MAANA YA WOKOVU
“Kwasababu
ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako yakuwa
Mungu alimfufua katika wafu, UTAOKOKA. Kwa maana kwa moyo mtu
huamini hata kupata haki, na kwa kinywa mtu hukiri hata KUPATA WOKOVU”. (Rum
10:9-10.)
Baada ya
kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako, ni muhimu sana kupata mafundisho ya
awali, yatakayokusaidia kujua kwa hakika, maana ya KUOKOKA au WOKOVU;“ili tusiwe
tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa
elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.” (Efe
4:14)
Ndio maana
Yesu alisema, tukishawahubiri na kuwasaidia kuokoka, tuwafundishe
yote!“Yesu akaja kwao akasema nao, akawaambia, nimepewa mamlaka yote
mbinguni na duniani. Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa
wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
na mkiwafundisha kuyashika yale yote niliyowaamuru ninyi; na
tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote hadi ukamilifu wa dahari”. (Math
28:18-20).
“Basi kama mlivyompokea
Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye; wenye shina na wenye
kujengwa katika yeye; mmefanywa imara katika imani, kama
mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani”. (Kol 2:6-7)
“Wakawa
wakidumu katika fundisho la Mitume, na katika ushirika, na katika kuumega
mkate, na katika kusali” (Mdo 2:42)
“Muwe tayari
siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu,
lakini kwa upole na kwa hofu” (1Pet 3:15)
Watu wengi wamechanganya sana maana halisi ya neno “kuokoka”. Unaweza
kupewa tafsiri nyingi na watu, juu ya neno “kuokoka”. Wengine hudhani kuokoka
ni dini au dhehebu Fulani la “walokole”. Wengi hudhani wokovu ni maisha Fulani
ya kujinyima raha na kujitenga na jamii. Wengi hudhani wokovu ni maisha duni
nay a umasikini au kutokuwa na mali za kifahari. Ndani ya fikra za watu, kuna
tafsiri nyingi tofauti juu ya “kuokoka” na hizo tafsiri nyingi si sahihi. Lakini
hii hapa chini nadhani ndio tafsiri rahisi zaidi kueleweka.
NINI MAANA YA KUOKOKA?
KUOKOKA ni lugha
ya kawaida kabisa, yenye maana ya;
Kunusurika,
kusalimika, kupona, kukombolewa, kufunguliwa au kutoka katika janga au hatari
fulani.
Mfano:-
- Kunusurika; Paulo
aliposafiri mashuani pamoja na watu wengine mia mbili na sabini na sita,
alisema;“safari hii itakuwa na madhara na hasara nyingi, si ya shehena na
merikebu tu, ila na ya maisha yetu pia … baada ya muda mchache, ukavuma upepo
wa nguvu wa namna ya tufani … na kwa maana tulikuwa tukipigwa sana na ile
tufani, siku ya pili yake, wakaanza kuitupa shehena baharini. Siku ya tatu
wakatupa vyombo vya merikebu kwa mikono yao wenyewe. Jua wala nyota
havikuonekana kwa siku nyingi, na tufani kuu ikatushika, basi tukakata tamaa
ya kuokoka … na baharia walipotaka kukimbia na kuiacha
merikebu … Paulo akawaambia akida na askari, hawa wasipokaa ndani ya merikebu,
hamtaweza kuokoka … Shauri la askari lilikuwa kuwauwa
wafungwa, mtu asiogelee na kukimbia. Bali akida akitaka kumponya Paulo,
akawazuia wasifanye kama walivyokusudia, akawaamuru wale wawezao kuogelea,
wajitupe kwanza baharini, wafike nchi kavu … na hivyo watu wote wakapata
kuifikilia nchi kavu salama. Tulipokwisha kuokoka, ndipo
tulipojua ya kuwa kisiwa kile chaitwa Melita”. (Mdo 27: 1-44. 28:1)
H Hivyo tunaona
“KUOKOKA” katika mistari hii, imetumika kama “KUNUSURIKA”.
- Kupona; Wayahudi
walimdhihaki Yesu , “Jiponye nafsi yako, ushuke
msalabani.
( Mk 15:30)
Sisi je,
tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu
namna hii? Ambao kwanzaulinenwa na Bwana, kasha ukadhibitishwa kwetu na wale
waliosikia. (Ebr 2:3)
“KUOKOKA”
katika mistari hii imetumika kama “KUPONA”.
“Na niseme nini
tena? Maana wakati usingetosha kuleta habari za Gideoni, na Baraka, na Samsoni,
na Yefta, na Daudi, na Samweli, na za Manabii; Ambao kwa imani, walishinda
milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba,
walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga.
- KUOKOKA katika
mistari hii, imetumika kama KUPONA, KUSALIMIKA AU KUNUSURIKA!
- Kusalimika; Wakati Mungu
anaangamiza dunia kwa maji ya gharika, Biblia inasema;
“Wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi
Nuhu mjumbe wa haki na watu
wengine saba, hapo alipoleta gharika juu ya ulimwengu wa
wasio mcha Mungu. Tena
akaihikumu miji ya sodoma na Ghomora, akiipindua na
kuifanya majivu, akaifanya
akaifanya iwe ishara, kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu
baada ya hayo.
Akamwokoa Lutu, yule mwenye
haki, aliyehuzunishwa sana na mwenendo wa ufisadi
wa hao wahalifu. (2Pet 2:5-7)
“Hapa KUOKOKA” imetumika
kama “KUSALIMIKA” kutoka katika janga la gharika na moto.
- Kufunguliwa au
Kukombolewa; Herode alipomtia Petro gerezani ili amuuwe, Biblia
inasema;
“Panapo majira
yale yale, herode mfalme akanyoosha mikono yake kuwatenda mabaya baadhi ya watu
wa kanisa. Akamuuwa Yakobo ndugu yake Yohana kwa upanga. Na akiona yakuwa imewapendeza
Wayahudi, akaendelea, akamshika na Petro … akamweka gerezani, akamtia
mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde, akitaka baada ya
Pasaka, kumtoa na kumweka mbele ya watu. Basi Petro akalindwa gerezani, nalo
kanisa lilikuwa likimwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake. Hata wakati Herode
alipotaka kumtoa, usiku ule ule, Petro alikuwa analala katikati ya askari
wawili, alikuwa amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakailinda
gereza. Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle
chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi! Minyororo
yake ikamwanguka mikononi. Malaika akamwambia, jifunge, kavae viatu vyako.
Akafanya hivyo. Kisha akamwambia, jivike nguo yako, ukanifuate. Akatoka nje,
akamfuata; wala hakujua yakuwa ni kweli, yaliyofanywa na malaika. Bali alidhani
kwamba anaona maono. Na walipopita lindo la kwanza na la pili, wakaja hata
mlango wa chuma wa kuingilia mjini, ukawafungukia wenyewe. Wakatoka nje,
wakapita katika njia moja; mara malaika akamwacha. Hata Petro alipopata fahamu
akasema, “sasa nimejua yakini yakuwa, Bwana amempeleka malaika wake
na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote
kwa taifa la Wayahudi”. Na alipokuwa akifikiri hayo, akafika nyumbani kwa Mariamu,
mamaye Yohana Marko … na watu wengi walikuwa wamekutana humo wakiomba. Naye
alipobisha, kijakazi jina laki Rhoda akaja kusikiliza. Alipoitambua sauti ya
Petro, hakufungua mlango, kwa ajili ya furaha, bali alipiga mbio, akaingia
ndani, akawaambia kwamba, Petro anasimama mbele ya lango. (Mdo
12:1-14-19)
“KUOKOKA” katika
mistari hii, imetumika kama “KUFUNGULIWA” au “KUKOMBOLEWA” katika
kifungo.
UHAKIKA WA WOKOVU
Kwahiyo KUOKOKA ni KUNUSURIKA,
KUSALIMIKA, KUKOMBOLEWA, KUFUNGULIWA au KUPONA kutoka katika JANGA au HATARI
fulani.
Yesu alikuja
kuleta wokovu (kuokoa) na Biblia inataja mistari mingi sana juu ya koukoka au
wokovu.
Kwa mfano:-
- Yoh 3:16-18; Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanae wa pekee ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyehamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la mwanawe wa pekee.
- Luk 9:59; Kwa maana mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, balikuziokoa,
- Yoh 12:47; Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi si mhukumu, maana sikuja niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu.
- 1Tim 1:15; Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa ya kwamba, Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi.
- 1Tim 2:14; Mungu … hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yalio kweli.
- Efe 2:5,8; Hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo, yaani, mmeokolewa kwa Neema, Kwa maana mmeokolewakwa Neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
- 1Kor 1:18; Kwa sababu neno la Msalaba kwao wanaopotea ni upuuzi, bali kwetutunaookolewa ni nguvu ya Mungu.
- Mdo 4:10-12; Jueni nyote na watu wote wa Israel ya kuwa, kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulubisha, na Mungu akamfufua katika wafu … kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu. Yeye ndiye jiwe lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limekuwa jiwe kuu la pembeni. Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina lingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Mdo 2:22-24,
36-40, 43-44, 47; Enyi waume wa Israel, sikilizeni maneno haya:
Yesu wanazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na
ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe
mnavyojua; Mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa
kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulubisha kwa mikono ya watu wabaya,
mkamwua; ambaye Mungu alimfufua, akifunga uchungu wa mauti, kwa sababu
haikuwezekana ashikwe nao…
Basi nyumba
yote ya Israel nawajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo
mliyemsulubisha kuwa Bwana na Kristo. Walipoyasikia hayo wakachomwa mioyo
yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? Petro
akamwambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate
ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa kuwa
ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali,
na kwa watu wote watakao itwa na Bwana Mungu wetu wamjie. Akawashuhudia
kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, jiokoeni na
kizazi hiki chenye ukaidi …
Kila mtu
akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume. Na wote
walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika … Wakimsifu Mungu na
kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale
waliokuwawakiokolewa.
