WEKA UFAHAMU WAKO
HURU.
Mungu wetu
ametuumba kwa namna ya kipekee kabisa na anatujua vizuri sana hata kwa majina
yetu,na zaidi ya hayo ametupangia kila kitu katika maisha yetu. Kabla
hajatuumba alikuwa ameshaandaa kila kitu katika maisha yetu. Lakini mipango
mingi ya Mungu inashindwa kutimia katika maisha yetu kutokana na mawazo
tuliyonayo yanavyoweza kuathiri na kuzuwia mapenzi Mungu juu ya mafanikio yako.
Ni muhimu kujua jinsi ufahamu wa mwanadamu unavyofanya kai na jinsi ambavyo
unaweza kuutawala na aina ya mawazo unayopaswa kuyawaza ukiwa kama kiumbe
muhimu kwa Mungu. Zipo athari zinazopatikana kutokana na kuwaza vibaya. Kuna
magonjwa na kutokufanikiwa kunakoandamana na sababu za kuwaza vibaya. Ni muhimu
kujifunza namna ya kuukomboa na kuuweka huru ufahamu wako ili uwe unawaza yale
yaliyo na umuhimu tu. Utabadirika katika maisha yako kutokana na jinsi
utakavyobadilika katika kuwaza kwako kwa kuwa “Ajionavyo (awazazvyo) mtu nafsini
(akilini) mwake ndivyo alivyo.”
UFAHAMU NI
NINI?
Mwili wa
binadamu hujiendesha kwa sehemu kubwa kwa kutumia akili (MIND) yake yaani
ufahamu. Sehemu hii muhimu sana kwa binadamu inaratibu utendaji wa mwili na
viungo vyote vya mwili kuanzia kichwani mpaka unyayoni. Huratibu kiasi cha damu
kinachotakiwa kichwani na katika mwili mzima. Huratibu pia usagaji wa chakula
muda wa kupumzika yaani kila kitu katika mwili wa binadamu. Katika ulimwengu wa
sasa wenye shinikizo na mahangaiko mengi ya maisha wandamu wamekuwa wakiishi
katika wakati mgumu sana. Watu wamekuwa wakisongwa na mawazo ya kila aina na
mengi yakiwa ni mawazo hasi (negative). Mawazo hasi ni mawazo yasiyokuwa na
uvumbuzi ni kuwaza shida, matatizo pamoja na masumbufu yanayomzunguka mtu. Kwa
kutumia mawazo yetu adui anatuongoza katika kukata tama, kutojiamini na
kutomwamini Mungu. Kuanzia mwanadamu alipoanguka katika bustani ya Eden uwanja
wa vita kati ya Mungu na shetani kwa binadamu upo katika ufahamu (akili) MIND
ya binadamu. Kwenye ufahamu huko ndiko ambako shetani hupigana vita na sisi
binadamu. Iwapo atafanikiwa kukamata ufahamu wako sawasawa, basi itakuwa ni
vigumu sana kwako kufanikiwa. Utakosa uhuru wa kuamua au kufuata mapenzi ya
Mungu na mwishowe kuishia kwa waganga wa kienyeji. Lakini ukiweza kumwondoa na
kufanikiwa kumshinda shetani katika ufahamu wako wewe utakuwa huru.
AKILI NI
NINI?
Neno akili
ukilitafiri kutoka katika neno la kiingereza MIND ambalo maana yke ni Nia,dhamiri,akili,ufahamu,
kumbukumbu. Akili ni eneo muhimu sana ndani ya mwanadamu ambalo linaratibu
shughuli zake zote ndani na nje ya mwili wa mwanadamu. Ubongo ni kama kompyuta
kubwa ambayo inahifadhi vitu vingi na muhimu lakini akili ni zaidi ya ubongo.
Baadhi ya kazi za akili ni kama zifuatazo. (1) kukumbuka (2)kuelewa(3) utashi
(kufanya maamuzi) (4) uendeshaji wa mwili n.k. vilevile akili huwa inafanya
kazi pamoja na uelewa na mazoea. Kuhisi vitu na kusafirisha kumbukumbu. Kuamini
(kuhukumu) kutokana na tukio lililotangulia na la sasa.
UMAKINI
KATIKA MAAMUZI.
akili si ubongo na wala akili haionekani wala haushikiki bali
akili ipo na kila mtu anayo na anaitumia kwa viwango tofauti. Akili hutunza
kumbukumbu za matukio yote kuanzia alitungwa mimba mpaka hapo ulipo. Japokuwa
si rahisi kukumbuka matukio yaliyotokea wakati akiwa mtoto mchanga. Lakini bado
yapo ndani mwako na yana athari ndani mwako. AKILI HUFANYA KAZI KWA KUAMINI NI
LAZIMA UAMINI ILI JAMBO LITOKEE.(Mathayo 17:20) kwa mstari huu tunaona kuwa
Yesu ametutaka tuamini,ndivyo tulivyoumbwa. Sisi tunaishi kwa imani ndio maana
akili huamini hata kile inachopokea katika masomo au mafundisho mbalimbali.
Vilevile Mungu ametujalia wanadamu uwezo wa hali ya juu wa kutumia akili kama
chombo cha mafunuo katika hali isiyokuwa ya kimwili mfano maono ndoto n.k. watu
wengine wamejaliwa kuota ndoto na baadae tukio linatokea kweli. Au anahisi kuwa
kuna mgeni anakuja nyumbani na baada ya
muda mgeni huyo anatokea kweli. Hii ni kuonyesha kuwa ufahamu wa mtu huyo
ulijua kuwa huyo atakuja kabla ya kumuona. Wakati mwingine unaweza kuimba wimbo
fulani,mara hiyohiyo ukausikia wimbo huo kwenye radio unaanza kuimbwa.
JINSI AKILI
INAVYOENDESHA YETU.
Kama
tulivyojifunza kwamba akili hurtibu utendaji mzima wa mwili kama kusafirisha
damu.kuamuru kutengenezwa kwa chembechembe zinazohitajika kwa wakati. Kuamua
misuli ya kusaga chakula au mikono na miguu au aina yoyote ya misuli ya mwili
ifanye kazi. Shughuli hizi hufanyika kwa namna mbili (a) ukiwa una uelewa yaani
ukiwa na fahamu.(b) ukiwa hauna uelewa yaani umelala au umezimia. Mfano unaweza
kukunja mkono wako na vidole mpaka kuwa mfano wa ngumi,kitendo ambacho unaweza
kukifanya ukiamua. Lakini huwezi kula chakula na ukaamua kuwa sasa chakula hiki
kisagwe, huwezi kuamua kupunguza kiasi cha damu inayoelekea mkono wa kulia na
kuilekeza mkono wa kushoto au mguuni.
HIVYO NDIO KUSEMA KUWA KUNA UTENDAJI
MKUBWA SANA NA MUHIMU AMBAO HUFANYIKA NDANI MWETU BILA YA SISI WENYEWE KUJUA
kazi mojawapo ya akili ambayo ambayo ningependa tujifunze sana ni hii ya kutunza
kumbukumbu na mawasiliano. Eneo hilo ndilo lililo na umuhimu wa kipekee katika
maisha yetu yajayo na linaloendesha mfumo mzima wa maisha yetu kiroho zaidi na
kimwili.
SEHEMU KUBWA
TATU ZA AKILI
SEHEMU YA
KWANZA (Conscious Mind) sehemu hii huhusika na kufikiria na kuweka kumbukumbu
za muda mfupi pamoja na kutambua vitu. Hutumia milango mitano ya fahamu
kutambua na kuvipambanua vitu. Huwa inafanya kazi wakati mtu anapokuwa macho au
hajalala,akiwa anajitambua.sehemu hii huwa haitunzi kumbukumbu bali huwa
inazipokea na kuzipeleka sehemu ya pili. Eneo hili pia unaweza ukaliita sehemu
ya nje ya akili au uelewa. Matukio yote unayoyafanya kwa kuelewa,kujitambua
yanaratibiwa tayari kwa kukumbukwa mfano,sura ya mtu,rangi
mbalimbali,mitaa,barabara n.k. eneo hili ndilo linalopambanua kila kitu,ndilo
linaloratibu shughuli na utashi wa mtu wa kila siku kwa mfano avae nini,ale
nini n.k. matukio maneno au mawazo yanapojirudiarudia na haswa maneno ya
kujisemea mfano mimi nina shida,nateseka Napata taabu, nina amani,ninaweza nina
akili ninaweza jambo. Mawazo ya aina hii yanapojirudiarudia ndani ya sehemu hii
ya awali, akili huamini na inapoamini hupeleka imani katika sehemu ya pili
kuhifadhiwa tayari wakati wa baadae.kwa kutumia sehemu hii mtu hutambua na
kuelewa vitu vinavyotokea kwa kupitia ya fahamu mtu hupata kuelwa kwa kupitia
sehemu hii. Tunaweza kuiita utashi au moyo,hutoa maamuzi madogo madogo ya mtu
na huwa haihifadhi kumbukumbu ya muda mrefu. Hutambua vitu vya kawaida na
vilivyozoeleka kuwepo hujishughulisha pia na mambo ya kila siku kama uchaguzi
wa nguo,chakla maamuzi n.k.(mazuri na mabay ya kila siku hufanywa hapa.vilevile
hufnya kazi ya kufikiri na wakati mwingine huwa na mjadala wa ndani ya mtu.
Utakuwa unawaza na kujiuliza maswali na kupata majibu ya maswali unayojiuliza.
Mjadala au mabishano ya mwanzo ambayo wakati mwingine inakuwa ni shida kupata
majibu au suluhisho lake yanaanzia sehemu hii. Japokuwa mara nyingine suluhisho
linapatikana lakini kwa uzoefu mawazo yanayodumu kwa muda mrefu hayapati
suluhisho zuri katika eneo hili. Mawazo na majadiliano hayo yanayochukua muda
mrefu yanapelekwa kuhifadhiwa katika sehemu ya pili (Sub conscious) kwa ajili
ya kufanyiwa kazi baadae. Sehemu hii hufanya kazi mtu anapokuwa na ufahamu
(akiwa macho) sehemu kubwa huacha kufanya kazi wakati mtu anapolala au
anapokuwa amezimia. Mawazo yote huwa yanaanzia hapa yawe mazuri au mabaya
mawazo haya huwa hayatokei hivihivi tu bali huwa chini ya mamlaka ya mtu
mwenyewe. Mtu anao uamuzi wa kuwaz au kutokuwaza mawazo haya pia huwa yantokana
na mazoea ya mtu mwenyewe. Mtu kama amezowea kuwaza mawazo
uovu,mabaya,shida,taabu,hasi basi kila wakati atawaza hayo tu. Mawazo yenyewe
huja kama vile yanajiendesha yenyewe (automatic) lakini kumbe sivyo. Vilevile
kuna mtu amezowea kuwaza mema,mazuri,furaha,amani,mafanikio nayo vilevile huja
yenyewe (automatic) na kila wakati alivyojizoesha. Baada ya kufanya kazi kutwa
nzima na kupata vitu mbalimbali huyahifadhi yote hayo kwenye eneo la pili la
akili ambayo ni Sub conscious) kwa ajili ya kufanyiwa kazi baadae. Sehemu hii
hufanya kazi mtu anapokuwa na ufahamu yaani akiwa macho sehemu kubwa huacha
kufanya kazi wakati mtu anapolala au anapokuwa amezimia. Mawazo yote huwa
yanaanzia hapa yawe mazuri au mabaya.
SEHEMU YA
PILI YA AKILI (Subconscious mind)
Hii ni
sehemu katika akili ya mwanadamu iliyopo bila kujulikana kwa mwenye kuwa nayo.
Ni sehemu ambayo inawea kumtawala mwanadamu japokuwa mwanadamu haioni wala
kuitambua. Eneo hili ndilo hufanya kazi kubwa sana kwa binadamu kama vile
kuhifadhi kumbukumbu zote na kuzileta baadae kuzifanya ziwe dhahiri. Mawazo
yote awazayo mtu kwa muda mrefu,maneno ambayo mtu huyasema mara kwa mara
huhifadhiwa hapa na baadae kuwa dhahiri, au hufanya mtu huyo awe kama jinsi
anavyowaza. Huendesha viungo vyote vya mwili mfano hutawala mapigo ya
moyo,mzunguko wa damu. Kiasi cha damu kinachotakiwa sehemu mbalimbali.
Huendesha usagaji wa chakula,na kijamii viwango vya kemikali vinavyohitajika
katika kusaga chakula au katika damu. Kwa kifupi sehemu hii ndio ndio
iendeshayo mzima wa binadamu. Eneo hili hupokea kila kitu kinachotoka katika
sehemu ile ya kwanza bila kujali kitu hicho ni cha kweli au cha uongo,kizuri au
kibaya huyapokea na kuyafanyia kazi,yaani huyafanya yawe dhahiri angalia
(Mithali 10:24) huhifadhi kila kitu kinachopelekwa huko na kukifanya kiwe
halisi huanza kutunza kumbukumbu za matukio mbalimbali yaliyotokea tangu akiwa
tumboni mwa mama. Hapo ni sawa na kusema huamini yote au kazi yake ni kuamini
kupokea na kutoa kumbukumbu au tunaweza kuziita stoo ya binadamu na imani
huhifadhiwa hapa. Kadri unavyojaza neno la Mungu ndani ya sehemu hii ya pili
ndivyo imani yako inavyoongezeka na kuzidi kukua. Hufanya kazi kwa
kuelewa(Intellegence_ kujiendesha yenyewe kwa kasi sana na kuweza kuratibu kila
kitu ndani ya mwili kwa kasi ya ajabusio kwa maamuzi binafsi.huwezi kutawala
kitu kilichoingia humo zaidi ya kuingiza mbadala wake yaani (opposite). Yaani
kama umeingiza mawazo ya kuwa wewe ni wa shida sana huwezi kuyaondoa mpaka
uingize mawazo mbadala kwamba wewe ni wa mafanikio na ushindi katika jina la
Yesu. Tumejifunza kwamba huyafanyia kazi yote
iliyopokea yawe ni hasi,au chanya ndio maana tunapatwa na yote
tunayowazia si yale tunayohitaji. Hupokea na kuyafanyia kazi mawazo yanayochukua
muda mrefu au zile hisia kali Deep fearing
zilizotoka sehemu ya kwanza. Pia hupokea na kutoka sehemu ya tatu ya
akili (Super conscious) yaani hupokea na kuhifadhi kumbukumbu zote zinazotoka
katika ulimwengu wa Roho na hufanya yaeleweke yale yanayotoka rohoni au roho
mafunuo na maono huhifadhiwa hapa . pia kinapotokea kitu cha kuogofya na ama
mtu kushtuka inafanya mwili kutumia nguvu ya ndani Inner Power ambayo si rahisi
kwa binadamu kuamua kuitumia anavyotaka. Zinakuja zenyewe mfano huamsha kinga
Immune za mwili kumfanya mtu aweze kukimbia sana anapostuka ghafla na
kurekebisha hali ya mwili mtu anapoumia n.k. kwa kweli tumeumbwa kwa jinsi ya
ajabu na ya kutisha Zaburi 139:14
Sehemu hii
huhusika katika kuhifadhi kumbukumbu,mambo yote yaliyofanyika au kutokea katika
maisha yako yamehifadhiwa mahali hapa. Iwe unayakumbuka au umeyasahau bado yapo
huendesha na kufanya kila kitu kinachofanyika katika mwili wa binadamu yaani
kuratibu utendaji wa mwili
SEHEMU YA
TATU YA AKILI (Super subconscious mind)
Hii ni
sehemu ya juu sana ya akili ya mwanadamu ni eneo ambalo mwanadamu hana uamuzi
nalo kabisa. Ni eneo ambalo ni muunganiko war oho ya mwanadamu na ulimwengu wa
Kiroho. Ni roho ya mwanadamu inapoungana na nafsi ya mwanadamu . ni Universal
lipo ndani ya akili ya mwanadamu lakini linaweza kutoka na kupokea ungamuzi
pasipo kutumia milango mitano ya fahamu. Ni chanzo cha vitu vinavyotoka kwa
Mungu yaani furaha,upendo,amani n.k. mambo yote yanayotoka kwa Mungu au kwa
shetani kuja kwako huingia kupitia eneo hili. Kwa mfano unapotaka uwe na furaha
na unapomuomba Mungu furaha,sehemu hii ya tatu hupokea furaha kutoka kwa Roho
wa Mungu na kuiambia sehemu ya pili kwamba ipokee na kupeleka furaha ndani ya
mhusika na mara mtu huyo anakuwa na furaha. Hii ni sehemu mojawapo
inayotutofautisha na wanyama. Hata waganga wa kienyeji na wachawi hutumia
sehemu hii ili kuwasiliana na mapepo na shetani,pamoja na kupokea nguvu kutoka
kwa pepo na mashetani wao kwa kutumia eneo hili. Kama unavyojua kwamba shetani
hajaumba kitu kitu chochote ila anatumia vitu vilivyoumbwa na Mungu kwa faida
yake. sehemu hii huweza kuwasiliana nje ya mwanadamu,yaani huweza kuwasiliana
na mtu mwingine wa mbali. Mfano wewe umekuwa mbali na familia yako na inatokea
mtu mmoja wa familia yako anaugua au anakufa na wewe uliye mbali unajua au unahisi kuwa hilo limetokea na baada ya
muda unathibitisha tukio kwa kupata taarifa. Hata Roho Mtakatifu hutumia eneo
hili kwa kutupa mambo ya kufanya maelekezo mbalimbali pamoja na tahadhari nayo
mfano ajali,hatari ya wanyama,mashambulizi ya kiroho na hata mambo mazuri
yajayo. Wakati kuna watu wamejaliwa kwa hali ya juu sana kutumia kipawa hiki
wana uwezo wa ajabu kuna wengi wao ambao huutumia vibaya uwezo huu kwa kumika
na nguvu za giza na mapepo. Naamini kuwa baada ya mafundisho haya hata wewe
unaweza kuitumia eneo hili la akili kwa utukufu wa Mungu.
NAMNA YA
KUTUMIA ENEO LA SUPER SUB CONCIOUS MIND KWA FAIDA.
Anza kwa
kusoma sehemu fulani ya Biblia inavyoelezea tukio fulani. Rudia tena na tena
kusoma na baadae funga macho na ujione kama upo katika tukio hilo. Jione ni
mmoja wa wahusika wa tukio lenyewe. Kwa kufanya hii mara kwa mara utajikuta
unakua hatua kwa hatua. Kumbuka ni muhimu sana kutumia neno la Mungu vinginevyo
ni hatari sana kwako. Watu wengi wa mashariki ya mbali huwa wanatumia sana eneo
hili la akili vibaya kwa uchawi. Lakini watu wa ulaya magharibi huwa
hawalitumii kabisa kwa kuwa hawaamini sana mambo ya imani za kiroho. Wao mambo
yao mengi wanayoamini ni lazima yawe na sababu Reasoning kupitia sayansi na teknolojia.
Ni muhimu sana kumuomba Mungu akupe uwezo wa kulitumia eneo hili la akili naye
atakupa. Atakupa uwezo wa kuona maono na kuota ndoto kwa maana hiyo ni ahadi
yake biblia inasema vijana watapata maono(maono ni mipango) na wazee wataota
ndoto si ndoto za kutisha au majinamizi bali ni ndoto za mambo yatakayokuja.
Iwapo wewe ni muhudumu wa kazi ya Mungu ni vizuri sana kutumia eneo hili sana
ili Mungu awe anakuonyesha na kukuelekeza jambo la kufanya wakati au kabla ya
huduma. Fahamu kwamba shetani hupenda kutumia vitu vizuri vya Mungu kwa faida
yake. hivyo hupenda sana kutumia eneo hili kwa kuleta maono ya uongo na
utabiri(unabii) wa uongo. Ni lazima upime kila unabii na maono kwa kutumia neno
la Mungu kwa kila kitu unachokipata.
MAWAZO NA
MANENO YANAVYOATHIRI MAISHA YETU.
Kutokana na
jinsi mtu anavyoamini, ndivyo jinsi anavyowaza na ndivyo jinsi anavyosema na
jinsi unavyosema ndivyo jinsi ulivyo. Hapo ninaweza kusema kwamba uko jinsi
ulivyo kutokana na mawazo uliyojiwazia na maneno uliyojisemea jana (Isaya 57:19).
Akili ya mtu inanasa kila kitu anachowaza mtu kuhusu yeye mwenyewe na kwa namna
ya pekee kabisa (Kwa uwezo wa Mungu). Akili inakifanyia kazi kile unachokiwazia
na kukitamka kuwa kitu halisi. Hivyo basi kila wakati unapowaza kitu ni sawa na
kupanda mbegu katika maisha yako. Ambayo itakuja kumea siku za usoni ziwe mbaya
au nzuri. Mfalme Daudi alimwambia mwanawe
Sulemani kwamba Mungu huchunguza mawazo (1Nyakati 28:9-10). Sisi
tumeumbwa kama watawala (Mwanzo 1:26) kwa maana hiyo tunatakiwa kuishi kama
watawala lakini pia tunatakiwa kuwaza kama watawala Mungu hapendi tuwaze mabaya
(Mithali 6:16-19) na wala usiyakumbuke mambo ya nyuma ambayo ulikosea (Isaya
43:18) unapongangania kuyakumbuka mambo ya nyuma na kuyatafakari kila wakati.
Ni sawa na gari lililokwama kwenye matope mchanga haliwezi kwenda. Hivyo ni
lazima ujinasue hapo ulipo katika fikra. Sisi tumeumbwa kwa ajili ya leo tu na
tunatakiwa kuitumia jana katika kujifunza na si katika kujuta. Ukianza kujuta
na kujihukumu au kuhukumu wengine kwa yale ya jana utakuwa unajiletesa mwenyewe
na kukwamisha maendeleo yako.
CHUKUA HATUA
YA KUBADILIKA.
Usipoamua
kubadilika mwenyewe hakuna atakayeweza kukubadilisha. Uamuzi na ufunguo wa
kubadilika unao wewe. Ukibadilika unavyowaza utabadilika unavyoishi. Kuna
uhusiano mkubwa sana kati ya mawazo yako na jinsi ulivyo. Kuna wale wanaoumia
kwa ajili ya mawazo ya kesho. Si vibaya kuwaza na kupanga mambo ya kesho yaani
siku zijazo,vilevile ni vyema na haki kujiandaa kwa maisha yako ya baadae kwa
kuanzisha miradi na kuweka akiba n.k. tunachoshauri hapa kwamba hakifai ni
kusikitika kwa jambo ambalo bado halijakupata au kukutokea kwa mfano unaanza
kuhofu jinsi utakavyofukuzwa kazi au jinsi utakavyoshindwa masomo au mitihani
yako. Mtu mwingine anaona labda baada ya miezi mitatu kodi ya nyumba itaisha
badala ya kufikiria jinsi atakavyoipata yeye anafiri jinsi mwenye nyumba
atakavyomfukuza na kumtukana usisahau kwamba Yesu Kristo alituonya.(Mathayo
6:34) kumbuka hakusema tusijipangie mipango ya baadae wala hakusema tumia vyote
unavyopata leo. Mungu anajua hayo tunayoyafanya na tunatakiwa tuyafanye (Mt
6:26) kwa kujisumbua na mawazo na mawazo
ya kesho ndio adui anapata nafasi ya kukushambulia. Akili zetu hazijaumbwa ili
kukaa na hasi, sasa unapokuwa mtu wa hasi, yaani unawaza hasi,unasema hasi ile
sehemu ya pili ya akili huyahifadhi hayo. Baada ya kuwaza kwa muda mrefu mawazo
hayo huhamishwa sehemu ya pili ili kuhifadhiwa kwa ajili yatokee dhahiri. Sasa
yanapofika sehemu ile ya pili hutokea mambo 3 ambayo ni.
(a) Kwa kuwa hatujaumbwa ili kuwaza
hasi,basi mfumo mzima wa uendeshaji wa mwili huvurugika. Damu itaenda kasi au
itapunguza kasi na hapo kuna hatari ya kupatwa na shinikizo la damu BP. Nyongo
itamwagika tumboni wakati isipohitajika na hapo kusabababisha hatari ya kupatwa
na vidonda vya tumbo na maradhi ya tumbo. Pamoja na chakula kutokusagika vizuri
zaidi hayo figo,bandama na viungo vingine vingine vya mwili vinaweza kushindwa
kufanya kazi inavyotakiwa na kusababisha magonjwa mengi mwilini. Pia ubongo
huvurugika na kuanza kuchanganyikiwa na kuwa na msongo (depression)kali ya
maisha.
(b) Tukio lingine ambalo hutokea na
ambalo pia ni baya ni kwamba ndani ya kumbukumbu zako kutajaa akiba mbaya
(hasi) na kama kukijaa akiba mbaya utakuwa ni mtu wa kuwaza hivyo tu maisha
yako yote kwa kuwa umepanda mahindi utavuna mahindi tu na wala si vinginevyo.
Kila siku utakuwa mtu wa huzuni hata kama utataka ziondoke hazitaondoka kwa
kuwa zina mizizi ndani kabisa ya akili yako.
(c) Jambo jingine ambalo litatokea ni
kwamba yale yaliyojaa katika sehemu hiyo ya pili yanapelekwa sehemu ya tatu ili
yaandaliwe mazingira ya kuwa kuwa dhahiri kama eneo hilo limejaa hasi basi
shetani atachukua hatamu na kuanza kutengeneza mazingira ya kuteseka kwako.
Wingi wa mawazo hasi ndani ya akili ya mtu huleta “tension” hali ya kuwa na
mchecheto au mashaka na wasiwasi wa mambo yajayo. Ukitaka kujua athari ya
mawazo hasi yanavyoleta uharibifu utaona mambo yafuatayo na jinsi yanavyotokea
mwilini mwako.
·
Kulala
sana au kukosa usingizi.
·
Shinikizo
la damu BP.
·
Kupungua
uzito mara kwa mara.
·
Kukosa
hamu ya kula chakula.
·
Kutokuhisi
njaa au kula kupita kiasi.
Haya ni
mambo ya awali kabisa yanayoashiria kuwa mwili wako umeathirika na mawazo hasi.
ITAENDELEA...
KAIZA nzuri sana mpendwa.
JibuFutaWasomaji wanaweza pia kupitia Kitabu cha WEKA UFAHAMU WAKO HURU. kilichoandikwa na John f. Paul.