BADO
TUNAWAKUMBUKA VIJANA WA Christ Ambassadors wa Rwanda
pamoja na kwamba siku nyingi zimepita lakini Wapenzi wangu wa Blog waliomba niwakumbushe kile kilichoipata Kwaya ya Christ Ambassadors Kutoka kule nchini Rwanda. Na kama kawaida imebidi nihangaike na. Kwa Msaada Mkubwa wa marafiki zangu na kupitia katika mitandao mbalimbali, hatimaye nimekusanya taarifa kama ifuatavyo.
pamoja na kwamba siku nyingi zimepita lakini Wapenzi wangu wa Blog waliomba niwakumbushe kile kilichoipata Kwaya ya Christ Ambassadors Kutoka kule nchini Rwanda. Na kama kawaida imebidi nihangaike na. Kwa Msaada Mkubwa wa marafiki zangu na kupitia katika mitandao mbalimbali, hatimaye nimekusanya taarifa kama ifuatavyo.
Hali ya Gari la kundi hilo baada ya ajali
Ambassadors of Christ Choir ni kwaya ambayo kwa sasa inafanya Vizuri sana na nyimbo zake zimekuwa zikipendwa sana hapa nchini. Kundi hili lenye maskani yake nchini Rwanda katika jiji la Kigali hivi sasa limetimiza miezi takribani mwaka na miezi minne tangu baadhi ya wanakikundi hicho kufariki dunia tarehe 9/05/2011 walipokuja nchini kwa mualiko wa kwaya ya Acasia Mwenge SDA ya jijini Da es salaam.Baada ya kupata Mualiko huo, tarehe 5/05/2011 Kundi hilo lilianza safari ya kuja jijini Dar es salaam kwa ajili ya Uzinduzi wa DVD ya kwaya ya Acasia ambao ulipangwa kufanyika katika ukumbi wa PTA ulio katika viwanja vya Sabasaba jijini Dr es salaam.
Ambassadors
of Christ walifanikiwa kufika Dar es salaam tarehe 6/05/2011. Kundi hili
liliweza kushiriki ibada ya sabato siku ya jumamosi ya tarehe 7/5/2011 na
lilialikwa katika Interview katika kituo cha Redio cha Morning Star Adventist
Radio of Tanzania kilichoko jijini Dar-es salaam kwenye kipindi kiitwacho
“LULU ZA INJILI”
Wakiwa
Redioni hapo, kundi hili lilivutia wasikilizaji wengi hasa kwa uwezo wao wa
kuimba Live. Tarehe 8/05/2011 ndio siku iliyokuwa ikisubiriwa kwani ilikuwa
siku Maalumu kwa kwaya ya Acasia Mwenge SDA Kufanya uzinduzi wa dvd yao ya Pili
iitwayo “MNAZARAYO” katika ukumbi wa PTA.
Watu
kutoka kona tofauti tofauti za jijini Dar walifurika kutaka kuwaona vijana hawa
Live wakiwa jukwaani wakimtukuza Mungu. Muda uliwadia na ndipo vikundi
mbalimbali vya injili vilitangulia kuimba wakiwemo Voice of Victory wakifuatiwa
na Triumph Generation pamoja na Harvesters vyote vya jijini Dar es salaam.
Muda
uliwadia ambapo ukumbi mzima ulizizima kwa furaha na vifijo pindi Ambassadors
of Christ walipotajwa kuwa ndio wanafuata kupanda jukwaani. Taratibu huku ala
ya nyimbo yao maarufu iitwayo Twapaona
vijana hawa walipanda jukwani na ukumbi mzima ulizidi kupiga kelele za furaha.
Miongoni
mwa nyimbo ambazo Ambassadors of Christ walizimba Live siku hiyo ni pamoja na Kazi Tufanye, Yesu Ndiye Njia, Twapaona,
Kuna Siku, Huyo ni Yesu, pamoja na nyimbo yao maarufu iitwayo Kwetu Pazuri. Watu wote waliofika
ukumbini hapo walibarikiwa na kazi za kundi hili kwa utukufu wa Mungu.
Kuhusu
Ajali
Baada
ya kumaliza huduma tarehe 8/05/2011, kundi zima la Ambassadors of Christ
lilianza safari ya kurudi Kigali asubuhi ya tarehe 9/05/2011 kwa njia ya basi.
Walipofika Wilaya ya Kahama mkoani shinyanga mnamo saa tatu usiku walikutana na
Lorry likiwa limepaki barabarani likiwa halina reflector yeyote. Dreva wa gari
la kundi hilo hakuweza kulina lorry hilo na pindi alipoliona na kutaka
kuliovatake ndipo lorry lingine lilikuwa likija kwa kasi hivyo wakakutana
uso kwa uso na ajali ikatokea.
Baada
ya ajali hiyo iliyotokea kilometa kadhaa kabla ya kufika Rwanda,
wanakwaya watatu wa kundi hil Filbert
Manzi, Gatare Ephraim pamoja na mtanzania Amos Fares ambaye nayee ni muimbaji wakundi hilo aliyekuwa
mbele akielekeza njia walifariki papo hapo.
Muda
mfupi baada ya ajali hiyo kutokea serikali ya Rwanda ilituma Helkopta ya Jeshi
la ulinzi la nchi hiyo [RDF] pamoja na Ambulance mbili kwa ajili ya
kusafirishia wagonjwa kutoka Kahama kwenda Hospitali ya Mkoa wa shinyanga.
Baada ya kufika Hospitali ya shinyanga wahanga hao waliweza kupata huduma ya
kwanza na hatimaye walikimbizwa nchini Rwanda katika Hospitali iitwayo King
Faisal kwa matibanu zaidi.
Kwa
msaada wa Mungu majeruhi wane wa ajali hiyo walipata nafuu na hatimaye
kurutuhusiwa kutoka Hospitali. Taratibu za mazishi zilifanywa ambapo Marehemu
Filbert Manzi aliyekuwa mmoja wa vingozi wa kwaya hiyo na pia mtangazaji wa
kituo kimoja cha Redio nchini Rwanda, pamoja na Gatare Efraimu ambaye alikuwa
ni muanzilishi na kiongozi wa kwaya
hiyo wa walizikiwa nchini Rwanda, wakati Mtanzania Amos Fares yeye alizikiwa
nyumbani kwao mkoani Kigoma.
Zifuatazo
ni baadhi ya matukio ya kundi hilo wakati wakiimba jijini Dar na baada ya ajali
hiyo
Waliotangulia
Twakumbuka hili tukio kwa huzuni.
JibuFuta