(Mdo
2:22-24, 36-40, 43-44, 47)
Rum 10:9-10;
Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, nakuamini mioyoni
mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa
maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, kwa kinywa hukiri hata
kupata wokovu.
Mdo 16:30-31;
Kisha akawaleta nje akasema. Bwana zangu, Yanipasa nifanye nini
nipate kuokoka? Wakamwambia, mwamini Bwana Yesu
nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.
2Kor 6:2; Kwa
maana asema, wakati uliokubalika nalikusukia, siku ya wokovunalikusaidia;
Tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; Tazama, siku ya wokovu ndio
sasa.
Ebr 2:1-3; Kwa
hiyo, imetupasa kuangalia zaidi hayo yaliyosikiwa, tusije tukayakosa, kwa
maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika, lilikuwa imara, na kila kosa na
uasi, ulipata ujira wa haki. Sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu
namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukadhibitika kwetu na wale
wanaosikia.
TUMEOKOLEWA KUTOKA KWENYE NINI?
1. TUMEOKOLEWA
KUTOKA KATIKA NGUVU YA DHAMBI / UASI
Maana sijui
nifanyalo; kwasababu lile nilipendalo silitemdi; Bali lile nilichukialo ndilo
nilitendalo … naikiri kuwa ile sheria ni njema. Basi sasa si mimi nafsi yangu
ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. Kwa maana najua kuwa,
ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema, kwa kuwa kutaka
nataka, bali kutenda lililo jema sipati … lakini katika viungo vyangu, naona
sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya
mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu. Ole wangu, masikini
mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? NAMSHUKURU MUNGU, KWA YESU
KRISTO BWANA WETU. (Rum 7:15-15)
“Nanyi mlikuwa
wafu kwasababu ya makosa na dhambi zenu. Ambazo mliziendea zamani kwa
kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuaata Mfalme wa uwezo wa
anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani,
sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tama za miili yetu, tulipo yatimiza
matendo ya mwili na nia, kukawa kwa tabia yetu watoto wahasira kama na hao
wengine. Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake
makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwasababu ya makosa yetu;
alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, mmeokolewa kwa neema akatufufua pamoja
naye akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo
Yesu.”(Efe 2:1-1-2-6)
“Sasa basi
hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu
sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na
sheria ya dhambi na mauti”. (Rum 8:1-2) … “tukijua neno hili, ya kuwa, utu wetu
wa kale ulisulubishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike. Tusitumikie
dhambi tena … Basi dhambi isitawale ndani ya miili yenu … kwa maana mlikuwa
watumwa wa dhambi. Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa
dhambi, lakini mli-itii kwa mioyo yenu, ile namna ya elimu (Injili ya wokovu),
ambayo mliwekwa chini yake. Na mlipokwisha kuwa huru mbali na dhambi, mkawa
watumwa wa haki … kwa maana mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na
haki. Ni faida gani mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayo yatahayarikia
sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti. Lakini sasa mkiisha kuwekwa
huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu,
ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima. … Roho itendayo dhambi, ndiyo
itakayokufa. (Ezek 28:20-23) … kwa maana mshahara wa dhambi nimauti
wa milele, bali karama (zawadi) ya Mungu ni uzima wa milele katika
Kristo Yesu Bwana wetu. (Rum 6:23)
Pia
soma; Tito 2:11-12; Tito3:3-4; 2Kor 4:3-4; Efe
4:18-19; 1Tim 1:13-15
TUMEOLOKEWA
KUTOKA KATIKA NGUVU ZA GIZA.
“Naye
alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa
mwana wa pendo lake”. (Kol 1:13)
“Na ninyi
mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili
wenu, mliwafanya hai pamoja naye, akisha kutusamehe makosa yote; akisha
kuifuata ile hati iliyoandikwa kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui
kwetu; akaiondoa isiwepo tena akaigongomea msalabani; akiisha kuzivua enzi za
mamlaka, na kuzifanya kwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba
huo”. (Kol 2:13-15)
Tazama,
nimwewapa amri ya kukanyaga nge na nyoka na nguvu zote za yule adui, wala
hakuna kitu kitakachowadhuru. (Luk 10:19)
Pia
soma; Math 27:45,50-54; Ebr 2:14-15; Luk 11:21-22; Yoh
19:28-30
3. TUMEOKOLEWA KUTOKA KATIKA LAANA YA TORATI.
“Fahamuni basi,
yakuwa wale walio na imani, hao ndio wana wa Ibrahim. Na andiko, kwa vile
lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki mataifa kwa imani,
lilimhubiri Ibrahim habari njema zamani, kusema, katika wewe mataifa
watabarikiwa.Basi hao walio na imani hubarikiwa pamoja na Ibrahim aliyekuwa
mwenye imani. Kwa maana wale wale wote walio wa matendo ya sheria,
wako chini ya laana maana imeandikwa amelaniwa kila mtu asiyedumu katika yote
yaliyoandikwa katika kitabu cha Torati, ayafanye. Ni dhahiri ya kwamba hakuna
mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu mwenye haki
ataishi kwa imani. Na torati haikuja kwa imani, bali ,ayatendaye hayo,
ataishi katika hayo. Kristo alitukomboa katika laana ya Torati, kwa kuwa
alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa , amelaaniwa kila mtu
aangikwae juu ya msalaba; ili kwamba baraka ya Ibrahim iwafikirie mataifa
katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya roho kwa njia ya imani”. (Gal 3:7-14,
23-29).
“Kwa maana
Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki. (Rum 10:4)
Kwa kule
kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu
kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka”. (Ebr 8:13)
Basi twaona
ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria
…
Basi, mtu
asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au
mwandamo wa mwezi, au Sabato; ( Rum 3:28; Kol 2:16)
Pia Mdo 15:1-10-29; Gal 2:16; Rum 8:3; Rum 7:12,14-16; Rum 8:1-4; Yer 31:31-34
4. TUMEOKOLEWA
KUTOKA KATIKA DUNIA (UOVU WA DUNIA).
“Neema na iwe
kwenu, naamani, zitokazo kwa Mungu Baba, na Bwana wetu Yesu Kristo; ambaye
alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, ili atuokoe na dunia hii mbovu,
iliyopo sasa. Gal 1:3-4
“Wala mimi simo
tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako.Baba mtakatifu,
kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi
tulivyo. Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako
ulilonipa, nikawatunza;wala hapana mmoja wapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa
upotevu, ili andiko litimie.Na sasa naja kwako; ili wawe na furaha yangu
imetimizwa ndani yao. Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umechukia; kwa
kuwa wao si waulimwengu, kama mimi nisivyo na ulimwengu. Mimi siombi
kwamba uwatoe katika ulimwengu; basi uwalinde na yule muovu. Wao sio wa
ulimwengu, kama mimi nisivyo waulimwengu. Uwatakase kwa ile kweli; neno
lako ndio kweli kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami hivyohivyo
naliwatuma hao ulimwenguni. Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili
na hao watakaswe katika kweli”. Yoh 17:11-19 (14-16)
Pia Yoh
8:21-24 (23); 1Kor 5:9-11; Rum 12:1-2
5. TUMEOKOLEWA
KUTOKA KATIKA JEHANUM YA MOTO.
“Kwahiyo dunia ile ya wakati ule
iligharikishwa na maji ikaangamia, lakini mbingu za sasa na nchi, zimewekwa
akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na
kuangamia kwao wanadamu wasio mcha Mungu. Lakini wapenzi, msilisahau neno hili
… Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyodhani kukawia, bali
huvumilia kwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikie toba.
Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwizi; katika siku hiyo, mbingu zitatoweka
kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na
kazi zilizomo ndani yake zitateketea.. Basi kwakuwa vitu hivi vyota
vitafumuliwa, hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani? Katika mwenendo
mtakatifu na utauwa! Mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza;
ambayo katika hiyo, mbingu zitafumuliwa na zikiungua, na viumbe vya asili
vitateketea na kuyeyuka. Lakini kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya
na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake”. 2 Pet 3:6-13
“Kisha nikaona
kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, nayeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu
zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu, wakubwa kwa
wadogo wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa;
na kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni cha uzima; na hao wafu
wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa
na matendo yao. Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake;
Na mauti na
kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa
kadri ya matendo yake mauti za kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndio
mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. Naiwapo mtu yeyote hakuonekana
ameandikwa katika kitabu cha uzima alitupwa katika lile ziwa la moto.” Ufu
20:11-15 “Amini, amini nawaambia, yeye asikiaye neno langu na kumwamini yeye
aliyenipeleka yuna na uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali
amepita kutoka mauti kuingia uzimani”.(Yoh 5:24) Pia Lu 10:20; Fil 4:3;
1Yoh 3:14; Rum 5:6-9;
6. TUMEOKOLEWA
KUTOKA KATIKA MAGONJWA.
Nanyi
mtamtumikia Bwana Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako na maji yako.
Nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. (Kut 23:25) … Na Bwana atakuondolea
ugonjwa wote, wala hatatia juu yako maradhi yeyote, mabaya uyajuayo …”
(Kumb 7:15)
Hata kulipokuwa
jioni, wakamletea wengi wenye pepo, akawatoa pepo kwa jina lake, akawaponya
wote waliokuwa hawawezi (wagonjwa). Ili litimie lile neno lililonenwa na Nabii
Isaya akisema; “Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu na kuyachukuwa magonjwa yetu.”
(Math 8:16-17) “Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji,
akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya
magonjwa yote, na udhaifu wa kila aina”. (Math 9:35) “ … Akawaita
wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu; wawatoe na
kupoza, magonjwa yote na udhaifu wa kila aina (Math 10:1)
Yeye mwenyewe
alizichukuwa dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya
dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; Na kwa kupigwa kwake mliponywa (1Pet
2:24) “Hakika ameyachukuwa masikitiko yetu, amejitwika huzuni zetu …. Bali
alijeruliwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu. Adhabu ya amani yetu
ilikuwa juu yake; Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. (Isa 53:4 -5)
Damu ya Msalaba iliyoondoa dhambi, ndiyo iliyoondoa magonywa pia. Yatupasa
kuyaona magonjwa kama tunavyoiona dhambi. Hatupaswi kuyaona kuwa ni sehemu ya
maisha yetu. Magonjwa ni matokeo ya anguko la mwanadamu katika dhambi. Tukiisha
okolewa toka dhambini, yatupasa kuokolewa kutoka katika magonjwa pia. Afya
njema ni matunda ya msalaba kama ilivyo wokovu.
Tunatakiwa
kuchukia magonjwa kama tunavyochukia dhambi, kwasababu yote haya, ni
kazi za shetani. Yatupasa kuzikataa na kuzivunja katika maisha yetu. Kifo
cha Yesu, kitakuwa hakina maana kamili, kama tutaokolewa katika dhambi, halafu
tubaki katika magonjwa pia, wakati Yesu aliyefia dhambi, ndiye aliyefia
magonjwa pia. Msalaba ulifanya vyote, uliondoa dhambi na magonjwa pia.
“Mwenyewe aliutwa udhaifu wetu na kuyachukuwa magonjwa yetu.” (Math 8:16-17)
7. TUMEOKOLEWA
KUTOKA KATIKA UMASKINI
Angalia,
utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake. Na
fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka. Na kila kitu ulichonacho
kitakapoongezeka; Basi hapo moyo wako usiinuke ukamsahau Bwana Mungu wako,
aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa … hapo usiseme moyoni
mwako, nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu, ndio ulionipatia utajiri huo; Bali
utamkumbuka Bwana Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri,
ili alifanye imara agano lake … (Kumb 8:12-18) Lakini hawatakuwepo
masikini kwenu, kwakuwa Bwana atakubariki kweli, katika nchi akupayo Bwana
Mungu wako, uimiliki, iwe urithi wako. (Kumb 15:4)
Naye Abrahamu
alikuwa tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha na kwa dhahabu (Mwa 13:2)
Maana mmejua
Neema ya Bwana wetu, Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa masikini kwa ajili yenu,
ingawa alikuwa tajri. Ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa
umaskini wake. (2Kor 8:9) … mkitajirishwa katika vitu vyote, mpate
kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu. (2Kor 9:11)
… Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri
wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. (Fil 4:19) … Maana yeye yule ni
Bwana wa yote, mwenye utajiri kwa wote wamuitao; kwa kuwa, kila
atakayeliitia jina la Bwana ataokoka. (Rum 10:12)
Leteni zaka
kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia
hiyo, asema Bwana wa majeshi, mjue kama sitawafungulia madirisha ya
mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha,
au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya
ardhi yenu; wala mzabibu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake
katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni
heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi. (Malaki
3:10 – 12)
Thawabu ya
unyenyekevu, ambao ni kumcha Bwana, ni utajiri na heshima, nayo ni
uzima.
(Mith 22:4)
Itakuwa
utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo
yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu
ya mataifa yote ya dunia; na baraka hizo zote zitakujilia na kukupata
usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na
mashambani, utabarikiwa na uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao
wa wanyama wako wa mifugo. Maongeo ya Ngombe wako, na wadogo wa kondoo
zako: utabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. Utabarikiwa
uingiapo, utabarikiwa na utokapo Bwana atawafanya adui zako wainukao juu
yako kupigwa mbele yako watakutokea kwa njia moja; lakini watakimbia mbele kwa
njia saba. Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote
utakayotia mkono wako; naye atakubariki katika nchi akupayo Bwana wako
Mungu wako.
Bwana atakuweka
uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia; utakapoishika maagizo ya Bwana
Mungu wako na kutembea katika njia zako na mataifa yote ya dunia
watakuona umeitwa kwa jina la Bwana, nao watakuwa na hofu kwako. Bwana
atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa
wanyama wako, na uzao wa nchi yako, kama Bwana alivyowaapia baba zako kwamba
atakupa.
Atakufunulia
Bwana hazina yake nzuri, nayo ni Mbingu , kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa
wakati wake, na kwa kubariki kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa
mengi wala hutokopa wewe. Bwana atakufanya uwe kichwa wala si mkia; nawe
utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapo yasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wako,
nikuagizayo hivi leo,kuyaangalia na kuyafanya; msipokengeuka katika maneno
niwaamuruo leo kwa lolote, kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto kwa kuifuata
miungu mingine na kuitumikia. (Kumb 28:1-14)
Damu ya msalaba
iliyoondoa dhambi, ndiyo iliyoondoa umasikini pia, Yatupasa kuuona umasikini
kama tunavyoiona dhambi. Umaskini ni matokeo ya anguko la mwanadamu katika
dhambi. Tukiisha okolewa katika dhambi, yatupasa kuokolewa katika umasikini
pia. Utajiri ni matunda ya msalaba kama ilivyo wokovu. Yatupasa kuchukia
umasikini kama tunavyochukia dhambi. Kifo cha Yesu, kitakuwa hakina
maana kamili, kama tutaokolewa katika dhambi, halafu tubaki maskini katika
mwili pia, wakati Yesu aliyefia dhambi, ndiye aliyefia umasikini pia. Msalaba
ulifanya vyote, yaaani uliondoa dhambi na umasikini pia. Biblia inasema; “Maana
mmejua Neema ya Bwana wetu, Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa masikini kwa ajili
yenu, ingawa alikuwa tajiri. Ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa
umaskini wake. (2Kor 8:9) … mkitajirishwa katika vitu vyote, mpate
kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu. (2Kor 9:11)
JE UMEOKOKA?
UMEOKOLEWA KATIKA HUKUMU IJAYO?
Yesu alikuja
kutafuta na kuokoa sisi tuliopotea. Ndio maana alileta wokovu. Kuokoka
si dini Fulani au dhehebu Fulani. Kuokoka uzima wa milele ndani
ya mtu. “Amini , amini, nawambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye
aliyenipeleka, yuna (ana) uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali
amepita kutoka mautini kuingia uzimani”. Ina maana AMEOKOKA kutoka mautini
(jehanum). Jehanum ndio mauti ya pili. (Ufu 20:14-15)
Watu wengi
wnadhani kutokunywa pombe, kutovuta sigara, kutofanya zinaa, kutoiba, n.k ndio
kuokoka na hukumu ya Mungu. Wengi wanadhani, kwenda kanisani, kuimba kwaya,
kuhubiri, kuwa mzee wa kanisa au kiongozi wa kikundi, n.k ndio kuokoka na
hukumu ya Mungu. Si kweli. Kuna wokovu halisi na matendo au maisha ya wokovu.
Watu wengi wanaishi maisha ya wokovu, lakini kwa uhalisi, hawajaokoka bado,
hawajampa Yesu mioyo yao na maisha yao.
Kushika sheria
za dini na kuishi maisha ya wokovu, siko kunakompendeza Mungu, kama huyo mtu
hajampokea Yesu na kumwamini kama Bwana na mwokozi wa maisha yake.Yesu alisema
hivi kwa Mungu Baba, “ Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu
wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma” (Yoh 17:3). Hatuokoki na
hukumu ya Mungu kwa kushika sheria, bali kwa kuipokea neema ya wokovu kwa
kumwamini Yesu Kristo. “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya
imani, ambayo hiyo haitokani na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu (zawadi). Wala
si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu (Efe 2;8-9)
Kushika sheria
za dini na kuishi maisha ya wokovu, siko kunakompendeza Mungu, kama huyo mtu
hajampokea Yes una kumwamini kama Bwana na mwokozi wa maisha yake.“hali tukijua ya
kuwa, mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo
Yesu; Sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya
Kristo, wala si kwa matendo ya sheria. Maana kwa matendo ya sheria, hakuna
mwenye mwili atakayehesabiwa haki” (Gal 2:16; Gal 3:7-14) Kuna
wokovu halisi na matendo au maisha ya wokovu. Watu wengi wanaishi maisha ya
wokovu, lakini kwa uhalisi, hawajaokoka bado, hawajampa Yesu mioyo yao na
maisha yao.
Kuna habari ya
mtu wa namna hiyo katika Biblia; aliye shika sheria, aliyedumu katika sala,
aliyefunga na kuomba, aliyetoa sadaka nyingi kwa watu maskini, n.k lakini
alikuwa hajafanya hatua muhimu kuliko zote ya kumwamini na kumpokea Yesu
Kristo, ilia pate uzima wa milele na kuokolewa. Aliitwa Kornelio. Isome katika Matendo
ya Mitume 10:1-8, 23-48.
Mungu
akamhurumia kuwa, japo amekuwa mwaminifu kushika sheria na kuishi maisha ya
kumcha Mungu, lakini kwasababu hajamjua Yesu bado, asingeokoka na hukumu ya
milele, kwa maana hana uzima wa milele. Mungu akamtuma malaika kumwambia
Kornelio, amfuate Petro, naye atamweleza cha kufanya. Ndipo Petro akaja na
akamweleza habari za Yesu, Kornelio na familia yake, wote wakamwamini na
kumpokea Yesu. Wakapata wokovu halisi (uzima wa milele). Baada ya hapo, maisha
ya wokovu ndipo yanakuwa na maana. Kushika sheria za dini na kuishi
maisha ya wokovu, siko kunakompendeza Mungu, kama huyo mtu hajampokea Yesu na
kumwamini kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Inawezekana nawe
umekuwa mcha Mungu kama Kornelio, lakini hujampokea Yesu moyoni na kumkiri.
Mpokee sasa!
NAMNA YA KUPATA WOKOVU (KUOKOKA)
HATUA YA
KWANZA; TAMBUA KUWA WEWE NI MWENYE DHAMBI NA UTUBU
DHAMBI ZAKO,
KWA KUMAANISHA KUZIACHA.
“Kwa maana
mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele” (Rum
3:23). “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo, mpate ondoleo la
dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” (Mdo 2:38)
HATUA YA
PILI; MWANINI NA KUMPOKEA YESU MOYONI MWAKO. TOA
MAISHA YAKO
KWAKE, AWE BWANA NA MWOKOZI WAKO.
Yule mlinzi wa
gereza akamwambia Paulo na Sila “Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate
kuokoka? Wakamwambia, mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako”
(Mdo 16:30-31).
“Kwasababu,
ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya
kuwa Mungu alimfufua katika wafu, UTAOKOKA. Kwa maana moyo mtu
huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri, hata KUPATA WOKOVU.
(Rum 10:9-10)
HATUA YA
TATU: ISHI MAISHA YA WOKOVU, MAISHA SAFI YA KUMPENDEZAMUNGU NA KUZISHIKA
AMRI ZAKE (NENO LAKE)
“nawaandikia
haya ili kwamba msitende dhambi… Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye
(Mungu) ikiwa tunashika amri zake. Lakini Yeye asema neno lake, katika
huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli, katika hili twajua ya kuwa tumo
ndani yake….” (1Yoh 2:1-6). Kwahiyo sasa, anza maisha mapya ndani ya Yesu.
“…mtu akiwa
ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa
mapya”. (2Kor 5:17) Jitenge na uovu wote na Usiishi katika maisha ya dhambi
tena.
Pia soma Josh 1:8 na Rum 6:1-23.
MAMBO 12 YALIYOKUTOKEA MAISHANI
MWAKO BAADA YA KUMPOKEA YESU AWE BWANA NA
MWOKOZI WAKO.
Mpendwa,
nataka ujue kwamba, Mungu amefanya mambo mengi makubwa katika maisha yako,
tangu saa/siku ile ulipompokea Yesu, kuwa Bwana na Mwokozi na Mwokozi wako.
Ni muhimu uelewe kwamba, wewe si yule wa zamani tena. Sahau yaliyopita,
kwasababu umefanyika kiumbe kipya. (2 kor 5:17)
Yafuatayo ni
baadhi ya mambo yaliyotokea kwako tangu ulipofanya uamuzi huu mzuri na wa
busara, wa kumpokea Yesu Kristo, kuwa Bwana wako na Mwokozi wa maisha yako.
KWANZA:
UMEFANYIKA MWANA WA MUNGU
Umefanyika
mwana wa Mungu, kwasababu umempokea Yesu Kristo na
kuliamini Jina lake; Kwasababu Biblia inaema “Bali wote
waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale
waliaminio jina lake (Yoh 1:12) … Roho (Mtakatifu) mwenyewe, hushuhudia
pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu…” (Rum 8:16)
Tangu sasa,
wewe ni mmoja wa wana-familia ya Mungu. Nasi tunakukaribisaha kwa upendo wa
Kristo. Karibu sana, Baba (Mungu) na sisi tumefurahi kukuona
umerudi nyumbani. This is where you belong. We missed you so much.
Karibu!
PILI: DHAMBI ZAKO ZOTE ZIMEOSHWA NA KUSAFISHWA KWA DAMU
YA YESU NA UMESAMEHEWA KABISA.
Biblia
inasema, dhambi zako zote zimeoshwa na kusafishwa kwa damu ya Yesu naumesamehewa
zote kabisa, kwasababu umekuja kwa Yesu na umekiri dhambi zako; Kwa
maana imeandikwa “katika yeye huyo (Yesu), kwa damu yake, tunao ukombozi wetu,
msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake (Efe 1:17)… Dhambi zenu
zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa nyeupe kama sufu (Isa 1:18)… maana
nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.” (Yer 31:34b) pia
soma: Kor 1:14, Ufu 1:5.
TATU:
UMEFANYIKA KIUMBE KIPYA
“Hata
imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo; amekuwa kiumbe kipya; (mambo ya kale yamepita
Tazama! Yamekuwa mapya (2Kor 5:17)… Najua neno moja kuwa, mimi nilikuwa kipofu,
na sasa ninaona” (Yoh 9:25)
Kwahiyo
sahau maisha yaliyopita, sasa anza maisha mapya ndani ya Yesu.
NNE: ROHO
MTAKATIFU ANAISHI NDANI YAKO NA ATAKUWA
PAMOJA NAWE MILELE
“Mkinipenda,
mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba (Mungu), naye atawapa msaidizi
mwingine, ili akae nanyi hata milele; Ndiye Roho wa kweli, ambaye ulimwengu
hauwezi kumpokea, kwakuwa haumwoni wala haumtambui, Bali ninyi mnamtambua,
maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu”.
(Yoh
14:15-17) “… Hamjui yakuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu? Na yakuwa Roho wa
Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu alikiharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu
mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.” (1Kor
3:16-17)
TANO: UMEHAMISHWA KUTOKA KATIKA NGUVU ZA HETANI au MAMLAKA YA
SHETANI au UFALME WA SHETANI, NA KUINGIZWA KATIKA UFALME (MAMLAKA) WA YESU
KRISTO.
“Naye (Mungu
Baba) alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme
wa mwana wa Pendo lake (Yesu Kristo)” (Kol 1:13)
“Nanyi
mfahamu kwamba, mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu,
mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa …” (1Pet 1:18)
SITA: UMEHAMISHWA
KUTOKA MAUTINI KUINGIA UZIMANI
“Amini amini
nawaambia, yeye aliskikiaye neno langu, na kumwamini yeye aliyenipeleka, yuna
(ana) uzima wa milele, wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini
kuingia uzimani (Yoh 5:24) “Sisi tunajua yakuwa tumepita kutoka mautini
kuingia uzimani…” (1Yoh 3:14). Sasa basi, hakuna hukumu ya adhabu, juu yao
walio katika kristo Yesu; kwasababu sheria ya Roho wa uzima, ule ulio katika
kristo Yesu, imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. (Rum 8:1-2)
SABA: UMEOKOLEWA
AU UMEOKOKA KUTOKA KATIKA GHADHABU NA ADHABU YA MUNGU.
“Kwa maana,
ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia
katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu. Wala hakuachilia
ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi (alimwokoa) Nuhu mjumbe wa haki, na watu
wengine saba, hapo alipoleta gharika, juu ya ulimwengu wa wasiomcha
Mungu. Tena akaihukumu miji ya Sodoma na gomora, akiipindua na kuifanya
majivu. Akaifanya iwe ishara kwa wtu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya
hayo” (2 Pet 2:4-6)
“Dunia ile ya
wakati ule, iligharikishwa kwa maji ikaangamia, lakini mbingu zasasa na nchi,
zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilohilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na
(siku) ya kuangamia kwao, wanadamu wasiomcha Mungu … Bwana hakawii kuitimiza
ahadi yake, kama wengine wanavyodhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana
hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikie toba …waokolewe na
kupata kujua yaliyo kweli.
((2Pet 3:6-7;
1Tim 2:4)
“Lakini siku ya
Bwana itakuja kama mwizi katika siku hiyo, mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu
na vioumbe vya asili vitaunguzwa na kufumuliwa na nchi na kazi zilizomo ndani
yake zitateketea…. mbingu zitfunuliwa, zikiangua na viumbe vya asili
vitateketea na kuyeyuka. Lakini kama ilivyo ahadi yake, tunatazamia mbingu
mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake. (2Pet 3: 9 -13)
Basi zaidi sana
tukiisha kuhesabiwa haki, katika damu yake (Yesu),tutaokolewa na ghadhabu
kwa yeye. (Rum 5:9)
(Kwahiyo)ukimkiri
Yesu kwa kinywa chako na kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako yakuwa
Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka kwa maana, kwa moyo mtu
huamini hata kupata haki, Na kwa kinywa mtu hukiri, hata kupata
wokovu, (Rom 10:9 -10)
Kwa maana
mmeokolewa (sio, mtaokolewa) bali; MMEOKOLEWA kwa neema, kwa njia ya imani,
ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu, wala si kwa
matendo, mtu awaye yote asije akajisfu. (Efe 2:8)
Maana neema ya
Mungu, iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa (Tito 2:11) na itakuwa, kila
atakayeliitia jina la Bwana, ataokolewa (Mdo 2:21) …. (Petro)Akawashuhudia
kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya; akisema, jiokoeni na
kizazi hiki chenye ukaidi (Mdo 2:40)
Walipoyasikia
haya, wakachomwa mioyo yao, wakmwambia Petro na mitume wengine; Tutendeje ndugu
zetu? Petro akawaambia, Tubunimkabatizwe, kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo,
mpate ondoleo la dhambi zenu nanyi mtapokea kipawa cha Roho mtakatifu (Mdo
2:37-38). Nao waliopokea neno lake, wakabatizwa. Na siku ile
wakaongezeka watu (waume) wapata elfu tatu (41)………Bwana akalizidisha
kanisa kila siku, kwa wale waliokuwa wakiokolewa (Mdo 2:47)
NANE: JINA LAKO
LIMEANDIKWA KATIKA KITABU CHA UZIMA.
“Lakini
msifurahi kwa vile peopo wanavyowatii, bali furahini kwa sababu majina yenu
yameandikwa mbinguni (Luk 10:20)…“Na ndani ya mji mtakatifu) hakitaingia kamwe
chochote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale
walioandikwa katika kitabu cha uzima cha mwanakondoo” (Ufu 21:27) …“Na iwapo
mtu yeyote, hakuonekan ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa
katika lile ziwa la moto” (Ufu 20:15)…“Naam, nataka na wewe pia,
mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao, maana waliishindania injili,
pamoja nami, na wale waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo
katika kitabu cha uzima (Fil 4:3)
TISA: UMEPEWA
(UNAZO) NGUVU NA MAMLAKA YOTE JUU YA SHETANI NA NGUVU ZOTE ZA GIZA.
Hata wakati ule
tulipokuwa wafu kwasababu ya makosa yetu, alituhuisha pamoja na
Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. Akatufufua pamoja naye, akatuketisha
pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika kristo Yesu. (Efe 2:5-6)….. juu
sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina (au
cheo) litajwalo (Efe1:21) (akasema)
”Tazama
nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui (shetani),
wala hakuna kitu kitakachowadhuru (Luk 10:19)… “Nami nitakupa funguo za ufalme
wa mbinguni, na lolote utakololifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni, na
lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni (Math 16:19)…
Angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung’oa, na
kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza, ili kujenga na kupanda (Jer 1:10).
Kila mahali
utakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, mimewapa ninyi …. hapatakuwa mtu yeyote
atakeyeweza kusimama mbele yako, siku zote za maisha yako; kama ulivyokuwa
pamoja na Musa, ndivyo nitakanyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala
sitakuacha (Josh 1:3,5) … Muwe na kiasi na kukesha; kwakuwa mshitaki wenu
ibilisi, kama simba aungurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu
ammeze. Nanyi mpingeni huyo mkiwa thabiti katika imani … (Basi mtiini
Mungu. Mpingeni shetani, naye atawakimbia (Yak 4:7) … “Na ishara hizi,
zitafuatana na hao waaminio, kwa jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha
mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha (kuua), hakitawadhuru
kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya (Mk 16:17-18)
Pia
soma: Dan 7:13,14,27; Yer 51:20
KUMI: UNALINDWA
KWA ULINZI WA MALAIKA WA MBINGUNI
Malaika wa
Bwana hufanya kituo, akiwaangalia wamchao (Mungu) na kuwaokoa
(Zab 34:7) …“Kwakuwa (Mungu) atakuagizia
malaika zake, wakulinde katika njia zako zote (Zab 91:11) … Je? hao (Malaika) wote si roho watumikao, wakitumwa
kuwuhudumia wale watakaourithi wokovu? (Ebr 1:7,14) Nani (Yohana) nikaanguka
mbele ya miguu yake (Malaika) ili nimsujudie; akaniambia, angalia, usifanye
hivi, mimi (Malaika) ni nyoli (Mtumishi) wako na w ndugu zako walio na ushuhuda
wa Yesu. Msujudie Mungu…(Ufu 19:10) … Awagusaye ninyi, aigusa mboni ya jicho
lake (Mungu). Kwa maana, tazama, nitatikisa mkono wangu juu yao … (Zek
2:8-10). Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu, kwa njia ya imani… (1Pet 1:5)
KUMI NA
MOJA: UMEFANYIKA MTUMISHI WA MUNGU.
Watu wengi
waliookoka hawajioni au hawajihesabu kuwa ni watumishi wa Mungu. Bali
huwaona Wachungaji na Wainjilisti kuwa ndio watumishi wa Mungu. Pengine na wewe
unajiona hivyo. Lakini neno la Mungu linasema; SisiKanisa (Yaani:
Jamii ya waaminio au watu waliookoka), sote kwa pamoja, ni mwili
wa Yesu Kristo …
Mungu
alipomfufua Yesu Kristo kutoka katika wafu, alimtukuza, akamweka mkono wake wa
kuume katika ulimwengu wa roho; Juu sana kuliko falme zote na mamlaka zote,
“Akavitia vitu vyote chini ya miguu yake. Akamweka awe kichwa juu ya vitu
vyote, kwa ajili ya kanisa, ambalo ndilo mwili
wake…”(Efe 1:20-23) “Naye (Yesu) ndiye kichwa cha
mwili, yaani cha kanisa….”(Kol 1:18) … Basi ninyi nimekuwa mwili
wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake… kwa maana katika Roho
mmoja, sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu wayahudi, au kwamba tu
wayunani; ikiwa tu watumwa, au ikiwa tu huru;
Nasi sote
tulinyweshwa Roho mmoja, kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi… Maana
kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na vioungo vyote vya mwili ule
navyo ni vingi, na viungo vyote vya mwili ule navyo ni vingi, ni mwili mmoja,
vivyo hivyo na Kristo. (Kor 12,27,13-14,12) … “Basi pana tofauti za
karama; Bali Roho ni (mmoja). Tena pana tofauti za huduma, (lakini) Bwana
ni mmoja. Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni (mmoja)
azitendaye kazi zote katika wote. Lakini Kila mmoja hupewa
ufunuo wa Roho kwa kusaidiana. (1kor 12:4-7)
Angalia hili neno “kila mmoja”
“…Mungu
amevitia viungo kila Kimoja katika mwili, kama alivyotaka. Lakini kama
vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi? Lakini sasa viungo ni
vingi, ila mwili ni mmoja. kila mmoja katika mwili,
kama alivyotaka.Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa
wapi? Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja. “(1Kor 12:18-20)
Angalia hilo
neno tena “kila kimoja” limejirudia.
“ Maana mtu
mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa (kama)
apendavyo Roho yeye yule; mwingine (hupewa) imani katika Roho (huyo huyo); na
mwingine hupewa kaama za kuponya katika Roho yule mmoja; na mwingine (hupewa)
unabii; na mwingine (hupewa) kupambanua roho; na mwingine (hupewa) aina za
lugha; na mwingine (hupewa) tafsiri za lugha; Lakini kazi hizi zote, huzitenda
Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawiakila mtu peke yake,
kama apendavyo yeye. (!Kor 12:8-11)
Angalia hilo neno “kila mmoja” limejirudia tena
Kwa hiyo,
kama vile katika mwili, kila kiungo kina kazi yake (ya kujenga mwili); Vivyo
hivyo, katika mwili wa Kristo, yaani Kanisa, kila muumini, ana kazi yake ana
huduma yake, na karama yake na wajibu wake, katika kujenga mwili wa Kristo.
Wewe na mimi, tu watumishi wa Mungu.Jione hivyo na ujihesabu hivyo. Mungu
anataka utumie karama na uwezo aliokupa, ili kuuvunja ufalme wa shetani, na
kujenga ufalme wa Kristo duniani. Neno la Bwana likamjia, kusema,
kabla sijakuumba katika tumbo, nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa;
Nimekuweka kuwa nabii wa Mataifa. Ndipo niliposema, Aah! Bwana Mungu!
Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto lakini Bwana akaniambia, usiseme
mimi ni mtoto; … usiogope kwasababu ya hao, maana mimi nipo pamoja nawe
nikuokoe, asema. Bwana.
Ndipo Bwana,
akanyoosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; Bwana akaniambia; Tazamani,
nimetia maneno yangu kinywani mwako; Angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na
juu ya falme, ili kung’oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; Ili
kujenga na kupanda (Yer 1:4 -10) “… enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa
wanafunzi (wangu) mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho
Mtakatifu; Nakuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi
nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. (Math 28:18-20).
KUMI NA
MBILI: UMEPEWA AHADI KUBWA MNO NA ZA THAMANI NA MUNGU
Tangu
umeingia katika familia ya wana wa Mungu umepewa urithi wa baraka za
Mungu. Umeingizwa katika mkondo wa baraka na ahadi kubwa na nyingi mno
katika kriso Yesu.
“Na kwa
kuwa ninyi mmekuwa wana (wa Mungu), Mungu alimtuma Roho wa mwanawe mioyoni
mwetu, aliaye Aba, yaani Baba. Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena, bali u
mwana (wa Mungu); Na kama u mwana, basi u mrithikwa Mungu” (Gal
4:6-7)
“Kristo
alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu…,
ili kwamba, Baraka ya Ibrahimu, iwafikie mataifa ktika Yesu Kristo, tupate
kupokea ahadi ya roho kwa njia imani … Na kama ninyi ni
wa kristo, basi mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawa sawa na ahadi”
(Gal 3:13-14,29).
“Atukuzwe
Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa Baraka zote za rohoni,
katika ulimwengu waro ho, ndani yake Kristo. (Efe 1:3)… Tena kwa hayo,
ametukirimia ahadi kubwa mno za thamani, ili kwamba, kwa hizo (ahadi na baraka)
mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani,
kwa sababu ya tamaa.”(2Pet 1:4) Kwa mfano:-
Ahadi ya
Baraka – Kumb 28:1 – 14; Law 26:1-13
Ahadi ya
mafanikio – Zab 1:1 -3; Josh 1:8-9
Ahadi ya
utajiri – Kumb 15:14; 2Kor 8:9 / 2Kor 9:8,11
Ahadi ya Afya
njema – Kut 15:26: Kumb 7:15
Ahadi ya Ulinzi
– Zab 91:11; Zab 121:1-8
Ahadi ya Akili
nzuri – Zab 119:97-100; Zab 111:10
Ahadi ya
Wokovu kwa familia - Mdo 16:31; Isa 54:13 – 14
UHAKIKA WA WOKOVU.
Sasa elewa
vizuri kuwa, TAYARI UMEOKOLEWA, hapa hapa duniani, na si baada ya
kufa. Kwasababu Biblia inasema, “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa
mara moja, na baada ya kufa (ni) hukumu”
(Ebr 9:27).
Mungu ametuletea wokovu hapa hapa duniani, ili tuupokee hapa hapa duniani.
Baada ya kufa, hakuna wokovu tena, bali hukumu. Mtu anayesubiri wokovu baada ya
kufa, atakuwa amechelewa!
Kumbuka
habari ambayo Yesu alisema “Palikuwa na mtu mmoja tajiri, aliyevaa nguo za
rangi ya zambarau na kitani safi, na kula siku zote kwa anasa. Na alikuwepo
masikini mmoja, jina lake Lazaro, aliyewekwa mlangoni pa tajiri, na ana vidonda
vingi. Naye masikini alitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza
ya yule tajiri, hata mbwa wakalamba vidonda vyake”.
Hii ina
maana kwamba, tajiri hakuwa mcha Mungu; Kwa maana hakumjali masikini, pamoja na
kwamba alikuwa na uwezo. Masikini alikuwa na hali mbaya sana, ya njaa na
ugonjwa, hata hakuweza tena kuwafukuza mbwa waliomkaribia. Ndio maana, Tajiri
alipokufa, alikwenda motoni. “ikawa yule masikini alikufa, akachukuliwa na
malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu”. (Hii ina maana, masikini alikuwa mcha
Mungu). “Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi kule kuzimu aliyainua macho
yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali na Lazaro kifuani
mwake. Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha
ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwasababu ninateswa katika
moto huu. Ibrahimu akasema, mwanangu, kumbuka ya kwamba, wewe uliyapokea mambo
mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo
hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi,
kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala
watu wa kwenu, wasivuke kuja huku.
(Tajiri)
akasema, basi, Baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu (duniani),
kwakuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali
hapa pa mateso. Ibrahimu akasema, (kule duniani) wanao Musa na Manabii; na
wawasikilize wao. (Tajiri) akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea
mtu atokaye kwa wafu, watatubu. (Ibrahimu) akamwambia, wasipowasikia Musa na
Manabii (wahubiri mbalimbali), hawatashawishiwa, hata mtu akifufuka katika
wafu”.
BAADA YA KUFA
NI HUKUMU! HAKUNA WOKOVU! Mungu ametuletea wokovu hapa hapa duniani, ili
tuupokee hapa hapa duniani, kabla ya kifo kutujia. Baada ya kufa, hakuna wokovu
tena, bali hukumu. Mtu anayesubiri wokovu baada ya kufa, atakuwa amechelewa,
kama yule Tajiri!
Ni muhimu pia
uelewe kwamba, tajiri hakwenda motoni kwa sababu alikuwa tajiri; wala masikini
hakusalimika au hakuokoka kwasababu alikuwamasikini. Utajiri si dhambi,
wala umasikini si utakatifu. Uhusiano wako na Mungu ndicho kitu
kitakachoamua utakwenda kuishi wapi milele. Wala si fedha yako, wala elimu
yako, wal dini yako! Kitu pelee kitakachoamua wapi utaishi milele, ni uhusiano
wako na Mungu. “Basi tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote
NA HUO UTAKATIFU (ucha Mungu) ambao hapana mtu atakayemwona Mungu, asipokuwa
nao” (Ebr 12:14)
Unaweza
ukaupata ulimwengu wote, ukawa na kila kitu duniani; utajiri, elimu nzuri, dini
nzuri, kazi nzuri, nyumba nzuri, mshahara mzuri, magari mazuri, viwanda hata
migodi ya thamani. Lakini kama huna wokovu, yaani uhusiano mzuri na Mungu,
hutaweza kuingia mbinguni. “Kwani itamsaidia nini mtu, akiupata
ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake?” (Math 16:26)
Hakuna faida!
Utajiri halisi
ni ule wa ndani (wokovu) ukiunganishwa na wanje (mali na pesa). Ndio maana Yesu
anasema “Nayajua matendo yako, yakuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa
heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi kwasababu una uvuguvugu, wala hu baridi
wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. Kwakuwa wasema, mimi ni
tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe ni
mnyonge, na mwenye mashaka, na masikini, na kipofu, na uchi.” (Ufu
3:15-17).
Kumbe unaweza
ukavaa na kupendeza mbele za watu, na kumbe mbele za Mungu uko uchi kabisa!
Unaweza ukawa mbabe na mjanja mbele za watu, na kumbe mbele za Mungu ukawa
mnyonge na si kitu kabisa! Unaweza kudhani unaona kwa macho, na kumbe umefichwa
vitu vingi halisi, huvioni! Unaweza ukawa tajiri wa mali za ulimwengu, na kumbe
mbele za Mungu ukawa masikini kabisa, kwasababu huna ule utajiri halisi,yaani
wokovu. Yesu anamalizia kwa kusema “Nakupa ushauri, ununue kwangudhahabu
iliyosafishwa kwa moto (yaani WOKOVU), UPATE KUWA TAJIRI, na mavazi upate
kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako,
upate kuona.”
Dhahabu
inayotajwa hapo ni WOKOVU, kama ilivyoandikwa katika Mathayo 13:44-46; “Tena
Ufalme wa mbinguni umefanana na HAZINA iliyositirika
katika shamba, ambayo mtu aliopoiona, aliificha; na kwa furaha yake, akaenda
akauza vyote alivyo navyo, akalinunua lile shamba. Tena Ufalme wa mbinguni
umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta LULU NZURI; naye
alipoona LULU MOJA YA THAMANI KUBWA, alikwenda akauza vyote alivyo
navyo, akainunua”. Hapa, tunaambiwa habari za wokovu kuwa ni KITO cha
thamani! Wokovu ni LULU! Wokovu ni DHAHABU Ya thamani nyingi! Wokovu ni HAZINA
njema!
Maadam
umempokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako, Mungu anakwambia “unao uzima
wa milele” sasa hivi ukiwa hapa hapa duniani. “Amini amini nawaambia, yeye
alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka, YUNA (ANAO)
UZIMA WA MILELE; WALA HAINGII HUKUMUNI, BALI AMEPITA KUTOKA MAUTINI
KUINGIA UZIMANi” (Yoh 5:24). Mungu anakwambia “unao uzima
wa milele” sasa hivi ukiwa hapa hapa duniani. Sio kwamba “utakuwa
nao” bali ansema “unao” yaani sasa! Na tena anasema, kwa kuwa unao uzima
moyoni mwako, hutaingia hukumuni, bali “umepita” kutoka mautini kuingia
uzimani! Sio “utapita”, bali Mungu anasema, “tayari umepita” kutoka
mautini, kuingia uzimani.
Pia imeandikwa
hivyo katika 1Yoh 3:14. Na tena 2Wakorintho 6:2 inasema; “… Tazama,
wakati uliokubalika ndio sasa; TAZAMA, SIKU YA WOKOVU NDIO SASA.
Baada ya kufa,
hakuna wokovu tena, bali hukumu. Mtu anayesubiri wokovu baada ya kufa,atakuwa
amechelewa!
UWE NA UHAKIKA
WA WOKOVU WAKO. JUA KWAMBA, KWA NEEMA YA MUNGU, UMEOKOKA! Kwa maana
imeandikwa “MMEOKOLEWA KWA NEEMA, KWA NJIA YA IMANI; HIYO
HAIKUTOKANA NA NAFSI ZENU, NI KIPAWA CHA MUNGU”. (Efe 2:8)
KANUNI ZA MAISHA YA KILA SIKU YA KIKRISTO.
(KANUNI ZA MAISHA YA WOKOVU)
Mpendwa,
inabidi ufahamu kwamba, kuokoka haimaanishi tayari umefika mbinguni; Bali
inamaana kwamba; ndio tu umeanza safari salama ya kwenda mbinguni. Mtu ambaye
hajaokoka, ni kwamba hajaanza kabisa safari ya kwenda mbinguni. Na unafahamu
kwamba, wakati mwingine, si wasafiri wote humaliza safari zao; Kwasababu katika
safari huwa kuna vikwazo mbalimbali. Wengine huishia mwanzoni kabisa mwa
safari, wengine huishia katikati ya safari na wengine huishia mlangoni kabisa
na kushindwa kuimaliza safari.
Safari ya
mbinguni pia, ina vikwazo vingi. Ndio maana Biblia inasema “mlango
ni mwembamba na njia imesonga, iendayo uzimani” (Math 7:14). Ni
shauku ya Mungu na yetu pia, kwamba uimalize salama safari yako ya kwenda
mbinguni, ambayo uliianza siku uliyompa Yesu Kristo maisha yako na kuokoka. Si
njia rahisi. Kuna mambo mengi ya kukukwaza na kukuzuia. Lakini Mungu amekuahidi
ushindi katika mambo yote hata kukufikisha mbinguni salama.
Biblia
inasema; “Hata (Mitume) walipokwisha kuihubiri injili katika mji ule, na kupata
wanafunzi wengi, wakarejea mpaka Listra na Ikonio na Antiokia, wakifanya imara
roho za wanafunzi, na kuwaonya wakae katika ile imani, na yakwamba imetupasa
kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi” (Mdo 14:21-22). Yesu
alisema; “Ulimwenguni mnayo dhiki, lakini jipeni moyo, mimi (Yesu) nimeushinda
ulimwengu” (Yoh 16:33). Lakini “Katika mambo yote tunashinda na zaidi ya
kushinda, katika yeye (Yesu) aliyetupenda” (Rum 8:37). Hebu sema kama Paulo
“Nayaweza mambo yote, katika yeye (Mungu) anitiaye nguvu” (Fil 4:13)
Ebr
11:32-38 inasema “Na niseme nini tena? Maana wakati usingetosha kuleta
habari za Gideoni, na Baraka, na Samsoni, na Yefta, na Daudi, na Samweli, na za
Manabii; Ambao kwa imani, walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata
ahadi, walifunga vinywa vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali
ya upanga, walitiwa nguvu baada ya kuwa wadhaifu, walikuwa hodari katika vita,
walikimbiza majeshi ya wageni. Wanawake walipokea wafu wao, waliofufuliwa.
Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuwawa … wengine walijaribiwa kwa
dhihaka na mapigo, naam kwa mafungo na kwa kutiwa gerezani. Walipigwa kwa mawe,
walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuwawa kwa upanga, walizunguka-zunguka
wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; … wakiteswa, wakitendwa mabaya;
… Walikuwa
wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima, na katika mapango na mashimo
ya nchi.”
Haiwezekani
hawa mashujaa wa imani, washinde vita na upinzani huo, na kuingia mbinguni kwa
ushindi, kwa nguvu zao wenyewe. Ni lazima kuna siri fulani iliwasaidia kumaliza
safari yao kwa ushindi. Siri hizo na kanuni hizo ndizo zilizowasaidia wengi na
ndizo zinazotusaidia wengi, kuishi maisha ya wokovu kwa ushindi.
Mpendwa, fahamu
kwamba, NEEMA YA WOKOVU ambayo umepewa na Yesu, ni ya thamani
kuu kuliko kitu chochote duniani. Hakuna fedha wala dhahabu inayoweza
kununua wokovu. Wala hakuna kitu chochote duniani kinachoweza
kulingana na wokovu ambao Yesu ametupa. Si fedha, wala dhahabu, wala almasi,
wala elimu, wala cheo, wala pesa au chochote kinachoweza kulingana na zawadi ya
wokovu tulionao katika Yesu. Wokovu ulionao sasa, ndicho kitu cha gharama zaidi
na cha thamani zaidi kuliko vitu vyote duniani.
Kila kitu cha
gharama kama vile redio, televisheni, friji, gari, compyuta, n.k. hutengenezwa
na kuuzwa pamoja na kitabu chenye maelezo ya jinsi ya kukitumia (manual book),
kinachokuwezesha kukitumia hicho kifaa au chombo, kwa usahihi bila kukiharibu.
Kama mmiliki wa kifaa au chombo hicho hatafuata maelekezo ya watengenezaji wa
chombo kile, basi kifaa hicho kitaharibika na kushindwa kulitimiza kusudi lake.
Vivyo hivyo, na
WOKOVU huu tuliopewa na Bwana Yesu, ni wa thamani na gharama kubwa, tena
unaweza kuharibika kirahisi (very fragile). Hivyo, unatakiwa kuutunza kwa
umakini na uangalifu mkubwa, kwa kufuata maelekezo, kanuni na siri za maisha ya
wokovu. Siri hizo na kanuni hizo, ndizo zilizowasaidia wengi na ndizo
zinazotusaidia wengi, kuishi maisha ya wokovu kwa ushindi, bila kuharibu. Bwana
Yesu mtoa uzima, na aliye mwanzilishi wa wokovu wetu, ametupa kitabu cha
maelekezo (manual book) cha namna ya kuutunza wokovu wetu, ili tusiuharibu,
tusiuchafue wala kuupoteza. Kitabu hiki kinaitwa BIBLIA TAKATIFU!
Kila siku
hakikisha unasoma maelekezo ya kutosha kwa ajili ya wokovu wako. Na kwa
kuyafuata maagizo ya NENO LA MUNGU, hautaweza kamwe kuuharibu,
kuuchafua au kuupoteza wokovu, yaani uhusiano mzuri na Mungu. Nawe utaweza
kuimaliza safari yako ya mbinguni kwa salama na uhahika, kama wale mashujaa wa
imani. Angalia
maandiko yanavyosema; “Kitabu hiki cha torati (Neno la Mungu) kisiondoke
kinywani mwako; bali uyatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia
kutenda sawa sawa na maneno yake yaliyoandikwa humo; maana ndipo
utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana”. (Joshua 1:8)
KANUNI ZA MAISHA YA USHINDI
1. DUMU
KATIKA MAOMBI – ONGEA NA MUNGU KILA SIKU
KWA SALA NA MAOMBI.
“Dumuni sana
katika kuomba, mkikesha katika kuomba, huku na shukurani …” (Kol 4:2) “…
imewapasa kumwomba Mungu siku zote, wala msikate tamaa” (Luk 18:1) … “Kwa
sala zote na maombi, mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo
na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote”
(Efe 6:18) …
“Furahini siku zote; ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo, maana hayo
ni mapenzi ya Mungu kwenu katika kristo Yesu.” (1Thes 5:16-18)
Kwanini Biblia
inasisitiza sana tudumu katika maombi? Maombi ni namna ya wewe kuwasiliana na
Mungu Baba. Tangu umeokoka, umefanyika mwana wa Mungu. Maongezi huunganisha
familia. Maongezi huimarisha uhusiano. Ili uzidi kukua katika kumjua Mungu na
uhusiano wako na Mungu uweze kuimarika, yakupasa kudumu sana katika maombi na
sala. Tamani kujifunza kuomba, tena tamani kiwango chako cha maombi kiongezeke.
“Ikawa (Yesu) alipokuwa mahali fulani akiomba, alipomaliza, mmoja katika
wanafunzi wake akamwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha
wanafunzi wake” (Luk 11:1).
Katika maombi
kuna faida nyingi;-
Kwa mfano:
(i) Katika
maombi unapata kumjua Mungu na kuwa karibu nae zaidi.
ii) Katika
maombi unapata uongozi wa Mungu na kujua mapenzi ya Mungu
(iii) Katika
maombi unapata nguvu za kushinda dhambi na majaribu.
(iv) Katika
maombi anapata nguvu za kumpinga shetani na kuvunja kazi zake.
(v) Katika
maombi unapata kumweleza Mungu mahitaji yako na haja zako.
(vi) Katika
maombi unapata kukua katika karama, huduma na vipawa.
(vii) Katika
maombi unapata amani na kujaa furaha ya Roho Mtakatifu.
(viii) Katika
kuomba unapata baraka na kibali cha Mungu (favour) maishani .
Ndio maana Neno
la Mungu linasisitiza kudumu katika maombi. Tenga muda wa kuomba kila siku. Na
uwe mwaminifu. Utaona furaha, amani, Baraka, Ushindi na Mafanikio katika maisha
yako na kazi zako.
Uwe na muda
wako binafsi, wa kufanya maombi. Biblia inasema, Yesu alituonyesha mfano;
“Walikwenda kila mtu nyumbani kwake; naye Yesu akaenda mpaka mlima wa Mizeituni
(kuomba) (Yoh 8:1) … Hata alfajiri na mapema sana, akaondoka, akatoka akaenda
zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko. (Mk 1:35) Naye alipokwisha
kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. (Math 14:22-23) …
Yeye (Yesu) siku hizo za mwili wake, alimtolea (Mungu) maombi na dua na kulia
sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu. (Ebr 5:7)
2. SOMA
BIBLIA – MRUHUSU MUNGU ASEME NAWE KILA SIKU KWA NENO LAKE.
“Neno la
Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana”
(Kol 3:16)
…” kila andiko lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu
makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa
Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema” (2Tim 3:16-17) …
“kama watoto wachanga waliozaliwa sasa, yatamanini maziwa ya akili
yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu”. Kitabu hiki cha torati
(Neno la Mungu) kisiondoke kinywani mwako; bali uyatafakari maneno yake mchana
na usiku, upate kuangalia kutenda sawa sawa na maneno yake yaliyoandikwa humo;
maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana”.
(Joshua 1:8) Neno la Mungu li hai lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga
ukatao kuwili…” Ebr 4:12-13, Pia soma Ebr 5:12-13.
3. KUSANYIKA
/ JUMUIKA NA WAAMINIO WENGINE, KUMWABUDU MUNGU
NA KUJIFNZA NENO LA MUNGU.
“Bwana
akalizidisha kanisa kila siku, kwa wale waliokuwa wakiokolewa … na watu
walioamini, walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika … na siku
zote kwa moyo mmoja, walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa
nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha, na kwa moyo mweupe, wakimsifu
Mungu na kuwapendeza watu wote … wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na
katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali. (Mdo 2:42-47) …Tena
nawaambia, ya kwamba, wawili wenu watakapo patana duniani katika jambo lolote
watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo
wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu; nami nipo papo hapo katikati yao
(Math 18:19-20). Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima
yote, mkifundishana na kuonyana (Kol 3:16)
Pia soma
2Tim 2:22; Heb 5:12-13.
4. ISHI
MAISHA MASAFI NA MATAKATIFU, YANAYO MPENDEZA MUNGU
“Tuseme nini
basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia
dhambi, tutaishije tena katika dhambi? … Tukijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa
kale, ulisulubishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilika, tusitumikie
dhambi tena; … Vivyo hivyo, ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu wa dhambi, na
walio hai kwa Mungu, katika Kristo Yesu … Basi, dhambi isitawale ndani ya miili
yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zenu; wala msiendelee kuvitoa
viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; Bali jitoeni wenyewe kwa Mungu,
kama walio hai baada ya kufa, na (vitoeni) viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha
za haki. Kwa maana dhambi haita watawala ninyi, kwasababu hamuwi chini ya
sheria, Bali chini ya Neema.
… Lakini
Mungu na shukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa
mioyo yenu ile maana ya elimu (wokovu) ambayo mliwekwa chini yake; na
mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki … kwakuwa kama
mlivyovitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na uasi mpate kuasi, vivyo hivyo
sasa, vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa.
Kwa maana
mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na haki. Ni faida gani basi
mliyoipata siku zile kwa mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa? Kwa maana mwisho
wa mambo hayo ni mauti. Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na
dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na
mwisho wake ni uzima wa milele. Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; Bali
karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu, Bwana wetu. (Rum 6:1-2,
6, 11-14, 17-23)
Basi nasema
neno hili, tena nashuhudia katika Bwana, tangu sasa msienende kama mataifa
waenendavyo, katika ubatili wa nia zao; ambao akili zao zimetiwa giza, nao
wamefarakanishwa na uzima wa Mungu, kwasababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwasababu
ya ugumu wa mioyo yao; ambao wakiisha kufa ganzi, wanajitia katika mambo ya
ufisadi (uchafu), wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani. Bali
ninyi, sivyo mlivyojifunza Kristo; ikiwa mlimsikia mkafundishwa katika yeye,
kama kweli ilivyo katika Yesu, mfue kwa habari ya mwenendo wa kwanza, utu wa
zamani, unao haribika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya. Na mfanye wapya
katika roho ya nia zenu, mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika
haki na utakatifu wa kweli (Efe 4:17-24)
“Iliyobaki
ndugu, tunawasihi na kuwaonya kwamba, mwenende katika Bwana Yesu; kama
mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi
mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana. Kwakuwa mnajua ni maagizo gani
tuliyowapa kwa Bwana Yesu. Maan hayo ndiyo mapenzi ya Mungu, (ndiyo) kutakaswa
kwenu, mwepukane na uasherati; Kila mmoja wenu, ajue kuuweza mwili wake katika
utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama mataifa wasiomjua
Mungu. (1Thes 4:1-5) … “Jitengeni na ubaya wa kila namna” (1Thes 5:22),
“Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na (pia tafuteni kwa
bidii kuwa na) huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana,
asipokuwa nao.” (Ebr 12:14) …“Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu,
ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana
imeandikwa, mtakuwa watakatiku, kwa kuwa mimi ni mtakatifu” (1Pet
1:15-16)
5. UWE SHAHIDI WA YESU KWA WATU WENGINE.
“Mtu na
atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu”
(1Kor 4:1) … Kwa urahisi kabisa, mwambie mtu mwingine, mambo ambayo Mungu
amekutendea, ya kwamba Mungu ameyabadilisha maisha yako. Waambie kwamba,
ulikuwa na maisha maovu na kwamba Yesu amekusamehe, amekuokoa na amekupa maisha
mapya, ambayo ndiyo maisha ya uzima milele. Kisha waambie kuwa, Yesu
anawapenda, na anataka kuingi katika maisha yao. Waulize kama wako tayari
kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao. Kama wako tayari, waombee
wapokee wokovu kama wewe; Nawe utakuwa mtumishi wa Mungu kwa kuifanya kazi ya
Mungu.
Wewe ni
mtumishi wa Mungu (1Kor 4:1) Yesu anakwambia “Enenda zako, nyumbani kwako, na
kwa watu wa kwenu, kawahubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi
alivyokurehemu. Akaenda zake, akaanza kuhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani
makuu, Yesu aliyomtendea; watu wakastaajabu”. (Marko 5:19)
NAMNA YA
KUSHUHUDIA INJILI KWA WATU WENGINE.
Waeleweshe
kwamba;
WANADAMU WOTE TUMEFANYA DHAMBI.
“…
(wanadamu) wote tumefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Rum 3:23)
ADHABU YA MUNGU INAUJIA ULIMWENGU WOTE.
“…mbingu na
nchi zimewekwa akiba kwa moto, zikilindwa hata siku ya hukumu, na kuangamia
kwao wanadamu wasio mcha Mungu” (2Pet 3:7)
HAKUNA MWANADAMU ANAYEWEZA KUJIOKOA MWENYEWE.
“ni nani
awezaye kuokoka? Yesu akawakazia macho akawaambia, kwa wanadamu, hilo
haliwezekani; Bali kwa Mungu, yote yanawezekana” (Math 19:25-26)
IKO NJIA MUNGU AMEANDAA, YA KUOKOKA KATIKA ADHABU HIYO.
YESU NDIYE NJIA YA KUOKOKA NA HUKUMU YA MUNGU.
“ Yesu
akamwambia, Mimi ndimi Njia, na Kweli, na Uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa
njia ya Mimi” (Yoh 14:6) “Aniaminiye Mimi , anao uzima … haingii hukumuni, bali
amepita kutoka hukumuni kuingia uzimani” (Yoh 5:24) Ukimkiri na kumwamini
……utaokoka”
(Rum
10;9-10)
MUULIZE KAMA YUKO TAYARI KUMWAMINI NA KUMPOKEA YESU.
MWONGOZE SALA YA TOBA NA KUPOKEA WOKOVU. (Mdo 8:35-39)
Kwa mfano;
Ee Bwana
Yesu, ninakuja kwako. Ninakiri mimi mwenye dhambi na makosa mengi.
Nazijutia dhambi zangu na kutubu kweli. Ninaomba unisamehe na kuniosha kwa damu
yako ya thamani. Ninaomba uniokoe maisha yangu. Nafungua moyo wangu na
ninakukaribisha. Ingia ndani yangu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Uwe Bwana na
Mwokozi wangu tangu sasa. Weka ndani yangu, uzima wa milele na uhakika wa
wokovu. Asante Yesu kwa kuniokoa. Naomba unipe nguvu za Roho wako Mtakatifu,
nianze maisha mapya, nisirudi nyuma tena. Katika jina la lako takatifu, Yesu
Kristo, ninaomba na kushukuru, Amen.
WEWE NI MSHINDI.
Mpendwa,
nataka kukwambia, tunaishi katika ulimwengu mbaya na mchafu sana. Lakini
katikati yake, kuna watu walioipata furaha na amani ya kweli, ambayo ni bora na
ya thamani mno kuliko vitu vyote. Watu hawa wanadharauliwa na kutukanwa,
wengine wanateswa na kunyanyaswa, lakini wao hawajali. Wanachukiwa na ulimwengu
wote lakini siku zote , wamejaa furaha na amani ya Mungu. Ni mabwana wa nafsi
zao, wameushinda ulimwengu na hakuna kinachoweza kuwazuia. Wanaonekana wako
katika upande wa washindi tu.
Watu hawa
wanaitwa WAKRISTO. WAMEOKOKA, WAMEJAZWA NA ROHO MTAKATIFU na WANAKWENDA
MBINGUNI. Nataka ujue kwamba, MIMI PIA MMOJA WAO! Na kwasababu NA WEWE UMETUBU
DHAMBI ZAKO NA KUMPOKEA YESU KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO, WEWE PIA NI
MMOJA WETU. NASI TUNAKUKARIBISHA KATIKA FAMILIA YA MUNGU, KWA UPENDO MKUBWA.
YESU
ANAKWAMBIA; “…USIOGOPE WALA USIFADHAIKE, KWA KUWA BWANA MUNGU WAKO YUKO PAMOKA
NAWE KILA UENDAKO … SITAKUACHA WALA SITAKUPUNGUKIA ….NIKO PAMOJA NAWE HATA
MWISHO WA DUNIA …. UWEMWAMIIFU HATA KUFA, NAMI NITAKUPA TAJI YA UZIMA.
(Joshua
1:9,5 Math 28:20 Uu 2:10)
“Kwasababu
hiyo, tangu (sisi) tulipopata habari za imani yenu katika Bwana Yesu, na pendo
lenu kwa watatakatifu wote, hatuachi utoa shukrani (kwa Mungu) kwa ajili yenu
na tukiwakumbuka katika sala zetu, ili Mungu wa Bwana Yesu Kristo, Baba wa
utukufu, awape ninyi roho ya hekima naya ufunuo katka kumjua yeye; macho ya
mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la wito wake jinsi lilivyo, na utajiri wa
utukufu wa urithi wake kwa watakatifu jinsi ulivyo; na ubora wa ukuu wa uweza
wake ndani yetu tuaminio jinsi, kwa kadri ya utendaji wa nguvu za uweza wake
….” (Efe 1:15-19),
“Desciples
of Christ” tunakuombea sana. Ni kwasababu tunakupenda na tunakujali. Ni maombi
yetu kwa Mungu Baba kwamba, uweze kukuwa katika neema ya wokovu na katika
kumjua sana Yesu Kristo Bwana na kuimaliza safari yako salama ya kwenda
mbinguni. Nasi tunaamini kabisa ya kuwa “Yeye (Mungu) aliyeanzisha kazi njema
mioyoni mwenu, ataimaliza (ataikamilisha) hata siku ya Kristo Yesu.” (Fil 1:6)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni