Ijumaa, 10 Agosti 2012

KUSIFU NA KUABUDU



KUSIFU NA KUABUDU.

Kusifu na kumwabudu Mungu katika roho na kweli, ni jukumu kuu la wakati wote katika maisha yetu binafsi na katika makanisa yetu hii ni kwa sababu Mungu alituumba sisi kwa ajili yake mwenyewe. Anasema (Isaya 43: 21) “watu wale niliojiumbia nafsi yanguili watangaze sifa zangu. Hii inatuthibitishia kuwa tuliumbwa ili siku zote hisia zetu zimwelekee yeye na tutangaze sifa za Mungu wetu.  ( Ezekieli 28: 11 – 15) Mungu anavyojiumbia. 1Petro 2:9. 

Kuabudu ni huduma ya hali ya juu ya mkristo, ndio msingi wa huduma zingine.  
Siku zote Mungu asili yake ni kuwa na uhusiano wa ndani na watoto wake. 
Anapenda watoto wake wamtambue kuwa yeye ni Baba anataka awaguse  na kuwaliwaza Yeremia 7:13,Isaya 50:2,66:12 -14. 

Anapenda tutambue wokovu wetu aliouleta ili tushirikiane naye na kumfurahia 1Nyakati 16:4-36 Kumbukumbu 31:30-32, Zakaria 8:7-8 Tazama nitawaokoa watu wangu nami nitawaleta nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao,katika kweli.

MUNGU ANAKAA JUU YA SIFA. ZABURI 22:3
Uhusiano wako na Mungu na mwendelezo wa mafunuo juu yake (Udhihirisho wake kwako) vimefungwa ndani ya kumwabudu yeye Daudi alijua ukweli huu kutokana na uzoefu wa maisha yake. Zaburi 42:5. Ndio maana anatoa ushauri 1Nyakati 28:9 nawe,Sulemani mwanangu,mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu,na kwa nia ya kumkubali kwa kuwa BWANA hutafuta-tafuta mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira ukimtafuta,ataonekana nawe, ukimwacha atakutupa milele. Na ukiangalia Zaburi 37:4 Nawe utajifurahisha kwa Bwana,Naye atakupa haja za moyo wako. Yohana 4:23 Yesu anatangaza kwa kusema hivi, lakini saa inakuja,nayo sasa ipo ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Watu watakaompenda kwa mioyo yao yote Isaya 49:15-16, 66:10-14 ambao wataungamanishwa naye katika mapenzi ya kupendana. Bila kujali mambo yanayotuzunguka tuko katika hali gani,tunapaswa kumwabudu kwa kumpa thamani yake jinsi alivyo Marko 16:1-8,matendo 13:22 kwa utayari huo tutaona maajabu yake na vifungo vyetu kufunguliwa. Zaburi 139:1-18,45:1,4-6 sisi tumwambie haya naye aseme hivi, Isaya 66:9-10 Yesu alionyesha umuhimu wa kutanguliza kumwabudu Mungu kila alipofundisha. Mathayo 6:9-10 atoaye dhabihu za sifa ndiye anayenitukuza Mimi, nitamwonyesha wokovu Zaburi Zaburi 51:17. Sifa za namna hii hazimpiti Mungu kwa sababu popote zinapotolewa,wazee walioko mbele ya  kiti cha enzi huanguka kuzipitisha zimwendee 



anayestahili Ufunuo 4:9-11. Kutoka 3:12 utakapokuwa umekwisha kuwatoa hao watu katika Misri mtamwabudu Mungu. Ufunuo 7:9-12. Sifa za kweli,zinapatikana kwa wale waliokombolewa,(malaika wana sifa za kupangwa). Ndilo tunda pekee ambalo Mungu analifaidi toka katika moyo wa binadamu. Ufunuo 14:13. Mungu anawatafuta watu watakaokuwa na jukumu la kujitolea kikamilifu kumtii yeye, watu wenye shauku ya kumtafakari yeye. Zaburi 63:108;48:9-10. Watu watakaojihusisha kwa kuwajibika wa kumtanguliza katika kila jambo nay a kuwa yeye ndiye kiini cha yote. Sio washiriki au wachangiaji. Zaburi 50:23, 1Petro 2:9 bali ninyi ni mzao mteule,ukuhani wa kifalme,taifa takatifu,watu wa milki ya Mungu,mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; Ezekieli 28:11-15 hii ndiyo asili yake,Anajifanyia yote haya kwa sababu zake mwenyewe. (kwa ajili yake mwenyewe). Tazama nitawaokoa watu wangu nami nitawaleta nao watakuwa watu wangu,nami nitakuwa Mungu wao,katika kweli na katika haki. Zakaria 8:7-8.
Wokovu hudai sifa,ufunuo 7:9-17 mkutano mkuu wa kila taifa,lugha na jamii wakisema unastahili wewe Ufunuo 5:6-10, Ufunuo 15:3-4 wimbo unaimbwa na watu waliouthibtisha wokovu wa Mungu (wanamtambua Mungu na kazi zake au jinsi alivyo).
Ø  Ufunuo 1:12-16 Mtu mfano wa mwanadamu.
Ø  Mwanzo 1:26. Mathayo 6:6-10. Amevaa vazi lililofika miguuni,( kuhani mkuu anayejishughulisha na kuwahangaikia upatanisho)
Ø  Mathayo 6:11-13a na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.(moyo wa umama Isaya 66:10-14. Amejaa upendo huruma,neema na huruma.
Ø  Kichwa chake na nywele zake zinakuwa nyeupe kama sufu nyeupe kama theruji; Daniel 7:9,13,22. Mzee wa siku,umilele ndani yake,anayejua kila kitu amejaa hekima.
Ø  Na macho yake kama mwali wa moto. (mamlaka katika utawala wa ufalme wake,anaona kila kinachoendelea katika mambo yote aliyoyaumba maana anamiliki yote na hakuna kitakachomshinda.
Ø  Na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana. Inamwezesha kuhukumu kwa haki kila mahali na kwa wakati mwafaka. Ufunuo 19:12
Ø  Na sauti yake kama sauti ya maji mengi(mara zote huzungumza kwa mamlaka na nguvu na ni lazima asikiwe).
Ø  Upanga mkali,wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake;(neno la Mungu lililo hai). Waebrania 4:12 hupigana na maadui zake kwa kutumia neno lake. Ufunuo 2:16.
Ø  Mawe ya thamani (fahari na thamani ya Mungu isiyoweza kulinganishwa na chochote,(KAMA).
Ø  Upinde wa mvua (Maagano yake siku zote yako mbele yake hawezi kusahau kutimia yote kwa ukamilifu,maana ni mwaminifu).
KUSIFU.
Kabla ya maelezo juu ya kuabuduni vizuri kwanza tugusie juu ya kusifu ni nini. Kwa sababu ukiangalia kwa makini kusifu na kuabudu ni vitu viwili tofauti,ingawa vinaenda pamoja. Unaweza kuwa na ibada ya sifa bila kuabudu,lakini siyo rahisi kuwa  ibada ya kuabudu bila kusifu.ni mara chache kutokea kuwa na ibada ya kuabudu bila kusifu,hii hutokea tu mtu anapovamiwa na mguso war oho wa Mungu. Kusifu kwa vyovyote huwa ni tendo la kutangaza kwa nguvu na kwa uwazi hadharani,ukielezea na kuonyesha uhakika ulionao juu ya unachokitolea sifa.popote panapokusudiwa kuwa pawepo na sifa,kuna hekaheka na matendo,sauti na nyimbo,vyote huonekana na kusikika. Ni utaratibu unaopangwa na ufahamu wako jinsi gani udhamirie kusifia. Kusifu ni njia ya lango kuu la kuingilia katika kiini cha kuabudu. Hivyo kusifu ni ibada yenye umuhimu wa kipekee kwa Mungu wetu Zaburi 22:3.
1.      Jinsi alivyo, Zaburi 117: 1-2 Haleluya; Enyi mataifa yote, msifuni Bwana, Enyi watu wote,mhimidini. Maana fadhili zake kwetu sisi ni kuu, na uaminifu wa Bwana ni wa milele 2Nyakati 20:5-6.
2.      Jinsi anavyotenda (mfano) 2Nyakati 20:7
3.      Jinsi anavyotegemewa.(mfano) 2Nyakati 20:12
Kwa Mungu wetu ii sadaka ya sifa hutolewa kwa uhiyari wa mtu bila kujali ana matatizo gani au yuko katika hali gani, bali shauri la moyoni mwake ni kwamba ameazimia kummsifu Mungu na kumwinua jinsi alivyo kutegemea anavyomfahamu Mungu ni nani na yukoje. Matendo 16:24-34.
TUNAFANYAJE.
Ufunguo ni shauku ya kiu Zaburi 42:1-2,3 inapatikana wapi Zaburi 42:5,11 kwenye nafsi Zaburi 63:1-11;66: 1-7, Mithali 16:3, Marko 12:30 kusifu kunaweza kuwa;-
KUSIFU KWA KUTUMIA SAUTI
·         Kinywa change kitazinena sifa za Bwana Zaburi Zaburi 145:21.
·         Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai,midomo yangu itakusifu (Zaburi 63:3
·         Mpigie Mungu kelele za shangwe,nchi yote,imbeni utukufu wa jina lake. (Zaburi 66: 1-2)
·         Mpigieni Bwana vigelegele. (Zaburi 33:1a)  
KUSIFU KWA VITENDO.
·         Enyi watu wote mpigieni makofi. Zaburi 47:1a
·         Msifuni kwa mvumo wa baragumu,msifuni kwa kinanda na kinubi msifuni kwa matari na kucheza msifuni kwa zeze na filimbi,msifuni kwa matoazi yaliayo,msifuni kwa matoazi yavumayo sana. (Zaburi 150:3-5)
·         Kwa jina lako nitainua mikono yangu.(Zaburi 63:4)
·         Ndivyo Israeli wote walivyopandisha sanduku la agano la Bwana kwa shangwe na kwa saut ya tarumbeta,na kwa baragumu,na kwa matoazi, wakipiga kwa sauti kuu kwa vinanda na vinubi. Hata ikawa,sanduku la agano la Bwana lilipofika mjini kwa Daudi,Mikali binti Sauli akachungulia dirishani,akamwona mfalme Daudi, akicheza na kushangilia,akamdharau moyoni mwake.
MATENDO MBALIMBALI YA KUABUDU
·         Kushukuru kwa midomo yetu (kuimba au kusema kwa midomo yetu.
·         Kutenda mema ka kushirikina.
·         Kuanguka mbele za Bwana ili kunyenyekea.
·         Kupiga vyombo mbalimbali,
·         Shangwe na upigaji wa vyombo
·         Kuinua mikono.
·         Kupiga magoti mbele za Bwana
·         Kucheza kwa nguvu zote
·         Kwa kucheza.
·         Muziki na kucheza.
·         Makofi.
·         Kelele za shangwe
·         Kufanya mapenzi ya Bwana
·         Kwa kutoa matoleo(zaka)
·         Ukimya na mengine mengi.
·         Kutoa kwa moyo wa ukunjufu,upandacho ndicho utakachovuna.
·         Acheni mjue ya kuwa mimi ni Mungu,nitakuzwa katika mataifa,nitakuzwa katika nchi.
ILI UABUDU LAZIMA UWE NA SABABU.
1.      Mungu ni nani.
2.      Mungu amefanya nini.
3.      Kiini cha kuabudu(chanzo)Roho wa Mungu au neno la Mungu.
4.      Mwitikio(matokeo) lazima kuwe na udhihirisho udhihirisho huleta kusherehekea.
5.      Matokeo uwepo wa Mungu unaachiliwa(dhihirika) nguvu za Mungu zinaachilia.
6.      Ni lazima iwe kitu unachokifanya sio unachofanyiwa. Ikiwa hivyo hakuna atakayetoka bila kuguswa maana amejihudhurisha mbele za Bwana binafsi. Tunafanya hivyo kwa kushangaa jinsi alivyotuumba na anavyotutendea. Mungu anatafuta watu watakaofungulia (SHEKINA) utukufu na nguvu zake ili zitiririke,Yeye ni kama ngombe anaelia kwa kujaa maziwa akamuliwe.
Zaburi 139:1-18 kwa kujipendekeza kwake Zaburi 139:21-22 tukisema Baba nakupenda sina baba mwingine aliye mzuri kama wewe **(BABA UWE MFANO MZURI,ILI PICHA NZURI IWE). Naye atakwambia nakupenda mwanangu hata bila kikomo Zaburi 45:1-7,17. Ndio maana shetani anapiga vita ushirika huu. Isaya 49: 15-16
MATOKEO YA KUABUDU.
·         Zakaria aliguswa. Luka 1:18-20
·         Sifa na kuabudu katika roho na kweli. 1nyakati 16:1-36
Azimia kuthamini(kuabudu) utaona milango imefunguka Marko 16: 1-8 kuna nguvu za ajabu sana Matendo 16:25-34 Paulo na Sila. Kuna pendo la ajabu,uponyaji,wokovu,Luka 7:36-50 mwanamke Malaya. Kuna utukufu wa Mungu(nguvu,fahari yake,uweza wake,uzuri wake n.k) Ufunuo 7:9-12.kuna utakaso,utakatifu Isaya 6:1-7. Kuna kumfahamu Mungu 2Nyakati 20:14-30 Mungu hupata fahari yake(utashi wake) Ezekieli 28:11-15
KUABUDU.
1.      Katika kamusi ya kiyunani LATREIA kumtolea Mungu (sadaka) Warumi 12:1,Waebrania 9:6 Kumtumikia kwa hiari kama mtumishi AU PROSKYREA ni kujinyenyekesha kwa kujitoa,kuinama kwa hiari. Ni lile tendo la unyenyekevu linaloonyeshwa na mtumwa kwa Bwana wake. Tendo la kujishusha kwa nia ya kumtanguliza Bwana wake kwa kumwonyesha kuwa undani wa mawazo yaliyoelekezwa kwa Mungu ili kuthibitisha ukweli unaogusa uhusiano wetu na Mungu kwa jinsi tunavyomjua,mhisi au kumsikia,ili uwepo wake utiririke katika maisha yetu. Kwa kulisha roho na nafsi zetu zielekee katika utakatifu na uwepo wa Mungu Zaburi 42:1-2 ili tuuone uzuri wake.
2.      Neno abudu au sujudu maana yake ni;- A: PENDA MNO au BUSU.wimbo uliobora 5:2a Bibi arusi,Bwana  arusi, :3-4 Bibi arusi anafurahia lakini anamizaha, :5-6 matokeo ya mizaha,Aliondoka kwa sababu hapendi mizaha,(ndio maana watu wanaimba “Usinipite mwokozi,unapozuru wengine,usiinipite”). :8 Mwelezeni naugua kwa mapenzi. (nimetekewa naye,mawazo yangu yako,yawe YEYE ni wa kwanza daima. 2Nyakati 20:5-19 Mungu anaupenda moyo(nafsi) inayochemka au kutokota kwa mapenzi ya thati yenye shauku



B. KUSALIMU KWA KUINAMA.
Kujitolea kumpenda kwa hiari, na kujinyenyekesha kwa kuyaweka maisha yetu chini ya utawala wake,na kukubali kumwachia ayaongoze atakavyo Zaburi 119:18-24
3.      Ni kuruhusu nguvu za Mungu zitiririke kati yetu Zaburi 63:1-11,kwa kuogelea katika uwepo wake) Zaburi 63:1-11. Kuabudu ni kufungua ukweli wa moyo wako wa uhusiano wako ulionao na Mungu wako,huku ukithibitisha kwa vitendo kwa kuruhusu uwepo wa Mungu utiririke katika maisha yako nawe upate kuogelea katika undani wa mawazo yaliyoelekezwa kwa Mungu. Chochea dhamiri katika utakatifu wa Mungu lisha nafsi kwa ukweli wa Mungu kwa kuunganisha mawazo yako (fikara) zako katika uzuri wa Mungu. Toa utashi wako uwe kwa ajili ya kusudi la Mungu.(Yahweh). Kumbukumbu la torati 6:5 Nawe mpende, Bwana Mungu wako, kwa moyo wako wote,na kwa roho yako yote,na kwa nguvu zako zote.
Ina maana kutumia vyote tulivyo navyo kwa utashi wa uhiyari wetu kumwelekezea Mungu mioyo yetu,akili zetu,nguvu zetu ili ziwe kwa kujishughulisha kwa ajili yake,na huku tukiruhusu maisha yetu yatawaliwe na Roho wake mtakatifu atuongoze katika kutukamilisha katika makusudi ya tabia za kiungu na mpango wa Mungu katika maisha yetu. Na hii ndiyo maana halisi ya kumcha Mungu. (kumbukumbu la Torati 10:12) kumhofu na kumuheshimu na kuwa makini kwa mwenyeenzi aliyetukuka.


TUNAHUSISHA NINI KATIKA KUMWABUDU MUNGU.
Kuabudu Mungu kunahusisha vitu vitatu ambavyo ndivyo ukamilifu wa mtu,navyo ni moyo,roho na mwili.
MOYO:- Ni nafsi  - imebeba hisia (ufahamu wa hofu,kupenda),utashi,shauku katika Moyo(Nafsi) kuna uhiyari wetu unaoweza kutoa sadaka tatu;-
                        (i ). Kumwabudu Mungu kwa midomo yetu,Waebrania 13:15. Kumbariki
                               Bwana,Kumshuhudia,kumshukuru,kumwimbia.
                        (ii). Kujitoa, (charity) kuwasaidia wengine Math.25:31-46,1yohana 4:20
                         (iii) Miili yetu (Dhabihu iliyo hai) Warumi 12:1 Basi ndugu zangu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai,takatifu ya kumpendeza Mungu ndiyo ibaada yenu yenye maana 1nyakati  16:29 ,Ufunuo 14:1-7,5:8 Marko 16:1-8. 1
Kuanzia hapo ndipo kuna kucheza,kusujudu,kuinua mikono,n.k. Mathayo 15:8-9 mioyo iko mbali.
Mathayo 2:2 tumekuja kumsujudia,(kumbusu mtoto) kwa hiari,si kwa kusukumwa: 11b wakafungua hazina zao. Isaya 26:8-9  Zaburi 63:1-6, Wimbo ulio bora 3:1, Zaburi 34:1-11 sehemu hii ndiyo inahusika kujihudhulisha mbele za Mungu Ebrania 4:16. Basi na tukiendee(tukikaribie) kiti cha neema kwa ujasiri,kwa imani pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu. ABEL (Mwanzo 4:4) Wimbo ulio bora Usiku kucha kitandani nalikutafuta mpendwa wa nafsi yangu, Moyo unachemka (tokota). Hisia zote ziko kwake ampendaye. Zaburi 42:1-4 shauku katika nafsi.
Zaburi 35:9 Na nafsi yangu itamfurahia Bwana. Hapo ndipo panapotakiwa kumwabudu Baba katika kweli. Ingia katika chumba chako cha ndani,ujihudhurishe mbele za Baba yako (fika,jipeleke),kwa hisia zako mawazo yako yamtafakari Mungu aliyeko sirini,atakuwepo hapohapo. Mathayo 6:6 ndivyo Ayubu1:6 Alimwona Mungu tu, na Mungu alijishughulisha na maadui zake. Jisahau nafsi yako ukamwaze yeye tu.
ROHO. Ni uhai wa mtu.(uzima wa Mungu ndani mwetu) mahala hapa ndipo penye kifo cha kiroho na kimwili,pia hapa ndipo mtu huzaliwa mara ya pili kwa njia ya Yesu Kristo na kuwa kiumbe kipya chenye uzima na kujazwa Roho Mtakatifu wa Mungu. Kuabudu katika roho ni kubudu kama malaika, malaika hawana NAFSI bali wana ROHO, wao huabudu kwa maelekezo ya utaratibu ulioandaliwa na Mungu. Luka 2:13-14,7:16,Ufunuo 4:8,11. Kuabudu kwetu katika roho hutokea wakati roho zetu zinapoguswa na Roho wa Mungu,ndipo hisia zetu hutawaliwa na hisia zitokazo kwa Mungu mwenyewe. Na mpango wote wa kuabudu hutawaliwa na utaratibu wa uongozi wa Roho Mtakatifu. Yohana 4:24 Mungu ni Roho wamwabuduo halisi wamwabudu katika roho.
MWILI. (NGUVU), Zaburi 95:6 mwili hutenda matendo yanayohudhihirisha hisia zilizo jaza roho na mioyo yetu. Kuabudu ni kitu kinachoonekana kwa matendo.1nyakati 16:29 mpeni mwenyezi Mungu heshima ya utukufu wa jina lake,leteni dhabihu na kuingia nyumbani mwake, mwabuduni mwenyezi Mungu patakatifu ni pake. Ufunuo 4:9-11 wanampa utukufu na heshima,
Tusimwabudu Mungu kama vile tumelazimishwa na sheria,bali tumwabudu kwa kutaka kwa utashi wetu kwa sababu tunataka kumwabudu tunayempenda sana tumetekewa naye (akili zetu 

zinamuwaza yeye tu). Tufungamane naye uso kwa uso tumbusu tuwajibike kwa kumwonyesha shauku yetu kwake toka katika kilindi cha undani wa mioyo yetu. Hicho ndicho anachokitaka. Matendo 13:22. Nimemwona Daudi mtoto wa Yese ni mtu anayepatana na moyo wangu,mtu ambaye atayatimiza yale yote ninayotaka kuyatenda.1Samweli 13:14,16:12-13 Aketiye mahali pa siri pake aliye juu atakaa katika uvuli wake Mwenyezi. 1Nyakati 28:9 Nawe Sulemani mwanangu,mjue Mungu wa baba yako,ukamtumikie kwa moyo mkamilifu,na kwa nia ya kumkubali,kwa kuwa BWANA hutafutatafuta mioyo yote,na kuyatambua mawazo yote ya fikra,ukimtafuta,ataonekana nawe,ukimwacha,atakutupa milele.
Ushauri wa Daudi kwa mwanawe Sulemani ni kwamba mjue Mungu wa baba yako, utakapomjua,mtumikie kwa hiari kwa moyo wa kweli. Maana Bwana huchunguza na kuyajua mawazo yote bila kificho ushauri huu ungekuwa ni ushauri wa kila mzazi kwa mwanawe,maana uhusiano wetu na Mungu na kupata mafunuo zaidi ya kumjua yeye kumefungwa katika kumwabudu yeye.
Hosea 6:3 Nasi na tujue,naam,tuendelee kumjua BWANA,kutokea kwake ni yakini kama asubuhi,naye atatujilia kama mvua,kama mvua ya vuli iinyeshayo nchi.
Yeremia 9:23-24 BWANA asema hivi,mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake,wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake,bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii,ya kwamba ananifahamu mimi,na kunijua ya kuwa mimi ni Bwana,itendaye wema,na hukumu,na haki, katika nchi,maana mimi napendezwa na mambo hayo,asema BWANA. Tunamwabudu Mungu kwa mali zetu pia,Kumbukumbu 12:6, 14:22-29 unapata maana ya jinsi Mungu anavyokusudia kutumia matoleo yetu. Kwa nini umwabudu Mungu kwa mali? Malaki 3:6-18 Mathayo 10:40,25:34-40 huku ndiko kumtumikia Bwana Mungu na kumwelekea kwa unyenyekevu. Zakaria 7:4-7 mstari 8-10 funga inayokubalika.1Yohana 4:20-21 utoshelevu wa kumpenda Mungu,pawepo na juhudi za kupendana ili Mungu awe katikati yetu Efeso 4:25-32. Kila mtu afanye juhudi apate cha kutoa,kumtunza Bwana. Maana panapokuwa hakuna mhitaji furaha huongezeka, Na Mungu hufurahia watoto wake naye atawavuta wengi ili waone upendo halisi. Matendo 2:43-47, 4:25 mali zetu ni mali zake BWANA.
WAKATI GANI WA KUABUDU,KUSIFU?
Zaburi 113:1-9 Toka maawio ya jua hata na machweo yake Jina la Bwana husifiwa
Zaburi 22:3  uketiye juu ya sifa za Israel.
Zaburi 22:22 wakati tukiwa na ndugu zetu na katika makusanyiko.
Zaburi 34:1-3 kila wakati
Zaburi 40:1-10 wakati wote kutangaza matendo yake makuu na uaminifu wake
Zaburi 104:33-35 wakati wote wa maisha yetu (milele).
Zaburi 105:1-4 siku zote tumtake na kutafakari uzuri wake.
Zaburi 119:164 mara saba kwa siku
Zaburi 147:1 maana ni vyema kumsifu wakati wote
Kolosai  3:15-17 na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu,ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja tena iweni watu wa shukrani. Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote,mkifundishana na kuonyana kwa zaburi,na nyimbo,na tenzi za rohoni,huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfnyalo,kwa neno au kwa tendo,fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu,mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.

KWA NINI TUNAABUDU.
Zaburi 22:3 Bwana hukaa juu ya sifa za watu wake
Zaburi 92:1-2 Ni neno jema kushukuru na kutangaza.
Kutoka 20:1-6 Tumeamriwa,kwa sababu ni yeye peke yake ni mtakatifu.
Kumbukumbu 10:12 Na sasa,Israel,(weka jina lako hapa) Bwana, Mungu wako,anataka nini kwako,ila Umche Bwana Mungu wako,na kwenda katika njia zake zote,na kumpenda na kumtumikia Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote” Kumwabudu ndilo tunda la pekee limwendealo Mungu,kazi zingine ni kwa ajili yetu wenyewe. 2Nyakati 5:13-14.
WAONGOZA IBAADA
Kuongoa ibada ni jukumu zito linalohitaji unyenyekevu na usikivu wa hali ya juu sana kwa sababu unachukua jukumu la kuwa kiunganisho kati ya Mungu na watu. Ukikosea kidogo tu,basi umeharibu maana yote ya Mungu kuabudiwa. Unajukumu la kuhakikisha unatimiza makusudi ya Mungu kwa watu wake. Hivyo kabla hujaabudisha watu lazima wewe umwabudu Mungu, uwe mahala ambapo unataka kuwapeleka watu,uijue njia sahihi ya kufika unapotaka kuwapeleka watu,unaabudu nao waone na kuiga sio unawaongoza. Fikiri juu  yake,mwelekezee mawazo yako yeye, hisia zako zishikwe kwake.

Kuongoza ibada ni taaluma jifunze sana na ni huduma ya Rohoni,mtegemee Mungu akuwezeshe usiyoyaweza.(upako ni wake na ni yeye pekee awezayekupaka) 2Wafalme 3:15-20 ila sasa niletee mpiga kinanda.Anatabiri baada ya kinanda kumwalika Roho wa Bwana akashuka na ujumbe kwa nabii. Inakubidi kiongozi wa ibada uwe mnyenyekevu na utii kwa Mungu lakini pia unyenyekevu na utii kwa uongozi wa kanisa. Unyenyekevu,heshima na upendo kwa watu uaowaongoza,huku ukijua kuwa msingi na huduma na vipawa mbalimbali vya Mungu hutiririka kwa mtu aliyefurika upendo kwa Mungu na watu pia. Ukitaka ufanikiwe katika huduma hii ni lazima hudama yako ijengwe katika msingi wa upendo. 1Nyakati 16 Tunaona Mungu anawaita watu maalumu kuongoza,kupiga kuimba katika kwaya kwa niaba ya ndugu
2Nyakati 5. Maelekezo jinsi huduma ya kweli ya kuabudu inavyofanya uwepo wa Mungu uonekane na Mungu kujulikana kwa nguvu na ajabu.
UWE NA MATAYARISHO YAKO BINAFSI
Lazima uwe mahala ambapo unataka kuwapeleka watu. Ujiandae kuteka hisia za watu ambazo zina matatizo,zimejaa michezo ya TV,vyakul Wachumba wa kike au wa kiume n.k.
a.      Kujitakasa tafuta uhusiano na Mungu kabla hujaenda kwa watu ili uwende na Mungu.
b.      Mwombe Roho mtakatifu mwelekeo, wakati unapanga nyimbo akupe thyme inayoeleweka.
c.       Fanyia mazoezi nyimbo ulizochagua huku ukizitafakari maana zake kwa undani.
d.      Jiombee mwenyewe pamoja na nyimbo zako mpate upako.
e.      Jiandae kuteka hisia za watu zimwelekee Mungu,kwa maneno ya Mungu ambayo atakupa nawe uyaamini.
f.        Wakati wa ibada,uwe makini katika mawasiliano na watu unaowaongoza, hakikisha wanakusikia vizuri,nenda nao hatua kwa hatua kwa kutumia lugha nzuri ya kujenga na kutia moyo,maneno ya kinabii (tabiri yale unayoyatarajia).
g.      Uwe na ujasiri kuwa unaijua njia unayowaelekeza waiendee na uwe mwepesi kutambua Roho wa Mungu anapoanza kufanya kazi mwachie aendelee kuwahudumia watu,hili ndilo kusudi la kuabudu(tuogelee katika Bahari ya upendo wa Roho mtakatifu)
h.      Uwe tayari kutumika jinsi ulivyo bila kujaribiwa kuwa kama fulani. Mungu amekuchagua wewe jinsi ulivyo,mtegemee Roho mtakatifu,huu ni mwito mkuu na wa heshima yeye atakuongoza mtegemee.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni