TUNAYO MAMLAKA
Mungu ametupa mamlaka juu ya shetani na kwa kuwa
tumepewa mamlaka hayo,Mungu ametukabidhi
sisi wenyewe uweza wa kumharibu na kumsambaratisha shetani na kazi zake kila
tunapokutana naye.
Kwa hiyo tumia mamlaka uliyopewa kubomoa ngome za shetani
vunja vunja nguvu zake na mipango yake mfunge shetani sambaratisha shughuli zake.
Yak 4.
Katika kila jaribu nyuma ya hilo jaribu
kuna pepo.
·
Huyo pepo ndiye anayesababisha hilo
jaribu kuwepo.
· Kwa hiyo basi unashauriwa usipigane
na na jaribu hilo, bali pigana na Yule
pepo anayesababisha hilo jaribu.
·
Hii ni sawa na ugonjwa, mtu akiwa
mgonjwa akienda hospital daktari
hutafuta kile kijidudu kilichosababisha huo ugonjwa. Baada ya kukijua ni kijidudu ganikinachosumbua,daktari
humpa mgonjwa huyo dawa yenye uwezo wa kukiua hicho kijidudu.
na baada ya kukiua hapo ndipo ugonjwa
unaomsumbua huyo mtu hutoweka.
Kwa hiyo wewe pigana na pepo aliyesababisha jaribu
usipigane na jaribu lenyewe bali pigana na ile roho ovu iliyosababisha jaribu hilo
na wala usipigane na tatizo.
Watu wengi hupigana na jaribu badala ya kupigana na
pepo, biashara yako inapojaribiwa wewe
pigana na hilo pepo linaloshambulia hiyo biashara yako kwa kutumia mamlaka uliyonayo.
Mfunge shetani mtupe kuzimu, Usikubali kushindwa na
shetani. neno la Mungu linatuagiza kumpinga shetani naye atatukimbia.
Unapokutana na shetani sio wakati wa kukimbilia kwa
Yesu au kwa Mungu huo ni wakati wako mwenyewe kutumia mamlaka uliyopewa na
Mungu.
·
Watu wamekuwa wakimwita Yesu katika kila
hitaji.
·
ni kweli yapo mambo ambayo Mungu ametaka
tumwite.
lakini unapokutana na shetani Mungu
amekuagiza umpinge wewe mwenyewe naye
atakukimbia.
·
usipompinga shetani hataweza kukukimbia
kwa maana hiyo jaribu halitaondoka.
·
litaendelea kwa maana hujamfukuza
aliyesababisha hilo jaribu.
Hebu fikiria mtu akiwa amepagawa na pepo aletwe
kwako umuombee lakini maombi yako unamwambia Yesu aje kumtoa huyo pepo au
unamwambia Mungu aje kumtoa huyo pepo. Hilo halitawezekana Utamaliza miaka kumi
ukiomba huyo pepo hatatoka.
lakini siku
ukiamua kumwamuru atoke kwa kutumia mamlaka uliyonayo kwa jina la Yesu huyo
pepo atatii na kuondoka.
·
Hii ni kwa sababu Mungu ameagiza hivyo
Mungu amesema tumpinge shetani naye atakimbia.
·
Mungu hajasema tumuite yeye Mungu au Bwana
Yesu aje ampinge shetani.
Yesu alisema Kwa jina langu mtatoa pepo(
Marko 16.17) tumia mamlaka uliyopewa kutoa mapepo kwa jina la Yesu.
·
Toa pepo wewe siyo umuite Mungu aje atoe
pepo. Ni sehemu nyingi katika maandiko Mungu ametuagiza tumshinde shetani sisi
wenyewe,
Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza
kuzipinga hila za shetani (Waefeso 6.11). hapa ina maana kuwa kama hujavaa
silaha hutaweza kumpinga shetani. Hii ni pamoja na kuishi maisha matakatifu. Ni
pamoja na uombaji wa kiwango cha kupata mpenyo. YAPO MAANDIKO MENGI YENYE
KUTUAGIZA KWAMBA TUTAMSHINDA SHETANI SISI WENYEWE.
Mwisho
ELIYA MTISHBI ALIJUA
KUTUMIA MAMLAKA 1Wafalme 17.1
Katika maandiko haya
tunamuona Eliya anamtambia mfalme Ahabu kwamba mvua haitanyesha mpaka aseme
yeye. Eliya alifanya hayo kabla hata jina la Yesu halijaletwa. Sisi tuna
mamlaka na tuna jina lenye nguvu la Yesu unachotakiwa ni kusimama tu kwenye
zamu yako. Watu wamemuasi Mungu maovu mengi yanfanyika, maonevu mengi
yanafanyika na wenye wanafanya maovu
hakuna wa kuwakemea hakuna wa kuwaonya
maana hakuna watu wa Mungu wenye
kuibeba mamlaka. Watu waMungu wamejichanganya kwenye dhambi na Mungu
amewanyanganya mamlaka yake kama alivyomyanganya lusifeli,inatakiwa watu
wamuogope Mungu wako. Watu wote wamuheshimu Mungu wako kazini kwako wafanyakazi
wenzako wakubwa wako kazini hata wakuu wan chi wanatakiwa wamuogope Mungu wako
pia. Watu wanahubiri injili isiyokuwa na mamlaka wala nguvu ya Mungu,waaogopa
hata kukemea maovu. Injili wanaihubiri lakini watu walioko kanisani kwao bado
wamefungwa na shetani,ni wagonjwa na masikini n.k.
Mtume Paulo anasema
katika Rumi 1.6 huu sio uweza wako hata uone haya kuutumia . ni uweza wa
Mungu,Mungu ndiye ameuweka uwezo wake ndani yako,wewe kazi yako ni kuupalilia
kwa maombi na kuutunza kwa kuishi maisha matakatifu. Tena si kwamba uko kwa
viongozi wa dini tu,hapana ni kwa kila aaminiye. Katika kanisa la kwanza
kulikuwa hakuna cha kiongozi wala cha muumini wote walikuwa motomoto cha msingi
ni kusimama kwenye zamu yako. Paulo alibarikiwa sana na uweza wa
Mungu,akawaombea hata wale ambao pengine macho yao kiroho ni vipofu hawalijui
hili hili kwamba wanayo mamlaka ndani yao anagalia waefeso 1.17,23 kisha
angalia 1Wakorintho 12.6 kila mwamini ni kiungo katika mwili wa kristo na
kristo yeye ni kichwa,kiwiliwili chake ambacho kina kina viungo vingi hicho
ndicho kanisa. Ndio waamini mbalimbali wote duniani, huyu ni mkono huyu ni
ukope huyuni kucha mwingine ni nywele ,utumbo,miguu n.k.
Yesu ni kichwa
kiwiliwili chake ndio watu wa Mungu,Mungu
alimuweka Yesu juu sana kuliko ufalme wote,mamlaka,nguvu,usultani na kila jina
litajwalo akavitia vitu vyote chini ya miguu yake kwa ajili ya kanisa. Wewe
ndugu ni kiungo fulani katika mwili wa Kristo,Kristo yuko juu ya vitu
vyote,aliwekwa hivyo kwa ajili yako wewe uliye kiungo katika mwili wake. Kama
Yesu yuko juu,viungo vyake pia viko juu. Kuna msemo mmoja wa kishetani usemao
kwamba shetani kajiinua juu ya jambo fulani,wewe mtu wa Mungu shetani yuko
chini yako daima labda ukitoka ndani ya Yesu,shetani anajua nafasi yake ya
kukaa chini miguu yako,hawezi kujiinua ,hana uwezo huo,bali wewe mwenyewe
ambaye unao uwezo juu yake ndiye unaweza kumuiua aje juu yako. Usikubali kukiri
hivyo tena kwamba shetani kajiinua. Huo ni msemo wa watu wa dini za kikristo,
wakristo hao wanapookoka wanahama na msemo huu na kuingia nao katika wokovu
mtume Paulo anawaombea waamni ili wafunuliwe wajue jinsi walivyo juu ya
shetani. Tuko juu kuliko jina lolote litajwalo,kuna majina mengi saa ya kutisha
hapa duniani,majina kama malaria ,Ukimwi ,Ebora saratani n.k. pamoja na kwamba
tumewekwa juu ya kila jina litajwalo mtume Paulo alipogundua siri hii alifurahi
sana ,uwezo huu ukamfanya aseme siionei haya injili ya Kristo. Hata wewe huwezi
kukionea aibu kitu cha thamani namna hii. Nchi zenye bomu la nyuklia
zinajigamba sana kwa sababu zinajivunia nguvu za bomu la nyuklia.lakini sisi
tuna nguvu kubwa katika ulimwengu wa r oho kuliko bomu la nyuklia.
Tupo juu ya kila jina la mtu mashuhuri yeyote aliyepo na atakayekuja. Askari trafiki anasimamisha lori kubwa linaloendeshwa na jitu la miraba minne kwa kunyoosha mkono wake tu. Haijalishi hata kama ni kasichana kadogo tu,tena hana bunduki na yuko peke yake tu. Hata kama gari hilo lipo katika kasi kubwa kiasi gani dereva atahangaika mpaka atasimama. Kinachosababisha asimame ni mamlaka aliyonayo trafiki ambayo kimsingi sio yake binafsi bali ni ya serikali. Hata sisi katika ulimwengu war oho tuko na mamlaka zaidi ya trafiki. Sisi tuna mamlaka ya kifalme kila kitu kinatii,umewahi kusikia wapi kwamba mfalme anabishana na raia,na ni afadhali raia lakini shetani ndio hawezi kabisa kwetu hizi ni nyakati za shetani kupigwa kuliko wakati wowote ule aliowahi kuwepo hapa duniani,Mungu ameshusha nguvu kubwa sana ya lala salama angalia Yohana 14:12. ni afadhali shetani akutane na Yesu kuliko kukutana na mwamini anayejua kutumia mamlaka yake kikamilifu. Yesu anatutumaini sisi tufanye kazi kubwa zaidi kuliko aliyoifanya yeye.
Tupo juu ya kila jina la mtu mashuhuri yeyote aliyepo na atakayekuja. Askari trafiki anasimamisha lori kubwa linaloendeshwa na jitu la miraba minne kwa kunyoosha mkono wake tu. Haijalishi hata kama ni kasichana kadogo tu,tena hana bunduki na yuko peke yake tu. Hata kama gari hilo lipo katika kasi kubwa kiasi gani dereva atahangaika mpaka atasimama. Kinachosababisha asimame ni mamlaka aliyonayo trafiki ambayo kimsingi sio yake binafsi bali ni ya serikali. Hata sisi katika ulimwengu war oho tuko na mamlaka zaidi ya trafiki. Sisi tuna mamlaka ya kifalme kila kitu kinatii,umewahi kusikia wapi kwamba mfalme anabishana na raia,na ni afadhali raia lakini shetani ndio hawezi kabisa kwetu hizi ni nyakati za shetani kupigwa kuliko wakati wowote ule aliowahi kuwepo hapa duniani,Mungu ameshusha nguvu kubwa sana ya lala salama angalia Yohana 14:12. ni afadhali shetani akutane na Yesu kuliko kukutana na mwamini anayejua kutumia mamlaka yake kikamilifu. Yesu anatutumaini sisi tufanye kazi kubwa zaidi kuliko aliyoifanya yeye.
KWA MUUMINI AMBAYE
UWEZA UMO NDANI YAKO INAKUPASA KUJIHESHIMU KAMA CHOMBO KILICHOBEBA KITU CHA
THAMANI.
Kwa vile nguvu hii
hukaa katika kinywa chako basi unatakiwa kuchunga sana maneno unayozungumza.
Maneno yako ni ya thamani sana tofauti na watu wengine wasiomwamini Yesu. Usiwe
mtu mwenye kuropoka maneno yasiyo na maana,usiwe mtu wa kusogoa sogoa maneno kwenye
vijiwe visivyo na maana. Unapoongea tafakari na kulipima kwanza neno unalotaka
kulisema kama litampedeza litampendeza Mungu au
halitampendeza. Angalia Mathayo 12.36,37
Maneno yako yataamua
uingie mbinguni au usiingie. Hii ni pamoja umeokoka na umeacha kutenda hambi
zingine,lakini bado utahukumiwa kutokana na maneno yako. Lakini watu wa Mungu
wengi hawalijui hili. Wanajali zaidi kuacha dhambi zingine lakini bado midomo
yao ni michafu sana. Wanaitumia kulaani na kuwaangamiza watu wengine. Utakuta
mchungaji anaposhindwa kuelewana na muumini wake katika eneo fulani yeye
anakimbilia kulaani. Muumini ni mtoto wako,hata akikukosea ni mtoto wako
tu.hata kama atahama kanisa linguine bado ni talanta yako tu utalipwa hiyo
talanta. Sasa wewe umetofautiana na muumini wako kiroho unakimbilia ile fimbo
yako ambayo umepewa ili upigie nyoka,unampigia muumini wako. Muumini wako ni
mtoto wa Mungu ukimpiga kwa fimbo na wewe subiri kupigwa rungu la Mungu wewe
mzazi baba au mama jifunze sana kubariki watoto wako
na watu wote wa nyumbani
kwako. Acha mambo ya kuwalaani kabisa,baba usimlaani mke wako wala mama
usimlaani mume wako acha unaoishi nao wawe na furaha na amani bila kuogopa
kulaaniwa. Kama kuna makosa wanayoyafanya yashughulikie kwa njia nyingine na
wala sio ya kuwalaani angalia Yakobo (3:2-12) yaliyomo moyoni mwako ndiyo ambayo
hukutoka,wewe ni mtu wa Mungu hakikisha unazungumza maneno yanayompeneza Mungu.
Sio wewe mmoja uzungumze maneno yanayompendeza Mungu tena wewe huyohuyo mmoja
unazungumza maneno yanayompeneza shetani.
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni