MWL Furaha Amon
Utangulizi
Kuabudu ni jambo pana sana
kuliko watu wengi wanavyo lifahamu. Watu wengi wanafikiri kuabudu kunaishia
kwenye kitendo cha kufanya ibada au misa peke yake. Ibada au misa ni sehemu
ndogo sana katika kuabudu. Kuabudu ni maisha unayoishi. Kuabudu ni maisha
unayoishi. Kuabudu ni kuishi maisha fulani. Kuabudu ni mtindo fulani wa maisha
ambayo Yule Mungu unayemwabudu anakutaka uyaishi. Hivyo siyo swala la
kwenda kanisani kwenye ibada au misa na
ukishaondoka huko kila kitu unakiacha kanisani. Mungu unayemwabudu anakutaka
uishi maisha ya aina fulani hata unapokuwa nje ya ibada, huwezi kuishi maisha
ambayo hayafanani nay ale anayoyataka unayemwabudu halafu wewe ukazingatia ili
mradi unahudhuria katika misa na ibada peke yake. Kuishi maisha yale
anayoyataka Mungu huko ndiko kumcha Mungu. Kwa maana hiyo sehemu kubwa ya
kuabudu Mungu iko nje ya nyumba za ibada zetu. Ni jinsi unavyoishi na watu huko
nyumbani kwako, majirani zako, mtaani kwako, kazini pamoja na sehemu mbalimbali
za maisha ya kijamii. Mungu wetu ana jinsi fulani ya anavyotaka watu wake
waishi huko katika maisha ya nje na ibada. Hebu tuangalie mfano wa mambo
machache tu yafuatayo;-
Biblia inasema,
Tafuteni
kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu
atakayemwona Bwana asipokuwa nao (Waebrania 12:14).
Mcha Mungu anatakiwa asiwe
na ugomvi, chuki, kinyongo na mtu yeyote. Na kama hali kama hiyo inajitokeza ni
lazima ahakikishe anatafuta kwa bidii kuwa na amani na huyo mtu hata kama
mazingira yanakataa.
Biblia inasema,
Bali
wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na
thawabu yenu itakuwa nyingi, nanyi mtakuwa wana wa aliye juu. Kwa kuwa yeye ni
mwema kwa wasiomshukuru, na waovu. Basi iweni na huruma, kama baba yenu alivyo
na huruma. Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa;
achilieni nanyi mtaachiliwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni nanyi
mtaachiliwa. Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa (Luka 6: 35-38
Upendo wa mcha Mungu sio wa
hiari bali ni amri wala siyo ombi. Utake usitake Mungu anatulazimisha tuwapende
watu wote pamoja na adui zetu.
Biblia inasema;-
Heri
mtu Yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki wala hakusimama katika njia ya
wakosaji wala hakuketi barazani pa wenye mizaha (Zaburi 1:1).
Hayo ni maisha anayotakiwa
kuishi mcha Mungu. Mambo hayo niliyoyataja ni baadhi tu ya mtindo wa maisha
ambayo Mungu anataka tuishi. Kuna mambo mengi ambayo Mungu anamtaka mtu
anayemcha Mungu aishi kwa hayo.
Hivyo kuabudu Mungu siyo ibada peke yake bali
ni aina ya maisha. Hivyo kwa kifupi ni kuwa, kuabudu siyo ibada pekee, bali
hata katika maisha ya nje ya ibada. Lengo la somo hili ni kuzungumzia kumwabudu
Mungu katika ibada ya maombi. Zaidi nitazungumzia kumwabudu Mungu kwa maombi
baada ya mwombaji kufika kileleni katika maombi yaani Patakatifu pa patakatifu.
Kabla ya kuedelea mbele kwanza nigusie kidogo kuhusu ibada. Ibada ni lazima iwe
katika kiwango cha patakatifu pa patakatifu. Hii ndiyo ibada ambayo Mungu
atakutana na shida za watu. Ibada inapokuwa ya mwilini au kwenye nafsi, Mungu
hawezi kukutana na shida za watu. Baada ya mwombaji kufika patakatifu pa
patakatifu anakuwa amefika kwenye kiti cha enzi, yuko mbele za Mungu. Mungu
ametuumba ili tumwabudu. Hivyo Mungu anachokihitaji kwetu ni kumwabudu.
Unapofika patakatifu pa patakatifu Biblia inasema, kabla hujaomba nalikusikia.
Hivyo hakuna haja ya kuanza kueleza shida zako mara ufikapo patakatifu pa
patakatifu. Mungu anataka tumwabudu siyo wakati wa kumueleza shida zako.
Unapofika patakatifu pa patakatifu majaribu yote uliyonayo huyeyuka yenyewe.
Lengo la kufika patakatifu pa patakatifu ni kukutana na Mungu ili tumwabudu.
Unapomwabudu Mungu, yeye naye anajua wajibu wake kwa watu wake, hivyo naye anashughulikia
shida zako. Kumwabudu Mungu kwa njia ya ibada, kuomba au kuimba ni kukiri ukuu
wake, kumtukuza, kumwinua, kumbariki, kumshukuru, kumtukuza kwa matendo makuu
aliyokwisha kuyatenda, nk.
Madam Vick Shedafa |
Madam Lilian Kimola |
Unaweza kumwabudu Mungu kwa
kuzungumza yaani kwa kusemelea maneno ya kumtukuza Mungu, n.k. unaweza
kumwabudu Mungu kwa kuimba nyimbo za kumtukuza zenye mahadhi ya kuabudu.
Ukifika patakatifu pa
patakatifu unakuwa uko mbele za Mungu. Wakristo wengi waombaji wa kiwango cha
kufikia patakatifu pa patakatifu wanajua aina moja tu ya kuwa mbele za Mungu
wakati mtu akiwa katika maombi, aina hiyo ni ya kusemelea maneno kwa Mungu au
njia ya kuimba nyimbo za kuabudu. Pamoja na njia hiyo inayojulikana sana, kuna
njia nyingine, njia hiyo ni KUKAA KIMYA
baada ya kupata mpenyo, unaweza ukasikia Roho Mtakatifu anakutaka ukae
kimya mbele za Mungu. Siyo kwamba ukatishe maombi bali uendelee kuwa katika
uwepo wa Mungu lakini ukiwa kimya. Usiombe, usihofu bali uwe kimya. Hapo ni
kumtafakari Mungu na kusikiliza kutoka kwake.
Biblia inasema;-
Nyamazeni,
ninyi wenye mwili, mbele za Bwana kwa maana ametamka, na kutoka katika maskani
yake takatifu (Zakaria 2:13).
Kuna wakati Mungu hataki
tuzungumze tukiwa mbele zake, hasa anapokuwa tayari ameamka kutupigania. Hivyo
utakapoona tayari ameamka kutupigania, hivyo utakapoona Roho Mtakatifu
anakutaka kukaa kimya, ujue uko kwenye mpenyo wa kiwango cha hali ya juu. Tendo
la kumwamsha Mungu ni tendo kuu sana. Hivyo wakati Mungu ameamka, mtu mwingine
hatakiwi kuzungumza. Hii inafanana hata na wakati wa wana wa Israeli Mungu
alipowapigania katika bahari ya Shamu, ambapo wana wa Israeli walikuwa
wamemlilia Mungu sana kufuatia jaribio la Farao na majeshi yake, kuwarudisha
Misri ili wakaendelee kuwatumikia.
Biblia inasema;-
Musa
akawaambia watu, msiogope simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia
leo; kwa maana hao wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. Bwana
atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya (Kutoka 14:13-14)
Hivyo wana wa Israeli
walinyamaza kimya. Mungu alifanya maangamizi makubwa kwa adui. Maandiko
yanaendelea kusema
Lakini
BWANA yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele
zake (Habakuki 2:20).
Huwezi kukaa kimya mbele za
Mungu ukiwa mwilini au kwenye nafsi. Mungu yupo patakatifu pa patakatifu, wewe unatakiwa
ukae kimya. Hivyo kitendo cha kukaa kimya ni kitendo au ni tukio linalofanywa
na mtu ambaye yuko patakatifu pa patakatifu hivyo baada ya kupata mpenyo ndipo
unaweza kukaa kimya. Hii ni kusema kuwa, unapokaa kimya wakati uko patakatifu
pa patakatifu ina maana unakuwa unamwabudu Mungu.
Ukimwabudu Mungu ukiwa
kimya ikiwa Roho Mtakatifu atakuongoza kufanya hivyo,kuna upako mkubwa sana
ambao unashuka ndani yako sawasawa na kumwabudu Mungu kwa njia nyingine baada
ya kupata mpenyo. Upako unaoshuka wakati unamwabudu Mungu kwa kukaa kimya
unaweza kuwa mkubwa kuliko ule wa aina nyingine. Maana wakati huo Mungu
husimama na huwa katika kukutendea au kukupigania kwa nguvu zake zote.
Hivyo using’ang’anie
kumwabudu Mungu kwa kuimba nyimbo za kuabudu au kusemelea maneno tu, hivyo hata
kama itatokea Roho Mtakatifu amekuongoza kukaa kimya wewe kaa kimya bado ni
maombi yenye nguvu tena ya kiwango cha patakatifu pa patakatifu.
Biblia inasema,
Ukae
kimya mbele za BWANA, nawe umngoje kwa saburi (Zaburi 37:7)
Kunyamaza mbele za Mungu, ni muhimu wakati mwingine ni
kungoja jibu au maelekezo kutoka kwa Mungu, waombaji wengi wanataka kuwa
wasemaji wakuu wanapokutana na Mungu. Wao hawataki kumpa Mungu nafasi ya
kuzungumza nao, ili nao wamsikilize. Biblia inasema, njoo tusemezane. Mungu
anataka tusemezane naye. Hivvyo huko ni kusema kuwa, umpe nafasi, Mungu naye
aseme mbadilishane mawazo.
Biblia inasema;-
Bali
wao wamgojeao BWANA watapata nguvu mpya (Isaya 40:3)
Unapokuwa kimya mbele za Mungu, unamgoja Mungu akupe
nguvu mpya juu ya jaribu, shida, n.k. uliyonayo. Unapokuwa umekaa kimya
unamtafakari Mungu, unamwabudu kwa kumtafakari ukuu na uweza wake.
MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUFUATILIA SOMO HILI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni