Jumamosi, 18 Agosti 2012

ZIARA YA MAPANGONI: FURAHA MWAKASEGE




       Gari lililowabeba vijana wa KLPT likiingia katika eneo la mapango ya Amboni.





vijana wakishuka katika eneo la kuegesha magari katika mapango ya Amboni






 vijana wakiangalia mapango kwa nje kabla ya kuingia ndani ya mapango haya na hapa wanawasubiri waongozaji ambao wamepeleka kundi mojawapo ndani ya mapango hayo.

hapo ni nje ya ofisi ambapo tunasubiri utaratibu wa kuingia ndani kwa kupewa historia na maelekezo.


Aston Mwakasege na yeye pia hakupendwa kupitwa na tukio hili la kihistoria kwake.

vijana wadogo wakipewa maelekezo ya kuingia na viongozi wa mapango hayo.       


Baada ya maelekezo safari ikaanza kuingia kwenda sehemu ya kwanza,


Lovenes Shangali yeye hakuingia kwenye mapango kabisa,nilimuuliza ni kwa nini hataki kushiriki zoezi hili muhimu akaniambia anaogopa kwamba atakwama kwenye mapango, nikamwambia hiyo haijawahi kutokea lakini tulipenda kufuata anavyojisikia. hakuna sheria ya kumlazimisha kijana.


baada ya kuingia ndani ya mapango kuna ukumbi mzuri ambao pia hutumiwa kwa ajili ya maswali na majibu kabla ya kuingia ndani.




Wale vijana wadogo sana waliowasindikiza vijana Junior wao tuliwaacha nje wakiwasubiri dada

vijana wanazamia ndani ya pango
Wageni mbalimbali wakipewa maelezo na wafanyakazi wa mapango kabla hawajaamua kuingia ndani ya mapango hayo.


Kwa kawaida sehemu unayoingia katika mapango ya Amboni sio ndio njia utakayotokea na hii ndio njia wanayotokea na ukiwa kwa ndani pangoni ni kama unapanda kuingia katika lango la ndege na ndipo unajikuta upo nje. kwa kweli inavutia sana.

nje ya mapango ya Amboni kuna duka la kuuza vitu vya asili ni maalumu kwa ajili ya wageni wanaotoka nje ya nchi lakini si haba hata vijana wetu waliweza kununua vitu hivi vya gharama sana



 




vijana kutoka kanisa la kiluvya ambao waliambatana na vijana wa KLPT wakipata picha ya ukumbusho katika lango la kuingia katika mapango ya amboni.




viongozi wa kanisa la vijana Cecilia Sakara na Grace Jackob wakiwa pamoja na washirika katika ufukwe wa Raskazone.





       wakati mwingine vijana hupenda kuogelea katika fukwe za bahari ya hindi, walimu wao huwatenganisha kwa jinsia tofauti na wanaoga chini ya uangalizi mkubwa wa walimu wao.

      

      

        Vijana wa kanisa la K.L.P.T. wanapenda sana wakipata nafasi kwenda baharini kutazama mandhari nzuri ya bahari ya hindi na kula vyakula vitamu walivyoandaliwa na wachungaji wao.

    

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni