Mungu alitaka kuwe na mahali maalumu ambapo Mungu atakutana
na watu wake Israel. Mungu akamuagiza Musa atengeneze maskani ambayo itatumika
maalumu kwa shughuli za kumwabudu. Hii maskani ilikuwa ni ya hema. Ilikuwa ni
ya hema kwa sababu Waisraeli walikuwa safarini kutoka Misri kwenda Kanaani,
hivyo nyumba zao zilikuwa za mahema ambayo walipiga na waliposafiri waliyabeba.
Hii ndiyo maana hata hiyo maskani ambayo waliitengeneza ilikuwa ya hema. Hiyo hema
inajulikana kwa jina maarufu la HEMA YA JANGWANI. Hema ya jangwani ni somo lefu
na pan asana. Hatutajifunza somo lote katika Blog hii bali tutajifunza mambo
machache sana ambayo yatatusaidia kuelewa kuomba katika Roho Mtakatifu na
kupata mpenyo.
Hema ya janngwani ilikuwa ni kama ifuatavyo
Hema hii ilikuwa na sehemu tatu. Patakatifu pa patakatifu
ndiko kulikuwa kunakaa sanduku la Bwana. Juu ya sanduku kulikuwepo kiti cha
rehema. Upande huu wa kiti na upande wa pili kila upande kulikuwepo makerubi
mmoja waliotazamana. Sehemu ya pili yaani
Patakatifu kulikuwepo madhabahu ya kufukizia uvumba ambao
ulitakiwa uwake daima, kulikuwa na taa ya vinara saba ambayo ilitakiwa iwake daima na kulikuwa na
meza ya mikate ya wonyesho,mikate ambayo ilitakiwa ibadirishwe kila siku siku
kuwekwa mikate mipya. Ua wan je kulikuwa na madhabahu ya kuteketezea sadaka .
Patakatifu pa patakatifu aliruhusiwa kuingia kuhani mkuu peke yake,mtu mwingine
angeingia angekufa papohapo.
Patakatifu waliingia makuhani wote kwa ajili ya huduma
mbalimbali za mahali hapo. Makuhani wadogo hawakuruhusiwa kuingia patakatifu pa
patakatifu. Waisraeli wengine wote waliruhusiwa kuingia ua wanje pekee.
Makuhani wadogo walikuwa wanafanya shughuli mbalimbali zinazohusiana na ibada,
patakatifu na ua wan je.
Mungu alikuwa anakutana na kuhani mkuu,patakatifu pa
patakatifu. Kuhani mkuu alikuwa anaingia patakatifu pa patakatifu akiwa amebeba
damu ya mwana kondoo kwenye bakuli, ili kuzifunika dhambi zake na za Waisraeli
wote. Angeingia bila hiyo damu angekufa. Kuhani aliingia na kukaa kwenye kiti
cha rehema. Mungu alizungumza naye pale. Baada ya kuhani mkuu kukaa kwenye kiti
cha rehema Mungu alikuwa anashuka hapo kwa udhihirisho wa uwepo wa Mungu
uliokuwa ni utukufu wa Mungu wa wingu lililowaongoza wana wa Israeli,usiku
nguzo a moto mchana nguzo ya wingu,wingu hilo maarufu kwa jina la Shakina
Glory.
Mungu alikuwa hawezi kuzungumza na kuhani mkuu mahali popote
pale bali alizungumza na kuhani mkuu patakatifu pa patakatifu tu. Hakuzungumza
na kuhani kwenye ua wan je,patakatifu au nyumbani kwa kuhani na mahali popote
pale pengine. Na baada ya kuhani mkuu
kuondoka patakatifu pa patakatifu ule uwepo wa Mungu nao uliondoka.
Waisraeli baada ya kufika Kanaani waliendelea na kumwabudu
Mungu hapohapo kwenye hema kwa muda wa miaka sana,hadi wakati wa mfalme
Sulemani alipojenga hekalu kwa mfano uleule wa hema. Hivyo sanduku la Bwana na
vitu vyote vya ibada vilihamishiwa kwenye hekalu. Huduma zote zilizokuwa
zikifanywa na makuhani zilihama kutoka katika hema na kuhamia hekaluni humo.
Hapo ndipo kukawa mwanzo wa hekalu.(soma 1Wafalme 8:14-21)
Kuanzia hapo ndipo kukaanza kutumika jina la hekalu badala ya
Maskani au hema ya jangwani. Wakati wa huduma hii ya makuhani na
hekalu,waisraeli wote katika nchi nzima walitakiwa kwenda kupata huduma za
maombezi kwenye hekalu hilo. Ambalo lilijengwa Jerusalemu. Hivyo Israeli
hawakuruhusiwa kuedesha shughuli za kuabudu mahali popote isipokuwa hekaluni
Jerusalemu. Hivyo watu wote waliokuwa na mahitaji yanayohusu ibada,maombezi na
huduma zingine zozote za Mungu, iliwabidi waende Jerusalemu,hekaluni waonane na
makuhani. Makuhani ndiyo waliokuwa wanazungumza na Mungu kwa niaba ya Waisraeli
wote. Huduma hii ya makuhani na hekalu iliyofanyika agano la kale iliishia pale
msalabani wakati Yesu alipokufa msalabani. (Luka 23:44-47)
Kama tulivyoona Waisraeli hawakuruhusiwa kuingia patakatifu
wao waliishia ua wan je, kama angeingia ambaye si kuhani angekufa
hapohapo. Katika mlango kulikuwa na pazia la unene wa inchi
nne,ambalo halingeruhusu mtu ambaye siye kuhani achungulie ndani hata kama ni
kwa bahati mbaya. Baada ya Yesu kufa msalabani Biblia inasema paia la hekalu
lilipasuka katikati kiasi cha kwamba mtu yeyote hata ambaye si kuhani aliweza
kuona ndani au kuingia hadi patakatifu pa patakatifu na kukaa bila madhara
yeyote. Hata kuhani mkuu aliingia patakatifu pa patakatifu na kukaa kwenye kiti
cha rehema wala shakina Glory haikushuka. Tangu siku hiyo Mungu hakushuka tena
kwenye hekalu.
Tangu siku hiyo Yesu alifanyika kuhani mkuu,yuko mbinguni ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba
anatuombea badala ya kuhani mkuu wa agano la kale. Pamoja na hivyo Mungu
alikataa kuendelea kukaa kwenye hekalu la jengo.(angalia Isaya 66:1)
Hekalu la sasa hivi ni watu wa Mungu. Mungu anakaa ndani ya
watu wake. Baada ya mtu kumpokea Yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yeke,Mungu
huja kukaa ndani yake.(Yohana 14:23) kwa hiyo wewe mtu wa Mungu ni makao ya
Mungu,wewe ni hekalu (1Wakorintho 3: 16-17) Agano jipya ni kivuli cha agano la
kale. Agano jipya ni kivuli cha agano la kale. Agano la kale lilikuwa
linaiandaa njia halisi ya kumwabudu Mungu. Hekalu la zamani linafanana na
hekalu la sasa.
HEMA YA JANGWANI
MTU WA MUNGU
(hekalu la zamani (hekalu
la sasa)
Ua wan je.
Mwili.
Patakatifu
Nafsi
Patakatifu pa patakatifu
Roho
Hekalu la sasa lina sehemu tatu,Mwili,Nafsi na roho. Mwili ni
ua wa nje,Nafsi ni patakatifu na roho ni patakatifu pa patakatifu. Agano la
kale kuhani alikuwa mtu na hekalu lilikuwa jengo. Hekalu la sasa ni wewe mtu wa
Mungu na kuhani ni wewe mwenyewe pia huyohuyo. Hivyo wewe ni vitu viwili katika
kimoja. Kuhani wa agano la kale akitaka kuongea na Mungu alikuwa anaianza
safari hiyo kutokea nyumbani kwake ,baadae anafika ua wan je, Patakatifu na
baadae aliingia patakatifu pa patakatifu. Mtu wa Mungu, wewe mwenyewe ni kuhani
na unatakiwa uingie hekaluni mwako kwa imani. Kuhani wa agano la kale alikutana
na Mungu patakatifu pa patakatifu tu.hangeweza kukutana na Mungu patakatifu,Ua
wan je,nyumbani kwake au mahali pengine popote pale. Wewe mtu wa Mungu ni
kuhani pia ni hekalu la leo,patakatifu pa patakatifu pako ni rohoni. Huwezi
kukutana na Mungu kwenye nafsi, mwilini au mahali pengine popote pale.(Zaburi
63:1-2) huyu ni Daudi mfalme anajieleza jinsi ambavyo yeye alivyokuwa
anamtafuta Mungu mapema akiamka asubuhi sana.kumtafuta Mungu ni kumuomba Mungu.
Daudi alikuwa anaamka alfajiri na mapema kabla ya shughuli nyingine yeyote,kwanza
alikuwa anamwomba Mungu. Daudi katika maombi yake anasema kuwa,alikuwa na
malengo ya kumtafuta Mungu hadi azione nguvu za Mungu na utukufu wa Mungu.
Wakati wa agano la kale mambo ya kuabudu yalikuwa hayafanyiki kwa imani kama
hivi sasa. Zamani waliabudu kwa vitendo na kwa kuona. Waisraeli walizowea kuona
utukufu wa shekina ukishuka wakati kuhani mkuu alipokuwa ameingia patakatifu pa
patakatifu. Hivyo kuhani mkuu hangeweza kuwaambia waisraeli kwamba leo ameongea
na Mungu wakati shekina haikuonekana. Kutokana na hili tunaona Daudi katika
kuomba kwake ili ahakikishe kuwa ameongea na Mungu,alihakikisha ameuona ameuona
uwepo wa Mungu, huo ulikuwa uwepo wa shekina.
Wakristo waleo wanaomba bila malengo kama hayo ya Daudi
wanaomba bila kuhakikisha kuwa Shekina imejidhihirisha,Mungu hujidhihirisha. Ni
sawa na kuhani mkuu alipokuwa anaongea na Mungu, alipokaa kwenye kiti cha
rehema Mungu ili kuonyesha kuwa yuko pale alikuwa anajidhihirisha kwa wingu
(Shakina Glory) Daudi naye alikuwa anaomba hadi akutane na Mungu. Mungu
alikutana na Daudi alikuwa akijidhihirisha kwa nguvu nguvu na utukufu wake
hivyo Daudi alipokuwa akimtafuta Mungu,alikuwa akijidhihirisha kwa nguvu na
utukufu wake. Wakristo wa leo wanaomba bila malengo hayo. Wao wanaomba kwa
kubahatisha bila kujua kuwa je Mungu amekutana nao? Wanafikiri kila kuomba
kutawakutanisha na Mungu. Hii imesababisha wakristo hawapati majibu japokuwa
wanaomba. Kuhani mkuu alipokaa kwenye kiti cha rehema patakatifu pa patakatifu
utukufu wa Mungu ulijidhihirisha kuonyesha kuwa Mungu yupo. Bila ya utukufu
kuonekana hiyo ilikuwa na maana kuwa kuhani Mkuu hajakutana na Mungu.
Safari ya kuhani mkuu kwenda kwenye maombi kutoka nymbani
kwake ilikuwa ni ya miguu. Mkristo wa
leo wewe ukiwa ni kuhani safari yako ya kuingia hekaluni ni ya imani wewe ni
kuhani wewe ni hekalu,unaingia hekaluni kwa njia ya maombi. Unapoanza kuomba
hiyo ndio safari ya kuingia hekaluni. Kuhani akitokea nyumbani kwake alikuwa
anapitia sehemu kuu tatu.
1.
Sehemu
ya kwanza ni kutoka nyumba kwake hadi ua wa nje sehemu pili ni patakatifu. Na
sehemu ya tatu ni patakatifu pa patakatifu. Katika sehemu ile ya kwanza yaani
kutoka nyumbani kwake hadi ua wan je,kuhani alitoka nyumbani kwake alikuwa
anakutana na watu na mambo mbalimbali yaliyokuwa yanamzunguka kama vile, watoto
wakicheza michezo mbalimbali watu wakifanya biashara n.k. hadi kuhani
alipoingia katika ua wan je bado alikuwa anakutana na watu mbalimbali ambao
wamekwenda hekaluni kupata huduma mbalimbali za kimungu kutoka kwa makuhani
hekaluni. Kuhani alipoingia patakatifu hakuendelea kuona hayo mambo tena. Ukiwa
patakatifu huwezi kuona mambo yaliyo nje ya patakatifu,bali utaona shughuli za
kimungu ambazo makuhani wadogo huzifanya mahali patakatifu. Pia huwezi kuona
mtu yeyote patakatifu isipokuwa makuhani peke yake. mtu wa Mungu unapoanza
kuomba,katika hatua yako ya kwanza kabisa ya kuomba,huwa ni sehemu ngumu sana
kwa kuomba. Mwambaji hujisikia au huhisi kama anapanda mlima mrefu. Kuongea
maongezi ambayo si kuomba unaweza hata saa kumi bila ugumu wowote. Maongezi ya
kawaida huwa hayana upinzani wa shetani,maombi huwa yana upinzani kutoka kwa
shetani ndio maana huwa kunakuwa na ugumu mfano wa kujisikia kama unapanda
mlima. Sehemu hiyo ya kwanza kabisa katika maombi ni sawa na sehemu ya kwanza
ya kuhani wa agano la kale alipotoka nyumbani kwake hadi kwenye ua wan je wa
hema. Kuhani alikuwa anakutana na mambo mbalimbali yaliyokuwa yanamzunguka.
Mkristo unapoanza maombi japokuwa utakuwa umefumba macho,pamoja na kuwa
umefumba macho,kuna vitu ambavyo huwa vinaendelea kuonekana katika fahamu zako.
Vitu hivyo huwa ni vitu ambavyo viko karibu sana katika maisha ya muhusika vitu
vinavyotuzunguka,kama vile watoto,mume,mke,mali,elimu,kazi.n.k kuhani aliviona
vitu vinavyomzunguka wakati akienda hekaluni kwenye sehemu ya kwanza. Yaani
kutoka nyumbani hadi ua wan je,aiona watu mbalimbali aliokuwa akikutana nao
njiani,pengine aliona watu wakicheza, n.k. hivi ni vitu ilikuwa ni lazima
avione maana vilikuwa njiani,vilikuwa vimemzunguka. Ni hivyohivyo hata wewe unapoingia kwenye maombi. Sehemu ya kwanza ya
hekalu lako ni mwili hivyo ni lazima uvione vitu vya kimwili vinavyokuzunguka. Pamoja na
kuviona vitu mbalimbali pia unaweza kuona dhambi fulanifulani. Dhambi
unazoziona mara nyingi huwa ni dhambi ambazo zinakuotea kukushambulia. Pengine
unaweza kuiona dhambi ambayo uliitenda zamani na ulishaitubu na
ilishasamehewa,lakini shetani anaweza kuileta ili akuchanganye. Wakristo wengi
wanapoona hivyo hukatisha maombi yao na kuanza kukemea ili vitu kama hivyo
visiendelee kuonekana. Lakini nakwambia hivi hata ukemee hiyo hali isiendelee
kuonekana hiyo hali haiwezi kuondoka kwa kukemewa,bali itaendelea kuonekana
maana ni vitu ambavyo vimekuzunguka ni lazima uvione kwa sababu uko mwilini.
2.
Sehemu
ya kwanza ya wewe kuingia ni mwilini. Hivyo kipindi chote utakachokuwa mwilini
ni lazima uendelee kuviona vitu hivi,hivyo usipambane navyo kwa kuvikemea kwa
sababu ni lazima vionekane. Hivyo usipambane navyo kwa kuvikemea kwa sababu ni
lazima vionekane. Hivyo wewe utakapoona vitu hivyo vinakuja kwenye fahamu zako
wakati ukianza maombi wewe endelea na maombi yako vitu hivyo vinavyoonekana
kwenye fahamu zako wakati wa mwanzo mwanzo wa maombi ndivyo husababisha ugumu
na uzito katika maombi. Vitu hivi huitwa miungu. Kitu chochote ambacho
ukikiweka kiwe cha kwanza,Mungu
ukamuweka awe wa pili basi kitu hicho kinakuwa miungu. Vitu hivi vinaweza kuwa
ni baadhi ya Baraka mbalimbali ambazo ametupa Mungu,sasa wewe unapoviweka vya
kwanza halafu Mungu anakuwa wa pili,basi kitu hicho kinakuwa miungu kwako. Vitu
viile mume,mke,wazazi,watoto,rafiki,kazi,elimu,mali,dini tabia
mbaya,ubinafsi,n.k. vitu hivi shetani huvitumia kuvuruga uhusiano wetuna Mungu
kwa kuvifanya vichukue nafasi ya kwanza na Mungu awe nafasi ya pili. Hivyo
unapokuwa unaomba vinapoonekana mbele yako kwenye fahamu zako japokuwa umefumba
macho hiyo ina maana kwamba vinakuzuwia usiongee na Mungu,vinakuzuwia usimfikie
Mungu katika maombi yako.
3.
Mungu
huanza kuwashughulikia hao miungu kwa kuwatoa wasikae mbele katika fahamu zako
hivyo unapokuwa unaona kitu fulani mbele yako wakati ukianza kuomba,basi ujue
kuwa Mungu anakuonyesha miungu anaoushughulikia kwa wakati huo. Wewe unatakiwa
uendelee kuomba tu. Usijishughulishe kwa lolote kuhusu miungu hiyo,wala
usisimamishe maombi na kuanza kuikemea.kushughulikiwa kwa hiyo miungu tunaweza
kusema kuwa ni kuiangusha chini ili itoke kwenye nafasi ya kwanza na kumpisha
Mungu achukue nafasi ya kwanza. Fahamu kwamba miungu hiyo ndiyo inayokuzuwia
kumuona Mungu,inakuzuwia kuwasiliana na Mungu,hadi miungu hiyo itoke ndipo utaweza
kumfikia Mungu katika maombi,kushghulikiwa kwa miungu ni kuuawa kwa hiyo
miungu. Mungu anaiua hiyo miungu,bila miungu kufa huwezi kupata mpenyo katika
maombi yako.huwezi kumfikia Mungu wala huwezi kuwasiliana na Mungu.miungu ni
kikwazo katika mawasiliano na,kama ingekuwa zamani tungeweza kusema kwamba
miungu ndio kutu katika nyaya za simu ya mbinguni kuna miungu ya aina nyingi
mingine unaweza usiione katika maombi,lakini inaonekana katika macho ya mwili
ikijidhihirisha katika matendo ya wakristo. Baadhi ya miungu hiyo ni tabia
zisizo za kiutu,mila mbovu,mapokeo ya kipagani,ukabila,hasila,wivu,chuki n.k.
wakristo waliookoka wamengagania vitu hivi kama hawatamruhusu Mungu akaiua hii
miungu,hawatakwenda mbinguni. Kuwa na miungu hii ni kuiabudu na yeyote anayeabudu
miungu hawezi kumona Mungu. Wakristo wengi wameweka kazi,biashara,elimu,watoto,mke,mume,n.k.
view vya kwanza Mungu wamemuweka awe wa pili.huo ni kuvifanya vitu hivyo viwe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni