FREEMASON
BIBLIA INASEMAJE?
Wapendwa
wana wa MUNGU, naamini hamjambo na mnaendelea vizuri katika kuukulia WOKOVU!
Sina shaka kwamba maoni na ushauri unaotolewa na watu mbalimbali kuhusu jamii hii ya siri ya masonry,unalenga
kuwaweka wacha MUNGU wa ukweli kuwa katika tahadhari si kwa kundi la Masonry peke
yake,bali pia hata kwa kazi zote za yule Adui (SHETANI). Kwanza niwatoe wasiwasi
kuwa Masonry si kundi la siri kama ambavyo, yeye mwenyenalo (shetani)
anavyojaribu kuongopa! Shetani tangu mwanzo ni muongo,hivyo anatumia welevu
wake mkubwa kudanganya kuwa yeye hufanya kazi kwa siri kubwa akitaka “ADUI”
zake….yaani wacha MUNGU wakweli waamini kuwa ati yeye anauhakika wa ushindi!
Ndg zangu mulio katika BWANA YESU KRISTO, jueni hivi kabla ya kujadili jambo
lolote unalodhani kuwa ni tata au ni mhimu kulijadili liwe linaonekana kuwa ni
la SIRI au si siri ki-ROHO,JIULIZE HIVI: je, BIBLIA ILISHAPATA KULIZUNGUMZIA
JAMBO TAJWA MAHALI NA WAKATI WOWOTE? Sababu ya kufanya hivyo ni, Biblia ndiyo
pekee neno la MUNGU,limehakikishwa na ndilo pekee linafaa kwa mafundisho,kwa
kuonya(kukuweka katika tahadhali kuu) kukuongoza nakuwaadabisha watu,lakini uwe
makini hapa watu wanaozungumziwa hapo ni wale tu WALIOOKOLEWA NA BWANA YESU
KRISTO,Maana wote walio nje ya WOKOVU hawana bahati hata kidogo ya kujua
ufafanuzi utolewao na ROHO Mtakatifu ili kuzijua zile lugha au vitendo anavyo
jaribu shetani kuzitafsiri kuwa ni”SIRI AU MAFUMBO MAKUU”ROHO MTAKATIFU kupitia
Neno la MUNGU- Biblia, yeye ndiye mwalimu. kama mwalimu hawezi kutoa ufumbuzi
wa jambo lolote analolifundisha, Mwalimu huyo ANAPOTEZA SIFA YA KUWA MWALIMU
mara moja!! Vivyohivyo,Mwanafunzi asiyeweza kujifunza kwa hamu,kwa
bidii,hafuatilii mifano na mazoezi yatolewayo na mwalimu wake,mwanafunzi huyo
ANAPOTEZA SIFA YA KUWA MWANAFUNZI maramoja! (wakati enzi sisi tunafuta ujinga
ktk kisomo chetu,ambacho vijana waleo wanweza kuiita ni “Ngumbalu”)Wale wote
waliokuwa hafuatilii masomo tuliwaita “WASINDIKIZAJI” Sasa jiangalie je wewe si
msindikizaji?Lakini pia nikueleweshe hivi,mwanafunzi wa chini hujua elimu ya
chini – yaani kila mwanadalasa kwa elimu ya dalasa lake tu,ili mtihani uletwe
kwa kiwango cha dalasa lako,lakini si kwa ujuzi wako! sasa jiulize hivi,
unashida gani, KUJUA au KUELEWA habari juu ya Masonry? Hilo ni swali la
kwanza,maana wanafunzi wasio makini husoma KUJUA jambo na si KUELEWA
jambo,ndiyo maana wanaigia na vikaratasi ktk mtihani! baada ya swali la kwanza
jiulize swali la mwisho kuwa ukisha JUA au KUELEWA jambo unaloliataka
utafanyaje?! Kwakuwa naamini kuwa naongea na wana wa MUNGU, basi hebu ni
nimnukuu BW.YESU KRISTO. BABA yetu huyu aliyajua yote haya,kama ujuavyo ni BABA
tu,ndiye huwajali watoto wake,maana ni lahisi kuwa mzazi ila “ngoma”
inakua,kama unapotakiwa kuwa BABA, labda mtu atajiuliza inawezekanaje kuwa
mzazi na usiwe baba au mama? inawezekana,..sitaki kuzungumzia hilo! Ndiyo maana
MUNGU huitwa BABA YETU,ila ukitaka kumuuita kuwa ni mzazi wako mimi hapo
nanyamaza! Kwa hiyo, YESU akasema…watu wangu wanaangamia kwa kukosa
MAARIFA,YAANI watu hufuata akili zao wenyewe ili wapotee! NENO linasema LIPO
JAMBO LIONEKANALO NI JEMA MACHONI PA MWANADAMU, LAKINI NI NJIA YA MAUTI!
Kwakifupi watu hawataki kukaa chini ya miguu ya Mwalimu apaswae kuwafundisha
ili waelewe waokolewe yaani chini ya huyo ROHO MTAKATIFU ,HATUPASWI KUJILAUMU
KUWA KTK HALI HIYO maana kama alivyo mwanafunzi wa kawaida hayuko tayari na
hapendi kabisa kitu kinachoitwa MITIHANI ,maana kiwago cha ubora wa mwanafunzi
yeyote ni kwa kiwango gani anafauru mitihani apewayo na mkufunzi wake! SASA
jiulize hauingii na vikaratasi katika mitihani ya mwalimu ROHO MTAKATIFU! Maana
huenda iko siku ilijisifia kuwa UNA UPAKO, na kuona kuwa MUNGU amekuokoa wewe
tu,kwa vile ulimuombea tasa akajifungua mtoto ukashindwa kuelewa pia kwamba
IMANI YA MHUSIKA MWENYEWE IMEMPONYA? kwa wale wanaoamini kuwa YESU ndiye
huyohuyo ROHO MTAKATIFU nasemanao hivi, BWANA.YESU KRISTO. mara kwa mara katika
kufanya uponyaji alizoea kusema, IMANI Yako imekuponya au na iwe kama
ulivyoomba(maana hakuna maombi yakawa maombi bila imani) nk. Ndg zangu
nisiwachoshe kwa maneno mengi mno ,ila huo ni mfano mmoja kati ya mifano elfu
nyingi inayoonyesha wazi kuwa hatuzijui habari na lugha za mbinguni kwakuwa
hatutaki kukaa chini ya miguu ya mwalimu GAMALIERI (ROHO MTAKATIFU) YESU
alisema “Zitambueni nyakati” kama ndege na wnyama wanajua sasa ni jioni
wanawahi kwenye usalama, je, inakuwaje ninyi watu wa MUNGU? BIBLIA inasema
SHETANI yupo, sasa unashangaa nini juu ya masonry na habari za kuwepo kwao?
sisemi nivibaya kuyachunguza mambo,ila yafanyeni mambo kwa kumtumia roho mtakatifu,
na wala si kwa kuumiza akili kwa namna yoyote ile. Neno la MUNGU si gumu wala
si maalumu kwa wachungaji peke yao,limewekwa ili kuwa njia ya wokovu wetu
mkuu.MUNGU si kama shetani kwa tabia,shetani hufanya mambo yake kwa siri,lakini
MUNGU hufanya mambo yake kwa uwazi na ukweli ili watu wapate kuokolewa. mwisho
JILINDENI NA ROHO ZIDANGANYAZO NA MAFUNDISHO YA MASHETANI. Kweli masonry
wapo,wawe wanabudu uchi,wanakunywa damu za watu,wanapesa sana wako milioni 6 au
zaidi,washirika wao ni watu maarufu nk, ni sawa tu, acha wazidi kuwepo na wale
watakao jiunga nao acha wafanye hivyo kadri watakavyo.Maadam NENO la MUNGU
linasema jambo hilo litakuwepo kwa sababu zilizonenwa! Kuwepo kwao au
kutokuwepo kwao sisi kwa nini? MUNGU ndiye hasa anajua sababu yakuwepo au
kutokuwepo kwa jambo lolote.cha msingi MUNGU atupe kinga,ambayo kwakweli alisha
tupa,hoja tu ni kwa kiasi gani tunatii-BWANA YESU KRISTO, alisema BILA MIMI
NYINYI HAMUWEZI NENO LOLOTE (Ulishapata kujiuliza maana ya ‘KUTOWEZA NENO AU
JAMBO LOLOTE?’)
Nimefurahi kuona watu wengi wana hamu sana ya
kutaka kuujua ukweli kuhusu FREEMASON nimesoma sana katika mitandao mbalimbali
kuhusu ukweli wa hili jambo labda niseme tuu kifupi nimepata elimu kiasi na
naamini kila mmoja anaweza kuendelea kuperuzi kwenye mtandao, kuna siri kubwa
sana kuhusu hili shirika au hii taasisi ya masonic.ukiangalia ktk mitandao
utaona inatumia alama nyingi za kishetani kama alama zao za kuwasilina, na kwa
kuwa dunia imekumbwa na hili wapo wanaojua na wasiojua wanazitumia hizo alama katika
kila kitu au vitu tunavyomia katika maisha yetu iwe marashii, nguo, alama za
magari, urembo, na ishara za mikono na mengine mengi …kimsingi hapa penda
usipende unakua unaabudu au kusifu na kutangaza hizo logo na signs ambazo
huuziita kitaalam Occult..Manake ni ficha katika kuonekana kwake..Inatisha sana
kusikia habari hizi kwa nchi za magharibi kama Marekani iko wazi na si jambo la
kificho. Mfano kama pesa ya Marekani imetengenezwa na hao masons angalia dola
moja nyuma ina piramidi ambayo haijaishaa na juu kuna jicho. Imendikwa maneno
fulani kirumi yakisema kwa Kiswahili .tangaza kuzaliwa. na lingine likimalizia
kuanza kwa New word order au ina
maana ingine god favour our ages
..huyo mungu wao ambae ni lucifer yaani shetani…anawasaidia vizazi na vizazi
ipo wapi na unaweza soma na ukaona mwenyewe mambo yao ni siri na yenye kificho
sana wana kivuli cha kwamba sisi ni brotherhood sijui charity, hakuna ni
ushetani mtupu…kifupi hawa ni wapinga KRISTO .Ipo jinsi ya mji wa WASHINTON DC
umejengwa kwa alama zao ambazo ziko wazi kabisa ….wanaamini katika uchafu wao
ila hawaamini WOKOVU kabisa wapo kila mahali ni ngumu kuwaepuka hivyo yatupasa
kusimama katika imani kisawa sawa ..lakini pia ni wazi mtaona makanisa mengi
yapo na hayana muamko au kuwa hai kiroho na wengi wetu ndio tunaoyapenda kwa kuwa
tunaona hayagusi maovu yetu,au kila ukienda hubadiliki kiroho kanisa la hivyo
nalo linakosa maana kabisa na wengi wetu tumefungwa na historia kuwa nilizaliwa
katika dhehebu hili au dini hii ..hivyo yanipasa kuwa hapo hivyo hata kama
hawakutibu kiroho …mimi kwa hapo nakataa yatupasa kubadilika na kuwa hai
KIROHO.Acha kufungwa na historia badilika kuna umuhimu gani kusali kama sehemu
unayosali haikutibu kiroho? au unajua kabisa na kuona madhaifu yake? Sehemu za hivyo
iwe ya UKRISTO au ya dini yeyote inayomwamini MUNGU haifai ….! yapo leo
makanisa mengii kila mmoja anasema kwangu ni bora na kwa yule si bora wana mali
nyingi na wanasisitiza sana matoleo ,wapo wanaounda miujiza …mimi hadi naogopa
kwani wanajua ukweli halafu wanalaghai watu ..Maskini ya MUNGU wengi wa waumini
ni maskini wanaotaka kuzikomboa nafsi zao lakini pia wanaingia katika mikono
isiyo salama ..hawa pia ni wakuwafanyia maombi sana maana hawana tofauti na
freemason ambao wanajificha katika vivuli vya vitu vizuri kama misaada mingi
mingi ….haya ma hall kama YMCA ,WYMC ,yote ni product za freemason …tunatakiwa
tuombe sanaa saanaa..jaman
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni