Ijumaa, 10 Agosti 2012

UFUNUO WA YOHANA



UTANGULIZI  WA MWANDISHI

1.   Yohana mwenyewe mwanafunzi aliyependwa na Yesu, nabii (Ufu. 22:9 Naye akaniambia, Angalia usifanye hivi; mimi ni mjoli wako, na wa ndugu zako manabii, na wa wale wayashikao maneno ya kitabu hiki. Msujudie Mungu.) Kiongozi wa makanisa ya Asia Minor (Ufu. 2-3) mmoja wa wanafunzi wa awali wa bwana Yesu. Soma Ufu. 1:4, Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; na zitokazo kwa roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi; 1:9 Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu. Ufu. 22:8 Nami Yohana ndimi niliyeyasikia na kuyaona mambo hayo. Na hapo nilipoyasikia na kuayona nalianguka mbele ya miguu ya malaika yule mwenye kunionyesha hayo.

        Jadi inasema kwamba Yohana alikaa pale Efeso akisimamia makanisa 7 ya Asia Minor na halafu alipelekwa uhamishoni katika kisiwa cha Patmos, kufanya kazi katika machimbo ya migodi huko.

2.     Kwa miaka 30 ya kwanza tangu kanisa lianze mfalme wa Urumi alivumilia Ukristo ukienezwa. Hatimaye mfalme Nero aliona utofauti kati ya dini ya Kiyahudi na Ukristo. Kwa hiyo dini ya Kiyahadi, ilitambuliwa hadi kiserikali,hali Ukristo haukutambuliwa hadi wakati wa mfalme Konstantino (306 – 337 AD).

3.     Yohana alipelekwa Patmos wakati wa mfalme Domitian, (94-95 AD). Baada ya kifo cha Domitian, (AD 96) aliruhusiwa na mfalme Trajani kurudi tena Efeso na yasemekana kuwa hapo ndipo aliandika kitabu cha Ufunuo. Wataalamu wengi wa maandiko hata hivyo bado wana sadiki kuwa kitabu hiki kiliandikwa katika kisiwa cha Patmos.

KUTAFASIRI UFUNUO

Ziko aina 4 za kutafasiri kitabu cha Ufunuo
1.     Ufunuo ni mafundisho matupu: (Non – literal or allegorical).       

        Maelezo haya yalianza katika shule ya Theologia ya Alexandria, na yanaelezea kwamba kitabu hiki ni mafumbo ya ndani sana ya kiroho. Hakuna tukio la kawaida lililotokea ama litakalotokea, bali Ufunuo ni mifano tu ya mambo magumu na mfambo ya Kiroho. Ni picha ya vita ya kiroho kati ya ubaya na wema katika ulimwengu war oho.

2.     Ufunuo ni mambo yaliyoshapita (Preterest.)
        Mambo haya ya Ufunuo ni rekodi ya yale ambayo yalishatokea katika Historia ya kanisa, hasa milango ya 5 – 11 yasemekana kweli z ushindi wa kanisa dhidi ya dini ya Kiyahudi, (Judaism). Mateso nadhiki kuu wanasema ni yale ya Nero na Domitian na kitabu chote kilikamilika wakati wa Konstantino, AD 312.

        Mtindo huu wa maelezo unaharibu mambo yote yajayo, nayo huonekana kuwa hayana maana, maana yamekwisha tokea.

3.     Fasiri ya Kihistoria: (Historical).
        Hapa ufunuo unachukuliwa kuwa ndiyo jumla yote ya Historia ya kanisa na utimilifu wake ni kurudi kwake Yesu mara ya pili. Joakim, msomi wa kanisa Katoriki, ndiye aliyeanza nadharia hii na alimhusisha Baba Mtakatifu kama yule mnyama wa Ufunuo Mlango wa 13.

4.     Nadharia ya baadaye: (Futuzist.)
        Katika nadharia hii matukio yote kuanzia Ufunuo mlango 4, yanachukuliwa kuwa yanatokea baadaye, kwa jinsi ya kawaida kabisa, halisi, kama ambavyo Ufunuo kinasema. Waamini pia kuwa kutakuwepo unyakuo kabla ya dhiki kuu. Nadharia hii ndiyo inayokubalika na wengi.

        Matumizi ya alama na mifano katika Ufunuo

        Baadhi ya mifano na alama katika Ufunuo lazima zilichukuliwa kuwa kama zilivyo isipokuwa zingine zifasiliwe kufuatana na maana zake mahali pengine katika maandiko. Namba zinazo tumika mara nyingi ni                 7 = mara 54 (Ukamilifu)
        12 = 10 na 4 na 6 = Namba ya mwanadamu.
        12 = Serikali ya mitume.
10 = Amri 10.
Namba 666 inaonyesha
6 = Uanadamu – yule mnyama alikuwa mwanadamu (Ufu. 13)
666 = Ni utatu wa shetani yaani
-       Shetani
-       Nabii wa uongo.                            
-       Mnyama.

JINSI YA KUKIELEWA KITABU CHA UFUNUO

1.     Chukua kila neno kumaanisha kama linavyosema, mpaka hapo inapotokea kwamba neno hilo likilinganishwa na maneno ya mistari ya awali na hiyo inafuaa, halina maana inayeeleweka. Hapo tafuta fasiri ya kibiblia tokana na maandiko ya Biblia nzima.

2.     Lazima kuelewa kama tukio linatokea duniani, ama mbinguni.

3.     Kumbuka kuwa Ufunuo hakijaandikwa kwa utaratibu wa matukio yaliyotokea kama yalivyoandikwa (Chronologically).

        Kumbuka:-
        a.     Ni Ufunuo wa Bwana Yesu Kristo. Ufu. 1:1 Ufunuo wa Yesu
Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatumwa kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana;

b.           Kuonyesha watumwa wake. Ufu. 1:1.

c.      Heri wasomao, wasikiao, na kuyashika Ufu. 1:3. Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu.

c.           Ni kwa wakati uliopita, wa sasa, ujao, Ufu. 1:19 Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, nay ale yatakayokuwa baada ya hayo.

YALIYOMO.(OUTLINE)

a.           Mambo aliyoyaona Yohana Ufu. 1:1-19.
b.           Kanisa wakati huu. Ufu. Mlango 2-3.
c.           Hali ya mambo baada ya kanisa kukamilika, mlango 4 – 22.


PICHA YA MHITASARI DHIKI KUU

KUNYAKULIWA  KURUDI NA UTUKUFU
 


Hukumu za mihuri  Hukumu za Tarumbeta                        Hukumu za vitasa
Ufu.6                     Ufu. 8,9                                             Ufu. 15, 16


½ ya kwanza ya dhiki kuu                                          ½ ya pili ya dhiki kuu


Mambo uliyoyaona
Mlango wa 1:1-8. Salamu na utangulizi

1:1    Ufunuo wa Yesu Kristo = uliotolewa na Bwana Yesu Kristo mwenyewe. Yatakuwako upesi = Itatokea ghafla, kuja kwake.

1:7.   Kiini cha kitabu cha Ufunuo.
        - Kama alivyoenda ndivyo atakavyo kuja.

        Luka 21:27 Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi.

        Mathayo 24: 29-30. Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; 30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.
-Kila jicho (wote watamwona) na kumwombolezea.

Jumla. Hapa Kristo anaonekana kuwa yeye ndiyo chanzo cha ufunuo huu. Ndiye Njia ya ushuhuda kwa neno lake, anaahidi baraka kwa neno lake
 lililofunuliwa. Ni shahidi mwaminifu. Mtawala wa wafalme wote wa dunia. Yeye anasamehe dhambi zote na kutufanya makuhani na wafalme, naye hampi utukufu wake mwingine. Atarudi kwa utukufu mkubwa na nguvu nyingi.
MAONO YA KRISTO 1:9 – 16.

“Yale uliyoyaona”
1:9. Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushirikia pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu. Mtume Yohana, anajiita mshiriki wa dhiki na mateso yale yaliyotokea na mtawala wa Kirumi – Nero na Domitian, wanadamu walijaribu kuwazuia wakristo wasihudumu, kamwe hawakumzuia Roho Mtakatifu asiende kazi, Kisiwani Patmo, Yohana anapewa ufunuo mkuwa.

1:10. Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu. Nalikuwa katika Roho “siku ya Bwana” maana yake alichukuliwa katika Roho mpaka siku za mbele ambapo Bwana atafanya hayo aliyomwonyesha.

Kristo alivyoonekana na Yohana 1:13-16.

1.     Kama mwana wa adamu linganisha Dan. 7:13 Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliyemfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbinguni akamkaribia huyo mzee wa siku, akamleta karibu naye.

2.     Vazi alilovaa kama kuhani mkuu alihudumu hekalini.

3.     Mshipi wa dhahabu Alama ya nguvu mamlaka, mshipi uliovaliwa na wenye mamlaka.
4.     Nywele nyeupe kama sufi nyeupe – Hekima na usafi (utakatifu) wake – kasha yukijana bado. Dan 7:9-13. Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama thuluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. 10 Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na

vitabu vikafunuliwa. 11 Nikatazama wakati huo; kwa sababu ya sauti ya yale maneno makubwa iliyoyasema ile pembe;
nalitazama hata mnyama yule akauawa. Mwili wake ukaharibiwa, akatolewa ateketezwe kwa moto. 12 Na kwa habari za wale wanyama wengine, walinyang’anywa mamlaka yao; walakini maisha yao yalidumishwa kwa wakati na majira. 13 Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa usiku, wakamleta karibu naye.

5.     Macho kama mwali wa moto; 1:14. Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa. Kuonyesha kusudi lake la kutoridhika na hali ya yale makanisa 7. 1 Kor 3:13. Maana siku ile itadhihirishwa, kwa kuwa ni ya namna gain.


6.     Miguu – shaba iliyosuguliwa sana – hukumu kwa ajili ya dhambi katika makanisa haya.

7.     Sauti – kama ya maji mengi siku ya hukumu sauti ya Yesu atasikika na kila mtu ingawa leo watu hawataki kuisikia sauti yake tuhubiriyo.

8.     Nyota 7 mkono wa kuume mahali pa utawala na mamlaka. Malaika wa makanisa 7 Hapa “malaika” maana yake mjumbe, kwa hiyo ingeweza kumaanisha wachungaji wa makanisa hayo.

9.     Upanga mkali – makali kuwili katika kinywa chake upanga huu “Romphaia” unawakilisha upanga wenye hukumu ya mateso makali, situ kama ule wa Ebrania 4:12 Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viuongo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Unafunua imani ya mtu. Mpinga Kristo atahukumiwa na Yesu arudipo mara ya 2.

10.    Uso wake – kama jua liking’aa. Kristo kama Mungu 100% soma mathayo 17 na yohana 3:2 Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa


Mungu yu pamoja naya.

Matokeo ya maono hayo. 1:17-19

        Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akawaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, 18 na aliye hai, nami nalikuwa nimekufa na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. 19 Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, nay ale yatayokuwa baada ya hayo.

        Yohana aliyezoea kulala kifuani pa Bwana Yesu akiwa hapa duniani sasa anaanguka na kusujudu.

        Soma. Abrahamu. Mwanzo. 17:3.
        Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia akasema,

        Dan. 8:17 Basi alipokaribia mahali niliposimama; nami naliogopa alipokaribia, nikaanguka kifudifudi; lakini aliniambia, Fahamu, Ee mwanadamu, kwa maana maono haya ni ya wakati wa mwisho.

        Ezek. 3:23. Basi, nikaondoka, nikaenda uwandaji, na tazama, utukufu wa Bwana ulisimama huko, kama utukufu ule niliouona karibu na mto Kebari; nami nikaanguka kifudifundi.

        Waamuzi 6:22-23 Gideoni akaona ya kuwa ni malaika wa Bwana; Gideon akasema, Ole wangu, Ee Bwana Mungu! Kwa kuwa nimemwona Bwana uso kwa uso. 23 Bwana akamwambia, Amani iwe pamoja nawe; usiogope; hutakufa.

        Luka. 1:13. Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia motto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana.

1:18-19
Kristo aliye mwenye funguo za kuzimu (Hades or Hell) (sio Jehanamu) (Gehena) kuzimu ambapo ni mahali roho za watu (wasioamini sasa, wote kale) huenda kabla ya ufufuo wa milele.

Mambo yaliyopo; makanisa 7  2:1-3 Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika;
Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu. 2 Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, nay a kuwa huwezi kuchukulia na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo; 3 tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka.

2:22 Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake.

Barua hizi ni kwa makanisa 7 yaliyokuwepo wakati wa Yohana, ambayo yaliwakilisha makanisa yote katika Historia ya kanisa.

Orodha ya makanisa 7.

1.     Efeso kanisa la kimitume 30 – 100 AD.
2.     Smirna kanisa la mateso 100 – 312 AD.
3.     Pergamo – kanisa lililochanganyika na uovu 312 – 606 AD.
4.     Thyatira – kanisa la kipagani 606 AD – 1520 AD.
5.     Sardis – kanisa lililokufa kabisa 1520 – 1750 AD.
6.     Philadelphia – kanisa lililopendwa na Kristo 1750 – 1900.
7.     Laodephia – kanisa vuguvugu. 1900 – sasa.

Kila barua katika hizi 7 ina mambo yafuatayo.

1.     Kanisa mhusika 5 Ahadi.
2.     Sifa (Commendation)
3.     Lawama (Condemnation).
4.     Ushauri (Exhostation).
5.     Ahadi.

1.     Efeso; 2:1-7 kanisa lisilo na upendo
Neno Efeso – A – kupendeka (desirable). Ni mji alipoishi Yohana mwenyewe. Mji Mkuu wa Jimbo la ……..palikuwepo Hekalu la Diana kanisa lililosimamishwa na Paulo katika ziara yake ya 3 ya umisionari, Mdo. 19. Timotheo, Pricilla, Aqinla na Yohana walikwisha kufanya uongozi katika kanisa hili.

a.     Sifa
Aliwasifu kwa kazi (matendo) uvumilivu, na kwa kuwakataa wanikolai na kuwachukia kama Bwana alivyowachukia. Nikolai – dhehebu ambalo lilizuka maelezo yake yanatatanisha tazama lilijihusisha na matendo machafu. Walichanganya Ukristo na sikukuu za kipagani na mambo ya mapenzi ya kipagani. Yasemekana kwa mwanzilishi alikuwa “Nikolai” kutoka Antiokia.

b.           Lawama.
Waliacha (hawakupoteza) upendo wa kwanza kwa kutojali kutotilia maanani.

c.           Ushauri
Warudi hadi walipouachia upendo.
(1)        Watubu
(2)        Warudie upendo wao wa awali.

d.     Ahadi
        Washindao watakula mti wa uzima.

e.     Historia ya kanisa la Mitume (Efeso). A.D 30 – A.D 100.
Lililopendwa sana wakristo wengi walikuwa Wayahudi, walihubiri Injili iliyo hai pande zote za dunia ya wakati ule. Warumi. 16:26. Ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, ili waitii Imani. 1 Kor 1:23 bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibishwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi; Wayahudi watakuja kuhubiri tena Injili hai pande zote duniani tena, wakati wa dhiki kuu (Ufu.7).

2.     Kanisa la Sminra; kanisa la mateso; 2:8-11
a.     Sminra maili kama 5 hivi kaskazini mwa Efeso. Bandari muhimu, Hekalu la ukumbusho wa mfalme wa kirumi Tiberius lilisimamishwa hapo. Hapo palikuwepo Wayahudi wengi ambao walikuwa mstari wambele katika kuwatesa wakristo. Smminra. Maana yake “chungu ama uchungu”

b.     Barua iliyoandikwa kwa malaika wa kanisa hili anaonyesha kuwa wengi wa wakristo wa kanisa hili watateswa sana. Ila Yesu anawaahidi kuwa yeye Yesu ndiye ambaye alikufa, naye yu hai,

hivyo hata wakifa, wanao ufufuo wa heri.
c.      Sifa.
        Kanisa hili ni maskini kwa nje, lakini ndani ni tajiri sana Polycapo kiongozi wa kanisa hili, aliuawa mwaka 168 AD kabla hajafa alisema maneno haya miaka yote 80 hii nimemitumikia naye hakuacha kuwa mwaminifu kwangu, nimkane vipi sasa, Bwana wangu na mwokozi wangu, akachomwa hafi kufa ndani ya mafuta yachemkayo.

d.     Ushauri.
        Usiogope mambo haya ya mateso uwemwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima. Yakobo 1:12. Heri mtu astahimiliye majaribu, kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao. Na majaribu siku 10 yanawakilisha wafalme 10 wa kirumi waliotesa kanisa.

1.     Nero 54-96 AD. Paulo akikatwa kichwa Petrol kusulubiwa.
2.     Domitian 81 – 96 AD. Yohana kupelekwa patmo.
3.     Trajan 98 – 117 AD. Ignatus kuchomwa moto.
4.     Marcus Awelin – 138 – 163. Polycap kuchemshwa ndani ya mafuta.
5.     Septimius sevens – 222 – 235
6.     Maximinius – 235 – 238.
7.     Decius – 249 – 251.
8.     Valerian – 253 – 260.
9.     Awelian – 270 – 275.
10.    Diocletian – 284 – 305.
Aliyetesa kanisa kuliko wafalme wote wa Rumi. Alijaribu kila njia kufuta kabisa biblia na Ukristo. Karne za 2 na 3 wakristo waliletwa kwenye uwanja wa maonyesho Rumi ili waliwe na walionekana simba wenye njaa mbele ya maelfu wa watazamaji. Wengi walisulubishwa wengine walifunikwa ngozi za wanyama mbweha wa porini na kuteswa hadi kufa na walipakwa lami na kuwashwa moto ili wawe taa za barabarani, walichemshwa katika mafuta, kama Polycap wa Smirna. Yasemekana wakristo 5,000,000 waliuawa kipindi cha kanisa la mateso. Ila katika mateso hya, kanisa liliongezeka sana.

3.     Kwa kanisa la Pergamo 2:12-17
        Kanisa lililovumilia uovu uingie ndani (lililoonelewa na serikali).

a.           (1)    Lilikuwa kama maili 45 kaskazini mwa Smirna.

(2)    Pergamo maana yake “Iliyoinuka” pia maana yake “ndoa” mwingi ulioitishwa chini ya utawala wa Kirumi 133 BC. Ulikuwa mji tajiri wenye mahekalu mengi ya kipagani.

b.           Sifa.
Kuendelea kusimama katikati ya kiti cha shetani hapa kuabudu mfalme wa Kirumi ama miungu wa Kiyunani, kama Zeus, katika madhabahu yake huko Acropolis, ama yote matatu.

        c.      Lawama
Habari za Baalamu na Baaki na jinsi Balaam alivyomshauri baalaki kunajisi Israel kwa miungu yao na uzinzi. Fundisho hili linaonyesha kuabudu ibada za kidunia kuingia kanisani soma 2 Petro. 1:15. Walakini nitajitahidi, kwamba kila wakati baada ya kufariki wangu mpate kuyakumbuka mambo hayo.

Yuda 1:11 Ole wao! Kwa sababu walikwenda katika njia ya Kaini, na kulifuata kosa la Balaamu pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika maasi ya Kora.

        d.     Ushauri 2:16
Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu. Toba kwanza, onyo, hukumu kwa kutumia neon la Mungu.

        e.     Ahadi
                Ashindaye atapewa mana iliyofichwa – Kristo mkate utoshao.
(1)        Jiwe jeupe – alipewa kiongozi wa kikosi kilichoshinda vita.
(2)        Alipewa mtumwa ambaye muda wake ulikwisha na sasa anafunguliwa.
(3)        Alipewa mtu aliyeshinda kesi.
(4)        Lilitolewa kama alama ya Agano (convenant) baina ya watu wawili kwa ushahidi, jiwe moja liligawanywa vipande viwili.

f.            Historia
Shetani alitambua tokana na historia ya Smirna kuwa mateso yalifanya kanisa liongezeke kiroho na kiidadi.

Konstantino aliurithi Dercletian kama mfalme wa Rumi. Yasemekana aliona ishara ya moto wa msalaba angani na maneno yakasema kwa alama hii “utashinda” Alifanikiwa kumshinda Galerius na kuwa mfalme pekee. Aliwaita maaskofu wa kikristo wamweleze dini yao. Aliipokea na kutangaza kuwa atailetea. Ila Konstantino mwenyewe hakuokoka kwa moyo wake. Alimwamuru Ausebio Askou wa Rumi kusimamia uandikaji wa nakala 50 za maandiko matakatifu. 312 AD. Ukristo ulitangaza kama dini ya serikali ya Rumi na Kostantino. Serikali ilitoa fedha kuendesha kanisa.
Viongozi wa dini ya kipagani waliruhusiwa na maofisa wa kikristo kuingia na kujiunga na makanisa. Ili kumpendeza mfalme, wakuu wa kanisa walihusika na jadi zilizolingana na zile za kipagani. Baraka ya kuondolewa matesoni iligeuka kuwa laana kuu. Upagani uliongezeka hatua kwa hatua kansiani, hata moto wa Uinjilisti ukafa.

Yafuatayo yalitokea kipindi hiki

1.     AD. 300 – Kuombea wafu.
2.     AD. 300 – Alama ya msalaba kutokana na Tau (T) ya Kikaldayo.
3.     AD. 375 – Kuabudu watakatifu na malaika.
4.     AD. 394 – Misa zinaanza.
5.     AD. 394 – Kuabudu bikra maria.
6.     AD. 500 – Mapadre kuowa tofauti na watu wenyewe wengine.
7.     AD. 526 – Kuwekwa wakfu.
8.     AD. 593 – Mafundisho ya Purgatio.
9.     AD. 600 – Ibada (misa) zote kuendeshwa kilatini.
10.    AD. 600 – Maombi yapitie kwa Maria

Kanisa hili lililelewa na serikari ya Kirumi na kuwa la Kirumi kuliko kuwa la Kikristo. Baraza la Nikea lilitokea mwka 325 AD. Katika kipindi hiki.

KANISA LA THIATIRA. 2:18-19.

1.     a.     Kanisa lenyewe 2:18
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana Wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.

Kama maili 35 kusini mashariki mwa Pengamo Koloni la Makendonia. Palifanyika biashara za sufu na pamba, na kutia rangi vitambaa. Yasemekana Lidia huenda ndiye aliyeleta Injili huko. Mdo. 18:14.

b.     Thiatira maana yake “dhabihu” isiyochoka” Huwakilisha kanisa la kipagani.

2.     SIFA
Aliwasifu kwa kuongeza matendo ya imani na upendo, huduma, uvumilivu.

3.     LAWAMA
Yezebeli. Soma 1 Waf 16:19 kwa sababu ya makosa aliyoyakosa, akifanya mabaya machoni pa BWANA, kwa kuiendea njia ya Yeroboamu na makosa yake aliyofanya akiwakosesha Israel.

1 Waf 19:2 Ndipo Yezebeli akampeleka Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao.

1 Waf 21:1-6. 2 Waf 9.
Hapa yasemekana alikuwa mke wa kiongozi wa kanisa la Thiatira. Aliingiza zinaa na kuabudu miungu. Mambo ya ndani ya shetani.

4.     AHADI
Ashindaye sehemu katika utawala wa Kristo nyota ya Asubuhi hapa ni (Yesu mwenyewe).

5.     HISTORIA
Kanisa hili lililetwa kipindi cha kanisa kiitwacho kipindi cha giza” Nuru yote ya Kristo katika kanisa sasa ilitoweka, na upagani ukamiliki. Hakuondolewa mpaka nyakati za uamsho.

YAFUATAYO YALIONGEZEKA KATIKA KANISA

1.     AD. 607 Boniface afanywa papa wa kwanza.
2.     AD. 709 Kubusu mguu wa papa.
3.     AD. 786 kuabudu sanamu na mabaki ya maiti za watu.
4.     AD. 850 Maji matakatifu kugunduliwa. n.k.

KWA KANISA LA SARDI 3:1-6 KANISA LILILOKUFA.

1.     a.     Kanisa lenyewe
Kama maili 30 kusini mwa Thiatira mji mkuu wa Lydea mji wa viwanda vya nguo, kutia rangi na biashara za lulu.

b.     Sardi maana yake “pumziko” ama “mabaki” “masalia”  liliwakilisha kanisa lililokufa.

2.     SIFA 3:4
Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.
Hakuna sifa, ila Bwana awajua wachache walio waaminifu hapo. Kanisa zima lilikufa.

3.     LAWAMA
a.     Kufa kwake – Mungu hadhihakiwi walioneakana wanajitahidi kwa nje tu, lakini walikufa kiroho.

b.     Hawakukamilika 3:2 Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.

4.     USHAURI 3:3
Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako.

a.           Kumbuka ulilopokea siku za awali.
b.           Kuangalia kuja kwa Bwana na kuwa tayari.

E.     AHADI
        Mavazi meupe kwa mwamini wa kweli katika kanisa hili ni alama ya
a.           Karamu.
b.           Ushindi.
c.           Utakatifu.
d.           Mbingu ya milele.

F.     HISTORIA
        Kanisa hili liliambiwa na Bwana kwamba limekufa kwasababu mbili
a.           Lilifanyika kanisa la serikali kwa hiyo mtu hakuwa na nafasi ya
kupata toba ya kweli na kumgeukia Yesu. Angalia tu ndani ya serikali.

b.     Makanisa ya uamsho hayakubadili jadi nyingi na mafundisho ya kanisa la Roma. Ubatizo wa watoto uliendelea. Kubatiza kwa kunyunyuzia kuliendelea n.k.

KWA KANISA LA FILADELFIA 3:7-13 KANISA LILILO NA UAMINIFU KWA KRISTO

1.     a.     Kanisa lenyewe.
                Kama maili 28 kusini mashariki kwa Sardis.
                Filadelfia maana yake “Upendo wa ndugu”
                Mji uliitwa hivyo kwa kumbukumbu ya mfalme “Attalus Philadephus”
                na kanisa la umissionari.

b.     Neno Philadephus linatajwa mara 6 katika vitabu vingine vya Agano jipya
(1)    Warumi 12:10 Kwa pendo la ndugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;

(2)    1 Thesalonike 4:9 Katika habari ya upendano, hamna haja niwaandikie; maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana

(3)    Waebrania 13:1 Upendano wa ndugu na udumu.


(4)    1 Petro 1:22 Mkisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo.

(5)      2 Petro 1:7 na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.

Mara ya saba nay a mwisho neon hili linatajwa katika Ufunuo 3:7
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga hapana afuguaye. Nayajua matendo yako.

2.     SIFA 3:8.
Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neon langu, wala hukulikana jna langu.

a.           Walizitumia nafasi wazi.
b.           Wana nguvu kidogo.
c.           Walitunza neon lake.
d.           Walijitenga na uovu wakawa waaminifu.

3.     LAWAMA. Hakuna

4.     MASHAURI. 3:11.
Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.
        Linda sana ulichonacho.

5.     AHADI. 3:9-13
9 Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya  miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda. 10 kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika sasa ya kujaribiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi. 11 Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa

taji yako. 12 Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika
hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya. 13 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

Ahadi 5 kwa kanisa hili.

a.           Maadui zao kutiishwa chini yao.
b.           Kanisa litakombolewa toka saa ya majaribu katika dunia yote.
c.           Bwana atarudi upesi (ghafla).
d.           Wateule wataheshimiwa.
e.           Watakatifu watapewa jina la Mungu wao.

6.     HISTORIA
        Kanisa lilianza 1750 na litaendelea hadi dhiki kuu.
Uamsho ulitokea Ulaya, Uingereza, hadi Amerika. Kanisa la umishonari wa kipentekoste lilianza.
William Garey, Adoniram Judson, David Livingstone, Jouathan Gofoth.

7.     SABABU ZA UAMUSHO HUU.
        a.     Biblia kufasiriwa kwa lugha za wenyeji.
        b.     Fundisho la kunyakuliwa kabla ya dhiki kuu.


KWA KANISA LA LAODIKIA. 3:14-21. KANISA VUGUVUGU

1.     KANISA LENYEWE
Kama maili 90 mashariki mwa Efeso mji uliowekwa Autiokus II naye akampa jina la Laodikia kwa heshima ya mkewe Laodike. Mji maarufu kwa nguo za sufu. Hakuna maandiko kuonyesha kama Paulo alifika kuhubiri Laodekia, ila anautaja katika Kol. 2:1 Maana nataka ninyi mjue jinsi ilivyo kuu juhudi yangu niliyo nayo kwa ajili yenu, na kwa ajili ya wale wa Laodikia, na wale wasioniona uso wangu katika mwili;

4:15 Wasalimuni ndugu walioko Laodikia, na Nimfa, na kanisa lililo katika nyumba yake.

2.     Laokikia = Hukumu ya watu huwakilisha kanisa la kisasa.

3.     SIFA. Hakuna

4.     LAWAMA. 3:15-17
15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. 16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. 17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

ARKIPO./Bila shaka alikuwa kiongozi wa kanisa hili, kol. 4:17 Mwambiei Arkipo, Iangalie sana huduma ile uliyopewa katika Bwana, ili uitimize. Je kanisa lilipoa tokana na uongozi wake dhaifu?.
Kanisa lilionekana na nguvu kwa nje, ila Bwana hakuona cho chote cha kulisifu kwa kiroho. Umasikini wa kiroho wa kanisa hili 3:17 Utajiri ni wa nje tu, mashirika makubwa tajiri, majengo mazuri, kumbe mbele za Bwana kanisa hili ni maskini, kipofu, uchi n.k.

5.     USHAURI. Ufunuo. 3:18-19
18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri; na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane; na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. 19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

a.           Tafuta utajiri wa kweli kwa Kristo.
b.           Dhahabu iliyojaribiwa kwa moto.
c.           Vazi jeupe utakatifu wa kweli macho ya kiroho.

6.     AHADI. 3:20-21
20 Tazama, nasimama malangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, nay eye pamoja nami. 21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
Kuketi pamoja na Bwana katika kiti cha Enzi kwa hao washindao.


KITI CHA ENZI MBINGUNI UFUNUO MLANGO 4

4:1 Baada ya ha hayo naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu, ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo.

Mlango unafunguliwa kwa maono ya mbinguni Yohana anapelekwa mbinguni katika roho, aona yanayotokea huko.

1.     Mtu aliyeopo katika kiti cha Enzi. 4:2-3
2 Na mara nalikuwa katika Roho; na tazama kiti, cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja amekiti juu ya kile kiti; 3 na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki, na upinde wa mvua ukizunguka kile kiti cha enzi, ulionekana mithili ya zumaridi.

Yeye aliyeketi (GK) maana yake yeye aliye katika utatu kasha yu mmoja, naye huketi hapo milele.

2.     Mawe. Soma kutoka 28:17-20
17 Nawe ukijaze viweko vya vito, safu nne za vito; safu moja itakuwa ni akiki, na yakuti ya rangi ya manjano, na baharamani, hivi vitakuwa safu ya kwanza; 18 na safu ya pili itakuwa zumaridi, na yakuti samawi, na almasi; 19 na safu ya tatu itakuwa hiakintho, na akiki nyekundu, na amethisto; 20 na safu ya nne itakuwa ni zabarajadi, na shohamu, na yaspi; vito hivyo itakazwa ndani ya dhahabu kwa kujaa mahali pake.
       
a.           Yaspi – humwakilisha Ruben.
b.           Sardiusi – humwakilisha Benjamini

3.     Kuzunguka kiti.
a.     Upinde wa mvua alama ya Agano la Mungu na Nuhu – hataangamiza dunia kwa ghalika tena, Mwanzo 9:11-17
        11 Na agano langu nitalithibitisha nanyi; wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika, baada ya hayo, kuiharibu nchi. 12 Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati
        yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele; 13 Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi. 14 Hata itakuwa nikitanda mawingu juu na nchi, upinde utaonekana winguni, 15 nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi; na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili. 16 Basi huo upinde utakuwa winguni, nami nitaungaalia, nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi. 17 Mungu akamwambia Nuhu, Hii ndiyo ishara ya agano nililoliweka kati yangu na wote mwenye mwili alioko katika nchi.

b.     Rangi ya kijani. Kut. 28:17-20. Naftari rangi ambayo Mungu huivika duninia kwayo, majani n.k. Kijani humwakilisha uhai mpya.

4.     Katika kiti 4:5-6
5 Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti na ngurumo. Na taa saba za moto zilikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu. 6 Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa ahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma.
Taa 7 za moto ukamilifu wa Roho wa Mungu

a.     1:4 Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; na zitokazo kwa roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi;

b.     3:1 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.
c.      5:6 Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wane, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilitumwa katika dunia yote.

Bahari ya kioo – huonyesha hakuna dosari yo yote hapo, ama siyo ingeonekana.

5.     Wazee 24.
        a.     Ni alama ya wanadamu 24.
b.     Katika Agano Jipya wazee ndiyo viongozi wa kanisa nao hawakilisha
kanisa zima soma Mdo 15:6 Mitume na wazee wakakusanyika wapate kulifikiri neon hilo. 20:28 Jifunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpae kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.

c.      Bila shaka hawa wanawakilisha wanadamu waliokombolewa, na siyo malaika.

d.     Bila shaka 12 wanawakilisha waliokombolewa Agano la Kale na 23 wale wa Agano Jipya.
e.     Wamekaa katika viti vya Enzi na taji za ushindi. Soma 1 Kor 9:25 Nakila ashindaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika.

1 Thes. 2:19 Maana tumaini letu, au furaha yetu, au taji ya kujionea fahari, ni nini? Je! Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu, wakati wa kuja kwake?

2 Tim 4:8 baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.

Hawa lazima wawe watu, maana malaika hawapewi taji za kushinda.
Mavazi meupe – hupewa (huahidiwa) watu, sio malaika.


6.     Sifa za wenye uhai. 4
Wenye uhai – viumbe – yawezekana kuwa ni makerubi. Linganisha hawa 4 na
a.           Simba       –      Ufalme wa Kristo         –     Mathayo.
b.           Ndama      –     Utumishi wa Kristo      –     Marko.
c.           Mtu           –      Uanadamu wa Kristo   –      Luka.
d.           Tai            –      Uungu wa Kristo         -      Yohana

Wanadamu pasipo kukoma.

MIHURI 7 UFUNUO MLANGO WA 5.

1.     Hiki ni Kitabu chenye mihuri (seals)
Saba kila muhuri ni siri ya tukio kubwa la uangamizi na hukumu. Ni nani atakifungua? 5:2-5 Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N’nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake? 3 Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. 4 Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. 5 Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba. Hakuwapo.
2.     Jibu
        a.     Simba wa kabila la Yuda. Mwanzo 49:8-10
                8 Yuda, ndugu zako watakusifu,
                Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako.
                Wana wa baba yako watakuinamia.
                9 Yuda ni mwana-simba,
                Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda;
                Aliinama akajilaza kama samba,
                Na kama samba mke; ni nani atakayemwamsha?
                10 Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda,
                Wala mfanya sheria kati ya miguu yake,
                Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki,
                Ambaye mataifa watamtii.

b.     Mzao wa Daudi – Mathayo 22:42-45 akisema, Mwaonje katika habari za Kristo? Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi. 43 Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema, 44 Bwana alimwambia Bwana wangu, uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako? 45 Basi, Daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni mwanawe?

c.           Kristo kama mfalme wa mzao wake Daudi ndiye aliyestahili kufungua.

3.     Kufunuliwa kwa Kristo
        Kama mwana kondoo.

a.           Abasunana katikati ya kiti cha Enzi.
b.           Amewauwa amefunuliwa maana anasimama hajaanguka yu Hai.
c.           Nguvu – Pembe ni alama ya nguvu, kifo hakikudhofisha nguvu.
d.           Hekima – macho 7 utimilifu wa Roho wa Mungu.

4.     Kumbuka.
Kristo alikuja kwanza kama mwana kondoo. Atarudi tena kama Simba wa Yuda.

5.     Sifa toka kwa wazee 24.
        a.     Wanamwangukia katika kiti cha Enzi.
        b.     Maombi ya watakatifu pamoja na uvumba.
        c.      Wanamtukuza kwa sababu.
                (1)    Aliuawa
                (2)    Alileta ukombozi
                (3)    Tukawa wafalme makuhani.
                (4)    Tutatawala naye (miaka 1000) duniani.

MIHURI 6 DHIKI KUU DUNIANI UFUNUO 6
Daniel 9:24-27 Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu. 25 Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalem hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na

majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu. 26 Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu;na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuweko; ukiwa umekwisha kukusudiwa. 27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.

Majuma 70 ya miaka ya Daniel.
Israeli uhamishoni miaka 69, mwaka wa 70 kurudishwa Yerusalemu.
Jumla = Kiebrania = Heptad=
          = Kifungu cha ama vifungu 7.
Majuma 70 = 7 x 70 = miaka 490.
Majuma 7 = 7 x 7 = miaka 49.
Kutoka Koreshi – hadi Hekalu kujengwa Yerusalem

KUSUDI LA DHIKI KUU

1.     Kumaliza uovu.
Uasi wa Israeli dhidi ya Mungu wao utamalizika, pamoja na kumkana masihi wao. Israeli watamgeukia Kristo, nao wataleta uamsho na kuhubiri Injili duniani kote. Ufunuo. 7.

2.     Kukomesha dhambi
Yaani kutia muhuri. Shetani atafungwa mwanadamu atakutana na hukumu ya Mungu duniani kwa kumkataa Mwana wa Mungu.

3.     Kufanya upatanishao kwa ajili ya dhambi
Hii pia yahusu Israeli kupatanishwa na Mungu kwa yeye waliyemkataa kwanza.

4.     Kuleta haki ya milele
Baada ya Israeli kupata uamsho Enzi ya Kristo duniani itaingia kuanzia wakati huo, ufalme wa milele wa Kristo utaingia kwa wateule, kanisa, Israeli.
24
5.     Kutia muhuri maana na unabii
Baada ya Israeli kumgeukia Kristo, hapatakuwa na haja tena ya manabii maono ama unabii wowote.

6.     Kumtia mafuta mahali patakatifu sana
        Ama ni mlima Moria, au miaka 1000 ya utawala wa Kristo dunaini.

MIHURI 6.

MPANGO WA MATUKIO KATIKA DHIKI KUU

1.     Mlango wa 6 – unaanza maelezo.
2.     Mlango wa 7 – unatoa utangulizi.
3.     Mlango wa 8-9 – unaendelea na maelezo.
4.     Milango 10 – 15 – maelezo ya utangulizi zaidi.
5.     Mlango wa 16 – unaendelea na maelezo.
6.     Milango ya 17 – 19 Utangulizi zaidi.

Wakati mwingine maelezo ya utangulizi – yanakwena mbele kuliko utangulizi habari na wakati mwigine yanakuwa nyuma ya maelezo ya dhiki kuu.



 


KUNYAKULIWA                                                          KRISTO KURUDI
                                                                                  KWA UTUKUFU

 



MIHURI 7               TARUMBETA 7                    HUKUMU ZA VITASA 7
Ufu.6                       Ufu. 8,9                             Ufu. 15,16.




Nusu ya kwanza                                                           Nusu ya Pili
(Miaka 3½).                                                                 (Miaka 3½)


1.     Muhuri ya kwanza
        Farasi mweupe na mpanda Farasi
Bila shaka ni mpinga Kristo. Anataji, upinde, bila mshale, Atashinda kwa kupiga kampeni ya amani sio kwa vita.

2.     Muhuri 2 6:3-4 mpanda ji wa farasi mwekundu
Na alipoifungua muhuri wa pili, nikamsikia yule mwenye uhai wa pili akisema, Njoo! 4 Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, nay eye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.
Amani inaondolewa na vita vinaanza Rangi nyekundu hapa inawakilisha damu.

3.     Muhuri 3. Farasi mweusi. Mpanda farasi ana mizani mkononi mwake.
Rangi nyeusi hapa inawakilisha shida ya chakula soma Yeremia 4:28 Kwa ajili ya hiyo nchi itaomboleza, na mbingu zitakuwa nyeusi; kwa sababu mimi nimeyanena haya, na kuyakusudia, wala sikujuta wala mimi sitarudi nyuma niyaache. Maombi 4:8-9 Kwa sababu hiyo jifungeni nguo za magunia; ombolezeni na kulia kwa uchungu; kwa maana hasira kali ya BWANA haikugeuka na kutuacha. 9 Na katika siku hiyo itakuwa, asema BWANA, moyo wa mfalme utapotea , na moyo wa wakuu wake; na makuhani watastaajabu, na manabii watashangaa. Pia nyeusi = kifo.
Mizani – chakula kwa kupimiwa chakula kitakuwa 1/8 tu ya chakula chote cha kawaida duniani au rupia ½.

Vyakula vya uthamani, mafuta na mvinyo lazima vya kila siku vitabakia 1/8 tu, na ni gharama hivyo. Nani ataviweza hivyo vya gharama (tarehe) zaidi?

4.     Muhuri 4. Farasi wa kijivu juu yake mauti na kifo.
        ½ ya dunia wanauawa kwa
a.           Upanga
b.           Njaa.
c.           Kifo (maradhi – mapigo ya maradhi mbalimbali)
d.           Wanyama wakali.

5.     Muhuri wa tano. Matukio mbinguni
        Kundi la waliouawa kwa ajili ya Kristo.
        Kipindi cha kanisa?

Sehemu ya kwanza ya dhiki kuu, bila shaka kwa kuwa kanisa litakuwa likiisha kunyakuliwa kabla ya dhiki kuu.

6.     Muhuri wa sita.
        Matukio mabaya duniani
a.           Tetemeko kuu la ardhi.
b.           Jua kutiwa giza.
c.           Mwezi kuwa mwekundu kama damu.
d.           Nyota kuanguka duniani.
e.           Mbingu inafunguliwa kwa muda na wanadamu wanamwona Kristo na hasira ya hukumu yake.
f.            Milima yote na visiwa vyote vitaondolewa toka mahali pake.
g.           Wanadamu kwa hofu, wataacha kumgeukia Mungu, bali watajaribu kumkimbia Hosea 10:8. Mahali pa Aveni palipoinuka, yaani, dhambi ya Israeli, pataharibika; mwiba na mbigili itamea juu ya madhahabu zake; nao wataiambia milima. Tusitirini; na vilima, Tuangukieni.

WALIOKOMBOLEWA WAKATI WA DHIKI KUU UFUNUO 7.

Mapigo ya ufunuo mlango wa 6 yatakatishwa au onyesho la hao waliokombolewa katika dhiki kuu vitasa 6 vya mwanzo.

1.     Waisraeli 144,000 watiwa muhuri.
Malaika wanasimamisha hukumu duniani kwa muda mpaka wateule wa Israeli watiwe muhuri. Mihuri hii ni kutambulisha kuchaguliwa kwao na Mungu, nao hawakudhurika katika mapigo yaliyopita, watapona na kwa hayo yajayo.
Kumbuka. Hao 144,000, sio kanisa ni wana wa Israeli. Andiko linasema wazi Ufu. 7:4 Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu. Ni kabila la Israeli.
Katika orodha hii.
a.     Lawi – ameingizwa ambaye katika orodha zingine za maandiko anakosekana sababu hakuwa na urithi.

b.           Efraim – ameachwa badala yake Yoseph ametajwa.
c.           Dani – hakutajwa kabisa.


2.             Kwa nini Dani na Efraim wameachwa kabisa?
a.     Wote hawa 2 walihusika sana na kuingiza ibada za mingu katika Israeli Kumb. 29:18-21 asiwe mtu katikati yenu, mume wala mke, wala jamaa, wala kabila, ageukaye moyo wake leo amwache BWANA, Mungu wetu, kwenda kuitumikia miungu ya mataifa hayo; lisiwe katikati yenu shina lizaalo uchungu na pakanga; 19 ikawa asikiapo maneno ya laana hii, ajibarike mtu huyo moyoni mwake, na kusema, Nitakuwa katika amani, nijapotembea katika upotoe wa moyo wangu kwa kuangamiza mbichi na kavu. 20 BWANA hatamsamehe mtu huyo, lakini wakati huo hasira ya BWANA na wivu wake vitafuka moshi juu ya mtu yule, na laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki itamkalia juu yake, na BWANA atalifuta jina lake chini ya mbingu. 21 BWANA atamtenga kwa uovu, kutoka kabila zote za Israeli, kwa laana zote za agano lililoandikwa katika chuo hiki cha torati.

b.     Wengine wanaona kuwa Dani na Naftari, kwa kuwa wana mama mmoja, Bilha, kutajwa kwa Naftari kunamjumuisha Dani.

c.      Mwanzo 49:17 Dani atakuwa nyoka barabarani, Bafe katika njia, Aumaye visigino vya farasi. Hata apandaye ataanguka chali. Inaonyesha kuwa mpinga Kristo anaweza kutoka kabila la Dani.
3.             Watokao katika dhiki kuu.
        a.     Ni nani hao?
(1)    Mkutano makubwa. Watu wa kila taifa kabila, lugha, mbele za kiti cha Enzi, mbele ya mwana Kondoo. Mavazi meupe matawi ya mitende, n.k.

(2)    Hao ni wale watakaokolewa kwa Injili ya wale 144,000 waliotiwa mihuri wakati wa dhiki kuu. Watakapookolewa. Wateseka sana na kuuawa wakati wa dhiki ndipo watafika mbinguni na kufutwa machozi yao mbele ya kiti cha Enzi cha mwana Kondoo.

BARAGUMU 4 ZA KWANZA UFUNGUO 8

Kabla baragumu kupigwa, malaika mmoja anachanganya maombi ya watakatifu na uvumba kasha moshi unapanda juu, halafu anakitupa chetezo duniani. Bila shaka hii ina maana kuwa maombi ya watakatifu yana sehemu kubwa, kasha katika kazi ya Mungu ya kuhukumu ulimwengu nyakati za mwisho yatakuwa hukumu kwa wasioamini.

1.     Baragumu ya kwanza 8:7
7 Malaika wa kwanza akapiga baragumu, kukawa mvua ya mawe na moto vilivyotangamana na damu, vikatupwa juu ya nchi; theluthi ya nchi ikateketea, na theluthi ya miti ikateketea, na majani mabichi yote yakateketea.
Mvua yam awe damu juu ya nchi 1/3 ya nchi, miti, majani mabichi kuteketea.

2.     Baragumu ya pili. 8:8-9
8 Malaika wa pili akapiga baragumu, na kitu, mfano wa mlima mkubwa uwakao moto, kikatupwa katika bahari; theluthi ya bahari ikawa damu. 9 Wakafa theluthi ya viumbe vilivyomo baharini, vyenye uhai; theluthi ya merikebu zikaharibiwa.
Mfano wa mlima mkubwa uwakao moto 1/3 ya bahari yawa damu.

3.     Baragumu ya tatu. 8:10-11
10 Malaika wa tatu akapiga baragumu, nyota kubwa ikaanguka kutoka mbinguni, iliyokuwa ikieaka kama taa, ikaanguka juu ya theluthi ya mito, na juu ya chemchemi za maji. 11 Na jina lake ile nyota yaitwa Pakanga; theluthi ya maji ikawa pakanga, na wanadamu wengi wakafa kwa maji hayo, kwa kuwa yalitiwa uchungu.
Nyota kubwa yaanguka toka mbinguni. Pakanga 1/3 ya maji yawa Pakanga. Chungu sana na yenye madhara.
4.     Baragumu ya nne. 8:12-13.
12 Malaika wa nne akapiga baragumu, theluthi ya jua ikapigwa, na theluthi ya mwezi, na theluthi ya nyota, ili kwamba ile theluthi itiwe giza, mchana usiangaze theluthi yake, wala usiku vivyo hivyo. 13 Kisha nikaona, nikasikia tai mmoja akiruka katikati ya mbingu, akisema kwa sauti kuu, Ole, ole, ole wao wakaao juu ya nchi! Kwa sababu ya sauti zisaliazo za baragumu za malaika watatu, walio tayari kupiga.
1/3 za jua mwezi nyota, zapigwa na kutiwa giza. Mchana haukuangaza 1/3 yake siku inasalia na masaa 16 tu katika 24.

BARAGUMU 3 ZA MWISHO UFUNUO 9

5.     Baragumu ya tano. Ole wa Kwanza. 9:1-12
1 Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu. 2 Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni. 3 Nzige wakatoka katika ule moshi, wakaenda juu ya nchi, wakapewa nguvu kama nguvu waliyo nayo nge wan chi. 4 Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya nchi, wala kitu cho chote kilicho kibichi, wala mti wo wote, ila wale watu wasio na muhuri ya Mungu katika vipaji vya nyuso zao. 5 Wakapewa amri kwamba wasiue, bali wateswe miezi mitano. Na maumivu yao yalikuwa kama kuumwa na nge, aumapo mwanadamu. 6 Na siku zile wanadamu watatafuta mauti, wala hawataiona kamwe. Nao watatamani kufa, nayo mauti itawakimbia. 7 Na maumbo ya hao nzige yalikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita, na juu ya vichwa vyao kama taji, mfano wa dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama nyuso za wanadamu. 8 Nao walikuwa na nywele kama nywele za wanawake. Na meno yao yalikuwa kama meno ya samba. 9 Nao walikuwa na dirii kifuani kama dirii za chuma. Na sauti ya mabawa yao ilikuwa kama sauti ya magari, ya farasi wengi waendao kasi vitani. 10 Nao wana mikia kama ya nge, na miiba; na nguvu yao ya kuwadhuru wanadamu miezi mitano ilikuwa katika mikia yao. 11 Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni. 12 Ole wa kwanza umekwisha pita. Tazama, bado ziko ole mbili, zinakuja baadaye. 

a.     Nyota kuanguka toka mbinguni, Nyota hasa ni kiumbe, bila shaka malaika mwenye mamlaka kufungua shimo la kuzimu.

b.     Nzige watoka shimoni, shimo hili ni mahali pa mapepo
Luka 8:2 na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba.
Luka 10:18 Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme.

c.      Nzige hawa si wakawaida ni mapepo kwa asili yanauma kwa uchungu kama ng’e si rahisi kuwepa wala kuzuia kwa kuwa wanaruka kila upande na kudhuru watu tena watu tu, siyo mimea.

6.     Baragumu ya sita. Ole wa pili. 9:13-21
13 Malaika wa sita akapiga baragumu, nikasikia sauti moja iliyotoka katika zile pembe za madhahabu ya dhahabu iliyo mbele za Mungu, 14 ikimwambia yule  malaika wa sita aliyekuwa na baragumu, Wafungue hao malaika wane waliofungwa kwenye mto mkubwa Frati. 15 Wale malaika wane wakafunguliwa, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ile saa na siku na mwezi na mwaka, ili kwamba waue theluthi ya wanadamu. 16 Na hesabu ya majeshi ya wapanda farasi ilikuwa elfu ishirini mara elfu kumi; nilisikia hesabu yao. 17 Hivyo ndivyo nilivyowaona hao farasi katika maono yangu, nao waliokaa juu yao, wana dirii kifuani, kama za moto, na za samawi, na za kiberiti; na vichwa vyao kutoka moto na moshi na kiberiti. 18 Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo matatu hayo, kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho, yaliyotoka katika vinywa vyao. 19 Kwa maana nguvu za hao farasi ni katika vinywa vyao, na katika mikia yao: maana mikia yao ni mfano wa nyoka, ina vichwa, nao wanadhuru kwa hivyo. 20 Na wanadamu waliosalia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, zisizoweza kuona wala kusikia wal kuenenda. 21 Wala hawakuutubia uuaji wao, wala uchawi wao, wala uasherati wao, wala wivi wao. 

        a.     Maono ya madhabahu sauti toka madhabahuni.
Malaika waliofungwa mto Frati karibu na mto Frati.
(1)    Dhambi ya kwanza ilitendwa mwanzo. 3.
(2)    Mauaji ya kwanza yalifanyika Mwanzo. 4:8 Kaini akamwambia Habili nduguye  (Twende uwandani) Ikawa walipokuwapo , Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua.

(3)    Mnara wa Babeli ulijengwa Mwanzo 11.
(4)    Nimrodi aliujenga Babeli baadaye, Nebukadreza naye Mw 10:9-10 na Daniel 5,7.
(5)    Israel walipelekwa uhamishoni Babeli.

b.     Wapanda Farasi wengi. Farasi hawa wanaonekana kuwa mashetani silaha zao ni:-
        (1)    Moto.
        (2)    Moshi.
        (3)    Kiberiti.

c.      1/3 ya wasioamini wanauawa. Waliosalia bado wanakataa kutubu

UFUNUO MLANGO WA 10

Malaika mwenye kitabu kidogo.
Malaika huyu ana mamlaka sana Yohana anameza kitabu, ili atabiri na baadaye. Lakini hakuruhusiwa kuandika maneno ya yule malaika. Neno halina budi kutufaa sisi kabla halijawafaa hao tuwahubirio, Jeremia 15: 16 Maneno yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu; maana nimeitwa kwa jina lako, Ee BWANA, Mungu wa majeshi.

Ezekieli 3:1-3 Akaniambia, Mwanadamu, kula uonacho; kula gombo hili, kasha enenda ukaseme na wana wa Israeli. 2 Basi nikafunua kinywa changu, naye akanilisha lile gombo. 3 Akaniambia Mwanadamu lisha tumbo lako, ulijaze tumbo lako kwa hili gombo nikupalo. Ndipo nikalila, nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu, kama utamu wa asali.

HEKALU MASHAHIDI 2 NA BARAGUMU UFUNUO 11

Bila shaka Hekalu linajengwa tena Yerusalem katika mlima Moria, ambapo Abrahamu alienda kumtoa Isaka dhabihu, ambapo hekalu la Selemani lilijengwa na ambapo sasa pana msikiti wa Doom of the Rock, utavunjwa?

Kama hekalu hili litajengwa inaonyesha kuwa Waisraeli bado hawajampokea Yesu mionyoni mwao. Hekalu linapimwa Patakatifu pa patakatifu na mahali patakatifu tu. Sehemu ya nje inaachwa, maana itavunjwa na mataifa.
1.     Mashahidi 2 Ufu, 11:3-14
3 Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali wamevikwa magunia. 4 Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele za Bwana wa nchi. 5 Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa. 6 Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinye katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, watakapo. 7 Hata watakapumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao, naye atawashinda na kuwaua. 8 Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu, uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wao aliposulibiwa. 9 Na watu wa hao jamaa na kabila na lugha na taifa wataitazama mizoga yao siku tatu u nusu, wala hawaiachi mizoga yao kuwekwa kaburini. 10 Nao wakaao juu ya nchi wafurahi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi. 11 Na baada ya siku hizo tatu u nusu, roho ya uhai itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama juu ya miguu yao; na hofu kuu ikawangukia watu waliowatazama. 23 Wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama. 13 Na katika saa ile palikuwa na tetemeko kuu la nchi, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka; wanadamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na hofu, wakamtukuza Mungu wa mbingu. 14 Ole wa pili umekwisha pita, tazama ole wa tatu unakuja upesi.
Watakuwa na nguvu kuzuia mvua, kushusha moto, na kuleta mapigo kama Misri. Katika kufuatilia maandiko na huduma zao, inapendezwa kuwa hawa waweza kuwa wawakilishi wa torati na manabii, yaani Musa na Eliya.  Wanapouawa (Yerusalemu) wanadamu wanafurahia sana, kufufuka kwao mbele ya macho ya wengi kunawatisha wengi nao wanampa Mungu utukufu lakini wanaokolewa?

2.     Baragumu ya saba. (11:15-19)
15 Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele. 16 Na wale wazee ishirini na wane waketio

mbele za Mungu katika viti vya enzi vyao wakaanguka kifulifuli, wakamsujudia Mungu 17 wakisema, Tunakushukuru wewe, Bwana Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako, kwa sababu umeutwaa uweza wako ulio mkuu, na kumiliki. 18 Na mataifa walikarika, hasira yako nayo ikaja, na wakati ukaja wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako manabii na watakatifu, na hao walichao jina lako, wadogo kwa wakubwa, na wa kuwaharibu hao waiharibuo nchi. 19 Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua yam awe nyingi sana.

Kristo anatwaa utawala wa dunia mwisho umekaribia sana. Utawala wa Kristo sasa unatangazwa.

VITA UFUNUO MLANGO WA 12.

1.         Ufunuo 12:1
Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili.          


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni