Ijumaa, 10 Agosti 2012

MSIBA WA ERNEST MWAKASEGE

Wanakwaya wakiimba katika ibada ya kuuaga mwili wa Marehemu Ernest Mwakasege Tukuyu.
Mheshimiwa Mary Mwanjelwa akiweka shahada la maua kwenye kaburi
Ibrahimu Tom Mwakasege ambaye amefariki hivi karibuni.
Mwili wa mchungaji Ernest Mwakasege ukiwasili nyumbani kwa mtoto wake Steven maeneo ya Mbezi. ambako ndugu walikusanyika kabla ya kuanza safari ya kwenda Nyumbani kwake Tukuyu Mkoani Mbeya kwa ajili ya maazishi.
baba yetu Mchungaji Ernest Mwakasege ambaye alifariki tarehe 24/08/2011 alizaliwa tarehe 07/07/1928 tunamshukuru sana Mungu kwa kutupa baba na rafiki mwema.ambaye alikuwa ni moja kati ya nguzo imara katika ukoo wa Mwakasege historia ya maisha yake ilifuta huzuni zetu kwani tunaamini kwamba yupo mahali salama kabisa amepumzika nyumbani kwa baba yake akishangilia na kutazama nyuma matunda ya kazi yake aliyoifanya akiwa hapa duniani. tutazidi kumkumbuka kwa furaha kubwa huku tukitumaini kwamba ipo siku tutaonana na kuishi pamoja tena milele.
WASIFU WA MAREHEMU MCHNGJ ERNEST MWAKASEGE 

KUZALIWA: Marehemu mchungaji Ernrst Ndinganya Mwakasege alizaliwa  tarehe 07 Julai 1928 katika kijiji cha Masebe II;Mwakaleli,wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya. baba yake aliitwa Mzee Ndinganya Mwakasege na mama yake aliitwa Tundalusyege Sandele. mchungaji Ernest Ndinganya mwakasege alibatizwa katika kanisa la Lutheran usharika wa Masebe Mwakaleli. Marehemu alisoma shule ya msingi ya Mwakaleli,halafu akasoma Middle School ya Mpuguso,na baadaye akasoma katika shule ya Sekondari ya Malangali. pia mwaka 1965 hadi 1967 alisoma kozi ya utunzaji wa N'gombe wa maziwa katika jimbo la Nebraska,Marekani. aliongeza ujuzi wake katika ufugaji wa n'gombe wa kisasa alipokwenda huko Uganda mwaka 1973. Ndoa ya mchungaji Ernest Ndinganya Mwakasege kwa Thamali Kajubili ilifungwa mnamo mwezi March 1958 katika kanisa la Moravian usharika wa Tukuyu mjini. Katika uhai uhai wake marehemu alifanikiwa kufanya kazi mbalimbali na baadhi ya kazi hizo ni kama ifuatavyo;

  1. Mwalimu wa shule ya msingi Ikolo(Kyela) na ndembela
  2. mwanzilishi na mwalimu wa kilimo cha kahawa 1957       
  3. mwandishi na msambazaji wa magazeti ya ukulima wa kisasa
  4. Meneja wa shamba la kilimo na mifugo la Uyole Mbeya
  5. Mtafisiri wa katekisimo ya Morevian toka lugha ya           kiingereza kwenda kwa lugha ya kiswahili                                           
Mtoto mkubwa wa marehemu Mwalimu Christopher Mwakasege akiwasili kwenye eneo la msiba nyumbani kwa mdogo wake Steven maeneo ya Mbezi.
hapo ni mimi mwenyewe mjomba wangu Nyabu na wadogo zangu  Isabella Philip na Cecilia Brown tukiwa katika eneo la msiba muda mfupi kabla ya kuupeleka mwili katika ibada kanisani.
mwili wa Baba Ernest ukiwasili katika kanisa la KKKT Mbezi kwa ajili ya sala kabla ya kuanza safari kuelekea Tukuyu kwa ajili ya maazishi.
Askofu Malasusa akitoka kwenye ibada baada ya kumaliza misa maalumu ya kuuombea mwili wa marehemu na kuaga kwa mara ya mwisho kwa ndugu waliokuwa Dar es salaam.
mwili wa baba Ernest ukiwa katika kanisa la KKKT mbezi kwa ajili ya kuuombea kabla ya kuanza ibada.
Isabella Mwakasege akikusanya maua ambayo yatakwenda kutumika siku ya mazishi Tukuyu
Mdogo wa Marehemu Brown na mama tukiwa pamoja katika safari ya kuusindikiza mwili wa marehemu.
Mke wa Marehemu akisindikizwa kwenye gari kwa ajili ya kuendelea na safari.
kaka wa marehemu Mzee Angetile 
hapa ndipo ulipopumzishwa mwili wa baba yetu nje ya nyumba yake huku Tukuyu.
Mwalimu Christopher na mke wake wakiweka shada la maua juu ya kaburi.
Mjukuu wa Marehemu Sara naye akiweka shada la maua.









































Hakuna maoni:

Chapisha Maoni