Jumamosi, 18 Agosti 2012

LALA KWA AMANI MZEE ELIAS LUDAMILA

Mwili wa marehemu Elias Ludamila ukifika nyumbani kwake kwa ajili ya kuuaga kabla ya kwenda nyumbani kwao Shinyanga


waimbaji wa kanisa la KLPT Majani Mapana wakiwa wanaimba nyimbo za maombolezo kupitia katika vitabu vya tenzi za rohoni.

Mafundi mitambo Ben Mngumi na Steven Malima wakiwa kazini kuhakikisha kwaya zinaimba na matangazo yanakwenda kama ilivyopangwa.


Baadhi ya umati wa waombolezaji wakiwa nje ya viwanja nyumbani kwa mzee Ludamila tayari kwa kuuaga mwili wa marehemu mzee wetu.

Baadhi ya ndugu wa karibu wa marehemu wakiongozwa na mke wake wakiwa ndani ya nyumba ya marehemu baada ya mwili kuwasili kabla ya kutolewa nje na kuagwa na watu wote.


Mchungaji Christina Nywage akitoa neno la Mungu kwa waliohudhuria katika mazishi.
Mtoto mkubwa wa Marehemu akitoa historia ya marehemu iliyoandaliwa na familia ya marehemu.

Wachungaji Christina na George Nywage wakiwa na mchungaji Mchungaji Bombo wa Elim Pentekoste.


Mzee Makupa akisoma historia fupi ya utumishi wa Mzee Ludamila mbele ya watu waliohudhuria siku ya kuuaga mwili wa marehemu nyumbani kwake Nguvumali Majani mapana.

Jeneza lenye mwili wa kamanda wa polisi  mstaafu Tanga mzee Elias Lugenzi Ludamila ukiwa nyumbani kwake eneo la Majani mapana kwa shughuli za kuuaga kabla ya kusafirishwa kwenda kupumzika katika nyumba ya milele huko kwao Shinyanga.
Mke wa marehemu mama Lucy Ludamila akiwa katika uso wa majonzi muda mfupi kabla ya kuuaga mwili wa marehemu mzee wetu Elias Ludamila. kwa kawaida siku kama hii huwa ni ngumu kwa mtu yeyote kustahimili lakini Mungu ni mwema anayetuwezesha kustahimili. aliyekaa katika
 ni mchungaji Sara Makupa.



Mchungaji George Nywage akitoa maelekezo kwa watu waliohudhuria siku ya kuuaga mwili wa marehemu Ludamila.



























watoto wa marehemu Ludamila wakiwa mbele ya jeneza la baba yao wakati wa kuuaga mwili wa marehemu.

















Hakuna maoni:

Chapisha Maoni