kimejiimarisha zaidi na
kujikinga ili kuzuwia Quinen isikipate, pengine kiliweka gamba gumu na kufumba
mdomo wake. Matokeo yake dawa inaonekana haifai.
Hapo inabidi itafutwe dawa ambayo kwanza
itakwenda kuvunja lile gamba na kisha itakibana mdomo kile kijidudu na ndipo
Quinen itapitapenya na kukipata kile kijidudu na kukiua. Ndio maana siku hizi
kuna dawa mseto ya maralia maana yake ni mchanganyiko wa dawa zaidi ya moja hii
ndio maana ya neon mseto.
Nimetoa mfano huu kukuonyesha kwamba kama
kijidudu kidogo cha maralia kimetusumbua na tumekibadilishia dawa mara nyingi
kiasi hicho nab ado kinatusumbua je itakuwaje kwa shetani. Ni wazi kwamba
hatuwezi kupambana na shetani kwa staili ileile iliyotumika kwa mfano miaka
kumi tu iliyopita.
Kwa wale watu wa siku nyingi kidogo
watakumbuka kwamba baada ya kupata uhuru nchi yetu iliamua kufuata mfumo wa
siasa ya ujamaa na kujitegemea ambayo ilimlazimisha kila mwenye uwezo wa
kufanya kazi anafanya kazi na wakati huohuo serikali ilijitahidi kuhakikisha
huduma zote muhimu na za msingi watu wanazipata bure kwa hiyo watu waliishi
kijaa zaidi.
Kwa sababu hiyo hakukuwa na wizi kabisa,
katika nyumba zingine watu waliweka pazia tu wala wezi hawakuiba,lakini baadae
baada ya kutoka kwenye misingi ile ya ujamaa ambayo ilijali zaidi utu wa mtu na
kuingia katika siasa zinazochanganyikana na ubinafsi watu walianza wizi,ilibidi
watu wabadilishe na waanze kutengeneza milango mingine ya mabati na baadae
milango ya mbao. Lakini wezi nao walikuwa wanabadilisha mbinu na kuvunja
milango ya mbao kwa kutumia mawe makubwa yanayowekwa kwenye magunia na kurushwa
kwa nguvu kwenye milango ya mbao na kuivunjilia mbali. Mawe haya wanayaita jina
la “fatuma.”
Siku
hizi watu wanajenga majumba makubwa yenye milango ya chuma na walinzi wenye
bunduki na majibwa wakali lakini bado wezi wanaiba. Mlinzi analeweshwa au
ananyongwa,mbwa wanapewa maini ya sumu na wezi wanakuja na gesi ya kukatia
vyuma wanaingia na kuharibu
Tena katika hali nyingine ni afadhali nyumba
yako uweke vitasa kuliko kuweka kufuli maana ukiweka kufuli ni sawa na kuweka
tangazo kwamba mwenye nyumba hii hayupo.
Mifano hii miwili ingawa inaweza kuwepo na
mingine mingi ambayo itatusaidia kufahamu kwamba mbinu zinabadilika kulingana
na hali na nyakati.
Tukumbuke kwamba kila nyakati zina watu wake
na stahili zao za maisha, wakati Yohana mbatizaji analeta injili kwa watu wa
kizazi chake walimpokea na walimkubali kwa staili aliyoingia nayo ya kuvaa
mavazi ya ngozi na kula asali na matunda watu walimuelewa na walitubu. Lakini wewe mtu wa kizazi cha leo ukija na staili
kama hiyo ya Yohana mbatizaji ni lazima ukamatwe na ndugu zako na utapelekwa
kwenye wadi za wagonjwa wa akili. Maana mahali ilipofikia dunia huwezi
ukaipeleka kwa staili hiyo utakuwa pia hujaitende haki.
Wakati nchi yetu ya Tanganyika inapata uhuru Elimu ya rais wa wakati
huo JK Nyerere ya digrii mbili ilitosha kabisa kuendesha nchi na kwa sehemu
kubwa mpaka leo hii bado watu wanamheshimu na kumuona kwamba alikuwa na akili
nyingi sana .
Lakini leo hii hao watu wenye digrii mbili ni watoto wadogo sana na wengine bado hawajapata kazi za
uhakika. Kuna makanisa mengine yana vyama vya akina mama ambao wengi wao
wamezidi miaka 45 na kutokana na mavazi yao kwa umri walionao wanataka na
mabinti wa chini ya miaka 18 wavae mavazi kama wanayovaa wao,ambayo hata wao
walipokuwa mabinti hawakuvaa mavazi kama hayo. Ni lazima tukubaliane kwamba
kila nyakati zina watu wa aina yake na mitindo yake ya mavazi, hata siku hii ya
leo unaweza ukavaa aina Fulani ya mavazi na watu wakakushangaa kwamba huyu
ndugu mbona amevaa mavazi ya zamani sana .
Hapo ni lazima tukubaliane kwamba lengo kubwa la mavazi ni kusitiri maungo ya
miili yetu na suala la kujipamba au kupendeza ni kitu kingine. Mchungaji mmoja
rafiki yangu alitoa onyo kwa akina mama wa kanisa lake
kuacha kuwasumbua mabinti wanaokuja
kanisani kuhusiana na mavazi na mapambo ya nywele aliwaambia ni afadhali kama
wao wanaona shida kukaa nao basi waondoke wao na wasifanye kazi ya kuwafukuza
vijana hao kwani hata wao wakati wanaingia kanisani hawakuwa kama
walivyo sasa.
KANISA
NI NINI?
Je kanisa ni jengo? Hapana! Kanisa ni mtu
aliyezaliwa mara ya pili na ambaye amejazwa na roho mtakatifu na Mungu
anamtumia katika kuujenga ufalme wake. Hii hasa ndio tafsiri halisi ya kanisa.
Tukilijua hili litatuwezesha kufikiria namna ya kumtayarisha mkristo mmojammoja
kibinafsi na hatimaye tukiwa kama kikundi ndio tunapoweza kuwa na kanisa imara
la mahali. Hatutaweza kuacha jukumu la wito wetu kwa Mungu na kuanza kushindana
na kupigana vijembe kwa mambo yasiyokuwa na maana baina ya watumishi au
kufukuzana kwenye majengo ya dini zetu. Huu ni wakati wa kuwafundisha watoto wa
Mungu jinsi ya kujipanga na kupambana na changamoto mbalimbali wakati dunia
inakwenda na mabadiliko ya kasi kubwa. huu ni wakati wa viongozi wa kiroho
kuzisoma nyakati na kujipanga kukabiliana na changamoto zinazolikabili kanisa
kama mtu mmojammoja na kanisa kama kundi la watu wa mahali fulani katika zama hizi za utandawazi na information
Technolgy. Ni lazima tujue tunatumiaje maarifa yaliyoko duniani katika kuujenga
ufalme wa Mungu na sio kupingana nao.
Mchungaji
Rwakatare ni mmoja kati ya wachungaji wanaoitumia vizuri sana teknolojia ya
habari na mawasiliano. Ana kituo cha redio FM na pia hurusha vipindi katika
televisheni kila wiki
Wakati matumizi ya Internet yanaanza kuingia
kuna baadhi ya makanisa walifanya maombi maalumu ya kufunga na kuomba kuzuwia
mitandao ya yahoo na mingineyo isiingie katika nchi yetu kwa madai kwamba ni
alama ya mpinga Kristo lakini walishindwa na leo hii wao wenyewe ndio
wanaonufaika nayo kwa kuwasiliana na watumishi wenzao wan chi za mbali. Tukijua
kwamba kanisa ni mtu basi ni lazima tuhakikishe tunamuandaa mtu kwa umakini
mkubwa kulingana na mazingira yaliyopo, siku hizi kuwa mtu wa kiroho sio lazima
uwe mtu wa kuzubaazubaa na kuvaa makoti makubwa kama mtu wa kutoka mashambani.
Kuwa mtu wa kiroho siku hizi ni kuwa na maono na maono ni mipango ya namna
utakavyoutumia wakati na mazingira yaliyopo katika kujenga ufalme wa Mungu,
hapo haijalishi kwamba umeweka dawa nywele au una nywele zako za kipilipili.
Hapa tutaangalia una uwezo gani wa kuwapelekea ndugu zetu wa mataifa ya kiarabu
ambao bado hawajafikiwa na injili ukaongea nao
COPY
AND PASTE SYNDROME (KUNAKIRI NA KUCHOMEKA)
Mojawapo ya mambo ambayo athali zake
zinaonekana haraka sana katika utandawazi ni tabia ya kuiga haraka tabia na
utamaduni wa mataifa mengine ambapo pengine huku kwetu ni tatizo.
Lakini pamoja na hayo yote hakuna sehemu hata
moja ambayo inaweza kukwepa mabadiliko haya iwe kwa kutaka ama kwa kutokutaka.
Kwa hali hiyo hata kanisa haliwezi kukwepa kuingia katika mabadiliko haya.woga
wa aina yoyote utakuwa ni woga ambao hauna sababu,
Hii ni kwa sababu kanisa linavuna waumini
wake kutoka katika jamii ya watu waliopo katika sehemu lilipo kanisa kwa hiyo
ni lazima watu walio katika jamii hiyo wataingia kanisani wakiwa katika hali
waliyonayo kabla mabadiliko ya kiroho yatakayoletwa kwa msaada wa roho
mtakatifu na sio kwa nguvu ya kianadamu na roho mtakatifu atawafinyanga watu
katika namna ambayo anaitaka mwenyewe kwa manufaa ya Mungu.
Ni jambo la kusikitisha sana kuona baadhi ya
makanisa yanawazuwia watu wanaokuja makanisani kwao wakiwa katika hali Fulani
ambayo inaoneana wameathiriwa na mambo ya utandawazi na tabia zake.
Kuongezeka
kwa kasi ya uvukaji wa mipaka
.
Katika eneo hili ni lazima litakuwa na faida
lakini pia litakuwa na athari kwa kanisa na hasa makanisa ya mijini itakuwa ni
vigumu sana kwa wachungaji kuwasimamia watu wanaowachunga kwa sababu hakutakuwa
na utulivu wa watu makanisani kwani watu wengi watakuwa wanaingia na kutoka,na
kila wanapotoka na kuingia watakuwa na mitazamo tofauti kulingana na mila na
desturi za sehemu wanakotoka na sehemu wanazotembelea,kwa sababu ya changamoto
hii ni lazima kanisa litegemee kukabiliana na migogoro mingi itakayohusiana na
tabia mbaya za kuambukiza kutoka sehemu nyingine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni